Search This Blog

Saturday, December 29, 2012

WENGER: SITOMSAJILI DEMBA BA - SIJAKATA TAMAA KUMRUDISHA HENRY



Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema, hana nia ya kumsajili mshambulizi wa Newcastle Demba Ba.
Ba, 27, ameonyesha mchezo mzuri msimu huu na tayari amefunga magoli 11 msimu huu.
Mshambulizi huyo kutoka Senegal alifunga magoli kumi na sita msimu uliopita.
Kocha wa Newcastle Alan Pardew amekiri kuwa Ba, huenda akauzwa ikiwa hataondoa kipengee kimoja katika mkataba wake unaosema klabu yeyote inaweza kumsajili mchezaji huyo mradi ilipe pauni milioni saba.
''Namkubali sana Demba Ba'' alisema Wenger.'' lakini ukiniuliza ikiwa tutamsajili Demba Ba basi jibu langu ni hapana''
Wenger aliongeza kusema kuwa huu sio wakati muafaka wa kuzungumzia suala hilo, kwa kuwa yeye ni mpinzani wetu kwa sasa.

Arsenal ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimehusishwa na mchezaji huyo ambaye alijiunga na Newcastle kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka klabu ya West Ham, Juni mwaka uliopita.
Wakati huo huo, Wenger amesema hajakata tamaa ya kumsajili mshambulizi wake wa zamani kutoka Ufaransa Thierry Henry, kwa mara ya tatu kwa mkataba wa muda mfupi.
Thiery ambaye aliifungia Arsenal Magoli mawili msimu uliopita, amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu kumalizika kwa ligi kuu ya Marekani MLS.

MBWANA SAMATA - 'NAKIRI NIMEKOSA, SIJAKAMILIKA NAWATAKA RADHI WATANZANIA'



KABANGE TWITE AZUIWA KUCHEZA YANGA NA TFF


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemzuia kiraka Kabange Twite kuchezea Yanga hadi pale suala lake litakapoamuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba,aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa Kabange hatacheza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwani suala lake liko mikononi mwa Fifa baada ya Yanga kushindwa kupata idhini ya FC Lupopo ya kumsajili mchezaji huyo aliyesaini mkataba wa miaka miwili Jangwani.

Kamati ya Haki za Wachezaji ya Fifa ndio itatakiwa kumuidhinisha kwani muda wa mwisho wa kuwasajili wachezaji wa kigeni ulikuwa Desemba 15 ilivyokuwa imepangwa na TFF.

Licha ya kwamba atakuwapo kwenye msafara wa Yanga utakaoondoka kesho Jumapili alfajiri kwenda kambini Uturuki, Tekinolojia ya Uhamisho wa Wachezaji kwa Kompyuta (TMS) ndio imetibua mipango ya Kabange kujiunga na pacha wake Mbuyu Twite, ambaye alijiunga na Yanga mwezi Agosti mwaka huu.

Kawemba alisema kuwa viongozi wa Yanga walifanya mawasiliano na watu wa Lupopo kwa TMS, lakini hawakupata majibu yoyote.
 Yanga waliwasiliana na Lupopo masaa mawili kabla ya dirisha dogo la usajili wa wachezaji wa kigeni kufungwa Desemba 15,  alisema Kawemba.
 Hata hivyo walikwama kwani hawakupata majibu yoyote kutoka kwa watu wa Lupopo. 

Fifa ilianzisha utaratibu wa uhamisho wa wachezaji kwa njia ya TMS, ambayo husaidia klabu kuwasiliana moja kwa moja
na pia vyama vya soka vya nchi husika vikifuatilia mawasiliano hayo kwa ukaribu.

Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio ilikuwa inammiliki mchezaji huyo kama ilivyokuwa kwa pacha wake, Mbuyu.

Kawemba alisema kufuatia hali hiyo, Yanga wanapaswa kusubiri mawasiliano kutoka kwenye klabu hiyo kwenye TMS.
Alisema, hata hivyo, pale watakapopata majibu ya Lupopo ndio taratibu zitaanza kushughulikiwa na TFF lakini wenye maamuzi ya mwisho watakuwa Fifa.

 Yanga wakipata mawasiliano na Lupopo watapaswa kurudi kwetu ili tupeleke suala lao Fifa, alisema.

 Itabidi tuwaeleza sababu za kuridhisha Fifa kuwa kwanini Yanga waliingia TMS muda mfupi kabla ya muda wa mwisho wa usajili, pia (Fifa) watapenda kujua sababu za Lupopo kuchelewa kujibu. 

Kawemba alidokeza ikiwa Kamati ya Haki za Wachezaji itaridhika na maelezo ya pande hizo mbili basi watatoa kibali lakini wasiporidhika basi watamzuia Kabange kuchezea Yanga.

Aliongeza kuwa Kamati ya Haki na Uhamisho Wachezaji ndio yenye uamuzi wa mwisho na kuongeza ikiwa Yanga watanyimwa kibali basi hawatakuwa na ubavu wa kukata rufaa kokote.

 Hakuna chombo chenye mamlaka juu ya Kamati ya
Haki na Usajili ya Fifa. Kwa hiyo Yanga wanapaswa kuelewa hilo, aliongeza. 

Ninawashauri Yanga wafanye kila njia wawapate Lupopo kwani kadiri watakavyochelewa ndio watakuwa wanajiweka pabaya zaidi.

Hatua hiyo itakuwa pigo kwa Yanga kwani ilikuwa inamtegemea Kabange angeimarisha kikosi chao kutokana na umahiri wake wa kucheza nafasi nyingi.

Kama ilivyokuwa Mbuyu, kiraka huyo alikuwa ametolewa kwa mkopo kwenye timu ya APR ya Rwanda na Lupopo.

Lupopo ndio ilikuwa inatakiwa kuidhinisha uhamisho wa nyota huyo kwa njia ya TMS lakini bahati mbaya utaratibu huo umekuwa ukitumika kwa nadra nchini Congo kwa kuwa timu zao nyingi ni za ridhaa.

Kama ikishindikana, Yanga itakuwa ina wachezaji wanne tu wa kigeni baada ya kumwachia kipa Yaw Berko, ambaye amejiunga na Lupopo.

Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano na usajili wa Yanga Abdallah Binkleb aliiambia Mwanaspoti jana akisema: Sisi tulikamilisha kila kitu, tatizo liko kwao Lupopo na tumeshawaeleza TFF tunasubiri jibu nadhani kesho (leo Jumamosi) tutapata ufafanuzi zaidi.

SAMSON MFALILA - MWANASPOTI

Friday, December 28, 2012

MEIRELES APUNGUZIWA ADHABU YA KUFUNGIWA MECHI 11 MPAKA MECHI 4 - YATHIBITIKA HAKUMTEMEA MATE MWAMUZI

Mchezaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea kiungo Raul Meireles amepata nafuu ya kupunguziwa adhabu ya kutocheza mechi 11 mpaka kufikia mechi 4.

Mchezaji huyo wa Fenerbahce, 29, alikata rufaa baada ya kuhukumiwa kwa kosa la kumtemea mate mwamuzi kufuatiwa kupewa kadi nyekundu katika mechi ya iliyowakutanaisha mahasimu wao ligi ya Uturuki klabu ya Galatasary.

Shirikisho la soka la Uturuki limesema ilikuwa ni vigumu kwa mchezaji kutema mate kwa kuwa alikuwa anaongea wakati wote wa tukio hilo, hata hivyo bado atakabiliwa na adhabu ya kukosa mechi nne kwa kumtukana mwamuzi.

JINA LA ZLATAN LAONGEZWA KATIKA KAMUSI YA SWEDEN

 

2012 - umeendelea kuwa mwaka mzuri kwa Zlatan Ibrahimovic, baada ya kupata mafanikio ya uwanjani na kiuchumi sasa jina lake limeongezwa katika kamusi ya kisweden na taasisi inayoshughulikia lugha nchini Sweden - Neno 'Zlatanera' lenye maana ya Zlatan au 'kutawala' limeongezwa katika kamusi rasmi ya Sweden.

Hii imekuja kama kumtunuku mchezaji huyo ambaye amekuwa akiletea sifa nchi hiyo ndani na nje ya nchi hiyo kwa miaka takribani 10 sasa.

Neno 'Zlatanera' limetokana na neno la kifaransa 'zlataner' lenye maana ya kutawala, hivyo wasweden wakalinyambua na kuongeza herufi 'a' katika 'zlataner'.

FEDHA ZILIZOCHUKULIWA NA TRA KWENYE AKAUNTI YA TFF NI ZA VILABU VYA LIGI KUU - VYATISHIA KUGOMEA LIGI WASIPORUDISHIWA

Klabu 14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Novemba 23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.

Serikali ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo malimbikizo kufikia sh. 157,407,968.

TFF bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.

OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.

Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.

Utekelezaji wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja husika na Ofisa Usalama wa TFF.

HAWA NDIO WACHEZAJI WANAOENDA NA YANGA UTURUKI JUMAPILI - NANI KATOSWA??

Mabingwa mara mbili mfululizo wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki al maarufu(Kagame Cup )timu ya Young Africans inatarajia kuondoka alfajiri ya jumapili kuelekea nchini Uturuki ambako itaweka kambi ya mazoezi kwa muda wa wiki mbili.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema timu itaondoka alfajiri ya jumapili kwa shirika la ndege la Turkish Airline, ambapo itakua na msafara wa watu 34, wachezaji 27 na viongozi 7.
Timu itaondoka majira ya saa 10:30 alfajiri na itafika katika mji wa Instabul majira ya saa  5 kasoro dakika 10, kisha baadae majira ya saa 9 alasiri itaondoka kwenda katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki ambapo itafika saa 10 ndio haswa itakapokuwa kambi ya timu alisema 'Kizuguto'
Kizuguto amesema timu itafikia katika hotel ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Majina ya watakosafiri keshokutwa alfajri ni:
Walinda Mlango: Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul
Walinzi wa Pemebeni: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na Oscar Joshua
Walinzi wa kati: Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani
Viungo: Athumani Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari na Omega Seme
Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza 
Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni
Kocha Mkuu: Ernest Brandts,
Kocha msaidizi: Fred Felix Minziro,
Kocha wa makipa: Razaki Siwa,
Daktari wa timu: Dr.Suphian Juma,
Meneja wa timu:  Hafidh Saleh,
Afisa wa Habari : Baraka Kizuguto
na kiongozi mkuu wa msafara: Mohamed Nyenge ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya

Thursday, December 27, 2012

KENYA YATOA MAREFA WAWILI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA - TANZANIA, UGANDA MMMMMMH

Waamuzi wawili wakubwa nchini Kenya wamechaguliwa kwenda nchini Afrika ya Kusini kwenda kuamua mechi ya Africa Cup of Nations (Afcon) zitakazoanza mwezi ujao huko kusini mwa bara la afrika. 

Aden Marwa, ambaye ni mwalimu kutoka Nyanza kusini, amechaguliwa pamoja na refa mwingine Sylvester Kirwa, kutoka Eldoret. 

Wawili hao wamechaguliwa kuamua mechi za michuano hiyo baada ya kushiriki katika kozi ya CAF ya marefa iliyofanyika huko Egypt mapema mwezi uliopita.

Marefa hao wa pekee kutoka ukanda huu wa Afrika mashariki wataenda South Africa siku ya jumanne tarehe 15, siku nne kabla ya michuano kuanza.

Marwa – ambaye alishiriki katika 2012 AFCON, zilizofanyika nchini  Gabon na Equatorial Guinea – amesema kuchaguliwa kwao kwenda AFCON ni ishara nzuri kwa soka la Kenya.

CHRIS KATONGO ATUNUKIWA NA WANAJESHI WENZAKE ZAMBIA

Nahodha wa mabingwa wa Afrika Chris Katongo ametunukiwa na jeshi la Zambia.

Katongo, ambaye ni ofisa wa jeshi la nchi hiyo, alitunukiwa tuzo ya heshima ya jeshi la Zambia na meja jenerali Toply Lubaya katika sherehe zilizofanyika huko Arakan barracks mwanzoni mwa wiki hii.

Tuzo hii ya heshima imekuja baada ya mshambuliaji huyo wa Zambia kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa BBC African Footballer of the Year award. 

Jeshi la nchi hiyo pia lilitoa tuzo na maua kwa wachezaji wengine wa Chipolopolo ambao ni maofisa wa jeshi - Felix Katongo na Nathan Sinkala. 

TUKIO LINGINE AMBALO SITALISAHAU MWAKA 2012- KIFO CHA PAPA MAFISANGO! R.I.P KAKA.

BRUNO GOMES MBRAZIL ANAYEKUJA OLD TRAFFORD MWAKANI - AIPA UBINGWA TIMU YAKE - ACHUKUA KIATU CHA DHAHABU

Mchezaji aliyesajiliwa na Manchester United kutoka Brazil Bruno Gomes ameiongoza klabu yake ya Desportivo Brasil kutwaa ubingwa nchini hiyo wa vijana wenye miaka U17. 

Gomes, 16, atajiunga na United kipindi kijacho kiangazi, alifunga hat trick katika fainali ya pili ya kugombea ubingwa huo dhidi  Marília, na mwishowe Desportivo wakashinda 6-0

Mshambuliaji huyo hatari, tayari amekuwa chaguo muhimu katika kikosi cha Brazil cha vijana chini ya umri wa miaka 17, amefunga mabao 27 katika mechi 32 na kubeba kiatu cha dhahabu.

United wana mahusiano rasmi na klabu ya Desportivo Brasil, ambao wachezaji wao wamefunga mabao 88 katika mechi 32 msimu huu.

Inaeleweka kwamba pamoja na Gomes, United wapo katika mazungumzo ya kumsajili winga wa Desportivo aitwaye Welder.
Desportivo pia walishinda ubingwa Milk Cup huko Northern Ireland mwaka huu.

ASILIMIA 82 YA MASHABIKI WA MADRID WANATAKA MOURINHO ATIMULIWE KAZI REAL MADRID

Mashabiki wa Real Madrid wameamua. Wanataka Mourinho aondoke Bernabeu.

Kufuatia kupigwa benchi kwa Casillas katika mechi dhidi ya Malagamtandao wa gazeti maarufu nchini Hispania MARCA.com uliuliza "Je inabidi Real Madrid imtimue Mourinho?" na majibu ya takribani wasomaji 100,000 yalikuja yakisema ndio kwa asilimia  82.4%.

Kwa mujibu wa MARCA, mapenzi baina ya washabiki wa Los Blancos na Mourinho yamekwisha kabisa. Madrid wamekuwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika kipindi cha hivi karibuni na kusababisha maneno mengi juu ya mustakabli wa kocha Jose Mourinho ndani ya klabu hiyo.

Real Madrid wapo nyuma kwa 16 dhidi ya viongozi wa La Liga Barcelona, na tayari Mourinho ameshasema kwamba ubingwa wa La liga msimu huu hawawezi kushinda tena, na inasemekana kwamba ikiwa atashindwa kuiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa 10 wa mabingwa wa ulaya basi Mreno huyo atatemeshwa kibarua chake mwishoni mwa msimu.

JAVIER CHICHARITO MWOKOZI AIPA UNITED USHINDI DHIDI YA NEWCASTLE - WAONGOZA LIGI KWA POINTI 7

 


Manchester United vs Newcastle 4:3 MOTD by UCL2410

ADAM JOHNSON AWAFUNZA ADABU MAN CITY - SUNDERLAND WAKISHINDA 1-0



Sunderland vs Manchester City 1:0 MATCH HIGHLIGHTS by UCL2410

GARETH BALE APIGA HAT TRICK - SPURS WAKIIFUNGA VILLA 4-0



Aston Villa vs Tottenham 0.4 GOALS HIGHLIGHTS by UCL2410

LIVERPOOL HALI YAZIDI KUWA TETE EPL - YATANDIKWA 3-1 NA STOKE CITY



Stoke vs Liverpool 3:1 GOALS HIGHLIGHTS by UCL2410

CHELSEA MWENDO MDUDNDO - YAIKUNG'UTA NORWICH 1-0



Norwich vs Chelsea 0.1 MATCH HIGHLIGHTS by UCL2410

Wednesday, December 26, 2012

YANGA YASAJILI SHABIKI WA SIMBA IKIDUNGWA MOJA MTUNGI NA TUSKER

Aliyekuwa Shabiki Mkuu wa timu ya Simba akiwadhihaki mashabiki wa timu hiyo baada ya kutangaza kwamba kuanzia leo atakuwa anaishabikia Simba.


 Jamani mi ni Yanga Siyo Simba tena
Mchezaji wa timu ya Tusker FC ya Kenya aliyewahi kuichezea Yanga, Joseph Shikokoti mwenye jezi 18 akisalimiana na wachezaji wa Yanga kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.
Joseph Shikokoti wa TuskeR FC akipiga mpira na kichwa mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. Yanga yafungwa 1-0 kwa njia ya Penalti (PICHA ZOTE KWA HISANI YA http://amanitanzania.blogspot.com/)

EXCLUSIVE: SHABAAN KADO ASAJILIWA COASTAL UNION


NINI BALLON D'OR - RONALDO ATOSWA KATIKA TUZO ZA MASHABIKI WA MADRID - CASILLAS MCHEZAJI WAO BORA 2012

Hivi sasa inaonekna ni wazi Lionel Messi atatajwa kuwa mchezaji bora wa dunia mapema mwezi ujao, akimshinda mpinzani wake wa karibu Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa hakubaliki hata na mashabiki wa klabu yake ya Real Madrid.

Katika utafiti rasmi uliofanywa na taasisi moja huko jijni Madrid umeonyesha kwamba Nahodha wa timu hiyo Iker Cassilas na beki wa kulia Sergio Ramos ndio wachezaji bora wa klabu hiyo kwa mwaka huu wakifuatiwa na mreno Cristiano Ronaldo - kwa mujibu kura za washabiki 30,000.

Katika utafiti huo mashabiki wamewapa Wahispani Casillas na Ramos wastani wa 6.9 huku Ronaldo akiwafuatia kwa kupata wastani wa 6.6.

Hali hii inaonekana itazidi kumfanya Ronaldo kukosa furaha kama mwenyewe alivyosema huko nyuma, na kwa hakika itazidi kuongeza tetesi za mshambuliaji huyo kutaka kuondoka Santiago Bernabeu huku vilabu vya Man City, Man United na PSG wakiwa tayari na ndoano zao kumvua samaki wa gharama zaidi katika bahari ya soka.

ZENGWE: HII NDIO TIKETI ALIYOUZIWA UHURU SELEMANI KWA AJILI YA MECHI YA YANGA VS TUSKER



Tuesday, December 25, 2012

CHEMSHA BONGO YA CHRISTMAS: HUYU NI NANI?


KATONGO: SHOMARI KAPOMBE NI HATARI - AENDE AKACHEZE SOKA LA KULIPWA NJE

KIUNGO msumbufu wa Zambia, Felix Katongo, amemkubali sana  Shomari Kapombe wa Simba na Taifa Stars na amemshauri kusaka timu nje ya nchi.

Katongo alisema: "Nafikiri Tanzania (Taifa Stars) ilicheza vizuri. Lakini nilivutiwa zaidi na beki wa kushoto, (Shomari Kapombe)," alisema staa huyo anayekipiga na klabu ya Green Buffaloes.

Felix, ambaye kaka yake ni nahodha wa Zambia, Christopher Katongo aliongeza: "Nafikiri bado ni mchezaji mdogo. Pia, anatakiwa kujiendeleza kisoka kufikia malengo aliyojiwekea.

"Nilivutiwa zaidi na jinsi alivyokuwa akicheza hasa utulivu wake. Pia, kusaidia timu kushambulia, alitusumbua sana," alisisitiza.

Katongo ndio aliongoza kwa kupiga mashuti kwenye lango la Stars kama ilivyokuwa kwa Kapombe licha ya kucheza nafasi ya ulinzi. 


Source:Mwanaspoti

STOPPILLA SUNZU: MDOGO WAKE FELIX SUNZU ANAYEKWENDA KUPAMBANA NA AKINA ROONEY EPL

STOPPILA Sunzu anaaminika kuwa miongoni mwa mabeki bora barani Afrika kutokana na mchango wake kwa mafanikio ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na timu ya Taifa ya Zambia, Chipolopolo.

Beki huyo wa timu ya Taifa ya Zambia, ambaye ni mdogo wake mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu, amepata mafanikio makubwa kisoka katika siku za karibuni.

Unaweza kutumia ule msemo maarufu kuwa huyu jamaa `kila anachogusa basi kinageuka dhahabu' kutokana na mafanikio haya.

Kumbuka ndio shujaa huko kwao Zambia kwani ndio aliifungia nchi yake penalti ya mwisho iliyowasaidia kutwaa Kombe la Afrika baada ya kuibuka na ushindi mabao 10-9 kwa penalti dhidi ya Ivory Coast mwanzoni mwa mwaka huu.

Yalikuwa ni mafanikio makubwa kwa soka la Zambia kwani kumbuka ilikuwa imeshiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mara 15 bila ya mafanikio.

Baada ya fainali zile, Stoppila alitajwa katika kikosi bora katika mashindano yale yaliyofanyika katika nchi za Gabon na Equatorial Guinea.

Pia Stoppila amefanya makubwa na klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwani amekuwa nguzo ya timu hiyo kutwaa mara mbili mfululizo taji la Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka ya 2009 na 2010.

Pia ilipofika fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia mwaka 2010.

Stoppila pia alishika nafasi ya pili katika kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika anayecheza barani humu wakati wa sherehe zilizofanyika Accra, Ghana, wiki iliyopita.

Kufuatia mafanikio ndio maana Stoppila anatakiwa Ulaya na anakwenda Uingereza kujiunga na Reading inayoshiriki Ligi Kuu England.

Stoppila alikuwa Tanzania akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' na kucheza dakika 45 za mwishoni akiwa na jezi namba 13 kwenye mechi ya kirafiki na Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Stoppila anafanana kwa sura na kaka yake, Felix kwa rangi ni maji ya kunde, mrefu na ana umbo linalomfaa kucheza soka sehemu yoyote duniani.

Watanzania walipata bahati ya kumshuhudia nyota huyo 'kitasa' ambaye hataki mchezo anapokuwa katika himaya yake kutokana na uwezo wake wa kucheza kwa kutumia akili.

Anajua anachokifanya hana majivuno wala majigambo ndani au nje uwanja licha ya kuwa na mafanikio makubwa kisoka katika siku za karibuni.

Ujio wake uliifanya Mwanaspoti imtafute ili kufanya mahojiano naye ya kina naye alifunguka kila kitu.

Safari ya Ghana
Stoppila aliwasili Ijumaa iliyopita tofauti na wenzake ambao walitua nchini Jumatano iliyopita kwa ajili ya mechi na Taifa Stars.

Alichelewa kutokana na kwenda Ghana alikokuwa amehudhuria sherehe za Tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika ambako alishika nafasi ya pili nyuma ya nyota wa Al-Ahly ya Misri, Mohamed Aboutrika kwenye kuwani tuzo ya wale wanaosakata soka barani Afrika.

Hata hivyo, pamoja na kukosa tuzo hiyo bado alipata mafanikio kwani kikosi cha Zambia ndio kilitajwa kuwa ndio timu bora ya Afrika kwa mwaka 2012.

"Kitendo cha Zambia kupata tuzo hiyo ni mafanikio makubwa kwa upande wangu na zawadi kwa Wazambia na Waafrika wote kwa ujumla.

"Nafikiri mafanikio yote haya yanatokana na kujituma na kushirikiana vizuri na wenzangu," anaongeza Stoppila.

Amepania kung'ara Ulaya
"Nakwenda kuchezea Reading na nategemea kuondoka Zambia kwenda Uingereza baada ya siku chache na nikifika huko nitakwenda kukamilisha mkataba," anaeleza Stoppila.

Stoppila, hata hivyo, mara ya kwanza alitajwa kuwa anakwenda kujiunga na Arsenal ingawa amekwama baada ya klabu hiyo kutaka kumfanyia majaribio.

"Sitaenda kucheza Arsenal kwa sababu wanataka kuniona nikicheza mechi zaidi. Kocha Arsene Wenger anataka kuona uchezaji wangu.

"Ninategemea mambo yatakwenda vizuri Reading ingawa kwa sasa akili yangu ni kuisaidia Zambia kuibuka kidedea huko Afrika Kusini,"anasema Sunzu.

Sunzu anaeleza amefurahia nafasi ya kwenda kucheza England kwani malengo yake mara zote yamekuwa kucheza Ulaya.

"Hii ni nafasi muhimu katika maisha yangu ya soka. Nitajituma ili kila kitu kiende sawa."

Kutetea ubingwa wa Afrika huko Afrika Kusini
Pamoja na kufungwa na Taifa Stars bao 1-0, Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Sunzu anasema hilo haliwachanganyi kwa sababu wana kikosi imara na cha ushindi.

Zambia inajiandaa kutetea taji lake wakati wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Afrika Kusini mwaka 2013.

"Mashindano ya Afrika Kusini yatakuwa magumu lakini tumejiandaa vya kutosha kuhakikisha tunashinda mechi zote na kutetea ubingwa wetu,"anasema Stoppila.

"Kwa sasa tuko vizuri na hatuogopi timu yoyote tutakayokutana nayo huko Afrika Kusini.

"Wengi waliocheza mechi ya Stars ni yosso. Wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza wako Afrika Kusini na klabu zao.
"Kocha alitumia mchezo huu kuwajaribu yosso. Mimi mwenyewe nilicheza nikiwa na maumivu.

"Tumetoka Ghana bila kupumzika. Niliingia uwanjani nikiwa na maumivu ya mguu na misuli lakini nikacheza tu."

Historia
Stoppila amechanganya damu kwani baba yake mzee Felix Sunzu ni Mkongomani aliyezaliwa Jimbo la Katanga na mama yake ni Mzambia.

Alikulia Zambia ambako ndiko wazazi wake waliweka makazi katika mji wa Ndola kabla hawajahamia kwenda Chilambo nchini humo.

Stoppila ni wa tatu kuzaliwa kati ya watoto saba na Felix wa Simba ndiyo wa kwanza, Leticia wa pili, Stoppila wa tatu.

Jackson ambaye anaichezea Konkola Blades pamoja na Boniface wanafuatana wakiwa wa nne na wa tano, Ngossa ni wa sita na Chrementine wa saba.

Yeye ni baba wa mtoto mmoja aliyempa jina lake la Stoppila hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi maisha yake.

STOPPILA FELIX SUNZU
Amezaliwa: Juni 22, 1989
Mahali: Ndola, Zambia
Urefu: Ft 6 na inchi 3
Nafasi: beki ya kati na kiungo mkabaji
Klabu: Konkola Blades 2005�2008,
Zanaco 2008�2009,
LB Chateauroux 2008�2009,
TP Mazembe 2009�
Taifa: Zambia


SOURCE: MWANASPOTI

Monday, December 24, 2012

KUELEKEA MATAIFA YA AFRIKA: SHOLA AMEOBI AKATAA KUICHEZEA NIGERIA - VICTOR MOSES ARUHUSIWA KUICHEZA SUPER EAGLES

Mshambuliaji wa Newcastle United Shola Ameobi amesema kuwa hatashiriki katika michuano ya kuwania Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika na timu ya taifa ya Nigeria.
Haya ni kwa mujibu wa kocha mkuu wa klabu hiyo Allan Pardew.
Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21, ametajwa katika kikosi kitakachoakilisha Nigeria katika fainali hizo zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini.
Kocha wa Nigeria Stephen Keshi amesema ana mataumaini makubwa kuwa mchezaji huyo atabadili uamuzi huo na kujiunga na timu hiyo kabla ya kuelekea nchini Afrika Kusini.
Lakini Pardew amesema mchezaji huyo mwenye umri wa maika 31, hataweza kushiriki katika fainali hizo za Afrika zitakazoanza tarehe kumi na tisa Januari.
Ameobi alizaliwa katika eneo la Zaria, Kaskazini mwa Nigeria kabla ya kuhamia Uingereza kuishi na wazazi wake akiwa na umri wa miaka mitano.

Chini ya sheria za FIFA wachezaji ambao wamewakilisha taifa moja katika mashindano ya vijana chipukizi anaweza kuichezea timu ya taifa lingine ikiwa atatimiza masharti yaliyowekwa
Ameobi alijumuishwa katika kikosi cha Super Eagles miaka kumi iliyopita lakini alikataa kujiunga nalo akisema nia yake ilikuwa ni kuichezea timu ya taifa ya Uingereza.
Mchezaji huyo hata hivyo alipewa kibali na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA kuichezea taifa lake mwezi uliopita pamoja na mchezaji wa Chelsea Victor Moses.
Alicheza mechi yake ya kwanza na Super Eagles mwezi uliopita wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Venezuella ambapo Nigeria ilishinda kwa magoli matatu kwa moja.
Nigeria imo katika kundi la C na itacheza na mabingwa watetezi Zambia, Ethiopia na Burkina Faso katika mechi za raundi ya kwanza.

MWANGALIE RAISI WA MADRID MARA BAADA YA KUTOLIONA JINA LA CASILLAS KWENYE KIKOSI.

SERENGETI BREWERIES NA KAMPENI YA SAY IT WITHOUT SAYING IT

Meneja wa Kampuni ya Kioo Ltd Bw. Kishir, akipokea oda ya vinywaji vikali vya Johnnie Walker kutoka kwa balozi wa vinywaji vikali wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd baada ya kufanya oda hiyo na kufungiwa kwenye mfumo mzuri wa zawadi. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Kioo Ltd zilizopo Chang’ombe. Kampeni hii ya kutoa zawadi za mwisho wa mwaka zinaendeshwa kwa msemo usemao ‘Say it Without Saying it’. Maana yake toa zawadi kwa uwapendao badala ya kusema kwa maneno. Hivyo zawadi ya Johnnie Walker ndio muafaka kwa kipindi hiki.





SOWETO FC YAANZA VIBAYA LIGI YA MKOA WA KILIMANJARO

Na Fadhili Athumani, Moshi

23, Desemba

BINGWA mtetezi wa Ligi daraja la Tatu ya Mkoa wa Kilimanjaro, Timu ya Soweto FC kutoka Moshi mjini, imeanza vibaya kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa kukubali kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa Newgeneration FC nayo ya Mjini hapa ya goli 4-2.

Mabingwa hao, walijikuta wakiruhusu goli la mapema, katika dakika ya 22 tu, kipindi cha kwanza, baada ya mabeki walionekana kumsahau Mchezaji hatari wa Newgeneration FC, Peter Julius, aliyeunganisha krosi ya Chikoma Jafari na kuiandikia timu goli la kuongoza.

Mara baada ya goli hilo wachezaji wa Newgeneration waliamka huku wakitandaza soka safi na kuishambulia lango la Soweto, mashambulizi yaliyozaa matunda katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza, kwa goli la Chikoma Julius ambaye alikuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Soweto FC.

Ikiwa imesalia dakika moja tu kipindi cha kwa kimalizike, Chikoma Julius ambaye anatarajia kufanya majaribio na tinu ya Azam FC ya Dar es salaam, mapema Januari mmwakani alirudi tena kumsalimia mlinda mlango wa Soweto FC, Bruno John na kufanikiwa kufanya timu yake iende mapumziko ikiongoza kwa goli 3-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Soweto wakionesha uhai na kufanya mashambulizi ya kushtukiza ambapo katika dakika ya 52, walifankiwa kupata goli la kwaza kupitia kwa Brian Shilela, aliyepiga mpira wa adhabu uliokwenda moja kwamoja wavuni na kufanya matokeo yasomeke 3-1.

Magoli mengine yalifungwa na Chikoma Julius, aliyeondoka na mpira kwa kufunga magoli matatu kwa mguu wake, “Hat-trik” huku goli la pili la Soweto likifungwa na Mrisho Mindu na hadi mwamuzi wa mchezo, Thomas Mkombozi anapuliza kipenga matokeo yalikuwa ni 4-2.

Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa Jumamosi ambayo ilikuwa ni siku ya Uzinduzi wa ligi daraja la Tatu mkoani hapa kwa msimu wa mwaka 2012/2013, ukiacha mchezo huu, uliochezwa katika kituo cha Moshi, kwenye uwanja wa Mimoria Jamhuri, Machava FC ya Moshi mjini ilioibamiza Kurugenzi FC ya Same, 4-1 katika kituo cha Holili.

Katika kituo cha Himo, Kilototoni ikiwakaribisha Kilimanjaro FC, ilijikuta iking’ang’niwa shati na vijana hao wa mjini, kwa kufungana goli 1-1. Ligi hiyo itaendelea leo (Jumapili) kwa michezo mitatu katika vituo vya Hino, Moshi na Holili ambapo katika kituo cha Moshi kwenye uwanja wa Jamhuri Mimoria, Forest FC iliumana na Kia Junction.

Kituo cha Holili, kitashuhudia Tarakea FC ikiumana na Mwanga FC, wakati huo huo Vijana FC ikushuka dimbani kutafuta heshima kutoka kwa Kralle FC.

Tanzania Video Tournaments at Coco Beach on X-Mas Eve

Good news, once more the Tanzania Video Games Tournament community brings together the best gamers in Dar this Monday at Coco Beach beach from 19 hrs for FIFA 13 and Mortal Kombat 9 tournament.This is the inter-networking tournament for gamers and winners will walk away with cash prizes. This is the second and last event for 2012. Be there.."Game on"

Merry X-Mas and Happy New year.

TAARIFA KUTOKA TFF!

MTIGINJOLA KUONGOZA KAMATI YA RUFANI YA UCHAGUZI TFF
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Idd Mtiginjola kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF iliyoundwa kutokana na marekebisho ya Katiba yaliyofanyika hivi karibuni.

Mtiginjola ambaye ni Wakili wa kujitegemea ataongoza kamati hiyo yenye wajumbe watano ambayo sasa itakuwa chombo cha mwisho kusikiliza rufani zinazotokana na uchaguzi wa TFF, na wanachama wa TFF ambao hawatakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Kabla ya uteuzi huo, Mtiginjola alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana. Nafasi yake katika kamati hiyo na ile ya mjumbe mwingine Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shabani Semlangwa aliyefariki dunia Julai mwaka huu zitajazwa hivi karibuni.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambayo vinara wake (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) wanatakiwa kitaaluma kuwa wanasheria ni Francis Kabwe. Kabwe ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Wajumbe wengine walioteuliwa na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake cha jana (Desemba 23 mwaka huu) ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Mohamed Mpinga ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria.

Wengine ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Profesa Madundo Mtambo ambaye kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, na mdau wa soka Murtaza Mangungu ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini.



MECHI YA STARS, CHIPOLOPOLO YAINGIZA MIL 109/-
Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia (Chipolopolo) lililochezwa juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh. 109,197,000.

Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi sh. 5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina (technical support) sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000.

Nyingine ni bonasi kwa Taifa Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 8,138,070.

Mapato ya mechi nyingine za Taifa Stars ilizocheza nyumbani mwaka huu yalikuwa Taifa Stars vs Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) iliyofanyika Februari 23 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sh. 32,229,000. Taifa Stars vs Msumbiji (Mambas) iliyochezwa Februari 29 mwaka huu sh. 64,714,000.

Taifa Stars vs Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 40,980,000. Taifa Stars vs Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zilipatikana sh. 124,038,000 na Taifa Stars vs Kenya (Harambee Stars) iliyofanyika Novemba 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza iliingiza sh. milioni 45.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

YANGA KUUMANA NA TUSKER YA KENYA KESHO TAIFA

Klabu ya Young Africans Sports Club itashuka dimbani siku ya jumatano (Boxing Day) kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tusker FC ya nchini Kenya, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 
Akiongea na waandishi wa habari Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema Kocha wa Yanga anatarajiwa kuwatumia wachezaji wake wote katika mchezo huo ambapo Yanga itatumia nafasi hiyo kuwatumia karibu wachezaji wake wote ambapo timu hiyo inajiandaa kwa maandalizi ya safari ya kuelekea nchini Uturuki kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
 
Mchezo huo utakua mchezo wa kwanza kwa Yanga tangu ligi iliposimama mwezi novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi Kuu ya Vodacom, hivyo itakua ni fursa kwa wanachama kuona timu yao ambayo ilianza mazoezi tangu tarehe 26 Novemba kujiandaa na mashindano mbali mbali aliesema "Kizuguto"
 
Pili itakua ni zawadi ya sikuuu ya X-Mass kwa wapenzi, wanachama na washabiki wa soka nchini, ambapo wapenda soka nchini watatumia fursa hiyo kusherekea sikukuu kwa kutazama soka safi ambalo hawajaliona kwa kipindi kirefu.
 
Tatu utakua ni mchezo wa mwisho katika kufunga mwaka kabla ya kusafiri kuelekea nchini Uturuki, pia ikitumia mchezo huo kuwaaga wapenzi, washabiki na wanachama wake kabla ya safari hiyo ya kambi ya mafunzo itakayochukua  ya takribani wiki 2.

Aidha Kizuguto ametangaza Viingilio vya mchezo huo kuwa ni Tsh 15,000/= VIP A, Tsh 10,000/= VIP B, Tshs 7,000/= VIP C, na Tsh 5,000/= kwa Orange, Blue na Green.

Kwa upande wa waandaji wa mchezo huo,  George Wakuganda amesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya Yanga na kwamba Yanga itatoa zawadi kwa mashabiki wake
 
Aidha amesema tayari wachezaji wa Tusker wameshawasili jijini Dar es Salaam, na kwamba mashabiki wa Yanga wajipange kupata burudani waliyo ikosa kwa kipindi kirefu kwa timu yao.

source:http://www.youngafricans.co.tz

HILI NI MOJA YA TUKIO KWANGU LILI-MAKE HEADLINES IN 2012 ?JE WEWE UNAKUMBUKA TUKIO GANI LA KI-SPOTI IN 2012 ?

Now Think Who Deserve Ballon d'Or :- Messi or Ronaldo ?

Photo: Now Think Who Deserve Ballon d'Or :- Messi or Ronaldo ?

Sunday, December 23, 2012

AZAM BINGWA UHAI CUP - YAIFUNGA KWA PENATI COASTAL UNION

Mchezo wa fainali ya kombe la Uhai Cup umeisha hivi punde katika uwanja wa Karume kwa Azam FC kushinda kwa penati baada ya kutoka sare ya 2-2 katika dakika 120 za mchezo huo.
Kwa maana hiyo Azam FC ndio mabingwa wapya wa Uhai Cup wakijizolea fedha taslimu shilingi 1.5 na nusu huku Coastal Union wakiambulia shilingi million 1 kama zawadi ya washindi wa wa pili.
ZAWADI NYINGINE ZILITOLEWA KAMA IFUATAVYO
Nafasi ya 3-Simba SC - 500,000
 
Kocha Bora-Bakari Shime(Coastal Union) -
300,000

Kipa Bora-Mansur A.Mansur(Coastal Union) -
300,000

Mfungaji Bora-Ramadhan magoli 6(Simba) -

300,000
Timu Yenye Nidhamu-Ruvu Shooting - 400,000
Mchezaji Bora - Joseph Kimwaga(Azam Fc) - 350,000
Refa bora-Isiaka Mwalile

SIMBA YASHIKA NAFASI YA TATU UHAI CUP - YAITIMBA 3-0 MTIBWA

Simba imetwaa nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu zenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuitandika Mtibwa Sugar ya Morogoro mabao 3-0.

Hadi mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa leo asubuhi (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam, Simba ilikuwa mbele kwa bao 1-0.

Mabao yote ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Ramadhan Mkipalamoto. Mfungaji alifunga bao la kwanza dakika ya 43 wakati mengine alipachika dakika za 57 na 70. Kwa kunyakua nafasi ya tatu, Simba imeondoka na kitita cha sh. 500,000.