Search This Blog

Saturday, December 10, 2011

RATIBA YA CAF CHAMPIONS LEAGUE

DOUBLE CLICK TO ENLARGE

CAF WATOA RATIBA: YANGA KUANZA NA ZAMALEK, SIMBA NA KIYOVU


Shirikisho la soka barani Afrika - CAF limetoa ratiba michuano ya kombe la ligi ya mabingwa wa afrika pamoja na kombe la shirikisho.

Wawikilishi wa Tanzania katika kombe la klabu bingwa ya afrika Yanga wamepangwa kuanza na Zamalek ya Misri na mshindi kati yao atacheza dhidi ya Missile ya Gabon au African Sport ya Ivory Coast, huku Mafunzo ya Zanzibar wakianza dhidi ya Muculmano ya Msumbiji na endapo watashinda watakutana na Dynamo ya Zimbabwe.

Klabu ya Simba ya Tz ambayo ni wawikilishi wetu katika kombe la shirikisho wenyewe wamepangwa kuanza na Kiyovu na Rwanda na mshindi wa mechi kukutana na Estif ya Algeria, huku Jamhuri la Zanzibar wakianza na Hwange ya Zimbwabwe na mshindi wa mechi hii atacheza na Amal ya Sudan.

JUVENTUS YAMTAKA TEVEZ KWA £20MILLION

Juventus wamekuwa klabu ya kwanza kuonyesha ishara ya kwamba wapo tayari kulipa £20 million kwa ajili Carlos Tevez mwezi ujao.

Sources in Italy zinasema Raisi wa Juventus Andre Agnelli amezungumza na kocha wa Manchester city Roberto Mancini jana Ijumaa kuhusu Tevez.

Inasemekana kwamba City wapo tayari kumuachia Carlitos atleast kwa ada isiyopungua £20million , na Agnelli aliweka wazi kuwa anataka kumnunua Tevez kwa dili la permanently.

AC Milan walikuwa ndio timu ya kwanza kuzungumza na City kuhusu kumchukua Tevez lakini mkopo kitu ambacho City hawataki hata kusikia.

HIVI NDIVYO NEMANJA VIDIC ALIVYOUMIA

UNITED KUWAKOSA WACHEZAJI 9 LEO DHIDI YA WOLVES


Manchester United imethibitisha kua beki wake Nemanja Vidic hawezi kuonekana tena uwanjani katika msimu mzima baada ya kuondolewa uwanjani kwa kutumia machela baada ya kuumia goti kwenye mechi na Basel ndani ya Ligi ya mabingwa.

kocha Ferguson amesikitika kwasababu alihisi jamaa angetibiwa na kuwa poa ndani ya kipindi kifupi, kumbe sivyo, ambapo nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Jones au Smalling.

BBC wamesema Ferguson anakabiliwa na kigezo cha kupoteza hadi wachezaji tisa jumamosi hii wakati watakapocheza na Wolves, ambapo Miongoni mwa wachezaji wasioweza kumsaidia Ferguson ni Michael Owen, Anderson, Tom Cleverley, Fabio, Rafael na Javier Hernandez pamoja na mshambuliaji wa upande wa kushoto Ashley Young alionekana kuzidi kutonesha jeraha la kidole chake katika mechi dhidi ya Basel ambapo ilibidi aondolewe mapema kwenye kipindi cha pili.

MillardAyo.com

Friday, December 9, 2011

THIERRY HENRY AMWAGA MACHOZI BAADA YA ARSENAL KUMTUNUKU NA SANAMU LAKE NJE YA UWANJA WA EMIRATES


KUELEKEA EL CLASSICO KESHO: TUANGALIE MAGOLI 11 BORA KATI YA MADRID VS BARCA

NAMBA 1: LIONEL MESSI

NO.2: SANTIAGO ARAGON

N0.3: RONALDO DE LIMA

NO.4: ROBERTO CARLOS

NO.5: DAVID VILLA

NO.6: JULIO BAPTISTA

NO.7: RAUL

NO.8: XAVI

NO.9: JOHAN CRUYFF

NO.10: ZINADINE ZIDANE

NO.11: RONALDINHO

PMI hosts Football Business Seminar in Tanzania

Mwanzilishi wa Kampuni ya PMI MR MICHAEL HITCHCOCK ATAKUEPO Kwenye semina hiyo.






For Immediate Release
PMI Media
214-335-3865
media@playbookmanagement.com

PMI hosts Football Business Seminar in Tanzania

Dar es Salaam, Tanzania (December 8, 2012) – On Saturday,

December 10th, 2012 9am at the Paradise Express Hotel; Playbook Management International, a Dallas Texas based sports management company will host a Football Business Seminar in East Africa for football leaders from the Tanzania Premier League, CECAFA, Tanzania Football Federation. The Business Seminar will cover topics that range from a historical study of the growth of Major League Soccer, growing the global brand of a professional football league, sustainable business management of a professional football club, strategies to monetize professional football assets, sponsorship strategies, community outreach for professional football clubs including the sharing of best practices from the US and International football clubs and associations.

PMI Founding Partner shared his thoughts on the seminar, “PMI is extremely proud to be here in Tanzania to share our experience and expertise in the business of professional football. It’s an incredible country with a great football future. There’s strong leadership and passionate fans which means that there is tremendous potential. I’m very optimistic in where Tanzanian Football will be in 10 years, on and off the pitch.”

PMI would like to thank seminar partners: Tanzania Premier League, African Lyon FC, Clouds FM and the Paradise Express Hotel.

About Playbook Management International (“PMI”):
PMI is a Dallas, Texas based Sports Management Company that works with professional sports teams, venues and events all over the world to assist our partners in running a more efficient and profitable business operation. PMI brings over 50 years of professional sports management experience to our hand selected clients. For more information on PMI, please visit www.playbookmanagement.com

ASANTE KOTOKO YATUA TANZANIA KUIKABILI SIMBA.





VIONGOZI WA ASANTE KOTOKO WAKIWA NA MWENYEJI BI HELLEN MASANJA




TIMU ya soka ya Kumasi Asante Kotoko iliwasili jana kwa ajili ya mechi maalum dhidi ya Simba iliyopangwa kufanyika kesho kwenye uwanja wa Uhuru huku ikitoa tambo kibao dhidi ya wapinzani wao hao.
Kocha msadizi wa timu hiyo, Isaac Sarfo alisema kuwa wamekuja na kikosa cha wachezaji wanaofanya vyema katika ligi ya Ghana na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi ili kuona mchezo huo.
Alisema kuwa kwa sasa wamekusajia jumla ya pointi 21 na wachezaji wake wamekuja kuendeleza wimbi la ushindi kwa timu yao na si vinginevyo.
“ Hakuna sababu ya kushindwa katika mchezo huo, tumejiandaa vilivyo na bila shaka tutaibuka na matokeo mazuri, ” alisema Sarfo.
Alisema kuwa wamefurahia sana kuwepo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Tanzania kwani waasisi wa mataifa yao Marehemu Kwame Nkurumah na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wameacha historia kubwa hapa duniani.
“Hatujasita kuja mara baada ya kuambia madhumuni ya mchezo huu, tutaomba chama chetu cha soka kuharisha mechi zetu ili kuja kujumuika na watanzania, nao walikubali ombi letu huku tukiwa tumebakiza mechi nne za ligi, hii ni mechi muhumu na ya kihistoria,” alisema.
Nahodha wa timu hiyo, Danielnii Adjei alisema kuwa Simba wasitarajie mteremko kutoka kwao kwani wamedhamilia kushinda kwa mabao mengi.
“Nashukuru kwa kupewa heshima hii, ni faraja kwetu kushiriki katika mechi kubwa ya kuadhimisha miaka 50n ya Uhuru, tumekuja kamili na tunashinda tu,” alisema Adjei.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Future Century, Hellen Masanja alisema kuwa maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na kabla ya mchezo huo, timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC itacheza na mechi ya utangulizi kwa kupambana na timu ya kombaini ya wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam, Mzizima Queen United.
Masanja alisema kuwa mchezo huo utaanza saa 8.30 na mashabiki wanaombwa kufika kwa wengi ili kuona vipaji vya wachezaji wa timu ya Kotoko na Simba.
Mwisho…
Wachezaji wa timu ya Asante Kotoko wakiwasili nchini jana tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya timu ya Simba kwenye uwanja wa Taifa. Mchezo huo umeandaliwa kwa ajili ya sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.

WAPINZANI WA MANCHESTER UNITED WAFANYA PARTY KUSHEREHEKEA KUTOLEWA KWAO KWENYE CHAMPIONS LEAGUE

HII NI EMERGENCY PART YA MAN U ILIYOANDALIWA NA FANS WA ARSENAL, LIVERPOOL, CHELSEA, BARCA, REAL MADRID ETC NI YA KUWAPA POLE MAN U KWA KUTOLEWA KTK CHAMPIONS LEAGUE.

ALINUNULIWA MBUZI NA KUOKEA SEHEMU NI BM BARBERSHOP! MBUZI KANUNUALIWA KWA MICHANGO LEO ASUBUHI KWA KUFUATWA NA BAJAJI TOKA VINGUNGUTI.

BAAHI YA FANS NI SIZA, DULA QPLUS SAID QPLUS, DENGO, BEN MNGONI, BENNO, DENYA ETC WALE WA MAN NI MC FIKIRINI, MAALIM SEIF, MREMA, BONGE, AFANDE, CHUDA ETC




Thursday, December 8, 2011

KILI STARS YAPIGWA 3-1 NA UGANDA: OKWI AIBUKA SHUJAA

TIMU YA TAIFA YA TANZANIA BARA IMETOLEWA KATIKA MICHUANO YA CECAFA CHALLENGE CUP, BAADA YA KUFUNGWA KWA MABAO 3-1 KWA NA UGANDA. MAGOLI YA UGANDA YALIFUNGWA NA NAHODHA WAO ANDREW MWESIGWA, OKWI, ISINDE. GOLI LA TANZANIA LILIFUNGWA NA MRISHO NGASSA.
TANZANIA SASA INATEGEMEA KUCHEZA MECHI YA MSHINDI WA 3 DHIDI YA SUDAN, HUKU RWANDA WAKIPEPETANA NA UGANDA KATIKA FAINALI.

PAMOJA NA USHINDI MAN CITY WATOLEWA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

MANCHESTER UNITED 1-2 FC BASEL: HIGHLIGHTS


Vipigo vitano vya mwisho vya Manchester United katika Champions League vyote vilitolewa na timu zinazoanzia na herufi 'B' Basel, Barcelona, Bayern Munich, Barcelona and Besiktas.

MASIKINI ROONEY

WAYNE ROONEY AKIWA AMESIMAMA NJE YA CHUMBA CHA KUIFADHIA MAKOMBE YA UEFA - SIKU MOJA BAADA YA TIMU YAKE YA MANCHESTER UNITED KUTOLEWA KATIKA LIGI YA MABINGWA WA ULAYA.

ROONEY APOOZWA MACHUNGU: APUNGUZIWA ADHABU YA KUFUNGIWA NA UEFA


Mshambuliaji wa England na Manchester United Wayne Rooney leo amepunguziwa na UEFA kifungo chake cha mechi 3 na sasa atatumukia kifungo cha mechi mbili tu kufuatia rufaa yake iliyosikilizwa hivi leo huko Nyon, Uswisi huku mwenyewe akihudhuria.
Rooney, Miaka 26, alifungiwa mechi 3 na UEFA baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumpiga teke Beki wa Montenegro Miodrag Dzudovic England ilipocheza na nchi hiyo mwezi Oktoba na kutoka sare 2-2 na kufuzu kuingia Fainali za EURO 2012 zitakazochezwa Juni Mwakani huko Nchini Poland na Ukraine.
Kupunguziwa kwa adhabu hiyo kutamfanya Rooney aweze kucheza mechi ya mwisho ya Kundi D dhidi ya wenyeji Ukraine hapo Juni 19 na kuzikosa mechi mbili za kwanza dhidi ya France na Sweden,
MECHI ZA ENGLAND Kundi D EURO 2012:
Continue reading the main story
11 Juni - France (Donetsk)
15 Juni - Sweden (Kiev)
19 Juni - Ukraine (Donetsk)
Msemaji wa UEFA amesema adhabu ya kufungiwa kwa mechi ya 3 imesimamishwa kwa Miaka minne kuangalia mwenendo wake na itarudi ikiwa tu atafanya kosa kama hilo tena kwenye michuano ya UEFA inayohusisha Timu ya Taifa tu.
Pamoja na kusimamishwa adhabu hiyo Rooney itabidi atumikie kazi ya kijamii kwa Siku nzima kwenye miradi ya UEFA.
Rufaa ya Rooney ilisikilizwa na Jopo la Watu watatu na ilichukua muda wa Saa moja na Nusu huku Rooney akiwa pamoja na Kocha wa England Fabio Capello na Mawakili wao.

ASANTE KOTOKO KUWASILI NCHINI KESHO

Mkurugenzi wa Future Century Albert Albano akizungumzia ujio wa Asante Kotoko.

MAGWIJI wa soka Ghana, Asante Kotoko sasa itacheza na timu ya Simba peke yake katika mechi maalum ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Awali Asante Kotoko ilipanga kucheza na timu ya kombaini ya Simba na Yanga, hata hivyo Yanga wakabadili maamuzi na kuamua kutotoa wachezaji katika mchi hiyo muhimu ya historia.Mkurugenzi wa kampuni ya Future Century, Alberto Albano alisema jana kuwa hakuna taarifa za kimaandishi ambazo timu hiyo ya Jangwani imetoa kwao zaidi ya kutumia vyombo vya habari pekee.“Ni taarifa ambazo hazikuwa rasmi, lakini kutokana na hali ilivyokuwa, tumeamua bora kuachana nao na siku hiyo kuwapa nafasi Simba kuonyesha uwezo wao ikiwa pamoja na kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara,” alisema Albano.Alisema kuwa maandalizi yamekamilika na Asante Kotoko inatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya mchezo huo ambao umedhaminiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF. Wadhamini wengine ni….Abano pia alisema kuwa mchezo huo ni sehemu ya kumtambulisha kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa Simba, Mserbia, Cirkovic Milovan ambaye amechukua mikopa ya kocha wa Uganda, Moses Basena.Viingilio vya mchezo huo ni sh. 30,000 for VIP A, shs. 15,000 (VIP B), Shs. 10,000 for VIP C and shs. 7,000 kwa viti vya orange. Viti vya kijana ni shs. 3.000.Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zinapatikana Steers, Big Bon, Oilcom, Benjamini Mkapa secondary school, Zizou fashion na Uwanja wa Taifa.

MSIBA: MANCHESTER UNITED YATOLEWA CHAMPIONS LEAGUE SASA KUCHEZA MECHI ZA ALHAMISI

Wednesday, December 7, 2011

SIKU KAMA YA LEO: MAN UNITED YAIFUNGA 4-0 GALATASARY LAKINI YASHINDWA KUFUZU 16 BORA-BECKHAM'S UCL DEBUT

NINI HATMA YA JIJI LA MANCHESTER LEO KATIKA CHAMPIONS LEAGUE

Hatma ya klabu mbili kubwa za jiji la Manchester kwenye michuano ya klabu bingwa ya ulaya itajulikana leo wakati vikosi vya Roberto Mancini na Sir Alex Ferguson vitakuwa vikicheza mechi zao za mwisho za makundi huku vikihitaji kupata matokeo chanya ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kuweza kupata nafasi ya kuingia katika 16 bora ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

Kwa upande wa Man City wenyewe wapo katika hali mbaya zaidi ya kuweza kuingia 16 bora, kwani wanahitajika kuifunga Bayern Munich iliyo katika form nzuri huku wakiomba Villareal amfunge Napoli ili waweze kushika nafasi ya pili katika kundi lao.

Vijana wa Sir Alex Ferguson wenyewe wanahitaji japo pointi moja ili kuweza kupita, lakini watakabiliwa na ugumu wa hali ya juu kutokana na upinzani watakaoupata kutoka kwa FC Basel ambao nao wanahitaji kuifunga United kwa ushindi wowote ili kuweza kuungana na Benfica ku-qualify in the last 16 stage. Timu hizi mbili zilitoka sare ya 3-3 katika uwanja wa Old Trafford katika mechi yao kwanza.

Ikiwa United watafungwa leo basi watakuwa wamefuata rekodi yao waliyoiweka miaka 6 iliyopita baada ya kushindwa kufuzu kuingia hatua ya pili ya champions league walipofungwa na Benfica kushika mkia katika kundi lao.

JE UNITED WATADHARIRIKA KAMA ILIVYOKUWA MWAKA 2005

RATIBA YA MECHI NYINGINE ZA CHAMPIONS LEAGUE LEO

MAN CITY VS BAYERN MUNICH

BENFICA VS OTELUL GALATI

VILLAREAL VS NAPOLI

LILLE VS TRABZONSPOR

INTER MILAN VS CSKA MOSCOW

FC BASEL VS MAN. UNITED

DINAMO ZEGREB VS LYON

AJAX VS REAL MADRID

MATUMLA NA MTAMBO WA GONGO KUMALIZA UBISHI KRISIMASI


MLEZI wa mchezo wa ngumi 'Masimbwi 'Mawe' Tanzania kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova anatarajia kuwa mgeni rasmi katika pamabano kati ya Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi Dar es Salaam.

Pambano hilo lisilo la ubingwa linatarajia kuwa katika uzito wa middle
weihgt raundi 10.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Maneno Osward alisema atahakikisha
anamtwanga mpunzani wake ili kufuta machungu ya kumzidi kwa pointi
katika pambano lao walilocheza hivi karibuni.

"Matumla alinizidi kwa pointi sasa nataka kumonyesha kama ninauwezo wa
kumuangusha katika hatua za awali za pambano letu kwani nimejiandaa na
bado naendelea kujifua kwa ajili ya pambano hilo," alisema Maneno.

Naye kwa upande wake Rashid alisema, anaendelea kujifua ili kuweza
kuwapa raha mashabiki wake ikiwa na kuwapa zawadi ya Christimas kwa
kumtwanga kwa mara nyingine Maneno.

"Ushindi wangu ndio utakuwa zawadi kwa mashabiki wangu kwani
sinachazaidi cha kuwapa," alisema Rashid.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'mwayamwaya'
ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema kabla ya kufanyika kwa
pambano hilo mabondia hao watapima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi
na madawa ya kuongeza nguvu ili kuweza kuwatayari kwa ajili ya
mpambano.

Mapambano ya utangulizi yatakuwa kati ya mabondia Venas Mponji
atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia Rashidi Ally
atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi
wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet
Kalulu na Saleh Mtalekwa

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki
kujua sheria za masumbwi.

NGORONGORO YATOLEWA COSAFA KUREJEA BONGO KESHO



TIMU ya soka ya vijana ya Tanzania ya umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, inatarajia kurejea nyumbani kesho Ijumaa alfajiri ikitokea jijini hapa ambapo ilikuwa inashiriki kwenye mashindano ya vijana ya COSAFA ambayo leo yanaingia katika hatua ya nusu fainali.

Ngorongoro Heroes iliyokuwa kwenye kundi C ilimaliza hatua ya makundi ikiwa katika nafasi ya pili baada ya kutoka sare na Zambia na Afrika Kusini na ikishinda mchezo mmoja dhidi ya Mauritius uliofanyika juzi.

Zambia ambao ndio mabingwa watetezi wa mashindano haya ndio timu iliyofuzu kutoka kundi C huku yosso wa Afrika Kusini wakimaliza wakiwa kwenye nafasi ya tatu na Mauritius ikishika mkia.

Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Kim Poulsen, alisema jana kuwa ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mashindano haya na kusema kwamba wamejifunza mambo mengi ikiwemo uchezaji wa timu nyingine ambazo wanaweza kukutana nao kwenye mashindano mengine ya kimataifa.

Kim alisema kuwa mechi zote zilikuwa ngumu na wachezaji walijipanga kuhakikisha hawapotezi mchezo jambo ambalo limewasaidia kutofungwa.

Aliongeza kuwa kila mchezaji alionyesha uwezo wake na wale ambao ilikuwa ni mara ya kwanza kushiriki katika mashindano ya kimataifa wamepata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.

Nahodha wa Ngorongoro Heroes, Issa Rashid, ambaye anachezea klabu ya Mtibwa Sugar inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, alisikitika kuona wametolewa kwenye mashindano hayo na kushaanga kutokuwepo kwa hatua ya robo fainali wakati ni mashindano yanayoandaliwa na shirikisho lenye uwezo.

Wakati huo huo, mechi za hatua ya nusu fainali ya mashindano ya vijana ya umri chini ya miaka 20 yanayoandaliwa na COSAFA inaanza leo jijini hapa kwa wenyeji Botswana kuikaribisha Zambia mchezo utakaofanyika kuanzia saa tisa mchana kwenye uwanja wa Molepolole ulioko nje kidogo ya jiji.

Botswana ilifuzu kutinga hatua hiyo juzi baada ya kuifunga Swaziland magoli 3-0 wakati Zambia yenyewe iliingia hatua hiyo kwa kuipa kichapo cha magoli 5-1 timu ya Afrika Kusini ambayo ndio timu pekee iliyokuwa inajiamini kwamba italibeba kombe hilo.

Nusu fainali nyingine itakayochezwa leo itakuwa ni kati ya Malawi dhidi ya Angola ambayo itaanza kurindima kuanzia saa 11:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Mbali na Tanzania timu nyingine zilizotolewa ni pamoja na Swaziland, Afrika Kusini, Msumbiji, Namibia, Madagascar, Mauritius, Shelisheli, Lesotho na Zimbabwe.

Zambia ndio bingwa mtetezi wa mashindano hayo akiushikilia ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo.

VIINGILIO VYA NUSU FAINALI YA CHALLENGE CUP.

NUSU FAINALI CECAFA TUSKER CHALLENGE

Mechi mbili za nusu fainali kuwania ubingwa wa 35 wa michuano ya CECAFA Tusker Challenge Cup inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) zinachezwa kesho (Desemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nusu fainali ya kwanza itakayozikutanisha Rwanda na Sudan itachezwa kuanzia saa 8.00 mchana na kufuatiwa na ile ya pili kati ya mabingwa watetezi Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na Uganda (The Cranes) itakayoanza saa 10.00 jioni.

Viingilio katika mechi hizo ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B, n ash. 20,000 kwa VIP A.

Mechi ya fainali na ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Desemba 10 mwaka huu. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) atapata dola za Marekani 30,000, makamu bingwa dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000.

BARUA YA YANGA KUTHIBITISHA USHIRIKI WA YANGA KATIKA MECHI DHIDI YA ASANTE KOTOKO -KABLA YA KUBADILI MAWAZO.

ARSENAL YAFUNZWA SOKA NA OLYMPIAKOS - YAPIGWA 3-1

DORTMUND YATOLEWA MABINGWA WA ULAYA

BARCELONA YAKAMILISHA RATIBA UEFA NA USHINDI WA REKODI

CHELSEA YATINGA 16 BORA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Mc​hezaji wa zamani wa Prisiner MADESHO MOYE amefariki dunia katika hospitali ya KCMC

Na Dixon Busagaga,Moshi.

TASNIA ya mchezo wa soka nchini imepata pigo kufuatia kifo cha
mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Prisiner Madesho Moye
kilichotokea leo majira ya saa nne asubuhi katika hospitali ya rufaa
ya KCMC.

Madesho aliyekuwa Rais wa timu ya soka ya Moshi Veterani aliugua
ghafla juzi muda mchache baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki
kati ya timu yake ya Moshi veterani na timu ya Wazee kutoka mkoani
Arusha ambayo alicheza kwa muda wote wa mchezo.

Taarifa za awali zilisema kuwa mara baada ya mchezo kumalizika
kulifanyika sherehe ndogo ya kupongezana kwa timu hizo mbili ambapo
mara baada ya sherehe hiyo kwisha Madesho alipanda gari yake na
kuelekea nyumbani ndipo hali ilibadilika ghafla na kusadiwa na
wachezaji waliokuwepo uwanjani hapo.

Baadae Madesho alikimbizwa katika hospitali ya Kilimanjaro hali
ilivyozidi kuwa mbaya alihamishiwa katika hospitali ya rufaa ya Kcmc
ambako alipokelewa na kulazwa katika chumba cha uangalizi kwa wagonjwa
mahututi(ICU) ndipo hado kufikia leo saa 4 asubuhi taarifa za kifo
chake ndipo zilipotangazwa.

Marehemu Madesho aliwahi kuzichezea timu za Prisner,Boma Fc,Kiboko
Msheli na timu nyingine nyingi kabla ya kuamua kustaafu na kuendelea
na kazi aliyokuwa akifanya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)katika mkoa
wa Kilimanjaro.

MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI ,AMEEN.

Madesho Moye akiwa amebeba kombe baada ya kufanikiwa kushinda kikombe
hicho katika mashindano ya Pasaka ambayo huandaliwa kila mwaka na
mamlaka ya bandali ya nchini Kenya.

Madesho Moye wa pili kutoka kulia (waliopiga magoti)akiwa na kikosi
cha timu ya soka ya Moshi veterani ya mkoani Kilimanjaro kilipofanya
ziara nchini Kenya April Mwaka huu katika mashindano ya kombe la
Pasaka ambalo timu hiyo ilifanikiwa kunyakua.



Madesho Moye akiwa katika picha ya pamoja na mchezaji wa timu ya soka
ya Standard Chartered ya jijini Nairobi ambaye jina lake
halikufahamika mara moja mara baada ya mchezo wa fainali uliopigwa
katika uwanja wa KPA mwaka huu.



Madesho Moye akiwa amebeba kikombe mara baada ya kukabidhiwa baada ya
kuwa washindi katika mashindano ya Pasaka yaliyofanyika nchini Kenya.

Tuesday, December 6, 2011

KILIMANJARO STARS YATINGA NUSU FAINALI CECAFA CUP

Timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars imefanikiwa kuingia nusu fainali ya CECAFA Senior Challenge Cup 2011, baada ya kuifunga timu ya Malawi kwa goli moja kwa bila. Goli la Stars lilifungwa na kiungo Nurdin Bakary katika kipindi cha kwanza na kudumu mpaka mwisho wa mchezo.

Kwa matokeo hayo Kili stars sasa itacheza na Uganda katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali siku ya Alhamisi.


MECHI ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE LEO: NINI HATMA YA CHELSEA?


CHELSEA VS VALENCIA

PORTO VS ZENIT

GENK VS LEVERKUSEN

DORTMUND VS MARSEILLE

BARCELONA VS BATE

PLZEN VS AC MILAN

LUIS SUAREZ MATATANI TENA - ANGALIA ALICHOFANYA.


Akiwa bado na kesi ya kumtolea maneno ya kibaguzi Patrice Evra, mchezaji wa Liverpool Luis Suarez anaweza kujikuta yupo kwenye matatizo zaidi baada ya kuwaonyeshea ishara ya kidole cha kati mashabiki wa Fulham baada ya mchezo uliozikutanisha timu zao katika muendelezo wa ligi kuu ya England usiku wa jana.

Suarez jana alikuwa katika wakati mgumu baada ya mashabiki wa Fulham katika uwanja wa Craven Cottage walipokuwa wakimzomea kwa kumuita “mdanganyifu” kutokana na kitendo chake cha kujiangusha katika mechi hiyo.

Kutokana na kitendo alichofanya Suarez ambacho mara nyingi hutatafsiriwa kuwa ni tusi, then anaweza akajikuta katika balaa la kukumbana na adhabu kutoka FA, ikiwa kamati ya nidhamu itaona ana makosa pindi watakapokaa kumjadili leo Jumanne.

MSAADA TUTANI: HUYU NI NANI? ALISHAWAHI KUWA MCHEZAJI GHALI ZAIDI DUNIANI.

Go long: Christian Vieri prepares to launch an American football
On target? Vieri watches his pass

KIBOKO YA TOP 4 LIVERPOOL AKALISHWA NA FULHAM

NANI KUUNDA KIKOSI BORA CHA MWAKA CHA UEFA.


Shirikisho la soka barani ulaya limetangaza majina ya wachezaji 56 pamoja na makocha 5 watakaogombea nafasi ya kuunda timu ya mwaka ya shirikisho hilo katika mwaka huu wa 2011.

Jumla ya wachezaji watano wamechaguliwa katika kila nafasi, huku final line up ikitarajiwa kutangazwa mwezi January 2012, tarehe 18. Mashabiki wanatakiwa kuwapigia kura na kuwachagua wachezaji 11 watakaounda kikiosi cha wachezaji bora wa barani ulaya ndani ya mwaka 2011.


Goalkeepers:
Manuel Neuer (Bayern Munich)
Edwin van der Sar (Retired)
Iker Casillas (Real Madrid)
Victor Valdes (Barcelona)
Joe Hart (Manchester City)

Right-backs:
Dani Alves (Barcelona)
Philipp Lahm (Bayern Munich)
Christian Maggio (Napoli)
Darijo Srna (Shakhtar Donetsk)
Maxi Pereira (Benfica)

Centre-backs:
Gerard Pique (Barcelona)
Nemanja Vidic (Manchester United)
Thiago Silva (AC Milan)
Mats Hummels (Borussia Dortmund)
Sergei Ignashevich (CSKA Moscow)
Benedikt Howedes (Schalke)
Javier Mascherano (Barcelona)
Vincent Kompany (Manchester City)
Rolando (Porto)
Adil Rami (Valencia)

Left-backs:
Eric Abidal (Barcelona)
Fabio Coentrao (Real Madrid)
Marcelo (Real Madrid)
Alvaro Pereira (Porto)
Ashley Cole (Chelsea)

Right midfielders:
Xherdan Shaqiri (Basel)
Arjen Robben (Bayern Munich)
Mario Gotze (Borussia Dortmund)
Gervinho (Arsenal)
Nani (Manchester United)

Central midfielders:
Yaya Toure (Manchester City)
Xavi (Barcelona)
Jack Wilshere (Arsenal)
Joao Moutinho (Porto)
Luka Modric (Tottenham)

Attacking midfielders:
Andres Iniesta (Barcelona)
Mesut Ozil (Real Madrid)
David Silva (Manchester City)
Marek Hamsik (Napoli)
Wesley Sneijder (Inter)

Left wingers:

Gareth Bale (Tottenham)
Eden Hazard (Lille)
Angel Di Maria (Real Madrid)
Juan Mata (Chelsea)
Ashley Young (Aston Villa)

Forwards:
Lionel Messi (Barcelona)
Radamel Falcao (Atletico Madrid)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Hulk (Porto)
Javier Hernandez (Manchester United)
Robin van Persie (Arsenal)
Sergio Aguero (Manchester City)
Mario Gomez (Bayern Munich)
Edinson Cavani (Napoli)
Antonio Di Natale (Udinese)

Coaches:
Pep Guardiola (Barcelona)
Andre Villas-Boas (Chelsea)
Jurgen Klopp (Borussia Dortmund)
Alex Ferguson (Manchester United)
Rudi Garcia (Lille)

Monday, December 5, 2011

USHINDI 4-0 WA ARSENAL DHIDI YA WIGAN


5 – Namba ya wachezaji wa Arsenal walio na assists nne au zaidi katika premier league.

37 – Wachezaji wanne wa Arsenal walifunga magoli katika mechi moja kwa mara ya kwanza baada ya mechi 37 tangu walipoifunga Aston 4-2,November 27th 2010.

179 – Goli alilofunga Thomas Vermaelen dhidi ya Wolves ended a run of 179 corners without a goal katika Premier League. Mechi ya mwisho Arsenal kufunga goli la kichwa ilikuwa dhidi ya (Feb. 23 2011 – Arsenal 1-0 Stoke – Sebastien Squillaci)

721 – Namba ya pasi zilizopigwa na Arsenal dhidi ya Wigan.

633 – Namba ya pasi zilizokamilika zilizopigwa na Arsenal dhidi ya Wigan.

11 – Namba ya magoli aliyofunga Thomas Vermaelen akiwa na Arsenal.

6 – Namba ya assists alizotoa Gervinho tangu aanze kuichezea Arsenal in EPL.
4 - Number ya Assists alizopiga Gervinho kumuendea Robin Van Persie.

31 – Career assists za Theo Walcott tangu ajiunge na Arsenal.

13 – Number ya assists za Walcott kumuendea Robin van Persie.

11 – Walcott assists for Arsenal in calendar year 2011.

18 – Namba ya magoli yote aliyoyafunga Robin van Persie katika mashindano yote msimu huu.

4 – Namba ya magoli yote aliyoyafunga Theo Walcott katika mashindano yote katika mashindano yote msimu huu..

3 – Idadi ya magoli waliyofunga Gervinho, Arteta, and Vermaelen katika mashindano yote msimu huu.

14 – Premier League matches played by Arsenal
30 – Magoli waliyofunga Arsenal msimu huu.
23 – Magoli waliyofungwa Arsenal msimu huu in EPL.
8 – Idadi ya mechi walizoshinda Gunners in EPL.
2 –
Idadi ya mechi walizotoa sare Gunners in EPL.

4 – Idadi ya mechi walizofungwa Gunners in EPL.