Search This Blog

Friday, June 14, 2013

KEVIN PRINCE BOATENG ATANGAZA KURUDI KUICHEZEA GHANA BAADA YA KUSTAAFU

Chama cha soka cha Ghana Kevin-Prince Boateng amekubali kurudi kuichezea Ghana kwa mara nyingine tena.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alistaafu kuichezea Ghana mnamo November 2011 akisema kwamba mwili wake hauwezi kuhimili tena soka la kimataifa.
"Kabla ya Ghana haijacheza na Sudan alimthibitishia kocha kwamba anarudi kuiichezea timu ya taifa", raisi wa GFA Kwesi Nyantekyi aliiambia South African TV. 

"Kwa bahati mbaya akapata majeruhi wakati wa mazoezi na AC Milan na hakuweza kucheza mchezo huo."
Hajaichezea Ghana tangu wakati wa michuano ya AFCON dhidi ya Congo October 2010.
Boateng ambaye amezaliwa na wazazi kighana na kijerumani aliamua kuichezea Ghana mnamo mwaka 2010 wakati wa kombe la dunia baada ya kuona kutokuwa na nafasi kwenye timu ya taifa ya Ujerumani. 
Boateng aliweza kuisadia Ghana kwenda mpaka kwenye robo fainali ya Kombe la dunia kabla ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kuichezea timu hiyo michezo tisa tu ukiwemo mchezo mmoja uliochezwa kwenye ardhi ya Ghana. 

Uamuzi huo ulipelekea mashabiki kuwa na hasira dhidi yake wakimwambia kaitumia timu ya taifa kupata umaarufu wa kimataifa kupitia kombe la dunia. 

Hatua hii ya Boateng inakuja siku kadhaa baada ya watoto wa Abeid Pele Andrew na Jordan Ayew kutangaza kurudi kuitumikia timu yao ya taifa ya Ghana.

No comments:

Post a Comment