Search This Blog

Saturday, April 21, 2012

Azam FC katika kilele cha mafanikio, Je kuweka rekodi hapo Jumatatu?


Azam FC Jumatatu tarehe 23 April 2012 itaingia katika historia mpya endapo itafanikiwa kuifunga Mtiwa Sugar. Historia inayotarajiwa na Azam FC kesho ni kushika nafasi ya pili na hivyo kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Afrika. Endapo Azam FC itashinda kesho basi itafikisha pointi 53, idadi ambayo haiwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote ukiondoa Simba ambayo tayari ina pointi 56.
Kutinga kwenye mashindano ya Afrika kunaondoa mazoea ya zaidi ya miaka 10 iliyopita ambapo vilabu vya Simba na Yanga vilikuwa vimetawala mpira wa Tanzania na kufanya nafasi mbili za juu kama mali yao.
Ni kama siasa za chama kimoja vile, mpira wa Tanzania ulikuwa umeshikwa na vilabu vikongwe vya Simba na Yanga kiasi cha kutengeneza mgando wa mawazo kwa mashabiki wengi nchini kuwa haiwezekani na haitakuja kutokea kwa timu nyingine nje ya wababe hao wa kariakoo kuweza kupata nafasi ya kuwakilisha nchi.
Ikumbukwe kuwa kuna wakati huko nyuma vilabu vya Prisons na Mtibwa Sugar vilishika nafasi za juu lakini historia inaonyesha kuwa kulikuwa na migogoro mikubwa Simba au Yanga iliyotoa nafasi kwa vilabu vya Prisons na Mtibwa na kama hali isingekuwa hivyo leo tungekuwa tunasherekea kuondoa zaidi ya miaka 20 ya utawala wa Simba na Yanga.
Mafanikio ya Azam FC yameanzia kuanzishwa kwake mwaka 2006 na hadi kupanda ligi kuu msimu wa 2008. Mafanikio ya timu hii hayawezi kukamilika bila kuwataja watu kama Boniface Pawasa, Stephen Nyenye, Yahaya Tumbo, Shaabani Kisiga, Said Swedi, Iddi Abubakar, Khamis Japhar nk ambao walifanya kazi kubwa huko nyuma chini ya uongozi wa watu kama Katibu mkuu Nassor Idrissa, Selemani Mabehewa na mwenyekiti Abubakar Bakhresa.
Leo picha ya nje ya Azam FC wanaonekana watu wapya lakini viongozi na wachezaji hawa wapya wamerithi misingi mizuri iliyoachwa na viongozi wa mwanzo kama Habib Kondo, Itamar Amorin, Mohammed King, Sylverster Marsh, Naider Dos Santos, Meneja Jeshi, Abubakar Mapwisa, nk.
Kwenye kikosi cha Azam FC kuna nyota kama Luckson Kakolaki, Salum Abubakar na John Bocco ambao walikuwa sehemu ya kuileta timu ligi kuu na mpaka leo ni wachezaji muhimu ndani ya kikosi. Pongezi za dhati kwao. Duniani kote wachezaji kama hawa huthaminiwa sana na ndivyo klabu ya Azam FC inavyofanya kwao.
Azam FC ambayo ni timu pekee kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na kituo cha michezo chenye ubora wa hali ya juu cha Chamazi huku uwekezaji wake ukiendelea kufanyika kwa awamu inategemewa na wengi kutikisa kwenye soka la Afrika kama ilivyo kwa TP Mazembe.
Tayari bodi ya wakurugenzi wa Azam FC wameweka wazi kuwa, dhamira ya kuanzishwa kwa Azam FC ni kuondoa dhana kuwa watanzania hatuwezi na stahili yetu ni jina la “kichwa cha mwenda wazimu”. Uongozi wa Azam FC chini ya mwenyekiti wake umedhamiria kugeuza hali hii na kuifanya Tanzania nchi ya kuogopwa na kuheshimika kwenye soka la Afrika. Kufikia malengo hayo inahitaji muda, kuungwa mkono na wadau na uvumilivu kitu ambacho kimeoneshwa kuwa kinawezekana ndani ya Azam FC.
Kuna mtu mmoja ambaye ametoa mchango mkubwa sana kwenye mafanikio ya Azam  FC msimu huu, huyu ni mwalimu Stewart Hall, mwalimu huyu ni mjuzi sana, anafanya kazi zake kwa uweledi wa hali ya juu ndani na nje ya uwanja, Azam FC inajivunia kuwa na mtu kama yeye. Uwepo wake unatengeneza imani kubwa kwa klabu kutawala soka la Afrika katika kipindi kifupi kijacho.
 Kila la Kweli Azam FC hapo Jumatatu katika safari ya historia mpya.
Source: azamfc.co.tz

Mbeya kushuhudia Ligi kuu kwa mara nyingine

Jiji la Mbeya litashuhudia tena ligi kuu ya vodacom msimu ujao wa 2012/13 baada maafande wa magereza Tanzania Prisons kufanikiwa kurejea ligi kuu hii leo.

Prison leo wamewalaza goli 2-0 timu ya Rhino Ranger ya Tabora katika mchezo wa hatua ya 9 bora ligi daraja la kwanza uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Prisons ilihesabu goli lake la kwanza katika dakika ya 35 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Peter Michael na dakika ya 65 waliandika goli la pili kwa shuti kali lililopigwa na Jeremia Juma na kupelekea mchezo kumalizika kwa Prison kuibuka kidedea kwa goli 2-0.

Kwa matokeo hayo Prison imeitimisha idadi ya timu tatu zitakazo panda ligi kuu ya Vodacom, ambazo ni Mgambo Shooting ya Tanga, Polisi Moro ya Morogoro na Tanzania Prinson.

Katika mchezo mwingine uliochezwa leo kwenye uwanja huo ulio wakutanisha Trans Camp ya Dar es salaam dhidi ya Polisi Tabora na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Source:tp://aboodmsuni.blogspot.com

PICHA

NIPO NA MWALIMU WANGU WA MICHEZO ENZI HIZOOOO! ,Mr Hatia PALE AZANIA SEC SCHOOL.

GIGGS AMESABABISHA PENATI 5 KATIKA MIAKA 20 - ASHLEY YOUNG NDANI YA MISIMU MIWILI ANAZO 9. YOUNG INABIDI AFUATE MFANO WA RONALDO.

Muingereza huyu amefanikiwa kupewa penati nyingi kuliko mchezaji yoyote katika ligi kuu ya England katika kipindi cha misimu miwili iliyopita - pia kwa idadi ya ya penati 9 alizopewa amemfunika Ryan Giggs ambaye katika miaka 20 aliyocheza soka amefanikiwa kusababisha penati 5 tu.

Wakati wa mkutano wa waandishi wa habari jana Ijumaa, Sir Alex Ferguson alitoa ofa ya takwimu ambayo wengi hatukuwa tunaijua: Ryan Giggs amefanikiwa kupia United penati 5 tu tangu aanze kuichezea klabu hiyo miaka 20 iliyopita.

Ukiangalia namna winga huyo alivyokuwa na kasi na uwezo wa kuuchezea mpira tena huku akiwa na mbinu nyingi za kuwatoka mabeki , bila kusahau namna timu nzima ya United isivyochoka kupeleka mashambulizi katika goli la wapinzani - unaweza ukaanza kujiuliza labda Giggs hakuwa akichezewa sana faulo katika eneo la penati.

Lakini Ferguson alisema veteran Giggs anajua sana ku-ubalance mwili wake, kwa makusudi au vinginevyo kuonyesha utofauti kati ya Giggs na winga mpya wa United, Ashley Young.

Young lazima atakuwa mwangwi wa malalamiko dhidi yake baada ya kulalamikiwa kwenda chini kirahisi sana katika wikiendi mbili mfululizo - dhidi ya QPR na baadae dhidi ya Aston Villa - na kuwasaidia viongozi wa ligi kupata penati muhimu.

Katika mtandao wa Twiiter watu tofauti wamekuwa wakimfananisha na Olympic diver Tom Daley, wakati Young pia amekuwa akionywa na legend wa United Bryan Robson kwamba anajitengenezea sifa mbaya ambayo hahitajiki na amabyo inaweza ikaigharimu klabu yake maamuzi makubwa katika mechi tano za mwisho za msimu.

Alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo mwanye miaka 26, Ferguson alikiri kwamba: "Nimeongea na Ashley", na kwa hakika sijamwambia maneno ya "Endelea vizuri mwanangu."

Huku bosi huyo wa United akiendeleza utamaduni wa kuweka maongezi ya ndani ya klabu siri, Jarida lenye nguvu la msahabiki wa United, Fanzine Red Issue lilimshambulia winga huyo na kumuita "mjirushaji anaetia aibu". Pia jarida hilo lilikariri maneno ya legend boss wa United Matt Busby likisema: "Kama kuna kitu chochote kinapatikana kutoka kwenye soka, basi inabidi kipatikane kwa kushinda au kutoshinda na heshima."

Young kwa hakika itabidi ajirekebishe baada ya manager wake na mashabiki wa klabu yake kujitokeza kukemea na kumshawishi aache tabia yake, ambayo imetafsiriwa kama kitendo cha aibu kabisa.

Tangu kuanza kwa msimu wa 2010-11, Young tayari ameshapata penati 9, mara mbili zaidi ya mchezaji yoyote katika Premier league na 4  zaidi ya alizopata Giggs katika maisha yake yote pale OT.






THE YOUNG ONE
 YOUNG'S DEBUT SEASON SO FAR
GAMES PLAYED
AS SUBSTITUTE
GOALS
ASSISTS
26
5
7
8


Makocha wa timu pinzani lazima sasa watakuwa wanachukua hatua muhimu na kuwaonya mabeki wao wachukue tahadhari kubwa dhidi ya mchezaji huyo ambaye hana tatizo la kujirusha na kwenda chini kirahisi pale anapohisi ameguswa japo kidogo.

Lakini kama historia inaweza ikafanya kitu, then Young atajifunza. Tena kwa haraka sana kwamba kujirusha hakukubariki Old Trafford.

Wote Cristiano Ronaldo na Nani, waliotolewa Ureno, walikuwa na tabia ya kujirusha  mwanzoni mwa carrer zao pale OT na kwa haraka zaidi walifanikiwa kupewa jina la wadanganyifu.

Lakini haikuwachukua muda mrefu kwa wili hao kugundua kwamba kujirusha hakukuwa kunakubalika katika ligi kuu ya England, hasa Ronaldo.

Mreno huyo baada ya kupewa lecture na Ferguson, aliacha tabia ya kujirusha, na kuanza kukaza, kupambana na changamoto za kimchezo, na kuwa mchezaji aliyekamilika zaidi. Aligundua kwambani bora badala ya kujidodondosha, angeweza kujikaza nakwenda mbele kufunga na kutenengeneza magoli.

Young inabidi afuate  mfano wa Ronaldo, kuhakikisha anakumbukwa kwa soka lake na sio matukio yake ya utata, ambayo yanaishia kuharibu msimju wake wa kwanza na United.
                                                                                                                                                                                                                                          

MKUTANO MKUU WA TFF WAFUNGULIWA RASMI HII LEO JIJINI DAR ES SALAMM.

   Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Rais wa TFF Leodegar Tenga akiwahutubia wajumbe leo hii
MGENI WA HESHMA NAIBU MKURUGENZI WA MICHEZO Bi m. YASODA

UCHAWI AKA MISUMARI HAUPO TU KWENYE SOKA BONGO - BALI MPAKA KWENYE MASUMBWI - CHEKA , MATUMLA NA WENGINEO WAFUNGUKA.



Mbabe wa wababe katika ngumi za kulipwa Tanzania, Francis Cheka

LIMEKUWA ni jambo la kawaida kwa wanamichezo kuhusishwa na imani za ushirikina, ambazo zimezoeleka hasa katika mchezo wa soka, na zimeonekana kushamiri kwenye klabu, mchezaji mmoja mmoja na hata timu za taifa.
Hali hiyo haiko katika soka peke yake, kwani hata kwenye masumbwi imani hizo za ushirikina zimeshamiri huku mabondia, hasa wa ngumi za kulipwa, wakibainisha kwamba kurogana kupo katika mchezo huo.
Huenda wangekuwa wakilipwa baada ya pambano tungesema wanafanya hivyo kwa ajili ya maslahi, lakini mabondia hawa hupewa chao mapema hata kabla ya kupanda ulingoni ili wakikung'utwa wajihudumie vizuri. Lakini, je, ni kwanini hali hiyo inajitokeza.
Francis SMG Cheka
"Ushirikina upo, mimi mwenyewe niliwahi kurogwa mwaka 2009 katika pambano lililofanyika jijini Dar es Salaam na bondia (alimtaja), katika pambano hilo mpinzani wangu alimwaga madawa 'live', lakini nashukuru niliweza kustahimili na kucheza licha ya kwamba mashabiki wake walianzisha fujo baadaye na kuvunja pambano," alisema.
Cheka, anayeshikilia usukani wa ubora Tanzania, alisema mtu anayefanyiwa ushirikina kama alivyofanyiwa hujisikia mzito ulingoni na pumzi kukata.
Hata hivyo, anasema 'mchawi wake' alishindwa baada ya yeye Cheka kufika raundi ya sita ya pambano hilo kwa sababu 'alikuwa fiti'.
Rashid Matumla Snake Boy
"Hizo ni imani tu na mambo ya Kiswahili, kama mtu una mazoezi lazima utashinda na kama huna mazoezi usitarajie kushinda," alisema bondia huyo namba tano kwa ubora Tanzania.
Matumla alisema yeye binafsi hajawahi kupigwa misumari licha ya kwamba amekuwa akisikia mabondia wakizungumzia hali hiyo ingawa haamini kama vitu hivyo vipo.
Karama Nyilawila
Karama, ambaye aliwahi kuvuliwa ubingwa wa Shirikisho la Ndondi za kulipwa la Dunia (WBF), anasema anapocheza huwa haelewi kama amepigwa misumari ama la.
"Huwa nacheza tu lakini sielewi kama wanapiga misumari ama vipi kwa kuwa sijui mtu aliyefanyiwa hivyo anakuwaje, huenda nikawa napigwa misumari bila kujijua," alisema bondia huyo anayezichapa katika uzani wa Middle.
Ashraf Suleiman
Huyu ni bondia mbishi pengine kuliko wote Visiwani Zanzibar, ubishi wake ulianzia pale alipompiga Awadh Tamim na kuwa bingwa wa Afrika Mashariki na Kati na kucheza naye pambano la kutetea mkanda huo.
Katika pambano hilo lililofanyika mwaka 2010, Suleiman alicheza vizuri raundi nne za mwanzo licha ya kwamba upepo ulimbadilikia na kupigwa kwa KO katika raundi ya saba huku mashabiki wake wakidai alirogwa na mpinzani wake.
"Kila mmoja ana imani yake, kuna anayemwamini Mwenyezi Mungu na yule anayeamini ushirikina. hata hivyo, sielewi kama wenzangu wanakwenda kwa 'Karumanzira' ili washinde," alisema bondia huyo.
Mada Maugo
Sifa kubwa ya bondia huyo ulingoni ni kucheza na mashabiki na mara nyingi amekuwa akitoka mchezoni akizongwa na kuzomewa na mashabiki hali inayomlazimu kucheza kwa hasira pasipo mipango, hivyo kutos mwanya kwa wapinzani wake kumshambulia kirahisi.
Maugo anasema; "Sisi wenye dini hatuna mambo hayo, ukifanya hayo ina maana hutapigana vizuri, lakini ukifanya mazoezi na kumwamini Mwenyezi Mungu kwa hakika utafanya vizuri."
Maugo anasema hajawahi kupigwa misumari na mabondia wenzake, lakini akasema kwamba kushindwa kwake kunatokana na majaji kwa kumbania huku akisisitiza ishara hizo za majaji ni dalili pia za kupigana misumari.
Maneno Oswald 'Mtambo wa Gongo'
Mbali na Matumla, bondia huyo ndiye mkongwe anayeendelea kupanda ulingoni, enzi zake alikuwa akipanda ulingoni mashabiki wake wakijua tayari mbabe wao ameshinda.
Je, hali hii ilikuwa inahusiana na mambo ya ushirikina? Anajitetea kwamba hajawahi kufanya hivyo na wala haamini kama mambo hayo yapo.
"Ingekuwa mtu anajua atapiga misumari ili ashinde kusingekuwa na haja ya kufanya mazoezi kwa kuwa anajua tayari ameroga, lakini tunafanya mazoezi ili kuhimili ushindani, hakuna mambo hayo," alisema.
Japhet Kaseba
Bondia huyo aliwahi kutangaza kustaafu masumbwi kabla ya kurejea na kupigwa na Mada Maugo ingawa sasa amejikita zaidi kwenye mchezo wa ngumi na mateke (kick boxing).
Kaseba anasema kupigana misumari kunafanyika na si kwenye ngumi tu, hata katika michezo na mambo mengine ya kisiasa na kijamii.
Hata hivyo, anaeleza kwamba mambo hayo yanafanywa na wale wanaoyaamini.
"Mambo haya pamoja na kufanywa, lakini hayasaidii, kwani anayetendewa kama haamini imani hizo za kishirikina hawezi kudhurika," alisema.
Kaseba alisema yeye binafsi hafanyi mambo kama hayo ulingoni na mara zote anapopanda ulingoni humtanguliza Mwenyezi Mungu huku akiamini mazoezi ndiyo mchawi tosha wa mafanikio ulingoni.

BARCELONA VS REAL MADRID: MATUKIO MUHIMU KATIKA HISTORIA YA EL CLASICO

Muda umekaribia tena kwa mara nyingine! El classico nyingine hii hapa ndani ya wikiendi hii.

Mtanange mkali kati ya Barcelona na Real Madrid siku zote umekuwa ukileta hisia tofauti na raha kwa mashabiki wa soka ulimwenguni, matukio ya kutatanisha na ya kukumbukwa zaidi. Kesho Jumamosi pale Nou Campkutaweka moto mkubwa sana, pamoja tu na hali ya upinzani kati ya timu hizi mbili lakini mchezo huu unaongezewa utamu kwa kuwa unaweza ukaamua nani awe bingwa wa La Liga.

Wamekutana karibia mara 200 na ndani ya kipindi cha miaka 100, kila kitu kutoka katika mpambano kimekuwa kikotoa matukio ya ushindani wa hali juu pindi vigogo hawa wawili wanapokutana.

Ebu leo tujikumbushe baadhi ya matukio mengi ya kukumbukwa katika El Classico.


KURUDI KWA ABIDAL BAADA YA OPERATION

Eric Abidal, ambaye ka sasa anaendelea kujiuguza baada ya kufanyiwa ubadilishwaji wa ini, mwezi Machi 2011 alifanyiwa upasuaji wa ini. Alirudi uwanjani na kucheza mechi yake ya kwanza baada ya operesheni katika mechi dhidi ya Real Madrid katika champions league  semi final.


KUSHANGILIWA KWA RONALDINHO @BERNABEU

Baada ya kuwatesa Real Madrid katika mechi ambayo Barca waliwafunga wapinzani goli 3-0, wakati mbrazili huyo alipofunga mabo mawili katika uwanja wa Bernabeu mjini Madrid - Na mechi ilipoisha akiwa mashabiki wote uwanja mzima waliinuka kumshangilia.


GOLI LA KWANZA LA CRISTIANO RONALDO DHIDI YA BARCA

Baada ya kucheza mara sita dhidi ya Barca, na kufeli kuwafunga, Cristiano Ronaldo hatimaye alifanikiwa kuwafunga Barcelona kwa mara ya kwanza mwezi wa April 16, 2011 katika suluhu ya 1-1 katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Tangu wakati huo mpaka leo tayari ameshawafunga Barca mabao manne likiwemo la ushindi katika mechi ya fainali ya kombe la mfalme.   



USHINDI WA 11-1

 Ushindi mkubwa zaid kuwahi kutokea katika  El Classico, ulikuwa ushindi wa 11-1 wa Real Madrid dhidi ya Barca katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya pili ya Copa del Deneralisimo ambalo la sasa linaitwa Copa del Rey mwaka 1943. Real walifungwa na Barca 3-0 katika ngwe ya kwanza.


USAJILI WA KWANZA WA KUTOKA BARCA KWENDA MADRID

Mwezi May 1902, Alfonso Albeniz alikuwa mchezaji wa kwanza kuweka rekodi ya kuhama kutoka Barcelona na kujiunga na Madrid. Luciano Lizarraga nae alikuwa mchezaji wa kwanza kuondoka Madrid kwenda Barca. in 1905.


REKODI YA UFUNGAJI WA MAGOLI

Huku wakiwa wameshafunga mabao 107 katika La Liga msimu huu msimu huu, Madrid wanahitaji goli moja tu kuweka rekodi ya klabu na ligi kwa kufunga magoli mengi katika msimu mmoja. Barcelona wenyewe wana rekodi ya kufunga mabao 105, kwa sasa wameshafunga mabao 96. Huku pia Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wameshaweka rekodi zao binafsi ya kufunga mabao mengi katika La Liga wikiendi iliyopita walipoweza kufunga magoli 41 msimu huu.


MADRID WANAONGOZA KWA KUIFUNGA BARCA

Barcelona na Madrid wameshakutana mara 217 katika mashindano yote. Madrid kwa sasa ndio wanaoongoza kwa kuwafunga wapinzani wao wakiwa wameshinda mechi 86, wakati Barca wakiwa wameshinda 85. Katika La liga pekee Los Blancos wameshinda 68 wakati Catalans wameshinda 64.H | Head-To-Head advantage to RealH | Head-To-Head advantage to Real

JOHAN CRUYFF NA DRAM TEAM YAKE
Johan Cruyff akiwa na kikosi chake maarufu cha Dream Team aliweza kuwafunga Real Madrid goli 5-0. In 1973 akiwa mchezaji , aliisadia Barca kuifunga 5-0 Real @Santiago Bernebau, na baadae akiwa kocha wa The Dream Team ya Barca aliiongoza La Blaugurana kuwafunga tena Madrid  5-0 pale Nou Camp, lakini nae akapokea kipigo cha idadi hiyo hiyo mwaka 1995 mjini Madrid.


GOLI LA MAPEMA ZAIDI YA BENZEMA.

Katika mechi ya mwisho ya wapinzani hawa mwezi December 10, 2011, Karim Benzema alifunga goli la mapema zaidi katika historia ya El Clasico alipofunga goli sekunde ya 22 ya mchezo.


MICHEAL LAUDRUP NA REKODI ZAKE

Michael Laudrup sio tu kwamba aliwahi kuizchezea timu hizi mbili zote lakini pia alihusika na kuwa katika ushindi wa 5-0 kwa timu zote mbili. Aliwasaidia Barca kuwafunga Madrid kwa idadi hiyo mwaka 1994, lakini msimu uliofuata akiwa upande wa Madrid. Pia ndiye mchezaji pekee kuweza kushinda makombe matano ya la liga kwa mfululizo akiwa na klabu mbili tofauti.


MESSI NA REKODI YA CESAR RODRIGUEZ

Lionel Messi hivi karibuni alivunja rekodi ya Cesar Rodriguez iliyokaa muda mrefu kama mfungaji bora wa muda wote wa katika historia ya Barcelona, katika mechi rasmi, lakini bado anaikimbiza rekodi nyingine ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi katika El Clasico, Rodriguez alifunga mabao 14 dhidi ya Madrid - 12 kwenye La Liga na mawili katika Copa del Rey, wakati Messi ameshafunga 13 - nane katika La liga, matatu katika Spanish Supercopa na mawili katika Champions league.

SARE TASA

Katika mechi 217, ni mechi nane tu ambazo ziliisha kwa sare tasa ya 0-0. Mechi hizi zote ni la liga. Na ilikuwa mwaka 1973 ambapo kulikuwa na mechi za mfululizo zilizoisha kwa sare tasa.



KICHWA CHA NGURUWE

Ingawa wachezaji 26 walishatoka klabu moja na kwenda nyingine kati ya Barca na Madrid, lakini uhamisho wa Figo kwenda Madrid kutoka Barca ulileta utata mkubwa. Aliporudi Nou Camp kwa mara ya kwanza in 2002, mreno huyo alitupiwa kila aina ya kitu kilichokuwepo karibu na mashabiki - kikiwemo kichwa cha Nguruwe huku akiitwa Judas.

KUTOLEWA KATIKA MICHUANO YA ULAYA

Barcelona ndio ilikuwa timu ya kwanza kuitoa Madrid katika kombe la ulaya pindi Wakatalunya walipomaliza utawala wa miaka mitano wa Madrid kama Mabingwa wa ulaya kutoka 1961-61 kwa kuwafunga Real katika raundi ya kwanza na kuwatoa kwa idadi ya 4-3.


REKODI YA RAUL DHIDI YA BARCA

Raul ni mfungaji namba mbili katika listi ya wafungaji bora wa Clasico nyuma ya Di Stefanoakiwa amefunga mabao 15 - 11 kwenye La Liga, 3 mkatika Spanish supercopa na moja katika UCL. Cesar Rodriguez, Gento, na Ferenc Puskas wote wana mabao 14.


MOURINHO VS GUARDIOLA


Rekodi ya Jose Mourinho (akiwa na Inter, Chelsea na Madrid dhidi ya Barca inaonyesha ameshinda mechi nne, droo 7 na vipigo 9, huku timu zake zikgunga mabao 24 na kufungwa mabao 34. Pep Guardiola rekodiyake dhidi ya Real, inayonyesha ameshinda mara 9, droo nne na kufungwa moja.



VALDES VS CASILLAS

Barcelona keeper Victor Valdes ameshinda tuzo ya Zamora mara nne, na sasa yupo nyuma kwa kwa ushindi mmoja kuifikia rekodi ya Antoni Ramallets. Iker Casillas ameshinda tuzo hiyo mara moja tu. Mbele ya mchezo wa kesho - Valdes tayari ameshafungwa mabao 23 katika mechi 32, wakati Casilas amefungwa mabao 29 katika mechi 33.


MADRID NA UKAME WA KUIFUNGA BARCA KWENYE LA LIGA


Madrid hawajafanikiwa kuwafunga Barcelona katika La Liga katika mechi 14 ndani ya dakika 90.


XAVI MFALME WA ASSISTS

Barcelona playmaker Xavi ameshacheza Classico 30, akifunga mabao 4 na akitoa assists nane japokuwa katika hizo pasi za mwisho 8, nne kati hizo alizitoa katika mchezo waliofungwa Madrid 6-2 katika uwanja wa Bernebau in May 2009.


ZIDANE ZINEDINE


Kuafuatiwa na usajili wake uliovunja rekodi ya dunai baada ya Madrid kulipa €75 million kwa Juventus IN 2001. Zinedine Zidane alifunga katika mechi zake zote mbili za kwanza katika uwanja wa Santiago Bernebeu.

Friday, April 20, 2012

TAARIFA KUTOKA TFF

Release No. 061
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 20, 2012

KOCHA NGORONGORO HEROES AAHIDI USHINDI
Kocha Kim Poulsen anayeinoa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 cha Tanzania (Ngorongoro Heroes) ameahidi kikosi chake kufanya vizuri kwenye mechi dhidi ya Sudan.

Akizungumza jana (Aprili 20 mwaka huu) kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, Poulsen amesema timu yake imejiandaa vizuri kwa mechi hiyo na kiu yao ni kushinda.

Kwa upande wake Kocha wa Sudan, Azhari Osman El Tahir amesema ingawa haifahamu vizuri timu ya Tanzania, lakini wamejiandaa kushinda kwani kwa muda mrefu walikuwa hawajashiriki mashindano ya vijana ya kimataifa.

Mechi hiyo ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri huo itachezwa kesho (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000.

Sudan iliwasili nchini jana (Aprili 19 mwaka huu) ikiwa na kikosi cha wachezaji 20, viongozi kumi na mwandishi wa habari mmoja kwa ajili ya mechi hiyo ya kwanza kabla ya timu hizo kurudiana jijini Khartoum kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.

Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Brian Miiro atakayesaidiwa na Mark Ssonko, Lee Patabali na Denis Batte wote kutoka Uganda. Ejigu Ashenafi wa Ethiopia ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo namba 15.

Fainali za Afrika kwa michuano hiyo zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria wakati za Dunia zitafanyika nchini Uturuki kuanzia Juni hadi Julai mwakani. Katika fainali za Dunia, Afrika itawakilishwa na timu nne za kwanza kwenye fainali za Algeria.


MALINZI MGENI RASMI MKUTANO MKUU TFF
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika kwa siku mbili (Aprili 21 na 22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa mkutano huo watawasili jijini kesho (Aprili 20 mwaka huu) na watafikia kwenye hoteli ya Royal Valentino. Wajumbe wanatoka katika vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.

Mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi utakuwa na ajenda kumi na moja. Baadhi ya ajenda hizo ni hotuba ya Rais wa TFF, taarifa ya utendaji ya mwaka 2011, bajeti ya mwaka 2012 na taarifa ya ukaguzi wa hesabu (audited accounts).

MECHI ZA VPL WIKIENDI HII, MAREKEBISHO
Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya 24 wikiendi hii kwa mechi mbili zitakazochezwa Aprili 22 jijini Dar es Salaam. Villa Squad itaumana na African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Yanga itakuwa mwenyeji wa Polisi Dodoma katika Uwanja wa Taifa.

Azam na Mtibwa Sugar zilizokuwa zicheze Aprili 21 mwaka huu sasa zitacheza Aprili 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati siku hiyo hiyo jioni kutakuwa na mechi kati ya Simba na Moro United. Mechi zote zitaanza saa 10.30 jioni.

Aprili 25 mwaka huu Oljoro JKT itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Raundi ya 25 itakamilika kwa mechi nne; Aprili 28 mwaka huu Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi. Azam na Toto African zitacheza Chamazi, Aprili 30 mwaka huu wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.

Ligi hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi), Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro), Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).

WASWAZI KUCHEZESHA SIMBA, AL AHLY SHANDY
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Swaziland kuchezesha mechi ya kwanza ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Aprili 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao wa mechi hiyo namba 71 ni Nhleko Simanga Pritchard atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Mbingo Petros Mzikayifani na Sibandze Thulani. Mwamuzi wa mezani atakuwa Fakudze Mbongiseni Elliot.

CAF pia imemteua Kayijuga Gaspard wa Rwanda kuwa Kamishna wa mechi hiyo.

KAMPUNI NNE ZAPITA TENDA YA TIKETI
Kampuni nne kati ya sita zimepita hatua ya kwanza ya mchakato wa kupata moja itakayofanya kazi ya kutengeneza tiketi za elektroniki kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na nyingine zinazosimamiwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Shughuli ya ufunguzi wa maombi ya hatua ya awali ya kuonesha nia (Expression of Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ilifanywa jana (Aprili 19 mwaka huu) na Kamati ya Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi ya Tenda ya shirikisho.

Kampuni ambazo zimepita hatua hiyo ya kwanza sasa zinatakiwa kuwasilisha rasmi tenda zao kwa ajili ya shughuli hiyo ndani ya kipindi cha wiki tatu tangu ulipofanyika ufunguzi wa hatua ya kwanza.

Baadaye Bodi ya Tenda itakutana tena kupitia tenda zitakazokuwa zimewasilishwa na kufanya uteuzi wa kampuni moja itakayofanya kazi hiyo.

Kampuni ambazo zimefanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya pili ni CRDB Bank PLC, SKIDATA People Access Inc., Prime Time Promotions na Punchlines (T) Limited.

Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


SABABU ZA BARCELONA KUSHUKA KIWANGO

Kila nabii ana nyakati yake , nyakati ambazo huanza taratibu na baada ya muda uwe mrefu au mfupi nyakati hizi hufikia mwisho . Vivyo hivyo kila falme hakika ina zama zake m zama ambazo zina mwanzo na mwisho . Kwenye soka kumekuwa na falme mbalimbali ambazo huwekwa na timu tofauti kwa nyakati tofauti.

 Wakati soka la ushindani kwa maana ya soka la kimataifa lilipoanza mwishoni mwa miaka ya 20 timu ya taifa ya Uruguay ndio ilikuwa baba wa soka ulimwenguni, Uruguay mpaka kufikia mwaka ambao kombe la dunia lilichezwa kwa mara ya kwanza likuwa imeshatwaa ubingwa wa michuano ya olimpiki mara mbili na waliendeleza  ubabe wao mwaka wa kombe la dunia ambapo walitwaa ubingwa wa kwanza wa kombe la dunia.

 Baada ya hapo Italia waliingia kwa muda mfupi ambapo walitwaa kombe la dunia mara mbili katika miaka ya 1934 na 38 . Kwenye miaka ya 50 Uruguay walirudi kwa muda kabla ya kuwapisha wababe wapya Brazil ambao walitawala kipindi cha kati ya miaka 1958 mpaka 1970.

 Katika miaka yote hiyo timu zimekuja na kundoka na kuja na kuondoka tena lakini hakuna hata moja ambayo ufalme wake ulidumu milele.
Kwa upande wa vilabu Real Madrid waliatawala sana miaka ya kuanzia 1955 mpaka 70 kabla ya timu nyingine kama Ajax , Liverpool, Bayern Munich na Ac Milan mpaka kufikia kati ya muongo wa 1990 .

Katika miaka ya 2000 hakuna klabu ambayo imetawala mchezo wa soka barani ulaya kama Fc Barcelona . Hata kabla ya uji wa Pep Guardiola Barca walikuwa wanatisha wakiwa na safu ya hatari ya kiungo na ushambuliaji ambayo ilikuwa na watu kama Ronaldinho Gaucho ,Samuel Etoo ,Thierry Henry, Deco , Henrik Larson, na wengineo wengi . Kizazi hicho kilipita kikaja kizazi cha kina Lionel Messi , Sergio Busquets , Pedro Rodriguez, Gerard Pique ambao waliungana na wakongwe waliokuwepo tangu wakati wa Rijkaard kina Carles Puyol , Xavi Hernandez na Andres Iniesta pamoja na baadhi ya wachezaji walionunuliwa kama Eric Abidal , Seydou Keita na wengine .
Katika vipindi vyote hivi Barcelona imetawala bila kupingwa huku ikitwaa ubingwa wa Ulaya mara tatu tangu mwaka 2006 na mataji manne ya ligi ya nyumbani.

 Hata hivyo alipokuja Pep Guardiola ndio Barcelona inaonekana kushika kasi kuliko hata hapo awali. Chini ya Pep Barca imetwaa mataji 13 kati ya 16 ambayo imeshiriki huku Lionel Messi akiibuka kama mchezaji bora pasipo kipingamizi chochote .
Hata hivyo utawala huu wa Barcelona hatimaye unaonyesha dalili mbaya za kuanza kufifia taratibu.

 Hii si kusema kuwa Barcelona wameshuka kufikia kiwango kibaya kama ilivyokuwa kwa timu kama Ac na Inter Milan au hata Man United ambayo msimu huu umekuwa mbaya sana kwake hasa kwenye michuano ya ulaya.

 Pamoja na hayo Barcelona msimu huu hawajarejea kwenye kiwango cha kutwaa mataji yote inayoshiriki kama msimu uliopita na hata misimu miwili mitatu nyuma.
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaonekana kutishia ufalme wa Barcelona .
Ukiangalia Barcelona ya sasa bado ina watu muhimu kama Xavi, Iniesta, Messi na Puyol.

 Hata hivyo tofauti iliyoko sasa na Barcelona ile ya mwaka 2009 ambayo iliilaza Man United maba mawili bila pale Rome utagundua jambo moja kubwa . Barcelona ya sasa inamtegemea sana Lionel Messi tofauti na miaka mitatu iliyopita . Inawezekana kuwa Messi kwa sasa amekuwa kiuchezaji tofauti na hapo awali lakini ukweli unabaki kuwa Barca inamtegemea sana kijana huyu toka Rosario Argentina.

Hadi kufikia mwisho wa msimu wa mwaka 2008-2009 Fc Barcelona ilitwaa ubingwa wa La Liga huku ikiwa na uwiano wa ufungaji wa mabao mzuri ambao ulikuwa umesambaa kwa wachezaji watatu. 

Samuel Etoo alikuwa na mabao 31, Leo Messi alikuwa na mabao 23 na Thierry Henry alikuwa na mabao 19 , hii ilitengeneza jumla ya mabao 74. Wingi wa mabao ya jumla sio hoja kuu ila jinsi mabao haya yalivyosambaa kwa wachezaji wengi na sio mmoja.

 Ukiangalia takwimu za ufungaji zinavyoonyesha msimu huu utaona Leo Messi ana mabao 41, Xavi Hernandez na Alexis Sanchez wakiwa na mabao 10 kila mmoja . Tofauti ya mabao ya jumla kwa mara nyingine sio hoja kwani ukiangalia jumla ya mabao ni 70 huku tofauti ikiwa ndogo tu ya mabao manne.

 Hata hivyo tofauti kubwa ambayo inaogopesha hapa ni ukweli kwamba Messi peke yake ana mabao 41 na anayefuatia ana mabao 10. Ishara inayopatikana hapa ni kwamba Barcelona si lolote s chochote bila Messi. Rudi nyuma kwenye mwaka huo huo wa 2009 halafu angalia hali ilivyokuwa kwa mahasimu wa Barca Real. Takwimu zao zilinyesha kuwa mfungaji bora alikuwa Gonzalo Higuein akiwa na mabao 22 akifuatiwa na Raul Gonzalez akiwa na mabao 18. Baada ya hapo angalia takwimu za Real mwaka huu Cristiano Ronaldo ana mabao 41 , Gonzalo Higuein ana 22 na Karim Benzema ana 18 . Kwa mara nyingine tena jumla ya mabao si issue kubwa ila mgawanyo wa mabao kwa maana ya kwamba Real hawana tatizo lililoko Barcelona la kuwa tegemezi sana kwa Messi.

Hili si tatizo ambalo linaikuba Barca kwenye La Liga peke yake bali hata kwenye Ligi ya mabingwa . Msimu ambao Barca ilitwaa ubingwa kwa kuifunga Man United mabao mawili kule Rome Messi alikuwa na na mabao 9, Henry mabao matano na Etoo Manne. Msimu huu Messi ana mabao 14 huku anayefuatia akiwa pedro mwenye mabao manne . Kwa upande wa Real kwa mara nyingine mabao yamegawanyika kwa wachezaji wengi , Ronaldo ana nane , Benzema ana saba , Jose Callejon ana mabao matano , Kaka na Higuein wana matatu kila mmoja. Picha unayoipata hapa ni kwamba Bila Messi Barcelona sio Barcelona lakini kwa Madrid bila Ronaldo Benzema atafunga na Higuein atafunga.

 Haimaanishi kuwa Barca hawana watu wa kufunga ila mabao yanayofungwa na wachezaji wengine ni machache sana kiasi cha kuifanya timu kuwa tofauti.
Ukweli wa hoja hii unapatikana kwenye mchezo wa jumatano kati ya Chelsea  na Barcelona . Kila ambapo Lionel Messi aligusa mpira angezungukwa na wachezaji wawili watatu, matokeo yake yalikuwa Barcelona kufungwa.

 Japo waligongesha sana miamba lakini takwimu zinaonyesha kuwa mabao yanayofungwa na wengine hayatoshi na juu ya yote Messi ndio chief goalscorer jambo ambalo hata wachezaji wengine wa Barcelona wanaonekana wamelizoea.

Sababu ya pili kubwa ya ufalme wa Barca kufikia ukomo muda si mrefu ni ya kipuuzi sana lakini ina kila chembe chembe ya ukweli ndani yake . Mafanikio makubwa ambayo Barca imeyapata ndio sababu kuu ya waokushindwa kupata mafanikio mengine zaidi . Katika hali ya kawaida ni rahisi sana kupanda ngazi za mafanikio , lakini ni kazi ngumu sana kuendelea kubaki kwenye kilele cha mafanikio hasa pale ambapo mafanikio haya yamekuwa yakija kwa staili kama ambayo Barca ya Guardiola imepata mafanikio yake.


Mataji 13 kwenye mashindano 16 ambayo Barca imeshiriki kwa kipindi cha miaka yake mitatu ni mafanikio makubwa  sana kwa kipindi kidogo na kiukweli ni vigumu sana kwa wachezaji wa Barcelona kwa ujumla kupata sababu ya kutafuta nguvu ya ziada ya kuendelea kufanya vizuri baada ya mafanikio ya muda mfupi, hili ni jambo ambalo hata Pep Guardiola mwenyewe amekiri .

Wakati Barcelona inatwaa ubingwa wa Champions League mwaka 2009 Kazi kubwa sana ilikuwa imefanywa na Samuel Etoo japo messi alimaliza kama mfungaji bora wa michuano hiyo lakini Etoo ndiye alikuwa mfungaji bora wa michuano yote hivyo Lionel Messi ambaye ndio kwanza alikuwa anachipukia alikuwa na sababu ya kufanya vyema zaidi baada ya hapo kutokana na kuhisi kuwa mafanikio ambayo Barca iliyapata hayakuwa na mhuri wake kama mchezaji mwenye mchango mkubwa na ndio maana baada ya hapo Messi alifanya kazi kubwa ya kufika hapa alipo.

 Tofauti iliyopo sasa ni kwamba wachezaji kama Alexis Sanchez na Cesc Fabregas ambao wako kwenye msimu wao wa kwanza wana wakati mgumu sana kufanya yale aliyofanya Messi na hapo ndio unapokuja ukweli wa hoja hii ya kutafuta mafanikio ya kwako kama mchezaji badala ya yale ya timu.

Na zaidi ya hayo njia ya mafanikio ni kama mlima, wakati wewe unapanda unapishana na watu wanaoshuka na wakati utafika ambapo na ewe utashuka huku ukipishana na watu wanaopanda na kwa jinsi Barcelona walivyopata mafanikio yake kuna timu nyingine zitajipanga na kuwa bora kwa nyakati todauti na hii itamaanisha kutoa ushindani mkubwa sana kwa Barcelona jambo ambalo ukiunganisha na sababu nyingine zilizotajwa hakika zitachangia kushuka kwa ufalme wa Barcelona.

 Mfano wa hili ni jinsi Real Madrid walivyowapa upinzani mkubwa Barcelona kwenye La liga na hata kwenye ligi ya mabingwa . Tegemea hili kwenye michuano ya ulaya ambako timu kama Bayern Munich, Manchester United,Ac Milan zote zitawatazama Barcelona na kujipanga.

Mwisho wa siku haya yote yanaweza yakawa imani tu au propaganda dhidi ya Barcelona ambayo kiukweli inabakia kuwa timu bora ya kizazi hiki lakini ubora huu utafikia ukomo wake. Na ukomo huu umeanza kuonyesha ishara zake .

IDDI AZAN AMUUMBUA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO


MBUNGE wa Kinondoni, Iddi Azan, (CCM), amemuumbua Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, kutokana na kutoa taarifa za kupotosha bungeni kuhusu timu zilizoshinda katika Kombe la Chalenji na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.
Akitoa taarifa bungeni jana, mbunge huyo alisema, si kweli kwamba timu ya taifa, ilitwaa kombe hilo mara tano na timu za Simba na Yanga, zilishinda Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mara moja kwa kila timu.
Azan alisema usahihi ni kwamba, Simba ilishinda kombe hilo mara sita na Yanga mara tano, huku timu ya taifa ilishinda mara tatu Kombe la Chalenji, mwaka 1974, 1994 na mwaka 2011.
“Nimesikitishwa na majibu yaliyotolewa na serikali kuhusu matokeo ya michuano hiyo. Naomba kutoa taarifa Naibu Spika,” alisema Azan.
Katika swali la msingi la Mbunge wa Ziwani, Ahmed Ngwali, aliyetaka kujua ni mafanikio gani ya msingi na ya kujivunia yaliyopatikana kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mpaka sasa.
Akijibu swali hilo, naibu waziri huyo alisema kwa jumla shirikisho hilo limefanikiwa kukuza na kuendeleza mpira wa miguu kila kona ya nchi na kuweka muundo wa utawala katika kila ngazi, kuandaa wataalamu wa fani za ufundishaji, uamuzi, utawala na tiba kwa wanamichezo zaidi ya 10,000 na kuongeza kuwa, wataalamu hao wamepata mafunzo hayo tangu nchi ilipopata Uhuru.
“Shirikisho pia limefanikiwa kuandaa na kuendesha programu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mashindano ya timu za vijana, wanawake na watoto kama sehemu ya kuweka msingi bora wa maendeleo ya mchezo wa soka,” alisema.
Pia alisema timu ya taifa ilifanikiwa kucheza mara moja fainali za Kombe la Afrika na mara moja kwa timu za taifa za wachezaji wa ligi za ndani, (CHAN), pamoja na kujenga na kuimarisha uhusiano mwema kati ya shirikisho na serikali. 
 

Thursday, April 19, 2012

JAMANI THIS IS TOO MUCH !

WASIKILIZE BAKARI MALIMA ' JEMBE ULAYA ' NA MDAU HEAVY D JUU YA YANGA.

  BEKI WA ZAMANI WA YANGA BAKARI MALIMA ( kushoto )



ROGER MILLA AANZA MAPAMBANO NA FECAFOOT

Milla

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Cameroon, Roger Milla ameunda Kamati ya kupambana kuwaondoa madarakani viongozi wa Shirikisho la Soka nchini humo (FECAFOOT) na kumrejesha kikosini, Nahodha wa timu ya taifa, Samuel Eto'o.
Milla anahofia Cameroon, ambayo haikufuzu kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu, inaweza pia kukukosa fainali zijazo.
"Lazima tuirudishe soka yetu kwenye reli, hatua nzuri kwa sababu tunakoelekea sasa chini ya uongozi wa timu wa sasa hakuaminiki," alisema Milla baada ya kuzindua Kamati ya kuivisha tena nguo soka ya Cameroon, iitwayo COCIREFCA, Kifaransa yaani Comite Citoyen pour le Redressement du Football Camerounais.
"Hakuna anayeona kwamba tunaekelea kufeli kutoka kwenye kufeli. Hii lazima tuimalize na mambo lazima yasonge mbele.
Uongozi wa sasa wa FECAFOOT, lazima uondoke, (rais) Iya Mohamed na wenzake lazima waondoke. Soka ya haiwezi kuendelea kuongozwa kwa watekaji," alisema Milla.
Kamati hiyo imeundwa na kundi la wachezaji wa zamani, ambao wanataka kauli thabiti ya shirikisho.
Milla anaheshimika sana kwenye soka ya Cameroon, kutokana na kufunga mabao yaliyoiwezesha nchi hiyo kutinga Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1990.
Eto'o alisimamishwa baada ya kuongoza uasi katika timu ya taifa kutokana na madai ya maslahi ya wachezaji, hali iliyosababishwa kuahirishwa kwa mechi ya kirafi iliyokuwa ifanyike Novemba mwaka jana Algeria.

KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART III


BONYEZA HAPA CHINIUMSIKIE MZAZI!!

KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART II

BONYEZA HAPA CHINI UMSIKILIZE MZAZI

KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART 1

BONYEZA HAPA CHINI UMSIKILIZE MZAZI

KWANINI PAUL SCHOLES NDIO KIUNGO BORA KUWAHI KUTOKEA KATIKA ZAMA ZA PREMIER LEAGUE.


Cesc Fabregas, Frank Lampard, Steven Gerrard, Claude Makelel, Roy Keane na Patrick Vieira - wote ni viungo wakali waliowahi kutokea katika premier league, lakini sio category ya kiungo wa Manchester United - legend Paul Scholes.

Premier league sasa ina umri wa miaka 20 - na kumekuwepo na mjadala nani ni kiungo bora ambaye wanadhani amewahi kucheza katika ligi hiyo tangu ilipoanza katika mwaka 1992.

Watu wengi wakiwemo wachezaji na wachambuzi wa soka wamekuwa wakimtaja Paul Scholes kama kiungo bora kuwahi kutokea katika ligi hiyo.

Wakati candidates wengine, kama mchezaji wenzie wa zamani wa Roy Keane na Paul Ince, Fabregas, Gerrard, Lampard, Makelel, Matt Le Tissier na Emmanuel Petit walikuwa maestro wa hatari katika safu ya kiungo, lakini hakuna ambaye ana impact ya Scholes.

Kwa hili ni mchezaji ambaye anastahili kabisa kuitwa kiungo bora kabisa kuwahi kutokea katika premier league.

Katika miaka yote 19 ya kucheza soka katika level ya juu, Scholes ameshinda medali nyingi sana.

Na wakati akiwa mtu mwenye kuona sana aibu mbele ya vyombo vya habari, wale ambao walicheza nae au walicheza dhidi yake wamekuwa ndio wasemaji wa kipaji chake.

Thierry Henry: "Manchester United siku zote wamekuwa na wachezaji wazuri, lakini wakati wowote tulipokuwa tunakutana nao, siku zote nilikuwa naogopa kitu ambacho Paul Scholes atafanya.
Muulize mtu yoyote kutoka katika kikosi cha zamani cha Arsenal, watakuambia haya ninayokuambia.
Ikiwa utamuachia acheze, anaweza kukuua, na mimi najua wengi walikuwa wanamuona wa kawaida. Jinsi alivyokuwa akicheza, pasi moja, huku akiwa mtu wa mwisho kufika katika box, jinsi anavyopiga mashuti, muono wake, na pasi zake- alikuwa hatari sana.
Najua watu wamekuwa wakimsema kwwa tackling zake, lakini mimi nilipenda vile. Anajua namna ya ya kuipeleka timu mbele na kutuliza mashambulizi ya wapinzani. Kwangu mimi ni mmoja ya viungo bora kabisa ambao nimewahi kuwashuhudia maishani mwangu."

Na kama hiyo haitoshi, haya ndio aliyoyasema Xavi Hernandez - kiungo wa FC Barcelona ambaye wengi tunaamini ndio mpiga pasi bora duniani - aliyasema kuhusu mchezaji ambaye mara kwa mara amekuwa akimuongelea kwa pamoja na Xabi Alonso.

"Katika miaka 15 mpaka 20 iliyopita kiungo bora ambaye nimewahi kumshuhudia - ambaye amekamilika ni Paul Scholes. Nimeongea na Xabi Alonso kuhusu Scholes mara nyingi sana. Ni MCHEZAJI HATARI NA AKILA KITU.

Anaweza kucheza pasi ya mwisho, kufunga, ana nguvu, ni vigumu sana kumpora mpira na vigumu kuupoteza. Kama angekuwa Hispania then labda angekuwa amethaminiwa zaidi."

In fact, Zinedine Zidane,(ambaye alimuita Scholes mpinzani wake mkubwa) Socrates, Marcello Lippi, Laurent Blanc, Bobby Chalrton, Edgar Davids, Cesc Fabregas, Ryan Giggs wote wamekuwa wasemaji wakubwa wa uwezo na kipaji cha Scholes.

Tumesikia na kusoma mengi kuhusu wachezaji na makocha wengine wakimsifia Paul Scholes kama kiungo bora, lakini sababu kubwa kwanini ni kiungo bora tokea premier league ianzishwe inaangukiakatika msimu wa sasa akiwa na klabu yake ya Manchester United - ambayo alijiunga nayo tena miezi sabab baada ya kuamua kustaafu.

Tangu arudi dimbani kumsaidia boss wake na rafiki yake wa zamani Sir Alex Ferguson, Scholes ametoa msaada mkubwa ambao hata mashabiki wake wakubwa wasingwahi kufikiri.

Kurudi kwake katika kikosi cha Manchester United kumueleta tofauti kubwa ndani ya kikosi hicho ambacho tangu kuumia kwa Tom Cleverlley mwanzoni mwa msimu kulileta hali tete ndani ya timu hiyo hasa katika safu ya kiungo.

Msimu huu, Scholes ana wastani wa 9.9 wa kupiga mipira mirefu kwa mchezo na pasi zimefika kwenye target kwa wastani wa asilimia 92.5.

Hilo linamfanya ashike namba mbili katika listi ya  wapiga pasi nyingi zilizofanikiwa katika premier league - nyuma ya Leon Britton wa Swansea City, inashangaza - lakini Britton anapiga wastani wa 4.2 ndogo kuliko za Scholes kwa mechi.

Na katika sula la kusambaza mipira, hapo ndio anakamata usukani kwa kufanya hivyo - Mchezaji wa Tottenham na kiungo mchezeshaji Luka Modric anashika nafasi ya pili kwa sasa, akiwana wastani wa 7.5 wa kupiga mipira mirefu kwa mechi.

Lakini pamoja na kupiga sana pasi, Scholes pia amekuwa akifunga - bao lake la kwanza tangu arudi kutoka kustaafu alifunga katika mechi dhidi Bolton Wanderes, kabla ya kufunga bao muhimu katika mechi dhidi ya Norwich City, kabla ya kuwamaliza Queens Park Rangers.

Haya yote ameyafanya mchezaji ambaye katika nusu ya kwanza ya msimu alikuwa akiishi maisha ya mcheza soka mstaafu, akifanya mazoezi na timu za vijana katika klabu yake ili aweze kuwa fiti.

Hili linadhihirisha kwamba uwezo na kipaji cha Paul Scholes hakitopotea.
Tumeshuhudia nini kinatokea kwa wachezaji kama Roberto Pires na Robbie Fowler walipojaribu kuongeza muda wa kucheza soka walipofika umri mkubwa- walifeli.

Scholes akiwa na miaka 37, bado anacheza soka la kiwango cha juu, huku bado akiwa na umuhimu mkubwa katika klabu kubwa ya Manchester United.

Hakuna mchezaji yoyote katika premier league au duniani katika soka, angeweza kucheza soka la kiwango juu analocheza Scholes tena akiwa katika umri mkubwa wa miaka 37, tena hasa baada ya kukaa nje ya game kwa miezi saba bila kucheza soka la ushindani.

N a ndio maana Paul Scholes anastahili kuitwa mchezaji bora wa muda wote katika zama za premier league katika safu ya kiungo.

Ndio mchezaji ambaye amedumu katika soka la kiwango cha juu kwa muda mrefu kuliko wote duniani, tena hasa katika premier league na pia ni mmoja ya role models katika michezo duniani.

Roy Keane anatufungia mjadala huu kwa kusema: "Hakuwa na mbwembwe za umaarufu, hakujitangaza lakini ndio mchezaji aliyebarikiwa na kubakia kutodhurika na udhaifu unaotokana na ubinadamu."