Search This Blog

Saturday, June 4, 2011

ENGLAND YATOKA SARE NA USWISI NA LAMPARD AVUNJA REKODI


Timu ya taifa ya England imetoka sare na Uswisi katika michuano ya kugombea kucheza fainali za kombe la mataifa ya ulaya zitakozofanyika mwakani nchini Ukraine huku kiungo Frank Lampard akivunja rekodi kwa kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi kupitia mikwaju ya penalti akiwapita Alan Shearer na Rob Fowler.

Lampard ambaye alianza kuichezea England in October 10, 1999 dhidi ya Belgium akiwa na miaka 21 na siku 111, mpaka sasa ameshaitumikia Three Lions katika mechi 86, kati ya hizo 36 ni za kirafiki, kufuzu World Cup 20, World Cup finals 9, kufuzu EURO 15, EURO finals 4, michuano mingine 2.Amefunga magoli 22, 7 KATI YA HAYO AMETUPIA NYAVUNI KUPITIA MIKWAJU YA PENATI.

Amecheza jumla ya dakika 6385, amepata kadi 3 za njano, hajawahi kupata red card, goli lake la kwanza alifunga dhidi ya Croatia, amewahi kuwa kapteni mara 1 katika mechi dhidi ya Denmark.


TAIFA STARS YAWASILI SALAMA BANGUI



Timu imefika salama hapa Bangui, ambapo imefikia hoteli ya Hotel De Centre mechi inachezwa kesho saa 9 kwa saa za hapa ambapo nyumbani ni saa 11 kamili, kocha Jan Poulsen amesema "Lengo ni kushinda", na atatumia mfumo ule ule wa uchezaji ambao tayari wachezaji wake wameuzoea, leo timu imefanya mazoezi katika uwanja utakaotumika kwa mechi na muda ule ule ambapo mechi itaanza

NAIPENDA klabu ya Simba kiasili-MWANA FA











NAIPENDA klabu ya Simba kiasili, sitoweza kueleza ilikuaje nikaanza kuwa na mapenzi na timu hii”



Ndivyo anavyoanza kusema msanii Hamees Mwinjuma ‘MwanaFA’ kuhusiana na mapenzi yake kwa klabu ya Simba inayofahamika pia kama Wekundu wa Msimbazi.



Anasema anapendezwa na Simba kutokana uwezo mkubwa wa kucheza soka walionao wachezaji wengi wa timu hiyo, ambao baadhi yao ni marafiki zake.



Licha ya kuwa ni shabiki mkubwa wa Simba na msanii nyota wa Bongo Fleva, MwanaFA ni rafiki mkubwa wa wachezaji Juma Kaseja, Credo Mwaipopo na Athuman Idd ‘Chuji'. Pamoja na yote hayo, msanii huyu anavutiwa zaidi na uchezaji wa Kaseja.



“Kaseja, Credo na Chuji ni marafiki zangu wa ukweli na ndo maana mara kwa mara huwa nawatembelea nyumbani na hata wanapokua kambini,



“Nilianza kuingia uwanjani katika kila mechi ya Taifa Stars Kaseja aliporudishwa langoni, namuamini sana kipa huyu pindi anapowekwa katika nafasi yake,”

Friday, June 3, 2011

NATAKA NIKUMBUKWE KAMA PELE NA MARADONA - RONALDO



Mfungaji bora La Liga amesema ana matamanio na ndoto za kuwa katika level za Maradona na Pele, soma mahojiano yake aliyoyafanya na mtandao mmoja wa intaneti kuzungumzia ndoto zake.

Ni miaka miwili tangu ujiunge na Real Madrid, vipi unayafurahia maisha ya hapa? Nafurahia sana kuwa hapa , klabu ni nzuri sana na nilitegemea hili.Miundombinu , washabiki na uwanja uzuri wake hauwelezeki.

Unajisikiaje kucheza na mtu kama Kaka ndani ya Real Madrid? Ukiwa unacheza timu moja na wachezaji wazuri inakuwa rahisi zaidi na Kaka ni mmojawapo, nafurahia sana kucheza pamoja nae.

Unayatizama vipi mafanikio yako ndani ya kikosi cha Manchester United? Nafikiri nilifanya kila kitu nilichotaka nikiwa na United.Nimeshinda kila kitu ndani na nje ya England.Miaka 6 niliyokaa pale haiwezi kufutika kwenye kumbukumbu zangu. Sasa nipo Madrid hivyo nategemea vyote nilivyoshinda nikiwa na United.

Utajisikiaje ikiwa Real Madrid watapangwa na Man United katika Champions League msimu ujao? Sitaki kucheza dhidi ya Manchester United, sitojisikia vizuri lakini huwezi kujua katika Champions League kila kitu kinawezekana lakini sipendi kucheza dhidi ya United.

Kina nani ni marafiki zako wakubwa ndani ya Manchester United? Bado nina marafiki walewale.Muda mwingine naongea Rooney, Vidic, Ferdinand, Nani, Evra, na Anderson.Ni vizuri kujua nini kinaendelea kule na watu wanapenda kujua kama nina furaha hapa na vitu vingine vinaendeleaje hapa.

Umehawi kumzungumzia Sir Alex Ferguson kama Baba yako katika soka.Mna mahusiano gani kwa sasa? Mr. Ferguson amenisaidia sana kukuza kipaji changu, nilikuwepo pale kwa miaka 6 na amenifundisha vitu vingi sana.Tumeshinda vitu vingi pamoja, namuheshimu sana, ni rafiki yangu na nampenda sana.

Matarajio yako yaliyobakia kwenye soka ni yapi? Matamanio yangu ni kushinda makombe mengi zaidi, binafsi na kwa timu yangu.Napenda kucheza soka, haya ni maisha yangu bila soka sijui nitafanya nini.Soka ni maisha yangu na nataka kushinda vitu iwezekanavyo.

Ungependa vitabu vya historia vikukumbuke vipi? Bado nina miaka 7 au 8 ya kucheza soka na kama bado nitakuwa na nguvu ningependa kucheza mpaka nifikishe miaka 40, hivyo nataka kuwa katika ukurasa wa kwanza wa historia kama ilivyo kwa Maradona na Pele.Nataka kuwa sehemu hiyo ingawa najua ni vigumu lakini nafikiri inawezekana kama nikiendelea kucheza hivi na kushinda mataji. ni vigumu lakini inawezekana, ipo kichwani na nitatimiza ndoto yangu.

WAJENGA KIWANJA CHA SIMBA WAWASILI NCHINI

hii ni ramani ya jinsi kiwanja cha SIMBA kitakavyokuwa.


wawakilishi wa kampuni itayojenga uwanja wa simba sports club wameingia nchini kufanya majadiliano ya mwisho kabla ya project kuanza.
kesho uongozi wa simba utakua na kikao na wawakilishi hao pale hotel ya KILIMANJARO KEMPINSKI kesho saa tano asubuhi.

AZAM YASAJILI WAGHANA


aZAM FC LEO IMETANGAZA KUWASAJILI wachezaji kutoka nchini Ghana ambao ni mshambuliaji wa kati wa Kingfaisal ambaye anashika nafasi ya tatu kwa ufungaji magoli kwenye ligi kuu ya Ghana Abdul Wahab Yahya na nahodha wa Kingfaisal Nafiu Awudu naye pia anatoka King Faisal Babes. Wachezaji wote wawili wanachezea timu ya Taifa ya Ghana U-23. Nafiu Awudu pia anachezea kikosi cha Black Stars

FABREGAS NI WENU KWA PAUNDI MILLION 54- ARSENAL WAIAMBIA REAL


ARSENAL wameiambia Real Madrid kuwa bei ya kumuuza Cesc Fabregas inaanzia paundi millioni 54.

Director wa Real, Jose Angel Sanchez aliwasiliana na Arsenal saa moja baada ya Wenger kukiri kuwa hakujakuwa na timu yoyote iliowasilisha maombi ya kumtaka Fabregas, na Spanish giants sasa wapo tayari kukubaliana na Gunners na kuwapiku mahasimu wao wakubwa Barcelona.

Chanzo cha habari kutoka Madrid kilisema: Raisi Florentino Perez amesema kuwa Fabregas ni moja ya usajili mzuri na zaidi utawaumiza sana Barca.Anaamini kumsajili Cesc itakuwa ni jambo la maana msimu ujao na atafanya chochote kinachohitajika kuwapiku Barca next season.

Perz yupo tayari kuidhinisha matumizi ya £100m kwa kumpata Fabregas na mshambuliaji wa Atletico Madrid anayewania pia na Barca na Man City Sergio "Kun" Aguero.
Real sources wanadai kuwa Arsenal wameweka wazi kabisa kuwa hatamuuza Cesc kwa timu yoyote ya Uingereza.

Barcelona-born midfielder Fabregas, 24, mwaka jana aliweka wazi nia yake ya kutaka kurudi Nou Camp baada ya kukaa England kwa miaka 8, lakini newly-crowned European Champions hawapo tayari kuongeza dau la £30million ambalo lilikataliwa na Arsenal msimu uliopita

SAJILINI MAJINA MAKUBWA AU NAONDOKA


LUKA MODRIC ameiambia klabu yake ya Tottenham kusajili wachezaji wazuri na wakubwa ama atafungasha virago vyake na kuondoka.

The Croatian midfielder mwenye thamani ya paundi million 25 anasakwa kwa udi na uvumba na klabu za Manchester United na matajiri wa Eastlands the mega-rich Manchester City.

Modric, 25, alisaini mkataba wa miaka 6 msimu uliopita anansisitiza ana furaha kuwa kwenye kikosi cha Harry Redknapp lakini ana wasiwasi na mwenendo wa klabu msimu ujao.

Mtu wa ndani wa Spurs anasema Harry hataki kumuuza Modric lakini Luka mwenyewe ana ndoto za kupata mafanikio makubwa zaidi.

"Modric anasubiri kuona kama Redknapp atasajili wachezaji ambao ni wakubwa halafu ndio atajua nini hatma yake ndani klabu hii".

Wakati huo huo Roman Pavlychenko amesema yupo tayari kuendelea kubaki White Hart Lane, "Nia yangu ni kubaki hapa na kupata mafanikio makubwa, baada ya mapumziko nitarudi kujadili mkataba mpya.

Serengeti Fiesta Soccer Bonanza ni somo kwa soka letu


sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia Serengeti Fiesta Soccer
Bonanza mwaka 2011.


Na Ibrahim Masoud 'Maestro'
YAWEZEKANA hakuna ambaye alifikiri nini kitatokea pale matangazo ya kufanyika kwa Bonanza la Serengeti Fiesta katika mikoa mbalimbali nchini yalipoanza kusikika, lakini hali ilikuwa kinyume, mwitikio ulikisa katika mikoa yote lilikofanyika Bonanza hilo, ambalo lilizihusu timu nane kubwa za Bara la Ulaya.

Ukitaka kutambua tofauti ya mapenzi ya dhati waliyokuwanayo wapenzi wa soka nchini Tanzania kwa klabu za soka za barani Ulaya, na hata ukitaka kuvuta taswira ya kujua ukweli, hebu kumbuka wakati Bonanza hilo lilipoanzia jijini Dar es Salaam.

Hakukuwepo na mchezo rahisi, hasa baada ya wale waliokuwa wakizitetea timu zao wanazopenda wakiwa ndani ya uwanja.

Soka lilipigwa kwa kiwango cha juu kabisa, hakuna aliyekubali kushindwa kirahisi kwani wachezaji walitumia mbinu zote zinazotumiwa na wachezaji kote duniani wa klabu hizi ndani ya uwanja.

Kwa hakika, endapo hata wachezaji wetu wa klavu za nyumbani wangekuwa na ari ile basi tungekuwa na timu ambazo si rahisi kushindwa, na uwakilishi wa mashindano ya kimataifa ungekuwa wa kuvutia.

Ndani ya uwanja, kama nilivyosema, soka lilipigwa sana, lakini kila mkoa kulikuwa na tofauti, wakati ambapo mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, na Mbeya vita ilikuwa kubwa sana, mjini Zanzibar ufundi ulikuwa mkubwa sana na pia waliocheza wakiwa ni vijana zaidi tofauti na miji mingine.

Hakika vijana wa Zanzibar walicheza soka la ufundi wa hali ya juu na pengine kivutio kingine kikiwa ni binti mdogo Sabaha Hashim Yusuph ambaye anafahamika kama Messi kutokana na kupigia mguu wa shoto, na kipaji cha hali ya juu mno alichonacho, wakati akiichezea timu ya mashabiki wa FC Barcelona, huko Visiwani.

Hata jijini Mwanza, alionekana binti mdogo aliyecheza kwa mashabiki wa timu ya Liverpool, Hamisa Athumani, ambaye anatoka kwenye kituo cha kufundisha soka kwa vijana cha TSC, naye alionyesha kipaji cha hali ya juu mno.

Haikushangaza hata pale vijana wawili wa umri wa chini ya miaka 19 waliocheza katika timu za mashabiki wa Barcelona na Real Madrid kule visiwani Zanzibar kuchukuliwa na timu ya Simba ya kikosi cha pili, kutokana na vipaji vikubwa walivyokuwa navyo.

Wakati Bonanza hilo likitoka jijini Tanga, tayari matayarisho yamekwishaanza kule Arusha, ambapo Jumamosi ya Juni 4, litakuwa likifanyika katika mji ambao unasadikiwa kuwa na viunga vingi vya ving�amuzi kwa ajili ya kushuhudia soka la Ulaya, maarufu kama 'Vibanda Umiza'.

Sasa kutokana na sifa ya mashabiki wa jiji la Arusha ya kuthamini sana soka la Ulaya mpaka kuamua kuondoka kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati soka letu la ridhaa likiendelea kwa ajili ya kwenda kushuhudia lile la Ulaya linaloitwa la ukweli, basi yawezekana kabisa mji huo ukafunika kwenye Bonanza hilo kwa idadi ya watu watakaojitokeza, kwani hawa ni wadau halisi wa soka hili.

Kimsingi, Bonanza hili limekuwa fundisho kubwa kwa Watanzania na hasa wadau wa soka, kwa namna ambavyo kumeonaka kuwa na tofauti baina ya soka letu la lile la Ulaya.

Ingawa mechi zinazochezwa si za ushindani wa taji lolote, lakini kwa hakika ushindani huu ni somo kubwa kwa wadau kwamba tukiwa na mikakati mizuri na kuwa na ari ya kuzitetea timu zetu tunazozichezea, hasa wachezaji husika, kama tulivyoona walivyokuwa wakizitetea zile wanazozishabikia za Ulaya, tunaweza tukapiga hatua katika maendeleo ya mchezo huo katika ngazi ya kimataifa.

Kama mashabiki tu wanaojifanya kuzipenda Arsenal na Manchester United wanapambana ka jitahidi uwanjani kila mmoja akitaka kulinda heshima yake, si zaidi basi kwa wachezaji walioajiriwa na timu za Yanga, Simba, Azam na Kagera kucheza kwa ari kubwa kuzipatia ushindi timu zao?

Soka letu litakapopiga hatua kuanzia kwenye ligi ya ndani kwa kuonyesha ushindani halisi, ni dhahiri kabisa kwamba linaweza kutangazika kimataifa, na hiyo itakuwa fursa nyingine kwa klabu zetu kuuza jezi zao na pengine mashabiki wanaweza walau kubadilika kwa kuvaa jezi za timu za ndani badala ya 'kushaini' jezi za Man United, Real Madrid au Barcelona.
Bonanza hili liwe somo kwetu sote.

EXCLUSIVE INTERVIEW NA MACDONALD MARIGA

SHAFFIH DAUDA AKIMKABIDHI NAKALA YA JARIDA LA NUMBER 10,
KIUNGO WA INTER MILAN MCDONALD MARIGA MARA TU BAADA
MAHOJIANO.


Hivi karibuni kiungo wa kimataifa wa Kenya na klabu ya Inter Milan ya Italia McDonald Mariga alikutana uso kwa uso na Shaffih Dauda na kufanya mahojiano na Jarida la NUMBER 10,
Number 10: McDonald unaweza kuelezea kwa ufupi safari yako ya soka mpaka hapa ulipofikia.
Mariga: Nilianza kucheza timu ya Ulinzi, Kenya, baada ya kutoka shuleni na baada ya hapo nikajiunga na Pipeline FC na baadaye nikaenda Tusker; na hapo ndio nikavuka mpaka Sweden kujiunga na timu ya Enkopings SK. iliyokuwa inacheza ligi daraja la tatu, halafu nikahamia Helsinborg ya daraja la kwanza na ndio nikaenda Parma kabla ya kusajiliwa na Inter Milan mwaka huu.
Namber 10: Safari yako unaionaje, je ilikuwa ngumu au nyepesi?
Mariga: Hapana, unajua kila kitu kina ugumu wake.
Number 10: Ni nini siri ya mafanikio yako?
Mariga: Kwangu siri ya mafanikio ni bidii na juhudi katika kazi yangu na baada ya hivyo mengine yanafuatia.
Number 10: Wakati unajiunga na Inter Milan, Rais Massimo Moratti alikupa maneno gani wakati mlipoongea kwa mara ya kwanza?
Mariga: Nilizungumza na wakala wangu kwanza ambaye alizungumza na Moratti kabla yangu; lakini Moratti aliniambia kuwa timu yake inanihitaji na hilo lilinifurahisha kwani Inter ni timu kubwa.
Number 10: Na vipi kuhusu Jose Mourinho, alikueleza nini mlipoongea mara ya kwanza?
Mariga: Mourinho nilimuona mara ya kwanza nikiwa Parma na nilipokuja Inter nilifurahi kuwa naye na kucheza chini yake, kwani Jose ni kocha mkubwa sana hapa duniani.
Number 10: Utotoni ni mtu gani alikuwa shujaa wako?
Mariga: Kwa wachezaji ni Patrick Vierra ndio aliyenivutia, lakini shujaa wangu halisi alikuwa ni baba yangu mzazi Noah Wanyama ambaye aliwahi kuwa mchezaji na kocha akiwa na AFC Leopards na klabu za Uganda pia.
Number 10: Unaizungumziaje nafasi yako kwenye klabu kama Inter Milan ambayo ina wachezaji wengi nyota?
Mariga: Nafasi yangu pale Inter Milan ipo kama mchezaji na nafurahi kuichezea Inter na pia namwomba Mungu anijalie ili nifike mbali zaidi ya hapa.
Number 10: Unaelezeaje kuondoka kwa Jose Mourinho kocha ambaye alikuleta Inter Milan?
Mariga: Ni kweli Mourinho ndiye aliyenileta Inter, lakini unajua makocha wakati mwingine ni wapita njia kwenye timu; wanakuja na kuondoka kwa hiyo nafurahi kuwahi kucheza chini yake na pia namtakia mema huko aendako.
Number 10: Na ikitokea Jose Mourinho akikuhitaji ujiunge naye Madrid itakuwaje?
Mariga: Akinihitaji siwezi kusita kwani Madrid ni klabu kubwa, lakini kwa sasa sijui itakavyokuwa kwani mimi ni mchezaji wa Inter.
Number 10: Kama ungekuwa ‘Tour Guide’ ungempeleka mgeni sehemu gani ya Tanzania.
Mariga: Nafikiri Dar es Salaam ni sehemu nzuri lakini Zanzibar pia ni sehemu nzuri kwenda.
Number 10: Ipi timu bora kwako AFC Leopards au Gor Mahia?
Mariga: Zote ni timu nzuri na zilikuwa kubwa enzi zake, lakini naisapoti AFC.
Number 10: Unaweza kutuambia nini kuhusu rasimu ya katiba mpya iliyopigiwa kura hivi karibuni nchini kenya?
Mariga: Sikuwapo wakati wa kupiga kura kwa hivyo siwezi kujua; labda ningeisoma kwa makini ndio nichague upande upi uko sahihi.
Number 10: Ukiwa kama kijana unawashauri nini vijana wenzio kuhusiana na matatizo kama dawa za kulevya na Ukimwi?
Mariga: Ningewashauri waachane na mambo kama hayo na wazingatie yale ambayo yanaweza kuwasaidia maishani.
Number 10: Unatumiaje nafasi yako kama mchezaji wa kimataifa kusaidia soka la Kenya?

Mariga: Labda naweza kusema kwa vijana wadogo wanaochipukia, kuwafanyisha mazoezi na vitu kama hivyo.
Number 10: Mafanikio yako Inter Milan yana maana gani kwako na kwa taifa lako kwa ujumla?
Mariga: Kwangu ni kitu kikubwa kwa kuwa sikuwahi kutarajia kama ningeweza kufika hapa nilipo kwa hiyo namshukuru Mungu na nadhani hii pia itakuwa nafasi kwa wachezaji wengine toka Afrika Mashariki.
Number 10: Kwa wachezaji wengi ndoto kubwa ni kucheza vilabu vikubwa kama Barcelona na Real Madrid, vipi kwa upande wako?
Mariga: Kwangu hata hapa nilipo Imter Milan ni klabu kubwa kwani tumechukua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na ni timu kubwa Italia pia, kwa hiyo niko sawa hata hapa tu.

Maisha binafsi
. Baba yake Noah Wanyama, alichezea AFC Leopards nafasi ya winga ya kushoto, pia alichezea timu ya Taifa ya Kenya.
. Victor Wanyama ni mdogo wake kwasasa anacheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji kunako klabu cha K.F.C. Germinal Beerschot.
. Ndugu yake mwingine Thomas Wanyama anachezea Mabingwa wa ligi kuu ya kenya Sofapaka.
. Mdogo wao wa kike Mercy Wanyama ni mwananfunzi wa shule ya Lang’ata High School pia ni nahodha wa timu ya shule ya mpira wa kikapu
. Mariga alifuga bao lake la kwanza akiwa amevaa uzi wa Inter Milan mnamo mwezi April 24, 2010 dhidi ya Atalanta akiunganisha kimiani pasi ya Samuel Eto’o ,Inter ilishinda mabao 3–1


Source: NUMBER10 FOOTBALL MAGAZINE

MAN UNITED NA BARCELONA KUPAMBANA MAREKANI




On 28 July, Man United na klabu bingwa ya ulaya Barcelona watapambana mjini Washington DC katika uwanja wa FedEx Field katika mataarisho ya msimu ujao maarufu kama Pre-Season.

Uwanja wa FedEx Field utakuwa umejazwa na mashabiki wapatao 91000 wakiangalia marudio ya fainali ya Champions League.

Barca waliitandika United katika fainali ya UEFA na sasa Red Devils wamepata nafasi ya kulipiza kisasi kupitia mechi hiyo.

Man United pia watacheza na New England Revolution, Seattle Sounders, Chicago Fire na kikosi cha mastaa wa ligi ya USA maarufu kama MLS All-Stars.

Thursday, June 2, 2011

JACK WILSHARE - JINSI YA KUWA KIUNGO MZURI


Jack Wilshare ni moja ya viungo wazuri kuwahi kutokea katika katika historia ya soka katika vikosi vya Arsenal na England.

Wilshare ambaye msimu huu amejitokeza kuwa moja viungo wazuri na kuisaidia Arsenal kushika nafasi ya nne katika ligi kuu ya England anaelezea ni mbinu ambazo zinamfanya awe kiungo wa kutumainiwa.

KUJIPANGA UWANJANI
"Kiungo mchezeshaji mzuri anapaswa muda wote kupokea mpira, hapa Arsenal nina bahati kuwa pamoja na Febregas ni mchezaji ambaye utapenda kucheza nae kwa sababu muda wote anakuwa kwenye nafasi na anakupa mpira ukiwa katika nafasi, ananipa muda wa kufikiri jinsi gani anapaswa kutoa pasi na kuendeleza aina ya mchezo wetu"

KUJITAMBUA
"Angalia wenzako pindi mpira unapokujia.Inasaidia kujua nini kinaendelea katika duara lako, kujitambua huku kuna kuruhusu kujua mienendo ya adui na kukufanya ujue.

KUFIKIRIA MBELE
"Ni bora na muhimu kujua nini utafanya utakapopokea mpira kabla haujakufikia.Kabla haujaumiliki unakuwa tayari umeshafikiria nini cha kufanya na mpira unapokujia unaweza ukapiga one touch au ukaupiga mpira kwa mwenzio aliye kwenye nafasi nzuri zaidi"

KUCHEZA KWA NGUVU
"Aina ya mchezo wa Arsenal inanifaa sana kwa style ya kucheza kwangu, inanijengea mazingira mazuri ya kucheza vizuri.Tuna kiungo mmoja mkabaji na wawili wachezeshaji kwa hiyo mfumo wa wa 4-3-3 ni mzuri zaidi katika kuwezesha mchezo kwa kiungo mchezeshaji"

YANGA NA SIMBA KUPAMBANA AUGUST 20


Wakati pazia la Ligi Kuu Bara likitarajiwa kufunguliwa Agosti 20, watani wa jadi Simba na Yanga wanatarajia kukutana Agosti 13 katika mchezo wa Ngao ya Hisani kwa ajili kufungua pazia la ligi hiyo.Timu hizi pia zilikutana msimu uliopita

katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Yanga iliwafunga Simba, mabao 3-1 katika mechi iliyoamuliwa kwa 'matuta' baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya 0-0 katika Uwanja wa Taifa.

Yanga walipata penalti zao za ushindi kupitia kwa Godfrey Bonny, Stephano Mwasika na Isaack Boakye, wakati Simba walipata penalti moja tu iliyofungwa na kiungo wa zamani ya Yanga, Mohammed Banka.

Mghana, Ernest Boakye alikuwa mpigaji pekee wa Yanga aliyeshindwa kufunga baada ya penalti yake kupanguliwa na kipa wa Simba, Ali Mustapha 'Barthez' wakati wachezaji wa Simba waliopoteza penalti zao walikuwa, Emannuel Okwi, ambaye penalti yake ilipanguliwa, Uhuru Selemani aliyepiga juu na Amri Kiemba aliyegongesha mwamba.

Akizungumzana gazeti hili, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura wakati akitaja kalenda ya matukio ya 2011/12 alisema mchezo huo huwa unatakiwa kuchezwa kati ya bingwa wa Ligi Kuu na yule wa Kombe la FA, lakini kutokana ana kutokuwa na FA kwa sasa huwa anacheza na mshindi wa pili.

"Timu za Simba na Yanga zinatarajiwa kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani ambao utakuwa ni ishara ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao ambayo itaanza wiki moja baadaye", alisema.

Pia alisema kwa mujibu wa kalenda hiyo msimu wa Ligi Daraja la Kwanza kwa mtindo wa nyumbani na ugenini utaanza Septemba 3 mpaka Oktoba 31, Ligi ya Taifa ngazi ya wilaya Septemba 10 mpaka Desemba 31, Ligi ya Wanawake ngazi ya wilaya Septemba 11 mpaka Oktoba 31.

Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yanayoandaliwa na Shirikishola Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yataanza Julai, Ligi ya Mabingwa Julai na Shirikisho Julai.


WESLEY SNEIJDER-SIRI ZA KUCHEZA VIZURI


KUUJUA MWILI WANGU

"Kitu kimoja ambacho kiliharibu uwezo wangu nikiwa na Madrid ni kwa sababu nilikuwa sichezi , muda wote nilikuwa naumia kila siku.Nilipokuja Inter nilibadilisha mazoezi na nikapona, kama nilikuwa sijisikii vizuri niliwaambia makocha na nikawa nafanya mazoezi mepesi.Chini ya Mourinho tulikuwa tunafanya hivi na timu nzima ndio maana hatukuwa na majeruhi wengi.Wachezaji tulipewa muda mzuri wa kupona majeraha."


KUJIANDAA VIZURI

"Kabla ya mechi yangu ya kwanza nikiwa na Inter (match ambayo Inter ilishinda 4-0 dhidi ya AC Milan na Sneijder akawa man of the match) coach staff walinipa video za kuwaangalia wachezaji wenzangu na wapinzani wetu.Haikuchukua muda mrefu kuziangalia lakini ilinipa njia ni jinsi gani napaswa kucheza na my team mates dhidi ya wapinzani wetu, pia niliona udhaifu wa wapinzani na jinsi gani napaswa kuutumia udhaifu huo kuwaumiza.Kwahiyo kupitia kujiandaa kwa kuangalia videoz kabla ya match inakupa mwanga ni jinsi gani unapaswa kucheza."

KUPUMZIKA

"Mimi ni moja ya wachezaji ambao pindi mechi inapoisha huwa nafikiria kitu kingine.Huwezi kucheza kwenye kiwango kikubwa kila wiki kama kila siku unawaza kuhusu soka, inabidi ubadilike muda mwingine.Baadhi ya wachezaji wenzangu wa Inter wanacheza tennis na wengine wanakwenda kuvua samaki, mimi sipendi vitu hivyo ndio maana napenda kutumia muda wangu wa ziada kuendesha baiskeli na kuzunguka mitaani, ni njia nzuri ya kupumzika katikati ya mechi kubwa"


KULALA VIZURI

"Sio kitu ambacho wachezaji wengi wanafikiri kinaweza kudhuru jinsi ya kucheza au mazoezi yako siku inayofuata.Mimi napenda kulala japo masaa saba mpaka nane kwa usiku, chini hapo naweza nisicheze vizuri.Nafikiri ndio maana sio vizuri kufikiria kuhusu mpira muda wote kwa sababu kama utafanya hivyo unaweza kuchelewa kulala.Nafikiri kuchelewa kulala kunaweza kusababisha kiwango kupungua kwa hiyo ni vizuri kuacha kuchelewa kulala."

UTARATIBU
"Muda wote huwa najiandaa kwa kila mchezo katika njia moja.Najiandaa kwa mechi katika muda sahihi kila mechi, nitafika uwanjani nikiwa nasikiliza muziki wa Hip Hop ya kidachi, then navaa jezi na kwenda kupasha mwili.Sio vitu vikubwa lakini vinanisaidia kutulia kabla ya mchezo na kuwa katika akili nzuri".

KUTOJISAHAU

"Tuliposhinda makombe matatu kila mechi ilikuwa kubwa, tulikuwa tunacheza mechi ngumu kwenye ligi halafu na kwenye Champions League na Italian Cup, lakini Jose Mourinho alikuwa anatuambia msikirie kushinda treble, fikirieni kushinda kila mechi.Naamini ukifanya hivi makombe yote yatakuja.Ukiwa unashindania makombe makubwa hautakiwi kufikiria kuyachukua makombe hayo kwa sababu unaweza ukasahau vitu vidogo katika mechi ambazo zitakuletea makombe hayo, hivyo cheza vizuri na makombe utapata."


DIEGO FORLAN: MY 24-HOUR FOOD DIARY


Kuna washambuliaji wachache sana ambao unaweza kuwaita deadlier strikers katika ulimwengu wa soka ambao wanamzidi Diego Forlan. Records za Atletico Madrid hitman zinaongea zenyewe, amejishindia Pichichi mara mbili, amepata kiatu cha dhahabu cha ulaya, na amekuwa mchezaji bora ywa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010 akiwa kapteni wa Uruguay.

Anasema siri ya kucheza bila kuchoka na kuwa nguvu muda wote wa mchezo ni vyakula anavyokula kila siku.

Breakfast: Saa 2 asubuhi

Naianza siku kwa sahaniya mananasi, napenda vitu vitamu kwasababu vinauamsha mwili wangu.Baada ya kula matunda kinachofuata nakula brown bread pamoja na yoghurt. Muda mwingine napata mayai ya kukaanga na juisi nzuri ya machungwa, na hiyo inanipata nguvu ya kufanya vizuri mazoezi.

Lunch: Saa mchana

Baada ya masaa mawili au matatu ya mazoezi naenda moja kwa moja kupata chakula cha mchana, sometimes nakula lunch klabuni au katika mgahawa mjini Madrid nikiwa na marafiki na familia yangu.Kwa kawaida nakula tambi au wali na kuku wa kuchoma.


Saa 10: Afternoon snack

Baadae jioni, kawaida huwa napata matunda tofauti kama vile machungwa na mananasi


Saa 3 usiku: Chakula Cha Usiku

Nakula chakula cha mwisho cha siku muda huu, kawaida napata samaki na saladi, napenda sana nyanya na mboga za majani.Nakula vyakula hivi kwa sababu najua ni vizuri kwa afya ya mwili wangu, muda mwingine baada ya dinner napata maziwa kama kinywaji kwasababu mimi sinywi pombe, nilijaribu nilipokuwa mdogo lakini nilishindwa

SH 5BIL KUITANGAZA TANZANIA LIGI ZA ULAYA

SERIKALI imejipanga kuitangaza sekta ya utalii hapa nchini kwa kupitia michezo na kwa sasa imeweka mkakati wa kutoa matangazo ya utalii katika viwanja vinane vya soka ulimwenguni vinavyotumiwa na timu za ligi kubwa duniani.

Jumla ya sh5billioni zitatumika kwa zoezi hilo kuitangaza Tanzania katika ligi za England, EPL, Hispania- La Liga, Italia- Seria A, Ufaransa- Lique 1 na Ujerumani- Bundesliga.Mbali na viwanja hivyo pia nafasi hiyo itatumika kuutangana utalii wa Tanzania katika nchi za Ureno, Uholanzi pamoja na Uturuki.

Tamko hilo lilitolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa mechi baina ya Drake Univesity ya Marekani na Conadeip ya Mexico uliopigwa ndani ya dimba la Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Maige alisema kuwa mbali na wizara yake kutoa matangazo mbalimbali ya utalii katika viwanja mbalimbali vinavyochezwa Ligi Kuu ya England mwaka huu wamejipanga kutangaza vivutio vya utalii katika viwanja vinane vya soka.

Hata hivyo, alisema kuwa wizara yake imejipanga kutenga sh5 billioni kwa lengo la kutangaza vivutio hivyo katika bajeti ya mwaka huu huku akisema kuwa ingawa kiasi hicho cha fedha ni kidogo tofauti na nchi nyingine kama Kenya na wamekuwa wakitenga sh30 billioni kutangaza vivutio vyao.

Hatahivyo, alisema kuwa ugeni wa wanamichezo wa kimarekani 195 si haba kwani utasaidia kuitangaza Tanzania duniani na kusisitiza kuwa siri ya ujio huo ni amani na usalama ambao umetawala hapa nchini

NATAKA KUONDOKA CHELSEA - ZHIRKOV



Chelsea star Yuri Zhirkov jana amesema wazi kuwa anataka kuondoka Stamford Bridge.

The Russia international winger, 27, amesema anataka kurudi Russia baada ya miaka miwili ya misukosuko in West London.
"Kwa bahati mbaya sikuwa na msimu mzuri ndani ya miaka miwili niliyokaa hapa, nataka kucheza na sio kukaa benchi."

Zhirkov aliamia Chelsea kwa gharama ya £18million in 2009 akitokea CSKA Moscow kwa ushawishi mkubwa kutoka kwa Blues' billionaire owner Roman Abramovich, lakini ametumika katika mechi zisizozidi 22 na mingi kati michezo hiyo akiwa ametokea benchi.

"Sitaki kujadili kuhusu suala lolote kuhusu uhamisho kutoka Chelsea kwasababu bado nina mkataba na klabu, lakini nafikiria kuondoka hapa na kurudi Russia pindi ninapofikiria kuwa nataka kucheza".

Reports in Russia zinasema kuwa mahasimu CSKA Moscow na Spartak Moscow wanataka kupata saini ya mchezaji huyo.

TAFUTA TIMU YA KUICHEZEA MSIMU - FERGIE AMWAMBIA BROWN


Baada ya Owen Heagraves sasa Wes Brown amekuwa mchezaji wa pili kuangukiwa na panga la Sir Alex Ferguson ndani Old Trafford baada ya kuambiwa atafute timu ya kuichezea msimu ujao.

The Long serving defender mwenye umri wa miaka 31, amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara na hajaichezea United tangu alipoingizwa kama sub katika mechi na Bolton mwezi March mwaka huu.
Brown amepata upinzani mkubwa kutoka kwa Rafael, John Oshea na Fabio ambao wote wanacheza upande wa beki wa kulia.
Wes Brown ambaye alistaafu kuichezea timu yake ya taifa ya England in August 2010 na kuamua kuweka concentration yake katika kuitumikia klabu yake, alianza kuichezea Man United akiwa na miaka 18 mwaka 1998.

Msimu wake mzuri kipindi akiwa na United ni mwaka 2008 alipoichezea United katika michezo 50 na kufanikiwa kupata kombe la Champions League.

Timu ambazo zinaonyesha nia ya kutaka huduma za Brown ni pamoja na Everton na Sunderland.

PAUL SCHOLES TRIBUTE


PAUL SCHOLES juzi alitangaza kustaafu soka.
Blog hii leo inakuletea historia fupi na mambo aliyoyafanya Paul Scholes kipindi chote cha uchezaji wake akiwa na Man United na timu ya taifa ya England.

1974: Born Salford, November 16.

1991: Signs for Manchester United as a trainee.

1992: Helps United win FA Youth Cup.

1993: Signs professional forms with United.

1994-95: Makes Premier League debut on September 24 against Ipswich. Scores five goals in 17 league appearances during season.

1995-96: Scores 10 goals in 26 league appearances as the Red Devils win the Premier League and FA Cup double.

1996-97: Hits three goals in 24 league appearances as United retain the Premier League title.

1997: May 9 - Called into the England squad by Glenn Hoddle despite only being a reserve for United.

May 24 - Makes his international debut as a substitute against South Africa at Old Trafford.

June 4 - Plays for England in Le Tournoi, scoring on his first start against Italy.

September 10 - Scores opening goal in World Cup qualifier as England trounce Moldova 4-0.

1997-98: Makes 31 league appearances for United, scoring eight goals, as they finish runners-up to Arsenal.

1998: May - Selected for England's World Cup squad.

June - Scores second goal as England win opening match of finals 2-0 versus Tunisia.

1999: March - Scores hat-trick in 3-1 win against Poland in Euro 2000 qualifier at Wembley.

May - United complete a historic treble of European Cup, Premier League and FA Cup but Scholes misses the European Cup final triumph over Bayern Munich through suspension.

June - Sent off in 0-0 draw against Sweden in Euro 2000 qualifier at Wembley.

November - Scores twice for England in 2-0 win over Scotland in Euro 2000 play-off first leg at Hampden Park.

2000: January - Misses World Club Championship for Manchester United after undergoing hernia operation.

June - Scores England's opening goal after just three minutes in the 3-2 defeat to Portugal in Euro 2000.

December - Criticises the appointment of Sven-Goran Eriksson as England coach, saying: "It's the England team and I'd like to see them with an English manager."

2001: June - Nets the opener in the crucial 2-0 win over Greece in England's World Cup qualifier in Athens.

July - Agrees new six-year deal at Old Trafford, joining several others at United in committing long-term to the club.

2001-02: Ends the domestic season with eight goals in 35 league appearances and is part of England's World Cup squad which reaches the quarter-finals.

2002-03: Scores a best-ever 14 league goals as United win their eighth Premier League title, including a hat-trick in a 6-2 win at Newcastle. Adds six goals in other competitions to finish the season with 20.

2004: February 14 - Makes his 400th appearance for United in an FA Cup fifth-round derby clash with Manchester City, scoring the first goal in a 4-2 win.

February 20 - Charged with violent conduct towards an opponent, Middlesbrough's Doriva, by the FA after an incident missed by referee Paul Durkin.

April 3 - Books United's place in the FA Cup final with the only goal in semi-final win over Arsenal at Villa Park.

April 19 - Banned for three matches with immediate effect by the Football Association for charge of violent conduct in relation to Doriva incident.





June - Plays in all four of England's games in Euro 2004, scoring his first international goal for three years in the 4-2 win over Croatia.

August 3 - Makes shock announcement he is retiring from international football.

2005: May 21 - Misses a penalty in the FA Cup final shoot-out as rivals Arsenal triumph in Cardiff following a goalless draw.

August 12 - Signs a new four-year deal with Manchester United to keep him at Old Trafford until 2009.

2006: January 24 - Ruled out for three months with an eye condition. But is out for even longer and does not play again until final game of the season.

October 22 - Makes 500th appearance for United against Liverpool at Old Trafford, scoring the first goal in a 2-0 victory.

2007: May - Helps United win ninth Premier League title.

October 29 - Ruled out for three months with knee ligament injury.

2008: April 29 - Scores winner in Champions League semi-final second leg against Barcelona to secure 1-0 aggregate triumph.

May 21 - Helps United win Champions League in Moscow, beating Chelsea 6-5 on penalties after a 1-1 draw.

2009: March 1 - Part of United side that beats Tottenham on penalties in Carling Cup final.

May - United regain Premier League title but go down 2-0 to Barcelona in Champions League final in Rome.

2010: February 28 - Helps United retain Carling Cup with 2-1 win over Aston Villa.

April 16 - Signs new one-year contract.

May - Helps United retain Premier League title. Rejects approach from England manager Fabio Capello to return to international football ahead of World Cup.

2011: April 16 - Sent off as United lose 1-0 to Manchester City in FA Cup semi-final at Wembley.

May 14 - Helps United win record 19th English league title.

May 28 - Part of the United side beaten 3-1 by Barcelona in Champions League final at Wembley.

May 31 - Reveals he is retiring from football to persue a career in coaching.

Wednesday, June 1, 2011

VIINGILIO VYA TANZANIA UNDER 23 VS NIGERIA VYATAJWA


Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itafanyika Jumapili (Juni 5, 2011) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili jioni. Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 1,000 kwa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa (orange straight and curve), sh. 5,000 kwa VIP C na B na sh. 10,000 kwa VIP A. Tiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa saa 2 asubuhi kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, Bigbon Msimbazi (Kariakoo), Steers (Mtaa wa Ohio na Samora), Uwanja wa Uhuru, Ubungo OilCom na vituo vya mauzo vya Premier Sports Betting. Nigeria itawasili Juni 3 mwaka huu kama ilivyo kwa waamuzi wa mechi hiyo kutoka Kenya na Kamishna kutoka Ethiopia. Mwamuzi ni Sylvester Kirwa ambaye atasaidiwa na Peter Kiereini, Aden Marwa na Davies Omweno wakati Kamishna ni Sahilu Gebremariam. Pia TFF kupitia Kurugenzi ya Masoko imepiga marufuku wachuuzi wa viburudisho kwenye mechi hiyo, isipokuwa kwa kampuni maalumu iliyopewa kazi hiyo. Hivyo vijana wote watakaofanya biashara bila kibali cha TFF watakamatwa. Suala hili pia linawahusu wachuuzi wa jezi za timu ya Taifa uwanjani.

MRWANDA NA ABDI KASSIM WAZUIWA KUJIUNGA NA STARS

Dan Mrwanda na Abdi Kassim ni miongoni wa wachezaji saba wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi walioitwa na kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen kwa ajili ya mechi dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itakayofanyika Juni 5 mwaka huu jijini Bangui. Klabu yao ya Dong Tam Long ya Vietnam imekataa kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na Stars kwa madai kuwa iko kwenye hali ngumu katika ligi yao. Timu hiyo inashika nafasi ya mwisho kwenye ligi ya nchi hiyo inayoshirikisha timu 14, hivyo kudai kuwa wachezaji hao ni muhimu kwao kuwaokoa kutoka mkiani. TFF tumepinga hatua hiyo kwa vile ni kinyume na Kanuni ya Hadhi na Uhamisho wa Wachezaji (Regulations of Status and Players Transfer), hivyo tutawasilisha malalamiko yetu kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

ENGLAND FA YASHINDWA KUUSIMAMISHA UCHAGUZI FIFA


Jaribio la England Football Association kutaka kuharishwa kwa uchaguzi wa uraisi wa shirikisho la soka duniani FIFA limeshindwa vibaya leo.

FA chairman David Bernstein alikuwa anawashawishi wajumbe 208 wa FIFA kusimamisha kwa uchaguzi ambao Sepp Blatter anagombea pekee yake kiti cha uraisi, lakini wajumbe wa FIFA wamepiga kura na matokeo ni kuwa kura 172 zilikubali uchaguzi uendelee na na kura nyingine zikimuunga mkono jaribio hilo la FA.

Uchaguzi wa FIFA unafanyika leo.



HAPPY BIRTHDAY CHICHARITO


Javier Hernandez was born on 1st June 1988 in Guadalaja Jalisco and he 1st played in a recreation league when he was 7 yrs old.

HAPPY BIRTHDAY Javier Hernandez Chicharito.

DE GEA, THE NEW VAN DER SAR OR THE NEW TAIBI

Kwa Manager ambaye ana rekodi ya kununua na kugundua vipaji vya wachezaji wakubwa kwa takribani robo karne, Sir Alex Ferguson's record linapokuja suala goalkeeper huwa anapata wakati mgumu kidogo.
Baada ya kuondoka kwa moja ya magolikipa bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya Man United, Peter Schmeichel mwaka 1999 ilimchukua miaka zaidi ya sita Ferguson kupata mbadala sahihi wa kipa huyo raia ya Denmark pale ambapo alikuja kumsajili Edwin Van Der Sar kutoka Fulham kwa paundi millioni 2.
Mark Bosnich, Paul Rachubka, Massimo Taibi, Fabien Barthez, Raimond van der Gouw, Andy Goram, Roy Carroll, Tim Howard, Ricardo and Nick Culkin wote walijaribu kuvaa gloves za Schmeichel lakini hazikuwatosha mpaka alipowasili Van Der Sar.
Sasa miaka 6 ya kuitumikia United kwa Van Der Sar imefikia ukingoni baada ya Mdachi huyo mwenye umri wa miaka 40 kuamua kutundika daluga na sasa Sir Alex Ferguson yupo katika mtihani mwingine wa kumtafuta mrithi sahihi wa mlinda mlango huyo ambaye ameichezea kwa mafanikio makubwa United.

Majina kadhaa yametajwa kumrithi Van Der Sar kuanzia Manuel Neurer, Marteen Stakelenburg, Hugo Lloris na David De Gea lakini hivi karibuni Sir Alex Ferguson ambaye amesema hataki kurudia makosa aliyoyafanya kipindi alipostaafu Schmeichel amemtaja David De Gea kuwa ndio mrithi sahihi wa Van Der Sar.

David De Gea ni moja ya magoli kipa bora kabisa katika ulimwengu wa soka kwa kipindi, ni raia wa Spain na anaichezea Atletico Madrid inayoshiriki La Liga., ana umri wa miaka 20.

Scouting team ya United inayoundwa na Jim Lawlor, Martin Ferguson(Mdogo wake Fergie), kocha wa magolikipa Eric Steele na Les Kershaw wamemthibitisha Da Gea Kuwa anafaa kuwa anafaa kumrithi Mdachi Van Der Sar.

Swali linaulizwa na wachambuzi wa soka duniani ni kwamba, pamoja na talent na potential aliyonayo Da Gea, je atakuwa mbadala sahihi wa Van Der Sar au atakuwa Massimo Taibi mpya, golikipa ambaye alifanya madudu makubwa aliposajiliwa kama mrithi wa Schmeichel.

Ferguson huwa na kawaida ya kuamini kuwa magolikipa wazuri ni ambao wana umri mkubwa, akisema ubora wao unazidi kuongezeka wanapofikia miaka ya 30 na kuendelea.Je golikipa kama Da Gea ambaye ameanza rasmi kucheza mashindano ya maana mwaka 2009 atakuwa na experience ya kutosha kuweza kulinda vizuri milingoti mitatu ya Old Trafford?

Mbadala wa Fabian Barthez, Tim Howard alisajiliwa akiwa miaka 24 na akafanikiwa kupata nafasi kikosi cha kwanza lakini akaishia kuisababisha United kupoteza mchezo dhidi ya FC porto katika robo fainali ya Champions League in 2004, na sasa ameamia Everton akiwa na miaka 32 kipaji chake kimeanza kuongezeka na kuzidi kuipa nguvu hoja ya Ferguson kuwa golikipa anakuwa bora kadri umri unavyokwenda.

Kwa upande wa Joe Hart mwenye umri wa miaka 24 amei-prove wrong falsafa ya Fergie kwa kuwa msimu bora kabisa akiwa na Manchester City baada ya kulinda vizuri milingoti ya Eastlands na kumuweka benchi Shay Given mwenye miaka 35, huku akifanikiwa kujipatia nafasi katika kikosi cha England chini ya Fabio Capello

De Gea is a superb shot-stopper, ana kipaji kikubwa na rekodi nzuri akiwa na Atletico na timu ya taifa ya Spain under 20, lakini anakosa experience na pia umri wake unapingana na falsafa ya Fergie kuhusu umri wa magolikipa bora.

Ukweli utathibitika kama De Gea ataweza ku-handle pressure ya kuichezea timu inayotajwa kuwa kubwa kuliko zote ulimwenguni., kama ataweza kufuata nyayo za Schmeichel na Van Der Sar na kuwa moja ya United Legend au atakuja kuwa kama Massimo Taibi

I



OFFICIAL: BIG SAM KOCHA MPYA WA WEST HAM


Kocha wa zamani wa klabu ya Bolton na Blackburn Sam Allardyce jana usiku amesaini mkataba wa miaka 2 wenye thamani ya paundi millioni 3 wa kuifundisha West Ham, ambayo imeshuka daraja msimu huu.

Allardayce ambaye amekuwa nje ya soka tangu alipofukuzwa kazi na Blackburn atakuwa ndio the highest paid boss katika ligi ya daraja la kwanza, na akifanikiwa kuirudisha the Hammers in Premier League atapata bonus ya paundi million 1.25.

Big Sam anategemea kutambulishwa rasmi wiki ijayo na ataanza kazi haraka ya kukijenga kikosi ambacho kitakuwa na uwezo wa kupambana kuirudisha timu hiyo in EPL.

Wamiliki wa West Ham David Sullivan, David Gold na Karren Brady wamemwakikishia Big Sam budget nzuri ingawa kuna wachezaji itabidi wauzwe ili waweze kui-boost mkwanja wa kununulia wachezaji wengine,.

Wachezaji wanaotajwa kuuzwa na pamoja na Robert Green, Scott Parker and Calton Cole ambao kwa pamoja wanaweza kuiingizia klabu paundi millioni 18 ambazo zitatumika katika kununulia wachezaji wengine ambao watapambana ili kuwarudisha wagonga nyundo hao London katika ligi ya England.


Monday, May 30, 2011

HIVI NDIVYO ILIVYOKUA MECHI YA SIMBA NA WAYDAD CASSABLANCA.



GOLI LA KWANZA LILIKUA HIVI.


.
GOLI LA PILI LILIKUA HIVI



GOLI LA TATU LILIKUA HIVI...

MCHEZAJI WA AZAM KIPRE TCHETCHE ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU YA IVORY COAST.




INTER MILAN YANYAKUA UBINGWA WA COPA ITALY.


Na huko nchini Italia hapo jana usiku Inter Milan imemaliza msimu kwa kujipooza na kombe la Copa Italia baada ya kuifunga Palermo kwa mabao matatu kwa moja.
Samwel Etoo Fiis alikuwa nyota wa Mchezo huo baada ya kufunga mabao mawili huku Diego Milito akifunga bao la tatu na la mwisho kwa Inter ambao walishindwa kutetea ubingwa wao wa Seria A msimu huu...

SHIRIKISHO LA MPIRA ULIMWENGUNI FIFA LA SIMAMISHA VIONGOZI KWA MDA USIOJULIKANA KWA KESI YA RUSHWA


Kimataifa,Kamati ya maadili na nidhamu ya shirikisho la soka duniani FIFA limewasimamisha kwa muda usiojulikana Jack Warner rais Chama cha Soka bara la Ocean na Rais wa Shirikisho la Soka barani Asia Mohamed Bin Hammam kufuatia tuhuma za rushwa zinazowakabili.
Akitangaza uamuzi huo makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Petrus Damaseb alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuwaona Bin Hammam na Warner wanakesi ya Kujibu huku Rais wa sasa wa FIFA Sepp Blater akionekana hana hatia.

BONDIA FRANSIC CHEKA AKATAA KUPIGANA NA BONDIA MARCUS UPSHOW KUTOKA NCHIN MAREKANI.


Bondia Francis Cheka amesema hawezi kupigana tena na Bondia Marcus Upshow kutoka nchini Marekani kufuatia ubabaishaji unaofanywa na Promota wa pambano hilo Shomary Kimbau ambaye amekuwa sio mkweli juu ya pambano hilo.
Cheka akizungumza na Kipindi cha Michezo cha Clouds Fm hapo jana alisema Kimbau ni Promota ambaye kwa sasa hana jipya kwani amekuwa akiwadanganya watanzania kuhusiana na pambano hilo wakati uwezo wa kuandaa umeisha mshinda.

WACHEZAJI WA SIMBA SPORTS CLUB WAKIWA MISRI KABLA YA MCHEZO WAO NA WAYDAD CASSABLANCA.


KIONGOZI WA SIMBA AZIM DEWIJI AKIWA AMEVAA JEZI YA TP MAZEMBE AKIFUATILIA MCHEZO WA SIMBA NA WAYDAD KATIKA UWANJA WA PETRO SPORTS STADIUM.








VIONGOZI WA TFF WALIONGOZANA NA TIMU YA SIMBA.

BENCHI LA UFUNDI LA WAYDAD WAKIFUATILIA MCHEZO HUO.

BENCHI LA UFUNDI LA SIMBA LIKIWA LINAFUATILIA MCHEZO HUO.

KIKOSI KAMILI CHA SIMBA KILICHOCHEZA NA WAYDAD.

OWINO NA WACHEZAJI WENZAKE WAKIWA HOTELINI.

AMIRI MAFTA NA KELVIN YONDANI.