Search This Blog

Saturday, October 6, 2012

REFA ALIYECHEZESHA MECHI YA YANGA NA SIMBA AONDOLEWA LIGI KUU

Kamati ya Ligi imewaondoa waamuzi watatu wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa kushindwa kumudu michezo waliyopangiwa. Waamuzi hao ni Mathew Akrama wa Mwanza aliyechezesha mechi namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba iliyochezwa Oktoba 3 mwaka huu.
 
Wengine ni Paul Soleji wa Mwanza aliyechezesha mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons, na mwamuzi msaidizi namba mbili kwenye mechi hiyo Mwarabu Mumbi wa Morogoro. Pia mwamuzi msaidizi namba mbili wa mechi ya Yanga na Simba, Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam amepewa onyo.
 
Kamishna wa mechi namba 28 kati ya Yanga na African Lyon, Pius Mashera ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi hiyo kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (Pre match meeting) na uwanjani.
 
Vilevile Mashera kwenye ripoti yake aliwasilisha malalamiko dhidi ya msimamizi wa kituo cha Dar es Salaam, na kwa vile suala hilo ni la kinidhamu ametakiwa alipeleke kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
 
Nayo Simba imepigwa faini ya jumla ya sh. 600,000 kwa kuchelewa kufika kwenye pre match meeting ya mchezo wao dhidi Tanzania Prisons (sh. 100,000) na kwa washabiki wake kuwatupia chupa za maji waamuzi wa mechi hiyo (500,000).
 
Pia Kamati ya Ligi imeagiza kuwa kwa vile suala la kipa Shabani Kado wa Mtibwa Sugar kudaiwa kumpiga kiongozi mmoja wa Ruvu Shooting mara baada ya mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex ni la kinidhamu lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
 
YANGA, AFRICAN LYON KUTOVAA BEJI YA MDHAMINI
Kwa vile msimu huu mdhamini mwenyewe ndiye anayegawa vifaa kwa timu, Kamati ya Ligi imeagiza Vodacom iandikiwe barua na nakala kwa klabu zote ili kujua timu ambazo tayari zimekabidhiwa vifaa hivyo zikiwemo logo na siku ambapo timu husika zilipokea.
 
Baada ya majibu ya Vodacom ndipo Kanuni za Ligi Kuu zitakapotumika kutoka adhabu kwa timu ambazo zitabainika kuwa zilipokea vifaa lakini hazikuvitumia.

MTOTO WA MIAKA 6 ALIYECHANGIA KUFANYIKA KWA USAJILI WA WAYNE ROONEY MAN UNITED

Mtoto huyu wa miaka 6 aliwahi kuingia Old Trafford na Bango lake na baada ya mechi kuisha alibaki uwanjani peke yake hadi akaja kutolewa na security.

Siku iliyofuata alienda uwanja wa mazoezi na Bango lake hadi kwa Sir Alex na kumwambia
"Rooney will help us please Buy him" - (Rooney atatusaidia tafadhali mnunue)
Kweli baada ya muda fulani Sir Alex Ferguson alivunja benki na kumsaini Wayne Rooney - na yule kijana akawepo siku Wayne anatambulishwa pale Old Trafford.

Credits: Story na picha kwa niaba ya page ya Manchester United Supporters in Tanzania on Facebook

Friday, October 5, 2012

BREAKING NEW: RICK ROSS ATUA JIJINI DAR ES SALAAM USIKU HUU

 Meneja wa Bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Allan Chonjo akisalimiana na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Rick Ross mara baada ya kuwasili usiku huu ndani ya uwanija wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,akiwa na baadhi ya wanamuziki wenzake pichani nyuma,kati ni Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd,Balozi Kindamba ambao ndio waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalotarajiwa kufanyika hapo kesho.Picha nyingine baadae kidoogo wadau. 
 Rick Ross akitoa salamu ya salut kwa washabiki wake waliojitokeza usiku huu (hawapo pichani) kumlaki
 Operesheni Meneja wa Prime Time Promotions,Balozi Kindamba akiwaongoza wageni wake kuelekea kwenye gari tayari kuondoka kuolekea kwenye hoteli waliopangiwa kufikia usiku huu,Shoto ni Rick Ross na akiwa na baadhi wanamuziki wenzake aliombatana nao .
 Rick Ross akiingia ndani ya mchuma.
Rick Ross akiondoka na mchuma wake kuelekea hotelini usiku huu.
Mmoja wa mashabiki wa Rick Ross aliyezua tafrani kiaina akijifananisha na Rick Ross akizungumza na na baadhi ya watu waliojitokeza kumlaki The Big Boss mwenye Rick Ross.

RICK ROSS THE BOSS KASHATUA KWENYE ARDHI YA JAKAYA - BHAAAAAAAAAAASI



Muda mchache uliopita mwanamuziki wa kimataifa wa Marekani Rick Ross ambaye kesho ataivuruga Dar es Salaam katika show kali ya tamasha bora kabisa la Fiesta, ameandika kupitia akaunti ya Twitter kwamba ameshatua Bongo.

SUNDAY OLISEH: MWISHO WA FERGUSON MAN UNITED - NA WANAOWEZA KUMRITHI



Hakuna anayeishi milele. Kifupi hakuna kinachodumu milele. Fomu ya sasa au upungufu wa ubora wa kiwango kilichoonyeshwa hivi karibuni na Manchester United kwa mawazo ni dalili zinazoonyesha kwamba kuna vitu kadhaa vimefikia mwisho ndani ya Manchester United. Mojawapo ya vitu hivyo ni utawala wa Sir Alex Ferguson.

Kuna uwezekano kwamba kunaweza kukatokea mabadiliko ya utawala katika jiji la Manchester. Kwanza ni kutwaa ubingwa wa ligi kwa Manchster City msimu uliopita, walimaliza utani wa kuitwa "Majirani wenye kelel" kwa United kama ambavyo  Sir Alex Ferguson alivyokuwa akiwaita na kwa maoni yangu  naona huu ndio mwanzo wa mabadiliko yasiyozuilika. Kustaafu kwa Sir Alex Ferguson!

Alizaliwa 31 December 1941 - Ferguson ni mmoja wa makocha mwenye mafanikio makubwa katika historia ya mchezo huu wa soka. Amekuwepo Old Trafford tangu mwaka 1986, miaka 26 iliyopita!

Kwa kipindi chote hiki ameshinda makombe 37, kati ya hayo 12 ni makombe ya ligi kuu ya England. Maisha yake ya ukocha yalianza tangu mwaka 1976.

Kutoka wakati huo amekusanya makombe jumla 48 na ameshinda tuzo binafsi zipatazo 64 kama yeye binafsi na kama kocha. Japokuwa, unapoangalia mambo yanavyoenda pale United, kuna dalili nyingi kwamba ameanza kupoteza makali yake kama kocha na katika kuilinda heshima kubwa aliyojiwekea na mafanikio aliyoyapata, itakuwa vizuri sana kama msimu huu utakuwa wa mwisho kwake katika kufundisha soka.

KWANINI NAFIKIRI KUFANYA HIVYO KUTAKUWA NI SAHIHI

Timu ya United inazeeka na Ferguson ameendelea kuwatumia wachezaji wake wazee katika moyo wa timu, kitu ambacho mara kadhaa kimekuwa kinawagharimu points United. (Ryan Giggs, Rio Ferdinand, na hata muda mwingine Paul Scholes)

Najiuliza ni vipi Ferguson anawafanya chipukizi wenye vipaji wajisikie, kwa kukaa nje kwenye benchi kuwapisha wachezaji wazee ambao kwa mara kadhaa tumeona wakiigharimu timu. Kiukweli hili linaondoa balance kwenye timu!.

Usinifikirie vibaya, Rio, Giggs na Scholes ni magwiji walioifanyia makubwa sana timu yao, lakini kuna sababu muhimu sana inayosema kwamba muda mzuri na sahihi kustaafu soka katika ligi ya ushindani kama England ni miaka 33!

Paul Scholes bado ni mpiga pasi bora kabisa duniani, Giggs bado na ufundi wake katika kuisadia timu kwa kasi yake na ujuzi wa kuuchezea mpira na Ferdinand ambaye sasa mara kadhaa amejikuta akiwa hana kasi lakini bado ni mlinzi mzuri lakini mashabiki wa Manchester na klabu yenyewe inastahili wachezaji 11 kwa muda wote bila kuwa na matatizo ya hawa wazee.

Kwa miaka mingi United ilikuwa klabu tajiri zaidi duniani na chaguo la kwanza la wachezaji wengi, lakini sasa kwa uvamizi huu wa waarabu na warusi na fedha zao za mauzo ya nishati, wachezaji kadhaa siku za hivi karibuni wamekuwa wakizichagua City au Chelsea mbele Manchester United.
Hata kuna wakati mchezaji kipenzi wa timu hii Wayne Rooney alitaka kuhama United kwa ajili ya kwenda timu zenye uwezo wa kununua wachezaji wazuri na wenye majina!

United walipata mafanikio yao makubwa katika timu za miaka nyuma kutokana na nidhamu, umakini, mchanganyiko wa damu changa na wachezaji wakubwa ambao bado ni bora duniani waliounda timu nzuri ya ushindani. Sifa hizi zinakosekana kwenye United ya sasa na unapoangalia soka lao sasa utaliona hilo. Mfano mzuri ni soka bovu kuliko niliyoiwahi kuishuhudia United wakicheza hivi karibuni, katika mechi dhidi ya Tottenham kwenye kipindi cha kwanza, mechi ambayo mwishoni iliisha kwa vijana wa Sir Alex wakifunga na Spurs kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 23.


Mwisho wa Ferguson kwa mfano akaamua kustaafu mwishoni mwa msimu, je nani atakuwa mrithi wake.

WABADALA WANAOWEZA KUMRITHI Ni mtihani mgumu sana ambao bodi ya wakurugenzi wa Manchester United wanabidi kuutafutia majibu yake. Unaanzaje kumbadili kocha kama Sir Alex Ferguson? Lakini wapo baadhi ya vijana ambao wanatajwa kuweza kurithi nafasi ya Fergie. 

JOSE MOURINHO : The ‘Special One’ siku zote amekuwa akiweka wazi anatamani kurudi katika ligi kuu ya England na tetesi zinasema anapewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa Sir Alex, ingawa bado yupo kwenye mkataba na Real Madrid. Ana uwezo mkubwa wa kuongoza ambayo klabu inahitaji, lakini wasiwasi wangu pekee kwake ni  tabia yake ya kupenda kuvuta attention kutoka kwa vyombo vya habari inaweza isivumiliwe na United, lakini staili yake ya kufundisha soka la kujilinda na kucheza vizuri huku wakitaka ushindi linawafaa United.

JOSEP GUARDIOLA: Huyu kocha akiwa na Barcelona katika miaka 3 alishinda nusu ya makombe aliyoshinda Sir Alex Ferguson katika miaka 36. Sio muongeaji sana lakini ni mkali kiasi, kijana, ana nidhamu na staili yake ya kufundisha ni kumuliki mpira na kucheza soka zuri, akisisitiza kushambulia ndio njia sahihi ya kuzuia na kupata ushindi

Kitabia namuaona ndio mtu sahihi kwa Manchester United ikiwa Sir Alex Ferguson ataamua kustaafu.

KIZUIZI KINACHOWEZEKANA? Kutokujua vizuri lugha ya kiingereza. Naamini tutamuona akifundisha soka Uingereza muda mfupi ujao na ndio maana kwa sasa anaishi na familia yake jijini New York. Ni wapi sehemu nzuri unaweza kujiandaa kufundisha soka England kwa kujifunza lugha ya kiingereza kwa uwepesi zaidi ya Amerika?
Kwa Sir Alex Ferguson, naamini maisha yake baada ya United yatakuwa magumu, kwa mtu ambaye ambavyo alivyo mweledi na anayeipenda klabu ambayo amekaa nayo karibia nusu ya maisha yake, kuiacha nafasi yake ni ngumu, lakini gwiji huyu kama anataka kuondoka kwa heshima na kwa amani na furaha katika klabu ya Manchester United, naamini mwisho mwa msimu huu achukue maamuzi magumu na kuiacha United kwenye mikono ya kocha mwngine. 

Heshima kwa Sir Alex Ferguson
 *********************************************************************************
Makala hii ameandika kiungo wa zamani wa Nigeria Sunday Oliseh - akisisitza ni muda sasa Ferguson akaachia ngazi Old Trafford. Je wewe msomaji wa mtandao hu una Maoni gani? Unadhani yupo sahihi. 

MAMBO YANAVYOZIDI KUPAMBA MOTO LEADERS KUELEKEA FIESTA KESHO























YANGA KUKIPIGA NA SERENGETI BOYS KESHO KARUME

SERENGETI BOYS KUVUNJA KAMBI KWA MECHI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) ambayo imepata tiketi ya kucheza raundi ya tatu ya michuano ya Afrika baada ya Misri kujitoa itavunja kambi yake kwa mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi cha Yanga cha U20.
 
Mechi hiyo itachezwa kesho (Oktoba 6 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni. Kiingilio kwenye mechi hiyo kitakuwa sh. 2,000 tu.
 
MCHAKATO WA CHAGUZI MBALIMBALI ZA MIKOA
1.           Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika kikao chake kilichofanyika tarehe 03-04 Oktoba 2012 ilijadili michakato ya chaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa ya Rukwa (RUREFA), Arusha (ARFA), Shinyanga (SHIREFA), Pwani (COREFA), Dar es Salaam (DRFA) na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT). Kamati iliamua yafuatayo:
 
(a)        Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha (ARFA)
Uchaguzi wa ARFA utafanyika  Jumapili, tarehe 07 Oktoba  2012 mjini Arusha kama ulivyopangwa.
 
(b)        Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT)
Uchaguzi wa FRAT utafanyika Jumapili, tarehe 07 Oktoba 2012 mjini Dodoma kama ulivyopangwa.
 
(c)        Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA)
Uchaguzi wa COREFA utafanyika  Jumapili, tarehe 14 Oktoba  2012 Wilayani Mafia kama ulivyopangwa.
 
(d)        Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA)
Kamati ilibaini na kujiridhisha kuwa kulikuwa na udanganyifu uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya RUREFA katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba hususan, uteuzi wa baadhi ya  wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA. Pamoja udanganyifu huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imejiridhisha kuwa Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA imeshindwa kutimiza wajibu wake katika kusimamia uchaguzi wa RUREFA, hata baada ya kuwa imepewa onyo kuzingatia matakwa ya Kanuni za Uchaguzi.
 
Kutokana na udanganyifu uliofanyika katika uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 26(2) na (3) na Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), imeamua yafuatayo:
 
(i)  Imeifuta Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA. TFF itateua Kamati mpya ya Uchaguzi ya RUREFA itakayoandaa na kusimamia uchaguzi wa RUREFA.
 
(ii)Uteuzi wa Kamati mpya ya Uchaguzi ya RUREFA utafanyika wakati muafaka baada ya TFF kukamilisha taratibu za uteuzi, na ratiba ya uchaguzi ya RUREFA itatangazwa baada ya zoezi hilo.
 
 
 
 
 
 
 
(e)        Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA)
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ya SHIREFA wanaingilia mchakato wa uchaguzi wa SHIREFA kinyume na matakwa ya Kanuni za Uchaguzi  za wanachama wa TFF. TFF haitambui maamuzi ya uongozi wa SHIREFA wa kuivunja Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA inayosimamia uchaguzi wa Chama hicho. Zoezi la uchaguzi wa SHIREFA lililoanza tarehe 08 Septemba 2012 linaendelea na uchaguzi wa viongozi wa SHIREFA utafanyika tarehe 20 Oktoba 2012 kama ulivyopangwa.
 
 
(f)         Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA)
Kamati ya Uchaguzi ya TFF itakamilisha zoezi la kusikiliza rufaa zilizokatwa dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na kupitia mchakato mzima  wa uchaguzi wa DRFA, ili kujiridhisha kama matakwa ya Katiba ya DRFA na TFF yamezingatiwa. Kamati ya Uchaguzi itatoa uamuzi kuhusu rufaa zilizowasilishwa kwenye Kamati kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na kuhusu mchakato wa uchaguzi wa DRFA baada ya kikao chake kitakachofanyika Jumanne, tarehe 09 Oktoba 2012.
 
2.           Kuzingatia Kanuni za Uchaguzi:
 
(i)  Kamati ya Uchaguzi ya TFF itaishauri Mamlaka husika ya TFF kuwachukulia hatua za kinidhamu viongozi wa Kamati za Utendaji walioko madarakani wanaoingilia michakato ya chaguzi za wanachama wa TFF na kusababisha mikanganyiko katika chaguzi ili ama wandelee kuwa madarakani kinyume na matakwa ya Katiba ya TFF Ibara ya 12(2)(a) au wapitishwe kugombea uongozi kinyume na taratibu zilizowekwa na TFF.
 
(ii)Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza na kuzitaka Kamati za Uchaguzi za vyama wanachama wa TFF kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF wakati wote wa michakato ya uchaguzi wa viongozi wa vyama hivyo.
 
 

MAONI YA MDAU JUU YA MAPATO YA MECHI YA SIMBA NA YANGA

1. Juzi nilikuweka kwenye uzi nikikuomba usaidie kuibua hoja ya timu zetu kubwa kuwasajili na kuwatumia wachezaji wa ndani, badala ya wachezaji wa nje ambao kimsingi wana umri mkubwa na hawana value wanayo-add kwenye timu zao husika.
Mfano ni te likes of Kago, Ochieng etc

2. Jana tena, kumeibuka kiroja. Mapato ya Simba ya Yanga kuwa 390m tu. Ni kiroja kwa kuwa, kwa mujibu wa matangazo ya Supersport, mashabiki walioingia ni 59,000. Sina haja ya ku-validate idadi hii, maana kule orange straight nilipokaa, mashabiki walikuwa wamejazana hadi kubebana na kukaa kwenye njia za kuingilia.

Embu tufanye scenario zifuatazo kwa kuzingatia viwango vya viingilio:
- 59, 000 x 30, 000 = 1, 770, 000
- 59, 000 x 20, 000 = 1, 180, 000
- 59, 000 x 15, 000 = 885, 000, 000
- 59, 000 x 10, 000 = 590, 000,000
- 59, 000 x 7, 000 = 413, 000, 000
- 59, 000 x 5, 000. = 295, 000, 000

Hapa mtaona kwamba, tukifanya average (mliosoma hesabu na uhasibu ndo mahali penu hapa), basi walau kiingilio cha 10,000 ndo muafaka ya kuchukuliwa kama waliingia watu wote, mtaona kuwa mapato yalitakiwa yawe, walau 500, 000, 000.

Shaffih, mna deni kubwa sana kwa watanzania katika kuwaeleza, kuwafahamisha na kuwasaidia watanzania ili waepukane na taabu na masumbufu haya wanayoyapata.

SERENGETI YAFUZU KUCHEZA RAUNDI YA 3 MATAIFA YA AFRIKA KWA VIJANA

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imefuzu kucheza raundi ya tatu nay a mwisho kwenye michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Vijana baada ya Misri kujitoa.
 
Serengeti Boys ilikuwa icheze raundi ya pili dhidi ya Misri; mchezo wa kwanza ukichezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam na ule wa marudiano wiki mbili baadaye jijini Cairo.
 
Katika raundi ya kwanza Serengeti Boys inayofundishwa na Jakob Michelsen kutoka Denmark ilikuwa icheze na Kenya mwezi uliopita, lakini nchi hiyo ilijitoa katika michuano hiyo ambayo fainali zake zitachezwa Machi mwakani nchini Morocco.
 
Serengeti Boys sasa itacheza raundi ya tatu kwa kumkabili mshindi wa mechi kati ya Zimbabwe na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza itachezwa Novemba 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itafanyika ugenini wiki mbili baadaye.
 
Zimbabwe na Congo Brazzaville zitapambana zitapambana kati ya Oktoba 12-14 mwaka huu, Zimbabwe ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza wakati ya marudiano itafanyika kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu.
 
LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA SITA
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwan wa Tanzania Bara inaingia raundi ya sita wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Oktoba 6 mwaka huu) African Lyon itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
Nayo Ruvu Shooting itaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayochezeshwa na Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew Shamba.
 
Jumapili (Oktoba 7 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Oljoro JKT itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Yanga (Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba), Mgambo Shooting na Polisi Morogoro (Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga), Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza) na Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya).

Thursday, October 4, 2012

AARON RAMSEY KAMA KAWAIDA YAKE ANAPOFUNGA: JANA KATIA KAMBANI LEO WAZIRI MKUU WA SYRIA AFARIKI

*Mkosi wa Aaron Ramsey *

Kila mara mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey anapofunga goli, mtu anakufa siku inayofuata.


May 1, 2011 = Ramsey alifunga bao dhidi ya Man Utd.
OSAMA BIN LADEN akafa siku inayofuata


Oct 2, 2011 = Ramsey alifunga dhidi Spurs
STEVE JOBS muasisi na mmiliki wa kampuni ya Apple akafa siku iliyofuata.

Oct 19, 2011 = Ramsey akafunga dhidi ya Olympic Marsellie
MUNMMAR GADDAFI akafa siku iliyofauta.

Feb 11, 2012 = Ramsey akatia kambani dhidi Sunderland
WHITNEY HOUSTON akafariki siku iliyofuata.


Aug 4, 2012 = Ramsey akafunga dhidi ya South Korea
KIRK URSO akavuta siku ya pili yake.

Oct 3, 2012(Jana) = Ramsey alifunga dhidi ya Olympiakios
Waziri mkuu wa Syria amethibitishwa kuaga dunia leo hii.

GOLI LA SIKU!

RICK ROSS ATHIBITISHA YUPO NJIANI KUJA BONGO LEO



Masaa kadhaa yaliyopita msanii wa kimataifa wa Marekani Rick Ross ameandika kwenye ukurasa wake wa Twiter kwamba yupo njiani kuja nchini Tanzania ambapo atatumbuiza kwenye tamasha bora na kubwa kabisa hapa East Africa - Tamasha la Serengeti Fiesta Dar es Salaam, siku ya jumamosi.

SIMBA NA YANGA WAINGIZA MILLIONI 390 - KILA TIMU YAPATA MILLIONI 93

Pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.
 
Watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.
 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.
 
Wakati huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.
 
Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2

HAYA NDIO MAGOLI YA KIEMBA NA BAHANUZI KATKA MECHI YA SIMBA NA YANGA

KELVIN YONDANI ANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUPATA MSHTUKO WA MFUPA MKUBWA KWA RAFU YA BOBAN

Mlinzi wa kati wa kutumainiwa wa klabu ya Young Africans na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kelvin Yondani anaendelea vizuri mara baada ya kuanza kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha mifupa MOI jijini Dar es salaam.

Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz, Daktari wa timu ya Young Africans Dokta Suphian Juma, amesema Yondani alipata mshtuko katika mfupa wake mkubwa, baada ya kuchezewa vibaya na kiungo wa timu ya Simba Haruna Moshi 'Boban'.
Dr Suphian anatoa wasi wasi wapenzi na washabiki wa Young Africans, kwamba Yondani anaendelea vzuri na anatazamiwa kurudi dimbani baada ya wiki mbili. 'Unajua Yondani baada ya kukanygwa na Boban alipata mshituko katika mfupa wake mkubwa mguuni, hivyo anapata matibabu ya kumrejesha katika hali yake ya kawaida.
Katika hali ya kushangaza mwamuzi wa mchezo huo wa watani wa jadi, Mathew Akrama alishindwa kumonyesha kadi nyekundu Boban kwa mchezo mbaya uliopelekea Yondani kutolewa nje na kushidwa kuendelea na mchezo.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyowakutanisha watani wa jadi wakongwe Afrika Mashariki iliishia kwa sare ya mabao 1-1, mabao yaliyofungwa na Amri Kiemba Simba dakika ya 4 na Said Bahanunzi aliyesawazisha kwa upande wa Young Africans dakika ya 67.
Young Africans leo imeendelea na mazoezi katik uwanja wa shule ya sekeondari ya Loyola kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Kagera Sugar, mchezo utakaofanyika siku ya jumapili katika uwanja wa kaitaba mjini Bukoba. 

DAR- PACHA IMEIONYESHA DUNIA MSISIMKO WA SOKA NCHINI TANZANIA - HUKU REFA AKITIA AIBU

 






.Wachezaji walishindwa kutambua umuhimu wa mchezo huo
. Mwamuzi alikuwa zaidi ya ‘kituko’
.Kwa nini Haruna Moshi na Mwasika walimaliza mchezo?
Mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000 timu za soka za Yanga na Simba zilicheza soka la ‘aibu’ uku wakionekana kama vile wanacheza mchezo wa ‘rugby’.
Baada ya penati iliyopigwa na mshambuliaji Said Bahanuzi kuipatia Yanga bao la kusawazisha mwishoni mwa kipindi cha pili, kiujumla timu hizo ambazo zinachukuliwa kama kioo cha soka la bongo hazikuonesha soka lolote zaidi ya kucheza kibabe na kukamiana tu.
Upande wa pili mwamuzi alishindwa kuyatolea adhabu sahihi baadhi ya matukio makubwa kwenye mchezo huo, Haruna Moshi aliyeingia  dakika 20 za mwisho alistahili kuonyeshwa  kadi nyekundu, alimrukia kwa makusudi beki wa Yanga, Kelvin Yondan na ni dhahiri alitaka kumvunja. Ni aibu ambayo dunia imeishuhudia, lakini tumepata fursa nzuri ya kutangaza ‘msisimko’ uliopo katika mpira wetu kutoka kwa mashabiki.
                 HALI YA MCHEZO ILIVYOKUWA.
Simba walianza mchezo kwa kasi ambayo ilikuwa ikiongezeka kadri dakika zilivyokuwa zikisonga mbele, na dakika ya kwanza tu wakafika katika lango la kipa Yaw Berko, halikuwa shambulizi kubwa lakini lilionyesha kitu kutoka kwa timu hiyo ambayo iliwaanzisha makinda Edward Christopher, Jonas Mkude, Paul Ngalema na Shomari Kapombe katika kikosi chao cha kwanza.
Wakicheza zaidi kwa kutumia upande wa kulia kwa Nassoro Chollo, Simba iliweza kutengeneza bao la kuongoza na bao lao pekee katika mchezo huo baada ya Mwinyi Kazimoto  kupiga krosi ambayo ilimkuta kiungo, Amri Kiemba na kupiga shuti la kiufundi upande wa juu kushoto kwa kipa Berko ndani ya dakika tano Simba wakawa mbele kwa bao 1-0.
Goli La Simba
Mkude ambaye alicheza kama kiungo namba moja wa ulinzi akisaidiwa na Kiemba aliweza kuituliza timu hata pale Yanga walipotaka kupitisha mipira  mirefu, alikimbia kila eneo ambalo alikuwepo mshambuliaji namba mbili wa Yanga, Nizar Khalfan na pia alikuwa akitazama kila eneo ambalo alikuwa akitengeneza nafasi, akamzima Nizar naye akawa bora ndani ya eneo la pili la uwanja kutoka golini kwake, aliwalinda vizuri Juma Nyosso na Kapombe na hata pale alipokuwa akipanda kusaidia mashambulizi alitazama usalama kwanza, ndiye aliyemfanya Kiemba kusogea kwa uhuru katika eneo la hatari la Yanga na kufunga.
 Wakati Fulani Haruna Niyonzima alihitaji kucheza nje ya nafasi yake ili kuhakikisha, Mkude hasogei katika eneo lao la hatari na hapo ndipo zikaja dakika 45 ngumu za Athuman Idd ‘Chuji’ ambaye pamoja na kutambua alikuwa na jukumu la kumzima Mwinyi Kazimoto lakini akajikuta akiingiziwa mzigo mwingine wa kumkabili Kiemba pia.

 Msuva na Hamis Kiiza ambao walianza pamoja na Bahanunzi na Nizar katika safu ya mashambulizi hawakuwa na msaada wakati timu yao ‘ikipepesuka uwanjani’, walikufa na kutoa nafasi ya Simba kutawala mchezo kwa dakika 30 za kwanza. Kocha wa Yanga, Ernest Brandts alipoona Simba wametawala eneo la kati  aliamua kumtoa mshambuliaji Hamis Kizza dakika ya 37 na kumuingiza kiungo Frank Domayo ili kwenda kuongeza utulivu pamoja ubunifu wa kupitisha pasi za kupenyeza katika eneo la hatari la Simba ambayo ilioneka kuzidiwa kiasi katika robo ya mwisho ya kipichi cha kwanza.
 Simba wakaendelea kukaza hadi mapumziko wakawa mbele kwa bao 1-0.
             KITU KIPYA NA KILICHOVUTIA KATIKA NUSU YA KWANZA
Mbuyu Twite alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza wa ‘DAR-PACHA’ na hakika aliweza kutimiza vyema jukumu la beki namba mbili, alikuwa anahitaji kujibadilisha kutoka mchezaji wa ‘ridhaa’ haki kuwa mchezaji wa kimataifa mara mbili tu baada ya kumkabili kinda Edward Christopher. EDO alikuwa mchezaji mdogo zaidi katika mchezo huo na ilikuwa ni mara yake ya kwanza pia kucheza mechi ya mahasimu wa soka la bongo.
Wakati, Twite akimtazama, Edo  kabla ya mchezo kuanza bila shaka alikuwa akichekea moyoni na kusema ‘ duh, sasa Simba wameniletea aka katoto badala ya…..’ lakini mara baada ya mchezo kuanza Simba wakaamua ‘kutest’ upande wa Twite, kila mpira akawa anapelekewa Edo na na baada ya kufanywa hivyo mara tatu refarii alionekana kuwabeba Yanga kwa kushindwa kutoa penati baada ya Nadir Harooub kumchezea rafu Edo ndani ya eneo la hatari baada ya Edo kumuadaa Twite. Hapo Twite akatambua thamani yake mbele ya mashabiki wa Yanga, akajitoa katika uchezaji wa ridhaa na kuwa mchezaji wa kimataifa na kumzima kabisa kinda huyo, huku yeye akionekana mchezaji tishio zaidi kwa kipa wa Simba, Juma Kaseja kwani mara mbili allipiga mashuti ya mbali na moja akigongesha mlingoti wa juu,Twite Alicheza vizuri na alionyesha namna mchezaji anavyoweza kuendana na watakacho mashabiki na kujibadilisha mchezoni kwa manufaa ya timu.
          KILICHO HARIBU LADHA YA MCHEZO KATIKA KIPINDI CHA KWANZA.
Ernest Brandts alikuwa akiiongoza Yanga kwa mara ya kwanza kama kocha mkuu na amepata matokeo mazuri kiasi.
Lakini aliingiza timu yake uwanjani akiwa na mbinu mbovu. Wakati, Simba ilikuwa na mapengo ya wachezaji wake muhimu kama Amir Maftah na Emmanuel Okwi kutokana na kuwa na adhabu ya kadi na wakikosa huduma waliyotaraji kutoka kwa Haruna Moshi kutokana na kusumbuliwa na  maralia, kocha wa timu hiyo, Milovan Cirkovic aliweza kuingiza machaguo mapya kama Mkude, Ngalema  na EDO huku akijiamini.
Brandts akiwa na washambuliaji wake wote wanne tena wakiwa na afya bora alishindwa kuipanga timu yake katika aina nzuri ya wachezaji ambao wangeweza kucheza mfumo wa 4-3-3 ambao kimsingi timu kama Yanga si rahisi kuumudu, kimazingira na utamaduni. Huu ni mfumo wa Simba lakini bado siyo sababu ya kushindwa kuzaa matunda kama Yanga pia watautumia vizuri.
Kumuanzisha Nizar kama mshambuliaji namba mbili katika mfumo huo ilikuwa ni kosa kubwa, lakini bado alishindwa kutambua umuhimu wa Kizza akicheza kama mshambuliaji namba mbili na Nizar akicheza pembeni, angeweza kuwapanga Kizza na Bahanunzi kama washambuliaji wawili wa kwanza na kumsogeza Nizar eneo la Kati kisha Msuva akacheza kama mshambuliaji wa tatu. Lakini hata kama angewapanga hivi bado asingekuwa na machaguo bora katika mfumo huo. Angewaanzisha, Didier Kavumbangu, Kizza na Bahanunzi na Yanga wangeweza kupata ushindi katika kipindi hiki.
Pia tatizo la wachezaji wetu kukosa nguvu lilionekana dhahiri japo lilizidi zaidi kwa upande wa Yanga, hata Simba hawakuonekana kuwa na nguvu hasa pale walipohitajika kuzitumia katika maeneo muhimu, Ngassa na Edo kwa upande wa Simba walionesha udhaifu huu na hata pasi za viungo Kiemba, Mwinyi na Mkude hazikuwa na nguvu. Tatizo la kupigiana pasi ‘laini’ ni kubwa katika nchi yetu na kama hakutakuwa na mabadiliko bado tutaonekana ni walewale kila siku japo tuna vipaji. Tatizo la kuanguka anguka kwa wachezaji lilipunguza sana radha ya mchezo.
        NYOTA WA KIPINDI HIKI
Paul Ngalema aliingia kikosini baada ya Maftah kuwa na adhabu, lakini aliweza kuonyesha ni kwa nini timu hiyo ya Simba ilimsajili ili kuwa mchezaji ambaye anaweza kuziba pengo lolote pale anapohitajika, Ngalema akicheza mchezo wake wa kwanza mbele ya watazamaji zaidi ya 50,000 aliweza kuonekana  mchezaji anayeupenda zaidi mguu wake wa kushoto, kila alipoenda kukaba alifanikiwa kutibua ‘muvu’ za Yanga, alipopiga pasi basi ilikuwa safi na ilifika alipotaka, mara chache aliweza kuonesha kipaji cha kupiga pasi ndefu japo anahitaji kufanyia mazoezi zaidi. Aliweza kumzima kabisa Msuva na kupelekea ashindwe kusogea katika lango lao, alicheza kama alivyotaka kucheza yeye.
        KIPINDI CHA PILI
Hakikuwa cha ufundi sana, lakini inaonekana Yanga waliingia kwa nia ya kuhitaji kusawazisha zaidi na kupata ushindi kama ingewezekana, waliingia kwa nguvu uku Niyonzima akirejea katika eneo lake la kati kusaidiana na Domayo Yanga wakaanza kupeleka mashambulizi ya kasi lakini bado Juma Kaseja atabaki kipa bora katika historia ya  mchezo wa mahasimu hao, kwani aliweza kuzuia mashuti mengi ambayo yalipigwa na wachezaji wa Yanga. Na alipongia Kavumbangu katika nafasi ya Nizar mara baada ya mapumziko Yanga walionekana wapo vizuri zaidi ya Simba na walihitaji matokeo.
Mpira uliorushwa na Twite unashindwa kuondolewa na Ngalema ambaye anajikuta akiushika na kuwa penalti. Said Bahanunzi alifunga bao lake la kwanza msimu huu katika ligi kuu baada ya kupiga ‘kiki kali ya ufundi’ na kumdanganya kipa Kaseja. Yanga wakasawazisha na hapo ndipo ukaja muda mbaya zaidi katika mchezo huo kwa wachezaji wa timu hizo kuanza kuchezeana rafu zisizo na maana na kupelekea mwamuzi kushindwa kulimudu pambano hilo
Penati ya Saidi Bahanuzi
      KILICHOKERA KATIKA KIPINDI HIKI
Ni mwamuzi Mathew Akrama kushindwa kuwatoa nje kwa kadi nyekundu Haruna Moshi ambaye alitaka kumvunja kabisa Yondani, Haruna alidhamiria kabisa na hata wakati anakimbilia mpira ule alionekana haendi kucheza mpira. Pia alishindwa kutoa kadi nyekundu kwa Athumani Idd Chuji katika dakika ya 94 alipomchezea rafu Akuffor akiwa yeye ndio mchezaji wa Yanga wa mwisho. Pia alishindwa kumuadhibu Mwasika alimpomkanyaga kusudi Mwinyi Kazimoto nje kidogo ya eneo la penati, na hata Mbuyu Twitte alimpovuta Mrisho Ngassa.
Kwa kifupi akaivuruga kabisa mechi ya ikawa mechi ya ‘kipuuzi’ kuanzia kwa wachezaji hadi waamuzi.