Search This Blog

Friday, April 19, 2013

NADIR HAROUB ASHINDWA KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUIFUNGIA YANGA MABAO 16


Beki mahiri wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema huenda akashindwa kufikisha idadi ya mabao ambayo alijiwekea kufunga ingawa amekiri kufikisha nusu yake.
Nahodha huyo msaidizi wa Yanga alijiwekea malengo ya kufunga mabao 16 hadi msimu wa ligi utakapomalizika na kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa.
Lakini hadi sasa, Yanga ikiwa imesaliwa na mechi tatu kabla ya kumalizika kwa ligi, mlinzi huyo wa kati amefunga mabao manne sawa na beki Mnyarwanda Mbuyu Twite.
Cannavaro alisema jijini Dar es Salaam kuwa hajui kama ataweza kufikisha idadi hiyo ingawa atahakikisha nusu yake yanafika na kuiwezesha Yanga kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu huu.
"Nilijipangia kufunga mabao 16 hadi ligi itakapomalizika. Lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nafikiri itakuwa vigumu kutimiza ahadi hiyo."
"Mechi zimebaki tatu kabla ya kumalizika kwa ligi alafu nimefunga mabao manne tu."
"Nadhani inakuwa ngumu kwangu kufikisha idadi hiyo wakati tukiwa na mechi tatu." alisema mlinzi huyo alisiyekubali kushindwa.
Beki huyo amekuwa akitumia zaidi kichwa chake kupachika mabao akiunganisha mipira ya kona na faulo.

1 comment:

  1. Im glad with you el-captaine Nadir, Mungu akusaidie ktk utendaji wako!

    ReplyDelete