Search This Blog

Saturday, June 15, 2013

VIDEO - LIONEL MESS APIGA HAT TRICK NA KUMPITA RASMI MARADONA KWA MAGOLI YA KIMATAIFA



Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi jana usiku alifunga mabao matatu kwenye dhidi ya Guatemala hivyo kutimiza mabao 35 tangu aanze kuichezea Argentina. Mabao hayo 35 yanamfanya Messi amfikie Hernan Crespo mwenye mabao 35 na kumpita gwiji wa nchi hiyo Diego Maradona mwenye mabao 34.

Kinara wa mabao wa nchi ni Gabriel Batistuta ambaye alitumbukiza nyavuni mipira 56.

TABIRI KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOANZA KESHO DHIDI YA IVORY COAST - MSHINDI ATAJIPATIA VOUCHER YA 10000


CHEMSHA BONGO: HAWA NI WATOTO WA MWANASOKA MAARUFU DUNIANI?


MABADILIKO MAKUBWA KWENYE SHERIA ZA SOKA YAFANYIKA

Mkutano mkuu  wa 127 wa bodi ya vyama vya kimataifa vya soka (IFAB) ulifanyika huko Edinburgh (Scotland) tarehe 2 Machi 2013 . Mabadiliko ya sheria za mchezo wa soka yalipitishwa  kwenye mkutano huo pamoja na maelekezo kadhaa ambayo yameorodheshwa hapo chini.

Sheria za Mchezo na maamuzi ya bodi.

1.Sheria ya 11.- Tafsiri ya sheria za mchezo ( off side).

Mjadala wa ile dhana ya "kuingiliana na mpinzani wakati mchezo unaendelea yaani "Intefering with an opponent" pamoja na kujipatia faida kutokana na kitendo hicho yaani "ganing an advantage"

Dhana kwa jinsi ilivyo kwa sasa.

Katika mazingira ya sheria ya 11 ya kuotea au off side mambo yafuatayo huwa yanazingatiwa .

*"Interferring with play ina maana kuugusa mpira ambao umepigwa au kuguswa na mtu ambaye anatoka kwenye timu moja na mtu aliyeugusa .

* "interfering with an opponent" ina maana kumzuia mpinzani asicheze mpira kwa kukaa mbele yake makusudi kuzuia upeo wake wa kuuona mpira  yaani obstruction au kufanya vitendo au ishara ambazo kwa tafsiri ya mwamuzi vinaweza kumdanganya mpinzani au kumuondoa mawazo yake ya kuucheza mpira .

* "kujipatia faida kwa kuwepo kwenye nafasi husika kuna maana ya kucheza mpira ambao umedunda kwenye lango yaani rebound huku mfungaji akiwa kwenye eneo la kuotea .

Tafsiri mpya.

Katika mazingira ya sheria ya 11 , tafsiri zifuatazo zitazingatiwa .

* "kuingilia mchezo au interfiring with play" kunamaanisha Kuucheza au kuugusa mpira ambao umetoka kama pasi au umepigwa na mchezaji unaetoka naye timu moja "

* interferring with an opponent yaani kumzuia mpinzani asiucheze mpira inamaanisha kumzuia mpinzani asiwe kwenye uwezo wa kuucheza mpira kwa kumzuia kimwili pamoja na kuzuia upeo wake wa kuuona mpira pamoja na kupambana naye moja kwa moja kuupata mpira .

*Kujipatia faida kwa kuwa kwenye sehemu ya kuotea au off side kunamaanisha kuucheza mpira  ambao....

 Umedunda na kumfikia mchezaji toka kwenye mwamba au mchezaji ambaye yuko kwenye eneo la kuotea.

  Au kuucheza mpira ambao umebadilishwa mwelekeo yaani deflection au kuparazwa au ambao umeokolewa kwa kutemwa na golikipa au mpinzani wakati mpinzani mwingine akiwa kwenye eneo la kuotea .

Mchezaji aliyeko kwenye eneo la kuotea ambaye anapokea mpira kutoka kwa mpinzani ambaye anapiga mpira kuelekea nyuma yaani back pass ambayo sio jaribio la kuokoa mpira hahesabiwi kujipatia faida yaani gaining advantage.

Sababu za mabadiliko haya.

Maneno haya yanatoa mijadala mingi kwa kuwa yamekuwa na tafsiri nyingi na yanaonekana kuwa hayana ufasaha wa kutosha . Tafsiri hizi mpya zinaendana sanjari na nyakati halisi za kimchezo yaani actual in game situations na zitatoa mkanganyiko kwa kile ambacho watu wanadhani ni mpira uliodunda au rebound , mpira wa kuparazwa au deflection  na wakati ambapo mpira umeokolewa .


Maamuzi mengine ya IFAB 

1.GoalLine Technology ( kama ilivyotolewa na FIFA)

Iliamuliwa kuwa waandaaji wa mashindano wanapaswa kuamua juu ya matumizi ya GLT kwenye mashindano husika . Kulikuwa na makubaliano ya wote kuwa vifaa au nyenzo za GLT zinapatikana kwenye uwanja basi zitumike kwa kuwa hazileti faida kwa timu yoyote.


2.Waamuzi wasaidizi wa ziada. (Kama ilivyotolewa na FIFA)

Kama ilivyopitishwa kwenye mkutano wa mwaka wa kibiashara wa FIFA uliofanyika oktoba 2012 , taarifa hii mpya ya waamuzi wasaidizi wa ziada itaongezwa kwenye toleo jipya la sheria za mchezo la mwaka 2013/2014.

Utekelezwaji 

Maamuzi ya mkutano mkuu wa mwaka wa bodi ambao ulijadili mabadiliko ya sheria za mchezo yanayabana mashirikisho na vyama wanachama kutekeleza mabadiliko haya kuanzia julai mosi 2013 ,lakini mashirikisho na vyama wanachama ambao misimu yake haijaisha mpaka kufikia julai mosi wao wanaweza kuchelewesha utekelezwaji wa sheria hizi kwenye mashindano yake mpaka mwanzo wa msimu ujao.

WANASOKA WASOMI ZAIDI KWENYE ULIMWENGU WA SOKA DUNIANI - JUAN MATA, GLEN JOHNSON KIBOKO


1 SOCRATES

Gwiji huyu wa soka wa Brazil - alikuwa daktari kabisa lakini akachagua soka na kuachana na kuvaa koti jeupe.Socrates


2. MAROUANE CHAMAKH

Flop huyu wa ARSENAL pamoja na ubutu wake uwanjani lakini darasani alikuwa hatari - Chamakh ni mhasibu. 


Marouane Chamakh

3 NEDUM ONUOHA


Kijana huyu anayekipiga kwenye timu ya QPR ni kichwa sana darasani. Onuoha aliwahi kupata a tatu kwenye masomo yake ya Hesabu, Biashara na Information Technology - Onuoah alifaulu vizuri mno kwenye masomo yake chuoni.
Nedum Onouha

4 SHAKA HISLOP

Mchezaji huyu wa zamani wa Newcastle ana degree ya mechanical engineering — na hata alikuwa anatumia muda wake wa mapumziko kufanya kazi NASA katika porject ya Space Station Freedom huko Washington. Raia huyu wa Trinidad Hislop alihusika katika project kubwa sana huko katika visiwa Caribbean.Shaka

5 JUAN MATA

Mchezaji huyu wa CHELSEA inawezekana ndio akawa mwanasoka mwenye elimu zaidi kuliko wote ndani ya kikosi cha Jose Mourinho - ana digrii mbili za Masoko na Sayansi ya Michezo.
Juan Mata

8 GLEN JOHNSON

Wanafunzi wenzie walikuwa wanamuita (HUMAN calculator) Glen Johnson anatumia masaa mawili kwa siku kwenda Chuo Kikuu Huria kuhudhuria masomo yake ya Degree ya Mahesabu. Glen Johnson


MBWANA SAMATTA AENDELEA KUWAFUNIKA MASTAA WOTE TP MAZEMBE - ULIMWENGU NAE HAYUPO NYUMA

SAMATTA remains the key man
Kwa mujibu wa takwimu zilizotlewa na klabu ya TP Mazembe. kwa kutumia vigezo vya: Kucheza mechi, Pasi zilizozaa matunda na Mabao - mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu hiyo Ally Mbwana Samatta ameongoza kwa kipindi cha takribani miezi 2, April na May.

MECHI/MUDA WALIOCHEZA
Kwa kuzingatia muda wa kucheza, hakuna aliyeweza kutimiza michezo 13 ndani ya kipindi cha miezi miwili. Mwezi May wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza walicheza mechi zote saba, wakati katika kuleta utofauti KASUSULA na SAMATTA walicheza mechi zote sita. Katika dakika walizocheza Samata tayari alikuwa anashika nafasi ya 3 nyuma ya Richard KISSI Boateng na Kasongo Kabiona.
Dakika walizocheza kwa namba: 1. KIDIABA na KASUSULA dakika 900.
3. SAMATTA 873
4. BOATENG 79
5. KABIONA 720
6. SINKALA 655
7. KIMWAKI na HICHANI 630
9. MPUTU 610
10. ASANTE 518
11. KALABA 512
12. ILONGO 475, 13. NKULUKUTA 447, 14. KABANGU 430, etc.

Mabao - Samatta anaongoza
Hakuna shabiki yoyte wa TPM anayeweza kushangazwa na mshambuliaji huyu wa kibongo kushika nafasi ya kwanza. SAMATTA amefunga mabao 6 ndani ya miezi mwili, akifuatiwa na Bokanga aliyefunga 5, Awako na Tresor Mputu wamefunga mabao 4 kila mmoja huku mshambuliaji mwingine wa kibongo Thomas Ulimwengu akifunga mabao 2.


Pasi za mabao: MPUTU anaongoza ...
Tresor MPUTU ameendelea kuwa mfalme wa pasi za mwisho ndani ya TP Mazembe. Lakini Samata hayupo mbali - anashika nafasi ya pili. 
Waliongoza: 1. MPUTU pasi 6 , 2. SAMATTA pasi 5, 
3. BOATENG 2, 6. ASANTE, BOKANGA, KABANGU, KASONDE, ADJEI, NKULUKUTA, ULIMWENGU kila mmoja alitoa pasi 1 ya goli.

Friday, June 14, 2013

MANUEL PELLEGRINI ATHIBITISHWA KUWA KOCHA MPYA WA MANCHESTER CITY - ASAINI MIAKA 3 - ANGALIA INTERVIEW YAKE YA KWANZA KABISA BAADA YA KUSAINI MKATABA NA CITY

Kocha Manuel Pellegrini ameteuliwa rasmi kuwa kocha mpya wa Manchester City leo hii akiichukua nafasi ya kocha Roberto Mancini. Pellegrini ambaye aliiwezesha Malaga kufika hatua ya nusu fainali kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya msimu uliopita amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya jiji la Manchester. ANGALIA INTERVIEW YAKE YA KWANZA KABISA BAADA YA KUTHIBITISHWA KUWA KOCHA MPYA WA MAN CITY   

KEVIN PRINCE BOATENG ATANGAZA KURUDI KUICHEZEA GHANA BAADA YA KUSTAAFU

Chama cha soka cha Ghana Kevin-Prince Boateng amekubali kurudi kuichezea Ghana kwa mara nyingine tena.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alistaafu kuichezea Ghana mnamo November 2011 akisema kwamba mwili wake hauwezi kuhimili tena soka la kimataifa.
"Kabla ya Ghana haijacheza na Sudan alimthibitishia kocha kwamba anarudi kuiichezea timu ya taifa", raisi wa GFA Kwesi Nyantekyi aliiambia South African TV. 

"Kwa bahati mbaya akapata majeruhi wakati wa mazoezi na AC Milan na hakuweza kucheza mchezo huo."
Hajaichezea Ghana tangu wakati wa michuano ya AFCON dhidi ya Congo October 2010.
Boateng ambaye amezaliwa na wazazi kighana na kijerumani aliamua kuichezea Ghana mnamo mwaka 2010 wakati wa kombe la dunia baada ya kuona kutokuwa na nafasi kwenye timu ya taifa ya Ujerumani. 
Boateng aliweza kuisadia Ghana kwenda mpaka kwenye robo fainali ya Kombe la dunia kabla ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kuichezea timu hiyo michezo tisa tu ukiwemo mchezo mmoja uliochezwa kwenye ardhi ya Ghana. 

Uamuzi huo ulipelekea mashabiki kuwa na hasira dhidi yake wakimwambia kaitumia timu ya taifa kupata umaarufu wa kimataifa kupitia kombe la dunia. 

Hatua hii ya Boateng inakuja siku kadhaa baada ya watoto wa Abeid Pele Andrew na Jordan Ayew kutangaza kurudi kuitumikia timu yao ya taifa ya Ghana.

RAMBIRAMBI MSIBA WA ABDALLAH MSAMBA

Add caption
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Pan Africans, Simba na Taifa Stars, Abdallah Msamba kilichotokea juzi usiku (Juni 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Msamba akiwa mchezaji, na baadaye kocha wa timu kadhaa alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na kufundisha ikiwemo Villa Squad, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Msamba, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na klabu ya Villa Squad na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Maziko ya mchezaji huyo yamefanyika leo (Juni 14 mwaka huu) katika makaburi ya Ndugumbi mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiwemo wachezaji wa zamani na viongozi mpira wa miguu nchini. Mungu aiweke roho ya marehemu Msamba mahali pema peponi. Amina

LUNYAMILA, MKANDAWILE, NEMES, MWALALA, NSAJIGWA, MATOLA WAHUDHURIA KOZI YA UKOCHA

 

   Mkufunzi wa TFF Rogasian Kaijage akiwapa maelekezo.
    Lunyamila akionyesha 'DEMO'


    Shadrack Nsajigwa,Selemani Matola na Mohammed Hussein 'Chinga' wakimsikiliza kwa makini mkufunzi Rogasian Kaijage.
   Meneja wa Azam FC Jemedari Said pia naye yupo.


 Seleman Matola mwenye jezi nyekundu,katikati ni kiungo wa zamani wa Yanga Ngade Chabanga pamoja Steven Nyenge wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo..
    Ibrahim Masoud 'Maestro' pia yupo...




Makipa wa zamani Steven Nemes,Moses Mkandawile,Shadrack Nsajigwa na Benard Mwalala.

 Mshambuliaji wa zamani wa Simba Bakary Idd,Mimi mwenyewe,Matola na Mwalala.
Majina ya wanaohudhuria kozi ya ngazi ya kati (intermediate) inayofundishwa na mkufunzi Rogasian Kaijage kwenye viwanja vya Harbours Club, Kurasini.
1.      Abdallah K. Mohamed
2.      Abdulmalick Nemes
3.      Adam Juma
4.      Akida Said
5.      Ally Yusuph
6.      Athuman Kipao
7.      Bakari Idd
8.      Barton Msengi
9.      Bernard Mwalala
10.   Chaurembo Shomari
11.   Chiwanga A. Chiwanga
12.   Daniel Stephen
13.   David Wiliam
14.   Edgar Katembo
15.   Edibily Lunyamila
16.   Emanuel Gabriel
17.   Fredrick Mwasombola
18.   Grayson Swai
19.   Hassan Msonzo
20.   Herry Allen
21.   Herry Kaiza
22.   Ibrahim Masoud
23.   Iddy Abubakari
24.   James Changarawe
25.   Jemaderi Said
26.   Jeremia Dickson
27.   Kassango Pascal
28.   Medard Rwezaura
29.   Mohamed Hussein
30.   Moses Mkandawile
31.   Mtweve Abel
32.   Muhibu Kanu
33.   Mwanamtwa Kihwelo
34.   Nevelin Kanza
35.   Ngade Chabanga
36.   Omari Ally
37.   Omari Kafufi
38.   Omari Mbarouk
39.   Omary Mohamed
40.   Omega Ruzwiro
41.   Rahel Pallangyo
42.   Rajab Mohamed
43.   Ramadhan Juma
44.   Renatus Bernard
45.   Richard Mbuya
46.   Samwel Moja
47.   Seleman Matola
48.   Shadrack Nsajigwa
49.   Shaffih Dauda
50.   Shiza Mapunda
51.   Steve Nyenge
52.   Wambura Gaspar
53.   Zubery Katwila
54.   Zulkifri Iddi
55.   Zulu Tosiri

Kwa hisani ya : pallangyor.blogspot.com

HUU NDIYO UZALENDO WA KWELI!

MKUTANO MKUU WA TFF SASA KUFANYIKA MWEZI UJAO KUJADILI MAREKEBISHO YA KATIBA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametoa notisi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho utakaofanyika Julai 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam ukiwa na ajenda moja ya marekebisho ya Katiba.

Notisi hiyo imetolewa juzi (Juni 12 mwaka huu). Rais ameitisha Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(1) ya Katiba ya TFF baada ya kupata maagizo kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa barua yake ya Aprili 29 mwaka huu.

Ajenda rasmi na taarifa nyingine zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(4) ya Katiba ya TFF. Wanachama wa TFF ambao ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu wanatakiwa kutuma majina ya wajumbe halali.

TFF inapenda kuwakumbusha wanachama wake kutuma majina ya wajumbe halali ili kufanikisha maandalizi ya Mkutano huo. Ni vizuri kuhakikisha kuwa jina linalotumwa ni la mjumbe halali wa Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya TFF.

MSIBA WA ABDALLAH MSAMBA AZIKWA LEO NDUGUMBI MAGOMENI


Nipo na mshkaji wangu kitambo Athumani Kipao.
Peter Manyika na Mfaume Athumani wote walikuwa magolikipa wa Yanga.

Mwenye tshirt nyekundu na kofia ni mchazaji wa zamani Kangilila  Maufi pamoja na mdau Evarist Hagira
Anayeongea na simu ni Mshambuliaji wa zamani wa sigara na Simba Gebo Peter

Mwili wa Marehemu Abdallah Msamba ukiwa umebebwa kuelekea makaburini tayari kwa kuzikwa

Umati ukimsindikiza Msamba ambaye alikuwa mwanasoka huyo wa zamani wa klabu ya Sigara na Simba katika nyumba yake ya Milele.