Search This Blog

Saturday, April 20, 2013

LIVE MATCH CENTRE: AZAM FC 0 - 0 AS FAR RABAT FULL TIME

Dk 90+5 FULL TIME Azam 0-0 Rabat.

Dk 90+4 Tchetche wa Azam anaichambua ngome ya Rabat na kupia shuti kali linalotoka juu kidogo ya lango la Rabat. Azam 0-0 Rabat.

Dk 90+2 Youssef Anouar wa Rabat anaichambua ngome ya Azam lakini anapiga shuti hafifu linalookolewa.

Dk 89 Rabat wanafanya mabadiliko ametoka Abderrahim Achchakir ameingia Mostapha El Yousfi.

Dk 86 John Bocco wa Azam anapiga shuti kali langoni kwa Rabat lakini anaudaka mpira. Azam 0-0 Rabat

Dk 83 Bolou wa Azam anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kuonyesha mchezo usiofaa.

Dk79 Rabat imefanya mabadiliko ametoka Salaheddine Aqqal ameingia Soufiane Alloudi.

Dk 77 Azam inafanya mabadiliko ametoka Khamis Mcha ameingia Gaudence Mwaikimba.

Dk 73 Abderahim Achchakir wa Rabat anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo mbaya. Azam 0-0 Rabat.

Dk 71 Mustapha Murani wa Rabat anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Michael Bolou wa Azam.

Dk 65 Tchetche wa Azam anapiga shuti kali linalogonga mwamba wa kulia wa Rabat na kurudi uwanjani. Azam 0-0 Rabat

Dk 59 Mustapha Allaoui wa Rabat anaanguka akiwa peke yake katika lango la Azam. Mpira unasimama na Mustapha anatibiwa.

Dk 54 Azam wamekuja kwa kasi na kuwashambulia Rabat kila mara.

Dk 52 Kipre Tchetche anakosa bao la wazi

Dk 52 Kipre Tchetche anakosa bao la wazi

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA

Dk 45 HALF TIME

Dk 44 Rabat wanafanya shambulizi kali langoni kwa Azam lakini mpira unaokolewa na kuwa kona butu.

Dk 40 Mpira umechangamka lakini safu za ushambuliaji za timu zote hazipo makini. Azam 0-0 Rabat

Dk 30 Azam Fc 0 - 0 AS Far Rabat

Dk 20 Bado timu zinashambuliana kwa zamu huku umakini ukikosekana katika umaliziaji.

Dk 10 Azam Fc 0 - 0 AS Far Rabat

Mpira umeanza uwanja wa Taifa Azam FC vs AS Far Rabat

Dk 5 Timu zinashambuliana kwa zamu

Friday, April 19, 2013

UBINAFSI WA REAL MADIRD NA BARCELONA WAVIFANYA VILABU VINGINE VYA LA LIGA KUDAIWA KODI NA SERIKALI ZAIDI YA $870 MILLION

Malaga moja ya timu zinazoongoza kwa madeni na zipo kwenye hatari ya kufilisika
Vilabu vya soka vya Spain vinadaiwa kodi na serikali ya nchi hiyo inayokadiriwa kufikia 670 million euros ($874 million), limesema baraza la michezo la nchi hiyo juzi Alhamisi.  

Rais wa baraza hilo Miguel Cardenal alisema kiasi cha kodi ambacho vilabu vinadaiwa na serikali kimeshuka kutoka 750 million euros ($979 million).
Cardenal aliiambia radio taifa ya Spain kwamba kupungua kwa deni hilo ni jambo zuri lakini vilabu vinabidi vitafute namna nzuri ya kugawana mapato ya haki za matangazo ya TV ili vijihakikishie kuepukana na shida za kiuchumi. 

UEFA wameifungia Malaga kushiriki mashindano ya ulaya kwa msimu mmoja kwa kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji na kulipa kodi kwa muda - adhabu hiyo ikiwa moja ya njia ya kuilazimisha klabu hiyo kutimiza wajibu wake. 
 
Cardenal alisema kwamba wanataarisha sheria ya kuvilazimisha vilabu kuuza haki za matangazo za mechi kwa umoja, badala ya umimi uliopo kwenye biashara hiyo hivi sasa.

  Mwaka 2011, Real Madrid na Barcelona wote waliingiza kiasi 140 million euros kila mmoja, huku timu iliyowafuatia Atletico Madrid ikiingiza 50 million euros.

NADIR HAROUB ASHINDWA KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUIFUNGIA YANGA MABAO 16


Beki mahiri wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema huenda akashindwa kufikisha idadi ya mabao ambayo alijiwekea kufunga ingawa amekiri kufikisha nusu yake.
Nahodha huyo msaidizi wa Yanga alijiwekea malengo ya kufunga mabao 16 hadi msimu wa ligi utakapomalizika na kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa.
Lakini hadi sasa, Yanga ikiwa imesaliwa na mechi tatu kabla ya kumalizika kwa ligi, mlinzi huyo wa kati amefunga mabao manne sawa na beki Mnyarwanda Mbuyu Twite.
Cannavaro alisema jijini Dar es Salaam kuwa hajui kama ataweza kufikisha idadi hiyo ingawa atahakikisha nusu yake yanafika na kuiwezesha Yanga kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu huu.
"Nilijipangia kufunga mabao 16 hadi ligi itakapomalizika. Lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nafikiri itakuwa vigumu kutimiza ahadi hiyo."
"Mechi zimebaki tatu kabla ya kumalizika kwa ligi alafu nimefunga mabao manne tu."
"Nadhani inakuwa ngumu kwangu kufikisha idadi hiyo wakati tukiwa na mechi tatu." alisema mlinzi huyo alisiyekubali kushindwa.
Beki huyo amekuwa akitumia zaidi kichwa chake kupachika mabao akiunganisha mipira ya kona na faulo.

EXCLUSIVE: HARUNA NIYONZIMA AFANYIWA UPASUAJI LEO HII


Kiungo mahiri wa Yanga, Haruna Niyonzima leo Ijumaa amefanyiwa upasuaji wa kipele kwenye pua yake ingawa daktari wa timu hiyo Nassoro Matuzya amesema hauweza kuathiri utendaji wake wa kazi.
Matuzya alisema jijini Dar es Salaam kuwa kiungo huyo alifanya mazoezi asubuhi na wenzake, lakini baadaye alimtaka kwenda kujiandaa kwa ajili ya upasuaji huo mdogo.
"Ni kweli leo asubuhi Haruna (Niyonzima) tumemfanyia upasuaji mdogo wa kipele kwenye pua yake katika hospitali ya Mwananyamala."
"Kipele hicho kilimtokea kwenye pua yake. Hakikuwa sehemu nzuri, kwa hiyo tumelazimika kumfanyia upasuaji huo mdogo."
"Kidonda hicho hakiwezi kuathiri utendaji wake wa kazi. Kesho (leo) ataendelea na mazoezi kama kawaida na wenzake kujiwinda na mchezo wa JKT Ruvu." alisema Matuzya.
Alisema kidonda cha upasuaji huo kitakuwa kimepona mara baada ya saa 48 ambazo ni sawa na siku mbili.
"Hadi kufika Jumapili atakuwa hana tatizo lolote. Nafikiri suala la kucheza linabaki kwa mwalimu wa timu." alisema daktari huyo

VAN PERSIE, BALE, SUAREZ, CARRICK, HAZARD NA MATA - NANI KUWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA ENGLAND???

Hatimaye leo imetangazwa rasmi listi ya wachezaji ambao wanagombania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza - Man United imetoa wachezaji wawili, kiungo Micheal Carrick  na Robin Van Persie, Luis Suarez anaiwakilisha Liverpool, Gareth Bale, Juan Mata na Eden Hazard wakiliwakilisha jiji la london. Mabingwa watetezi Manchester City hawajatoa mchezaji hata mmoja katika listi hiyo iliyotangazwa leo.

Michael Carrick (Manchester United)
Gareth Bale (Tottenham Hotspur)
Robin van Persie (Manchester United
Luis Suarez (Liverpool)
Eden Hazard (Chelsea)
Juan Mata (Chelsea)


Washindi wa miaka iliyopita
2011-12: Robin van Persie (Arsenal)
2010-11: Gareth Bale (Tottenham)
2009-10: Wayne Rooney (Man Utd)
2008-09: Ryan Giggs (Man Utd)
2007-08: C Ronaldo (Man Utd)

BAADA YA MASHABIKI WAKE KUFANYA VURUGU UWANJANI - TIMU AEK ATHENS YASHUSHWA DARAJA

Moja ya klabu kongwe na kubwa nchini  Ugiriki AEK Athens imeshushwa rasmi daraja katika ligi kuu ya Ugiriki baada ya kukatwa pointi 3 kutokana na vurugu zilizofanywa na mashabiki wa klabu wikiendi iliyopita. 
 
Bodi ya nidhamu ya shirikisho la soka la Ugiriki lilikaa mapema leo na kutoa maamuzi hayo na pia timu pizani iliyokuwa inacheza nayo Panthrakikos imepewa ushindi wa 3-0.

Mashabiki wa AEK waliingia uwanjani baaada ya timu yao kuwa nyuma kwa 1-0 na mchezo ukasimamishwa kwenye dakika ya 88.

Huku wakiwa wamebakiwa na mchezo mmoja, adhabu ya kukatwa pointi 3 inamaanisha AEK itamaliza wapili kutoka chini hivyo kushuka daraja.

Timu hiyo pia imekatwa pointi 2 kwa msimu ujao na kupigwa faini ya $9,100.

ROONEY NA NAFASI YA KIUNGO NI SAHIHI?? MECHI DHIDI YA WEST HAM ALIPIGA PASI MOJA TU NDANI YA ENEO LA HATARI LA WAPINZANIWayne Rooney ni mshambuliaji au kiungo ndani ya kikos cha Manchester United siku hizi za hivi karibuni? 

Wengine wanasema ikiwa Rooney anataka kuendelea kuwa na nafasi ya kikosi cha kwanza ndani ya United inabidi arudi kucheza kwenye kiungo akiziba nafasi ya Paul Scholes kama ambavyo amekuwa akicheza kwenye michezo miwili iliyopita.

Huku wengine wakisema ikiwa United wameamua kufikia maamuzi ya kumuondoa kwenye jukumu la ufungaji basi siku zake ndani ya Old Trafford zinahesabika.

Vyovyote ilivyo - wakati mshambuliaji chaguo la kwanza la England amepiga pasi moja iliyoingia ndani ya eneo la hatari la wapinzani - kama ambavyo Rooney alifanya usiku wa juzi pale Upton Park - unaanza kupata shaka kwamba kuna kitu kisicho sawa.


Wayne Rooney touch map vs West Ham
Michael Carrick touch map vs West Ham
Picha hizi zinaonyesha movements zote na pasi alizotoa Wayne Rooney kwenye mchezo dhidi ya West Ham.

Alicheza vizuri sana dhidi ya Stoke jumapili iliyopita wakati Sir Alex Ferguson alipomchezesha nafasi ya kiungo. Lakini akaheza ovyo dhidi ya West Ham na kutolewa dakika 71 kumpisha Giggs United wakiwa nyuma kwa bao 2-1. 

Kama inavyoonekana kwenye picha Rooney akicheza kwenye kiungo anakuwa anarudi sana nyuma kwenye kukaba hivyo anakuwa hana tishio kwenye ushambuliaji - hapa kwenye picha ya chinitakwimu  zinayoonyesha namna Micheal Carrick ambaye anacheza nyuma zaidi yake alivyokuwa amepenyeza mipira mingi kwenye lango la wapinzani kuliko Rooney ambaye yeye alicheza juu.
 

SEHEMU YA MAGARI YANAYOMILIKIWA NA MASTAA WA MICHEZO NA MUZIKI AKIWEMO MESSI, RONALDO, TIGER, BALOTELLI, T.I , RICK ROSS NA WENGINE

 
Mario Balotelli
Mario Balotelli
Magari ya Chris-Brown yakiwa nje nyumbani kwake.
Magari ya Chris-Brown yakiwa nje nyumbani kwake.
David Beckham
David Beckham
El Hadj Diof
El Hadj Diof
Ya Floyd-Mayweather
Bondia Floyd-Mayweather
ferrari ya Kanye West na Kim K
ferrari ya Kanye West na Kim K
Kim-Kardashian-Rolls-Royce
Kim-Kardashian-Rolls-Royce
Frank Lampard wa Chelsea.
Frank Lampard wa Chelsea.
Lionel-messi
Lionel-messi
Messi
Messi na Maserati
Messi
Messi
Messi
Messi
Messi
Messi
Messi
Messi
Rapper Meek-mill-aston-martin
Rapper Meek-mill-aston-martin
Meek Mill Aston Martin
Meek Mill Aston Martin
Luis Nani Lamborghini gallardo
Nani Lamborghini gallardo
Obafemi Martins Lamborghini-Murcielago
Obafemi Martins Lamborghini-Murcielago
P-Diddy na Maybach yake
P-Diddy na Maybach yake
Diddy na Maybach yake
Diddy na Maybach yake
Rick Ross
Rick Ross
Rick Ross
Rick Ross
Rick Ross
Rick Ross
Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo
Wyne Rooney Aston Martin
Wyne Rooney Aston Martin
T.I kwenye Ferrari
T.I kwenye Ferrari
T.I NA Ferrari
T.I NA Ferrari
Tiger Woods
Tiger Woods
Will.i.am kwenye McLaren
Will.i.am kwenye McLaren
Rapper Young Jeezy na Bentley
Rapper Young Jeezy na Bentley

Kwa hisani ya mtu wangu wa nguvu: millardayo.com

MCHEZAJI ANAYECHEZEWA FAULO ZAIDI BARANI ULAYA MSIMU HUU - SIO MESSI WALA RONALDO - NI DIAMANTI

Hakuna shaka kwamba Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekuwa wakichezewa rafu sana timu pinzani dimbani, lakini hakuna hata mmoja kati yao anayefikia kuwa mchezaji ambaye anafanyiwa madhambi mengi kuliko brani ulaya msimu huu. 

Kwa mujibu wa kampuni inayokusanya data za kimichezo ya Opta, mchezaji anayechezewwa rafu nyingi kuliko wote ndani ya bara la ulaya msimu huu ni kiungo wa timu ya Serie A  Alessandro Diamanti.

Kama takwimu zinavyoonyesha hapo chini Diamanti amechezewa faulo mara 123 msimu huu, wakati Messi na Ronaldo wakiwa wamechezwa faulo mara zisizozidi 75 kila mmoja. Kiufupi wachezaji hawa wanaotajwa kuwa bora ulimwenguni kwa sasa hawapo hata kwenye top 5. Mchezaji wa Wolfsburg Diego ndio mchezaji mwingine ambaye kidogo anamsogolea Diamanti akichezewa rafu mara 100, wakati kiungo mwenye miaka 36 Francesco Totti akishika nafasi ya nne. 

 LISTI KAMILI YA WACHEZAJI WANAOCHEZEWA RAFU ZAIDI BARANI ULAYA MSIMU HUU


 Diamanti, mwenye miaka 29 kwa sasa alicheza msimu mmoja pale West Ham mwaka juzi, amekuwa kwenye kiwango kizuri kwa timu yake ya Bologna, huku akifanikiwa kuitwa timu ya taifa ya Italia iliyoshiriki Euro 2012 na kufika fainali.


)

MARIO BALOTELLI AWAFUNIKA MESSI, RONALDO NA BECKHAM KWA KUTAJWA KUWA NDIO MWANASOKA MWENYE USHAWISHI MKUBWA ZAIDI DUNIANI


Mario Balotelli amekuwa ndio mwanasoka pekee kutajwa kwenye listi ya watu mashuhuri ya jarida la Time kwa mwaka 2013. Listi hiyo ambayo iliwahi kuwaingiza wansoka kama Beckham, Drogba, Messi na wengine huko miaka ya nyuma mwaka huu wote wametoswa na mtoto mtukutu Balotelli amekula shavu la kuwemo kwenye listi hiyo ambayo imewajumuisha wasanii kama Jay Z, , Beyonce, huku wanamichezo wakiwa wanne tu Balotelli, Lebron James, Lindsey Vonn na mcheza Tennis Li Na.

Baada ya kutangazwa kwa listi hiyo gwiji wa soka wa Italia na Chelsea ambaye kwa sasa ni manager wa Watford Gianfranco Zola, alizungumzia Balotelli kwa kusema:
"Kwa mbali, watu wanaweza kudhani kichaa, lakini Mario ni kijana mzuri mwenye upendo na mcheshi. Ninakuhakikishia nimekuwa nikijisikia amani kila ninapokutana nae. Amerudi Italia akitokea England akiwa kama mshindi huku akiwa na nyota ya mvuto. Sasa anapaswa kutulia na kuwa mfano bora, anapenda presha, lakini ili kufanikiwa inabidi ajue namna ya kuidhibiti." Alisema Zola.

HATIMAYE LIONEL MESSI ATUMA JEZI YAKE KWA PAPA FRANCIS - ANGALIA NAMNA ILIVYOPOKELEWA NA PAPA MWENYEWE

Wote ni raia wa Argentina. Wote wanapenda mchezo mzuri. Na sasa wote wanamiliki jezi ya mchezaji bora wa dunia Lionel Messi.

Imerekodiwa video kwenye maeneo ya Vatican juzi Jumatano ikimuonyesha Padri wa Vatican akimkabidhi Papa mpya wa kanisa katoliki - Papa Francia jezi iliyosainiwa na Messi wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Papa huyo mpya na wana Vatican.

Baada ya kubusu mikono ya kiongozi wake, padri Miguel Delgado Galindo alimkabidhi Pope Francis jezi ya Messi ambayo ilionekana kumfarahisha sana kiongozi huyo mpya wa kanisa katoliki duniani. 

Hii ilikuwa jezi ya pili ya timu ya soka ambayo Papa aliipokea ndani ya wiki hii, baada ya waziri mkuu wa Spain Mariano Rajoy kumkabidhi Papa Francis jezi ya Hipania mapema wiki hii.

VIDEO

HAYA NDIO MABILIONI YA SHILINGI WANAYOINGIZA VILABU VYA NJE KUPITIA MIKATABA NA MAKAMPUNI YA UTENGENEZAJI WA VIFAA VYA MICHEZO - SIMBA NA YANGA VIPI??
Manchester United na Liverpool ndio timu zenye udhamini mnono wa seti nzima ya mavazi ya kimichezo katika premier league msimu huu - Liverpool wakiingiza kiasi cha £25m na United wakipata £25.4m kutoka na kwa kampuni za Nike na Warrior - lakini bado mafahari hao wawili wa England wapo nyuma ya mafahari wa  Real Madrid na Barcelona.
Mkataba wa Real na adidas, ambao unaisha mwaka 2020, unakadiriwa kuwa na thamani ya £31m kwa mwaka wakati Barcelona wakiingiza £27m kwa mwaka kutoka kwa Nike. 


Chelsea wanashika nafasi ya nne wakiingiza £20m kutoka kwa adidas, Bayern Munich wanafuatia wakiwa mbele ya Inter Milan, Manchester City, AC Milan na Juventus. England imeingiza timu nne kwenye listi ya vilabu vyenye mikataba minono na kampuni za utengenezaji wa vifaa vya michezo, wakati Spain kama kawaida ikiingiza timu mbili - Ujerumani moja, na Italia ikiingiza timu 3.Wakati tumeshuhudia vilabu ambavyo ni mfano kwetu hapa nchini vilabu vyetu vikubwa hakuna hata kimoja chenye mkataba na kampuni yoyote ya maana ya utengenezaji wa vifaa vya michezo. Kulwa na Doto zenye mamilioni ya mashabiki zimebaki kuwa maskini huku wakiishia kupewa vifaa vya michezo vyenye nembo ya moja ya kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo bila kuambulia chochote kupitia promotion wanayoifanyia kampuni hiyo husika. Huku kampuni hiyo ikiwa inafyatua jezi za timu hizo na kuziuza kisha kutengeneza faida kubwa huku vilabu vyetu vikiambulia patupu. 
Wapenzi wa Simba na Yanga wakinunua jezi feki za timu zao

Viongozi wa vilabu vyetu fuateni mfano bora wa timu kama Real, Barca na United na kuhakikisha timu zenu zinapata kile kinachostahili kupitia kuitangaza kampuni ya vifaa inayotengeneza karibia jezi za timu zote zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania.

Thursday, April 18, 2013

NGUMI KUPIGWA CHALINZE

Mabondia Mwaite Juma,Cosmas Kibuga na Shabani Kaoneka ni baadhi ya mabondia wa Dar es salaam watakaokwenda Chalinze kuhamasisha ngumi za kulipwa wilayani humo kwa kuzipiga na mabondia wakali wa Chalize.
Kampuni inayoandaa mapambano kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya mabondia chipukizi ya Bigright Promotion, imeandaa pambano hilo ili kutanua wigo wa michezo nchini kwa kuanzia kutembelea wilaya zinazohamasika kimichezo ikiwemo wilaya ya Chalinze.
Tumeamua kuifanyia Chalinze kwa sababu tunataka iwe ndio mfano kwa kuandaa pambano hili ambalo litawakutanisha chipukizi wakali wa Dar na wakali wa Chalinze,pia kutakuwepo na mapambano mengine yenye ushindani wa hali ya juu na vituko kama vile la Pius puto atakaezipiga na iddi mkatatiketi -hawa ni mbabe wa sokoni na mbabe wa stendi watazipiga kumaliza ubishi wao uliotanda kwa muda mrefu.

 ukiondoa pambano hilo Minyusi abdala atazipiga na shaban kaoneka, Baraka nuhu"chalinze hamjambo" atazipiga na goodluck suleiman, alex kdo atazipiga na herman shekivuli, iddi mwera atazipiga na ramadhan misugwa na mapambano mengineyo mengi likiwemo la ustadh mwenye msimamo mkali ustadh Kurasheni aliyeahidi kuchinja kama anachinja kondoo ulingoni atakaezipiga na makali wa bodaboda mzee kachacha.mgeni rasmi wa pambano hilo atakuwa ni diwani wa  Chalinze bwilingu bw naser Karama ambaye muda wote amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kushiriki michezo na ametoa basi kubwa kwa ajili ya mashabikitoka daresslaam kwenda kushangilia na kurudi.
wakati huohuo diwani Karama anategemea kujenga ukumbi mkubwa wa ngumi hapo chalinze, hivyo ngumi zote za kimataifa zitakuwa zikipigwa hapo

WATANZANIA WASHINDWA KUFANYA VIZURI KIPINDI CHA TANO CHA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

 Washindi wa kipindi cha tano cha Guinness Football Challenge Ken Muturi (kushuto) na Chis Mwamgi(kulia) wakishangilia ushindi walioupata huku wakiwa wamebeba pesa taslimu walizojishindia katika shindano hilo jana usiku na pembeni ni mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho Lary Asengo(anayepiga makofi kulia).
Washindi wa kipindi cha Tano cha Guinness Football Challenge, Chris Mwamgi(kushoto)  na Ken Muturi(kulia) katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego and    Flavia Tumsiime jana baada ya ushindi.


 Jana usiku kupitia Televisheni za ITV na Clouds TV timu ya Tanzania ilishindwa kutumia nafasi ya kipindi cha mwisho cha mashindano ya “Guinness Football Challenge” katika hatua ya Afrika Mashariki baada ya kutolewa na timu kutoka Kenya. Rangi nyekundu imeonekana kuwa ni rangi ya bahati kwa timu za Kenya kwani hii ni timu ya nne kutoka Kenya kufanikiwa kufuzu kuingia hatua ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGETM. Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi ndio walioibuka washindi jana usiku kwani walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta  wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola za kimarekani  1,500.

Ni vipi Kenneth na Chris wataweza kumudu hatua ya Pan-African? Sasa wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano ya Pan-African ambapo watakutana na wawakilishi pekee kutoka Tanzania, Daniel Msekwa na Mwalimu, washiriki kutoka Uganda Alex Muyobo na Ibrahim Kawoova pamoja na wenzao kutoka Kenya,Francis Ngigi na Kepha Kimani(washindi wa kipindi cha 2), Kenneth Kamau na Wills Ogutu(washindi kipindi cha 3) na Ephantus Nyambura na Samuel Papa(washindi kipindi cha 4).

Timu hizi tano zitakua uwanjani kutimiza malengo yao, ambapo watakutana uso kwa uso na washiriki kutoka Ghana na Cameroun kuonesha ni nani ana maarifa zaidi na ujuzi wa kusakata kabumbu,  hata kuvishwa ubingwa wa Pan-African na  kuondoka na dola za kimarekani 250,000.

Usikose kuangalia mashindano haya kupitia televisheni za ITV na Clouds TV huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.
                                                                                                                                         
Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.