Search This Blog

Saturday, December 10, 2011

CAF WATOA RATIBA: YANGA KUANZA NA ZAMALEK, SIMBA NA KIYOVU


Shirikisho la soka barani Afrika - CAF limetoa ratiba michuano ya kombe la ligi ya mabingwa wa afrika pamoja na kombe la shirikisho.

Wawikilishi wa Tanzania katika kombe la klabu bingwa ya afrika Yanga wamepangwa kuanza na Zamalek ya Misri na mshindi kati yao atacheza dhidi ya Missile ya Gabon au African Sport ya Ivory Coast, huku Mafunzo ya Zanzibar wakianza dhidi ya Muculmano ya Msumbiji na endapo watashinda watakutana na Dynamo ya Zimbabwe.

Klabu ya Simba ya Tz ambayo ni wawikilishi wetu katika kombe la shirikisho wenyewe wamepangwa kuanza na Kiyovu na Rwanda na mshindi wa mechi kukutana na Estif ya Algeria, huku Jamhuri la Zanzibar wakianza na Hwange ya Zimbwabwe na mshindi wa mechi hii atacheza na Amal ya Sudan.

2 comments:

  1. KAMA NDIO RATIBA IYO BASI YANGA WATAKUA WANASINDIKIZA ROUND YA KWANZA TU WANATOLEWA MANA WAMEWASHINDWA DEBEBIT ITAKUA HAO ZAMAREK! SO DAR YOUNG AFRICAN Kwishneeeeeeeey-By GADNER DIBIBI 4m Magomeni Dsm.

    ReplyDelete
  2. natumaini zote zitasonga mbele!

    ReplyDelete