Search This Blog

Saturday, February 9, 2013

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 1 - 1 JKT OLJORO FULL TIME

Mpira umemalizika Simba 1-1 JKT Oljoro

Mpira unawezaisha muda wowote na matokeo bado 1kwa1.Zimeongezwa dk 2

Dk ya 42 kipindi cha pili simba wanapoteza nafasi ya kupata bao la ushindi.

Dk 37 kipindi cha pili Jkt oljoro wanakosa goli la wazi.

Dk ya 28 kipindi cha pili, simba wanafanya mabadiliko Edward christopher anaingia na anatoka MudeJkt oljoro wanakosa goli la wazi na wanafanya mabadiliko kwa kumtoa Esau.

Ngasa ameingia kuchukua nafasi ya Rashid

Jkt wanasawazisha bao kufuatia uzembe wa beki ya simba.

JKT OLJORO wanakosa goli la wazi na wanafanya mabadiko ya mchezaji.

Mchezaji wa JKT anapewa kadi ya njano kwa kumkwatua Kazimoto.

Kipindi cha pili kimeanza hakuna mabadiliko yoyote.

Mashabiki wanaodhaniwa wa simba wanawashambulia watu waliovaa nguo zinazodhaniwa za CCM.

Dk 38 Oljoro wanalishambulia sana lango la Simba kwani wanaonyesha kuwakamata vilivyo

Hadi dk ya 34 simba wanaongoza goli moja lililofungwa na Kazimoto kwa shuti kali umbali wa mita 30

Paul Ngalema ameumia vibaya na kutolewa uwanjani ameshindwa kuendelea na mchezo

Dk ya 29 JKT OLJORO wanakosa goli la wazi ktk shambulizi baada ya mpira kumtoka mikononi na JKT wakazubaa.

Kikosi cha Simba kinachoanza leo dhidi ya JKT Oljoro


KASEJA, CHOLLO, NGALEMA, KAPOMBE, KEITA, JONAS, KIEMBA, MUDDE, RASHID ISMAIL, KAZIMOTO na Haruni CHANONGO.

MABONDIA FRANISIC MIYEYUSHO VS SADIK MOMBA KUPAMBANA PASAKA


Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka, wanashudia katikati ni Promota wa mpambano huo, Kaike Silaju na Makamu wa Rais wa PST, Aga Peter .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, February 8, 2013

MANCHESTER UNITED HAIJAPOTEZA MECHI HATA MOJA NDANI YA MIAKA 10 WANAPOCHZESHWA NA MWAMUZI ATAKAYECHEZESHA MECHI DHIDI YA EVERTON

Mechi ya mwisho ya United kupoteza mwamuzi akiwa Mark Halsey
Manchester United wanaikaribisha Everton Old Trafford wikiendi hii. Everton wamekuwa wakiisumbua United katika kipindi cha hivi karibuni na wanapewa nafasi ya kuisimamisha United inayoongoza ligi kwa pointi 9 mbele ya mahasimu wao Manchester City.

Lakini mambo yanaweza kuwa magumu kwa Everton. Tatizo ni refa Mark Halsey. Refa huyu ana bahati nzuri na United, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kila anapochezesha mechi inayoihusisha kikosi cha Sir Alex Ferguson, Red Devils hawajawahi kupoteza mchezo.

Mara ya mwisho United wamepoteza mchezo wakiwa wanaamuliwa na Halsey ilikuwa ni mwaka 2003, mwezi August katika dimba la St.Mary kwenye mechi ya EPL dhidi ya Southmpton ambao waliibuka na ushindi wa goli la dakika ya 88 lilofungwa na James Beattie. Kikosi cha United kipindi kilikuwa kikiundwa pia na wachezaji kama Kleberson na Djemba Djemba huku CR7 akitokea kwenye benchi lakini hakishindwa kubadili matokeo. 


Rio Ferdinand tries to get his point across to Mark Halsey at White Hart Lane

HIZI NI REKODI ZA MECHI ZA UNITED WALIZOCHEZESHWA NA MARK HALSEY.

2012/2013

01/12/12 - Reading (a) W 4-3 (pen for Utd)
23/09/12 - Liverpool (a) W 2-1 (pen for Utd, red card for Jonjo Shelvey)

2011/2012

15/04/12 - Aston Villa (h) W 4-0 (pen for Utd)
12/12/11 - Fulham (a) W 5-0
29/10/11 - Everton (a) W 1-0

2008/2009

02/05/09 - Middlesbrough (a) W 2-0
31/01/09 - Everton (h) W 1-0 (pen for Utd)
06/12/08 - Sunderland (h) W 1-0
18/10/08 - West Brom (h) W 4-0

2007/2008
29/03/08 - Aston Villa (h) W 4-0
16/12/07 - Liverpool (a) W 1-0

2006/2007

29/11/06 - Everton (h) W 3-0
Sol Campbell receives a red card from referee Mark Halsey in 2003
2005/2006
17/04/06 - Tottenham (a) W 2-1 (above, right)
2004/2005
07/05/05 - West Brom (h) D 1-1 (pen for WBA)
26/02/05 - Portsmouth (h) W 2-1
22/01/05 - Aston Villa (h) W 3-1
16/10/04 - Birmingham (a) D 0-0

2003/2004
13/04/04 - Leicester (h) W 1-0
21/02/04 - Leeds (h) D 1-1
13/12/03 - Man City (h) W 3-1
22/11/03 - Blackburn (h) W 2-1
31/08/03 - Southampton (a) L 0-1

2002/2003
03/05/03 - Charlton (h) W 4-1
16/04/03 - Arsenal (a) D 2-2 (red card for Sol Campbell, right)
17/11/02 - West Ham (a) D 1-1

2001/2002
16/03/02 - West Ham (a) W 5-3 (pen for Utd)
12/12/01 - Derby (h) W 5-0
10/04/01 - Charlton (h) W 2-1

10 WAKATA RUFANI KAMATI YA RUFANI YA UCHAGUZI TFF

RUFANI kumi zimewasilishwa mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuhusiana na uchaguzi utakaofanyika Februari 22 na 24 mwaka huu.

Wakati uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) utafanyika Februari 22 mwaka huu, ule wa TFF wenyewe utafanyika Februari 24 mwaka huu.

Waliowasilisha rufani mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa na Idd Mtiginjola ni pamoja na waombaji uongozi saba walioenguliwa katika kinyang’anyiro hicho. Warufani hao ni Omari Mussa Nkwarulo na Michael Richard Wambura walioomba kugombea urais na umakamu wa rais.

Wengine ambao waliomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda mbalimbali ni Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Omari Isack Abdulkadir (Dar es Salaam), Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya) na Shaffih Kajuna Dauda (Dar es Salaam).

Warufani wengine ni wadau ambao waliweka pingamizi dhidi ya baadhi ya waombaji uongozi katika TPL Board na TFF, pingamizi ambazo zilitupwa mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa sababu za kiufundi.

Wadau hao waliokata rufani ni Agape Fue dhidi ya Kamati ya Uchaguzi TFF kupinga kumpitisha Jamal Malinzi kugombea urais, Medard Justinian dhidi ya Kamati ya Uchaguzi TFF kupinga kumpitisha Athuman Nyamlani kugombea urais, na Frank Mchaki dhidi ya Kamati ya Uchaguzi TFF kupinga kumpitisha Hamad Yahya kugombea uenyekiti wa TPL Board.

Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF imetoa siku ya kesho (Februari 9 mwaka huu) kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana kwa wote wenye maslahi na rufani hizo (interested parties) kupitia rufani hizo na kuwasilisha hoja zao kwa maandishi.

Kwa watakaoshindwa kufanya hivyo watapata fursa ya kuwasilisha hoja zao kwa mdomo, ambapo wanaweza kuwa wenyewe au wanasheria wao siku ya usikilizwaji wa rufani hizo. Rufani zitasikilizwa Jumapili (Februari 10 mwaka huu) kuanzia saa 2 asubuhi.
 
OLJORO MWENYEJI WA SIMBA VPL 2012/2013
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 inaingia raundi ya 16 kesho (Februari 9 mwaka huu) kwa mechi nne ambapo Oljoro JKT itaikaribisha Simba jijini Arusha.

Mechi hiyo namba 129 itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid huku Simba ikiingia na kumbukumbu ya sare katika mechi yake iliyopita dhidi ya JKT Ruvu wakati wenyeji wao wakiwa wameshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 tu utatumika kwa mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mgambo Shooting. Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Amon Paul kutoka Musoma mkoani Mara.

Toto Africans baada ya kufanya vibaya katika mechi tatu zilizopita ugenini imerejea nyumbaji jijini Mwanza itakapoumana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo utaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Mwamuzi Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani ndiye atakayechezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons na African Lyon ambayo imepata huduma za kocha mpya Salum Bausi kutoka Zanzibar. Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kwa Bausi kuiongoza timu katika VPL.

Maofisa wengine wa mechi hiyo ni mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Rashid, mwamuzi msaidizi namba mbili Abdallah Mkomwa wote kutoka Pwani wakati mwamuzi wa mezani ni John Kanyenye wa Mbeya. Kamishna wa mechi hiyo ni Rashid Rwena kutoka Ruvuma.

Mechi kati ya Mtibwa Sugar na Azam iliyokuwa ichezwe kesho imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo sasa itafanyika Jumapili (Februari 10 mwaka huu) katika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro.
                     
FDL KUENDELEA KUTIMUA VUMBI WIKIENDI
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwania tiketi za kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao inaendelea kutimua vumbi wikiendi hii kwa mechi kumi na moja zitakazopigwa kwenye viwanja mbalimbali.

Kundi A keshokutwa (Februari 10 mwaka huu) Mbeya City itacheza na Polisi Iringa katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Mkamba Rangers itaumana na Burkina Faso (Uwanja wa CCM Mkamba) wakati JKT Mlale itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Green Warriors na Ndanda zitacheza kesho (Februari 9 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B. Mechi nyingine kundi hilo kesho ni kati ya Tessema na Villa Squad kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Keshokutwa (Februari 10 mwaka huu) Transit Camp itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam wakati Polisi Dar es Salaam na Moro United zitavaana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Kundi C kesho (Februari 9 mwaka huu) ni Polisi Dodoma vs Polisi Tabora (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Polisi Mara vs Mwadui (Uwanja wa Karume, Musoma), Morani vs Kanembwa JKT (Uwanja wa Kiteto, Manyara) na Rhino Rangers vs Pamba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF

TUTAIFUNGA TOTO AFRICANS KESHO- SELEMBE

Kweli siyo nzuri kwetu lakini sio  mbaya tumeanza vizuri lakini sisi malengo yetu ni nafasi za juu kwa hiyo mapambano yanaendelea mpaka mwisho” anasema kiungo wa pembeni wa timu ya soka ya Coastal Union iliyopo katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara. Coastal ambayo itasafiri na kwenda kuwakabili Toto Africans ya Mwanza hapo kesho katikas uwanja wa CCM Kirumba .
‘ Tuliwafunga Toto kaatika mchezo wa kwanza,  na nategeme kuwafunga tena unajuwa , Mwanza mbali lakini tuta safiri kwa ndege HILO  ni jambo zuri kwetu tuta punguza uchovu’ anasema, Selembe na kuongeza
Nikweli kutakuwa na ugumu katika mchezo kwa sababu ni ngumu sana kushinda katika uwanja ule ( Kirumba) lakini Coastal imejipanga vizuri msimu huu na dhamira yetu ni kuwa miongonui mwa timu mbili za juu, hali ya wachezaji wenzangu pamoja na ile ya viongozi ndiyo inayo nifanya nijiamini kuwa titashinda”
“Wamuzi mpaka sasa kwa upande wetu wamejitahidi ila makosa ya kibinadamu yapo huwezi kuwalaumu sana lakini mpaka sasa wanakwenda vizuri wajitahidi kwani wao ndiyo muhimili wa soka letu” anamaliza kiungo huyo wa timu ya taifa ya Zanzibar

CHAMSHA BONGO! NITAJIE HUYU JAMAA NILIYESIMAMA NAYE,UKIWEZA PIA MUELEZEE KIDOGO NAMNA UNAVYOMKUMBUKA.

SAMATTA: GOLI LANGU DHIDI YA CAMEROON NI OMBI LANGU LA MSAMAHA KWA WASHABIKI NA NAAMINI WAMENISAMEHE

MBWANA Samatta amesema kuwa anaamini goli la ushindi alilofunga dhidi ya Cameroon linatosha kumsafisha kwa mashabiki wake.
 

Hiyo imekuja baada ya mashabiki wa soka kuwazomea pamoja na Thomas Ulimwengu wakati Stars ikicheza na Zambia, mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa.
 

Nikutokana na kuchelewa kuripoti kambini kujiwinda na mchezo huo wa kirafiki na Chipolopolo mwakajana.
 

Kitendo hicho kilimkasirisha kocha Kim Poulsen ambaye aligoma kuwapanga kwenye kikosi ambacho kilicheza mtanange huo.
 

Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao hilo pekee, likizamishwa na Mrisho Ngassa kwa shuti la mwendo mrefu.
 

"Naamini ushindi huu utakuwa umewafurahisha mashabiki na kurudisha imani kwetu." alisema Samatta.
 

Alisema haikuwa lengo leo kuchelewa kujiunga na kambi ya timu isipokuwa ni mambo tu yaliingiliana.

RIGOBERT SONG: DHARAU NA KUJIAMINI KUPITA KIASI KUMEFANYA STARS WATUFUNGE


RIGOBERT Songs amesema dharau na kujiamini kupita kiasi ni vitu ambavyo vilichangia Taifa Stars kuifunga Cameroon katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa jana.
 

Stars ilishinda bao 1-0. Bao hilo likifungwa na Mbwana Samatta aliyeunganisha krosi ya Frank Domayo dakika 89 ya mchezo.
 

Meneja huyo alisema jijini Dar es Salaam kuwa Taifa Stars ilicheza vizuri lakini wachezaji wake walikosa umakini.
 

"Ukiangalia goli ambalo tulifungwa utafahamu hilo. Mabeki hawakuwa makini."
 

Alisema wakati Domayo anapiga krosi beki wa kushoto Assou Ekotto alikuwa akimtazama na mpira huo kutua kwenye miguu ya Samatta aliyetikisa nyavu za Cameroon kirahisi.
 

"Hatukuwa makini. Mazingira ya goli yenyewe yanajieleza." alisisitiza beki huyo wa zamani wa Cameroon na Liverpool ya England.

PAMOJA NA FEDHA ZOTE ZINAZOCHUKULIWA KWENYE MAKATO YA UWANJA - HALI YA USAFI NI MBAYA UWANJA WA TAIFAHali ya usafi katika uwanja wetu wa taifa sio nzuri na inatia kinyaa kwa kweli pia ni aibu kwa soka letu na nchi kiujumla.

Katika mchezo wa Jumatano kati ya Tanzania na Cameroon katika jukwaa la VIP C nilishuhudia kinyesi cha binadamu kikiwa kimezagaa katika ngazi za kwenye siti za uwanja huo.

Kutokana na kuona uchafu huo ikabidi nianze kufuatilia suala hilo kwanini kinyesi kile kipo pale, katika kuuliza kwangu nikagundua kwamba baadhi ya vyoo vilikuwa vimejaa na kutapika hivyo inawezekana kuna shabiki mmoja wapo aliyekosa ustaarabu aliamua kujisaidia kwenye eneo hilo baada ya kubanwa na haja.

Lakini uwanja huu wa taifa umetoka kuchezewa mechi mbili kubwa wikiendi iliyopita na katika mechi hiyo tuliambiwa kwamba kuna mamilioni yalikuwa yamekatwa, katika mechi ya Yanga na Mtibwa zilikatwa shilingi millioni 15,435,255.48, wakati kwenye mechi ya Simba vs JKT zilikatwa
8,869,704.64, hivyo ndani ya siku mbili uwanja ulichukua zaidi ya Millioni 24.

Sasa kweli kihulasia ni wapi fedha hizo zinakwenda kiasi cha kushindwa hata kutoa fedha za kusafisha uwanja pamoja na kuvuta vyoo au kurekebisha hali iliyopo vyooni ili kuepeuka uchafu unaokuwepo uwanjani?

Tunatia aibu kwa jambo hili na pia tunahatarisha afya za mashabiki wanaoingia uwanjani kuangalia mechi.


SPORTS EXTRA YA CLOUDS FM YAMPATIA MZEE ATHUMAN KILAMBO SHILINGI LAKI TANO - NA HIVI NDIO HALI YAKE ILIVYO SASA

Kipindi bora cha michezo nchini Tanzania kutoka kwenye super brand radio station, Sports Extra jana kilionyeshwa kuguswa na hali ya kiafya aliyonayo gwiji wa soka nchini aliyewahi kuipa mafanikio makubwa klabu ya Pan Africa, Mzee Athuman Kilambo.

Kama ambavyo mtandao huu ulivyowahi kuripoti kuwa muanzilishi huyo wa klabu kongwe ya Pan African amekuwa akiugua ugonjwa wa kansa ya koo na alikuwa akihitaji msaada wa matibabu, jana mchana mwakilishi wa Sports Extra Shaffih Dauda alienda kumtembelea Mzee Kilambo nyumbani kwake na kumpatia kiasi cha pesa cha shilingi laki 5 ili ziweze kumsaidia kujitibu.

Kiukweli hali ya Mzee wetu imezidi kuwa mbaya na anakosa msaada wa kutosha ili aweze kujitibia ugonjwa huo ambao umedhoofisha kabisa afya yake.

Wanamichezo tuungane kumsaidia huyu Mzee wetu ili aweze kutibiwa kwani anahitaji fedha nyingi ili aweze kufanyiwa upasuaji na matibabu mengine. Viongozi wa soka, wapenzi, wanasoka na mashabiki wa mchezo huu, huu ndio wakati kuonesha umoja kama waliona wacheza filamu kama walivyoonesha wakati mwenzao Sajuki anaumwa.

Athumani Kilambo, ameifanyia makubwa taifa letu na soka letu, amefanya mambo mengi makubwa ambayo nikiyataja sitoweza kuyamaliza leo, kwa ufupi Watanzania huu ni Muda wa kurudisha fadhila, huu ni muda wa wanamichezo kuonesha uwanamichezo wetu. 

Shirikisho la soka nchini na wanachama wake mna fursa za kuandaa japo mechi kwa ajili ya kuweza kupata mapato yatakayoweza kwenda kumsaidia huyu mzee, tusisubiri mtu afariki (siombei) ndio tuanze kujionesha kwamba tulikuwa tunamjali.  

Tumsaidie mwenzetu wanamichezo.  

Thursday, February 7, 2013

Bia ya Tusker Lite yatikisa jiji la Dar Es Salaam

 Kampuni ya bia ya Serengeti imezidi kukonga nyoyo za wapenzi wa bia jijini Dar Es Salaam  kupitia kinywaji  chake cha Tusker Lite . Kinywaji hicho cha ukweli  kilizinduliwa  mwezi Novemba mwaka jana . Tusker Lite ina wanga kidogo  na ladha halisi  ya kuburudisha. Kwa mujibu wa matukio yanayoendelea  katika baa mbalimbali jijini,  wapenzi wa bia wamepata fursa ya kuzungumza na mabalozi wa kinywaji hicho na  kukiri  kuwa Tusker Lite ina ladha murua na kukubali kuwa Tusker Lite ni Lite ya ukweli .

KILIMANJAR​O LAGER YARIDHISHW​A NA KIWANGO CHA STARS

· Yatoa pongezi kwa kuicharaza Cameroon
· Yataka mechi zaidi za kirafiki


Wadhamini wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium lager, wamesema wanarishishwa na kiwango cha timu hiyo kwa sasa hku wakiomba TFF iandae mechi nyingi za Staridi za kirafiki hapa nyumbani. Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe siku moja baada ya Stars kuicharaza Cameroon bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa katika Uwanja wa Taimu hiiifa Jijini Dar es Salaam.

“Kwa kweli tunafurahishwa na mafanikio ya timu hii tangu tuchukue udhamini mwezi Mei mwaka jana….tumeiangalia ikicheza ndani na nje na kwa kweli kikosi ni kizuri kwani kimewaletea watanzania ushindi,” alisema.

Aliwapongeza watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao kama kauli mbiu ya KIlimanajro Premium Lager inavyosema…”Sherekea kilicho chetu.
“Hawa walikuwa wanajulikana kama Simba wa Afrika lakini wameondoka wakiwa wamenyong’onyea baada ya kufungwa 1-0,” alisema.

Bw Kavishe alisema ushindi huu wa Stars umewapa nafasi nzuri ya kuendelea kuidhamini Taifa Stars ili kuwapa watanzania nafasi ya kusherekea kilicho chao kwa kupitia burudani ya mpira.“Dhidi watanzania wanavyozidi kutuunga mkono kwa kunywa bia yetu ya Kilimanajro Premium Lager ndio sisi tunazidi kupata fedha za kuidhamini timu na kuendelea kuwapa burudani ya mpira,” alisema Kavishe.

Alisisitiza kuwa TFF inatakiwa kuandaa mechi nyingi za kirafiki hapa nyumbani  ili watanzania wazidi kuiona timu yao ikicheza.
Huu ni ushindi mnono wa pili mfululizo kwa timu ya Taifa baada ya kuichapa Zambia 1-0 Disemba mwaka jana.

Kilimanjaro Premium Lager imetoa udhamini wa zaidi ya Shilingi Bilioni 10 kwa miaka mitano. Huu ndio udhamini mkubwa kabisa wa mpira ambao umewahi kutokea Tanzania

TAARIFA KUTOKA TFF:MAWAKILI RUKSA RUFANI ZA UCHAGUZI TFF

WAOMBAJI uongozi kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliokata rufani kupinga kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho wanaruhusiwa kuwa na uwakilishi wa kisheria (legal representation) wakati wa kusikilizwa rufani zao.

Uamuzi wa kuruhusu mawakili kwenye usikilizaji wa rufani hizo mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Idd Mtiginjola ni kuhakikisha kila upande unapata haki.

Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambayo ndiyo iliyosaili waombaji uongozi, hivyo kuwa mlalamikiwa katika rufani hizo, nayo inaruhusiwa kuwa na Wakili wakati wa usikilizaji wa rufani hizo.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua waombaji kumi na mbili wa uongozi kwenye nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kutokidhi matakwa ya kikatiba. Uchaguzi wa TPL Board utafanyika Februari 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Waombaji hao waliochujwa ni Omari Mussa Nkwarulo aliyeomba kuwania urais na Michael Richard Wambura aliyejitosa katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Makamu wa Rais.

Wengine waliochujwa wakiomba kugombea nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Hussein Musa, Mbasha Matutu, Charles Mugondo, Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja, Eliud Peter Mvella, Farid Nahdi, Omari Isack Abdulkadir na Shafii Kajuna Dauda.

Kwa upande wa uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu aliyechujwa ni Christopher Peter Lunkombe aliyekuwa akiomba nafasi ya ujumbe katika Kamati ya Uendeshaji.

Mwisho wa kukata rufani kwa waombaji uongozi walioenguliwa na wale walioweka pingamizi kwa wagombea na zikatupwa ni leo (Februari 7 mwaka huu) saa 10 kamili jioni.
                     
MECHI YA STARS, CAMEROON YAINGIZA MIL 148/-
Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Cameroon (Indomitable Lions) lililochezwa jana (Februari 6 mwaka huu) na wenyeji Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 limeingiza sh. 148,144,000.

Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 23,092 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 22,598,237.29, maandalizi ya mchezo sh. 58,000,000 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,340,900.

Nyingine ni bonasi kwa wachezaji wa Taifa Stars sh. 18,831,864.41, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 8,274,659.66, asilimia 15 ya uwanja sh. 6,205,994.75 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 2,068,664.92.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,823,978.98 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,241,199 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

EXCLUSIVE: NIYONZIMA KAMA YANGA ISIPOTWAA UBINGWA WA LIGI MSIMU NITAONDOKA


KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amefunguka na kusema kama Yanga itashindwa kutwaa taji la ligi msimu huu ataachana na timu hiyo.
Mnyarwanda huyo alisema jijini Dar es Salaam kuwa alijiwekea malengo yake kabla ya kutua ya Yanga, hivyo kama atashindwa kuyatimiza ataondoka na kutafuta maisha katika klabu nyingine nje ya nchi.
"Kuna malengo ambayo nilijiwekea kabla ya kuja Yanga. Nikuhakikisha tunashinda kila Kombe ambalo tunashiriki."
Alisema anaweza kujivunia kutwaa Kombe la Kagame mwaka jana na Yanga, lakini kwa sasa anafikiri ni wakati mwafaka kwake kubeba taji la Ligi Kuu Bara na kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
"Nafikiri kwa sasa tuna timu inayoundwa na wachezaji wazuri na wenye vipaji vikubwa vya soka." alisema Niyonzima.
Aliongeza; "Kama itatokea Yanga imeshindwa kufanya hivyo nitatafuta timu nyingine nje ya nchi kuichezea."
Hata hivyo, Yanga inaweza kumbana nyota huyo kutokana na mkataba wake kumalizika mwaka 2015.

OFFICIAL: SUNZU KUIKOSA MECHI YA SIMBA NA JKT OLJORO

UONGOZI wa Klabu ya Simba umethibitisha  kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Felix Sunzu hatokuwamo kwenye msafara wa timu hiyo utakaoelekea Arusha kesho kwa ajili mechi ya ligi dhidi ya JKT Oljoro.
Akizungumza jijini Dar es Salaam msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alimesema kuwa Sunzu ameondolewa katika kikosi  kitakachoivaa JKT Oljoro kutokana na kuwa majeruhi.
"Kama tulivyopanga awali kikosi chetu  kitaondoka kesho kuelekea Arusha kikiwa na wachezaji 20.
"Mpaka wakati huu mchezaji ambaye ninaweza kukuthibitishia kwamba hatokuwa miongoni mwa wale watakaosafiri ni Felix Sunzu ambaye bado anasumbuliwa na majeraha,".alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema kuwa, orodha kamili ya wachezaji 20 watakaosafiri kuelekea Arusha ilitarajiwa kutangazwa mapema baada ya kumalizika kwa pambano kati ya Timu ya Taifa(Taifa Stars) na Cameroon leo jioni.
"Nani na nani watakuwamo katika kikosi kitakachosafiri itajulikana leo jionibaada ya mechi kati ya Taifa Stars na Cameroon kama unavyojua tuna wachezaji kwenye timu ya Taifa. Hatuwezi kujua kuna nini kitatokea baada ya mchezo,".alisema Kamwaga.
Pambano baina ya Simba na JKT  litapigwa Jumamosi hii kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Katika pambano la mzunguko wa kwanza  lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Wekundu wa Msimbazi, Simba ilichomoza na ushindi wa mabao 4-1
........

EDWARD CHRISTOPHER: NAREJEA DIMBANI HIVI KARIBUNI KUISADIA SIMBA KUTETEA UBINGWA


Mshambuliaji chipukizi wa timu ya taifa na klabu ya soka ya Simba ambaye ni majeruhi kwa takribani, mwezi mmoja sasa, Edward Christopher, amesema anaendelea vizuri japo bado anasikia maumivu kwa mbali. 

Edo ambaye aliumia akiwa katika michuano ya Mapinduzi huko Visiwani Zanzibar mwanzoni mwa mwezi uliopita, alisema hayo mapema siku ya leo wakati akizungumza na tovuti hii. 
"Ninaendelea vizuri, lakini bado ninasihisi maumivu katika mguu wangu" anasema mshambuliaji huyo anayesubiliwa kwa hamu na mashabiki wa klabu yake ambayo inahaha kutetea ubingwa wake wa ligi kuu ya Vodacom.

" Mashabiki wawe na uvumilivu kwani muda si mrefu nitarejea uwanjani" anaongeza kusema kinda huyo ambaye wengi wanataraji ataziba pengo la mshambuliaji, Mganda, Emmanuel Okwi ambaye ameuzwa katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia, mwezi uliopita. Edo alitwaa tuzo ya ufungaji bora wa michuano ya Super8, agosti mwaka jana.

SIMBA YAMRUHUSU OBADIA MANGUSA KUKIPIGA AFRICAN LYON


Baada ya kusota kwa muda mrefu hatimaye mlinzi, Obadia Mungusa atakuwa huru kuitumikia timu ya African Lyon hadi mwishoni mwa msimu huu.

 Simba iliiandikia barua timu ya Lyon siku ya jana na kutoa ruhusa kuwa sasa wanaweza kumtumia mlinzi huyo aliyekosa nafasi klabuni, Simba walau hadi mwisho wa msimu huu. " Jana nilipigiwa simu na uongozi wa Lyon kuwa Simba imeniruhusu kuichezea timu yao hadi mwishoni mwa msimu kwa mkopo" anathibitisha, Mungusa wakati akiongea na tovuti hii asubuhi ya leo. Obadia ambaye alitibuana na makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Geofrey Nyange Kaburu kuelekea mwishoni mwa mzunguko wa kwanza kwa sababu za kimaslai na kuamua kujiondoa klabuni hapo baada ya kupeleka madai ya mshahara wake na pesa za usajili ambazo aliahidiwa kupewa wakati akijiunga na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu akitokea Mtibwa Sugar miaka miwili iliyopita. 

Ameondoka Simba huku akidai mshahara wa miezi mitano.  "Nimeondoka ili kunusuru kipaji changu, japo bado nawadai mshahara wa miezi mitano" anasema

HIVI NDIVYO TAIFA STARS ILIVYOWANYOOSHA WACAMEROON UWANJA WA TAIFA

Wachezaji wa Stars - Mbwana Samatta, Chuji, Kaseja na Mwinyi Kazimoto wakipongezana baada ya ushindi dhidi ya Cameroon.

Juma Kaseja akimpa pongezi Samatta baada ya mechi


Mrisho Ngassa vs Assou Ekotto - Mtu aliwekwa mfukoni leo

Samagoal na Assou Ekotto shughuli nyingine ilikuwa leo

Mrisho Ngassa vs Assou Ekotto shughuli ilikuwa pevu leo kwa Ngassa

Mchezaji wa Cameroon akitolewa nje ya uwanja kutibiwa baada ya kupata maumivu

Amri Kiemba langoni mwa Cameroon 


Mshikemshike wa Samatta na beki wa Tottenham Hotspur Assou Ekotto

Wachezaji wa Stars wakishangilia goli lao

Frank Domayo alipiga mpira mwingi sana 

Wednesday, February 6, 2013

BIASHARA YA KUUZA WATU SASA YAVAMIA SOKA

 NA. ALBERT G. SENGO: MWANZA
Biashara ya kusafirisha bianadamu ambayo kwa hapa nchini imekuwa ikionekana kutajwa kufanyika kwa baadhi ya wahamiaji haramu kutoka nje kupewa hifadhi na wazawa kwa njia za magendo pamoja na ile ya nchi kutumika kama njia ya wahamiaji kupitishwa kuelekea nchi za kusini mwa Afrika, sasa biashara hiyo imehamia kwa vipaji vya soka nchini Tanzania kutoroshwa kwenda nchi jirani.

Jijini Mwanza Mchezaji mahiri wa zamani wa timu za Pamba Fc na Kagera ambaye pia alikuwa kocha wa kituo cha timu ya vijana wadogo ya Alliance Academy ya jijini humo Furgance Novatus ametiwa mbaroni kwa kuhusishwa na tuhuma za kuuza vijana watatu nchini Uganda kwa thamani ya Shilingi milioni 60 za kitanzania...
Bofya play sikiliza zaidi kisa hicho...
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Atanas Mdaula alisema kuwa waliuzwa kwa kiasi cha shilingi milioni 60 na wakati wakisafirishwa walibadilishiwa majina yao katika hati zao za kusafiria kwa nia ya kuficha ukweli, na hapa alikuwa akionyesha kikaratasi elekezi alichopewa na kocha wake Furgaency Novatus ili kuweza kujibu maswali yote safarini.

Calvin Richard (16) alisema kuwa hati yake ya kusafiria ilionyesha kuwa anaitwa Mohamed Hassan Said, huku Atanas Mdaula akibadilishiwa jina na kuitwa Majid Said Maneno na Abdalah Juma akibadilishiwa jina na kuitwa Abdulatif Mohamed.

Hati ya kusafiria ilionyesha kuwa anaitwa Abdulatif Mohamed badala ya Abdalah Juma 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa,Mkurugenzi wa shule ya Alliance Academy James Bwire (pichani) alisema kuwa timu yake ya wachezaji chini ya miaka 15 ilialikwa kwa ajili ya kushiliki michuano ya soka nchini Uganda na kufanikiwa kutwa ubingwa hivi karibuni.

Bwire alisema kuwa baada ya kumalizika kwa michuano hiyo viongozi kadhaa wa soka nchini Uganda pamoja na Waziri wa michezo wan chi hiyo walivutiwa na uwezo wa wachezaji wake watatu ambao ni golikipa Calvin Richard(16), mshambuliaji Athanas Mdaulu(16) pamoja na mchezaji wa kiungo Abdallah Juma(15) na kuuomba uongozi kuwaruhusu kubaki nchini Uganda kwa ajili ya kuchezea katika timu za watoto za nchi hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa alikataa maombi ya waganda hao na kuwaeleza kuwa alikuwa nchini humo kwa ajili ya kushiliki michuano ya soka na sio kuwauza wachezaji na kuwataka viongozi hao kama kweli wana nia hiyo kuwasiliana na wazazi wa wachezaji hao.

Lakini hatimaye Waganda hao walifanikiwa kuchukuwa mawasiliano ya kocha Fulgence Novatus aliyeingia 'kingi' na kucheza mchezo huo mchafu.