Search This Blog

Friday, March 9, 2012

HAYA NI MAONI YA BAADHI YA WADAU KUHUSIANA NA SAKATA LA UBINGWA WA CDA WA LIGI YA MKOA WA DODOMA.

HABARI DAUDA
mimi ni mdau wa soka kutoka jijini dodoma nina malalamiko kuhusu ligi ya mkoa. tumefatilia toka mwanzo wa ligi mpaka mwisho na kwa matokeo ya ligi hiyo tumeona kuwa mshindi ni maskan fc na cha ajabu ushindi akapewa cda timu ambayo ilithubutu hadi kuchezesha mpaka wachezaji wa polisi undertwety na chama chetu cha mpira cha dorefa kimenyamaza kinasubili watu wakate rufaa. Sisi tunashidwa kuelewa hiki ni chama cha mpira au cha rufaa. Mimi kama mdau wa soka mjini dodoma naomba sauti zetu zifikishwe
 
hi mwana sport dauda
mimi naitwa omary miraj shabiki wa timu ya CDA DODOMA nasikitishwa na style ya ligi ya mkoa wa dodoma kisheria mchezaji haruhusiwi kucheza ligi mbili tunashangazwa uku dodoma wachezaji hao wanacheza ambao ni rajab mgalula na tenne huku wanachezea pia ligi ya mkoa na uongozi wa dorefa unaona unajua lakini una linyamazia timu zikikata rufaa zinaambiwa rufaa imetupiliwa mbali au wa natengeneza mazingira ya kupata kipato kupitia rufaa kwanza kuna ulazima gani wa kukata rufaa wakati uongozi unaona na unanyamaza au soka la mkoa ndo limetawaliwa na rushwa abubakari tambua rushwa ni adui wa haki wapeni tu ubingwa wao maskani
Hero Sangatiti
Kiukweli ubingwa wa CDA ni wa magumashi.
1-kiwango cha mpira hawana kiwanja walicho kuwa wana fanyia mazoezi "CENTRAL HIGH SCHOOL" nami ndipo ninapo fanyia mazoezi kiukwel hawana lolote so kwenye hiyo michuano kiukweli walibebwa mechi ...
nyingi.

2-Walibebwa coz chama cha soka mkoani Dodoma wana mahusiano mazuri na viongozi wa CDA so haikuwa tabu kwa watu hao kupendeleana ktk maswala ya mpira na ndo maana matokeo mengi ya CDA yalikuwa ya magumashi.

3-hata kama wame twaa ubingwa lakin kwa uchezaji wao hakuna kitu kabisaaaaa.
Mambo ya Dodoma nakumbuka kuna kiongozi mmoja wa soka alisema kua, ni bora kuzipandisha timu zenye majina kuliko timu zisizojulikana nakumbuka hiyo kauli na gazeti la Tanzania Daima liliandika hilo na kiongozi huyo huyo pia nilimshudia kituo kimoja cha redio akihojiwa akisema hivyo hivyo. By Andrew Chale
 
Kaka Dorefa hakuna viongozi ila walanguzi wa mechi me kwa muda wote ninakuaga Dom nikishuhudia mechi yanayosemwa ni kweli mtupu, kiukweli kama mpira ungekuwa unachezeshwa kwa haki basi Area A sportivo wangeshakuwa mabingwa siku nyingi na w...angeshapanda daraja maana jamaa wanawachezaji wazuri miaka yote afu wana udhamini mzuri so huwa wanabaniwa ili wasifikie malengo kwa kuwa wao sio chaguo la Dorefa! Iliniuma,inaniuma na itaendelea kuniuma mpaka Dorefa itakapobadilika coz inatunyima raha ya soka wana Dodoma! From Udsm
 

Kweli pesa uchawi wa kizungu..

Hili ndo sakata la ubingwa wa CDA huko Mkoani Dodoma !

Mwanzoni kabisa wakati ligi inaanza kulizuka tetesi kwenye wilaya, kwamba mwaka huu timu ya CDA, itapandishwa daraja.

Baada ya tetesi hizo, watu wakatulia wakisubiri kuona ukweli wa tetesi hizo.

Mara ligi ilipoanza , hapa sasa ndio ukweli ulipojidhihrisha. Ligi ikachezwa kwa makundi. Ikaja hatua ya tisa bora na wakazigawa timu katika makundi matatu.

Hap kilichotakiwa ni kila kundi inapita timu moja  na kuunda tatu bora, kisha bingwa wa wilaya.

Katika kundi la timu ya CDA, kulikuwa na timu nyingine ( GANAZ FC, na ……….)

Katika mechi yao ya mwisho dhidi ya GANAZ FC ya Jeshi, CDA, walishinda 2-1 huku CDA, wakiwa wamewatumia wachezaji watatu ambao walikuwa wachezaji wa timu za Under 20 ya polisi Tanzania, na golikipa wa Yanga ambao walicheza mashindano ya UHAI.

Tatizo likaanzia hapa…..



GANAZ ikakata rufaa chama cha wilaya kupinga wachezaji hao huku ikiwa na vielelezo vyote.
( mmoja kati ya wachezaji hao ni Yule aliyepata nafasi ya kwenda kwenye academy Senegal)
Matokeo ya rufaa hiyo yalikwenda vizuri, na Ganaz wakaonekana wako sahihi, wakapewa ushindi na chama cha wilaya wakaambiwa wajiandae na 3 bora na punde kidogo ratiba ikatoka ikiijumuisha ganaz, Polisi na AREA A, kugombania ubingwa wa Wilaya.

Mechi ya kwanza ikachezwa ya kwanza siku ya Juma tano POLISI  na AREA A, na ijumaa ikachezwa mechi kati ya GANAZ na AREA A.
Kwa mshangao wa wengi alhamis kukawa na kikao cha chama cha mkoa DOREFA, wakaipoka tena ushindi GANAZ, na ikaiagiza CDA, ijiandae kesho yake kwa mechi.
Asubuhi Ganaz fc inapokea barua kutaarifiwa maamuzi ya rufaa kwamba CDA walikata rufaa chama cha mkoa hivyo chama kimeona maamuzi yaliyoamriwa na DOREFA zile kamati za kuamua rufaa zilikaa kwa pamoja kwamba kamati ya rufaa na ya nidham na ilitakiwa kila moja ikae kivyake na itoe maamuzi.
Tukahoji inakuaje sasa isikilizwe upya wakasema haiwezekani tena hivyo kama tunataka tukate rufaa TFF taifa kumbuka saa 4 hiyo tunaambiwa hivyo na ilikuwa ijumaa na jioni tuna mechi.
Uongozi wa GANAZ ukaona isiwe tabu kwa kuwa mazingira yalikuwa yapo wazi na wao ndo wameshika mpini.

Kilichotokea sasa wakacheza CDA ile hatua ya 3 bora na DRFA wakasimamia mpaka wakapata ule ubingwa wa wilaya.
Wakati huo huo zile timu 3 zinatakiwa zisonge mbele kwenye hatua ya mkoa yani kutafuta bingwa wa mkoa kwa mujibu wa sheria ambapo ni timu 3.
Ganaz ikahoji gharama za kuiandaa timu kwa kipindi kile walipwe cha ajabu wakaambiwa watulie watapatiwa nafasi na wao ziwe timu 4 kutoka wilaya ya dodoma mjini hapo inaonyesha zahiri katiba imevunjwa maana miaka yote ni timu 3 iweje ziwe 4?
Sababu zikatolewa na kweli kwakuwa nafasi ilikuwa inahitajika ganaz ikatulia.
zikagawanywa timu kituo cha kongwa na dodoma mjini, GANAZ ikapelekwa kongwa na CDA ikabakishwa mjini na timu zingine za wilayani.
kituo cha kongwa kikaenda vizuri bingwa halali akapatikana GANAZ kimbembe kikawa town...
kila timu ya wilayani inapocheza na CDA kesho yake inatangaza kujitoa inarudi kwao kwa kuwa waliona wanapoteza muda bure na garama za bura, zikajitoa karibu timu 4 matokeo yake kati ya timu 8 ikapita CDA na point 4, polisi jamii na magereza mpwapwa wakapita na point moja moja wote maajabu haya.
Ikaja hatua ya 6 bora sasa 3 kutoka kongwa na 3 kituo cha town ambazo zilikuwa ni cda,polisi jamii,magereza mpwapwa,ganaz,magereza isanga na maskani.
Mechi zikaanza gemu ya kwanza CDA ikatoa droo ya 0-0,na maskani gemu ya 2 ikaifunga magereza isanga goli 7-0 yani style ikawa ni ile ile saidia ishinde, kesho yake magereza isanga ikatangaza kujito kwa kutiridhishwa na mwenendo wa ligi hivo cda ikafutiwa point zote 3 mechi ya 3 ikaifunga polisi jamii 2-0 ikawa na point 4 mechi ya 4 ikacheza na magereza mpwapwa ikatoa droo ya 1-1 na hapo ulikuwa sio mpira zaidi ya mbereko ya kufa mtu maana dakika za mwisho cda ilifungwa goli la wazi kabisa likakataliwa hivo wakawa na point 5,maskani point 5,polisi jamii point 4,ganaz 3.hapo sasa ndo pakawa patamu....
ila kabla ya yote ile gemu ya cda na polisi jamii cda walishinda 2-0 polisi wakawakatia tena cda rufaa kama ya ganaz kupinga kuwatumia wachezaji wawili na kwa kuwa hii ni polisi ndogo vile vigezo viliboreshwa zaidi kwa kuwa walikuwa wachezaji wao cha ajabu ile rufaa ikaanza kupigwa danadana ilipelekwa kwa kamati ya rufaa wakaambiwa wapeleke kwenye ya kamati ya nidham wakasema basi tunahitaji majibu haraka kabla ya gemu inayofuata.
viongozi wakaifumbia macho kana kwamba hakuna kitu na ligi ikawa inaendelea kama kawaida...!! basi mechi ya mwisho cda na ganaz halafu kesho yake polisi jamii na maskani...kwa zengwe lile lileganaz ikafungwa goli 2-0 ingawa magoli yalikuwa halali ila mazingira ya mechi kuhusu maamuzi hayakuridhisha kabisa hapo hapo wakajitangaza mabingwa kwa kuwa na point 8 na magoli ma4 ya kufunga wakati kuna mechi nyingine ya mwisho




kesho yake.... kwa mtaji huo maskani peke yake ndo akawa anauwezo wa kuwa bingwa kwakuwa na point 5 dhidi ya polisi j ina 4, na kwakuwa cda iliitesa kila timu kwa fitina zake

mechi ikachezwa na hapo maskani ikawa inahitaji magoli ma 4 ili imzidi cda kwa goli 1 ndo iwe bingwa ha haaa hadi dk ya 6 zikawa zimeshapatikana hizo zinazohitajika mpira ukawa unachezwa sasa hadi halftime ikawa 4-0 na hadi mwisho maskani ikaifunga polisi jamii 5-0 basi kimahesabu ikawa maskani ndio bingwa lakini hakuna chombo chochote cha habari kilichotangaza na hata DOREFAwakaondoka uwanjani...!! ila mji mzima ukawa unajua maskani ndio bingwa....

likaanza zengwe lingine wakati mechi inaendelea ile na cda wakaona hamna namna wakaanza kusema wanakata rufaa kwa kuwa hiyo maskani ilinunua jina wilayani na sheria inasema lazima kuwe na wachezaji 10 kutoka hiyo timu kitu ambacho maskani walikuwa hawana...lakini tokea inashiriki kituo cha kongwa hiyo maskani ilikuwa inatumia wachezaji wake ambao wameidhinishwa na hao hao dorefa[halafu sorry nilikuwa natumia DOREFA sasa iweje leo mwisho wa siku wajifanye kuwakatia rufaa....zengwe hilo..!!.....

Walikuwa na rufaa hao hao cda dhidi na mechi yao na magereza mpwapwa ile waliotoka 1-1 kwamba golikipa namba 2 wa magereza jezi yake haikwenda kwenye pre match hivo ilitumika kimakosa uwanjani wakawa wanadai wapewe ushindi...zengwe hilo sheria ya wapi hiyo...na hapo makosa si yanakuwa ya waamuzi..?....

basi ndo wakatoka na hiyo mpya ya kwamba hiyo gemu ya maskani na polisi eti matokeo yalipangwa wakakata rufaa na siku wanapeleka hiyo rufaa naona huku wanashangilia kana kwamba matokeo ya hiyo rufaa wanayajua... maana hata hiyo gemu ya maskani na polisi walitaka iwe droo au polisi ashinde matokeo yake waamuzi ndo wakawa mabeki wa polisi lakini pia ikashindikana....

na hao wanaosema wasimamizimwa mechi kwa nini wasimamie gemu moja ya mwisho kwa nini wasisimamie gemu zote kama wapo makini...? hivo kwa kauli moja na kwa mujibu wa timu zote shiriki wanapinga cda kupewa ubingwa sio halali hata kidogo na ndo wanaofanya hata polisi tanzania haifanyi vizuri ligi kuu gemu za polisi hazipewi promo yoyote na chama,wala hawawapi ushirikiano wowote kwakuwa wanaona ile ni timu ya taasisi hivyo wanataka ishuke waipandishe cda ili wapate maslahi ndio maana hata gemu za polisi tanzania ligi kuu sio ajabu ukasikia mapato sh 25,000/= timu ikapata 1250 ni kitu cha kawaida hapa...!!!!
Mimi ni mchezaji wa GANAZ na nimejionea ukiritimba wa hii michuano na mwaka jana ndo tuliofanya tukawanyima mji mpwapwa ubingwa kwa style hii hii kutaka fulani apande kwanini? kwakuwa yeye ndo kalipa ada ya ushiriki peke yake basi tukatoa droo na hao mji na gemu ya mwisho kwakuwa hatukuwa na nafasi tena tukawaachia majengo wakatufunga 2-0 wakawa mabigwa mji akazidiwa point akaula wa chuya..!!
Nahiyo rufaa cda waliyokatiwa na ganaz kuhusu hao wachezaji kwa style hiyo hiyo mji mpwapwa nao kuna baadhi ya wachezaji waliwatumia huko mpwapwa wa u20 ya polisi tanzania wakakatiwa rufaa wakapokonywa point 9 matokeo yake hawaakwenda kokote sasa kwa nini kwa cda iwe tofauti? na ni mwaka huu huu?
Ni hayo tu bro shaffih na kama una la kuniuliza 0717982800 sina pa kutolea dukuduku langu zaidi ya sports xtra kwa kuwa ni member na nyie mnasaidia sana sio siri kufichua na angalau hata kukuza soka letu ambalo linaporomoka balaa kwa uhuni wa watu wachache kama hawa maana wasingepanga fulani awe bingwa mbona mpira ungechezwa kwa raha tu
ni hayo tu bro usiku mwema....ggmu

LIGI KUU YA SOKA NCHINI CHINA INATARAJIWA KUANZA HAPO KESHO

LIGI KUU YA SOKA NCHINI CHINA INATARAJIWA KUANZA HAPO KESHO HUKU KILA MMOJA AKIITAZAMA KWA UMAKINI TIMU YA SHANGHAI SHENGHUA.

MACHO NA MASIKIO YA WENGI YATAELEKEZWA KWENYE TIMU HIYO AMBAYO ITAKUWA INAMCHEZESHA KWA MARA YA KWANZA MSHAMBULIAJI WAKE MPYA MFARANSA NICOLAS ANELKA AMBAYE SHENHUA IMEMSAJILI TOKA KLABU YA CHELSEA MWEZI JANUARI .

WACHAMBUZI WA MASUALA YA SOKA WANAGONJA KUONA KAMA UJIO WA ANELKA UTALETA MSISIMKO KWENYE LIGI YA CHINA KAMA ILIVYOKUWA NCHINI MAREKANI AMBAKO UJIO WA DAVID BECKHAM ULICHANGIZA KULETA MSISIMKO MKUBWA KWENYE TIMU YA LOS ANGELES GALAXY NA LIGI YA MAREKANI KWA UJUMLA . SHANGHAI SHENGHUA KWA SIKU ZA HIVI KARIBUNI IMEKUWA IKIFANYA USAJILI WA KUIMARISHA KIKOSI CHAKE AMBAPO IMEWASAJILI WACHEZAJI KAMA MUARGENTINA DARIO CONCA NA WASHAMBULIAJI TOKA BRAZIL CLEO NA MURIQUI AMBAO WANATARAJIWA KUUNGANA NA ANELKA

RORY MCILROY ALIJIKUTA AKIANZA VIBAYA

HUKU AKIWA AMEISHIKILIA NAFASI YA KWANZA KWENYE VIWANGO VYA MCHEZO WA GOLF DUNIANI KWA MUDA WA SIKU TANO , RORY MCILROY ALIJIKUTA AKIANZA VIBAYA KWENYE MICHUANO YA WGC –CADILLAC CHAMPIONSHIPS HUKO DORAL , FLORIDA NCHINI MAREKANI. MCILROY ALIPIGA MIPIRA MINNE YA BOGEYS HUKU AKIPIGA MINGINE YA BIRDIES KABLA YA KUMALIZA RAUNDI YA KWANZA NA MPIRA WA YADI 73 KATIKA UWANJA ULIOKUWA NA UPEPO MKALI . UCHEZAJI WA MCILROY ULIDHIHIRISHA KUWA PRESHA YA KUWA NAMBA MOJA KWENYE VIWANGO VYA GOLF DUNIANI IMEKUWA KUBWA HALI INAYOMTATIZA KIUCHEZAJI.KATIKA MICHUANO HIYO MCHEZAJI TOPKA AUSTRALIA ADAM SCOTT NA MMAREKANI JASON DUFNNER WALIMALIZA KATIKA NAFASI YA KWANZA HUKU WAINGEREZA LEE WESTWOOD NA LUKE DONALD WLAIOPANGWA KUNDI MOJA NA RORY WAKISHIKA NAFASI ZA NNE NA TANO .

RAHUL DRAVID AMETANGAZA KUSTAAFU

.KWENYE KRIKETI NAHODHA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA INDIA RAHUL DRAVID AMETANGAZA KUSTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA INDIA KATIKA MICHEZO YA KIMATAIFA.

DRAVID AMESEMA KUWA AMEFIKIA UAMUZI HUO ILI KUWAPA NAFASI WACHEZAJI WAPYA WEYE DAMU CHANGA AMBAO KWA KIASI KIKUBWA NDIO WENYE MUSTAKABALI WA MCHEZO WA KRIKETI YA INDIA.

DRAVID MWENYE UMRI WA MIAKA 39 AMEICHEZEA INDIA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 16 AMBAPO AMEFANIKIWA KUWEKA HISTORIA KAMA MCHEZAJI ANAYESHIKA NAFASI YA PILI KWENYE ORODHA YA WACHEZAJI WALIOFUNGA MBIO NYINGI KWENYE MCHEZO HUO AMBAPO KWA UPANDE WAKE AMEFUNGA MBIO ELFU KUMI NA TATU MIA MBILI THEMANINI NA NANE KATIKA MICHEZO MIA SITINI NA NNE

Manchester United 2-3 Athletic Bilbao: United yashindwa kuhimili presha na ukabaji wa Athletic Bilbao.

Timu zilivyoanza.
Athletic walianza mchezo kwa kasi kubwa na waliendelea na mchezo huo mpaka mwisho hali iliyowapa matokeo ya kuongoza ambayo wanarudi nayo mpaka Bilbao.
Sir Alex Fergusson aliamua kuwaacha bench Rio Ferdinand , Paul Scholes na Michael Carrick , Danny Welbeck huku akiwaanzisha Javier Hernandez na Wayne Rooney mbele na Chris Smalling na Johny Evans wakicheza kama mabeki wa kati.
Kwa upande wa Athletic , Marcelo Bielsa aliwachezesha wachezaji wake wale wale wa kikosi cha kwanza cha siku zote isipokuwa mchezaji Fernando Amorabieta ambaye alikuwa ana adhabu na nafasi yake ikachukuliwa na Mikel San Jose alianza kwenye nafasi yake . Athletic walikuwa timu bora tangu mchezo ulivyoanza wakishambulia kwa kasi huku wakimiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi.

Mifumo.
Bielsa kama tunavyomfahamu , anapenda kuchezesha timu ambayo nyuma anabakia mtu mmoja.Kama united wangechezesha mfumo wa 4-4-2 ya moja kwa moja basi Bielsa naye angechezesha wachezaji watatu kwenye defence yake badala ya kuchezesha mtu mmoja , lakini United walicheza na mfumo wa 4-4-1-1 na Bielsa alimpa Ander Iturraspe maelekezo ya kumkaba Wayne Rooney huku mtu mmoja akibakia kama mlinzi wa ziada hasa pale ilipotokea hali ya 1 v 1 dhidi ya Javier Hernandez.
Mfumo wa United ulikuwa mwepesi kwa Athletico kuukabili kwa kuwa walimtumia Ashley Young kulia , Ji sung park kushoto , wote hawa ni wachezaji wanaopenda kucheza kushoto lakini kwa kuwa jinsi Ashley Young anavyocheza inategemea kudrible mpira athari inayotokana na uwezo inategemea sana na upande wa uwanja anaocheza hivyo ingekuwa bora kama wangebadilisha winga park akaenda kulia na young akaenda kushoto. Park hata hivyo ni mzuri kwenye ulinzi na beki wa Athletic Andoni Iraola ni mzuri sana ilibidi Park acheze upande wake


Ukabaji
Athletic walikuwa wepesi sana katika mchezo wao huku wakiwa wanabadilishana nafasi mara kwa mara na walipokuwa hawana mpira walikuwa wanafanya pressing ya hali ya juu tangu upande wa mbele walipokuwa washambuliaji. Fernando Llorente alielekezwa kuwakaba mabeki wa kati huku wachezaji wa Athletic wa pembeni wakimsaidia Llorente na kufanya iwe hali ya  2v2 na badala ya kuwaelekea mabeki wa pembeni wa United ambao hawakuweza kupanda mbele bila bugudha ya wachezaji hawa.
     Kama ilivyokuwa kwenye mchezo wao dhidi ya Barcelona , Atheltic walikuwa wanawakaba wapinzani wao man to man kila kona ya uwanja  nah ii ilimaanisha kuwa Andre Herera na Oscar De marcos walipanda mbele kupindisha mianya ya kina Phil Jones na Ryan Giggs  huku wakicheza mbele ya Iturraspe. Mara nyingi kulikuwa na shimo kubwa mbele ya Iturraspe na japo United hawakuwa na mtu ambaye angeweza kushambulia eneo hili , walipaswa kuwa na movement kwenye wingi zote mbili toka kwa Young na Park , wangeweza kukabwa lakini hii ingemaanisha kuwa wakabaji wao wangeacha nafasi huko wanakotoka na hatari ingeendelea kuwepo.
Mfumo wa ukabaji wa Athletico.Athletic Bilbao hawakuwapa United muda wa kupumua . Llorente alikuwa akikabana na watu wawili ili kubakiza mtu wa ziada mwisho wa uwanja , lakini hata hivyo mawinga waliwakaba mabeki wa pembeni , viungo wa kati walikuwa wakiwakaba viungo wa kati wa United na mabeki wa pembeni walikuwa wakiwakaba mawinga .
Upande wa nyuma mabeki walipokezana kumkaba Javier Hernandez japo Javi Martinez alifanya hivi kuliko wenzie na mshambuliaji huyu toka Mexico alipata tabu na watu waliokuwa wakimganda  na beki aliyebakia alikuwa akicheza kama Libero.
Mashambuzli ya Athletic
Kitu ambacho Athletic walikifanya kwa ufasaha ni pale walipokuwa na mpira kwenye mashambulizi. Walikuwa wakiuhamisha mpira toka kwenye eneo moja hadi lingine kwa kasi kubwa huku wakicheza kwa uvumilivu wa hali ya juu pale waliponya’nganywa. Ufanisi kwenye mchezo wao ulikuja pale ambapo walipokuwa wanabadilisha kasi yao wakati walipokaribia eneo la hatari .
Mabeki wa pembeni walikuwa muhimu sana kwenye mchezo wa Athletic kwa kuwa walikuwa wakisambaza mpira kwa kutanua uwanja huku wakipanda na kushuka. Mara nyingi walikuwa wakipanda mbele sana karibu na goli la United na kuwa sehemu ya ushambuliaji na hakuna yoyote kati ya Park na Young aliyetaka kuwafuata na kuwakaba . Kwenye goli la kwanza la Athletico Iraola na Aurtenexte waliingia kwenye box la United na waliwazidi idadi wachezaji wa United na kumtengenezea nafasi Llorente.
Pasi
Jinsi pasi za Athletic zilivyokuwa zinapigwa hazikuwa na ufanisi sana lakini zilikuwa na malengo hasa ya kushambulia kwani ni kama wachezaji wa Athletic walitambua kuwa endapo watapoteza mipira wangewahi kuupata tena.
Kulikuwa na kitu cha kufurahisha kuhusu mipira mirefu . Bielsa aliwaonya Athletic kutocheza mipira mirefu iliyomuelekea Llorente tangu mwanzo wa msimu lakini bado wachezaji wa Athletic waliendelea kucheza mipira mirefu ya moja kwa moja iliyoelekezwa kwa Llorente huku mawinga wakihangaika kuwapita mabeki kupiga krosi .
Llorente alifanya kazi nzuri ya kukaa na mipira palie alipoipata kumngoja Llorente na viungo wa kati waingie eneo la hatari na kungoja krosi. Mabeki wa United kina Evans na Smalling bado hawajajenga ufanisi wa kucheza dhidi ya washambuliaji wenye maumbo makubwa .
Kosa walilofanya United ni kusimama eneo la mbele sana la uwanja mbali na lango lao wenyewe. Athletic waliwaelekeza washambuliaji wao kukaba lakini Rooney kwa upande wake hakuwa anafanya kitu alipokuwa hana mpira akimuacha Ituraspe adictate tempo ya mchezo na kuelekeza mipira pembeni mwa uwanja . Alielekezwa kufanya kazi kubwa kwenye kipindi cha pili wakati United wanafanya mabadiliko kwenye eneo la kiungo na kujaribu kuongeza nguvu na movement ya mpira .
Phil jones na Ryan Giggs walipata tabu sana , Jones hakuwa comfortable alipokuwa akipata mpira wakati mpinzani akiwa karibu yake . Giggs alikosa uwezo wa kukimbia maeneo mbalimbali ya uwanja na alipata tabu pale alipokabwa . Michael Carrick na Anderson waliingia kwenye eneo hilo na japo Carrick alifanya vizuri na kutengemaza midfield ya United .
     Mwisho.
United walijua  cha kutegemea toka kwa Athletic , lakini hawakujiandaa kwa aina ya mchezo wa kukaba toka kwa Athletic . Kiungo kilikosa movement na ufanisi pale wakati United ilipomiliki mpira . Hakukuwa na rotation ya nafasi na movement kwa ujumla haikuwa nzuri toka kwa United. Hernandez kwa upande wake hakuwa mzuri na alipoteza nafasi nyingi sana .
Huu pengine unaweza kuwa mchezo bora kwa Athletic kuliko yote waliyocheza msimu huu nah ii inatokana na mawazo ya kocha wao Marcelo Bielsa .

TALIB HILAL ATAKA KURUDI SIMBA KUENDELEZA HISTORIA

Beki wa zamani wa Simba SC, Talib Hilal amesema kwamba yupo tayari kurudi kuifundisha Simba kwa ajili ya mechi za Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika, dhidi ya  ES Setif ya Algeria. Akizungumza na bongostaz mchana huu kutoka Oman, beki huyo mrefu ambaye alimalizia soka yake Oman, alisema kwamba Simba wakimuita atakuja kupiga kazi kumsaidia Mseriba Milovan Curkovic aweke historia Afrika.
Talib alierejea kutoka Oman na kujiunga na benchi la Ufundi la Simba mwaka 2003 kuinoa timu kwa ajili ya michezo ya Raundi ya Tatu ya Ligi ya Mabingwa, dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Zamalek ya Misiri.
Talib alikwenda kuiweka Simba kambini Oman kwa wiki moja ambako ilifunfishwa mbinu za kucheza na Waarabu.
Ikiwa inajivunia ushindi wa awali nyumbani 1-0 kwa bao pekee la Emmanuel Gabriel, Simba ilikwenda ‘kukomaa’ na kufungwa moja tu baaada ya dakika 120, hivyo mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti.
Juma Kaseja alicheza penalti moja ya Waarabu kabla ya Christopher Alex Massawe kwenda kukwamisha nyavuni penalti ya mwisho na kuivusha Simba kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza nay a mwisho katika historia ya klabu hiyo.
Katika benchi la ufundi, Simba ilikuwa chini ya Kocha Mkuu James Aggrey Siang’a kipa wa zamani wa kimataifa wa Kenya, aliyekuwa akisaidiwa na Jamhuri Mussa Kihwelo, beki mwingine wa zamani wa Simba SC.
Mwaka 1993 ikifika Fainali ya Kombe la CAF, zamani likijulikana kama Kombe la Abiola kwa sababu lililotolewa na Chifu Mashood Abiola wa Nigeria, Simba iliitoa Al Harrach ya Algeria katika Nusu Fainali, ikifungwa 2-0 Algiers na kushinda 3-0 Dar es Salaam.  
Simba imesonga mbele Kombe la Shirikisho baada ya kuitoa Kiyovu Sport ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, wakianza na sare ya 1-1 Kigali kabla ya kushinda 2-1 Dar es Salaam na sasa itamenyana na 
ES Etif kati ya Machi 23 na 25 mwaka huu mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye ugenini. 

Je, Talib atapewa nafasi arudie maajabu yake ya 2003? Alhaj Ismail Aden Rage na Kamati yake ya Utendaji ya Simba, watatoa jibu.


Source:  bongostaz.blogspot.com/

YANGA NA AZAM NANI MBABE WIKIENDI HII?

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii kwa mechi tatu zitakazokutanisha timu sita kwenye viwanja tofauti.
 
Yanga itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa kesho (Machi 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Machi 11 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Simba na Toto Africans ya Mwanza itakayochezwa kwenye uwanja huo huo.
 
Viingilio katika mechi hizo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 15,000.
 
Mechi nyingine itakayochezwa Machi 11 mwaka itakuwa kati ya Polisi Dodoma na Kagera Sugar. Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 
Jumatano ya Machi 14 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili. Simba watakuwa wageni wa Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati Yanga watakuwa wenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ubingwa wa CDA Mkoani Dodoma, mkasa upo hivi................

Na Mdau Fredy Pastore kutoka Dodoma.

MWANZONI KABISA LIGI WAKATI INAANZA YA WILAYA ZIKAANZA TETESI KWAMBA MWAKA HUU WAMEPANIA KUIPANDISHA CDA,TUKAPIGA MOYO KONDE ILA ILIPOANZA NDO TUKAJUA WAPO SIRIOUS.

LIGI IKACHEZWA MAKUNDI IKAJA HATUA YA 9 BORA WAKAGAWA MAKUNDI MA3 AMBAPO KILA KUNDI INAPITA TIMU MOJA NA KUUNDA 3 BORA THEN BINGWA WA WILAYA.
KATIKA KUNDI LA CDA KULIKUWA NA TIMU ZINGINE KAMA GANAZ FC NA ....! KATIKA HATUA HIYO MECHI YAO YA MWISHO DHIDI YA GANAS YA JESHI HII,NA CDA WALISHINDA 2-1 ILA CDA WAKAWATUMIA BAADHI YA WACHEZAJI WA3 AMBAO WALICHUKULIWA KUTOKA TIMU ZA UNDER 20 ZA POLISI TANZANIA NA YANGA GOLIKIPA,AMBAO WALICHEZA YALE MASHINDANO YA UHAI CUP.MKASA UKAANZIA HAPO.
GANAZ IKAKATA RUFAA CHAMA CHA WILAYA KUPINGA HAO WACHEZAJI IKIWA NA VIELELEZO VYOTE (NA MMOJA WA HAO WACHEZAJI WALIOKATIWA RUFAA NDO YULE ALIYEPATA NAFASI YA KWENDA KWENYE ACADEMY SENEGAL)
MATOKEO YA RUFAA ILE IKATOKA VIZURI NA GANAZ WAKAONEKANA WAPO SAHIHI WAKAPEWA USHINDI NA CHAMA CHA WILAYA WAKAAMBIWA WAJIANDAE NA 3 BORA NA PUNDE KIDOGO RATIBA IKATOKA IKIIJUMUISHA GANAZ.

POLISI JAMII NA AREA A KUGOMBANIA UBINGWA WA WILAYA. IKACHEZWA MECHI YA KWANZA SIKU YA J5 POLIS NA AREA A NA IJUMAA YAKE KUKAWA NA GANAZ NA AREA A. KWA MSHANGAO WA WENGI ALHAMISI KIKAKAA KIKAO CHA CHAMA CHA MKOA DRFA NA KIKAIPOKA TENA USHINDI GANAS NA KUIAMBIA CDA IJIANDAE KESHO YAKE KWA MECHI.

ASUBUHI GANAZ FC INAPOKEA BARUA KUTAARIFIWA MAAMUZI YA RUFAA KWAMBA WAKAAMBIWA CDA WALIKATA RUFAA CHAMA CHA MKOA HIVO CHAMA KIMEONA MAAMUZI YALIYOAMRIWA NA DUFA CHA WILAYA HIKI ZILE KAMATI ZA KUAMUA RUFAA ZILIKAA KWA PAMOJA KWAMBA KAMATI YA RUFAA NA YA NIDHAM NA ILITAKIWA KILA MOJA IKAE KIVYAKE NA ITOE MAAMUZI.

TUKAHOJI KWAHIYO INAKUAJE SASA BASI ISIKILIZWE UPYA WAKASEMA HAIWEZEKANI TENA HIVO KAMA TUNATAKA TUKATE RUFAA TFF TAIFA KUMBUKA SAA 4 HIYO TUNAAMBIWA IVO NA ILIKUWA IJUMAA NAJIONI MECHI. UONGOZI WA GANAZ UKAONA BASI ISIWE TABU KWA KUWA MAZINGIRA YALIKUWA YAPO WAZI NA WAO NDO WAMESHIKA MPINI ITALIWA HELA ZAKE BURE IKAPOTEZEA LAKINI ROHO IKIWAUMA SANAAA.

WADAU NA MCHANGO WENU

Na Hassan Lemma

Wakati maximo anachukua timu ile nafasi ya 134 mnamo august 2006 imekua ikipanda nafasi kila kukicha tulikua katika wastani wa nafasi za tisini yaani tulikaribia nafasi ya 75 ammbayo ingemuwezesha mchezaji wetu kutoka ligi yetu na kwenda kucheza Premier League ya UK..mnamo december 2007 tulifikia kiwango ambacho sidhani kama tuliwahi kufikia huko nyuma yaani nafasi ya 89 lakini tulishuka kidogo miezi iliyofuata mpka ilipofika August 2009 tukifika nafasi ya 93 na nafasi mbaya aliyowahi kufika maximo ni miezi mitatu baada ya kuchukua timu ambayo ni nafasi 121 october 2006 ambayo bado nasema ni nzuri maana miezi miwili ya nyuma tulikua nafasi 134 lakini baada hapo kama ni nafasi ya juu aliyoshuka basi ili may 2007 na september 2008 yaani nafasi ya 117 basi majungu yakaan...za baadae tukashindwa kumuongezea mkataba sababu kubwa ikiwa ni kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao yeye aliona hawana nidhamu na baadhi ya wachezaji hao wameonyesha kuwa hawana nidhamu hata baada ya kuteuliwa na makocha wazawa na huyu Jan Poulsen na nikianza na huyu kocha wa sasa Jan Poulsen amepewa timu ikiwa nafasi ya 111 katika rank za fifa lakini kila siku timu inashuka mpaka february hii tupo katika nafasi ya 139...yaani imepita hata wakati ule tukiwa na kocha wazawa wakina mshindo Msolwa kama sijakosea.....Maswali ni haya; 1. TFF inaturudisha kule tulikotoka kabla maximo hajapewa kazi??? 2. Kuna sababu gani ya kuendelea na Jan Poulsen kwa sasa au ni kipya gani anachokionyesha kwa sasa???? 3. Nini kazi ya Mkurugenzi wa Ufundi TFF???? 4. Je Mikoani hakuna wachezaji ambao wanafaa taifa ambao hawapo timu za ligi kuu 5. Je Mfuko wa rais unamlipa kocha haufanyi tathimini maana kuendelea kumlipa mtu ambae kazi yakae kukurudisha nyuma ni upuuzi 7. Wadhamini wa TAIFA STAR NMB na SERENGETI huu udhamini usio na tija mnaondelea nao kwa timu ya taifa unamanufaa kwenu binafsi lakini sio kwa watanzani ??na mengine mengi nitaendelea kuuliza baadae :
SULUHISHO
1.Kuna kila sababu ya watanzania kugomea kwenda kuangalia mazoezi ya timu ya taifa na mechi zake
2. Wadhamini kuvunja udhamini kwa Taifa star na kuidhamini Twiga Star

Ndugu mdau niambie unachofikiri maana hii ni makala ndefu nimeomba magazeti mengi niweze kuitoa hapo juu ni kama kasamari kadogo kwa makala yenyewe kuhusiana na Timu ya Taifa na TFF na pia hayo ni baadhi ya maswali tu machache na kila swali pia lina makala yake.....


.kwa mawasiliano zaidi hlemmeh@ yahoo.com

majembe yetu Samatta & Ulimwengu.

REKODI ZA LIONEL "MESSIAH" MESSI KATIKA NAMBA



 
Historia imeendelea kutengenezwa. Magoli matano ya Lionel Messi katika ushindi wa Barcelona wa 7-1 dhidi ya Bayern Leverkusen katika usiku wa jumatano ya jana ulimfanya Muargentina huyo kuandika historia mpya katika vitabu vya champions league.
Akiwa anakaribia kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye  zaidi katika msimu kwa Barcelona na kwa ligi ya mabingwa ulaya katika msimu mmoja – blog hii inakuletea rekodi za kijana huyu kutoka Argentina kupitia namba.

3 – Messi sasa amefunga hat tricks tatu katika ligi ya mabingwa wa ulaya, akiifika rekodi ya Filippo Inzaghi. Ni wachezaji watatu wa Barcelona (Rivaldo, Ronaldinho na Samuel Eto’o) ndio huko nyuma waliweza kufunga hat tricks katika kombe hilo. Pia amekuwa ndio mchezaji wa kwanza kufunga hat-tricks mbili katika msimu mmoja wa Champions league.


3 – Muargentina huyo alishinda tuzo mchezaji bora wa dunia mwaka huu, akiwafikia washindi wa zamani walioshinda mara 3 Michel Platin, Johan Cruyff na Marco Van Basten huku ndio kwanza akiwa na miaka 24.


4 – Messi amemaliza akiwa mfungaji bora wa Champions league katika miaka mitatu iliyopita. Na sasa yupo karibuni kuweza kumaliza msimu akiwa mfungaji bora na kuweza kufikia rekodi ya gwiji wa Bayern Munich Gerd Muller akiwa ndio mchezaji pekee  kuwa mfungaji bora kwa misimu minne mfululizo katika UCL/European Cup.


5 – Messi ndio mchezaji wa kwanza  katika historia ya Champions league kufunga magoli matano katika mechi moja.


6 – Mshambuliaji huyo mzaliwa Rosario amefunga katika mashindano sita tofauti kwa Barcelona msimu huu; La Liga, Copa del Rey, Spanish Supercopa, Uefa Super Cup na kombe la dunia la vilabu pamoja Champions league; akiifikia rekodi ya mchezaji mwenzie Pedro aliyoiweka 2009.


12 – Messi sasa amefikisha idadi ya magoli 12 katika champions league msimu huu, akiifikia rekodi yake aliyoweka msimu uliopita na akiwa yupo sawa na Ruud Van Nistelrooy aliyoiweka msimu wa 2002-03 – huku akiwa amebakiwa na michezo zaidi ya mitano kama Barca wafika finali msimu huu.


18 – Tangu aanze kuichezea Barcelona mwaka 2005, Messi ameshinda makombe  18 na wakatalunya hao.

22 – Kufuatia hat-trick dhidi ya Switzerland wiki iliyopita, Messi sasa ana magoli 22 katika mechi 67 alizoichezea Argentina. Diego Maradona alifunga magoli 34 katika mechi 91 akiwa na Albiceleste (Argentina).


24 – Katika mechi ya kwanza dhidi ya Leverkusen, Messi aliweka rekodi ya kufunga magoli mengi (19) katika hatua ya mtoano . Jana usiku akafunga mengine matano na kuifanya idadi hiyo kuongezeka hadi kuwa 24.


49 – Muargentina huyu sasa amefikisha jumla magoli ya champions legue 49 – akiwapita Del Piero (44), Filippo Inzaghi (46), Eusebio (47), Andry Shevchenko (48) katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa UCL na European Cup. Magoli yake matano  yalimfanya amkute gwiji wa Real Madrid Alfred Di Stefano wote wakiwa nafasi ya nne, nyuma ya Thierry Henry (51), Van Nistelrooy (54) na Raul (71).

93 – Messi ana assists 93 kwa Catalan club, zikiwemo 73 katika misimu minne iliyopita na 20 za msimu huu.

188 – Tangu Pep Guardiola achukue majukumu ya ukocha Barcelona, Messi amefunga mabao 188 katika mechi rasmi 201.

228 – Kwa ujumla, Muargentina huyo ana magoli 228 kwa klabu yake, akiwa nyuma kwamagoli 7 tu kuweza kufikia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa Barcelona Cesar Rodriguez.

Thursday, March 8, 2012

HILI ZENGWE LA UBINGWA WA LIGI YA MKOA WA DODOMA!

   
 • CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA DODOMA

  YAH:KUFUTWA KWA MCHEZO KATI YA MASKANI NA POLISI JAMII
  mada ya hapo juu yahusika kamati ya mtendaji baada yakupitia kikao cha kamati ya mashindano imefuta mchezo kati ya timu yako na timu ya polisi jamii kutokana na kupanga matokeo kwa kutumia kifungu no:19 cha kanuni za mashindano timu yako italipa faini ya sh.200000/= na viongozi wako wataitwa muda wowot
  e na kamati.

  ABUBAKAR IBRAHIM
  K/MKUU DOREFA

  HOJA YETU:tunashindwa kufahamu matokeo yetu yamefutwa kwa ushahidi upi ambao wamejiridhisha nao kwamba matokeo yamepangwa sisi tumemaliza ligi tukiwa na point 8 na magoli 7 na cda wamemaliza ligi wakiwa na point 8 namagoli 5 sisi tumecheza mechi ya mwisho tarehe 4/3/2012 lakini tarehe 6/3/2012 tumeshangazwa CDA kutangazwa bingwa leo tarehe 8/3/2012 ndio tumepewa barua yakufutwa kwa matokeo yetu zidi ya polisi jamii barua ya dorefa haioneshi ushahidi wowote wa kupangwa matokeo. wala haijatuita kutuita katika kamati yao lakini kwenye barua yao wamedai watatupa onyo tunasikitika kwa haya yanaotokea kwani dorefa inaburuzwa na kigogo wa TRA DODOMA ambayeni kiongozi wa juu wa CDA pia ni makamu m/kiti dorefa mpira umechezwa uwanjani kila mtu kaona kwanini wamlete bingwa wa makaratasi timu imetumia gharama kubwa kuwaweka vijana kambini mwezi 1 tunaomba tusaidiwe swala hili kwani lina mikono ya watu wanaoharibu mpira wa dodoma tuko radhi kudai haki yetu mpaka tone la mwisho la damu kwani kuto kudai haki yako ni dhambi

  AZIZ CHIKAULA
  KATIBU WA TIMU

HIVI NDIVYO WASEMAVYO MASTAA WA BONGO KWENYE MTANDAO WA FACEBOOK


Thanks god. Jana 2mecheza mechi ye2 ya 2 ya Congo premier league na kupata ushindi mwembamba wa goli 1 ugenini dhidi ya SANGABALENDE.SANGABALENDE 0 - 1 TP MAZEMBE.mfungaji MBWANA SAMATTA.
Thanks god pia kwa kumjalia Tom ulimwengu kucheza mechi yake ya kwnza ya ligi akiwa na mazembe mungu mjalie nguvu zaidi.
 
.

 • ‎"If you can't fly then run, if you can't run then walk, if you can't walk then crawl, but whatever you do you have to keep moving forward." lengo ni moja....one love friends.

 • Samatta ni mshambualiaji anayetakiwa kuwemo katika kila mechi ambayo tunacheza iweje leo akose uzalendo......Tff wekeni mazingira mazuri kwa faida ya mpira wetu.......15,000 kama bonus au posho haileti changamoto.....mtazamo