Search This Blog

Saturday, August 10, 2013

SIMBA SC YAIFYATUA SC VILLA MABAO 4-1 UWANJA WA TAIFA KATIKA SIMBA DAYKiungo wa Simba, Amri Kihemba akimtoka beki wa Sports Club Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo., Simba imeshinda 4-1. (Picha na Habari Mseto Blog) 
 Kipa wa Sports Club Villa ya Uganda, Elungat Martins akiota mpira katika nyavu la lango lake baada ya mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki kuifungia timu yake bao la tatu katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Tunda Man, akitumbuiza katika tamasha hilo.

OFFICIAL: GERVINHO AHAMA ARSENAL BAADA YA MISIMU MIWILI - AS ROMA YAMNYAKUA KWA £8M


Usajili wa wachezaji mbalimbali unazidi kushika kasi barani ulaya.

Winga Mshambuliaji wa Ivory Coast, Gervais Lombe Yao Kouassi maarufu kama Gervinho amekamilisha uhamisho wa kuichezea As Roma ya Italia.

Gervinho alihamia Arsenal mwaka 2011 akitokea Lile ya Ufaransa. Uhamisho huo wa Gervinho umetajwa kuwa wa pound milioni 8 walizopewa Arsenal.

Msimu wake wa kwanza aliifungia Arsenal magoli manne kabla ya kufunga magoli saba msimu uliopita.

Amekuwa akipata ushindani wa kuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger, na huenda usajili wake wa kuhamia Seria A utakuwa changamoto mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

FRANCIS MIYEYUSHO ALIVYOMTANDIKA MZAMBIA KWA K.O JANA USIKU DAR LIVE


Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kulia  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane picha na SUPER D
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kushoto  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane picha na SUPER D
Bondia KaSIM rAJABU AKIPAMBANA NA kEVIN fABIAN WAKATI WA MPAMBANO WAKE ULIOFANYIKA SIKU YA SIKUKUU YA iDDI KATIKA UKUMBI WA dAR lIVE dAR ES SALAAM fABIAN ALISHINDA KWA pOINT
Bondia Godfrey Pancho kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Hamisi Mohamedi wakati wa mpambano wao uliofanyika sikukuu ya Iddi mosi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara
Bondia Godfrey Pancho kulia akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Hamisi Mohamedi wakati wa mpambano wao uliofanyika sikukuu ya Iddi mosi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara

Bondia Chipaki Chipindi akiwa na mashabiki wake baada ya kumkarisha raundi ya kwanza bondia Ramadhani Kido


Bondia Fidelis Lupupa wa Zambia akiwa chini amekaa akijifikilia kuwa aendelee au asienderee baada ya kupigwa na bondia Mtanzania Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane Picha na SUPER D
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kulia  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane picha na SUPER D
Bondia Fidelis Lupupa wa Zambia akiwa chini amekaa akijifikilia kuwa aendelee au asienderee baada ya kupigwa na bondia Mtanzania Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane Picha na SUPER D
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kushoto  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane picha na SUPER D

MIYEYUSHO AKISHANGILIA USHINDI

MIYEYUSHO AKIWA KATIKA POZI

MAKALA: CESC FABREGAS NA WACHEZAJI WATANO AMBAO WALIIKATAA MANCHESTER UNITED MSIMU HUU


Cesc Fabregas anakuwa mchezaji mwingine kukataa kujiunga na mabingwa wa ligi kuu ya England jana alhamisi wakati kiungo huyo alipothibitisha kwamba atabaki Barcelona msimu ujao.

Kiukweli, harakati za wazi za United kutaka kumsajili Fabregas siku zote lilionekana litashindikana, pamoja na utayari wa United kulipa £35 million ili kumsaini nahodha huyo wa zamani wa Arsena.


Moyes ana shauku wa kufanya usajili wa mchezaji mkubwa hasa kwenye nafasi ya kiungo kwenye dirisha hili la usajili. Hii nafasi imekuwa ni tatizo la muda mrefu hasa katika miaka ya mwisho ya utawala wa Sir Alex Ferguson hasa baada ya Darren Fletcher kuanza kuumwa na Paul Scholes kustaafu mara ya kwanza. 


Ndio, United wasingeweza kuendelea kutoa ofa mfululizo kwa Fabregas kama wasingepewa ishara kwamba mchezaji mwenyewe anaweza akavutiwa na kujiunga na klabu hiyo ya Trafford, lakini licha ya hivyo kauli kutoka Nou Camp tangu mwanzo wa dirisha la usajili ni kwamba kiungo huyo angebaki FC Barca angalau kwa msimu mmoja mwingine. 


Inaaminika United walimgeukia Fabregas mara baada ya kushindwa kumpata Thiago Alcantara, ambaye inasemekana alitakiwa na United japokuwa hakuwahi kufanya nao mazungumzo lakini mwishowe aliamua kumfuata kocha wake wa zaman Pep Guardiola huko Bayern Munich.

Lakini kabla ya wawili hawa, United tayari ilishakumbana na tatizo la kukataliwa na wachezaji wengine wanne waliowataka huko wakati dirisha la usajili lilipofunguliwa.

Kwanza, ofa ya £35m kwa ajili ya kiungo wa Real Madrid Luka Modric ilikataliwa na magwiji hao wa soka la Hispania mwezi uliopita, wakati huo huo pia kwa usiri mkubwa United waliwafuata viungo wa Juventus Claudio Marchisio na Artulo Vidal, na kiungo wa Paris Saint-Germain Marco Verratti, kote huku waligonga mwamba.  


United walipewa ishara kwamba Verratti alikuwa tayari kutoka PSG kwenda Juventus na sio timu yoyote jambo ambalo liliwapelekea United kuangalia upatikanaji wa viungo wa mabingwa wa Italia Vidal na Marchisio. Kwa haraka Juventus  walikawakatisha tamaa United kwa kuwaambia wachezaji hao hawauzwi.

Wakati pia hatma ya Wayne Rooney ndani ya klabu hiyo ikiwa inawasumbua - Moyes sasa hana jinsi zaidi ya kuangalia 'Plan F'.

Marouane Fellaini - ambaye siku zote ndio amekuwa wa mwisho kwwenye listi ya United ya viungo wanaowataka na kwa hali ilivyo inaonekana kwamba mbegijia huyu atamfuata kocha wake wa zamani Old Trafford akitokea Everton. 


Moyes anavutiwa na Fellaini mwenye miaka 25, kiungo mwenye nguvu na ana uzoefu wa premier league, lakini kama Fellaini angekuwa ndio kipaumbele basi wangekuwa wameshamsajili miezi miwili iliyopita.

Fedha inayohitajika kuvunja mkataba wa Fellaini na Everton ni £22m - ni kipengele hicho tayari kimeshakwisha muda wake - hivyo sasa itahitajika United kuanza majadiliano mapya kabisa na Everton katika kuhakikisha wanakubaliana bei ya mchezaji huyo. 


Wakati Fellaini ni mtu ambaye sifa zake zinampa nafasi ya kuweza kufiti kwenye mfumo wa United, lakini sio dizaini ya mchezaji (kijina) ambaye mashabiki wa United wangependa kuona Moyes akifungua utawala akiwa nae.

Zoezi la Moyes kuanza utawala wake mpya limekuwa gumu kwa kutofanikiwa kwa mipango yake ya usajili - lakini pia kukiwa na suala la Wayne Rooney.

Pia imekuwa shida sana kwa mkurugenzi mkuu mpya wa klabu hiyo Ed Woodward kurithi vizuri mikoba ya David Gill - akiwa tangu aingie madarakani United haijasajili. 


United ilishinda vizuri sana kombe la ligi msimu uliopita, lakini wanahitaji kufanya usajili mkubwa na wenye tija kabla ya kufunguliwa kwa pazia la lligi kuu dhidi ya Swanse - August 17.

Mpaka sasa sera ya United katika usajili imeanza kuonyesha kufeli - ingawa huwezi kuwalaumu kwa hamu yao ya kutaka kusajili mchezaji ambaye tayari ni miongoni wa wale waliobora duniani.                                                          

Friday, August 9, 2013

MMILIKI WA LIVERPOOL ASEMA "KUWAUZIA SUAREZ ARSENAL UTAKUWA NI UPUMBAVU - HAENDI POPOTE DIRISHA HILI LA USAJILI."


Luis Suarez amezidi kupata vizingiti vikubwa katika harakati zake za kutaka kuhama Liverpool, baada ya kuambiwa na mmiliki wa Liverpool John Henry warning: “Huendi popote”.

Mmiliki huyo wa Liverpool amesema kwamba ni upumbuvu kuanza hata kufikiri kufanya biashara na Arsena ya mshambuliaji huyo wa Uruguay.
Na mmarekani huyo amesema kwamba kitendo alichokifanya Suarez kilivuka mipaka, huku akisisitiza kwamba mshambuliaji huyo hatouzwa kwenda klabu yoyote mpaka dirisha la usajili litakapofungwa September 2 - pia akisema uamuzi wa kutokumuuza Surez hautokani na masuala ya fedha. Henry alisema: “Hatuwezi kumuuza Luis. Ni kwa sababu za kisoka kabisa, na sio masuala ya fedha.

“Hii ni kwasababu mpaka sasa ni vigumu kupata mchezaji wa kuziba pengo lake kwa maana wachezaji wazuri wote wameshahama. Hivyo ni sababu za kisoka, hatuwezi kumuuza - hasa kwa klabu ya Arsenal.

“Kuwauzia mahasimu wetu mchezaji huyu utakuwa ni upumbavu kabisa."

JOSE MOURINHO: "HATUTOKATA TAMAA KATIKA MPANGO WA KUMSAJILI ROONEY - TUTAFANYA KILA NJIA KUMLETA STAMFORD BRIDGE"


Jose Mourinho amesisitiza kwamba atapigana mpaka siku ya mwisho katika jaribio lake la kumsaini Wayne Rooney.
Chelsea tayari walishatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa na  Manchester United, ofa ya mwisho inayotajwa kuwa ni zaidi ya paundi million 25 ilitumwa jumapili. Lakini Mourinho alisema: "Hatuna kizuizi cha muda kwenye suala hili. 

‘Tumemuona Rooney kama ni mchezaji ambaye tungependa kuwa nae. Tumefanya kila kitu katika utaratibu unaopaswa na tutafanya hivyo mpaka siku ya mwisho ya usajili. Tunafnya kila kitu tukizingatia sheria, kutoa ofa rasmi kwa klabu moja kwa moja.
‘Hakujawahi kuwepo kwa mawasiliano na mchezaji, hakijatokea kitu kama hicho. Tusubiri tuone kama mambo yatabadilika.’ 
Rooney inaaminika kwamba amemwambia kocha wake David Moyes kwamba anataka kuondoka, lakini United imekuwa ikisisitiza kwamba hauzwi. 

Thursday, August 8, 2013

RAISI WA REAL MADRID: " £100 MILLION KWA AJILI YA KUMSAINI GARETH BALE NI FEDHA NYINGI SANA"

Raisi wa Real Madrid Florentino Perez ameonyesha wazi kutokubaliana na dau wanalolitaka Tottenham kwa ajili ya Gareth Bale, akisema ada ya uhamisho wanayotaka Spurs ni nyingi sana kwa thamani halisi ya Bale.

Mwenyekiti wa Daniel Levy alifanya mazungumzo na Raisi wa Madrid huko Florida wiki hii, huku klabu ya kaskazini mwa London akisemekana  kuihitaji £100 million kwa ajili ya kumuuza mshindi wa tuzo za PFA na FWA Player of the Year.


Lakini Perez amezungumza na kutoa maelezo yanayoonyesha dili la uhamisho wa Bale lipo mbali na kukamilika, na ameshangazwa sana na ada ya uhamisho wanayotaka Tottenham kwa winga huyo mwenye miaka 24.

Katika mahojiano na kituo cha ESPN, Perez alisema : "Tumeongea na watu wengi sana na ngoja tusubiri tuone nini kitatokea katika mazungumzo yetu - na huyu mchezaji [Bale] na wengineo.

"Hatuzungumzii kuhusu wachezaji wengine kwa heshima ya mchezaji, klabu na Raisi wa klabu bwana Levy, ambaye ni rafiki yangu wa dhati, ambaye nimejenga nae mahusiano mazuri tangu msimu uliopita wakati tulipomnunua Luka Modric.

"Kama sitaki kutaja majina, pia siwezi kutaja kuhusu kiasi cha pesa...... ikiwa unasema 100 million, basi hizo ni fedha nyingi sana kwa kitu chochote sio mchezaji husika tu - lakini kwa heshima niliyonayo kwa klabu ya Totenham sitotaka kuendelea kulizungumzia suala hili...."

BREAKING NEWS: FABREGAS AIKATAA RASMI MAN UNITED - ASEMA ANAHESHIMU KUMHITAJI KWAO LAKINI ANA FURAHA BARCELONA NA ANGEPENDA KUBAKI.


Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas hatimaye amevunja ukimya kuhusu suala la Manchester United kutaka kumsajili kwa kusema anataka kubaki nchini Spain.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Kuala Lumpur mahala ambapo  Barcelona wapo kwa ajili ya maadalizi ya msimu mpya. 

Fabregas alisema: 'Ndoto yangu siku zote imekuwa kuichezea Barcelona na hakuna kilichobadilika. Nina furaha sana kuwa hapa na sijawahi kufikiria kuhusu kuondoka.

"Sijawahi kuwa na shaka juu hilo. Haijanigharimu chochote kurudi Barcelona na sasa nataka kuwa mshindi nikiwa hapa.  

'Ni heshima kubwa kwa Manchester United kuleta ofa mbili kwa ajili yangu, lakini hakujawahi kuwa na mazungumzo. Sijawahi kuongea na klabu yoyote tangu nimejiunga na Barcelona miaka miwili iliyopita.
'Siku zote nimekuwa nikitambua ninavyothaminiwa na klabu. Kila mut ameniambia namna anavyonitegemea, sijwahi kupata ishara yoyote tofauti ya kuhisi sihitajiki.
'Sikutaka kusema lolote huko mwanzo kwa sababu kwangu mimi kila kitu kilikuwa wazi kwamba nilikuwa nataka kuendelea kubaki hapa. Niliiambia klabu nitaongea itakapofika zamu yangu.
'Kuna baadhi ya vitu vilitengenezwa, lakini havikuwa vya kweli - hasa la kusema kwamba nimeomba kuongezewa mkataba,' alisisitiza Cesc Fabregas

BAADA YA SUAREZ: SASA WAYNE ROONEY NAE AONDOLEWA KUFANYA MAZOEZI NA KIKOSI CHA KWANZA CHA UNITED - APELEKWA KIKOSI CHA PILI

Siku moja baada ya Liverpool kumuondoa Luis Suarez kama mazoezi ya kikosi cha kwanza na kumlazimisha kufanya mazoezi pekee yake, leo hii Wayne Rooney nae amefanyiwa kitendo hicho hicho na kocha wake wa Manchester United David Moyes kwa kumpeleka mshambuliaji huyo anayetaka kuondoka kufanya mazoezi na kikosi cha pili cha timu ya mabingwa wa England. 

Rooney alikuwa ndio mchezaji pekee wa kikosi cha kwanza kilichokuwa kikifanya mazoezi na wachezaji wa ziada katika uwanja wa mazoezi Carrington, in a session chini ya usimamizi wa makocha Warren Joyce na Nicky Butt.

Mchezaji huyo anayetakiwa kwa udi na uvumba na Chelsea leo alienda mazoezini asubuhi akitegemea kufanya mazoezi na wachezaji wenzie wa kikosi cha kwanza lakini akaondolewa na Moyes na kupelekwa wanapofanya mazoezi wachezaji wa kikosi cha pili.

CRISTIANO RONALDO AITUNGUA CHELSEA MABAO MAWILI NA KUMWAMBIA MOURINHO - "NAPENDELEA KUZUNGUMZA KUPITIA MATENDO YANGU YA UWANJANI"

Cristiano Ronaldo alikuwa na sababu nyingi zaidi ya kushangilia goli lake katika mechi ya pre-season - na kumuonyesha boss wa Chelsea Jose Mourinho aliyemdhiaki kabla ya mchezo kwamba yeye ni "Ronaldo" wa aina gani.

Ronaldo alifunga mabao mawili na kuiwezesha Real Madrid kuifunga 3-1 Chelsea katika Guinness International Champions Cup jijini Miami.

Baada ya goli lake la kwanza alilofunga kwa mkwaju wa faulo, hakushangilia bali aligeuka mbele ya jukwaa la mashabiki na kuonyesha kifua chake huku akitikisa kichwa.
 Baada ya mchezo huo Ronaldo alizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maneno ya maneno Mourinho kwamba Ronaldo orijino ni yule wa Brazil - Cristiano alisema: "Napendelea kuzungumza kwa vitendo vyangu vya uwanjani na sio mara pengine popote"


BAADA YA KUIPAKA LIVERPOOL - LUIS SUAREZ AAMRIWA KUFANYA MAZOEZI PEKE YAKE - BRENDAN ROGERS AKANA KUMPA AHADI YA KUONDOKA IKIWA HAWATOKUWA TOP 4


Mshambualiaji wa Liverpool Luis Suarez amepewa amri ya kufanya mazoezi peke yake na kocha Brendan Rodgers, ambaye amesema hatua hiyo inakuja baada ya mshambuliaji huyo kuikosea heshima klabu hiyo. 
Rodgers pia amekataa taarifa alizotoa Suarez kwamba klabu ilimhaidi kwamba ikiwa Liverpool watafeli kufuzu kucheza Champions League.
Suarez, 26, anajipanga kuwasilisha ombi rasmi la kuuzwa wiki hii ikiwa uhamisho wake utazuiwa. 
"Hakujawahi kuwa ahadi yoyote ya namna hiyo baina yetu - kwa kifupi ahadi yoyote, na kwa maana hiyo hakuna ahadi iliyovunjwa," alisisitiza Rodgers.
"Klabu na wawakilishi wake walikuwa na mazungumoz kadhaa na alijua kila kitu kilivyokuwa kinaendelea .
"Ameikosea sana heshima klabu - lakini klabu hii ilimpa na kumfanyia kila kitu. 
"Maneno yake niliyoyasoma kwenye vyombo vya habari yamenisikitikisha sana - lakini kazi yangu ni kubwa zaidi ya hili suala. "
Vyanzo vya karibu na Liverpool vinasisitiza uamuzi wa kumlazmisha Suarez afanye mazoezi kimpango wake ulifanywa kabla hata mchezaji huyo hajaongea jana na vyombo vya habari, hivyo uamuzi huo umetokana na kucheza kwake chini ya kiwango kwenye mechi za kirafiki. 
Rodgers aliongeza: "Nitachukua maamuzi magumu juu ya suala hili. Nadhani Luis anajua sapoti aliyokuwa akipata kwenye klabu hii na hilo limekuwa jambo la siku zote.

"Kazi yangu ni kupigana na kuilinda klabu hii. Mazungumzo niliyokuwa nayo na yeye, anajua yalikuwa na yataendelea kuwa binafsi kati yangu na yeye."

Wednesday, August 7, 2013

MANJI AITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA WA WANACHAMA WA YANGA KUJADILI KUHUSU DILI LA AZAM TV


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

1.   Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu (Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016

2.   Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha kuwamkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani na Azam Media.

Kwa kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGAhaina tatizo na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom Premier League katika Azam Television.

3.   Sote tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada” inatumika kupotosha msimamo wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA hadharani.

Juu ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu zinazojionyesha wazi.

Inadhihirika wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.

Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.

Kwa kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha mechi za YANGA.(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB

MOYES: "SIHITAJI KUMSHAWISHI WAYNE ROONEY AU MCHEZAJI YEYOTE KUICHEZEA MANCHESTER UNITED"


Huku tetesi mpya zikizuka kila siku juu ya hatma ya mshambuliaji  Wayne Rooney, kocha wa Manchester United David Moyes amesema jana Jumanne kwamba hahitaji kumshawishi mshambuliaji aendelee kubaki Old Trafford.
Alipoulizwa kuhusu namna Wayne Rooney alivyolipokea suala la United kukataa ofa mpya ya Chelsea ya £30m kwa ajili kumsajili, Moyes alisema, "Sijui, sijamuuliza kuhusu suala hilo."

Pia wakati akijibu swali la kama atamshawishi nyota huyo wa England aendelee kubaki kuitumikia klabu hiyo inayojinadaa kutetea ubingwa wake wa EPL, Moyes alisema: "Huhitaji kumshawishi mtu yoyote kuichezea Manchester United."
Moyes alikuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo wa kirafiki ulioisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya AIK jijii Stockholm.

LUIS SUAREZ: "TULIKUBALIANA NA LIVERPOOL IKIWA TUTASHINDWA KUFUZU CHAMPIONS LEAGUE WATANIUZA - SASA NATAKA WAHESHIMU AHADI YAO NA KUNIUZA"

Luis Suarez ameiambia klabu yake ya Liverpool kuheshimu makubaliano yao ya kumruhusu kuondoka endapo klabu hiyo isingeweza kufuzu kucheza klabu bingwa ya ulaya msimu huu unaokuja.

Mshambuliaji huyu amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu vya Arsenal huku ofa mbili tayari zikiwa zimekataliwa na Liverpool - ikiwemo ya £40m ambayo mshambuliaji huyo anasema ilitenguwa kifungu cha kumruhusu kuuzwa kwenye mkataba wake ambao alisaini miezi 12 iliyopita.

"Mwaka jana nilipata nafasi ya kujiunga na klabu kubwa barani ulaya lakini niliamua kubaki kwa maelewano kwamba ikiwa msimu huu ingeshindikana kufuzu kucheza Champions League basi ningeruhusiwa kuondoka," Suarez ameliambia gazeti la Guardian.

"Nilijitoa kwa yote msimu uliopita lakini haikutosha kutufanya kumaliza kwenye top 4 - sasa ninachokitaka ni Liverpool kuheshimu maelewano yetu."

Suarez pia ameonyesha wazi yupo tayari kuipeleka kesi yake kwa kamati ya Premier League ili kuhakikisha azma yake inafanikiwa.
Aliendelea: "Walinipa ahadi na tuliandika mkataba kuhusu hilo na sasa nipo tayari kulipeleka hili suala Premier League ili wao waamue kesi hii lakini sihitaji suala hili lifikie huko.
"Sidhani kama nimesalitiwa, lakini klabu iliniahidi mwaka mmoja uliopita na mimi nilifanya hivyo kwa kuwaambia kama tutafuzu ikiwa tungepata nafasi ya kushiriki Champions League.

"Walinipa ahadi hiyo mwaka mmoja uliopita na sasa nataka waheshimu ahadi yao. Sio kitu tulichokubaliana kwa mdomo tu bali kiandikwa kwenye mkataba. Siendi kwenye kwenye klabu nyingine ili kuiumiza Liverpool."

BAADA YA KAKA YAKE KUITIKISA DUNIA KWENYE SOKA - DADA WA CRISTIANO RONALDO AANZA KUFANYA VIZURI KWENYE MUZIKI WA KIMATAIFA - HUU NDIO WIMBO WAKE


Dada wa damu wa mwanasoka ghali zaidi duniani Cristiano Ronaldo amesaini mkataba mnono wa kutengeneza albam yake ya kwanza ya muziki na kampuni ya utayarishaji ambayo hufanya kazi na wasanii wakubwa kama Lady Gaga na J-LO.

Katia Aveiro ambaye single yake ya kwanza "Boom sem parar" imepata umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Youtube, tayari ameanza kuunda albam yake na watayarishaji kutoka RedOne huko jijini Madrid - mahala ambapo ndio ameweka makazi yake ya kikazi.

Ronaldo, ambaye jana alipigwa picha akiwa na mwanamuziki J-LO amezungumza kuhusu dili hilo la dada yake na kusema: "Nina furaha sana kwa ajili yake."

Aveiro anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha kubwa mwezi ujao jijini Madrid huku albam yake ya kwanza ikitarajiwa kutoka mwezi November. Alisema: "Huu ni mwanzo wa muziki wangu kuwa wa kimataifa." 


HII NDIO VIDEO YA WIMBO WA KATIA AVEIRO

COASTAL UNION YAMSAINISHA MGANDA ALIYEZINYANYASA SIMBA NA YANGA KUTOKA URA
Klabu ya Coastal Union imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kiganda Yayo Lutimba kutoka timu ya mamlaka ya mapato ya Uganda URA. 

Aliyefanikisha zoezi hilo ni meneja wa Wagosi, Akida Machai ambaye amepanda ndege mpaka jijini Kampala kunasa saini ya kijana mdogo mwenye miaka 19, Yayo Lutimba Kato kutoka timu ya mamlaka ya mapato Uganda (URA).

Nassor Ahmed ‘Binslum’, ambaye ni mkurugenzi wa ufundi amesimamia kwa kiasi kikubwa kufanikisha usajili wa wachezaji takriban tisa ukijumlisha na Kato amezungumza na blog hii usiku wa leo baada ya Meneja Machai kuenda kumtambulisha Kato kwa Binslum na kuweka wazi kuwa tatizo la ukame wa mabao litaisha kwa wana Mangush.

Itakumbukwa kocha Mkuu wa Coastal Union, Hemed Morocco wiki chache zilizopita wakati wa kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA, aliweka wazi bado kikosi chake kina matatizo ya umaliziaji.

Alibainisha kikosi hicho kipo vizuri kila idara kuanzia golikipa, mabeki na viungo ila hakuna mtu mwenye uchu wa mabao hivyo kuahidi kuwatumia wachezaji haohao kuwafundisha namna ya kuadhiri magolikipa wa timu pinzani.

Ndiyo maana winga Danny Lyanga alikuwa akichezeshwa namba kumi ili kumuangalia uwezo wake wa kupachika mabao lakini hakuonekana kucheza vema kwenye mechi ya URA.

Kwa usajili wa miaka miwili kuitumikia Coastal Union kinda huyu atakuwa na nafasi nzuri sana kujitengenezea jina nchini Tanzania hasa baaada ya kuwa na rekodi nzuri ya kuwafunga Simba na Yanga mabao mawili mawili katika mechi walizokutana nazo kwa vipindi tofauti.

Zipo taarifa kuwa Yanga nao walikuwa mbioni kumnyakua kinda huyu lakini Meneja Akida Machai amewazidi akili kwa kumfuata hukohuko kwao Uganda. Na hizi ni mbinu za ‘kimafia’ zinazotumiwa na timu kubwa duniani kote kunasa wachezaji mahiri.

Mungu akipenda kesho Kato ataungana na wachezaji wenzake katika kambi iliyopo pembezoni mwa bahari ya hindi Raskazone Hotel, jijini Tanga.

Wagosi wameanza vizuri mechi zao mbili za majaribio ambapo mechi ya kwanza walishinda bao 1-0 dhidi ya URA na siku tatu baadaye wakashuka dimbani dhidi ya Simba SC ambao nao walichapwa 1-0. Zipo taarifa za kucheza mechi ya kirafiki siku ya Eid pili uwanja wa Mkwakwani lakini zikishathibitishwa na timu tutakayocheza nayo tutawahabarisha.

HABARI KWA HISANI YA COASTAL UNION BLOG

Tuesday, August 6, 2013

EXCLUSIVE: MUSSA HASSAN MGOSI ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA WA KUICHEZEA MTIBWA SUGAR - MEXIME ATHIBITISHA

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Mussa Hassan Mgosi amejiunga rasmi na klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro.

Mgosi ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia klabu ya JKT Ruvu amejiunga na Mtibwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Akiongea na mtandao huu, kocha wa Mtibwa Sugar  Mecky Mexime amethibitisha kwamba klabu yake imemsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, "Mgosi anakidhi vigezo vya mshambuliaji tunayemhitaji baada ya kuondoka wa Javu aliyejiunga na Yanga. Ameshaini mkataba wa mwaka mmoja na atajiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya hivi karibuni."

PATRICK OCHAN ATEMWA TP MAZEMBE - ASHINDWA KUKIDHI MAHITAJI YA TIMU

Takribani miaka miaka mitatu tangu asajiliwe kwa mamilioni ya fedha kutoka klabu ya Simba ya Tanzania, kiungo wa kimataifa wa Uganda Patrick Ochan ametemwa na klaby yake ya TP Mazembe, kutokana na kutokidhi mahitaji ya klabu hiyo. 

Ochan, kwa pamoja na mganda mwenzie Mike Mutyaba ambaye alisajiliwa kutoka El Merrick, wameripotiwa kurudi kwao Uganda kwa sasa wakati TP ikiwa bado ianshiriki kwenye michuano ya CAF.

Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa TP Mazembe, wachezaji hao wawili wameruhusiwa kutafuta timu za kucheza za mkopo.

Ochan, tayari amehusishwa kutaka kujiunga na klabu ya KCCA kwa mkopo na tayari wameshaaanza mazungumzo, KCCA inashiriki michuano ya CAF Champions League msimu.

DR Congo football giants, TP Mazembe, have offloaded Ugandan duo, Mike Mutyaba and Patrick Ochan, due to failure to match the standards of the football club. - See more at: http://chimpreports.com/index.php/sport/11975-tp-mazembe-offload-mike-mutyaba-patrick-ochan.html#sthash.WaKL8ZFC.dpuf
DR Congo football giants, TP Mazembe, have offloaded Ugandan duo, Mike Mutyaba and Patrick Ochan, due to failure to match the standards of the football club. - See more at: http://chimpreports.com/index.php/sport/11975-tp-mazembe-offload-mike-mutyaba-patrick-ochan.html#sthash.WaKL8ZFC.dpuf

HATIMAYE WANAIGERIA WA YANGA WARUHUSIWA KUCHEZA MECHI ZAO TANZANIA

Timu ya 3Pillars Football Club ya Nigeria sasa inaruhusiwa kucheza mechi za kirafiki nchini baada ya kupata idhini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nigeria (NFF).

Awali tuliikatalia timu hiyo kucheza mechi za kirafiki nchini kwa vile haikuwa na barua kutoka NFF, lakini sasa Shirikisho hilo limetoa idhini hiyo. Pia ziara yake haikuwa inaratibiwa na wakala wa mechi anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) au mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Klabu hiyo kutoka Jimbo la Lagos ilipanga ziara hiyo kwa kuwasiliana na chama cha mpira wa miguu cha jimbo hilo ambacho nacho kilitakiwa kuomba idhini NFF kwa niaba ya 3Pillars.

Hivyo timu hiyo inaweza kucheza mechi, kwani ziara hiyo sasa inaratibiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambaye ni mwanachama wetu.

Tunapenda kukumbusha kuwa watu pekee wanaotakiwa kuandaa mechi za k

PATA MAHOJIANO YA GEORGE MASATU ALIYOFANYA NA MICHUZI TV.

PHOTOS OF THE DAY: CRISTIANO RONALDO NA JLO - NA SHAQUILLE O'NEALVIDEO: ANGALIA YANGA ILIVYOIFUMUA 3-1 MTIBWA SUGAR

EXCLUSIVE: MWINYI KAZIMOTO: "NIMEILIPA SIMBA $40,000 ILI NICHEZE SOKA QATAR - NAOMBENI MSAMAHA KWA KUTOROKA"

Wiki kadhaa baada ya kutoroka nchini na kukimbilia nchini Qatar kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa, leo hii kiungo wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba Mwinyi Kazimoto amezungumza rasmi na mtandao huu na kutoa taarifa nzima ya kuhusu sakata lake la kutoroka.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Doha Qatar na Shaffih Dauda, Mwinyi Kazimoto kwanza amekiri kwamba alitoroka kwenda Qatar kwa nia ya kwenda kufanya majaribio, "Safari yangu ya kuja huku Qatar ilibidi iwe kabla hata sijacheza mechi ya marudiano na Ivory Coast, lakini kwa sababu nilikuwa na majukumu nilivumilia nikabaki mpaka nilipocheza mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda, wakati tukiwa kambini kwa ajili ya mchezo wa pili ikabidi niondoke kwa sababu siku zilikuwa zinaenda na muda wangu wa kufanya majaribio ukawa unaisha," anazungumza Kazimoto

Alipoulizwa kama tayari ameshafuzu majaribio aliyoenda kufanya kiungo huyo wa zamani wa JKT Ruvu alisema: "Mwanzoni nilipata vilabu viwili vinavyoshiriki ligi daraja la kwanza ya huku, lakini nikachelewa majaribio na hivyo nikakosa nafasi. Baada ya hapo ndipo ikajitokeza timu ya Al-Markhiya Sports Club - inayoshiriki ligi ya daraja la pili na ikavutiwa nami na ikafanya mipango ya kunisajili."

Taarifa nchini zimeenea kwamba klabu ya Simba imepokea kiasi cha $35,000 kwa ajili ya kumuuza kiungo huyo, Je Kazimoto anasemaje juu ya hili? "Ni kweli kutokana na kwamba nilikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Simba ilibidi nitoe kiasi cha fedha ($40,000 na sio $35,000 kama inavyoripotiwa) kutoka kwenye ada ya usajili wangu kuununua mkataba wangu uliobakia na Simba.


"Sasa hivi nimefanikiwa tayari kupata timu hii lakini ndoto yangu ni kujitahidi na kuweza kucheza ligi ya juu kabisa hapa. Vilevile ningependa kuwaomba radhi watanzania wote na klabu yangu ya Simba kwa kitendo cha kutoroka wakati nikiwa nahitajika. Nafasi ya kucheza soka la kulipwa ilikuwa ni muhimu kwa maisha yangu na sikutaka niipoteze hivyo naomba wanielewe na kunisamehe."ANGALIA VIPANDE VYA MARUDIO YA MCHEZO WA SIMBA NA POLICE COMBINE - MABAO

Monday, August 5, 2013

PICHA ZA UTAMBULISHO WA ROBERTO SOLDADO BAADA YA KUKAMILISHA UHAMISHO WA KUJIUNGA NA TOTTENHAM HOTSPUREXCLUSIVE: MWINYI KAZIMOTO AKIWA NA RAUL GONZALEZ BLANCO MAZOEZINI QATAR - AONGEA RASMI KUHUSU HATMA YAKE

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba Mwinyi Kazimoto akiwa na Gwiji wa soka wa Hispania na Real Madrid Raul Gonzalez huko Qatar alipokuwa ameenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. Mtandao huu umepata nafasi ya kuongea na Kazimoto na kwa kifupi ameomba radhi kwa kutoroka - pia amesema amefanikiwa kupata timu huko alipo. Je ungependa kujua Simba imelipwa shilingi ngapi kwenye uhamisho huu wa Kazimoto???? - Endelea kutembelea mtandao huu.RAISI WA BARCELONA: MCHEZAJI YOYOTE ANAWEZA KUUZWA LAKINI SIO LIONEL MESSI - LABDA KWA ADA YA UHAMISHO WA €580 MILLIONI"


Raisi wa Barcelona Sandro Rosell amesema klabu yake kamwe haitoweza kumuuza Lionel Messi, na alipoulizwa kama ni bei gani ambayo inaweza kubadilisha uamuzi wa klabu ajibu kwa kifupi tu  "€580 million".
Akiongea katika mahojiano na gazeti la Sport.es, Sandro Rosell alisema: “Wachezaji wote wanaweza kuondoka ikitokea tumepata ofa nzuri yenye tija kwetu lakini sio Messi. Labda tulipwe kiasi cha  €250 million ($332 million) kama ada yetu, pamoja na asilimia 56 ya fedha hizo kwa ajili ya kulipa kodi. Hivyo itabidi alipe kiasi cha  €580 million.”

Kwa maana hiyo ili kumsajili Lionel Messi itabidi klabu inayomtaka ilipe fedha ambazo ingeweza kununua vilabu viwili kama Fulham - ambayo ilinunuliwa na billionea a kimarekani Shahid Khan kwa ($230 million).

Pia kwa kauli hiyo ya Rossell inaonekana FC Barcelona wapo tayari kumuuza mchezaji yoyote kwenye kikosi chao ikiwemo Cesc Fabgregas anayetakiwa na United ikiwa tu watapewa ofa itakayowaridhisha.

HATIMAYE KATIBA YA TFF YASAJILIWA NA MSAJILI - TENGA ASHUKURU


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amemshukuru Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini kwa kusajili Katiba ya TFF toleo la 2013 kutokana na marekebisho yaliyofanywa na Mkutano Mkuu Maalumu uliofanyika Julai 13 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Agosti 5 mwaka huu), Rais Tenga ameishukuru Serikali, Msajili, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Naibu wake Amos Makala na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ushirikiano ambao wametoa kwa TFF katika kufanikisha suala hilo.
Amesema baada ya kupokea usajili huo, kinachofuata ni Katibu Mkuu wa TFF kumwandikia rasmi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ili aanzishe mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TFF.
Kuhusu kauli ya Naibu Waziri Makala kuwa marekebisho hayo yasingeweza kusajiliwa kwa sababu hayakufuata Katiba ya TFF, Rais Tenga amesema alikuwa ana haki ya kusema hivyo kwa sababu hakuwepo kwenye Mkutano huo, na kuongeza:
“Makala hakuwepo kwenye mkutano ndiyo maana alisema hivyo. Ana haki ya kuuliza, nina hakika sasa atakuwa ameeleweshwa na ameelewa kwa sababu ni msikivu. Kuhusu marekebisho hayo kupigiwa kura, hilo lisingewefanyika kwa sababu hakukuwa na mjumbe aliyepinga marekebisho,” amesema.
Rais Tenga amesema marekebisho hayo yalipitishwa kwa kauli moja (unanimous) hivyo hakukuwa na sababu ya kuanza kunyoosha mikono kupiga kura, kwa maana hiyo mkutano ulipitisha marekebisho kwa asilimia 100 wakati Katiba ilikuwa ikihitaji theluthi mbili tu.
“Hakukuwa na dispute (mabishano) kuhusu marekebisho, isipokuwa wajumbe walitumia muda mwingi kuboresha kanuni na kutoa ushauri wa aina ya watu ambao wangeingia kwenye kamati mbalimbali zikiwemo zile mpya za Maadili,” amesema.
Ameongeza kuwa kwa vile wote walioingia kwenye Mkutano Mkuu huo Maalumu ni watu wa mpira wa miguu wasingeweza kupinga marekebisho kwa vile yametokana na maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
“Labda itokee aliyeingia kwenye mkutano alikosea njia. Mtu yeyote wa mpira wa miguu ni lazima afahamu kuwa maagizo ya FIFA ni lazima yatekelezwe, na Katiba ya TFF inasema hivyo,” amesema Rais Tenga.
Pia Rais Tenga amewataka wapenzi wa mpira wa miguu kushawishi watu wenye sifa na uwezo wa kuongoza kujitokeza kwa wingi wakati Kamati ya Uchaguzi itakapotangaza mchakato na tarehe ya uchaguzi huo.

CLOUDS MEDIA GROUP YAPATA IFTAR YA PAMOJA NA WADAU WAKE

 
 Kampuni ya Clouds Media Group mwishoni mwa wiki iliandaa Ftari ya pamoja kwa wafanyakazi wake na baadhi ya wadau mbalimbali,maeneo ya Sinza-jijini Dar Salaam.Pichani kushoto ni  Mkurugenzi wa vipindi na utafiti,Ruge Mutahaba pamoja na Meneja Vipi wa Clouds FM Sebastian Maganga wakiongoza wageni waalikwa mbalimbali kupata ftari.Pichani chini ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wadau wengine waalikwa wakijipakulia ftari safi kabisa.


Sehemu ya Wadau wakiendelea kupata ftari.Picha na Jiachie Blog.

BASKETBALL ALL STARS BONANZA ILIVYOFANA:

Jumamosi ya Tarehe 3,August 2013 Inaingia katika kitabu cha Kumbukumbu kwenye Ulimwengu wa Kikapu Tanzania baada ya Tamasha la mpira wa Kikapu liliolandaliwa na Vijana city bulls kwa ushirikiano na wadau wa Kikapu Tanzania kuonekana kufana Sana.Bonanza hilo Lililoshirikisha Wachezaji wakali wa Kikapu Jijini Dar es salaam.Likisindikizwa na Burudani ya Muziki Bonanza hilo lilishuhudia mechi mbali mbali za Kufurahisha na kuhamasisha sana
Akitoa Mchango wake kwa Moyo Moja MCHEZAJI wa Mpira wa Kikapu katika LIGI YA MAREKANI NBA HASHEEM THABEET aliungana na Vijana waliojitokeza kusherehesha tamasha hilo.Tamasha lilipambwa na mechi za WANAWAKE,VETERANS NA Vijana shupavu lilifanyika katika viwanja vya Leaders club.
 Baadhi wa Wachezaji waliojitokeza katika Bonanza la Basketball all stars.
 HASHEEM THABEET akipeana mikono ya pongezi na kuagana na baadhi ya Wachezaji wa Vijana wanao wakilisha Taifa kwenye michuano ya zone V huko Burundi.
 HASHEEM akifanya yake na Vijana wa Kitanzania uwanja wa Leaders Club

 Baadhi ya makocha waliojitokeza KUTOA SUPPORT kwenye Bonanza hilo.

 HASHEEM THABEET AKIFUNGUA MAPAMBANO WAKATI TIMU ZA WANAWAKE/WASICHANA ZILIPOKUTANA

SOURCE:http://www.bongobasketball.blogspot.com/