Search This Blog

Tuesday, January 3, 2012

YANGA WADUNGWA NA MAFUNZO, HUKU AZAM WAKING'ARA KTK MAPINDUZI CUP.


Azam FC wameanza vyema michuano ya Mapinduzi Cup kwa kuichapa goli 3-1 Kikwajuni FC, wakati Mabingwa wa Tanzania Yanga wakichapwa goli moja bila majibu toka kwa Mafunzo FC.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa saa kumi na nusu alasiri katika uwanja wa Aman, Azam FC walikuwa wakwanza kupata goli kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 13 kabla ya kumtengenezea John Boko goli la pili na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa Azam FC kuwa mbele kwa magoli 2-0.

Khamis Mcha Viali alihitimisha kalamu ya magoli kwa kuiandikia Azam FC goli la 3 katika dakika ya 75, kabla ya Kikwajuni kujipatia goli la kufutia machozi kwa mpira wa adhabu uliopigwa kwa ufundi mkubwa katika dakika ya ya 82.

Katika mchezo wa pili katika uwanja huo ulishuhudia Yanga wakijifunza soka toka kwa Mafunzo, baada ya kukubali kufungwa goli moja katika dakika 15 za mwisho.

Kwa matokeo hayo ya leo Azam wanakwea katika usukani wa kundi B, wakati Mafunzo wakishika nafasi ya 2 na Yanga nafasi ya 3 wakati Kikwajuni ikishika mkia.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Simba wanatarajia kuteremka kesho katika michezo ya kundi A katika uwanja wa Amana visiwani Zanzibar.

2 comments:

  1. Papic alisema timu haiko tayari kuingia mshindanoni wenyewe wakabisha wameipeleka ngoja wakiune cha mteme kuni hapo azam atajipigia ka sita ivi
    chela wa dom

    ReplyDelete
  2. mambo bado kwa yanga maana ndio kwanza professor papic amepewa timu hivyo lazima apewe muda, tatizo watanzania tunapenda kulipua ndio maana soka inatushinda, lazima tujue soka is the slow growing process like a human being, you can't guess the development without plan, so we have to set our goals in soccer before thinking of archievement in club, national and international wise . thanks yours passerby.

    ReplyDelete