Search This Blog

Saturday, February 2, 2013

LIVE MATCH CENTRE: YANGA 1-1 MTIBWA SUGAR - FULL TIME


DK 90 - YANGA 1-1 MTIBWA SUGAR 

Dk 85. Gooo..,! Kiiza anaipatia Yanga bao la kusawazisha akiunganisha krosi ya Said Bahanuz. Yanga 1-1 MtibwaDk 77. Yanga imefanya mabadiliko. Ametoka Frank Domayo ameingia Said Bahanuzi. 
Dk 72. Mtibwa imefanya mabadiliko. Ametoka Rashid Gumbo ameingia Awadh Juma. Yanga 0-1 Mtibwa

Dk 69. Mtibwa imefanya mabadiliko. Ametoka Ally Mohamed ameingia Jamal Mnyate. Yanga 0-1 Mtibwa

Dk 58 Mtibwa inatawala kiungo kutokana na Yanga kumtoa Chuji. 

Yanga imefanya mabadiliko. Ametoka Didier Kavumbagu ameingia Hamis Kiiza. Pia Yanga imefanya mabadiliko. Ametoka Athuman Idd Chuji ameingia Nurdin Bakar.

Kipindi cha pili kinaanza hapa uwanja wa taifa huku Mtibwa wakiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Yanga.
Mpira ni mapumziko, Young Africans 0 - 1 Mtibwa SugarDakika ya 45, Shaban Kisiga anaipatia Mtibwa Sugar bao la kwanza.
Young Africans 0 - 1 Mtibwa Sugar

Dk 34 Rashid Gumbo wa Mtibwa anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini kipa Ally Mustapha Barthez anaokoa hatari. Mpira unakuwa kona ambayo haina madhara.

Dakika ya 30, Young Africans 0 - 0 Mtibwa Sugar

Dk 24 Yanga inafanya mashambulizi kadhaa langoni kwa Mtibwa lakini kipa Hussein Sharrif Casillas anaokoa hatari zote.

Dk 12 Didier Kavumbagu wa Yanga anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Mtibwa

Mpira umeanza dakika ya tatu sasa! Timu zinashambuliana kwa zamu

Young Africans line-up to face Mtibwa Sugar today:
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Jerson Tegete
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Said Mohamed
2.Shadrack Nsajigwa
3.Stephano Mwasika
4.Juma Abdul
5.Nurdin Bakari
6.Omega Seme
7.George Banda
8.Nizar Khalfani
9.Said Bahanunzi
10.Hamis Kiiza
11.David Luhende
12.Rehani Kibingu


Mtibwa line up: Hussein Sharrif, Said Mkopi, Idrisa Rashid, Rajab Mohamed, Salum Sued, Shaaban Nditi, Vincent Barnabas, Rashid Gumbo, Hussein Javu, Shaaban Kisiga, Ally Mohamed

CAMEROON KUTUA KESHO NCHINI YATARI KUPAMBANA NA TAIFA STARS


Kundi la kwanza la Cameroon likiongozwa na kiungo wa zamani wa Toulouse ya Ufaransa ambaye sasa yuko Al Ahli ya Falme za Kiarabu (UAE), Achille Emana na Meneja wa timu hiyo Rigobert Song litatua nchini kesho (Februari 3 mwaka huu) saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM.

Wachezaji wengine katika kundi hilo ni Vincent Aboubakary anayechezea timu ya Valenciennes iliyoko Ligi Kuu ya Ufaransa, kipa Charles Itandje anayedakia timu ya POAK FC ya Ugiriki, Kocha wa viungo Sylvain Monkam.

Mshambuliaji wa Anzhi Makhachkala ya Urusi ambaye ndiye nahodha wa Cameroon, Samuel Eto’o ataongoza kundi la pili litakalowasili nchini Februari 4 mwaka huu (saa 3.45 asubuhi) kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi, Kenya.

Wengine katika ndege hiyo Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik wakati Kocha wa timu hiyo Jean Paul Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Afrika Kusini.

Februari 4 mwaka huu kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM ambalo lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya Ufaransa.

Wachezaji waliobaki wakiongozwa na kiungo wa Barcelona, Alexandre Song watawasili Februari 5 mwaka huu kwa muda tofauti kwa ndege za KLM na Kenya Airways.

SAMATA 'SAMAGOAL' NA ULIMWENGU KUTUA KESHO KWA AJILI YA MECHI YA CAMEROON


Washambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanatarajia kutua nchini kesho (Februari 3 mwaka huu) tayari kwa mechi ya Cameroon itakayochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Samata na Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) watawasili saa 11.10 jioni kwa ndege ya PrecisionAir na kwenda moja kwa moja kambi hoteli ya Tansoma.

Wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanaanza kuripoti kambini leo jioni (Februari 2 mwaka huu) mara baada ya mechi kati ya Yanga na Mtibwa Sugar.

Mechi hiyo iliyo katika Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) pia itatumika kwa ajili ya kutoa ujumbe wa vita dhidi ya Malaria viwanjani, ugonjwa unaoongoza barani Afrika kwa kusababisha vifo vya watoto na wajawazito.

TFF kama ilivyo Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA imekuwa msitari wa mbele katika kueneza kampeni ya vita dhidi ya Malaria inayoongozwa United Against Malaria (UAM). Rais wa TFF, Leodegar Tenga na nahodha wa Cameroon, Samuel Eto’o ni miongoni mwa mabalozi wa vita dhidi ya Malaria barani Afrika.

MASHINDANO YA KLABU BINGWA YA NGUMI KWENYE PICHA


Mabondia Kombe Ally wa Luaha Galax akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Said Hofu wa JKT Makao Makuu wakati wa mashindano ya Klabu Bingwa yaliyofanyika uwanja wa Ndani wa Taifa.Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Said Hofu
Mabondia wa timu ya JKT Makao Makuu kutoka kushoto ni Ismail Gaitano,Hmidu Alfani,Khamis Husein na Wambura Amiri klabla awajaingia kwenye mipambano yao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Wambura Amir akipasha misuri moto  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Kidunda wa Ngome kulia  akimuazibu Mohamedi Chibumbui wa Magereza wakati wa mashindano ya Klabu bingwa yaliyofanyika uwanja wa ndani wa taifa Kidunda alishinda kwa K,O rauni ya kwanza na kuzima ngebe za Chibumbui na kusababisha kumpoteza fahamu kwa takribani dakika 4 ambazo alikuwa akipewa uduma ya kwanza uringoni alipodondoka baada ya kupata makonde yenye kilo nzito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mohamedi Chibumbui kushoto akitafuta mbinu ya kumkepa bondia Selemani Kidunda wakati wa mashindano ya klabi bingwa ya Masumbwi Kidunda alishinda K,o raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Kidunda wa Ngome kushoto akipigwa konde na Mohamed Chibumbui wa Magereza wakati wa mpambano wa Klabu bingwa Kidunda alishinda kwa K,O raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Selemani Kidunda wa Ngome kushoto akipigwa konde na Mohamed Chibumbui wa Magereza wakati wa mpambano wa Klabu bingwa Kidunda alishinda kwa K,O raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Kidunda akikimbilia kona Nyeupe baada ya kumkalisha chini Mohamed Chibumbui kwa konde zito wakati wa mchuano wa Klabu Bingwa TAIFA iliyofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Kidunda alishinda  K,O raundi ya kwanzaPicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Kidunda akikimbilia kona Nyeupe baada ya kumkalisha chini Mohamed Chibumbui kwa konde zito wakati wa mchuano wa Klabu Bingwa TAIFA iliyofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Kidunda alishinda  K,O raundi ya kwanzaPicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

NIGERIA WAPEWA AHADI YA NGONO BURE WIKI MOJA NA CHAMA CHA MACHANGUDOA NCHINI KWAO IKIWA WATABEBA UBINGWA WA AFRIKA


Prostitutes
Machangudoa nchini Nigeria wamesema wamefurahia sana ushindi wa Super Eagles dhidi ya Ethiopia katika mashindano ya AFCON yanayoendelea nchini Afrika ya Kusini.
Machangudoa hao kupitia chama chao cha aegis of Nigeria Association of Prostitutes  wamewasisitiza wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria kujitahidi na kushinda kombe hilo. Katika taarifa iliyotolewa na kusainiwa na katibu mkuu wa chama hicho Jessica Elvis. 
 “Tunapenda kuwapongeza wachezaji na makocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles kwa kufuzu kuingia robo fainali raundi inayofuatia ya mashindano. Tungependa kuwapa uhakika wa sapoti yetu ili waweze kuleta ushindi nyumbani. 
"Katika kuonyesha sapoti yetu kwa timu ya taifa, tutatoa ofa ya wiki moja ya mapenzi bure kwa Super Eagles ikiwa watashinda ubingwa wa Afrika," alisema katibu mkuu wa chama hicho cha machagundoa.
Inasemekana baadhi ya wanachama wa chama hicho wapo nchini South Africa wakiisapoti timu hiyo kwenye mashindano ya AFCON.

Friday, February 1, 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HAFLA YA KUITATHMINI LIGI KUU YA VODACOM - WAHARIRI.

Baadhi ya wahariri wa magazeti ya michezo wakimsikiliza Katibu wa  TFF Angetile Osiah,wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.

 
Katibu wa  TFF Angetile Osiah(kushoto)akimsikiliza jambo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa, wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa,akizungumza  na wahariri wa vyombo mbalimbali wa michezo pamoja na wageni waaligwa wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa  chama cha waandishi wa habari Tanzania Bw.Juma Pinto akizungumza na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali wa michezo pamoja na wageni waaligwa wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.


Mwandishi wa habari wa Clouds radio Bw.Shafii Dauda (kushoto)akibadilishana mawazo na Afisa udhamini wa Vodacom Tanzania,Bw.Ibrahim Kaude, wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa  chama cha waandishi wa habari Tanzania Bw.Juma Pinto akizungumza na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali wa michezo pamoja na wageni waaligwa wakati wa Hafla ya kuitathmini ligi kuu ya Vodacom iliyoandaliwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.

EMMANUEL OKWI AANZA KWA KUWAFUNIKA MASTAA WENZAKE WALIOSAJILIWA NA ETOILE DU SAHEL


EMMANUEL Okwi ameanza vizuri katika kikosi chake kipya cha Etoile du Saleh ya Tunisia, baada ya kuwafunika mastaa wenzake watatu waliosajiliwa katika majira ya baridi.


Mtandao wa klabu hiyo Etoile-du-Sahel.com umewashindanisha Okwi raia wa Uganda aliyesajiliwa kutoka Simba pamoja na 

Mtunisia Oussema Boughanmi, Akoli Percy mshambuliaji wa Congo na Manzie Bidge kuwa nani mkali.
Ambapo mashabiki 367 walioanza kupiga kura kuanzia Januari 18 hadi leo Ijumaa wamemchagua Okwi kwa kura 225.


Mtunisia Oussema ambaye ni kiungo mkabaji yeye anafuatia baada ya kupigiwa kura 99, wakati Manzie amepata 27.


Akoli kutoka Congo ndiye anayeshika mkia baada ya kupigiwa kura za ndiyo 16 tu kwa mashabiki wote.


Kupata kura hizo ni kutokana na jinsi anavyowavutia mashabiki hao katika uwajibikaji wake kwenye mazoezi na mechi.

PAMOJA NA KUPATA USHINDI MARA MBILI MFULULIZO KOCHA WA AZAM HAJARIDHIKA NA KIWANGO CHA TIMU


KOCHA wa Azam FC, Stewart Hall amesema bado hajaridhishwa na safu yake ya ulinzi, licha ya kupata ushindi katika mechi mbili za awali. 
Azam FC imeshinda mechi mbili za kwanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar na Toto African na kuweka 'gap' la pointi mbili dhidi ya vinara Yanga yenye pointi 32 kibindoni.
Stewart aliliambia shaffihdauda.com baada ya mtanange huo kumalizika kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi kuwa pamoja na timu yake kushinda mechi mbili za awali kwa idadi ya mabao 3-1 kila mchezo, bado ana changamoto kubwa kuisuka safu yake ya ulinzi.
Mwingereza huyo alisema; "Nafikiri timu imeimarika kwa kiasi kikubwa. Lakini tuna tatizo sugu kwenye ngome yetu."
"Ukijaribu kufuatilia magoli mawili ambayo tumefungwa kwenye kila mechi dhidi ya Kagera na Toto hayana tofauti kubwa." alisema kocha huyo.
Alieleza kuwa mabeki wake wa kati Mkenya Jockins Atudo na Mtanzania David Mwantika kuna wakati wanajichanganya na kutoa mwanya kwa wapinzani kufunga mabao rahisi.
"Bado sijaridhishwa na uchezaji wao. Nimekuwa nikiwakumbusha kila wakati, lakini bado tatizo hilo wanalirudia." alisema Stewart.  
Aliongeza kuwa ni changamoto kwake kulifanyia kazi tatizo hilo na kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na Ligi Kuu Bara.
Azam FC imewasimamisha wachezaji wake wanne kwa tuhumu za kuchukua rushwa kwenye pambano dhidi ya Simba mzunguko wa kwanza wa ligi.
Nyota hao ni kipa Deogratius Munishi na mabeki Aggrey Morris, Said Morad na Erasto Nyoni. 

DOMAYO DIMBANI KESHO KUICHINJA MTIBWA

DAKTARI wa Yanga, Nassoro Matuzya amethibitisha kuwa Frank Domayo yupo fiti kuikabili Mtibwa Sugar kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jambo ambalo linamaanisha kuwa atasimama katika nafasi ya kiungo akishirikiana na Athuman Iddi 'Chuji'.
Domayo alishindwa kucheza pambano la kwanza dhidi ya Prisons ya Mbeya wikiendi iliyopita katika dakika za mwisho kutokana na kuugua ghafla akiwa tayari amepangwa kwenye kikosi cha wachezaji 11 watakaoanza mchezo huo. Yanga ilishinda mabao 3-1.
Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts alilazimika kufanya mabadiliko na kumpanga Nurdin Bakari badala ya Domayo. 
Hata hivyo, Nurdin aliimudu vizuri nafasi ya kiungo akishirikiana na Athuman Iddi 'Chuji' kuwalisha mipira mastraika Jerry Tegete na Mrundi Didier Kavumbagu.
Pia, Nurdin alitoa pasi ya bao la tatu, lililozamishwa na Jerry Tegete kama ilivyokuwa kwa Chuji aliyepiga pasi ndefu kwa Simon Msuva aliyepiga krosi iliyofungwa na Tegete aliyepachika mabao mawili na jingine likifungwa na Mbuyu Twite kwa shuti kali.
Matuzya aliiambia tovuti hii kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam kuwa hali ya Domayo kwa sasa imeimarika kwa asilimia kubwa isipokuwa uamuzi unabaki kwa kocha kumchezesha.
"Vipimo vilionyesha kuwa Domayo ana malaria," alisema Matuzya aliyerithi mikoba ya Juma Sufian aliyetupiwa virago na uongozi. 
Kwa upande wake, kocha Brandts amefurahishwa kurejea kwa kiungo huyo, kwani anaamini ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga hasa wakati huu wakiwa kwenye harakati za kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Nafikiri Domayo ni mchezaji muhimu kwetu. Kila mtu analijua hilo. Mchango wake unahitajika sana, hasa kipindi hiki tukiwa kwenye mbio za kuwania taji la ligi," alisisitiza.

MTIBWA KUISIMAMISHA YANGA KESHO UWANJA WA TAIFA?


Yanga na Mtibwa Sugar zinapambana kesho (Februari 2 mwaka huu) katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha ndiye atakayechezesha mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwani wakati Yanga ikiongoza ligi hiyo, wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mechi iliyopita walilala mbele ya Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo wa ligi kwa sasa.

Polisi Morogoro itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro wakati Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ruvu Shooting inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa.

Keshokutwa (Jumapili) kutakuwa na mechi mbili. Simba itaumana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Tanzania Prisons ikiikabili Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

VILLA SQUAD, MORO UNITED UWANJANI FDL
Villa Squad na Moro United zinaumana kesho (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoanza mzunguko wa lala salama.

Kundi A litakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea, na Polisi Iringa dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.

Mechi nyingine ya Kundi B itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Kundi C ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Morani dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi Mara na Pamba (Uwanja wa Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi wa kila kundi atapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

KUMUONA SAMUEL ETO'O DHIDI YA TAIFA STARS JUMATANO IJAYO NI SHILINGI 5000FECAFOOT YATAJA NYOTA WAKE 21, ETO’O NDANI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon (FECAFOOT) limetaja msafara wake wa watu 36 wakiwemo wachezaji 21 wa timu yao ya Taifa Indomitable Lions) wakiongozwa na nahodha Samuel Et’oo Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.

Kiongozi wa msafara wa timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari 3 mwaka huu) ni Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi. Naibu kiongozi wa msafara wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa ni Makamu wa Rais wa FECAFOOT, John Ndeh.

Mbali ya Et’oo, wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles Itandje, Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono, Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou.

Wengine ni Andre Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul Akono (Kocha Mkuu), Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque Songo’O (Kocha wa makipa), Dk. Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na Emmanuel Francis Ambane (Psychologist).

Pia wapo Tchonkontey Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa Timu), Aoudou Mvotoung (Team Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari FECAFOOT), Boubakar Ndou (Meneja Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky (Physiotherapist), Elias Kalaguem (Physiotherapist) na Justin Addo (Wakala wa Mechi).

Wakati huo huo, kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli ya Tansoma.

KUONA TAIFA STARS, CAMEROON 5,000/-
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya FIFA Date kati ya Taifa Stars na Cameroon itakayochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani.

Viti vya bluu ni sh. 7,000 wakati viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000. Kwa viti vya VIP viingilio ni kama ifuatavyo; VIP C sh. 15,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000.

Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohia/Samora, kituo cha mafuta OilCom Ubungo, Dar Live Mbagala na kituo cha mafuta Buguruni.


Thursday, January 31, 2013

SIKU YA MWISHO YA USAJIRI BARANI ULAYA - BECKHAM AENDA PSG KUTOA MSHAHARA WAKE KUSAIDIA JAMII

Mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa England David Beckham amesaini mkataba wa miezi mitano kuichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Katika kuonyesha uhamisho haukusababishwa na pesa kama kivutio David Beckham amesema mshahara wake wote wa £150,000 kwa wiki katika kipindi chote cha mkataba wake zitaenda kusaidia jamii watoto wasiojiweza huko jijini Paris Ufaransa.

Beckham amepewa jezi namba 32.

HUU NDIO USAJIRI AMBAO UMEKAMILIKA MPAKA SASA
1.Mario Balotelli (Man City to AC Milan, £19.5m),
2.Luciano Becchio (Leeds to Norwich, swap)
3.Urby Emanuelson (AC Milan to Fulham, loan),
4. Alejandro Faurlin (QPR to Palermo, loan),
5.Danny Graham (Swansea to Sunderland, £5m)
6.Steve Morison (Norwich to Leeds, swap),
7.Christopher Samba (Anzhi to QPR, £12.5m),
8.Paul Scharner (Hamburg to Wigan, loan),
9.Kieron Dyer (released by QPR to Middlesbrough)

MABAO 28 YATINGA KIMIANI MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU - TEGETE, NGASSA NA MCHA VIALI WATISHA

JUMLA ya mabao 28 yamefungwa kwenye mechi tisa za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulianza kutimua vumbi lake Januari 26, mwaka huu.

Kwa idadi hiyo ni sawa na wastani wa kila mchezo yamefungwa mabao matatu kwa mechi hizo tisa iliyochezwa kwenye viwanja vya mikoa tofauti.

Nyota Mrisho Ngassa wa Simba, Jerry Tegete wa Yanga, Khamis Mcha 'Vialli' wa Azam FC na Paulo Nonga wa Oljoro JKT walizifungia timu zao mabao mawili kila mmoja kwenye ushindi wa mabao 3-1.

Kiungo mchezeshaji wa Simba, Ramadhan Chombo 'Redondo' ameandika rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi.


Nyota huyo alipachika bao hilo katika dakika pili kwenye mchezo wa kukata utepe dhidi ya African Lyon uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda mabao 3-1.  

PINGAMIZI DHIDI YA MANJI, MALINZI, WAMBURA, NYAMLANI NA MENGINEY YOTE YATUPWA NA KAMATI YA UCHAGUZI TFF


Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi kama ifuatavyo:

1.                   Waombaji uongozi wa TPL Board

(a)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeid anayeomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na  Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:

(i)                   Si Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii)                 Si mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi  hiyo.


(b)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa  na  Ndg. Daniel T. Kamna na  Ndg. Juma Ally Magoma walioomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali Manji :

(i)                   Hana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) wa uendeshaji wa mpira wa miguu.
(ii)                 Hana sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(iii)                Hana elimu ya kidato cha nne
(iv)               Ameshindwa kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6), 18(1)b, 27 (2) na (5).

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma hazikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFFimezitupa pingamizi hizo.  

(c)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg.  Hamad Yahya Juma,kwamba Ndg. Hamad Yahya Juma:

(i)                   Si Mwenyekiti wa Klabu ya Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii)                 Si mkweli na mwadilifu na amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa klabu.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi ya Ndg. Frank M. Mchaki kwa kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake haikukidhi matakwa  ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.

2.                   Waombaji uongozi wa TFF

(a)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani K. Kambi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi aliwekewa pingamizi kwamba amefanya Kampeni kabla ya muda uliopangwa.

Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi.


(b)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Eliud P. Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella aliwekewa pingamizi na Ndg. Said Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter Naminga, kwamba Ndg. Mvella:

(i)                   Akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa kuleta maendeleo ya soka katika ukanda huo.
(j)                   Ana kesi ya rushwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa

Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.

(c)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Epaphra Swai anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie Chalamila, kwamba Ndg. Epaphra Swai:

(i)                   Alifanya ubadhilifu wa fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA).
(ii)                 Alitumia madaraka yake vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.
(iii)                Alivunja Katiba ya MZFA na FIFA
(iv)               Anavuruga shughuli za uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa wawekaji pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na vielelezo vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya hila na udanganyifu (collusion) dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) na hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.

(d)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Vedastus F.K Lufano na Ndg. Mugisha Galibona wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg. Galibona waliwekewa pingamizi  na Ndg. Paul Mhangwa kwamba  hawana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu wa miaka mitano (5).

Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).


(e)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Michael R. Wambura anayeomba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg. Josea Samuel Msengi kwamba Ndg. Wambura:

(i)                   Alikiuka Katiba ya TFF kwa kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu masuala ya uchaguzi.
(ii)                 Alikosa uadilifu kwa kutumia kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi aliyokuwa aniongoza akiwa Katibu Mkuu wa FAT.
(iii)                Amekuwa akijaribu kupotosha umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake kwa kutumia haki na kuviita ‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo Courts).
(iv)               Mwaka 2004 alikiri kwamba alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari kwa kuwa alikuwa akivipa pesa na kwamba vyombo vya habari vilimgeuka kwa sababu aliacha kuwapa waandishi pesa.
(v)                 Mwaka 2004 alikataa kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu Mkuu wa FAT iwe ya kuajiliwa.
(vi)               Alikosa uwezo wa kutekeleza wajibu na malengo ya TFF.

Ndg. Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg. Wambura. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Said Rubea Tamim kwa kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).

(f)                  Pingamizi dhidi ya Ndg. Jamal E. Malinzi anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF; Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape Fue kwamba:

(i)                   Alivunja Katiba ya TFF kwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa wanachama wa TFF kikiwemo Chama chake cha Mkoa wa Kagera haviheshimu wala kutekeleza maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na FIFA baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba kwa njia ya Waraka, ambayo yalihusisha pia  maagizo ya FIFA na CAF
(ii)                 Hana sifa ya uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
(iii)                Anakosa uadilifu na haiba ya kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.


Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Agape Fue kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi hilo.

(g)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na  Ndg. Mintanga Yusuph Gacha na Ndg. Medard Justiniani kwamba:

(i)                   Ni Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni mtumishi wa umma hivyo alikosa kigezo na sifa ya kugombea nafasi ya urais wa TFF.
(ii)                 Anakatazwa na Judicial Service Act, Public Service Act 2002 na Code of Conduct for Judicial Officers of Tanzania kugombea nafasi aliyoomba ya Rais wa TFF.
(iii)                Kutakuwa na Mgoganao wa kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais wa TFF.
(iv)               Amekosa umakini na uadilifu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha Akanunti za TFF kufungiwa na TRA.

Ndg. Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo halikujadiliwa na Kamati. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Medard Justiniani kwa kuwa alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa alikuwa na ufahamu wa kutosha wa pingamizi lake ikiwa ni pamoja na viambatanisho vyake, hali iliyotanabaisha kuwa pingamizi hilo lilikuwa na chembechembe nyingi za hila na udanganyifu.Angetile Osiah
KATIBU
KAMATI YA UCHAGUZI