Iliwahi kutabiriwa miezi kadhaa iliyopita kwamba mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi angeifikia rekodi ya mjerumani Gerd Muller aliyoiweka mwaka 1972 kwa kufunga mabao 85 katika mwaka mmoja.

Wakati kijana huyo mfupi alipofanikiwa kuifikia na kuivunja rekodi, kwa kufunga mabao 86 tarehe 9 Disemba mwaka huu, jamii ya soka iliachwa mdomo wazi kwa rekodi hii.

Sasa kwa takribani siku nne zilizopita kumekuwepo na maswali kadhaa yanayoizunguka rekodi hii ya ufungaji wa mabao mengi ndani ya mwaka mmoja.

Kwanza walikuwa chama cha soka cha Zambia ambacho kilisema kwamba gwiji wa soka wa nchi hiyo Godfrey Chitalu alifunga mabao 107 ndani ya kipindi cha mwaka 1972, rekodi ambayo imeifunika ile ya Messi.

Then, wakafuatia klabu ya Flamengo ya Brazil ambao walikuja wakasema kwamba mshambuliaji Zico alifunga mabao 89 katika kipindi chote cha mwaka 1979, namba ambayo ni zaidi ya rekodi ya Messi 9ingawa Messi anaweza kupita rekodi hiyo)

Hatimaye, wa mwisho ni hii rekodi mpya anayotajwa kuwa Pele alifunga mabao 127 mwaka 1959, rekodi ambayo inasapotiwa na FIFA katika wasifu kumhusu gwiji huyo wa soka wa Brazil.

Lakini pamoja na takwimu zote hizo, FIFA ambayo ndio taasisi kuu inayosimamia soka, imezungumzia suala hilo siku ya ijumaa: kwa kifupi hawazitambui rekodi za ufungaji za wakali hao.

Katika mahojiano na BBC Sport, msemaji wa FIFA Alex Stone alisema:
Hizi sio rekodi rasmi za FIFA.
Hatuna database ambayo inaweka rekodi zote za mchezo wa soka unaochezwa katika kila nchi dunaini kote kwa siku zote.
Hii haihusiani kabisa na kupendelea mtu -  ikiwa tutaweza kuthibitisha kutoka kwenye michuano yetu tungependa kufanya hivyo.
Hizi ni data ambazo mashabiki na media wanapenda kuziona.
Ni rekodi ambayo mtu fulani kwenye vyombo vya habari alikusanya takwimu kutoka mahala fulani na kusema kwamba Messi amekaribia kuivunja rekodi hiyo.

Kiujumla, rekodi ambayo Messi aliivunja haikuwa rasmi kwa maana ya kutotambuliwa na FIFA. Hivyo sio Messi wala Chitalu, wala Zico wala Pele atakuwa akitambuliwa kama mtu anayeshikilia rekodi hiyo ya ufungaji wa magoli mengi katika mwaka mmoja.

JE WADAU MNA MAONI GANI KUHUSU SUALA HILI.