Search This Blog

Friday, January 6, 2012

PRECISION AIR YATOA MSAADA TWIGA STARS


Kampuni ya ndege ya PrecisionAir imetoa msaada wa tiketi zenye thamani ya sh. milioni 27.8 kwa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) ambayo Januari 14 mwaka huu itacheza na Namibia jijini Windhoek kuwania nafasi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC).

Akitangaza msaada huo leo (Januari 6 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Dar es Salaam, Meneja Mauzo wa PrecisionAir, Tuntufye Mwambusi amesema wameamua kusaidia kwa vile Twiga Stars imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali inayoshiriki.

Mwaka juzi Twiga Stars ilicheza fainali za AWC zilizofanyika Afrika Kusini, Julai mwaka jana ilikuwa kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) nchini Zimbabwe na kushika nafasi ya tatu wakati Septemba mwaka jana ilishiriki michezo ya Afrika (All African Games- AAG) jijini Maputo.

Mwambusi amesema tiketi hizo ni kwa ajili ya kuitoa Twiga Stars kutoka Dar es Salaam- Johannesburg- Dar es Salaam kwa ndege yao ya PrecisionAir. Awali PrecisionAir ilitoa punguzo la nauli kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) iliyoshiriki michuano ya COSAFA nchini Botswana.

Amesema mpango wa kampuni yake ni kushirikiana na TFF katika kuisafirisha Twiga Stars na timu za Taifa za vijana (Ngorongoro Heroes) na ile ya umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwenye nchi ambazo ndege yao inafika.

Naye Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameishukuru PrecisionAir kwa msaada huo mkubwa na pia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kutoa kambi kwa Twiga Stars ambayo inatarajia kuondoka Januari 12 mwaka huu kwenda Namibia na kurejea Januari 15 mwaka huu.

Amesema TFF bado inahitaji msaada wa kuisafirisha timu hiyo kutoka Johannesburg hadi Windhoek na kurudi Johannesburg ambapo itachukuliwa na PrecisionAir. Jumla ya nauli pekee kwa Twiga Stars kutoka Dar es Salaam hadi Namibia na kurudi ni sh. milioni 36.

Hivyo amewataka wadau kusaidia nauli hiyo ya kutoka Johannesburg hadi Windhoek, gharama za malazi timu ikiwa Namibia na posho kwa wachezaji na benchi la ufundi ambapo jumla yao ni watu 25.

FINALLY THIERRY HENRY ARUDI EMIRATES.


Thierry Henry amekamilisha uhamisho wa muda mfupi kurudi Arsenal.

The Gunners wamekamilisha makubaliano ya bima na New York Red Bulls, kwa maana Henry sasa anaweza kuanza kuichezea Arsenal kuanzia Jumatatu katika raundi ya Kombe la FA dhidi ya Leeds.

The 34-year amesajiliwa kama mbadala wa Gervinho na Maroune Chamakh, ambao watakuwa wakielekea Africa kucheza CAN na timu zao za taifa Morocco na Ivory Coast.

Henry alisema: “Ni vigumu kuwa mkweli lakini linapokuja suala la Arsenal moyo ndio utakaokuwa unaongea.

“Tangu nilipojua the plan nyuma ya usajili wangu nilikuwa sawa na kurudi Gunners. Sijarudi Arsenal ili kuwa shujaa au ku-prove kitu chochote. Nimerudi kusaidia tu.

“Watu wanabidi waelewe kwamba Chamakh na Gervinho wanaenda kucheza CAN, hivyo niliitwa kuja kujaza gap waliyoiacha.”

Henry atavaa jezi namba 12 mpaka atakapomaliza mkataba wake wa miezi miwili.

Welcome The Greatest King Theirry Henry.

OWEN: GARY ANAWEZA KUWA MCHEZAJI WA CHELSEA KUANZIA JUMAPILI


Gary Cahil anaweza kuwa mchezaji wa Chelsea by Sunday, kwa mujibu wa kocha wa Bolton Owen Coyle.

Klabu mbili tayari zimeshakubaliana ada ya uhamisho kwa ajili ya beki huyo wiki iliyopita lakini mahitaji binafsi ya mchezaji ndio yalikuwa kikwazo baada ya kutaka kulipwa £120,000 kwa wiki.

Cahill alibaki north west na kucheza michezo muhimu dhidi ya Wolves na Everton.

Atapumzishwa katika mechi ya raundi ya 3 ya kombe la FA dhidi ya Macclesfied, Coyle akiwa hataki kum-stress kipindi hiki cha uhamisho. Inaonekana goli la ushindi aliloifungia Bolton dhidi ya Everton @Goodison Park on Wednesday ndilo liltakuwa la kuwaagawapenzi wa Bolton.

SIR ALEX FERGUSON - CHELSEA HAWAWEZI KUTUUZIA LAMPARD


Sir Alex Ferguson amesema Manchester United hatoweza kumsajili Frank Lampard kutoka Chelsea.

Mtandao wa Sportsmail wa Uingereza jana wali-reveal kwamba Ferguson alikuwa anafikiria kumsaini kiungo huyo wa kiingereza ambaye siku hizi karibuni amekuwa akipata nafasi chache za kuitumikia Chelsea.

Na inaeleweka kwamba Lampard isingekuwa vigumu sana kwa Lampard kuhamia United akizingatia na nafasi anayopewa na AVB ndani ya The Blues.

Akiongea leo Ijumaa asubuhi, Fergie alisema: “Huwezi kuniambia Chelsea watamuuza Frank Lampard kwa Manchester United in January. Unaamini kweli hilo linawezekana? Chelsea ni kama sisi, kuna kitu wanataka kufanya. Jambo la pili katika hii nusu ya pili ya msimu ni muhimu sana kwao. Kama watajaribu na kutaka kushinda ligi wanahitaji kuwa na wachezaji wao wote bora.

“Nimeshasema ni wachezaji wa namna gani tunaweza kuwasajili mwezi January, ni wachezaji ambao wapo available ambao ni top class players, ambao sio rahisi kuwapata katika dirisha dogo la usajili.

“Unafanyaje? Unamsajili second-rate player? Hapana. Of course huwezi. Majeruhi yanayowakabili wachezaji wetu kipindi hiki yamefanya mashabiki wetu waanze kupiga kelele wakitaka tusajili.

“Ni bora niendelee kuwa na wachezaji hawa nilionao kuliko kumsajili mchezaji ambaye hatopata nafasi hata ya kucheza mchezo mmoja.”

Wednesday, January 4, 2012

HAWA NDO WALIKWENDA NA MBWANA SAMATTA LUBUMBASHI...MSIKILIZE KWA MAKINI SALEH SAID KIONGOZI WA KIMBANGULILE FC...

UKIMUACHA GODFREY NYANGE KABURU NA MBWANA SAMATTA KWENYE HUO MSAFARA,HAO WENGINE NI KINA NANI ? WALIENDA LUBUMBASHI KUFANYA NINI ? WALIKUA KAMA NANI KWA MBWANA SAMATTA ?

BONYEZA HAPA CHINI UMSIKILIZE SALEH SAID..


SAKATA LA UHAMISHO WA MBWANA SAMATTA!

TIMU YA KIMBANGULILE ILIYOMLEA MSHAMBULIAJI MBWANA SAMATTA TANGIA AKIWA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 11 IMETOA VIELELEZO VINAVYOONYESHA UHALALI WA WAO kutaka ilipwe fidia ya mazoezi (training compensation). ( UKITAKA KUSOMA VIZURI HUU MKATABA WA MZAZI WA MBWANA SAMATTA NA KIMBANGULILE FC CLICK KWENYE DOCUMENT HUSIKA )

MBWANA SAMATTA WAPILI KUTOKA KULIA WALIOSIMAMA AKIWA NA KIKOSI CHA KIMBANGULILE FC.MTIBWA SUGAR YAENDELEA NA MAANDALIZI YA RAUNDI YA PILI YA VPL.

MTIBWA SUGAR LEO JIONI KWENYE UWANJA WA MANUNGU MKOANI MOROGORO WAMEENDELEA NA MAZOEZI MAKALI KWA AJILI YA RAUNDI YA PILI YA LIGI KUU YA VODACOM.PICHA KWA HISANI YA MDAU : DAMIAN JOSEPHMAN CITY YAWANYOOSHA LIVERPOOL

MAN CITY YAWANYOOSHA LIVERPOOL

Samuel Eto’o Aanzisha Kampuni ya Simu.

Samuel Eto’o mshambuliaji mkali wa timu ya Anzhi Makhachkala ameanzisha kampuni yake ya simu za mkononi nchini Cameroon, Kampuni hiyo itakayojulikana kwa Jina la SET mobile itakuwa ni kampuni ya tatu katika soko la simu za mikononi nchini Cameroon ikichuana na Orange Telecom ya Ufaransa na MTN ya Afrika Kusini.
Set’Mobile was launched on Thursday in Yaounde with more than 50,000 SIM cards already sold out, but the network will be activated on January 21, which is the opening day of the 2012 Africa Cup of Nations, the entity’s management said.With a capital base of 100 million francs cfa (€152,449), Set’Mobile, which also bears the initials of the famous Anzhi striker, is intended to provide mobile Internet service alongside telephony.The new mobile company expects to get a majority of its market share from the youth who are fans of Eto’o.

The 30yr old footballer now plays for Russian team Anzhi Makhachkala where he earns $29 million every season after tax, making him the highest paid footballer in the world currently, and one of sports highest paid earners.
The market penetration for mobile network in Cameroon is currently at 49 per cent below the fast growing rate of 75% in Cote D’Ivoire, Senegal and Ghana, which local observers see as enough room for the survivability of Eto’o’s new venture against stiff competition from giants Orange and MTN
SOURCE: www.darbase.com

MUOSHA HUOSHWA!ZAKI NA MIDO WATAJWA KATIKA KIKOSI KICHAJO KUPAMBANANA YANGAKlabu ya Zamalek ya Misri imewasilisha orodha ya wachezaji 26 ambao wamesajiliwa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu.

Zamalek ambayo imepangwa kucheza na Yanga ya Dar es Salaam raundi ya awali ya michuano hiyo , ina historia ya kulitwaa taji hilo mara tano mpaka mwaka 2002, lakini tangu imekuwa ikihangaika kurejesha ufalme huo, huku wapinzani wao wakubwa Ahly wakiwapiku kwa kulitwaa taji hilo mara sita mwaka 2008.

Ili kuhakikisha wanarejesha utawala wao kwenye soka la Afrika , Zamalek imefanya usajili wa nyota kadhaa ili kuimarisha kikosi chao na katika orodha hiyo ya wachezaji wamo Ahmed Hossam "Mido” na Amri Zaki, ambao hapo kabla walikuwa wakichezea klabu za Ligi Kuu ya England.

Zaki ambaye Julai 22 mwaka 2008, alimaliza mkataba wake wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu ya Ligi Kuu ya England ya Wigan Athletic, ambako alikuwa akilipwa pauni milioni 1.5, pia amewahi kuichezea kwa mkopo Hull City, alijiunga na Zamalek Januari 17 mwaka 2010.

Alitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kwa kuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao matatu katika mechi nne za mwanzo alizochezea timu hiyo , mbali na sifa hiyo pia ni

mchezaji anayejulikana kutokana na umahiri wa kupiga mipira vichwa pamoja na kuwa miongoni mwa wafungaji hodari barani Afrika.

Mshambuliaji mwenzake ‘Mido’ aliwahi kuichezea Ajax ya Uholanzi mwaka 2001, ambako baadaye aliondoka na kujiunga na Celta Vigo kwa mkopo mwaka 2003 kabla ya kwenda

Marseille ya Ufaransa ambako nako aliondoka na kujiunga na Roma ya Italia mwaka 2004.

Baada ya hapo alijiunga na Tottenham Hotspurs ya England kwa mkataba wa mkopo wa miezi 18 mwaka 2005 na mwaka uliofuata alipewa mkataba wa kudumu.

Aliondoka Spurs mwaka 2007 akijiunga na Middlesbrough ambako nako hakukaa akijiunga na Wigan Athletic na baadaye West Ham alikokwenda kwa mkopo na alirudi tena Ajax mwaka 2010 ambako klabu hiyo ilikubaliana kuvunja mkataba na mchezaji huyo Januari 4 mwaka huo ndipo alirejea, Zamalek.

Kwa mujibu wa mtandao wa Zamalek hiki ndicho kikosi kamili cha timu hiyo kilichowasilishwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya michuano hiyo ni Abdul-Wahed Al- Sayed - Mahmoud Abdul-Rahim "Jnc", Mahmoud Fathallah, Hany Said, Salah Suleiman, Karim Hassan na Mohamed Abdel Shafi.

Wengine ni Ahmed Samir, Omar Jaber, Hazem Imam, Ibrahim Salah, Merghany Ahmad, Ahmad Tawfiq, Ahmed Hassan, Alaa Ali, Mohammed Saeed, Shikabala, Ahmed Jaffar,

Hamdy Hussein , Ahmed Hossam "Mido", Amr Zaki, Razak Ahmed, Abdel-Kader, Mohammed Ibrahim na Hossam Arafat.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Cafa Yanga itawakaribisha Zamalek katika raundi ya awali ya michuano hiyo kati ya Februari 17 au 19 jijini Dar es Salaam na mchezo wa marudiano utafanyika Machi 2 au 4 jijini Cairo..”

Tuesday, January 3, 2012

BECKHAM NJIANI KUBAKI GALAXY - PSG WATHIBITISHA HATOJIUNGA NAO


Paris Saint Germain wamethibitisha David Beckham hatojiunga na timu hiyo.

Mkurugenzi wa ufundi Leornardo amekuwa akijaribu kwa muda mrefu kumsaini ex-England captain baada ya kumalizika kwa mkataba wake na LA Galaxy mwezi November 2011.

Lakini pamoja na kupewa ofa nzuri, Beckham, 36, aliamua kutokwenda Ufaransa kwasababu halikuwa chaguo zuri kwake na familia yake.

Na inaonekana Beckham ataongeza mkataba mpya na LA Galaxy baada ya kumkubalia kucheza katika michuano ya Olympics in summer 2012.

Leonardo alisema: “It’s over, Beckham hatokuja PSG. Inasikitisha lakini kwa sababu ya familia yake iliyopo Los Angeles, ameamua kutokubadilisha kila kitu katika maisha yake.”

Mapema wiki hii Leornardo alikiri nafasi ya PSG kumsaini Beckham ilikuwa ndogo sana.

Alisema: “Tatizo halikuwa la kikazi bali familia yake. Ni vigumu kuchagua kuileta familia yake Paris. Ni chaguo binafsi na rahisi kwake. Namjua Beckham. Nina imani kubwa kwake kama mchezaji na kama Baba. Nafahamu ni uamuzi mgumu kwake kuhama.

WACHEZAJI SABA WA TASWA HATIHATI KUFUNGIWA.

WACHEZAJI saba wa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za michezo nchini (Taswa FC) wanakabiliwa na adhabu kali baada ya kukacha mechi maalum ya kufunga mwaka 2011 dhidi ya Lebanon FC.
Mechi hiyo ilifanyika Desemba 31 kuanzia saa 4.00 usiku na wachezaji hao walishindwa kuheshimu makubaliano yaliyofanyika asubuhi yake na kukacha mchezo huo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa tabia hiyo imewasikitisha sana kwani imeonekana wazi kuwa ni hujuma kwani taarifa ya kuwepo kwa mechi hiyo ilitolewa asubuhi na wengine kupewa katika mechi ya kirafiki baina ya Simba SC na Mtibwa Sugar iliyofanyika kwenye uwanja wa Chamazi jijini.
Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Sweetbert Lukonge, Wilbert Molandi, Jimmy Haroub, Mohamed Akida, Fred “Chuji” Mbembela, Shedrack Kilasi na Calvin Kiwia. Majuto alisema wachezaji hao wamepewa barua na uongozi huo kujibu kwa nini wasichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kiendo hicho.
Kwa mujibu wa Majuto, wachezaji hao wanatakiwa kujibu barua hizo kabla ya Januari 6 ambapo kikao cha kamati ya utendaji kwa kujumuisha na makocha kitafanyika Ijumaa kwenye mgahawa wa Hadees kwa ajili ya kutoa maamuzi. Kwa mujibu wa kanuni za Taswa FC, wachezaji hao wanakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kati ya mwezi mmoja, mitatu na mwaka.
Wakati huo huo Taswa FC inaanza mazoezi rasmi ya kujiandaa na safari ya Tanga na Zanzibar jioni hii kwenye uwanja wa Chuo Cha Posta, Kijitonyama. Majuto aliwataka wachezaji wote kufika kwa wingi ili kufanikisha mazoezi hayo.

MSAADA TUTANI! HUYU NI NANI ?

Shaffih unamkumbuka huyu legend wa bongo? tupia hiyo picha kwenye blog yako uwaulize wadau kama wanamkumbuka huyo mzee kona bao!

FIDIA YA KIMBANGULILE KWA SAMATA.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya uenyekiti wa Alex Mgongolwa ilikutana Desemba 30 mwaka jana kupitia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa mbele yake ikiwemo taarifa ya uamuzi wa timu ya Kimbangulile kukata rufani Kamati ya Rufani kupinga uamuzi wake juu ya mchezaji Mbwana Samata.
Ikumbukwe kuwa Kimbangulile iliwasilisha malalamiko TFF ikieleza kuwa inastahili malipo baada ya Simba kumuuza Samata kwa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Kimbangulile ilitaka ilipwe fidia ya mazoezi (training compensation) na mchango maalumu (solidarity contribution) kwa mujibu wa Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Uamuzi wa Kamati ya Mgongolwa ulikuwa Kimbangulile imeshindwa kutoa vielelezo kuonesha kuwa iliingia gharama za mazoezi kwa mchezaji husika wakati akiichezea timu hiyo. Kwa upande wa solidarity contribution ambayo ni asilimia 5 ya mauzo ya mchezaji huyo TP Mazembe, fedha hizo zinatakiwa kulipwa na klabu yake hiyo mpya ambayo TFF itaitaka kufanya hivyo wakati Samata atakapoombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Hivyo Kamati itatengeneza utetezi wake na kuuwasilisha kwenye Kamati ya Rufani itakaposikiliza rufani ya Kimbangulile.

USAJILI WA DIRISHA DOGO 2011/2012


Kwa upande wa Daraja la Kwanza, Kamati hiyo imetoa siku saba kwa klabu ambazo zimezidisha idadi ya wachezaji ili zipunguze, kwani kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 30. Klabu nyingi baada ya kufanya usajili wa dirisha dogo zimepitisha idadi ya wachezaji 30 wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni.
Hivyo kwa klabu ambayo itashindwa kupunguza wachezaji ndani ya muda huo, TFF itahesabu hadi 30 na wachezaji watakaokuwa wamezidi wataondolewa. Kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), klabu ya Villa Squad ndiyo imekutwa na kasoro katika usajili wake ambapo imetoa kwa mkopo wachezaji wanne na imepokea wengine watano kwa mkopo.
Kwa mujibu wa kanuni ya mkopo, klabu haitakiwi kuwa na wachezaji zaidi ya watano iliotoa au kuingiza kwa mkopo kwa wakati mmoja. Hivyo Villa Squad imetakiwa kuwaandikia barua za kuwaacha wachezaji wanne iliowatoa kwa mkopo ili wawe huru (free agents). Pia Kamati imeagiza viongozi wa juu wa Majeshi ambayo yanamiliki timu za mpira wa miguu kupewa elimu ya kanuni za usajili, kwani mafunzo ya kijeshi na uhamisho wa wachezaji ambao ni askari vimekuwa vikiathiri viwango vya timu zao kwenye ligi.SIMBA KUMSIMAMISHA KOCHA BASENAMalalamiko ya Kocha Moses Basena kwa TFF baada ya klabu yake ya Simba kusimamisha mkataba wake yaliwasilishwa mbele ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji. Baada ya kupitia malalamiko hayo, uamuzi wa kamati ni kuwa suala hilo liendelee kuwa kati ya Simba na Basena na kuwataka wakae pamoja ili waweze kulipatia ufumbuzi.Licha ya Basena kuwa na mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, Kamati imebaini kuwa hauwezi kufanya kazi (functional) kwa vile kocha huyo hakuwa na kibali cha kufanya kazi nchini (work permit).Hivyo kisheria hakukuwa na mkataba kwa vile ili Basena aweze kuitumikia Simba ni lazima awe na kibali cha kufanya kazi nchini. TFF ilikataa maombi ya Simba kuiandikia barua Idara ya Uhamiaji kuthibitisha barua ya kumuombea work permit baada ya kocha huyo kushindwa kuwasilisha vyeti vyake vya ukocha.Kwa vile Simba imeshaajiri kocha mwingine (Milovan) kwa mkataba wa miezi sita na kupatiwa kibali cha kufanya kazi nchini, ufumbuzi wa suala la Basena unabaki kuwa kati ya klabu hiyo na kocha huyo.

MESSI VS RONALDO NDANI YA MWEZI DECEMBER 2011


DECEMBER STATISTICS*186MINUTES PLAYED
282
1GOALS
4
0PENALTIES
1
2ASSISTS0
8 / 3 (37.5%)
TOTAL SHOTS / ON GOAL
22 / 7 (31.8%)
157 / 141 (89.8%)
PASSES / COMPLETED125 / 95 (76%)
7.25
AVERAGE RATING
6.5
172011-12 LA LIGA GOALS20
29 (26)
2011-12 COMPETITIVE GOALS (APPEARANCES)
25 (23)

YANGA WADUNGWA NA MAFUNZO, HUKU AZAM WAKING'ARA KTK MAPINDUZI CUP.


Azam FC wameanza vyema michuano ya Mapinduzi Cup kwa kuichapa goli 3-1 Kikwajuni FC, wakati Mabingwa wa Tanzania Yanga wakichapwa goli moja bila majibu toka kwa Mafunzo FC.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa saa kumi na nusu alasiri katika uwanja wa Aman, Azam FC walikuwa wakwanza kupata goli kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 13 kabla ya kumtengenezea John Boko goli la pili na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa Azam FC kuwa mbele kwa magoli 2-0.

Khamis Mcha Viali alihitimisha kalamu ya magoli kwa kuiandikia Azam FC goli la 3 katika dakika ya 75, kabla ya Kikwajuni kujipatia goli la kufutia machozi kwa mpira wa adhabu uliopigwa kwa ufundi mkubwa katika dakika ya ya 82.

Katika mchezo wa pili katika uwanja huo ulishuhudia Yanga wakijifunza soka toka kwa Mafunzo, baada ya kukubali kufungwa goli moja katika dakika 15 za mwisho.

Kwa matokeo hayo ya leo Azam wanakwea katika usukani wa kundi B, wakati Mafunzo wakishika nafasi ya 2 na Yanga nafasi ya 3 wakati Kikwajuni ikishika mkia.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Simba wanatarajia kuteremka kesho katika michezo ya kundi A katika uwanja wa Amana visiwani Zanzibar.

ARSENAL WAUANZA MWAKA VIBAYA -BOBBY ZAMORA AWALIZA DK. ZA MWISHO

LAMPARD AMPA AHUENI VILLAS BOAS -CHELSEA WAKIPATA USHINDI DHIDI YA WOLVES

Monday, January 2, 2012

PHOTOS: GERVINHO ALIHUDHURIA KWENYE SHOW YA AIRTELBONGO 50 @LEADERS

VAN PERSIE ASHINDWA KUIFIKIA REKODI YA ALAN SHEARER - ARSENAL WAKIIFUNGA QPR

EPL ROUND UP: UNITED, CITY, CHELSEA WALA VIPIGO

Iko wapi ile kasi waliyoanza nayo BMT mpya?


Imani Makongoro
NI saa 24 zimepita tangu watu wa mataifa mbalimbali ikiwamo Tanzania waliposherehekea Sikukuu ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2012 na kuuaga ule wa 2011.
Tunamshukuru Mungu kwa kukufikisha kuona mwaka mpya najua ni wengi walitamani kuiona, lakini kwa mapenzi yake yeye muumba Mbingu na Ardhi hawakufanikiwa kuiona.
Kama kawaida nao mwaka 2011 umemalizika bila mabadiliko yoyote katika sekta ya michezo ambayo uwezo kwenda kokote ulimwenguni lazima utakutana nayo isipokuwa kama; hautaki michezo na utamaduni, haupendi michezo na utamaduni, haujui maana ya michezo na utamaduni, unafanya makusudi kukataa michezo na utamaduni, hauoni faida ya michezo na utamaduni na mengi mengineyo.
Wakati mwingine huwa nafikiria kwamba viongozi wa michezo na utamaduni wameingia madarakani hapa nchini wakati siyo wapenzi wa michezo na utamaduni kwa dhati na wanaangalia zaidi maslahi yao binafsi badala ya kuendeleza michezo na utamaduni nchini.
Mfumo wa michezo na utamaduni uliopo nchini unaonyesha wazi maendeleo ya michezo na utamaduni ni wajibu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na vyama vya michezo.
Kama mtakumbuka vizuri Oktoba 5 mwaka jana Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emannuel Nchimbi alizindua rasmi Baraza jipya la Michezo la Taifa kutoka lile la zamani lililokuwa chini ya Kanali mstaafu Idd Kipingu.
Baraza hilo likiongozwa na mwenyekiti Dioniz Malinzi, Katibu Mkuu, Henry Lihaya na wajumbe wengine 11 walioteuliwa na Wizara hiyo ambao wangeshirikiana bega kwa bega na vyama vya michezo hapa nchini siku hiyo walitema cheche zao na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike ili kuinusuru michezo ya Tanzania.
Malinzi alitoa ahadi mbalimbali ikiwamo kufanya mabadiliko ndani ya mwaka mmoja tofauti na ile mitatu aliyopewa na Waziri Nchimbi ambapo angeshirikiana na vyama vya michezo vilivyowakilishwa na Makatibu wakuu wake ambao ni wajumbe wa Baraza hilo.
Wakati Malinzi akikabidhiwa rungu hilo la kuendesha gurudumu la BMT kwa ajili ya maendeleo ya michezo yetu moja ya mikakati yake ilikuwa ni vyama kuwa na mipango endelevu huku akiahidi yeye kusimama kidete ili kuhakikisha hilo linafanyika ndani ya muda mfupi.
Mbali na hilo mwenyekiti huyo kwa kushirikiana na wajumbe wa BMT walipeana mikakati mbalimbali sambamba na kugawana majukumu yaliyonekana kuleta ahueni kwa taifa katika kuokoa sekta yetu ya michezo iliyopoteza dira.
Kuna msemo usemao, 'Mbio za Sakafuni Uishia Ukingoni,' ndivyo ilivyokuwa kwa mikakati ya Baraza hilo jipya wakati ule na sasa unaweza usinielewe namaanisha nini, lakini ukweli ni kwamba BMT ile ya ahadi imegeuka 'bubu' katika utekelezaji.
Leo ni Januari 2, siku zinazidi kukatika tangu ile ahadi ya Mabadiliko katika michezo itolewe na siku tatu zimesalia ili ahadi hiyo itimize miezi mitatu ya maneno bila utekelezaji.
Unaweza kuona ni muda mfupi, lakini ukweli ni kwamba miezi mitatu ni mingi sana na Watanzania wengi tulitarajia kuona cheche za BMT ndani ya muda mfupi tu ambazo zingevikumbusha vyama vinatakiwa kufanya nini kutokana na ule moto iliyoanza nao mara baada ya Baraza hilo jipya kuzinduliwa.
Lakini moto BMT waliouwasha Oktoba 5, umekuwa ni wakifuu kwani kila siku zinavyokwenda hakuna mabadiliko yoyote ya maana yaliyotokea katika kipindi hiki cha miezi mitatu.
Mwaka mmoja wa BMT wa kuleta mabadiliko katika sekta yetu ya michezo umegeuka mwaka wa viongozi wa vyama kurumbana bila sababu za msingi yote ikiwa ni uchu wa madaraka bila kuzingatia maadili na umuhimu wa kuleta maendeleo ya kweli katika mchezo.
Hivi viongozi wakurumbana kisa madaraka tena si kwa manufaa ya michezo bali kwa maslahi yao binafsi tunategemea kitu gani zaidi ya kujichimbia shimo ambalo tutatumbukia wenyewe.
Sidhani kama Baraza letu lenye dhamana ya kusimamia michezo hapa nchini haya ndiyo mliyotuahidi awali yanatekelezwa kwa sasa, ile mikakati yote imeishia pale uwanja wa Taifa ilipokuwa ikipangwa huku uozo katika vyama ukizidi kila siku inapokwisha na kuanza siku mpya.
Nilitegemea uozo huo ungekuwa wa kwanza kuvumbuliwa katika vyama sambamba na kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho, lakini ni kama mmenyeshewa na mvua mara tu baada ya kuanza kazi rasmi kutokana na ukweli kwamba yote mliyotuahidi hakuna hata moja lililotekelezeka.
Imekuwa ni kawaida ya viongozi wa vyama vya michezo kutokuwa wakweli hasa katika masula ya mapato na matumizi, lakini yote hayo yamefumbiwa macho na BMT ambayo tuliitegemea kama mkombozi wetu katika michezo.
Uozo ndani ya vyama umekithiri ili hali wanaoathirikia ni wanamichezo imefikia mahali hata misaada inayotolewa na wahisani kwa ajili ya kusaidia timu zetu inaishia mikononi mwa wachache ambao wanajiita viongozi wa michezo, lakini hadi leo hii yale tuliyoahidiwa kwamba yatakomeshwa hata mfano wake haujaonekana.
Kwa bahati nzuri Malinzi alikuwa kiongozi wa Gofu kabla ya kuwa mwenyekiti wa BMT hivyo anaelewa vizuri yanayotendeka nyuma ya pazia.
Mwaka mmoja mlioahidi kwa ajili ya mabadiliko inazidi kuyoyoma na sasa mmebakiwa na miezi tisa kwa ajili ya ile ahadi ya michezo ya manufaa kwa taifa ndani ya vyama zaidi ya 40.
Tunahitaji kutimiza zile ahadi kama tunataka kuona watanzania wanapata kile walichotarajia katika michezo yetu, suala la kujuana na kuoneana aibu limepitwa na wakati tufanye kazi kwa kuzingatia maslahi ya taifa na wanamichezo wetu kwa kutimza ile ahadi mliyoitoa.
Pia, waziri Dk Nchimbi anatakiwa kuhakikisha BMT, inapewe nguvu zaidi kifedha ili liweze kuvisaidia vyama hivi, lakini pia liwe na nguvu ya kutengua mamlaka ya viongozi ambao siyo waadilifu katika vyama hivi vya michezo.
BMT ni kama ipo haipo kwa kuwa haijaving'ata vyama, BMT haijakwenda ndani ya vyama kuona matatizo ni nini, na kubakia ofisini kulinda mafaili ya vyama.
Ninaamini hatutaweza kupata maendeleo ya kweli ya michezo nchini kama serikali haitaliboresha BMT iwe na ofisi za kisasa na kuliwezesha kuwa chombo kikuu cha kusimamia michezo kiutendaji kwa kulipa fedha za kutosha katika bajeti ya kila mwaka.

UWANJA WA KAMBARAGE MKOANI SHINYANGA WAGEUKA PORI

Wananchi wakifyeka uwanja kabla ya mpambano kuanza... HATARI KWELI KWELI !!!

Avital Makelele -SHINYANGA
Karibu wiki nzima mkoa wa shinyanga ulikuwa unasubiri mpambano wa kimataifa kati ya timu ya TOTO Africa ya jijini mwanza inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara dhidi ya ABUJA FC kutoka nhini Nigeria.
What happened watu wengi sana waliweza kujitokeza kutazama mpambano huo nikiwa mmoja kati yao,kufika katika lango kuu la kuingilia uwanja wa CCM Kambarage unaomilikiwa na chama tawala.mamia ya watu walikiwa nje wakisubiri kuingia ndani.nikajaribu kuuliza nini kinaendelea na kuambiwa kuwa uwanja unafyekwa nilishangazwa sana na habari hiyo.ikanibidi niingie ndani kwa kulazimisha na hatimae nikashangazwa na hali niliyoikuta.

Nikiwa kama mtanzania,kijana na msomi wa level ya chuo kikuu nimepata maswali na yanaitaji majibu:
Je uwanja una meneja? Ni kweli yupo na ninamfaham anaitwa MFANGA na ni kada wa chama kinachomiliki uwanja.anafahamu majukumu yake na baadae aliweza kuja akiwa kavaliam nguo za chama,tena bila aibu.
Je cha mpira wa miguu mkoa na wilaya vina taarifa na ziala hiyo?
je maandalizi yalifanyika?
Am not sure na hiyo timu kama ni kweli inatoka ABUJA-NIGERIA.
Toto Africa nusu ya wachezaji tunaowafaham ndo walikuwepo but sitaki kuliongelea sana kwa sababu sina facts.
My comments:
UMEFIKA WAKATI WA KUFANYA MABADILIKO,WANA SHINYANGA WABADILIKE KWA KUTAFUTA UONGOZI WA CHAMA CHA SOKA MKOANI.SIASA HAIFAI KATIKA SOKA KAMA TUNATAKA KUFIKA MBALI.LIGI KUU TUTAKUWA TUNAISIKIA TUU,TUNAITAJI KUWA NA TIMU YA LIGI KUU,TUTAWEZA KAMA WANASHINYANGA WAKIWA TAYARI KUBADILIKA.