Search This Blog

Saturday, August 25, 2012

VIDEO: ROBIN VAN PERSIE NA SHINJI KAGAWA WAIPA MANCHESTER UNITED USHINDI WA KWANZA EPL

IANDIKIE CAPTION HII PICHA


SERENGETI FIESTA 2012 ILIVYOZINDULIWA MOSHI

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh Leonidas Gama akimtaja mshindi aliyejinyakulia gari aina ya Vits iliyokuwa ikinadiwa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,maara baada ya kuchezeshwa droo usiku huu,pichani mwanzo kulia ni Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru,Muwakilishi kutoka michezo ya bahati nasibu ya Taifa,Abdallah Mohamed akishuhudia tukio hilo,na mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini,Mh Dr Msengi wakishuhudia tukio hilo usiku huu ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mh Leonidas Gama sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini, Mh Dr Msengia wakiingia kwa shangwe kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu kwa ajili ya kulizindua tamasha hilo ambalo limepokelewa vyema kwa wakazi wa mji huo na vitongoji vyake. Pichani kulia ni Dj Zero akikamua vilivyo.
Dj Pq kutoka Clouds FM akikamua vilivyo kwenye mashine,kati ni mtangazaji wa Clouds FM B Dozen na mdau mwingine wakifuatilia kwa makini makamuzi yanayoendelea usiku huu,ambapo washabiki kibao wamejitokeza ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika.
Pichani shoto ni msanii kutoka THT,Recho sambamba na wacheza shoo wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Moja ya kikundi mahiri  kutoka THT kkikionesha mbwembwe zake jukwaani.
Dj Zero akikamua vilivyo.
Moja ya kikundi cha  THT kikiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya Uwanja wa chuo cha Ushirika mjini Moshi.
 Baadhi ya wasanii nyota wa filamu nchini nao wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu.
 Hapatoshi usiku huu.
Msanii wa kizazi kipya Sheta akiwaimbisha washabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti.
Prezoo akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza jioni ya leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Pichani juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika mjini Moshi.
Mmoja wa wasanii wa hip hop Joh Makini akikamua vilivyo usiku huu mbele ya umati mkubwa wa watu uliojitokeza kwenye uzinduzi wa tamasha la Fiesta.
Msanii mahiri wa bongofleva,Lina akiwa na densaz wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Lina akiimba wimbo wake Yalaiti
Mkali mwingine wa hip hop Mwana FA akishusha mitindo huru.
Pichani juu na chini Mwana FA akilishambulia jukwaa vilivyo kwa mitindo yake huru iliyokuna vilivyo mashabiki wake,waliofika kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Wasanii wa nyota wa Filamu hapa nchini nao walijumuika kwa pamoja kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani jukwaani ni Wema Sepetu,Jacob Steven a.k.a JB,pamoja na Aunt Ezekiel wakilisakata sebene.
Ray nae akilisakata sebene vilivyo.

WEMA SEPETU, RAY, JB, NA AUNTY EZEKIEL NDANI YA SERENGETI FIESTA MOSHI

Wema akiwa kwenye Interview......
Wema,Steve Nyerere kati na pembeni ni Aunt Ezekiel
Jacob Steven "JB" Akiwa kwenye Interview na Millard Ayo wa Cloudz Fm
Aunt,Ray,Wema,Hartman na Steven Nyerere......
Mmmmmmh! BBM sasa kuchat na Vibwana'bwana.....
sjui walikua wanadanganywa kina nani hapo kwenye sim.. LOL!

MBWANA SAMATTA ANAVYOTISHIA UTAWALA WA TRESOR MPUTU TP MAZEMBE


Na Edo Kumwembe

Huu ni mfululizo wa makala za Mbwana Samatta ambaye anachezea TP Mazembe ya Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jumanne iliyopita tuliona Samatta akisema anafikiria kuoa mwanamke wa Kizungu iwapo atafanikiwa kucheza soka Ulaya.
Sasa endelea

Napata hamu ya kumwuliza Mbwana Samatta kuhusu Tresor Mputu, mtu ambaye inaonekana ufalme wake kwa TP Mazembe unakwisha na badala yake kila mtu anamzungumzia Samatta kwa sasa.

Inasemekana kwamba hata tajiri wa timu, Moise Katumbi ana mapenzi makubwa zaidi kwa Samatta akimpigia simu mara kwa mara. Inasemekana kitu hiki kimekuwa kikifanya Mputu awe na wivu kwa sababu mtu pekee aliyekuwa karibu zaidi na Katumbi ni yeye Mputu na si mtu mwingine kama sasa.

Katika pambano kati ya Mazembe dhidi ya Chelsea Berekum lililopigwa Lubumbashi, Samatta alipika bao la kwanza kwa Mputu baada ya kuwalamba chenga walinzi wawili wa Berekum na kutoa pasi maridadi kwa Mputu aliyefunga.

Hata hivyo, tofauti na ilivyo kwa wanasoka wengi wa kulipwa, Mputu hakumfuata Samatta kwenda kushangilia na badala yake alikimbilia kwingine kwenda kushangilia, kitu ambacho kiliwachukiza mashabiki wengi wa soka.

Lakini katika pambano dhidi ya Zamalek lililochezwa Lubumbashi namshuhudia Samatta akifunga bao kufuatia mpira wa adhabu wa Mputu na Samatta anakimbilia kwenda kumkumbatia Mputu.

Namwuliza Samatta kuhusu hili, pia kuhusu uhusiano wake na Mputu. Samatta anakuwa makini na mwanadiplomasia zaidi kuhusu jambo hilo.

�Sina tatizo lolote na Tresor yeye ndiye mfalme hapa. Tresor ndivyo alivyo tu. Inabidi umkubali kama alivyo kwamba yeye ni mfalme hapa. Ukishakubali hilo wala hutapata shida ya kuishi naye. Mimi sina tatizo naye, ni mtu wangu, anasema Samatta.

Achilia mbali Samatta, mashabiki wa Mazembe kuhisi kwamba Mputu anawaonea wivu mastaa. wengine wawili wa Zambia Rainford Kalaba na Given Sunguluma.

�Mimi kaka sijaona kitu kama hicho. Mashabiki ndio wanatutazama kwa nje labda wao wanaweza kuhisi kitu tofauti, lakini sisi tunaocheza uwanjani hatuhisi kitu tofauti. Kuna wakati wanasema Mputu anaweza kukunyima pasi sehemu ya kufunga, sidhani kama ni kweli kwa sababu huwa anatengeneza mabao, sema uwezo wake umepungua kidogo baada ya kutoka kifungoni, anasema Samatta.

Edo Kumwembe katikati akiwa na Mbwana Samatta na Patrick Ochan kwenye hostel ya TP Mazembe

Namwuliza shabiki mmoja anayeitwa Phillipo Kabongo anayeishi jirani na Samatta na anaonekana kulielewa suala hili kwa undani. Lakini analalamika kwamba Tresor ni mtu mwenye maringo mengi tofauti na Samatta.

�Tresor siku zake zinaelekea mwisho, mfalme hapa ni Samatta tu. Tatizo la Tresor ni kujisikia. Ana majivuno sana. Lakini ni jambo la kawaida kwa mchezaji wa nyumbani kujisikia vibaya pindi mgeni anapofanya vizuri zaidi, anasema Kabongo.

Wakati tunatoka katika mazoezi ya Mazembe, kila siku Mputu huwa analiziba kwa makusudi gari la Samatta lisitoke kwa madai kuwa Mfalme huwa anaondoka kwanza kisha wanakuja wafanyakazi wake. Tunalazimika kumsubiri Tresor.

�Nimekwambia Tresor ni mfalme hapa. Si unaona, kila siku anapaki hilo Range Rover lake mbele ya gari langu halafu utamsikia anasema Samatta mimi ndiye mfalme wako hapa lazima niondoke kwanza ndipo uondoke, anasimulia Samatta.

Baada ya muda Mputu anakuja, anamtania Samatta, anajiita mfalme na kisha anaondoka zake. Mputu ananukia fedha. Ana kila dalili ya kujiamini kuwa ni mtu tajiri. Leo atakuja na Range Rover, kesho atakuwa na Nissan Morano na keshokutwa anakuja na Lamborghini.

�Tresor ni tajiri sana, anasema Samatta bila ya kuficha. Huyu jamaa ana pesa sana, anamiliki vitu vingi sana. Ameingia hadi katika biashara za Moise Katumbi. Ana magari yake makubwa, ana majumba yake hapa na ana kila kitu, ndiyo maana hakutaka kucheza Ulaya.

Hili suala la Mputu kutotamani kucheza Ulaya ndilo ambalo linanifanya nigutuke kumwuliza Samatta, vipi na yeye katika hali kama hii kama amebakiwa na ndoto za kucheza Ulaya kitu ambacho mashabiki wengi wa Tanzania wanakisubiri kwa hamu.

Anapendwa na watu wengi Lubumbashi, anapendwa na tajiri wa timu Moise Katumbi. anaendesha magari ya kifahari, anamiliki nyumba mbili. Inaonekana kama ndoto zake zimetimia. Namwuliza Samatta kama ndoto zake za kucheza Ulaya katika timu kubwa kama zipo. Samatta anajibu bila ya kusita.

Je Samatta anasema nini kuhusu ndoto zake za kucheza Ulaya? Bado zipo? Tajiri Katumbi amesema nini kuhusu ndoto za Samatta kucheza Ulaya? Fuatilia simulizi hii ya maisha ya Samatta TP Mazembe katika sehemu ya mwisho toleo la Jumanne.


Source:Mwanaspoti

KALI YA LEO: ANGALIA NAMNA MCHEZAJI HUYU ALIVYOVUNJIKA MKONO BAADA YA KUCHEZEWA RAFU

CHEMSHA BONGO: JEZI HII YA LIVERPOOL IMETENGENEZWA KWA KUTUMIA KITU GANI?


KALI YA LEO: ANGALIA NAMNA MCHEZAJI HUYU ALIVYOVUNJIKA MKONO BAADA YA KUCHEZEWA RAFU

Friday, August 24, 2012

Bocco arejea Azam FC. Azam FC yakataa kumtoa kwa mkopo SUPERSPORTS UTD


Kwa mujibu wa tovuti ya Azam Fc Mchezaji John Bocco amerejea kwenye kikosi cha Azam FC baada ya majaribio ya wiki mbili.
Maribio hayo yaliishia kwa kukubalika na kocha mkuu wa Super Sport United Gavin Hunt lakini bahati mbaya uongozi wa SUFC ulishindwa kutoa ofa ya kueleweka kwa John Bocco na Azam FC.

SuperSport United FC ilimtaka Bocco kwa mkopo huku wakisema kuwa kwa sasa hana uwezo wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu yao.

Lakini pia SUFC ilishindwa kuweka wazi maslahi ya mchezaji. Maelezo ya Uongozi wa SuperSport United FC ilikuwa ni kumuomba Bocco kwa mkopo kwa kuwa wanahitaji kumuona kwanza akifunga kwenye ligi ya Afrika ya Kusini kabla hawajafikiria ofa ya kumnunua.

Wakala wa mchezaji John Bocco Bw. Yusuf Bakhresa aliwataka Supersport United kumuonesha mkataba ambao wataingia na John Bocco na kueleza maslahi ambayo watakuwa wakimlipa lakini ilishindikana zaidi ya kusisitiza kuwa wanahitaji muda kabla hawajaingia mkataba mzuri na Bocco.

Yusuf hakufurahishwa na kitendo hicho na aliwataka SUFC kuwa wawazi kama wanamtaka John Bocco na watoe ofa itakayoizidi Azam FC vinginevyo itakuwa vigumu kumpata.
Azam FC imeamua kubaki na nyota wake huyu mwenye umri wa miaka 23 lakini milango ipo wazi kwa SuperSport kuendelea kumfuatilia na itakapotokea kuwa wamejiridhisha na kiwango chake basi walete ofa yao.

John Bocco binafsi baada ya kurejea nchini alisema amefurahishwa na mazingira ya Supersport United lakini akaomba kuwa angependa kupata maslahi makubwa zaidi ya Azam FC vinginevyo haoni sababu ya kwenda  Afrika  ya Kusini bila maslahi mazuri kwani Azam FC sasa ni timu kubwa Afrika Mashariki na mwakani itashiriki mashindano ya shirikisho barani Afrika.

EXCLUSIVE: ANDY COLE: TUSIWALAUMU WACHEZAJI WETU - LAWAMA ZIENDE KWA MBINU ZETU ZA KUFUNDISHIA ZILIZOZPITWA NA WAKATI

Mwalimu wa zamani wa shule na polisi mstaafu waliniambia namna ya mshambuliaji wa kati anavyopaswa kukaa ndani ya uwanja. Nilikuwa nafanya kozi yangu ya ukocha chini ya beji ya UEFA na huku nikiwa sitaki kuwakosea heshima walimu wale wawili, walikuwa wananichekesha kwa ushauri wao. Lakini pia kubwa zaidi niligundua uzito wa matatizo yanayolikumbuka soka la kiingereza. Najua namna ya kucheza kama mshambuliaji wa kati. Nimecheza kama mshambuliaji wa kati kwa miaka 20, tena zaidi kwenye level ya juu. Kama Maradona au Van Basten wangekuwa wananifundisha, ingekuwa sawa, lakini sio mwalimu mstaafu au polisi.

Mabadiliko yanatakiwa kufanyika katika hatua zote ili kuiwezesha England kuimarika na kuwa bora. Watu wanaondesha soka hawajawahi hata kucheza mchezo wenyewe, watu wanafundisha soka wakiwa hawajawahi au wamecheza kwenye level ya chini sana. Kuna watu kwenye soka la Uingereza wanapata kazi fulani kwa sababu wana urafiki au undugu na watu ambao tayari wapo kwenye system. 

Sio kwamba wana makocha wengi. Pamoja na uwa wachezaji wachache waliosajiliwa, Spain wana makocha walio bora mara 10 kuliko sisi, wengi wao wakiwa wachezaji wa zamani. Walijenga msingi mzuri na sasa wanakula matunda..  

Ndio maana nasisitiza hatupaswi kuwalaumu wachezaji wa England kwa kutofanya vizuri. Wanafanya kile ambacho walifundishwa. Tusiwalaumu kwa makosa na mbinu za kufundishia zilizopitwa na wakati za England.

Mabadiliko pekee kwenye Euro 2012 ni kwamba England walienda kwenye michuano huku wakiwa na mategemeo madogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya historia ya kutofanya vizuri kwa miaka kadhaa mpaka pale tulipoongoza kundi bila kutegemea. Taifa likaanza kujipa moyo na kuanza kuwa na mategemeo makubwa na wengine wakaanza kuamini England itaifunga Italy. Sikumbuki hata kama Buffon aliokoa japo mara mbili mashambulizi ya hatari katika dakika 120. 

Roy Hodgson alifanya kama alivyotegemewa. Aliifanya England kuwa ngumu nyuma  - lakini kwa gharama ya kukosa mashambulizi . England ilirudi miaka 10 nyuma na washambuliaji kama Rooney walipata taabu na kikosi kilichoundwa kulinda zaidi.

England haina wachezaji wengi aina ya Paul Scholes, ambao wapo comfortable na mpira. mashabiki hawasaidii pia. Wanategemea kuona damu ikimwagika ushindi upatikane, wachezaji kucheza kwa miguvu na kucheza kwa vyovyote vile ili mradi mpira uende mbele. Soka limebadilika - timu bora duniani sasa inacheza bila kuwa na mshambuliaji wa kati, wakati England bado inacheza kwa mipira mirefu na kutegemea krosi.
 Wakati Ujerumani iliporudiwa mchezo kama huo dhidi ya Italy katika nusu fainali, waitaliano kwa urahisi waliifunga Ujerumani.

Mfumo wa soka la kiingereza inabidi kubadilika. Hakuna namna anaweza kutokea Xavi au Iniesta kwa mfumo huu wa kiingereza kwenye soka kwa sababu wataambiwa ni wadogo sana kwa maumbo yao. Kwa soka la kiingereza kilicho kuwa kikitakiwa ni kuwa kasi na nguvu basi - mpaka Barcelona walipoizima hiyo nadharia hiyo. Shukrani kwa Sir Alex Ferguson aliweza kumruhusu mtu mwenye umbo dogo asiye na kasi wala nguvu sana kama Paul Scholes kucheza.

Nchini England, watu wanauliza "Je anaweza kuzunguka uwanja wote?" wanaangalia namna mchezaji anayoweza kukimbia na kuzunguka uwanja akiwa anasaka mpira, wanaulizia namna mchezaji anayoweza kuweka mguu wake popote ili mradi kuhakikisha timu yake inapata matokeo. Waingereza tumeng'ang'ania kuangalia udhaifu kuliko uimara. Je Andrea Pirlo anazunguka uwanja mzima akisaka mpira kwa nguvu na kasi? Hapana. Kama ilivyo kwa viungo bora, anajipanga vizuri, anazuia, na ana intercepts na kugawanya mipira vizuri kwa wachezaji wenzie. Hahitaji kukimbia sana na kuingia kwenye miguu ya watu, au kutumia nguvu sana kukaba. Anachofanya zaidi ni kuji-position vizuri kuliko kutengeneza contact na wapinzani, soka la kiingereza sasa limekuwa kama NBA.

Timu sasa zinajua zinaweza kuidhuru England kwa kukaa na mpira tu. Niliwahi kuangalia michuano ya vikosi vya wachezaji nane nane nchini Hispania hivi karibuni ambayo pia iliwashirikisha wachezaji wenye umri wa miaka 15 kutoka kwenye vilabu vikubwa. Pia nimekuwa nikiangalia sana mpira wa vijana na nimemshuhudia mwanangu wa kiume Devante akicheza soka akitokea kwenye shule za soka za kiingereza kama mie. Level ya ufundi ya watoto wa kihispaniola ilikuwa kubwa sana kufananisha na England. Kucheza kwenye uwanja mdogo kunasaidia kwa sababu wachezaji wanagusa mpira mara kwa mara. Unaweza kuugusa mpira mara 15 kama straika katika mechi inahusisha wachezaji 11x2. Utapata mipira mingi zaidi katika mechi inayohusisha wachezaji nane na nane, lakini Wingereza wamekuwa wakiendekeza kuwafundisha wacheza wachanga kwa mechi za wachezaji 22 dimbani.

Sasa nini kinafuata kwa England? Ningekuwa mie ningewapa makinda nafasi; wachezaji ambao wamefundishwa kwenye level ya klabu kama Welbeck, Wilshare, Cleverley, Rodwell....

Fanya kila kitu ambacho wajerumani walifanya katika kubadilisha, then fikiria nini kitatokea katika miaka miwili, na sio miezi miwili. Kwa huzuni natamka, nina wasiwasi hakuna kitakachobadilika. Hilo linatokana na historia na sifa ya soka la Uingereza.

BEND IT LIKE BECKS - DAVID BECKHAM AFUNGA BAO KUTOKA KWENYE KONA

MABADILIKO YA RATIBA YA UCHAGUZI WA VYAMA WANACHAMA WA TFF


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko madogo katika ratiba za uchaguzi za wanachama wa TFF. Ratiba za uchaguzi za vyama wanachama wa TFF ambavyo vimekwishaanza mchakato na ambavyo havijaanza mchakato wa uchaguzi itakuwa kama ifuatavyo:

CHAMA MWANACHAMA WA TFF
Tarehe ya Kuanza Mchakato wa uchaguzi
Tarehe ya Uchaguzi
Arusha Region Football Association (ARFA)
27-Aug-2012
7-Oct-2012
Dar es Salaam Region Football Association (DRFA)
3-Sep-2012
14-Oct-2012
Geita Region Football Association  (GEREFA)
29-Sep-2012
10-Nov-2012
Iringa Region Football Association (IRFA)
28-Jul-2012
8-Sep-2012
Katavi Region Football Association
29-Sep-2012
10-Nov-2012
Kigoma Region Football Association (KRFA)
21-Jul-2012
1-Sep-2012
Kilimanjaro Region Football Association (KRFA)
31-Jul-2012
8-Sep-2012
Lindi Region Football Association (LIREFA)
8-Sep-2012
20-Oct-2012
Manyara Region Football Association (MARFA)
21-Jul-2012
15-Sep-2012
Mbeya Region Football Association (MREFA)
8-Sep-2012
21-Oct-2012
Mwanza Region Football Association (MZFA)
29-Sep-2012
8-Nov-2012
Njombe Region Football Association (NJOREFA)
4-Aug-2012
15-Sep-2012
Coast Region Football Association (COREFA)
3-Sep-2012
14-Oct-2012
Rukwa Region Football Association (RUREFA)
27-Aug-2012
7-Oct-2012
Football Association of Ruvuma (FARU)
22-Sep-2012
3-Nov-2012
Shinyanga Region Football Association (SHIREFA)
8-Sep-2012
20-Oct-2012
Simiyu Region Football Association (SIFA)
15-Sep-2012
27-Oct-2012
Tabora Region Football Association (TAREFA)
27-Aug-2012
6-Oct-2012
Tanga Region Football Association (TREFA)
22-Sep-2012
3-Nov-2012



Tanzania Football Coaches Association  (TAFCA)
29-Sep-2012
10-Nov-2012
Tanzania Sports Medicine Association (TASMA)
15-Sep-2012
27-Oct-2012
Soccer Players Union of Tanzania ( SPUTANZA)
15-Sep-2012
28-Oct-2012
Football Referee’s  Association of Tanzania (FRAT)
21-Aug-2012
30-Sep-2012
Tanzania Women Football Association (TWFA)
22-Sep-2012
4-Nov-2012



TFF inavitaka vyama wanachama wake kuzingatia kikamilifu ratiba hii iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF katika kutimiza wajibu wao wa kikatiba.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF haitabadilisha ratiba hiyo kutokana na wilaya yoyote kutokamilisha uchaguzi wake, na hivyo inazitaka Kamati za Uchaguzi za Mikoa kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwa mujibu wa ratiba hii.

Kamati pia inazitaka Kamati za Uchaguzi za Mikoa kusimamia kikamilifu na kwa umakini chaguzi za wilaya zinazoendelea kwenye wilaya zilizo mikoani kwao. Ni muhimu kwa kamati kuhakikisha Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF zinafuatwa na kusimamiwa kwa umakini.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF pia imebaini kuwa kuna Kamati za Uchaguzi za Mikoa ambazo hazikusimamia kikamilifu chaguzi za viongozi wa wilaya, kitu ambacho kinaweza kusababisha matatizo hapo baadaye. Kwa mara nyingine, Kamati ya Uchaguzi ya TFF inazitaka Kamati za Uchaguzi za Mikoa kuhakikisha wanaoomba kugombea uongozi kwenye wilaya, wana sifa zinazolingana na utashi wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na Katiba.

Wanachama ambao hawakuzingatia ratiba hiyo, hawatapewa fursa nyingine ya kubadilisha tarehe za uchaguzi na hilo litakapotokea hatua za kikanuni zitachukuliwa.

Angetile Osiah
KATIBU MKUU