Search This Blog

Saturday, November 26, 2011

BREAKING NEWS: SIMBA BINGWA UHAI CUP, YAITANDIKA AZAM.

Fainali ya mashindano ya Uhai Cup imemalizika dakika chache zilizopita na Simba sports club under 20 imefanikiwa kuchukua kombe hilo baada ya kuwafunga Azam FC kwa penati.

UDINESE YAIPIGA 2-0 ROMA - YAONGOZA SERIE A


szólj hozzá: Udinese Roma 2-0

KALI YA LEO: BORUSSIA YAONGOZA LIGI YA BUNDERSILIGA BAADA YA MIAK 26


Timu ya Borussia Moenchenglabach imeamaliza ukame wa maiak 26 baada ya ushindi wa jana kwenye ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya FC Colegne wa mabao 3-0, ushindi ambao umeawafanya waongeze ligi .

Klabu hiyo haijawahi kuongoza ligi hiyo tokea miaka 26 iliyopita.

EXCLUSIVE VIDEO: MAGOLI NA ASSISTS ZOTE ZA BECKHAM KATIKA LIGI KUU YA MAREKANI.

EXCLUSIVE: KOCHA MPYA WA SIMBA KUWASILI LEO BONGO


Baada ya aliyekuwa kocha wa timu ya Simba Moses Basena kutemeshwa kibarua chake kwa kukosa kibali cha kufanya kazi nchini, klabu hiyo inatarajiwa kupata kocha leo. Boss mpya wa benchi la ufundi la Simba, Mserbia Milovan Cirkovic, anatarajiwa kuwasili nchini leo, kabla ya kesho kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo kwenye Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Hii ni mara ya pili kwa Milovan kuja kuinoa timu hiyo ambapo awali aliifundisha mwaka juzi kabla ya kuiacha na nafasi yake kushikwa na Mzambia, Patrick Phiri.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Goefrey Nyange ‘Kaburu’, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, Milovan ambaye anambadili Mganda Moses Basena, anawasili leo usiku na pindi atakaposaini mkataba huo, atabaki kuendelea na shughuli nyingine.

Alisema walishafanya mazungumzo na kocha huyo na hivyo ujio wake unatokana na makubaliano waliyoafikiana baina yao.

MIZENGO PINDA KUTINGA TAIFA LEO KUWAPA SAPOTI KILI STARS.

Kiranja Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya CECAFA Chalenji 2011 ambapo wenyeji Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ wataumana na Rwanda ‘Amavubi’ kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema, Pinda angezindua michuano hiyo iliyoanza jana kwenye uwanja huo.

Kilimanjaro Stars inayonolewa na Charles Boniface Mkwasa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ambao ndio mabingwa watetezi, itashuka katika dimba hilo kukuvaana na Rwanda majira ya saa 10:00 jioni.

Michuano hiyo ilianza jana ambapo Burundi iliitandika Somalia mabao 4-1, katika mchezo wa kwanza, huku Uganda ikifunga Zanzibar mabao 2-1 katika mchezo wa pili.

Katika hatua nyingine, TFF imetangaza viingilio katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ambapo kwa mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni zaidi ya 30,000 kiingilio kitakuwa sh 1,000, wakati viti vya rangi ya chungwa zaidi ya 10,000 kiingilio kitakuwa sh 3,000.

Wambura alisema kwa watakaokaa VIP C na B ambayo jumla ya viti vyake ni 8,000 kiingilio kitakuwa sh 5,000 wakati VIP A yenye viti 700 kiingilio ni sh 10,000.

CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP: ZANZIBAR YAANZA KWA KIPIGO

Mchezaji wa Zanzibar Heroers Ali Badru akichuana na mchezaji wa Uganda Cranes Andrew Mwesigwa wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP

Waziri Mkuu wa Kenya Bw. Raila Odinga katikati akifurahia jambo kwa pamoja na Rais wa Shirikisho la vyama vya Michezo Afrika Mashariki Leodger Tenga kushoto pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mutinda Mutiso wakati walipkuwa wakishuhudia pambano la pili katika mashindano ya kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 linalofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Tayari mpira umekwisha ambapo Uganda Cranes imeifunga Zanzibar Heroers magoli 2-1 goli la kwanza la Uganda Cranes limefungwa na Mchezaji Danny Wagaruka katika kipindi cha kwanza, huku Mike Serumaga akifunga goli la pili katika kipindi cha pili, goli la kufutia machozi kwa upande wa Zanzibar Heroers limefungwa na mchezaji Ali Badru katika kipindi cha pili.

Wadau kutoka Serengeti Breweries nao walikuwepo kwani wao ndiyo wawezeshaji au wadhamini wa mashindano haya mtari wa juu kutoka kulia ni Moses Keba, Mr. Ssebo, mstari wa chini kutoka kulia ni Ritah Mchaki na Maurice Njowoka

Kocha Micho ambaye amewahi kuifundisha Yanga sasa ni kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda- nae alikuwepo uwanjani kuangalia mchezo

Wadau na mashabiki wa soka wakiwa wanatizama mchezo huo wa ufunguzi wa CECAFA Tusker Cup.

Friday, November 25, 2011

BECKHAM MBIONI KUJIUNGA NA PSG KWA £12M


David Beckham yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kusaini mkataba wa kujiunga na Paris Saint-Germain baada ya kupewa ofa ya mkataba wa miezi 18 wenye thamani ya £12m.

Beckham amekuwa kipenzi cha raisi wa PSG Nasser al-Khelaifi anayemuona Becks kama mtu sahihi wa kuipa mageuzi klabu hiyo kuwa moja ya timu kubwa barani ulaya.

Jana Al-Khelaifi alikiri kwamba uamuzi wa timu gani ya kujiunga nayo ulikuwa kati ya Tottenham na PSG, lakini inaeleweka kuwa muingereza huyo anapendelea zaidi kujiunga na wafaransa hao.

Fedha sio tatizo kwa PSG na wana imani kubwa watafanikiwa kumshawishi Beckham kusaini mkataba wa kuitumikia klabu yao in January. Spurs hawawezi kupambana na matajiri wa kiarabu wanaoimiliki klabu hiyo, ukiachana na mshahara pia hana uhakika kama atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha Harry Redknapp.

PSG wametoa ofa hiyo nzuri katika mazungumzo yao yanayoendela kati yao na wawikilishi wa Becks na wanaamini watashinda mbio za kumsajili kiungo huyo.


RIHANNA ALIPOKUTANA USO KWA USO NA JERMAIN DEFOE

RIHANNA ALIKUTANA NA MSHAMBULIAJI WA TOTENHAM JERMAIN DEFOE MARA TU BAADA YA KUMALIZA KUTUMBUIZA HIVI KARIBUNI JIJINI LONDON,
UNAJUA KILICHOTOKEA ?
KABLA YA TAMASHA KUANZA RIHANNA ALIAMBIWA MIONGONI MWA WATU MAARUFU WATAKAOHUDHURIA ONYESHO LAKE NI WACHEZAJI WA ARSENAL,
BAADA YA TAMASHA ALIENDA KWENYE ENEO LA WATU MAARUFU NDI O AKAMUONA DEFOE AKAMFUATA AKAMWAMBIA NAKUJUA WEWE SI JERMAIN DEFOE UNACHEZEA ARSENAL... DEFOE AKAMWAMBIA HAPANA MI NACHEZEA TOTENHAM WALA SI ARSENAL,BAADA YA HAPO RIHANNA AKAZUGA ETI NAJUA UNACHEZEA TOTENHAM LAKINI UNAONEKANA UTAPENDEZA ZAIDI UKIVAA JEZI NYEKUNDU YA ARSENAL...

INTERVIEW YA NIZAR KHALFAN

HIVI NDO VIGEZO VINAVYOTUMIKA KAMA TIMU ZINALINGANA POINTS KWENYE UEFA CHAMPIONS LEAGUE

HIVI NDO VIGEZO VINAVYOTUMIKA KAMA TIMU ZINALINGANA POINTS KWENYE UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ( nadhani hapa utata wa sababu ya Benfica kuwa kileleni umetatuliwa )

1) The results of games between the teams in the tie (if tied, by goal difference and then by away goals counting double).

2) Goal difference in all group games.

3) Highest number of goals scored in all games.

4) Highest Uefa ranking over the previous five seasons.

Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden


Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)


Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/

EXCLUSIVE: DANNY MRWANDA AULA VIETNAM- AONGEZEWA MKATABA MWINGINE/

Mshambuliaji wa kiamtaifa wa Tanzania Daniel “Danny” Mrwanda ameongezewa mkataba wamwaka mmoja kuendelea kuichezea klabu yake ya Dong Tam Long An ya nchini Vietnam.

Mrwanda ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea klabu ya Dong Tam Long An iliyoshiriki ligi kuu ya Vetnam msimu uliopita amesaini mkataba wa mwaka mmoja lengo likiwa ni kuhakikisha timu hiyo inarudi tena ligi kuu msimu ujao.


baada ya kuonyesha kiwango kizuri mchezaji huyo wa zamani wa Simba ya Tanzania amefanikiwa kuongezewa mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.




FAINALI YA UHAI CUP KATI YA SIMBA NA AZAM SASA KUCHEZWA JUMAMOSI ASUBUHI


Taarifa zilizotufikia hivi zinasema kuwa, baada ya wadau kupiga kelele juu ya umuhimu wa mchezo wa fainali michuano Uhai Cup kati ya Simba na Azam kuchezwa siku jumamosi na sio kesho jioni kama ilivyopangwa awali ili kuwapa nafasi mashabiki kwenda kuhudhuria mchezo wa timu ya Zanzibar dhidi ya Uganda, shirikisho la soka nchini TFF limeamua kwa uamuzi mmoja kuwa mchezo huo sasa utachezwa siku ya jumamosi asubuhi katika uwanja wa Karume-DSM.

Hongereni TFF kwa hili.

EXCLUSIVE: BASENA KUTOENDELEA KUIFUNDISHA SIMBA MSIMU HUU

*******************************KWAHERINI******************************************

Taarifa za kuaminika 100% ambazo blog hii imezipata ni kwamba kocha Moses Basena hatoendelea kuifundisha klabu ya Simba katika duru la pili la mzunguko wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Chanzo cha Basena kushindwa kuendelea na kazi katika klabu ya Simba ni kutokana na kukosa kibali cha kuendela kufanya kazi permanently nchini hali iliyopeleka klabu hiyo kushindwa kuendelea nae kama kocha mkuu wa ndani ya timu hiyo.

Simba kwa sasa wapo katika mchakato wa kutafuta kocha atakayeziba pengo la Basena na kuiwezesha klabu hiyo kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu na hatimaye kutwaa uchampion wa Tanzania bara.

Thursday, November 24, 2011

NIZAR KHALFAN AJIUNGA NA PHILADELPHIA UNION.

Klabu ya Vancouver Whitecaps ya nchini Canada inayoshiriki Ligi kuu nchini Marekani imemtoa kiungo wa kimataifa toka Tanzania Nizar Khalfan kwenda kwenye klabu ya Philadelphia Union ambayo kama Whitecaps inashiriki ligi ya MLS . Whitecaps imemruhusu Nizar kwenda Philadelphia katika mchakato wa maalum wa kubadilishana wachezaji wa ligi hiyo maarafu kama Waver Player Draft.
Nizar Khalfan ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Mtwara, ameichezea Whitecaps katika michezo 22 ya ligi ya MLS kwa mwaka 2011 ambapo alianza michezo 9. Katika dakika 1,066, kiungo huyu mwenye umri wa miaka 23 alifunga bao moja huku akitoa pasi 4 za mabao kwa wenzake .


Nizar alijiunga na Whitecaps katikati ya msimu wa mwaka 2009 wakati klabi hiyo bado ikiwa kwenye ligi daraja la kwanza na kwa jumla amecheza michezo 58 ambayo ni sawa na dakika 3,029 .
Khalfan alianza soka lake nchini Tanzania akiwa na klabu ya Mtibwa Sugar kwenye msimu wa mwaka 2005/06 na katika msimu wa mwaka 2006-7 aliichezea Moro United.


Katika misimu hiyo miwili Nizar alicheza michezo 57 akifunga mabao 16 akiwa na Mtibwa na mabao matano katika katika michezo 16 akiwa na Moro United. Katikati ya misimu hiyo miwili Nizar alicheza soka la kulipwa nchini Kuwait
Khalfan ameichezea timu ya taifa ya tanzania Taifa Stars katika michezo 25 ya kimataifa na amefunga mabao matano,

Khalfan alifunga bao la ushindi katika mchezo wa kihistoria dhidi ya Burkina Faso kwenye uwanja wa taifa wa Dar es salaam tarehe 2 septemba 2006 kwenye uwanja wa taifa Dar es salam, na pia alifunga bao la nne kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Mauritius septemba 6 mwaka 2008.

Hivi karibuni Khalfan aliichezea timu yake ya taifa katika mchezo wa kufuzu kwa mataifa ya afrika ambapo alitoa pasi ya bao lililofungwa na Mbwana Samatta kwenye mchezo dhidi ya Algeria ulioisha kwa sare ya 1-1, na pia alianza kwenye michezo yote miwili ya awali ya kufuzu kwa kombe la dunia 2014 ambako timu yake ilifuzu kuingia kwenye kundi lenye timu za Ivory Coast, Morocco na Gambia.

ASANTE KUWASILI NCHINI SIKU YA UHURU - KUCHEZA NA KOMBAINI YA SIMBA NA YANGA DES.11

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Future Centery Helene Masanja,akizungumza na wahandishi wa habari kuhusu mechi ya kombaini ya timu za Simba na Yanga dhidi ya timu ya Kumasi Asante Kotoko ya Ghana,katikati ni Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga na Mwenyekiti wa DRFA Amin Bakharesa.Picha na Michael Matemanga



TIMU ya soka ya Kumasi Asante kotoko ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa Taifa.


Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Future Century Limited, Helen Masanja.




Masanja alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata.


Alisema kuwa wanatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwani tayari kombaini ya timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.


Aliongeza kuwa makocha wawili, mkongwe, Abdallah “King Mputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi la ufundi la timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo baadaye. Wengine katika benchi la ufundi na meneja, Boniface Pawasa na daktari wa timu, Juma Sufiani.


Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.


Masanja alisema kuwa Yanga na Simba zimekubaliana na kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane mwaka 1935. Alisema kuwa historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja kuanzia mwa 1922.


Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa zinapotokea timu hizo zinacheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.


Wakati Nchunga akisema hayo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.


Alisema kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao.

MKWASA NA JULIO WATANGAZA WACHEZAJI 20 WALIOPITA KATIKA CHUJIO LA KILI STARS

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 20 kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza kesho.


Wachezaji waliobaki kati ya 28 waliokuwa wameitwa awali ni Juma Kaseja (Simba), Shabani Kado (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba), Ibrahim Mwaipopo (Azam) na Juma Nyoso (Simba), Said Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Nurdin Bakari (Yanga), Haruna Moshi (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Simba).


Wengine ni Said Maulid (Angola), Musa Mgosi (DC Motema Pembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC), Mrisho Ngassa (Azam), Ramadhan Chombo (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Rashid Yusuf (Coastal Union).


Kilimanjaro Stars itacheza mechi yake ya kwanza Novembe 26 mwaka huu dhidi ya Rwanda.

BREAKING NEWS: TENGA ACHAGULIWA TENA KUWA RAISI WA CECAFA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Tenga amechaguliwa leo (Novemba 24 mwaka huu) bila kupingwa baada ya mpinzani wake Fadoul Hussein wa Djibouti kutotokea kwenye uchaguzi.
Kutokana na hali hiyo, mjumbe kutoka Uganda alitoa hoja ya Tenga kupitishwa bila kupingwa, hoja ambayo iliungwa mkono na Kenya, Tanzania, Uganda, Sudan, Zanzibar, Ethiopia, Burundi na Eritrea.
Jumla ya nchi wanachama zilizopiga kura katika uchaguzi uliofanyika hoteli ya New Africa ni kumi na moja, na kila moja ilikuwa na kura moja tu.
Kwa upande wa nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji kulikuwa na wagombea wanane. Waliopita katika raundi ya kwanza na kura zao kwenye mabano ni Abdiqani Saeed Arab wa Somalia (8), Tariq Atta Salih wa Sudan (8) na Raoul Gisanura wa Rwanda (8).
Wengine katika raundi ya kwanza na kura walizopata kwenye mabano ni Sahilu Wolde wa Ethiopia (4), Justus Mugisha wa Uganda (4), Tesfaye Gebreyesus wa Eritrea (4), Hafidh Ali Tahir wa Zanzibar (2) na
Abubakar Nkejimana wa Burundi (3).
Mjumbe aliyefanikiwa kushinda katika raundi ya pili na kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ni Wolde wa Ethiopia aliyepata kura tano dhidi ya nne za Mugisha na mbili za Gebreyesus.
Mwenyekiti anakaa madarakani kwa miaka minne wakati wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanachaguliwa kila baada ya miaka miwili.

VALENCIA YAIPIGA GENK 7-0 NA KUWEKA REKODI ULAYA


BIGGEST CL WINS | THE TOP 10


MatchScore
Date
Liverpool-Besiktas8-02007-08
Valencia-Genk7-02011-12
Arsenal-Slavia Prague
7-02007-08
Juventus-Olympiakos
7-02003-04
Marseille-Zilina7-02010-11
Bayern Munich-Sporting7-12008-09
Man Utd-Roma7-12006-07
Real Madrid-Genk6-0
2002-03
Arsenal-Braga6-02010-11
Marseille-CSKA Moscow
6-01992-93

CHELSEA BADO WAPO ICU, WAPIGWA 2-1 NA LEVERKUSEN


Bayer Leverkusen v Chelsea by vermouther

XAVI NA LEO MESSI WAACHA MSIBA JIJINI MILAN


AC Milan v Barcelona by vermouther

VAN PERSIE AENDELEZA MAAJABU, ARSENAL WAKIFUZU CHAMPIONS LEAGUE


Arsenal v Borussia Dortmund by vermouther

LEO ZAMU WA MASHABIKI WA MAN UNITED - HUYU NI NANI?

Wednesday, November 23, 2011

Welcome To…The Balotelli Zone



ETI JAMANI HII KWELI NI OFFSIDE?





KWENYE MCHEZO WA MWISHONI MWA JUMA KATI YA AS ROMA NA LECCE MWAMUZI WA PEMBENI ALILIKATAA BAO HULI ETI MFUNGAJI ALIKUA AMEOTEA....

HIVI KAMA WEWE NDO MWAMUZI AFU LINAFUNGWA BAO ZURI KAMA LILE HATA USIPONYOOSHA KIBENDERA UTALAUMIWA KWELI?

RIBERY APIGA MBILI, BAYERN WAKING'ARA ULAYA


Bayern Munich - Villarreal footyroom.com by footyroom

MOURINHO AFANYA MAUAJI ULAYA


Real Madrid - Dinamo Zagreb footyroom.com by footyroom

MAN UNITED, CITY HATIHATI KUFUZU MABINGWA WA ULAYA


Manchester United - Benfica footyroom.com by footyroom

MASHABIKI WA ARSENAL, MSAADA TUTANI HUYU NI NANI?

COUNTDOWN TO CECAFA CHALLENGE CUP: TIMU ZAANZA KUWASILI-FAHAMU WATAKAPOFIKIA NA WATAKAPOFANYA MAZOEZI

Timu zinazoshiriki CECAFA Tusker Challenge Cup zinaendelea kuwasili Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoanza Novemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.
Somali na Djibouti tayari zimeshawasili. Timu hizo zilitua nchini jana mchana kwa nyakati tofauti. Ratiba ya ujio wa timu nyingine ni kama ifuatavyo;
Team Arrival: Accommodation:
Burundi Nov 23rd 1545hrs RwandAir - Lunch Time Hotel (Ubungo)
Djibouti Nov 22nd 1320hrs Ethiopian Airlines - Wanyama Hotel (Sinza)
Ethiopia Nov 24th Ethiopian Airlines - Johannesburg Hotel (Sinza)
Kenya Nov 27th Kenya Airways - Rungwe Hotel (Kariakoo)
Malawi Nov 27th Air Malawi - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Rwanda Nov 23rd 1545hrs RwandAir - Rungwe Hotel (Kariakoo)
Somalia Nov 22nd Kenya Airways - Wanyama Hotel (Sinza)
Sudan Nov 23rd 1320hrs Ethiopian Airlines - Marriot Hotel (Mabibo External)
Tanzania - Rainbow Hotel (Morogoro Rd)
Uganda Nov 23rd 1600hrs Air Uganda - Royal Valentino Hotel (Kariakoo)
Zanzibar Nov 23rd by boat- afternoon - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Viwanja vya mazoezi kwa ajili ya timu zinazoshiriki michuano hiyo ni; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (viwanja viwili), Shule ya Sekondari Loyola na Uwanja wa Karume.

HATMA YA TENGA CECAFA KUJULIKANA KESHO


Mkutano Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) utafanyika kesho (Novemba 24 mwaka huu) kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.
Moja ya ajenda katika mkutano huo utakaonza saa 4.00 asubuhi ni uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya CECAFA. Nafasi zinazogombewa ni tano; (Mwenyekiti na wajumbe wane wa Kamati ya Utendaji).
Wagombea uenyekiti ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye anatetea nafasi hiyo. Mpinzani wa Tenga ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Djibouti, Fadoul Hussein.
Nafasi nne za Kamati ya Utendaji zinagombewa na watu wanane. Wagombea hao ni Abdiqani Saeed Arab (Somalia), Tariq Atta Salih (Sudan), Justus Mugisha (Uganda), Tesfaye Gebreyesus (Eritrea), Hafidh Ali Tahir (Zanzibar), Sahilu Wolde (Ethiopia), Raoul Gisanura (Rwanda) na Abubakar Nkejimana (Burundi).
Baada ya Mkutano Mkuu, saa 7.00 mchana kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari ambao utafanyika hapo hapo hoteli ya JB Belmont.

BOBAN NA MKWASA WAKAMILISHA KAMBI YA KILI STARS


Kambi ya timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, imekamilika baada ya
mchezaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa nao kuripoti kambini.

Boban alishindwa kuripoti kambini mapema kutokana na matatizo ya kifamilia, lakini juzi Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alitishia kumtema kama asingejiunga
hadi kufikia jioni juzi, wakati Mkwasa alikuwa Afrika Kusini kuendesha mafunzo ya ukocha.

Akizungumza kwenye mazoezi ya timu hiyo jana, Julio alisema Boban aliripoti kambini juzi jioni. “Wakati nazungumza na waandishi mapema juzi alikuwa hajaripoti, lakini jioni tulipomaliza mazoezi tuliporudi hotelini tukamkuta tayari amefika,” alisema Kihwelo.

Kihwelo alisema ana furaha sasa idadi ya wachezaji 28 aliyowateua kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Chalenji, sasa imekamilika na kikosi chake kiko kamili kwa ajili ya mashindano hayo.

Kihwelo alisema ataandaa ripoti ya timu hiyo na kumpa Mkwasa ambaye alirejea juzi kutoka nchini Afrika Kusini alipokwenda kama mkufunzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili
kuijadili na kupata majina ya wachezaji 22 wanaotakiwa kwa michuano ya Chalenji ambao atawatangaza leo.

Alisema nidhamu, kujituma mazoezini na uwezo binafsi ndio vitu vya msingi atakavyoangalia kabla hawajateua majina hayo ya mwisho kwa ajili ya mashindano hayo.

Katika mashindano ya mwaka huu, Kilimanjaro Stars ambayo iko Kundi A na nchi za Nambia, Djibout na Rwanda, itaanza kampeni za kutetea kombe lake kwa kupambana na Rwanda ‘Amavubi’ Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tuesday, November 22, 2011

PHIL JONES AANZA MATANUZI, ANUNUA GARI LA MIL.377


Beki wa Manchester United na England Phil Jones amesherekea mwanzo wake mzuri wa msimu kwa kuamua kutumia zaidi ya £130,000 ambayo ni sawa Mil.377 za kibongo kununua gari aina ya Aston Martin.

Mchezaji huyo wa zamani wa Blackburn, 19. Amejihakikishia namba katika kikosi cha kwanza cha United baada ya uhamisho wake wa £16.5million in the summer.

Na sasa ni wazi Jones ameanza kuzoea maisha ya hali juu, baada ya kuvuta mkoko wa bei mbaya.