Search This Blog

Saturday, July 30, 2011

HAMIS KIIZA: NAICHEZEA YANGA KUMUENZI BABA YANGU


Umeshawahi kumshuhudia mchezaji mpya wa Yanga kutoka Uganda Hamis Kiiza akiwajibika uwanjani?

Anacheza kwa kasi, yupo kila sehemu huku akikaba kwa nguvu na kusaidia kupeleka mashambulizi mbele.

Je unaijua siri ya uchezaji wa namna ile wa Hamis Kiiza?Blog yako bora ya michezo inakuletea exclusive story ya Ugandan Golden Boy.

“Kiukweli naichezea Yanga kutokana na mapenzi makubwa niliyonayo kwa klabu hii, lakni sababu kubwa iliyonifanya nijiunge na Yanga mara tu walipoonyesha nia ya kunitaka ni kwamba marehemu baba yangu Mzee Kiiza wakati wa uhai wake alikuwa ni shabiki mkubwa wa Yanga, na kipindi nakuwa alikuwa akinunulia jezi za Yanga huku akinisisitiza nikifanikiwa kucheza soka la ushindani ukubwani nije niicheze klabu hii ya Jangwani, hivyo kujiunga kwangu na Yanga ni kufanikiwa kutimiza ndoto ya marehemu baba.

“Mzee Kiiza alikuwa ni mtanzania kabisa, lakini mwaka 1974 ilipotokea vita ya Uganda na Tz, alijiunga na jeshi la Tanzania kupigana na Iddi Amini, waliposhinda na kuingia Uganda, Baba alibaki Kampala na huko ndipo alipokutana na mama yangu,” alisema Hamis Kiiza ambaye kwa sasa yupo Uganda akiangalia familia yake baada ya mkewe kujifungua wiki iliyopita.

SAMATA NA OCHAN WAENDELEZA MAKALI MAZEMBE

MBWANA SAMATA(KUSHOTO) WALIOCHUCHUMAA AKIWA NDANI KATIKA KIKOSI CHA TP MAZEMBE
SAMATA "THE PRIDE OF TZEE" AKIWAPELEKA PUTA MABEKI WA TIMU PINZANI KATIKA MOJA YA MECHI ZA LIGI KUU YA KONGO.
PATRICK OCHAN DIMBANI AKIWA AMEKATA RASTA ZAKE

Friday, July 29, 2011

BREAKING NEWS: JURGEN KLISMANN KOCHA MPYA WA MAREKANI


Mchezaji na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Jurgen Klismann ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Marekani akimbadili Bob Bradley aliyetimuliwa wiki hii.

Bradley alitimuliwa jana Alhamisi baada ya miaka 5 ya uongozi, na sasa U.S soccer president Sunil Gulati amemtangaza Klismann kuwa manager mpya wa benchi la ufundi la watoto wa Obama.

Klismann ataiongoza U.S kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Mexico on August 10.

FERNANDO GAGO NAYE AVUTA JIKO

Msimu wa wacheza soka kuondokana na ubachela unaendelea.

Kiungo wa kimataifa wa Argentina na Real Madrid, Fernando Gago amefanikiwa kumuoa mchumba wake mcheza tennis Gisela Dulko.

Ndoa ilifanyika Jumatano katika wilaya ya Palermo jijini Buenos Aires, Aregentina.

MABINGWA WA KUPIGA PASI EUROPA KATIKA MISIMU 2 ILIYOPITA

DIABY NJE WIKI 10


Kiungo wa Arsenal Abou Diaby amefanyiwa operation ya enka na atakaa nje ya uwanja kwa wiki 10, Kocha Arsene Wenger ametangaza leo.

Kiungo huyo mfaransa alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya enka mwishoni mwa msimu uliopita, jambo ambalo limemkosesha kushiriki katika mechi za kujiandaa na msimu mpya.

Diaby anategemewa kuwa nje mpaka mwezi wa tisa, hivyo atakosa michezo ya premier league dhidi ya Newcastle, Liverpool na Manchester United kwa pamoja ya play off za champions league.

TFF YAPOKEA MAOMBI RASMI YA MGOSI KUSAJILIWA DC MOTEMA PEMBE

Shirikisho la soka la Tanzania TFF, limethibitisha kupokea maombi toka klabu ya Darlng club Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Simba Mussa Hassan Mgosi.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa shirikisho la soka la Tanzania TFF, Angetile Osiah amesema kwamba, maridhiano kwa pande zote mbili yamefikiwa, ambapo sasa Mgosi ataruhusiwa kuichezea klabu hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Arsenal yamnasa Juan Mata – Phil Jagielka is next

ARSENAL wanamatumaini makubwa ya kuwanasa kiungo Juan Mata na beki Phil Jagielka kwa kitita cha paundi milioni 34.
Winga wa Valencia Mata amewambia marafiki zake anajiunga na the Gunners kwa ada ya paundi milioni 19.
Wakati huo huo Arsene Wenger yupo mbioni kumnasa beki wa Everton Jagielka kwa ada ya paundi milioni 15.
Jagielka, mwenye umri wa miaka 28 anataraji kuhitaji mkataba wa miaka minne na mshahara wa paundi £100,000 kwa week.
Naye mshambuliaji Nicklas Bendtner yupo mbioni kujiunga na Sporting Lisbon kes sds ys psundi milioni 9.

BREAKING NEWZ: BANKA AASTAFU SOKA


Kiungo mkongwe wa Simba, Mohamed Banka aliyetolewa kwa mkopo Villa Squad amesema ameamua kuipa kisogo soka na kujikita kwenye biashara.
Uongozi wa Simba ulikutana na Banka juzi ili asaini mkataba mpya na waanze upya, lakini kiungo huyo aligoma kwa madai kuwa hawezi kucheza tena klabu iliyojaa majungu na maneno ya kila siku yasiyoisha.
Awali Simba ilitangaza kumpeleka kwa mkopo kiungo huyo kwenye timu ya Villa Squad kwa ajili ya kuimarisha kipaji chake, lakini mchezaji huyo amegoma na kwa sasa amejikita kwenye shughuli zake binafsi.

"Kiwango changu hakijaisha mpaka waniambie eti nikaimarishe kiwango, mimi sio wa kiivyo, wao walidhani wananikomoa kumbe wanajikomoa wenyewe mimi sasa hivi nafanya biashara zangu, tena imekuwa vizuri kwa kuwa napata muda mzuri wa kuzisimamia na kuziimarisha,"alisema Banka.

"Juzi baada ya kupeleka barua TFF waliniita na kutaka tuyamalize tuanze upya kwa kusaini mkataba mwingine, lakini siwezi, sina tena moyo wa kuichezea Simba, wamekuwa wakinituhumu mara kibao kuwa mimi ni Yanga, kila kitu kibaya wananiambia mimi, ni bora nisicheze mpira lakini niwe na amani kuliko nikae mahali sina amani, acha nifanye biashara zangu."alisisitiza Banka.

Alisema kilichomsababisha mpaka akaamua kuushtaki uongozi wa Simba TFF ni kitendo chao cha kuchelewesha kumtangaza kumuacha ili atafute timu nyingine na badala yake wamemuacha dakika za mwisho tayari usajili umeshapita hivyo anachotaka Simba wamlipe fidia na pia wavunje mkataba wake ili aweze kuangalia maslahi mengine.

source:www.mwananchi.co.tz

WENGER KUVUNJA REKODI YA USAJILI KWA MATA



Arsene Wenger yupo katika mipango kabambe ya kuvunja rekodi ya usajili katika klabu ya Arsenal kwa ajili ya Juan Mata huku akijipanga kuendeleza ugumu wa kumuachia Fabregas.

Wenger jana usiku alikubali kulipa ada ya £17million kwa Valencia kwa ajili ya Mata – na ameongeza ofa ya beki wa Everton Phil Jagielka kufikia £13million.

Lakini wakati Arsenal hatimaye wakijipanga kuanza kutumia katika usajili msimu huu, pia wamewapa Barcelona muda maalum wa kukamilisha uhamisho wa Cesc Fabregas.

The Gunners’ captain hatocheza katika kombe la Emirates wikiendi hii, na Arsenal wamewaambia walipe ada ya £40m au watasitisha dili hilo.

Wenger anaaminika kuweka deadline ya August 5 kupitia e-mail iliyotumwa kwenda kwa raisi wa Barca Sandro Rosell, ili mfaransa huyo apate muda wa kupanga mashambulizi ya msimu ujao.

Arsenal wamebariki uuzwaji wa Fabregas, lakini wamechoswa na kusubirishwa na Barca.

Dili la uhamisho wa Mata, 23, linawakilisha mapinduzi makubwa, baada ya ku-top kwa urahisi uhamisho wa £12m wa Andrey Arshavin in 2009.

Wenger pia ameongeza ofa nzuri kwa ajili Phil Jagielka baada ya kuona bid ya £10m ikakataliwa wiki mbili zilizopita, lakini Everton wanahitaji kiasi kisichopungua £15m.

Kama ikishindikana kumpata Jagielka, Arsenal wanaweza kurudi kwa Bolton centre-back Gary Cahil.


Kuwasili kwa Mata kunaweza kumaanisha Arshavin ataruhusiwa kuondoka, huku Galatasary wakijitokeza kumtaka, pia Sporting Lisbon wametuma ofa kwa ajili mshambuliaji Nicklas Bendtner, ingawa ofa hiyo ni pungufu kwa thamani waliyoipanga Gunners ya £12m na wareno hao wata-struggle kulipa mshahara wa £52,000.

THE MOST EXPENSIVE AGUERO @ ETIHAD STADIUM


Thursday, July 28, 2011

Ngassa arejea nyumbani,ATAJIUNGA RASMI NA SOUNDERS FEBRUARY MWAKANI KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MSIMU UJAO !




Mrisho Ngassa alikuja Seattle Sounders Fc kufanya majaribio kama sehemu ya juhudi za klabu ya Seattle Sounders kuongeza wigo wake kwenye masuala ya uskauti kwenye eneo la Afrika Mashariki.
Kwenye dakika ya 76 ya mchezo wa kirafiki baina ya Seattle Sounders na klabu bingwa ya England Manchester United wachezaji watatu waliingia kwa upande wa Seattle Sounders.
Miguel Montana mchezaji mwenye umri wa miaka 20 toka Colombia ni mmojawapo wa waliopata nafasi ya kuonyesha uwezo wao dhidi ya mojawapo kati ya vilabu vikubwa duniani Manchester United.
Mwingine alikuwa O’Brian White ambaye huu ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangu alipotolewa uvimbe wa damu kwenye mguu wake mwezi aprili .
Kivutio kilikuwa mchezaji wa tatu kwenye orodha hii ya wachezaji walioingia . Mrisho Ngassa aliingia akicheza kwenye eneo la kiungo wa upande wa kulia. Kuingia kwake kulikuwa kama hakuna maana ukizingatia kuwa tayari timu aliyopaswa kuchezea siku hiyo ilikuwa tayari imesharudi wavuni mara sita .
Ngassa aliingia kwa upande wa Sounders kama mchezaji anayefanya majaribio toka klabu ya ligi kuu nchini Tanzania Azam Fc .
Majaribio haya ya Ngassa yamejengwa kwa muda wa mwaka mmoja mzima. Seattle Sounders wamekuwa wakitengeneza mahusiano na nchi ya Tanzania tangu walipokuja mara ya kwanza msimu uliopita . Kocha msaidizi wa Seattle Sounders na mkuu wa maskauti au wasaka vipaji wa Seattle Kurt Schmid alifunga safari hadi nchini Tanzania mwaka jana kutazama mchezo na mazoezi ya timu ya Taifa ya Tanzania . Akisaidiwa na kupewa ushauri na kocha wa timu ya taifa Jan Poulsen , Schmid alimchagua Ngassa kama mchezaji aliyemvutia na atakayempa nafasi ya kufanya majaribio kwenye timu yake ya Seattle Sounders .
“Unapokwenda sehemu kama Tanzania na kumuona mtu ambaye amewazidi wenzie kwa mambo karibu yote ni lazima uulize kwanini? Alisema Schmid.
Jibu la swali la Schmid, kwanini Ngassa lilikuwa kwenye kasi na kipaji kilichopo kwenye miguu yake .
Akiwa na kimo kidogo cha futi 5 , Ngassa anatumia vyema kasi aliyo nayo kuwapita mabeki akiwapiga chenga za akili huku akiwatengenezea wenzie nafasi za kufunga . Hata kwenye mechi dhidi ya Man United kwa dakika chache alizopata za kuonyesha uwezo wake aliweza kupiga shuti moja , ambapo alikosa nafasi iliyookolewa na Rio Ferdinand .
“Ngassa ni mtu mwenye umbo dogo, ila tuna uzoefu wa kuwa na wachezaji wenye vimo vidogo ambao wanafanya vizuri na timu zao na hata kwetu pia na wanacheza vizuri tu. Ana kasi ya ajabu, nadhani kasi yake kwenye mbio fupi ni hatari sana , anasema Schmid,ana uwezo mkubwa sana kiufundi , anaweza kuwapiga chenga mabeki na kupiga mashuti pia. Ana uwezo wa kuusoma mchezo vizuri ila anahitaji kuwa na juhudi kwenye ukabaji kidogo ili akamilike kiuchezaji.
Huku kukiwa na ishara zote juu ya matunda ambayo yanaweza kuchumwa na Seattle Sounders kama matunda ya uhusiano wake na Tanzania , faida haitakuja kwa Seattle Sounders peke yake . Kwa mujibu wa Mmiliki wa Klabu ya African Lyon Rahim Zamunda Kangezi ambaye alikuwa sambamba na Ngassa kwenye safari yake nchini Marekani , nafasi kwa Seattle na Vilabu vingine vya MLS zitaongeza sifa na wigo wa soka la Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki kama ilivyofanya nchi ya Ufaransa kwa nchi za Afrika Magharibi.
“Vipaji ni vile vile kama vya Afrika Magharibi ila tofauti ni kwamba Afrika Magharibi wana mahusiano na nchi ya Ufaransa . Sounders inawapa nafasi kama hii wachezaji wa Afrika Mashariki kwa kutumia mahusiano na nchi za Afrika Mashariki , alisema Zamunda . “Unapozungumzia soka barani Afrika ni ndoto ya kila mchezaji . Kuwaona wachezaji hawa wakija Marekani kucheza soka ni faraja kubwa sana kwa soka letu.
Seattle Sounders wanakubali kuwa nguvu iliyoko kwenye uhusiano wa vilabu vya Marekani na wawakilishi toka Tanzania itasaidia kuleta mambo mazuri zaidi na yanaweza kuleta vipaji zaidi toka mahali ambako MLS bado haijapagusa .
“Tanzania ni mahali ambako hapajaguswa . Kuna watu wanaotoka sehemu hii wanaocheza Ubelgiji na Norway ambao wamezunguka sehemu mbalimbali ulimwenguni alisema Schmid,. Nadhani ni sehemu ambayo kuna vipaji vingi vya asili na hakika kuna watu wanaojua kucheza huko , kunahitaji maendeleo tu zaidi na kwa uhusiano huu kuna mengi mazuri yanakuja na tutawaendeleza wachezaji hawa.
Ngassa anatarajiwa kurudi Tanzania baadae na atarejea mnamo mwezi February mwakani kujiunga na Seattle Sounders kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa mwaka 2012.


SOURCE: www.soundersfc.com

SAMBA: NIACHENI NIJIUNGE NA ARSENAL


Chris Samba ameiomba klabu yake ya Blackburn: Niacheni nijiunge na Arsenal.

Nahodha huyo alisema: “Nataka kucheza kwenye ligi ya mabingwa.Mchezaji asiyeota kuhusu hili.”

Beki huyu mfaransa, 27, alisaini mkataba mpya wa miaka 5 ya kuitumikia klabu hiyo ya Ewood Park miezi michache iliyopita, lakini amesisitiza: “Mchezaji ambaye ana uchu wa kucheza katika ngazi za juu basi atakuwa amekosea na amechagua mhezo usiomfaa.”

“Sijui nini wanachofanya Arsenal kwa sababu sishughuliki na na mambo hayo, hivyo hilo sio tatizo langu.

“Kwa sasa mimi bado mchezaji wa Blackburn lakini nitakuwa muongo mkubwa nikisema kila kitu kipo sawa na sitaki kucheza kwenye champions league.”

Arsene Wenger amekuwa akimfuatilia Samba mwenye thamani inayokadiriwa kufikia £12million lakini mpaka sasa ameshindwa kukamilisha dili hilo.

KUN AGUERO MCHEZAJI GHALI ZAIDI NDANI YA JIJI LA MANCHESTER


Sergio Aguero amemalizana na matajiri wa Manchester City hivyo kutangazwa kuwa mchezaji rasmi wa kikosi cha Roberto Mancini.

City wamekubali kulipa £38 kwa Atletico Madrid kwa ajili mkwe wa Diego Maradona, ambaye amesaini mkataba wa miaka 5 huku akiwa anapata mshahara wa £200,000 kwa wiki, hivyo kufanya thamani ya jumla ya uhamisho wake kuwa zaidi ya £85million.

Uhamisho huu wenye thamani £85m wa Aguero, 23, ambaye atavaa jezi no.16 ndio wa ghali zaidi katika historia ya vilabu vya jiji la Manchester.

Wednesday, July 27, 2011

AGUERO ATUA ENGLAND KUMALIZANA NA CITY


Sergio Aguero ametua jijini Manchester kukamilisha uhamisho wake kutoka Atletico Madrid kwenda Eastlands kwa dili lenye thamani ya £38million.

Muargentina huyo alisafiri kutoka kwao jana Jumanne usiku mara baada ya klabu mbili kumalizana, na alitumia mtandao wa Twitter kuelezea kuwasili kwake in Manchester.

Aliandika: “Nimefika jijini Manchester kukamilisha details za ofa ya City.Kila kitu kipo sawa, muda mchache ujao nitawaambia zaidi.”

ARGUERO KWENDA UK KUMALIZANA NA CITY

Sergio Aguero anakaribia kujiunga na Manchester City kwa dili la uhamisho wa £40million.

Argentina striker atawasili jijini London kesho Jumatano kukamilisha mazungumzo ya kuhamishia makali yake @ Etihad Stadium akitokea Atletico Madrid.

Aguero anatazamwa kama ndiye mrithi sahihi wa Carlos Tevez, ambaye kwa sasa yupo katika harakati za kuhakikisha anahama Man City baada ya uhamisho wake wa kuelekea Corinthians kufeli.

Kun Aguero anatarajiwa atasaini mkataba wa miaka 5 huku akipata mshahara wa £200,000 kwa wiki baada ya kulazimisha kuhama Atletico Madrid.

The 23-year old atakuwa akisindikizwa na wakala wake Hernan Reguera .

Tuesday, July 26, 2011

DAVID GILL:UNITED TUTASAJILI MCHEZAJI MMOJA TU WA DARAJA LA JUU


Afisa mkuu wa klabu ya Manchester United David Gill amethibitisha kuwa klabu yake inajiandaa kusajili mchezaji mmoja mwenye hadhi ya juu katika kipindi hiki cha usajili.

Red Devils tayari wameshajili wachezaji watatu katika kipindi hiki cha usajili, Golikipa David De Gea akimrithi Van Der Sar, huku Ashley Young na Phil Jones wakiongezwa kuimarisha kikosi kwenye ulinzi na ushambuliaji.

Sir Alex Ferguson juzi aliweka wazi kuwa hakuna uhakika wa kuwepo kwa usajili mpya kabla ya mchezo wa ngao ya hisani at Wembley mwezi ujao tarehe 14, na sasa Gill amekiri kuwa hakuna usajili utakaofanyika katika siku za karibuni, ingawa CEO huyo amewahakikishia mashabiki na wapenzi wa United kuwa watafanya usajili wa mchezaji mmoja kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili August 31.

“Van Der Sar alisema mapema kuwa msimu uliopita ndio ulikuwa wa mwisho, hivyo tulijipanga kusajili golikipa, na nafasi nyingine zilipotokea tulizijaza vizuri,” aliiambia MUTV.

“Mpaka sasa tumesajili wachezaji watatu, nab ado tunajiandaa kusajili mwingine mmoja.

“Hakuna kinachofanyika kwa sasa, lakini tutaona nini kitatokea tutakaporudi nyumbani.Bado kuna siku zaidi ya 31 za dirisha la usajili, kwahiyo chochote kinaweza kutokea.Lakini kwa sasa sishughulikii na uhamisho wowote.”

Gill pia amethibitisha kuwa Ferguson anajiandaa kuimarisha sehemu Fulani ya kikosi, huku nafasi ya kiungo mshambuliaji ikitajwa sana kufuatia kustaafu kwa Paul Scholes.

Samir Nasri na kiungo mchezeshaji wa Tottenham Luka Modric wote wamekuwa wakihusishwa na United, huku speculation zikiendelea kuhusu kiungo wa kidachi wa Inter Milan Wesley Sneijder.

Wakati Gill akikataa kutaja mchezaji wanayemuwania, lakini United CEO amekiri kuwa ni mchezaji mwenye daraja la juu pekee ndio atakuwa anahitajika ndani kikosi cha Red Devils.

“Tumekuwa tukiwafuatilia wachezaji wawili au 3 wa nafasi moja, lakini mpaka sasa hakijafanyika kitu juu ya usajili wa mchezaji huyo.Suala muhimu ni kuwa Alex ameweka wazi kwamba tunahitaji mtu ambaye atakuja kusaidia kuongeza ubora wa kikosi.

“Tuna kikosi kizuri na kikubwa na ili uweze kupata nafasi ya kuingia ndani ya kikosi hicho inabidi uwe mchezaji wa daraja la juu.” Alimaliza David Gill.

BREAKING NEWS! SOUNDERS YATOA NAFASI 3 KWA WACHEZAJI WA KITANZANIA KILA MWAKA.

HAPA NIKIWA NA ADRIAN,GENERAL MANAGER AND OWNER ,SEATTLE SOUNDERS

PIA VIONGOZI WA VILABU WAALIKWA KUJA KUPIGWA MSASA NAMNA YA KUUENDESHA KISASA MCHEZO WA SOKA.

Mtendaji mkuu na mmiliki wa timu ya SEATTLE SOUNDERS Mr ADRIAN Hanauer ameahidi kuwapatia wachezaji 3 wa kitanzania kila mwaka nafasi ya kuja kufanya majaribio ya kujiunga na timu ya Seattle Sounders, lakini mmoja kati ya hao wachezaji lazima awe ni kijana mwenye umri chini ya miaka 17.
Adrian amesema sera nzuri za Mweshimiwa Raisi JAKAYA MRISHO KIKWETE kutaka kuinua michezo nchini ndizo zimemsukuma kutoa hiyo nafasi adimu kwa watanzania.

" Ligi yetu inazidi kupata umaarufu mkubwa kadri siku zinavyokwenda mbele na timu yetu kama unavyoiona inafanya vizuri na wachezaji wengi sasa wanataka kuja kuichezea,na hii ni kwasababu ya mipango madhubuti tuliyojiwekea kwa ajili ya kuindeleza timu yetu"

ADRIAN pia amesema SOUNDERS itawatumia mialiko baadhi ya viongozi wa timu zinazoshiliki ligi kuu ya VODACOM kuja nchini Marekani kujifunza namna mpira unavyoendeshwa kisasa.

" Hapa Marekani michezo ni moja kati ya sekta zinazotengeneza sana pesa,kwa miaka mingi michezo kama Basketball,American Football na Baseball imekuwa ikitengeneza sana pesa na hii ni kutokana na michezo hiyo kuwa na umaarufu mkubwa hapa, lakini tangu mchezo wa soka nao uanze ku-promotiwa vilivyo basi nao umeanza kuwa maarufu na sasa pesa nyingi zinatengenezwa,
kwahiyo nafikiri tutatoa fursa kwa viongozi wa vilabu vyenu kuja hapa wapigwe msasa kidogo ili wakaongoze mpira kisasa, mpira wa miguu ni bidhaa hadimu sana si ulaya au marekani pekee, bali mahala popote pale kama wahusika wanajua maana na umuhimu wa kuuendesha kisasa basi pesa zitatengenezwa "





TOP 10 YA WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI KWENYE KLABU YA SEATTLE SOUNDERS.

FREDY MONTERO ( kulia,mwenye namba 17 ) kushoto kabisa ni Mtanzania anayeishi marekani Mr Mudrick Majaliwa.

Mara nyingi ukifanya kazi kwa juhudi mwisho wa siku matunda huonekana,
Juhudi za mshambuliaji Fredy Montero raia wa Colombia zimemfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye klabu ya SEATTLE SOUNDERS ya nchini Marekani, SOUNDERS ndiyo timu anayotarajia kuichezea Mtanzania, Mrisho Ngassa,
Montero amepata ongezeko la kiasi cha $ 500,000 kwa mwaka katika mshahara wake na kumfanya sasa kupata kiasi cha $ 636,000 (zidisha mara 1,500 ili upate ni kiasi gani kwa pesa za kitanzania).

hapo awali Montero alikuwa anapata mshahara wa $ 136,000 kwa mwaka kiasi ambacho ni kama $11,333 kwa mwezi,
lakini juhudi zake ndani na nje ya uwanja sasa zinamfanya aweke kibindoni kiasi cha $ 53,000 kwa mwezi sawa na milioni 79.5 za kitanzania.
kutokana na SOUNDERS kuendelea kufanya vizuri kwenye ligi kuu ya soka nchini Marekani (MLS ) ambayo inaendelea,imepelekea kila mchezaji apate ongezeko la mshahara kutokana na namna alivyotoa mchango wake katika timu.


HUU NDIYO MSIMAMO KAMILI WA WACHEZAJI WA SOUNDERS WANAOLIPWA MSHAHARA MKUBWA ( KUANZIA KUSHOTO NI ONGEZEKO NA KULIA NI JUMLA ).

1. Montero Fredy $500,000.00 $636,000.00

2. Fernandez Alvaro $300,000.00 $366,666.67

3. Keller Kasey $250,000.00 $250,000.00

4. Jaqua Nate $200,000.00 $211,000.00

5. Zakuani Steve $90,000.00 $188,000.00

6. White O'Brian $100,000.00 $147,500.00

7. Evans Brad $126,500.00 $140,250.00

8. Alonso Osvaldo $140,000.00 $140,000.00

9. Parke Jeff $136,500.00 $136,500.00

10.Hurtado John Kennedy $135,000.00 $136,000.00

HAYA WACHEZAJI WA KITANZANIA MNATAKIWA KUJITOLEA MUHANGA KATIKA MAANDALIZI YENU KAMA KWELI MNATAKA KUJA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA KWENYE MLS MAANA KILA MWAKA KUNA NAFASI 3 KWA AJILI YENU ZA KUJA KUJIUNGA NA TIMU HII.



PODOLSKI AVULIWA UNAHODHA COLOGNE



Mshambuliaji wa Ujerumani Lukas Podolski amevuliwa unahodha timu ya FC Cologne na beki wa kibrazil Pedro Geromel ameteuliwa kama mrithi wake, kocha Stale Solbakken amesema jana Jumatatu.

Kocha huyo Mnorway, ambaye bado hajaanza kuiongonza timu hiyo katika mechi za ushindani tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi uliopita, amechukua uamuzi huo ikiwa ni wiki mbili kabla ya kuanza kwa ligi ya Bundesliga.

“Naelewa uamuzi niliouchukua utakuwa na athari zipi, na nitakubaliana kabisa na baadhi ya malalmiko ya mashabiki,” kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari.

“Lakini nataka mashabiki wauamini uamuzi wangu kuwa ni mzuri na una manufaa kwa timu, Pedro Geromel atakuwa ndio nahodha mpya katika kuhakikisha naleta utaratibu na utamaduni mpya ndani ya timu ninayoingoza.

“Nimeongea na Lukas, na amenielezea masikitiko yake lakini pia ameamua kuuheshimu uamuzi huu kwa sababu ameelewa maana na dhamira yangu.”

Podolski, 26, alirudi Cologne mwaka 2009 baada ya misimu 3 ndani ya Bayern Munich na amekuwa kipenzi cha mashabiki wa timu, amefunga mabao 13 kwenye Bundesliga msimu uliopita na kuisaidia klabu kumaliza ligi wakiwa kwenye top 10.

Geromel alijiunga na Cologne mwaka 2008 akitokea Vitoria Guimaraes ya Ureno.

BATISTA AFUKUZWA KAZI ARGENTINA


Chama cha soka la nchini Argentina (AFA) kimetangaza kusistisha ajira ya kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Sergio Batista baada ya timu hiyo kutolewa katika robo fainali ya Copa America.

Batista ambaye aliongoza Argentina katika michuano ya Copa America akichukua nafasi ya Diego Maradona na kuwa kocha wa nne ndani ya miaka 5.

“Batista ameachishwa kazi ya ukocha mkuu wa timu ya taifa” Ernesto Cherquis Bialo, msemaji wa chama cha soka cha Argentina alisema, jana Jumatatu.

Mpaka sasa kocha wa zamani wa Argentine Club Estudiantes Alejandro Sabella, na kocha wa Paraguay Gerardo Martino ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumrithi Batista.

Msemaji wa AFA, Cherquis Bialo amesema kocha mpya atatangazwa ndani ya wiki moja.

Heshima ya soka Argentina imeshuka kutokana matatizo ya makocha wanaoshindwa kuunda muunganiko mzuri wa timu yenye kama wengi, kitu kilichowafanya kukosa kushinda kombe lolote kubwa ndani ya miaka 18, sasa ni miaka 25 tangu Argentina wachukue kombe la dunia.

ADAM NDITI -CHELSEA , Thomas Ulimwengu vs Hamburg- ????



BABU KAJU AZINDUA KITABU CHA SOKA,SASA AWEKEZA KWENYE SOKA LA VIJANA....

Mdau mkubwa wa mchezo wa soka nchini Tanzania,ALEX Kajumulo akinikabidhi kitabu alichokiandika kinachohusiana na mambo ya soka,Kajumulo anaishi nchini Marekani.
Alex Kajumulo aliwahi kumiliki klabu ya soka nchini Tanzania,sasa ameamua kuwekeza kwenye soka la vijana,hapa ilikuwa ni baada ya kumvamia mazoezini na ikabidi nipige picha ya na kikosi hicho chenye mchanganyiko wa wavulana na wasichana.

SPURS WATAKA £9Mm KWA AJILI YA CROUCH


Tottenham wameweka bei ya kumnunua Peter Crouch kwa timu zinazomtaka kuwa £9million.

Newcastle wameonekana kuongoza mbio za kuisaka saini ya Crouch na Harry Redknapp amesema anataka kupata fedha aliyotoa kumnunua kutoka Portsmouth miaka miwili iliyopita.

Kiasi hicho cha pesa kinaonekana ni kizingiti kikubwa kwa watoto wa Mike Ashley ambao hawapo tayari kulipa fedha hiyo kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Sunderland ambao wamekuwa wakimtamani Crouch kwa muda sasa, na walikuwa tayari kumbadilisha na Asamoah Gyan earlier this summer, lakini sasa Steve Bruce akiwa tayari amempata wonderkid Connor Wickham, Black Cats wanaonekana kubadili mawazo juu ya Crouch.

Monday, July 25, 2011

EL CLASSICO KWENYE TUZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA

Upinzani baina ya Real Madrid na Barcelona maarufu kama “El Classico” umeamia kwenye tuzo za mchezaji bora barani ulaya baada ya Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Xavi Hernandez kuchaguliwa kugombea tuzo hiyo.

Tuzo hizo zimepangwa kufanyika mwezi ujao baada ya wachezaji hao watatu kuchaguliwa na waandishi wa michezo 53 kutoka katika kila mwananchama wa UEFA katika listi ambayo pia imewahusisha Wayne Rooney na Andres Iniesta.

Kura za kuchagua mchezaji bora atakayeshinda tuzo hiyo zitapigwa August 25.

HATIMAYE SASA NAAMINI NIMEFAULU MAJARIBIO YA KUJIUNGA NA SEATTLE SOUNDERS-MRISHO NGASSA

'' Mara tu baada ya mazoezi kabla ya timu kuelekea nchini Panama,kocha mkuu wa Sounders bwana Sigi Schmid aliniita na kufanya naye mazungumzo ya takribani dakika kama 20 hivi,
kimsingi alikuwa ananiuliza maswali mbali mbali, mfano aliniuliza kama nipo tayari kuichezea SEATTLE SOUNDERS pi akaniuliza kama ningefurahia kuishi hapa SEATTLE ,namimi nilimjibu kuwa nipo tayari ,
basi baada ya hapo akaanza kunielezea namna nilivyofanya vizuri kwenye majaribio na angependa niichezee Sounders,
mwisho kabisa akaniambia kwakuwa muda wangu wa majaribio umekwisha sina budu kurejea nyumbani taratibu husika zifanyike ili niweze lurejea hapa mapema mwezi december kwa ajili ya kujiunga na timu moja kwa moja ''- MRISHO NGASSA

HATIMAYE N'ZOGBIA KUTUA VILLA PARK


Hatimaye Aston Villa wamekubali kulipa £9.5million kama ada ya uhamisho wa winga wa Wigan Athletic Charles N’Zogbia.Wigan walikataa ofa ya £9m kutoka Villa kwa ya mchezaji huyo wa zamani wa Newcastle mwanzoni mwa July, lakini sasa wamekubali kumuuza.

Klabu hizo mbili walifanya mazungumzo ndani weekend na kukubaliana na ofa ya £9.5m.

Kocha mpya wa Villa A lex McLeish anahitaji winga mpya baada ya kuondoka kwa Ashley Young na Stewart Downing waliohamia Man United na Liverpool.

mrisho ngassa vs man utd

URUGUAY MABINGWA WA KIHISTORIA COPA AMERICA: VIDEO

BEKI MPYA WA ARSENAL, NI STRAIKA AU BEKI?

MADOIDO YAMPONZA BALOTELLI

Sunday, July 24, 2011

COPA AMERICA FINAL: PARAGUAY VS URUGUAY-LARISSA KUTIMIZA AHADI YAKE

Michuano ya kombe la mataifa ya marekani ya kusini Copa America inafika tamati kwa mchezo wa fainali kati ya Paraguay na Uruguay. Ni fainali ambayo hakika itakuwa na mvuto kwa kuwa kila timu hizi zinapokutana kuna uhakika wa magoli si pungufu ya matatu na kuna kila sababu ya takwimu hii kuendelea . Ukitazama Historia ya Copa America kama inawapendelea Uruguay kwa kuwa wametwaa Copa America mara 14 na wanatafuta kuweka rekodi ya kutwaa kombe hili kwa mara ya 15. Katika michezo michache waliyocheza Uruguay na Paraguay kwenye Copa America Paraguay wameibuka na ushindi mara nne na hiyo pekee inatosha kuwapa waparaguay sababu ya kushinda japo hadi fainali hawajaweza kushinda mchezo hata mmoja wakitoka sare mara zote wanazotia timu .

Paraguay wanaweza kuwa na sababu ya ziada ya kufanya vizuri kwenye mchezo huu nayo ni jina la mwanamitindo Larissa Riquelme. Mrembo huyu alileta balaa kwenye kombe la dunia nchini ‘ssauzi’ kwa nadhiri aliyoiweka ambayo iliwafanya mashabiki wengi waiombee Paraguay itwae kombe la dunia ili mradi tu waweze kumshuhudia mrembi huyu akitimiza nadhiri aliyoiweka . Larissa aliapa kuwa ikiwa Paraguay itatwaa kombe la dunia atasaula nguo zake zote katikati ya uwanja na kushangilia na wachezaji wa timu yake ya taiafa na akasema atarudia kufanya hivyo mitaani nchini kwao Paraguay . Bahati mbaya kwa watu walioomba Paraguay ishinde kwani haikuwa hivyo na hawakuweza kuona vimbwanga vya mrembo Larissa .

Maombi ya wato wote waliotaka kumshuhudia Larissa akitimiza nadhiri yake yanaonekana kutimia kwani Paraguay wamefuzu kucheza fainali ya kombe la mataifa ya marekani ya kusini ambapo wanakutana na Uruguay . Larissa Riquelme amerudia tena azma yake na amesema kuwa ikiwa Paraguay itashinda dhidi ya Uruguay basi atasaula nguo zake zote ana ataungana na wachezaji wa Paraguay uwanjani kushangilia na pia atarudia hayo tena nyumbani kwa Paraguay mitaani ambapo ataonyesha furaha yake kwa Paraguay kupata ushindi .Tungoje kuona kama tutapata bahati ya kushuhudia mrembo huyu aliyechizika na mchezo wa soka akitimza nadhiri aliyoiweka , kazi kwenu kina Lucas Barios , Roque Santa Cruz , Nelson Haedo Valdez na Justo Villar ,mpeni raha mwanadada Larissa Riquelme.

KWA UPANDE WANGU NGASSA AMESHAFAULU MAJARIBIO YAKE- Kocha Mkuu, Sigi Schmid

Kama Mrisho Ngassa angekuwa anafanya majaribio ya kuchezea moja ya klabu za nchini kwetu Tanzania basi muda huu angekuwa tayari ameshasaini form za kujiunga na klabu hiyo,
lakini utaratibu wa kumsajili mchezaji ni tofauti kabisa kwa wenzetu,kufahamu hilo fuatilia mahojiano yangu na kocha mkuu wa SEATTLE SOUNDERS bwana SIGI SCHMID,
kifupi ni kwamba kuna hatua za kiufundi zinazofuatwa kabla ya mchezaji kusajiliwa,ni tofauti na kwetu Tanzania ambapo kiongozi mmoja huwa na nguvu na ujasili wa ajabu wa kumsajili mchezaji kwa matakwa au mapenzi yake binafsi pasipokuweka UWELEDI mbele.

haya ni mahojiano maalumu na kocha wa SOUNDERS Mr SIGI SCHMID.

UNAZUMZUNGUMZIAJE UWEZO WA MRISHO NGASSA KWA KIPINDI ULICHOKAA NAYE ?
Mrisho ngassa amenifurahisha sana,ni mchezaji aliyekamilika kwa kiasi kikubwa,anaweza kusumbua sana kutokana namna anavyocheza, kwenye mazoezi kwa siku zote amefanya vizuri na hata kwenye mechi dhidi ya Manchester Utd alifanya vile nilivyomuelekeza kufanya

NGASSA NI MCHEZAJI WA NAMNA GANI ?
kitu kingine kizuri kwa ngassa ni msikivu kila majukumu niliyompatia ameyatekeleza vilivyo, ana uwezo wa kucheza sehemu zote za pembeni,
anapenda kushambulia akitokea pembeni kushoto kwasasbabu ana mbio sana na ni rahisi kuisaidia timu pindi inapokuwa inatafuta bao,lakini pia ni mzuri akiwa anatokea kulia kwa ajili ya kusaidia pasi ili wengine wafunge,

SEHEMU GANI ANA MAPUNGUFU ?
Sijaona mapungufu sana kwani kwa namna anavyotakiwa kutumika amekamilika lakini cha ziada ni kuongeza nguvu kidogo tu ili aweze kushindana pasipokuwa na wasiwasi kwenye MLS (MAJOR LEAGUE SOCCER )

NINI NAFASI YAKE Font sizeKWENYE KIKOSI CHAKO CHA SOUNDERS KWA SIKU ZA BAADAE?
Kwa upande wangu hakuna tatizo hata kidogo,kifupi nimemkubali ila kuna watu wengi sana wanaoamua mchezaji kusajiliwa, general manager ana mkono wake,chief scout naye ana mkono wake na pia kama ulivyooona kuna wasaidizi wangu wengi kwenye benchi la ufundi,kila mmoja ana jukumu lake kwahiyo nasubilia ripoti zao alafu nikae na wakurugenzi na viongozi wengine ili uwamuzi wa pamoja utolewe.

RIPOTI YAKO BINAFSI INASEMAJE KUMUHUSU NGASSA
Kama nilivyokwambia awali kwangu hana pingamizi. Tatizo ni kwenye management, wao ndiyo wanaojua yupo hapa kwa muda gani, kama maamuzi yangekuwa yangu pekee basi huyu mchezaji asingeondoka tena hapa.

hapa ilikuwa ni baada ya mazoezi ya leo kocha Sigi Schmid (kushoto ) akiteta jambo na mmiliki na General manager wa SOUNDERS Mr Adrian Hanauer ( mwenye pensi ya khakhi )


kocha mkuu wa SEATTLE SOUNDERS Mr SIGI SCHMID akiwa na MRISHO NGASSA mara baada ya mazoezi ya leo.






hapa ilikuwa baada ya kumaliza kufanya mahojiano yetu,pia haya mahojiano utayapata kupitia SPORTS XTRA ya CLOUDS FM.






NGASSA mara baada ya mazoezi ya leo akiwa na kiungoAMADOU toka nchini Gambia.ambaye pia wanaishi nyumba moja.












JAMANI! JAMANI! hili ni benchi la ufundi la SOUNDERS kila mmoja wao hapa ana jukumu lake, waangalie kila mmoja alivyokuwa makini akifuatilia NG'ADO KWA NG'ADO ( kwa ukaribu mno ) kila kinachoendelewa wakati wa mazoezi..














Historia ya upinzani baina ya miamba ya soka nchini Kenya AFC Leopards na Gor Mahia .

Mchezo wa soka duniani kote unaongezwa ladha na upinzani . Mahali kokote utakapokwenda hata uswahilini ambako kuna soka la mpira wa makaratasi lazima utakuta kuna timu mbili ambazo zina upinzani mkali ambao ndio hasa unanogesha mechi baina ya timu hizo.Hapa nchini kwetu kuna Simba na Yanga , Afrika Kusini kuna Orlando Pirates na Kaizer Chiefs ,nchini Misri kuna National Al Ahly na Zamalek,nchini Ghana kuna Asante Kotoko na Hearts of oak , Argentina kuna Boca Juniors na River Plate , Italia kuna AC na Inter Milan,Serbia Kuna Red Star na Partizan Belgrade ,na nchini Kenya kuna AFC Leopards na Gor Mahia .
AFC Leopards na Gor Mahia ni timu ambazo zina upinzani wa kifo na uhai. Timu hizi ziliundwa kama timu za makabila miaka ya sitini ambapo AFC Leopards walikuwa wakiwakilisha kabila la Abaluhya na Gor Mahia wakiwakilisha kabila la wajaluo na tangu kuundwa kwake zimeliteka soka la Kenya na katika wakati Fulani soka la Afrika .Timu hizi zilitoka kuwa klabu za makabila na upinzani wake umefikia kuwa upinzani uliotapakaa nchi nzima kiasi kwamba kila timu hizi zinapokutana zinaunda kitu kinachoitwa The Great Kenyan Derby tofauti na hapo awali ambapo mechi hii iliitwa The Western Derby kutokana na eneo la kijiografia ambako timu hizi zilipoanzishwa ambako ni mashariki mwa nchi ya Kenya .


Tangu vilabu hivi vilipoanzishwa hadi leo hii vimeweza kuchangia zaidi ya asilimia 90% ya wanasoka bora nchini Kenya ambapo wengi wao kabla ya kwenda kwingine walianzia kwenye eidha jezi za kijani ambazo ni za Gor Mahia au za michirizi myeupe na bluu ya AFC Leopards au kwa wengine wakicheza pande zote mbili kama vile James Siang’a , Wiolliam Chege Ouma na Dan Shikanda .
Katika miaka iliyopita ambapo timu hizi mbili zilikuwa miamba ya soka nchini Kenya mechi baina ya wapinzani hawa ilikuwa ikiamua ubingwa wa soka nchini Kenya .Kama Mojawapo ingeshinda mara mbili au mara moja na kutoka sare mchezo unaofuata basi ingetangaza ubingwa na hii ni kwa sababu timu hizi zilikuwa ndio hasa zenye uwezo wa kisoka na kifedha kuliko timu zingine kama ilivyo hapa Tanzania kwa Simba na Yanga au Hispania kwa Mdrid na Barca . Kama Gor Wangetwaa ubingwa mwaka huu basi AFC wangetwaa mwakani na huo ndio ulikuwa utaratibu miaka hiyo .
Zinapokutana timu hizi mbili mbinu zote za ushindi hutumika , ndani na nje ya uwanja hupiganwa vita kali ambayo inachagizwa zaidi na ukweli kwamba kila wanapokutana wapinzani hawa ni zaidi ya soka , ni zaidi ya matokeo ya uwanjani kwani watani hawa wajaluo na waluhya wameanzia upinzani wao kwenye kabila na soka ni moja ya maeneo ambayo utani wao unaamuliwa ambapo anajulikana mbabe na mnyonge .Msimu uliopita watu kadhaa walipoteza maisha baada ya kutokea mkanyagano kwenye uwanja wa Nyayo ambako vilabu hivi vilikuwa vikimenyana na hiyo itakuonyesha jinsi mechi baina ya watani hawa inavyowavutia watu nchini nzima .


Pamoja na ukweli kuwa timu hizi ni za wajaluo na waluhya ukweli ni kwamba upinzani hauko tu Mikoa ya nyanza kwa wajaluo na Western au magharibi kwa waluhya bali toka Mombasa hadi Machakos , Nairobi na Nakuru utakuta mashabiki wa Gor Mahia au AFC Leopards . Zamani mchezaji wa kiluhya ambaye angediriki kucheza Gor Mahia angejikuta akitengwa na jamii nzima ya wanakabila wenzie na si ajabu ukikuta mtu huyu akiwa mpweke akiugua au akiuguliwa na hata akifiwa au kwenye sherehe za kimila kwani anahesabika kama msaliti asiye na aibu na vivyop hivyo kwa Mjaluo ambaye angejaribu kuvaa jezi za bluu na nyeupe za AFC .
Afc Leopards ilizaliwa rasmi mwaka 1942 baada ya klabu za daraja la kwanza za watu toka kabila la luhya za Marama , Samia United na Bunyore zilipoamua kuungana na kuunda timu moja .
Moja ya wachezaji maarufu waliowahi kuvaa nyuzi za AFC ni kama Joe Kadenge ambaye ni sawa na Pele kwa Kenya , Jonathan Niva , Joe ‘jj’ Masiga , Wilberforce Mulamba , Mike Amwayi , Mickey Weche, Murila , Nyawanga , Aggrey Lukoye na Peter Lichungu na wengine kama Francis Oduor na nahodha gwiji wa Harambee Stars Musa Otieno.
Kwa upande wa Pili Gor Mahia yenyewe ilianzishwa miaka mine baada ya wapinzani wake AFC mwaka 1968 na kama wenzao kuzaliwa kwake kulikuja baada ya muungano wa timu mbili za watu wa kabila la Luo (wajaluo) Luo Union na Luo Stars . Gor kwa upande wao wametoa mchango mkubwa katika nyota waliowahi kulipaisha jina la Kenya kwenye ramani ya soka . Baadhi ya watu hao ni kama vile Allan Thigo, Sammy Owino Kempes , John Bobby Ogola, Nashio Oluoch Lule, Austin Oduor , David Ochieng Kamoga,John Okelo Zangi, Peter Otieno Bassanga, Ben ‘breakdance’ Oloo, Tobias Ocholla na Sammy Onyango Jogoo pamoja kocha wa sasa Zedekiah Otieno ‘zico’ ambaye ndiye nahodha wa mwisho wa Gor Mahia kubeba ubingwa wa ligi ya Kenya mwaka 1995.
Tangu miaka ya 70mpaka ya 80 Gor na AFC ndio vilbeba soka la Kenya vikibadilishana mataji ya ubingwa wa ligi ya Kenya kama mbio za vijiti huku wakihamishia upinzani huo kwenye ubingwa wa CECAFA japo katika mwaka wa 1987 Gor Mahia waliwazidi wenzao kete kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika katika kombe la Mandela .
Klabu hizi zilipata wakati mgumu kwenye miaka ya tisni ambapo hali ya ugumu wa uchumi iliyoikumba nchi ya Kenya ilishuhudia vilabu hivi vikikumbwa na ukata ambao ulimaliza utawala wao kwenye soka nchini Kenya .Sambamba na ukata vilabu hivi vilimalizwa na upinzani wa kisiasa ambao ulikuwa mkali nchini Kenya huku vilabu hivi vikitumiwa na wapinzani kukiua chama tawala cha KANU .
Huku vilabu hivi vikiwa sawa katika historian a vitu vingine vingi kama vile mapacha kwa pamoja vilijikuta vikishuka daraja kwenye ligi ya Kenya katika vipindi vya miaka 2004 na 2009.
AFC walishuka daraja mwaka 2006 na walicheza ligi daraja la kwanza mwaka 2007 na mwaka 2008 na waliweza kupanda msimu uliofuata .

Timu hizi zinakutana kwenye ligi ya soka nchini Kenya siku ya Jumapili tarehe 24 huku Gor mahia wakiwa na nguvu kulinganisha na wapinzani wao baada ya kuwa na msimu mzuri ambapo walimaliza ligi nyuma ya mabngwa Ulinzi Stars . Gor wanaonekana kuwa vizuri na nje uwanja pia ambapo chini ya uenyekiti wa Ambrose Rachier ambapo msimu huu wameweza kupata mkataba wa udhamini wa jezi zao kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu yao .
AFC Leopards wamekuwa na homa za vipindi huku wakihangaika sana kutafuta gia tangu waliporejea kwenye ligi kuu. Mabadiliko ya kia mara kwenye uongozi yamechangia sana kuiumiza klabu hii ya waluhya . Katika kipindi cha miaka miwili AFC Leopards wamebadilki makocha mara zisizopungua 9 na wenyekiti mara mbili na kwenye mazingira kama haya hakika mafanikio yanakuwa magumu kupatikana .
Pamoja na tofauti hiyo kwenye mafanikio , siku zote vilabu hivi ndio vionalitengeneza soka la Kenya kwa miaka yote na ukitaka kuhakikisha hilo tazama rekodi ya mataji ya ligi kuu ya Kenya na utaona hilo , timu hizi zimetwaa ligi ya Kenya mara 12 kila moja na siku zote zinapokutana kila mmoja antamba kuwa yuko juu ya mwenzie , je hiyo tarehe 24 ni Gor mahia mabao wamekuwa na nyumba tulivu hivi karibuni ambao wataweza kuwapa raha wajaluo au AFC Leopards ambao wamekuwa wakitibuana kila leo ambao wataanza maisha mapya ya mafanikio kwa kuwachapa wapinzani wao , dakika tisini ndio zaitakazoamua.