Search This Blog

Saturday, May 19, 2012

BAYERN YENYE SAFU KALI YA USHAMBULIAJI NA BEKI MBOVU DHIDI YA CHELSEA YENYE PENGO KUBWA LA RAMIRES: FAINALI ISIYOAMULIKA KIRAHISI

Ni fainali ambayo inatawaliwa na hadithi ya timu zote mbili kuwakosa wachezaji muhimu, Chelsea ikiwakosa wanne na Munich ikiwakosa watatu. 
Ni fainali inayofanyika kwenye uwanja wa nyumbani wa timu inayoshiriki mchezo wa fainali jambo ambalo linatokea kwa mara ya kwanza kwneye kizazi hiki .
Bayern Munich moja kwa moja wanaingia kwenye mchezo kama timu yenye nafasi kubwa ya kushinda . Ukiangalia baadhi ya factor nyingi za ushindi ziko upande wao. Ukiangalia wachezaji watakaowakosa ni tofauti na wale watakaokosekana na Chelsea. Munich itawakosa Luis Gustavo, David Alaba na Olger Badstubber. 
Moja ya matatizo makubwa ya Bayern Munich ni kwenye defense na hii ni kwa sababu tofauti na ilivyo Chelsea na timu nyingine toka England ambazo huanza kujengwa tangu nyuma kwenye defense, Bayern Munich ni timu ambayo imeanza kujengwa kwenye safu ya ushambuliaji ambako ndio hasa ilipo nguvu yake kuu.
Mario Gomez akisaidiwa na kina Toni Kroos,Thomas Mueller, Arjen Robben , Franck Ribery na Bastian Schweisteiger wote wamekuwa msaada mkubwa kwa Bayern wakati ikiwa inashambulia na ndio maana wakati mwingine mapungufu ya Bayern kwenye defense yanashindwa kuonekana. 
Hata hivyo defense ya Bayern Munich ambayo imekuwa kwenye wakati mgumu mara nyingi imekuwa ikisaidiwa na wachezaji watakaokosekana leo ambao ni Alaba, Badstubber na Gustavo .
Kukosekana kwa wachezaji hawa kutailazimu Bayern pengine kuwatumia Anatoly Tymoschuk ambaye ni midfielder mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kati , Philip Lahm huenda atatumika kwenye mojawapo kati ya pande mbili za safu ya ulinzi kwa maana ya kushoto au kulia huku Bastian Schweinsteiger akilazimika kushuka chini kucheza kama kiungo mkabaji .
Bayern ni timu ambayo ina mabao mengi ndani yake huku Mario Gomez akiwa katikati ya mipango yote ya ufungaji . Ukitazama takwimu za msimu huu a ligi ya mabingwa zinaonyesha kuwa Bayern Munich ni moja ya timu tatu zilizofunga mabao mengi tangu hatua ya makundi hadi kufika fainali .
Ukiitazama Chelsea ambayo itacheza leo ndio unapata taswira halisi ya jinsi walivyo kwenye wakati mgumu wakicheza na Bayern. Pengo la Ramires ni kubwa pengine kuliko mapengo ya wachezaji wote watakaokosekana kwenye line up ya Chelsea leo. Ukitazama kazi aliyoifanya ya kupunguza threat ya Dani Alves kwenye mchezo wa nusu fainali halafu jiulize umuhimu gani angekuwa nao kwa kumzuia mmojawapo kati ya Arjen Robben na Franck Ribery.
 Ukiachilia mbali kazi ya kukaba Ramires ametokea kurekebisha sehemu muhimu ya mchezo wake ambayo ni ufungaji wa mabao muhimu kama alivyofanya kwenye nusu fainali dhidi ya Barca na hata kwenye fainali ya kombe la FA .
Branislav Ivanovic naye atakuwa pengo kubwa sana kwa Chelsea. Ivanovic ni beki mwenye umuhimu wa aina yake kwa Chelsea hasa ukizingatia kuwa Terry hatakuwepo na Gary Cahill na David Luiz hawana match fitnesss . Bahati mbaya naye ni mchezaji mwingine anayeingia kwenye orodha ya watu watakaokosekana hii leo . Ukabaji wake wenye nidhamu ya ufundi hali wa jukumu la beki pamoja na mabao yake muhimu ambayo hufunga akipanda ni jambo ambalo linafanya kukosekana kwake kuwe mazingira magumu kwa Chelsea .
Raul Meireles ni jina lingine ambalo Chelsea italikosa, Meireles ni kiungo ambaye hutimiza jukumu analopangiwa na kocha na hulifanya kwa asilimia mia moja hamsini . Work Rate yake ni kubwa, na ana uwezo wa ziada ambao kocha yoyote huhitaji kwenye timu .
Wachezaji hawa watatu wanaifanya kazi ya Chelsea kuwa ngumu kwa kuwa wametokea kuwa misingi muhimu ya kikosi cha Chelsea chini ya Roberto Di Matteo ambapo timu hii imekuwa ikishinda mechi nyingi kwa kufanya kazi na kutumia nafasi chache ambazo zinapatikana .
Moja ya mambo ambayo yataamua mchezo wa fainali kwa Chelsea ni mfumo watakaotumia. Endapo wataamua kupaki basi kwa staili waliyoifanya dhidi ya Barca watadhurika kwa hakika kwa kuwa Bayern Munich ni timu ambayo haina matatizo ya kiufundi ambayo yanaonekana kuidhuru Barca . Bayern tofauti na Barca ina mpango mbadala pale mpango wake wa msingi unaposhindikana . Ukipaki basi  Bayern wanao wachezaji ambao watawatumia kwa kupiga mashuti ya mbali kama Schweisteiger, Kroos, Lahm na Thomas Mueller . Ukiamua kuwaelekeza mabeki au viungo wawili dhidi kucheza kwa kumkaba mmojawapo kati ya Robben na Ribbery Bayern watatumia shimo litakalobaki katikati ya uwanja kukudhuru na kama Chelsea watakuwa wakiokoa kwa kuwapa Bayern Umiliki wa mpira kwenye set pieces pia watadhurika kwa kuwa Bayern wanafunga kupitia ste pieces kwa kuwa wanae aina ya mshambuliaji ambaye Barcelona walimkosa ambaye ni Mario Gomez na hata Chelsea wakiridhika na kutafuta sare ili wajaribu bahati ya kwenye penati historia inaonyesha kuwa timu za ujerumani ni hatari sana kwenye penati kama walivyotambua Real Madrid kwenye nusu fainali.
 Hata hivyo Chelsea wamekuwa wakicheza vizuri wakiwa under pressure hasa kutokana na kuridhika kuwa under dog kwenye michezo kadhaa msimu huu.
Rudi kwenye mechi ya Barcelona na utagundua hilo. Haya yote hayamaanishi kuwa Chelsea hawana nafasi kwani bado wanae Didier Drogba ambaye ni mshambuliaji wa mechi kubwa . Wanaye Fernando Torres ambaye anabaki kuwa mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kuziona nyavu .
Itakuwa fainali ngumu na isiyoamulika kirahisi , dakika 90 zitaamua bingwa wa ulaya msimu .

ZANTEL MDHAMINI MPYA WA BONGO STAR SEARCH


Makamu wa Rais wa Kampuni ya Etisalat, Ahmed Mokhles akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampuni yao kudhamini shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search, kulia kwake ni mkurugenzi wa Benchmark Productions iyoandaa shindano hilo, Rita Poulsen.
Shindano la BSS mwaka huu litajulikana kama ‘Epiq Bongo Star Search’  ambapo mshindi atanyakua shilingi milioni 50,pamoja na zawadi nyingine kutoka Zantel, sambamba na mkataba wa kurekodi ili aweze kuendeleza kipaji chake baada ya shindano hilo. Aidha, mchakato wa mwaka huu utawahusisha washiriki kutoka  mikoa nane tofauti ikiwemo Zanzibar, Lindi, Mbeya, Mwanza, Arusha, Tanga, Dodoma na Dar es Salaam ambapo mchakato utaanza mwezi Juni.

IKIWA BAYERN WATABEBA KOMBE LEO HAPA NDIPO WATAKAPOSHEREHEKEA UBINGWA WAO



HII NI SEHEMU YA KUOMBA MATAMANIO YAKO YAKAMILIKE

MTANZANIA MULUMBU:CHELSEA WANA NAFASI KUBWA YA KUBEBA KOMBE LEO -ATOA USHAURI KWA WABONGO


Leo nimekutana mtanzania bwana Mulumbu ambaye nimepiga nae story tofauti kuelekea mechi ya leo usiku.


Shafih: Unauzungumziaje mchezo wa leo usiku kati ya Bayern vs Chelsea?



Mulumbu: Mchezo utakuwa mgumu sana lakini naipa nafasi Chelsea kwa sababu Bayern wana tataizo la defense, wanawakosa mabeki wao muhimu kama akina Alaba ambao wana uzoefu kiasi, pia waliopo kama replacement bado hawana uzoefu wa kupambana na deadly strikers kama Didier Drogba na Fernando Torres.



Shaffih: Chelsea nao watawakosa wachezaji wao muhimu kama John Terry, Ramirez na Meireles, huoni kama na wenyewe wana pengo kubwa?

Mulumbu: Utofauti kati ya Bayern na Chelsea kwa wachezaji, ni kwamba atleast kwa Chelsea wabadala kama wa akina Terry wana uzoefu, mtu kama Essien kila mtu anafahamu uwezo wake na uzoefu, David Luiz na Gary Cahil wamecheza kwenye level ya juu kwa muda mrefu sasa. Halfu kitu kingine Chelsea wataingia kwenye mchezo wakiwa wana presha ndogo sana ukiwafananisha na Bayern, hivyo hiyo ni advantage nyingine kwao.

Shaffih: Tangu nifike hapa nimegundua kwamba mashabiki wengi wa hapa wanaonekana kutoisapoti Bayern. Hii ni kwanini?

Mulumbu: Hapa Munich mashabiki wamegawanyika kutokana na timu zilizopo hapa, kama ilivyo nyumbani pale Dar es Salaam Uyanga na Usimba, na hapa kuna timu mbili kubwa Bayern na TSV 1860 Munich - hivyo kwa mtazamo mashabiki wengi wa hapa ni wa timu ya TSV 1860 na ndio maana unaona hali hiyo.


Shaffih: Unazungumziaje soka la nyumbani na ushauri kwa watanzania.
                             

BAADA YA TIKETI KUISHA - UWANJA WA ZAMANI WA BAYERN WAFUNGULIWA NA KWA AJILI YA KUONYESHA MPIRA KWENYE BIG SCREENS


Pamoja na tiketi za bei chini kabisa kuuzwa kwa EURO 2000 tena ukiwa unakaa kwenye siti za nyuma ya goli, leo hii mamlaka ya jiji la Munich wameufungua uwanja wa Olympia Stadium uliokuwa ukitumiwa na Bayern Munich kabla ya kuhamia Allianz Arena, kwa ajili ya matumizi ya kuonyeshea mpira wa leo katika uwanja huo.




Olympia leo pametengenezwa kwa kuwekwa TV screens kubwa ambazo mashabiki zaidi ya 60,000 watakaa na kuangalia mtanange kati ya Chelsea na Bayern Munich. Kwa taarifa nilizozipata ni kwamba kwenye uwanja huo pia napo pameshajaa na tiketi zote zimeshauzwa.

KUTOKA MUNICH: POMBE NDIO KINYWAJI KINACHOONGOZWA KUTUMIKA HAPA

Katika siku mbili nilizokaa hapa Munich nimegundua watu hapa hasa mashabiki wa soka wanapenda sana kunywa pombe.
Pombe ndio kinywaji wanachopenda sana watu wa hapa, mitaani mpaka viwanjani utawakuta watu wameshikilia maglassi ya pombe.

REDONDO NA CHUJI WAZUNGUMZIA PATRICK MAFISANGO

Kiungo wa Azam, Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema kifo cha Patrick Mafisango ni pigo kubwa kwake kutokana ndiye alimtaka aondoke Maisha Club ili akalale muda mfupi kabla ya kifo chake.

Redondo aliyekuwa na marehemu Mafisango kwenye ukumbi wa Maisha Club hadi saa 7 usiku ambako Mafisango alimtaka aondoke kwa madai kuwa muda ulikuwa umekwisha.

Akizungumza kwa shida kutokana na kuelemewa na uzito wa msiba huo alisema haelewi ni nini kimetokea na kwa nini alimfukuza pengine wangekuwa wote kwenye safari ya kurudi.

"Tulikuwa wote hadi mwisho kwenye ukumbi wa maisha klabu, lakini ilipofika muda ya saa saba nane kasorobo  Mafisango alinifukuza na kunichukulia taxi nirudi nyumbani na kuniaambia muda umeisha yeye atarudi na jamaa zake ambao alikuwa nao akiwemo mtoto wa dada yake,"alisema na kuongeza

"Nilikubali nikaondoka cha kushangaza napata taarifa alfajiri kuwa Mafisango amefariki Mungu amefanya kazi yake kumchukua, lakini mimi imeniathiri kutokana na mambo mengi niliyoongea nae"alisema na kushindwa kuendelea kuongea.

ATHUMANI IDD CHUJI

"Unafahamu wapo wachezaji wengi wa kigeni wanaocheza soka nchini na waliowahi kucheza soka nchini na kuondoka, lakini sikuwahi akuona mchezaji wa kigeni aliyekuwa akipendwa na wachezaji kama yeye,"alisema Chuji.

Alisema," Mafisango alipendwa na wachezaji wa timu tofauti za Ligi Kuu hasa walipokutana naye nje ya uwanja, alikuwa anapenda kuishi maisha ya kawaida tu na wachezaji wengi walikuwa wakimchukulia kama Mtanzania ila lafudhi yake tu.

PICHA: TIKETI ZINATAFUTWA KWA TAABU HAPA MUNICH

EURO 2000 - NI ZAIDI YA MILLIONI 3 ZA KIBONGO. MZUNGU YUPO TAYARI KUTOA KWA AJILI YA KUINGIA ALLIANZ ARENA.

NIMEKUTANA NA WAKONGO HAPA: WATHIBITISHA TIKETI KUUZWA EURO 1500-2500 LEO HII

Kama ambavyo niliripoti muda mfupi uliopita kuhusu upatikanaji wa tiketi kwa ajili ya kuangalia fainali ya champions league zilivyo ghali na shida kupatikana - jioni hii nikiwa kwenye matembezi yangu nimekutana na jamaa wawili raia wa Kongo ambao wamekuja hapa Munich kwa madhumuni ya kuangalia mtanange wa kesho kati ya Chelsea na Bayern Munich. Wakongo hawa wamenithibitishia kwamba ni kweli leo kuna baadhi ya sehemu ambazo ni chache sana zimebakiwa na tiketi lakini wanauza kwa EURO 1500 -2500 ambazo ni tiketi za hadhi ya juu.



KUTOKA MUNICH: IJUE KIUNDANI HISTORIA NA MAANA YA TIMU YA BAYERN MUNICH

HAPA NDIPO PATAKAPOAMUA BINGWA WA CHAMPIONS LEAGUE 2012 - ALLIANZ ARENA - IJUE HISTORIA YAKE.

Allianz Arena ni uwanja wa kuchezea soka uliopo kusini mwa Munich, Bavaria - Ujerumani. Huu ni uwanja unaotumiwa na timu mbili za mji wa Munich FC Bayern Munich na TSV 1860 Munchen kuchezea mechi zao za nyumbani kuanzia msimu wa 2005-06. Timu mbili zote zilikuwa zikicheza mechi zao za nyumbani kwenye uwanja wa Munich Olympic tangu mwaka 1972. Allianz Arena ni uwanja wa tatu kwa ukubwa nchini Ujerumani nyuma ya Signal Iduna Park mjini Dortmund na Olympiastadion mjini Berlin. Uwanja huu ulifunguliwa mwaka 2005, mwezi Mei 30. Ulijengwa kwa na gharama zisipungua Euro million 340 na kampuni ya Allianz ambayo wana haki ya kutumia jina lao kwenye uwanja huo kwa miaka 30. Uwanja una uwezo wa kuingiza watu 69,901.

RIPOTI KUTOKA MUNICH: HAPA NDIPO WALIPOFIKIA CHELSEA

BAYERN MUNICH WANATENGENEZA FEDHA NYINGI SANA KWA MAUZO YA JEZI

FAINALI YA MABINGWA WA ULAYA: TIKETI ZAPANDA MPAKA EURO 1500 -2500 ZA KIBONGO NA BADO ZAKOSEKANA

Football is business.......
Wakati jana nafika hapa Munich tiketi za mchezo wa fainali ambazo kwa jana tu zilikuwa zikipatikana kwa taabu, leo zimepanda bei maradufu kutoka Euro 1500 kwa jana mpaka EURO 2500 leo hii. 

Katika hali ya kushangaza pia tiketi hizo za EURO 2500 ambazo kwa haraka haraka ni kama shilingi millioni 4 za kitanzania, nazo zimeisha hivyo kusababisha uongozi wa jiji la Munich pamoja UEFA kuchagua sehemu maalum ambazo zimetengenezwa na kuwekwa Big screens.


Sehemu hizo pia nazo zimejaa na kuwa sold out kwa maana tiketi zote nazo zimeisha. Kwenye mabaa na pub nyingine nyingi hapa Munich ambazo huonyesha mipira napo kumekuwa sold out. Ni watu wengi inaonekana watakosa nafasi ya kuangalia mechi hii uwanjani.
Huyu mzungu ni mmarekani ambaye amesafiri kutoka Califonia kuja kuangalia fainali lakini amekosa tiketi.

 Kwa mfano nikiwa kwenye matembezi yangu leo nilikutana na Jamaa mmoja raia wa Marekani ambaye ambaye amesafiri kutoka Califonia mpaka Munich lakini maskini ya mungu amekosa tiketi.  


Kiukweli mpaka sasa kila sehemu ni Champions league final ndio kitu kinachotawala. Nimejifunza namna wenzetu wanavyoandaa matukio ya kuyafanyia promotions ya kutosha na ndio maana ni vigumu kwa matukio yao kufeli na mwisho ndio maana wanakuwa wanafanya biashara kubwa na kuwa matajiri.

Friday, May 18, 2012

KUTOKA MUNICH: MTANZANIA DJ MAX AMBAYE NI SHABIKI WA KUTUPWA WA BAYERN MUNICH

DJ Max mtanzania ambaye anaishi Munich. Huyu ndio mwenyeji wangu ambaye ananisaida kunitembeza mjini hapa na kuelekeza juu ya vitu tofauti kuhusu mechi hii pamoja na mambo mengine.

Hapa tukiwa wote nje ya jengo la hoteli waliyofikia klabu ya Chelsea wakati huu wakiwa hapa kwa ajili ya mechi ya fainali ya Champions league. Hii ni hoteli ya hadhi ya juu sana hapa Munich, Bayerischer Hof ni hotel ambayo huwa wanakaa mastaa wakubwa duniani wanapofika katika mji wa Munich.

JAY JAY OKOCHA AWAPA NAFASI BAYERN HUKU KAREMBEU AKITOA NAFASI KWA CHELSEA

Nikiwa na Jay Jay Okocha ambaye amesema kwa hali anavyooiona ni dhahiri anawapa nafasi Bayern Munich kuchukua ubingwa wa ulaya.

Mchezaji wa zamani wa Ufaransa Christian Karembeu yeye ameniambia Chelsea kesho watabeba kombe.

MASIKINI BOBAN: KIFO CHA MAFISANGO KIMEMUUMIZA MNO - WALIKUWA MARAFIKI WAKUBWA SANA.

Haruna Moshi Boban akiwa mwenye huzuni mkubwa leo wakati wa kuaga mwili wa Mafisango. Pole Boban mwenyezi mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu. (Picha kwa hisani ya http://bongostaz.blogspot.com/)

Pamoja na kuwa ni wengi tumeumizwa na msiba wa aliyekuwa kiungo wa timu ya Simba Patrick Mafisango Mutesa, lakini ni dhahiri wachezaji wenzie wa Simba wameumizwa zaidi hasa rafiki yake kipenzi Haruna Moshi Boban.
Haruna Moshi Boban akiwa na huzuni tele leo hii wakati wa kumuaga Patrick Mafisango.

Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba kwa takribani masaa 24 tangu kifo cha Mafisango kitokee Haruna Moshi ambaye wengi wetu tunamjua kama kama nunda na mtu mwenye aibu sana lakini kufuatia msiba huu wa Mafisango, Boban amekuwa mtu mwenye huzuni sana kiasi cha kushindwa hata kula. 
Emmanuel Okwi akiaga mwili wa Patrick Mafisango.
"Kiukweli msiba wa mwenzetu umetumuumiza sana, lakini Haruna umemuuma zaidi kwa kuwa Mafisango ndio alikuwa rafiki yake mkubwa kuliko wachezaji wote ndani ya Simba. Mafisango na Boban pale Simba walikuwa kama mapacha, yaani muda wote hata tukiwa kambini utawakuta pamoja. Kwa mfano hata tukiwa tumeenda safari kwa ajili ya mechi mara zote wenyewe walikuwa wakilala pamoja, kiukweli walikuwa wakipendana sana na ndioa maana haishangazi kumuona Boban kwenye hali ile." - alikaririwa akisema Emmanuel Okwi kupitia mawasiliano ya mtandao wa BBM.

JEZI YA MAFISANGO KUTOTUMIKA TENA SIMBA SC



JEZI namba 30, aliyokuwa anavaa kiungo wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika klabu ya Simba, Patrick Mutesa Mafisango kuanzi sasa haitakuwa ikitumika tena kwa heshima ya mchezaji huyo aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia jana, jijini Dar es Salaam.
Hayo yalisemwa jana Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage alipokuwa akihutubia mamia ya wadau wa soka waliohudhuria zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Mafisango kwenye viwanja vya Sigara Chang’ombe, Dar es Salaam, kabla ya kupelekwa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, tayari kwa safari ya kwenda kwao, DRC kwa ajili ya mazishi kesho.
Heshima kama hiyo alipewa kiungo wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Marc Vivien Foe na klabu yake, Manchester City ya England alipofariki Dunia Juni mwaka 2003, ambapo jezi namba 23 ilitunzwa moja kwa moja.
Aidha Rage alisema msiba huu ni mkubwa kwa Simba kwa kuwa mchezaji huyo alikuwa ni muhimili mkubwa kwa timu hiyo akiwashauri wachezaji na kuwa nao karibu ndani na nje ya uwanja.
“Mafisango alikuwa na mchango mkubwa kwa Simba na mara ya mwisho klabu kukumbumbwa na msiba mzito namna hii ilikuwa ni mwaka 1978 ambapo Simba ilimpoteza mchezaji wake mahiri Hussein Tidwa na ukweli ni kwamba wachezaji hawa tutawaenzi miaka yote na ndio sababu ya kutotumia tena jezi namba 30 kwa kuvaliwa na mchezaji yoyote,” alisema Rage.
Rage alisema licha ya umahiri wa Mafisango Dimbani pia alikuwa mchezaji ambaye alitoa mchango mkubwa na hasa wachezaji wawapo nje ya nchi kutokana na umahiri wake wa kujua lugha mbalimbali ambapo alikuwa akiwasaidia wachezaji wenzake.
“Ni pengo kubwa kwa kuwa mchezaji huyo alikuwa akijua lugha nyingi ikiwemo Kiswahili, Kingereza na Kifaransa  na kuwasaidia wachezaji walipokuwa nje ya nchi tutamkubuka sana Mafisango,” aliongeza.
Kutokana na machungu ya msiba huo Rage alishindwa kumaliza kusoma risala fupi ya marehemu mara baada ya kuishiwa nguvu na kumwaga machozi na kupelekea Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Godfrey Nyange ‘Kaburu’ kumsaidia kusoma risala hiyo.
“Mfisango ni mchezaji ambaye alikuwa akijituma nje na ndani ya uwanja na kabla ya kutua Simba Marehemu aliwahi kucheza soka katika timu mbalimbali ikiwemo Tp Mazembe ya DRC, APR ya Rwanda , Azam na Simba za Tanzania na pia alikuwa Nahodha wa timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ alisema Kaburu.
Wakati wa kutoa heshima za mwisho katika uwanja wa Sigara maelfu ya watu walijitokeza uwanjani hapo wakiongozwa na mchungaji Tito Kihame ambaye aliongoza ibada ya kuuga mwili wa marehemu, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara na viongozi mbalimbali wa serikali na viongozi kutoka klabu mbalimbali za hapa nchini.
Mukangara aliwataka wachezaji wa Tanzania kujituma na kuwa na moyo kama ambao alikuwa nao Marehemu Mafisango kwa kujituma na kuwa na jitihada za zaidi nje na ndani ya uwanja kama ambavyo marehemu alivyokuwa akifanya.
“Kifo chake ni pigo kubwa kwa Simba na Watanzania kwa ujumla na tunamshukuru kwa kuvuka mipaka na kuona umuhimu wa kuja na kucheza Tanzania na pia wachezaji wa Simba wasikate tamaa cha muhimu waendeleze kile ambacho alikiacha marehemu,” alisema Mukangara.
“Ukweli ni kwamba katika familia ya soka hapa nchini tumepoteza mtu muhimu sana na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani,” alisema Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Angetile Osiah.
“Sisi Simba ni watani zetu na tunakuwa pamoja katika shida na hivyo basi mimi kama kiongozi wa Yanga nimeiwakilisha klabu nzima na tutaendelea kuwa bega kwa bega na watani zetu katika kipindi hiki kigumu ila mchezaji Mafisango alikuwa ni mchezaji hodari uwanjani hivyo basi anastaili kuigwa na wachezaji wengine,” alisema Selestine Mwesigwa katibu Mkuu wa Yanga.
Nao wachezaji mbalimbali kutoka timu ya Taifa Taifa Stars walijitokeza na kubeba jeneza la mchezaji mwenzao na kuliingiza katika viwanja vya Sigara wachezaji hao Juma Kaseja, Jonh Bocco, Mwinyi Kazimoto, Shabani Nditi, Amiry Maftah, Nurdin Bakari, Agrey Moris na Juma Nyoso.
Profesa Philemon Sarungi akimsaidia Rage
Mara baada ya nyota hao kuufikisha mwili wa marehemu katika sehemu husika ambayo ilipangwa Kazimoto na Kaseja iliwalazimu watu wa ziada kujitokeza na kuwapa sapoti mara baada ya kushindwa kutembea na kuwapeleka katika eneo husika ambalo walikuwa wamepangiwa kukaa.
Katika hatua nyingine Ofisa habari wa wekundu hao wa Msimbazi Ezekiel Kamwaga ‘Mr Liverpool’ alisema kuwa katika msafara wa leo kuondoka kwenda Kongo kuusafirisha mwili wa marehemu kwa niaba ya wachezaji atawawakilisha Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye alikuwa karibu na marehemu pamoja na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Joseph Itang’are.
“Mwili wa marehemu utaondoka mapema alfajili ya kesho (leo) kwenda kwao Kongo ila pia leo mtoto wa marehemu Chris Paul, mwenye umri wa miaka mitano ameondoka na mchezaji wa Yanga Haruna Niyonzima ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda,” alisema Kamwaga.

Picha na habari kwa hisani ya http://bongostaz.blogspot.com/

YANGA NA SIMBA MNAONA HII - INAWAHUSU

Kawaulize Simba na Yanga wanaingiza kiasi kutokana na mauzo ya jezi zao zilizojazana mitaani, Huu mzigo mpaka kukamilika hivi ni Euro 150 karibia laki tatu ya bongo! TAFAKARI!

EXCLUSIVE INTERVIEW NA MASHABIKI WA CHELSEA HAPA MUNICH

TANZANIA BWANA: ETI NSAJIGWA AMEISHA? SOMA SABABU 5 KWANINI NAAMINI NSAJIGWA BADO NI HAZINA YANGA.

Shedrack Nsajigwa akifanyaiwa mahojiano na mchezaji mwenzie Shabaan Kado

Tanzania ni moja ya nchi zilizojaliwa neema barani  Afrika
 kama si Duniani kwa ujumla.
Hakuna kitu kinachoisumbua nchi yetu kama kuwepo kwa watu kwenye maeneo wasiostahili, watu wasiokua na sifa na uwezo ndio wamejazana kwenye sekta nyeti hapa nchini.


Hayo madudu ndio hasa yanasababisha uchumi wa nchi yetu unashuka kila kukicha, hivi karibuni baada ya mchezo baina ya watani wa jadi hapa nchini Simba na Yanga kumalizika kwa Yanga kupokea kipigo cha mabao 5:0 kuliibuka mambo mengi sana hasa kwenye klabu ya Yanga (leo sitazungumzia mapambano yanayoendelea kati ya wanaojiita wazee wa Yanga na viongozi waliopo madarakani ).

Kwenye mchezo huo mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi aliibuka nyota wa mchezo je kuna anayebisha juu ya hilo? Jibu ni hakuna, sasa kilichonisikitisha ni baada ya kusoma habari kibao za kutoa kontena la lawama kwa baadhi ya wachezaji kama vile Nurdin Bakari na Shadrack Nsajigwa eti hawastahili kuichezea tena Yanga viwango vyao vimeisha,jamani kiwango cha mchezaji kinaisha kwenye mchezo mmoja?
 Hayo ni mazungumzo ya wanaojiita wadau wenye sauti ndani ya Yanga ambao hutoa mapendekezo ya nani anatakiwa kuachwa na nani anatakiwa kusajiliwa, baada ya kusikia maoni ya juu ya kuachwa kwa beki na nahodha Nsajigwa nilipigwa na bumbuwazi, kwa mtazamo wangu hata kama wangetakiwa kubaki wachezaji wawili tu ndani ya Yanga kwa ajili ya msimu ujao Nsajigwa angekua mmojawapo, kwanini?

1. Kushushwa kiwango, kustaafishwa na Okwi


Shadrack anahukumiwa kwa kushindwa kumkaba Okwi, hili mimi nalifananisha na mwizi kuingia kwenye ofisi na kuiba halafu umuhukumu aliyekuwepo ofisini pasipo kujiuliza huyo mwizi kaingiaje mpaka ndani ya ofisi wakati kuna walinzi nje na mapokezi? Kwanini usijiulize kwanza hilo, mfano huu unafanana kabisa na kesi ya Nsajigwa, baada ya kujiuliza Okwi alikuwa anaipataje mipira ya hatari na kwanini Simba walikuwa wanashambulia kupita upande mmoja wa kushoto, mimi nadhani tatizo lilikuwa  ni la timu nzima kushindwa kuja na mpango mkakati wa kuizuia Simba kutengeneza mashambulizi upande huo, kwa kifupi Nsajigwa hakushuka kiwango kwenye mchezo dhidi ya Simba bali siku hiyo mfumo mzima wa timu ulikwama, hata kama ingekuwa mchezaji anatakiwa kustaafishwa kwa kushindwa kumkaba mchezaji wa timu pinzani basi leo Fernando Torres angekuwa kashamstaafisha Nemanja Vidic na kina Messi na Ronaldo wangekua wameshawastaafisha mabeki wote wa La Liga.


2. Wahusika kutokuwa na malengo ya mbali


Nsajigwa ni mmoja wa wachezaji wachache ambao ukiwa nao kwenye timu unatakiwa kumshukuru mungu, lakini tatizo la kuwa na watu ama viongozi wasiokuwa na maono linapelekea kuchukulia vitu kirahisi rahisi tu, ngoja nikupeni mfano ulio hai mwaka jana Simba walimstaafisha kiungo Nico Nyagawa kwa nguvu huku akiwa bado na msaada mkubwa kwenye timu tena naye alikua ni nahodha kama ilivyo kwa Nsajigwa, faida ya uwepo wa Nsajigwa kwenye timu ni zaidi ya kucheza jamani, kurudisha heshima kwa wachezaji vijana kutokana uwepo wa kaka yao, pia ni bahati kuwa na mchezaji ambaye ni rahisi kuambukiza siri ya mafanikio kwa wenzake na mwisho katika hili kuna aliyewahi kujiuliza kwanini kina Giggs na Scholes pale Man Utd, Carragher pale Liverpool wanaendelea kuwepo? Je ni kwasababu wana viwango vikubwa kushinda vijana waliopo kwenye hizo timu?, jamani muda mwingine baadhi ya wachezaji hulelewa ili waje wawe hazina hapo baadae, ila kwasababu vilabu vyetu vinaongozwa na wanasiasa na watu wasiokuwa na sifa za kuviongoza hawaoni kama wachezaji kama Nsajigwa wanaweza kuendelea kuwepo klabuni kwa ajili ya kuwalinda na kuwatunza vijana wapya.


3. Kumbadilishia majukumu


Yaani hakuna mtu pale klabuni anayeweza kuona kwamba Nsajigwa bado ni hazina kiwanjani ? Javier Zanetti wa Inter Milan anaweza kutumika kuuelezea umuhimu wa Nsajigwa kwasababu wote ni ma-wing back, namna ya kuendelea kuvuna matunda yao hawa jamaa ni kuwapunguzia majukumu kiwanjani, mfano kuna aliyewaza nini kitatokea kama Shadrack atapewa jukumu moja tu kiwanjani la kukaba ama kushambulia tu, kwa mtazamo wangu ili kuendelea kumfaidi Nsajigwa si kumstaafisha bali ni kumpunguzia majukumu kutokana na umri wake kuwa mkubwa.


4. Kuja kuwa sehemu ya benchi la ufundi.


Narudia tena kwasababu asilimia kubwa ya wanaojihusisha na vilabu hivi hawana Mitizamo ya mbali, Mipango na mikakati ya kuviendeleza hivi vilabu kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine basi njia pekee wanayoiona ni kuwafukuza wachezaji, kumbe wanaweza kuwekeza kwa wachezaji hawa kwa ajili ya faida ya baadae kwa klabu, wachezaji kama Pawasa, Matola, Salvatory Edward na Nsajigwa wanaweza kuendelea kuwepo na kupatiwa kozi za ukocha ili baadae waje wazifundishe hizo klabu.

Namalizia hivi :
Shadrack Nsajigwa bado yupo yupo kwanza!

NIMEFIKA SALAMA MUNICH - TIKETI YA BEI CHINI KUANGALIA FAINALI NI SHILINGI MIL.3 ZA KIBONGO - JEZI ZA BAYERN ZAONGOZA KWA MAUZO.

Nashukuru mwenyezi mungu nimefika salama hapa Ujerumani - tayari kwa ajili ya kuangalia na kukuletea baadhi ya matukio kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kati ya Chelsea  na Bayern Munich.
Tangu nifike hapa nimegundua baadhi ya vitu vifuatavyo:
Ticketi ya kiwango cha chini sasa zinauzwa euro 1,500 ambayo ni karibia milioni 3 ya kitanzania.
Hii inakuonyesha namna gani tukio hili la mchezo wa fainali ya UEFA Champions League lilivyo kubwa sana.
 Makampuni yanayofanya kazi na UEFA yanafanya sana biashara mfano bia zinazonyweka hapa ni Heineken tu huku bei ikiwa imeongeka kwa asilimia  100'mwanzoni glass ya bia ya heineken iliuzwa kwa euro 2.5 lakini sasa imepanda mpaka euro 5, jezi za Bayern ndio zinanunuliwa sana huku kila jezi ikiuzwa kuanzia euro 80, ambayo ni kama laki moja na sitini kwa pesa ya kitanzania, kwakifupi mzunguko wa biashara umeongezeka kwa takribani juma zima lililopita...

KUELEKEA SAFARI YA MWISHO YA KIPENZI CHETU PATRICK MAFISANGO ALIVYOAAGWA LEO ASUBUHI

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Shabaan Nditi, Juma Nyosso, na Bocco wakiwa wamebeba jeneza la mchezaji mwenzio Patrick Mafisango wakati likiingia katika viwanja vya TCC kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda kwao DRC Congo kwa ajili ya mazishi.



Taifa Stars wa kwanza kushoto ni kocha wa makipa, Juma Pondamali

Katikai Kim Poulsen kocha wa Stars, kushoto Msaidizi wake Sylvester Marsh na kulia Meneja Leopold Mukebezi


Azim Dewji kulia na Leonard Thadeo kushoto



Gwiji wa Simba, Abdallah Kibadeni kushoto na Uhuru Suleiman


Makocha wa Yanga, Freddy Felix Minziro na kocha wa makipa Mfaume Athumani wakiwa na beki wa zamani wa Yanga, Willy Martine 'Gari Kubwa' wa pili kutoka kushoto

Makumbi Juma katikati

Eric Sagala 'Cantona' katikati


Suleiman Matola kulia

Juma Nyosso kushoto na John Bocco 'Adebayor' kulia wakiwa wamebeba jeneza

Shabiki Mkongomani akidhibitiwa baada ya kupagawa alipoona jeneza la marehemu Mafisango

Amir Maftah aliyebeba msalaba na Mwinyi Kazimoto kashika picha



Nahodha wa Simba Juma Kaseja akisaidiwa baada ya kushindwa kujizuia na kuangua kilio kiasi cha kuishiwa nguvu

Kaseja ni huzuni na kilio


Jeneza la Patrick Mutesa Mafisango


Makamu Mwenyekiti wa Simba, Kaburu na Leslie Liunda kushoto




Kocha wa Simba, Milovan Cirkovick

Milovan kilio


Shabiki 'hayawani' la Yanga, maarufu kama J4 likicheka msibani

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dk Fennella Mukangara (wa pili kutoka kushoto)akiingia Uwanja wa TCC


Dk Fenella na Thadeo wakijadiliana




Jamal Malinzi mwenye miwani





Ibada

Mchungaji Tito Kyame akiongoza ibada ya kumuombea marehemu

Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa akitoa rambirambi

Ofisa wa Push Mobile, mmoja wa wadhamini wa Simba akitoa rambirambi

Mwenyekiti wa Simba, ALhaj Ismail Aden Rage akitoa hotuba 


Wazee wenye busara wa Simba

Rage akimuinua Dk Fenella akahutubie

Athumani Tippo 'Zozzou'

Kiggi Makassy kulia

Clement Kahbuka kushoto na Athumani Jumapili Chama kulia