Search This Blog

Saturday, November 5, 2011

TZ PREMIER LEAGUE: MABAO 185 YAFUNGWA, NGASSA AWEKA REKODI YA BAO LA MAPEMA ZAIDI.

RnkTeamMPWDLGFGA+/-Pts
1Simba SC138412181328
2 Young Africans138322091127
3 Azam13652125723
4 JKT Oljoro13652106423
5 Mtibwa Sugar136431712522
6 JKT Ruvu133821514117
7 Kagera Sugar133731312116
8 Moro United133551823-514
9 African Lyon133551116-514
10 Toto African132741416-213
11 Ruvu Shooting132741113-213
12 Coastal Union133281118-711
13 Polisi Dodoma131661015-59
14 Villa Squad131481026-167Mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara ulioanza kitimua vumbi Agosti 20, mwaka huu ilifika tamati katikati ya wiki, huku mabao 185 yakifungwa katika michezo 91.Simba na Yanga zikiendelea kuonyesha ukongwe kwa kushikilia nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.Timu hizo zinalingana mechi za kushinda, ambapo kila mmoja amezoa pointi tatu mara nane.
Simba imepoteza mmoja dhidi ya mtani Yanga na kutoka sare mitatu dhidi ya Kagera (1-1), Toto African (3-3) na Moro United (3-3).Watani Yanga wamepoteza miwili dhidi ya JKT Ruvu (1-0) na Azam FC (1-0) na kutoka sare mitatu dhidi ya Moro United (1-1), Mtibwa Sugar (0-0) na Ruvu Shooting (1-1).


Vibonde kwenye hatua hiyo, walikuwa timu za Villa Squad na Polisi Tanzania zimeshinda mechi moja tu. Polisi ilishinda Moro United mabao 5-2 na Villa ilionja ushindi pekee dhidi ya Polisi Tanzania kwa mabao 2-1.Washambuliaji John Boko 'Adebayor' wa Azam FC na Mghana Kenneth Asamoah wanafukuzana kwa kupachika mabao ikiwa kila mmoja ameifungia timu yake mabao nane.


Mshambuliaji Juma Semsue wa Polisi Tanzania ndiye aliyeweza kufunga mabao matatu katika mechi moja dhidi ya Moro United katika ushindi wa mabao 5-2.Katika hatua nyingine, kadi 21 nyekundu zimetolewa na waamuzi wa ligi hiyo. Villa Squad inaongoza kwa kuwa na wachezaji wanne.


Kiungo, Emmanuel Swita ameibuka kinara wa kulimwa kadi hizo katika mechi dhidi ya Mtibwa, Polisi na Kagera .
Timu za JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Coastal Union na Polisi Tanzania zimeonyesha nidhamu baada ya kumaliza mzunguko bila kuwa na kadi nyekundu.


Penalti 22 zimetolewa kwenye mzunguko wa kwanza, 15 zikifungwa na zingine kuota mbawa.Hata hivyo, Mrisho Ngassa wa Azam FC ameweka rekodi kwenye ng'we hiyo kwa kufunga bao la mapema zaidi. Alifunga bao katika sekunde ya 36 ya mchezo dhidi ya JKT Ruvu. Azam ilishinda 2-0.


Naye Abdallah Juma wa Ruvu Shooting ndiye mchezaji aliyefunga bao la kwanza msimu huu dhidi ya Kagera katika dakika ya tatu ya mchezo.


Lakini Hussein Sued wa Kagera Sugar, alijibu mapigo kwa kufunga bao la kufunga pazia hilo dhidi ya Coastal iliyolala bao 1-0.


Uwanja wa Kaitaba, Kagera umeweka historia ya kuwa wa mwisho kuchezwa mechi ya mzunguko wa kwanza.MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA SIR ALEX FERGUSON NDANI YA MANCHESTER UNITED


Ilikuwa November 8, 1986, at the Manor Ground, Oxford.

Tarehe na mahali Alex Ferguson ambapo Sir Alex Ferguson anapakumbuka vizuri sana.

“Nitaweza vipi kusahau mahala pale?” alisema wiki hii.

“Ulikuwa ni mchezo wa kwanza nikiwa katika benchi United na tulifungwa 2-0. Nilijisemea mwenyewe: “Oh , Yesu mkubwa, nimechagua kazi sahihi…’

Ferguson aliichukua Manchester United ikiwa katika wakati mgumu zaidi kisoka, chini ya utawala wa kisoka wa Liverpool FC. Klabu ikiwa na thamni isiyozidi £20m., lakini sasa United ndiyo klabu iliyofanikiwa zaidi katika historia ya soka nchini England na duniani.United sasa ndiyo inatajwa kuwa klabu ya michezo maarufu zaidi duniani ikikadiriwa kuwa mashabiki zaidi ya millioni 350 huku ikitajwa kuwa ndiyo klabu ya soka yenye thamni zaidi valued at £2billion.

Mafanikio yote haya yamepatikana chini ya uongozi imara na uliotukuka wa Sir Alex Ferguson.

Leo hii Ferguson anatimiza miaka 25 akiwa katika benchi la Manchester United.

TAKWIMU ZA SIR ALEX FERGUSON @ MANCHESTER UNITED


BIGGEST WINS

March 4, 1995 Ipswich (h) 9-0

Feb 6, 1999 Nottm F (a) 8-1

Oct 25, 1997 Barnsley (h) 7-0

Aug 28, 2011 Arsenal (h) 8-2

Apr 10, 2007 *Roma (h) 7-1

(All Prem, except *Champs League)

BIGGEST DEFEATS

Oct 23, 2011 Man City (h) 1-6

Oct 3, 1999 Chelsea (a) 0-5

Oct 20, 1996 Newcastle (a) 0-5

Sept 23, 1989 Man City (a) 1-5

Nov 30, 2010 *West Ham (a) 0-4

(All Prem, except *Carling Cup)

MOST WINS

1 Tottenham P58 W37

2 Everton P54 W34

3 Aston Villa P56 W34

4 Southampton P45 W29

5 Arsenal P68 W28

MOST DRAWS

1 Chelsea P65 D23

2 Arsenal P68 D19

3 Aston Villa P56 D15

4 Liverpool P59 D14

5 Tottenham P58 D13

MOST DEFEATS

1 Arsenal P68 L21

2 Chelsea P66 L19

3 Liverpool P59 L18

4 Everton P54 L9

5 Man City P43 L9

MOST GOALS SCORED

1 Tottenham P58 G101

2 Arsenal P68 G95

3 Southampton P45 G94

4 Chelsea P66 G92

5 Everton P54 G91

· AArsenal ndiyo klabu inayoongoza kwa kuifunga Manchester United chini ya uongozi wa Ferguson, wakiwafunga mara 21.

· Tottenham Hotspur ndiyo timu iliyofungwa zaidi na Manchester United chini ya uongozi wa Fergie, wakifungwa mara 37.

· Pia Spurs ndiyo timu iliyoruhusu nyavu zake kuguswa mara nyingi na United chini Fergie, wakiwa wamefungwa magoli 101.

· Chelsea nao wamefanikiwa kupata matokeo ya sare na United ya Fergie kuliko timu yoyote ya England, wakipata sare katika mechi 23.

· Manchester City ndiyo klabu iliyompa kipigo kikubwa Ferguson kuliko timu yoyote in England, baada ya kuitandika United mabao 6-1 mwezi uliopita.

· Ushindi mkubwa zaidi kwa Sir Alex Ferguson katika uongozi wake ndani ya United ulikuwa ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Ispwich Town, mwaka 1995, mwezi 3 katika premier league.