Search This Blog

Saturday, June 2, 2012

EURO COUNTDOWN: BALOTELLI NA WENZIE WAGONGWA 3-0 NA AKINA ARSHAVIN


Russia 3-0 Italy (Friendly) by goalsarena2012-3

BREAKING NEWS: FLOYD MAYWEATHER AANZA KIFUNGO CHA MIEZI 3 - 50 CENT AMSINDIKIZA JELA

Bondia Floyd Mayweather leo ameanza kifungo cha miezi 3 jela alichohukumiwa mwezi Desemba mwaka jana kutokana na kuvunja sheria kwa kufanya ugomvi. Wakati akielekea Jela Mayweather alisindikizwa na rafiki yake kipenzi mwanamuziki 50 Cent.
Mayweather akitiwa pingu na polisi kuelekea kwenye karandinga.
"Nenda dogo nitakumiss kaka yako" 50 Cent na Mayweather.
Hiki ndio chumba atakachokaa Mayweather kwa miezi 3
Hizi ndio sare zake kwa kipindi chote atakachokaa jela.

LIVE MATCH CENTRE: TANZANIA 0 - 2 IVORY COAST FULL TIMEDK 90: Ivory Coast 2-0 Tanzania
DK 86: Goaaaaaaaal Ivory Coast wanapata bao la pili na si mwingine ni Didier Drogba.
DK 80: Kipindi cha pili kinaelekea mwishoni na bado Tembo wanaoongoza kwa bao 1-0
DK 75: Matokeo bado ni 1-0, Ivory Coast wanaongoza.
DK 70: Aggrey Morris anapata kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

DK 68: Ivory Coast 1-0 Tanzania
DK 60: Ivory Coast 1-0 Tanzania
Second Half: Kipindi cha pili kimeanza
Half Time:  Ivory Coast 1-0 Tanzania

DK 43: Ivory Coast 1-0 Tanzania

DK: 24 - Solomon Kalou anaipatia goli la kuongoza Ivory CoastKocha Kim Poulsen ametaja kikosi cha Taifa Stars ambacho leo (Juni 2 mwaka huu) kitakuwa uwanjani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.
Amefanya mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu kilicheza mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
Amir Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia mazoezini siku moja kabla ya safari.
Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;
Kipa; Juma Kaseja
Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani
Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto
Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa
Wachezaji wa akiba; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.
Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).
Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.
Mwamuzi; Slim Jedidi (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba 1; Bechir Hassani (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba mbili; Sherif Hassan (Misri)
Mwamuzi wa akiba; Youssef Essrayri (Tunisia)
Mtathmini wa waamuzi; Rachid Medjiba (Algeria)
Kamishna wa mchezo; Saleh Issa Mahamat (Chad)

EXCLUSIVE INTERVIEW NA KOCHA WA UJERUMANI: TIMU YANGU INA NJAA NA MACHO YOTE TUMEWEKA KWENYE LENGO LA KUTWAA EURO 2012

Katika kuelekea michuano ya EURO 2012, nilitafuta nafasi ya kuonana na kocha wa timu wa timu ya taifa ya Ujerumani nikiwa nchini humo nilipoenda kwa madhumuni ya kuangalia fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya. Nilifanikiwa kuonana na Joachim pamoja na mchezaji Mario Gomez na kufanya mahojiano kuhusu michuano ya Euro 2012 na nafasi ya Ujerumani kwenye Michuano hii.
Kwa kuanzia tuanze na interview na kocha Low na ilikuwa kama ifuatavyo.


Shaffih: Unajisikiaje kupangwa kwenye group ambalo wengi wanaliita kundi la kifo?

Low: Kwa sura ya kundi, tumepangwa kwenye kundi ngumu zaidi kuliko yote. Uholanzi na Portugal  zote ni timu zenye wachezaji wa daraja la dunia na mechi zao dhidi yetu zitakuwa ni ngumu sana; nadiriki kusema mechi kufa na kupona. Kwa upande wa Denmark, kwa miaka kadhaa wameshaonyesha kwamba wanaweza kushindana kwenye michuano mikubwa. Hawaogopi timu zenye majina makubwa na hawana cha kupoteza na hilo linawafanya wawe hatari zaidi na wasiotabirika. Kwa maana hiyo nasema kwamba kila timu kwenye kundi B ina nafasi ya kupita.Shaffih: Mliwamaliza na kuwazidi kwa kila kitu Uholanzi kwenye mechi ushindi wa 3-0 mwezi November. Hilo linakupa nguvu yoyote kisaikolojia?

Low: Usiku ule tulicheza soka la aina yake na la kipekee na ndio maana tukapata matokeo chanya kutoka mchezo ule. Uholanzi tutakayokutana nayo kwenye Euro itakuwa na nguvu zaidi na yenye kubadilika sana hilo nina uhakika.Shaffih: Je rekodi yenu nzuri kwenye hatua ya kufuzu inaweza kuwaletea matatizo yoyote kwa maana ya wachezaji kujiamini sana?
Low: Sina wasiwasi kabisa kwenye matokeo yale. Kikosi nilichonacho kina njaa ya mafanikio, na kipo focused  kwenye lengo la kushinda kikombe. Hakuna aliye kwenye fikra kama tulimaliza kazi kwenye kufuzu tu japokuwa tulifanya vizuri sana.


Shaffih: Ujerumani wanaangaliwa kama moja ya timu zinazopewa nafasi sana na imani ipo juu hapa Ujerumani kwamba mnaweza kubeba kombe . . .
Low: Baada ya kufanya vizuri kwenye kufuzu, mategemeo yamepitiliza. Lakini droo ya kundi tulilopangwa kidogo imeshusha mategemeo. Sasa watu wanaangalia hali halisi kidogo. Lolote linaweza kutokea kwenye michuano. Majeruhi yanaweza yakabadilisha kila kitu. Kama makocha wengine, nitakuwa naomba tuepukane na balaa hilo na tumalize michuano tukiwa tuo salama ili kuweza kukamilisha ndoto ya ubingwa wa Euro 2012.


Shaffih: Nini nguvu yenu?
Low: Moja ya vitu vikubwa kwangu mimi ni kuona namna tulivyojimaarisha na kuendelea kuja kuwa timu ya ukweli, ambayo ina umoja ambao ndio nguzo yetu. Hakuna mchezaji ambaye moja kwa moja anajiangalia yeye. Kila mmoja wetu anamsaidia mwenzake, tunashirikiana kuiletea mafanikio timu yetu, na pale vijana wapya wanapokuja wanakuta mfumo huo na kuumudu vizuri. Spirit ya timu ilikuwa juu sana kwenye WOZA 2010 PALE South Africa  na hili limeendelea mpaka leo.


Shaffih: Je Euro 2012 inaweza ikawa vita ya kwenu pamoja na Spain?
Low: Spain wapo vizuri sana lakini sio kama ndio wagombea taji pekee. Uholanzi na timu nzuri sana. Siku zote nimekuwa na heshima kubwa juu ya uwezo wa Ureno, France wanaimarika, na tusiwatoe England..


EURO 2012 COUNTDOWN: UJERUMANI SIO WASINDIKIZAJI WA HARUSI TENA _ VIJANA WA JOACHIM WANA KILA KITU CHA KUWA MABINGWA MUDA HUU.

Washindi wa pili wa Euro 2008 na watatu kwenye kombe la dunia 2006 na 2010, Ujerumani wanaweza wakawa wanacheza soka la kuvutia huku wakikosa makombe kwenye michuano ya hivi karibuni lakini nilipata wakati mgumu sana kumpata shabiki ambaye alikuwa akilalamika kuhusu suala la ukosaji makombe.


Baada ya kuwa michuano mibovu zaidi kwenye Euro 2000, ambapo walishindwa kushinda hata mechi moja na hatimaye kutolewa kwa aibu kabisa kwenye raundi ya kwanza - lakini mabadiliko yaliyofanywa kuubadilisha mfumo wa maendeleo ya soka la vijana, taratibu taratibu, umerudisha soka la Ujerumani kwenye hadhi yake. Na mashabiki wameamini kwamba kikosi cha sasa kinachoundwa na vijana zaidi ni mwanzo tu wa safari ya kuelekea kubeba taji lao kwanza toka EURO 96.


    Utafiti uliofanywa na jarida maarufu nchini humo (Kicker) unaonyesha zaidi ya 2/3 ya watu waliohojiwa wanategemea nahodha wao Phillip Lahm atabeba kombe mjini Kiev, July 1, huku wakiamini wachezaji kiungo mchezeshaji Mesut Ozil na mshambuliaji Miroslave Klose watakuwa na tuzo mchezaji bora wa mashindano na mfungaji bora.


Ujeumani wamepangwa kwenye kundi ambalo wengi wanaliita la kifo - watacheza mechi zao tatu za mwanzo dhidi ya Ureno, Uholanzi na Denmark, na wachambuzi wengi wengi wa soka wamekuwa tu hawawapi nafasi ya kuvuka kwenye hatua ya makundi bali pia wanapewa nafasi kubwa ya kubeba kombe hili mwisho wa michuano hii. Wakiwa na kikosi cha vijana kabisa chenye wastani wa umri wa miaka 24 - ambacho ndio kikosi chenye wachezaji vijana zaidi waliowiva zaidi tangu mwaka 1934. Klose, Ozil, Mario Gomez, Thomas Muller na Lukas Podolski wataunda safu ya ushambuliaji ya kutisha zaidi kama tulivyoona kwenye WOZA 2010. Huku Manuel Neur akiiongoza safu bora ya ulinzi inayoundwa pia na Holger Badstuber, Boateng, Hummels na nahodha Lahm, Mario Gotze, Khedira, Toni Kroos na Bastian Schweinsteiger wakiunda safu bora kabisa ya kiungo.
Hawa ni vijana wenye umri mdogo lakini wamekamilika na wana uzoefu mkubwa, wana uwezo wa kucheza timu yoyote  wakiwa hawana woga na wala mashaka yoyote juu ya kujitoa kwa nchi yao - huku nyuma yao wakiwa na umati wa mamilioni ya mashabiki wa Ujerumani ambao wote wana imani kubwa sana  juu yao. Tegemea makubwa kutoka vijana wa Joachim Low kwenye michuano hii.

MAPINDUZI YA STAILI YA UCHEZAJI
Kitu kingine ambacho Ujerumani walichonacho kwenye timu, ni aina ya mchezo uliosukwa vizuri kiakili zaidi na management ya Low. Katika miaka 6 aliyokaa kwenye benchi la timu ameleta mapinduzi makubwa ya uchezaji wa soka la kuvutia na ushindi  tofauti na vikosi vya nyuma vilivyokuwa vikicheza la moja kwa moja na kushinda kwa vyovyote vile.
Ujerumani sasa inacheza soka la kuvutia na kushinda mechi kwa magoli mengi ya kiufundi zaidi, na ndio maana haikushangaza pale Bosi wa timu ya taifa ya Spain Vicente Del Bosque alipowaelezea kama ndio "kikosi cha Ujerumani kinachocheza zuri zaidi" ambacho Del Bosque amewahi kukishuhudia kwenye maisha yake.

 KUNDI LA B ILIPO UJERUMANI EURO 2012

Team Pld W D L GF GA GD Pts
 Netherlands 0 0 0 0 0 0 0 0
 Denmark 0 0 0 0 0 0 0 0
 Germany 0 0 0 0 0 0 0 0
 Portugal 0 0 0 0 0 0 0 0
RATIBA

9 June 2012
Netherlands  Match 3  Denmark
Germany  Match 4  Portugal
13 June 2012
Denmark  Match 11  Portugal
Netherlands  Match 12  Germany
17 June 2012
Portugal  Match 19  Netherlands
Denmark  Match 20  GermanyUJERUMANI ILIFIKAJE KWENYE EURO 2012
Team
Pld W D L GF GA GD Pts
 Germany 10 10 0 0 34 7 +27 30
 Turkey 10 5 2 3 13 11 +2 17
 Belgium 10 4 3 3 21 15 +6 15
 Austria 10 3 3 4 16 17 −1 12
 Azerbaijan 10 2 1 7 10 26 −16 7
 Kazakhstan 10 1 1 8 6 24 −18 4

Friday, June 1, 2012

KUTOKA KWA PLATINI MPAKA DAVID VILLA: WATU SABA WALIOITAWALA MICHUANO YA EURO


Mastaa wengi wamewahi kung'ara kwenye michuano ya Ulaya - lakini ni wachache wameweza kutawala kama majembe haya.

Huku michuano ya nchini Poland na Ukraine ikiwa karibuni kuanza, tunachukua nafasi hii kukuletea watu saba ambao waliwasha moto wa kutisha kwenye historia ya michuano ya Euro.

MICHEL PLATINI (1984)


Mfaransa huyu  kwa sasa anajulikana zaidi kama Raisi wa Uefa mwenye sheria za utata zaidi, lakini hakuna mchezaji aliyeitawala michuano ya 1984 kama yeye.

Kiungo huyu wa aina yake alifunga mabao tisa kwenye mechi tano huku akiiongoza nchi yake kushinda ubingwa wa ulaya kwenye ardhi ya nyumbani.

Baada ya kufunga hat-tricks mbili kwenye mechi za hatua ya makundi, Platini alifunga bao kwenye dakika za nyongeza za mechi ya nusu fainali dhidi ya Ureno.

Ufaransa wakaingia fainali na kwa mara nyingine alifanya balaa kwa kupiga faulo iliyotinga nyavuni kwa kumshinda golikipa wa Spain Luis Arconada.MARCO VAN BASTEN (1988)

 
Career ya Mholanzi iliishia njiani kutokana na balaa la majeruhi, lakini huyu jamaa alikuwa kwenye kiwango cha juu sana.

Unless, labda kama ulikuwa muingereza, baada ya timu zote mbili za mataifa haya kufungwa kwenye mechi zao za ufunguzi, mechi ya kundi B kati ya Uholanzi na England ilikuwa muhimu sana.

Van Basten akafunga hat-trickna kumsumbua sana kinda Tony Adams, wakati wadachi walipowafungasha virago England.

Mchezaji bora wa ulaya kwa mara ya tatu alienda na kufunga goli la ushindi la ushindi dhidi ya Ujerumani magharibi kwenye nusu fainali lakini balaa zaidi lilikuwa njiani.

Van alifunga bonge la bao kwenye 'impossible angle' dhidi ya Umoja wa Soviet - goli ambalo linatajwa kama moja ya mabao bora kabisa ya fainali za ulaya.

Alimaliza michuano hiyo kama mfungaji bora.


PETER SCHMEICHEL (1992)Ulikuwa umepita mwaka mmoja tu tangu Sir Alex Ferguson alipe £505,000 kumnunua mdenmark huyu.

Denmark haikuwa hata ikitakiwa kushiriki michuano hiyo lakini walichukua nafasi ya nchi iliyokuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe Yugoslavia na wakaweza kuwashangaza watu na kubeba ndoo ya ulaya.

Hilo liliwezekana zaidi kutokana na uwezo wa golikipa ambaye alitisha sana kwa kuzuia michomo ya hatari.

Schmeichel aliikoa mpaka penati ya Marco van Basten na kupelekea Uholanzi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa kutolewa kwenye mashindano katika hatua ya nusu fainali.

Hatari ya Denmark iliendelea huku Schmeichel akitoka na clean sheet kwenye ushindi wa 2-0 kwenye fainali dhidi ya Ujerumani.

ALAN SHEARER (1996)
 

Kwa kukumbuka kiangazi cha mwaka 1996, mshambuliaji huyu alikuwa akiwafanyia umafia mabeki wa pinzani    - akifunga magoli kutoka kwenye kila angle - alikuwa mshambuliaji wa kati aliyekamilika haswa.

Ndio ni rahisi kusahau kwamba alienda kwenye Euro 96 akiwa hajafunga katika mechi 12 ndani ya 21 akiwa na England.

Ingawa makelele yote aliyokuwa anapigiwa kocha Terry Venables kumtema mshambuliaji yalianza kuisha na kusahaulika mara tu alipofunga goli kwanza kwenye michuano hiyo katika dakika ya 22 dhidi ya Switzerland.

Kutoka pale akaendeleza balaa zaidi. Kwenye mechi dhidi ya Scotland na kabla ya kuwatesa sana Uholanzi kwenye mechi ambayo England iliwakandamiza wadachi 4-1 pale Wembley.

Shearer aliendeleza kufunga mabao katika mechi robo fainali England ikiwatoa Spain kabla ya kuwapa mashabiki wa England mwanzo mzuri alipofunga bao la kuongoza dhidi ya Ujerumani, ingawa England wakatolewa kwa mikwaju ya penati baada ya Gareth Southgate kukosa penati yake.

Shearer alimaliza michuano hiyo kama mfungaji bora na kubeba kiatu cha dhahabu.


ZINEDINE ZIDANE            

 
Wakati mwingine wa dhahabu wa michuano hii kwa Ufaransa ulihitimishwa na David Trezeguet.
Lakini wakitoka kushinda kombe la dunia miaka miwili nyuma, michuano hiyo iliyofanyika kwenye ardhi za Uholanzi na Ubelgiji ilimpa nafasi Zidane nafasi ya kuweka heshima zaidi kwamba ndio mchezaji bora wa wakati wake.

Wakisikia kelele za mwangi za ushindi wa akina Platini miaka 16 nyuma, Zidane akafunga bao kwenye extra time dhidi ya Ureno katika nusu fainali ya aina yake - kwa mkwaju wa penati.

Zidane alikuwa akitimiza miaka 30 siku tisa kabla ya fainali na akapokea zawadi ya siku ya kuzaliwa kwa kutajwa na UEFA kama mchezaji bora wa michuano hiyo.OTTO REHHAGEL (2004)

 
Shujaa aliyekuwa hategemewi, mjerumani, ambaye sasa ana miaka 73, akawa mungu wa soka nchini Ugiriki  baada ya kuiongoza nchi hiyo kwenye kubeba kombe mwaka 2004

Akiwa bingwa wa kuunda ukuta wa kupaki basi golini chini ya nahodha, Theo Zagorakis kutoka Leicester City, Rehhagel alifanya maajabu mwaka 2004.

Aliiongoza timu yake kupita kwenye hatua ya makundi huku wakishinda mechi zote kwa ushindi wa 1-0 - hata ushindi wa fainali dhidi ya Ureno ulikuwa wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji.

Siri ya mafanikio? Nyuma ya kila kocha aliyefanikiwa kuna mke mzuri wa kocha huyo na mama watoto wa Otto, Beate, ameripotiwa huwa anaenda kufanya scouting kwa wapinzani kwa ajili ya mumewe.

DAVID VILLA 2008

 
Ilikuwa ni michuano ambayo wahispania waliweka heshima baada ya kutaniwa kama warembaji kwa muda mrefu - lakini kipaji cha ajabu cha David Villa kiliiongoza Spain kujenga heshima mpya.

Mshambuliaji wa Valencia tayari alikuwa ameshafunga mabao 6 kwenye hatua ya kufuzu na akafungua michuano kwa kufunga hat-trick dhidi ya Russia.

Huku akiwa anamfunika patna wake mshambuliaji mpya wa Liverpool Fernando Torres, Villa then akafunga goli la muda wa majeruhi katika mchezo wa pili dhidi ya Sweden.

Alipumzishwa kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi, na akarudi kwenye robo fainali na akafunga bao la penati kwenye hatua ya mikwaju ya penati dhidi ya Italia na kuisadia timu yake kufika nusu fainali.

Alipata maumivu kwenye nusu fainali na akashindwa kupata nafuu kucheza mchezo dhidi ya Ujerumani ambao Fernando Torres akafunga bao la ushindi dhidi ya Ujerumani na kuwapa ubingwa Spain - huku David Villa akiibuka mfungaji bora wa michuano.


JE MWAKA HUU NANI ATAITAWALA  MICHUANO YA 2012.

EXCLUSIVE: KAPOMBE + JONAS + 50 MILIONI = IBRAHIM JEBA

Mauzauza kwenye soka la Bongo yameendelea kujidhihirisha leo.


Wakati klabu ya Simba ikiwa imejihakikishia kukamilisha usajili wa kinda la Azam under 20, Ibrahimu Jeba ambaye leo hii asubuhi alionekana kwenye mazoezi ya gym ya Simba - maeneo ya Chang'ombe. Uongozi wa klabu ya Azam FC umesema Simba inajidanganya kuhusu kumsajili mchezaji huyo ambaye Azam walimpeleka Villa Squad kwa mkopo kwa kujifua zaidi msimu uliopita.


Akizungumza na www.shaffihdauda.com kutoka nchini Marekani meneja wa klabu ya Azam FC, Patrick Kahemele amesema mabingwa wa Tanzania bara wanafanya uhuni kwenye uhamisho wa mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba na klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara Salim Bakheresa. "Simba wanafanya uhuni katika hili kama ilivyo kawaida yao, Jeba ni mchezaji wetu halali na bado ana mkataba na Azam. Kumbukumbu sahihi nilizonazo ni kwamba Ibrahimu Jeba alisaini mkataba wa kuichezea Azam kwa miaka miwili mwezi Desemba 2011 na akachukua kiasi cha fedha kama ada ya usajili - kabla ya kuelekezwa kwamba akacheze Villa Squad kwa mkopo ili apate nafasi ya kujifua then msimu huu arudi Azam FC. Simba wakaenda wakamrubuni asicheze Villa, na Jeba bado mdogo hivyo ikawa rahisi kumrubuni, na Azam hatukutaka kufanya nao malumbano kwa sababu suala hilo tayari tuna mkataba ambao umesajiliwa kabisa na TFF, ambao walishatuambia haki zetu za msingi zitalindwa."


Kahemele alipoulizwa ikiwa Simba wanataka kulimaliza hilo suala itabidi walipe kiasi gani alijibu, "Kiukweli sie tulishatangaza mapema kwamba hakuna mchezaji yoyote ambaye ameachwa wala yupo sokoni kwa msimu ujao. Hivyo kama Simba wanamtaka Ibrahimu Jeba kihalali basi atawagharimu sana kwa kuwa sisi tunamuona Jeba akiwa na thamani ya Shilingi millioni 50 na uwachanganye wachezaji wawili wa Simba Jonas Mkude na Shomari Kapombe, then hapo tunaweza kuwafikiria kuwaachia Jeba vinginevyo haitowezekana Jeba kuichezea klabu yao."


HIKI NDIO KIKOSI RASMI CHA AZAM KWA AJILI YA MSIMU UJAO.
Kikosi Kamili cha Azam FC msimu ujao ni kama ifuatavyo Magolikipa ni Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida" Aishi Salum na Jackson Wandwi
Mabeki wa Pembeni kulia ni Ibrahim Shikanda na Erasto Nyoni na kushoto ni Waziri Salum na Samih Haji Nuhu
Babeki wa kati ni Luckson Kakolaki, Said Moradi, Joseph Owino na Aggrey Morris
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, na Ibrahim Joel Mwaipopo
Washambuliaji wa pembeni ni Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha, na George Odhiambo "Blackberry" Washambuliaji wa kati ni Gaudence Mwaikimba na mchezaji bora wa Azam FC John Raphael Bocco "Adebayor"

EXCLUSIVE: TAIFA STARS WALIPOWASILI IVORY COAST - KIM POULSEN NA MATUMAINI TELE

EXCLUSIVE: TAIFA STARS WAKIWA KWENYE MAZOEZI JIJINI ABDIJAN

Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taifa Stars' wakiwa kwenye
mazoezi ya viungo
          
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taufa Stars' wakiwa kwenye
mazoezi chini ya Kocha Msaidizi Sylvester Marsh.

Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taifa Stars' wakiwa kwenye
mazoezi ya viungo chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen.
Juma Nyosso na John Bocco wakipambana kwenye mazoezi.

Kipa wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taifa Stars' akiwa kwenye
mazoezi ya viungo

Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taifa Stars' wakiwa kwenye
mazoezi ya viungo chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen.

HARUNA MOSHI ' BOBAN ' : CHEMSHA BONGO


Kiungo Haruna Moshi ' Boban ' hakusafiri kwenda nchini Ivory Coast na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa sababu ipi kati ya hizi mbili?

A. Kutokana na kuwa majeruhi.

B. Kutokana na kukosa Passport.

VIDEO: Hadhara Charles Mjeje awa msemaji wa PLAY FOR THE UNION.

HADHARA CHARLES AUNGANA NA KINA NWANKWO KANU NA PATRICK MBOMA KWENYE KAMPENI YA ' PLAY FOR THE UNION '

          Hadhara akifanya vitu vyake kwenye mitaa ya jiji la YOUNDE,nchini Cameroon

   Hawa ni Baadhi ya washiriki wa Kampeni ya PLAY FOR THE UNION, Kampeni ambayo mabalozi wake ni Wanasoka wa zamani wa kulipwa Nwanko Kanu kutoka nchini Nigeria pamoja na Mshambuliaji Patrick Mboma toka nchini Cameroon.