Search This Blog

Saturday, December 8, 2012

BARA ACHENI KUTUSHIRIKISHA KINAFIKI TUIPELEKE TANZANIA KWENYE FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA!

wachezaji wa Zanzibar Heroes wakishangilia baada ya kuifunga Kilimanjaro Stars kwa penalti 6-5 katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na wa nne katika mashindano ya Cecafa Challenge 2012.


Kocha Mkuu wa timu ya Zanzibar Heroes Salum Nasoro Bausi ambaye ameshatangaza kujiuzu akiwa amebebwa  baada ya kuifunga Kilimanjaro Stars kwa mikwaju ya penati 6-5 wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ya michuno ya Cecafa Challenge 2012 uliochezwa katika Uwanja wa Mandela Jijini Kampala
Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakishangilia baada ya kuifunga Kilimanjaro Stars kwa Penati

BREAKING NEWS! FIBERT BAYI NA GULAM RASHIDI WAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA TOC!


Waliokuwa viongozi wa kamati ya Olympic Tanzania ndugu Gulam Rashid (Raisi ) na ndugu Filbert Bayi (Katibu )wametetea  tena nafasi zao kwenye uchaguzi uliofanyika leo hii mkoani Dodoma.
Taarifa za matokeo ya nafasi zingine baadae !


VIKOSI VINAVYOANZA :UGANDA vs KENYA

CECAFA CUP FINAL LIVE SCORE: UGANDA vs KENYA


ZANZIBAR YATWAA NAFASI YA TATU BAADA YA KUIFUNGA KILIMANJARO STARS

 Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, John Boko akiwatoka mabeki wa timu ya Zanzibar Heroes wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda
 Mchezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,Athuman Chuji akimtoka beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Sbari Alliy Makame wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda
 Mlinda mlango wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanajro Premium Lager, Juma Kaseja (kushoto) akiokoa moja ya hatari mbele ya mshambuliaji wa timu ya Zanzibar Heroes, Khamisi Mcha Khamis wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela Kampala
Beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Haroub Nadir akimzuia mshambuliaji wa trimu ya Zanzibar Heroes, John Boko wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda

MATCH LIVE CENTER 3RD PLACE: ZANZIBAR VS TANZANIA BARA

VIKOSI : ZANZIBAR HEROES VS KILIMANJARO STARS


USIKOSE MICHEZO YA MWISHO YA CECAFA TUSKER CUP LEO!

Poulsen: Tulijiandaa vizuri lakini tulizidiwa

 Wachezaji wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakifanya mazoezi mepesi katika Hoteli ya Mount Zion jijini Kamapla tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Zanzibar  Heroes wa michuano ya Cecafa Challenge 2012 utakaochezwa katika Uwanja wa Mandela uliopo Nambole.


Na mwandishi maalumu,
Kampala
Kocha wa Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amekiri kuwa kikosi chake kilizidiwa na Cranes ya Uganda katika nusu fainali ya mashindano ya Cecafa Challenge huku akisema licha ya maandalizi mazuri, Waganda walikuja na mbinu ya kuwakabili.

Poulsen aliyasema hayo juzi (Alhamisi) baada ya mchezo huo ambapo Stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ililala kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0.

“Ukizingatia kuwa walikuwa katika uwanja wa nyumbani, waliwapa wachezaji wetu taabu sana na tulifanya makosa kuruhusu goli la haraka katika dakika ya kumi na moja hivi,” alisema.

Alisema kuelekea mwisho wa kipindi cha kwanza Stars ilijitahidi kuhakikisha hakuna bao lingine linaingia na walikuwa na matumaini kuwa mchezo ungebadilika katika kipindi cha pili.

“Hata hivyo tulifanya makosa tena kuwaruhusu waganda kupiga krosi na kuziunganisha na kupata goli tena na hapo wachezaji wa Uganda wakapata nguvu zaidi hasa ikizingatiwa mashabiki wao walikuwa wamejaa uwanjani wakishangilia,” alisema Poulsen.

Kocha huyo kutoka Denmark, alisema walikubali hali halisi kwani walicheza na timu yenye kiwango cha juu.
“Ila nataka kusisitiza tu kuwa hatujakata tamaa kwani vijana wamepata uzoefu mkubwa katika mashindano haya na itatusaidia kusonga mbele kwani tumejitahidi kufikia hatua za mwisho za mashindano ambayo yalikuwa magumu kwani timu zote zilikuwa zimejiandaa vizuri,” alisema.


Alisema kwa sasa wanajiandaa na mechi dhidi ya Zanzibar Jumamosi  ili kupata mshindi wa tatu wa mashindano hayo. “Huu nao utakuwa mchezo mgumu kwani tumeshaona namna Zanzibar wanacheza,” alisema.

“Tulianza mashindano vizuri na ombi langu tu sasa kwa wachezaji ni tumalize vizuri kama tulivyoanza angalau tuweze kupata nafasi ya tatu katika mashindano haya,” alisema.

Katika fainali, Kenya itamenyana na mwenyeji Uganda katika uwanja wa Mandela uliopo Nambole, Jijini Kampala.
Akizungumza kutoka Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager aliipongeza Stars kwa hatua iliyofikia katika mashindano ya Cecafa Challenge huku akisema sio mwisho wa safari kwani bado kuna mashindano mengine.


“Tunaamini vijana wamepata uzoefu mkubwa na sasa wana silaha ya kukabiliana na mashindano mengine mbele yao…hatua waliofikia ni kubwa tu na tunawaomba wasife moyo,” alisema huku akiwataka watanzania pia kuwa na subira kwani timu bado inaonesha matumaini.

Stars inatarajiwa kurejea nyumbani Jumapili hii baada y mashindano kumalizika ili kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Chipolopolo ya Zambia ambapo Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuizindua Taifa Stars rasmi kwa watanzania

Friday, December 7, 2012

MJADALA: WADAU MNAONAJE SASA UMEFIKA MUDA WA ZFA KUPEWA JUKUMU LA KUISIMAMIA TAIFA STARS KUTOKA MIKONONI MWA TFF.

                                       ZFA
                                                 TFF

THE LEGEND IS BACK AT SYNERGY LOUNGE

UGANDA YAINGIA FAINALI BAADA YA KUICHAPA KILIMANJARO STARS MABAO 3:0

 Beki wa Kilimanjaro Stars, Erasto Nyoni akitafuta mbinu ya kumpita beki wa timu ya Uganda, Godfrey Walusimbi wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Cecafa challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda jana. Uganda ilishinda 3-0.
 Mwinyi Kazimoto (mwenye mpira katikati) akiambaa na mpira wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini uganda jana. Uganda ilishinda 3-0.
 Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngasa akimuweka chini beki wa timu ya Uganda wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela jana. Uganda ilishinda 3-0.
 Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakiwasalimia mashabiki kabla ya kuanza kwa mchezo wa nusu Fainali ya pili ya michuano ya Cecafa Chalenge dhidi ya wenyeji, Uganda uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela jana. Uganda ilishinda 3-0.
 Mchezaji wa Kilimanjaro Stars, Mwinyi Kazimoto (kushoto) akimlamba chenga beki wa timu ya Uganda, Godfrey Walusimbi wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela jana. Uganda ilishinda 3-0.
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, John Bocco akiwania mpira na beki wa timu yaUganda, Isaac Isinde wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Cecafa challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela jana. Uganda ilishinda 3-0.

Thursday, December 6, 2012

MATCH LIVE CENTER : TANZANIA vs UGANDA

KENYA WAFANIKIWA KUINGIA FAINALI BAADA YA KUIFUNGA ZANZIBAR KWA MIKWAJU YA PENATI!

 Wachezaji wa Zanzibr Heroes wakishangilia goli la pili wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Mandela uliopo Nambole Jijini Kampala
 Wachezaji wa Zanzibar Heroes na wa Kenya wakiwani mpira wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Mandela Nambole Jijini Kampala.
Wachezaji wa Zanzibar Heroes na wa Kenya wakiwani mpira wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Mandela Nambole Jijini Kampala.

Mchezo huu umemalizika kwa Kenya kuifunga Zanzibar kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 120 kumalizika kwa timu hizo kufungana bao 1:1

LIVE MATCH CENTER: SEMI FINAL- ZANZIBAR 1-1 KENYA


WAJUMBE WAENDELEA KUPINGA WARAKA WA TFF!


BOBAN NDIYE MCHEZAJI BORA TANZANIA!


BOBAN,BEST PLAYER IN TANZANIA(my opinion)
BOBAN,BEST PLAYER IN TANZANIA(my opinion)

USIKOSE LIVE MATCH CENTER LEO KUPITIA HAPA HAPA!

MJADALA: NINI MAONI YAKO JUU YA HILI SAKATA LA KUUZWA MRISHO NGASA!

MMMMMMMMMH,KULIKONI TENA!

Wednesday, December 5, 2012

SERA NA DIRA YA MGOMBEA WA URAIS WA TOC

 
Watanzania sasa hivi wamekuwa wakitoa tuhuma na lawama mbali mbali kwa TOC. Hii ni fadhaa inayotokana na kwamba kwa muda mrefu sasa, Tanzanaia imekosa medali katika mashindano ya kimataifa. Kumekuwepo pia na malalamiko dhidi ya TOC ya kuwa mbali na Serikali na pengine taasisi nyengine nyingi katika kushaurikana na kuweka mikakakti ya pamoja ya kuratibu harakati za  kuleta ushindi nchini kwetu. Kuna lawama pia za kukiuka katiba na miongozo ya IOC ambayo haina budi kuangaliwa kwa makini.

Kwa ujumla, watanzania kwa kutumia sauti zao, wanakosa raha wanayoiptarajia katika medani za michezo Tanzania. Hivyo basi, kuna haja ya kuwa na Mabadiliko ndani ya TOC kwa kuingiza damu changa zenye nguvu, weledi na uzoezu wa kimataifa ili kuandaa mazingira mazuri ya ushindi.

Sababu kuu za kuomba nafasi hii ya juu ndani ya TOC (Rais) ni pamoja na kuwa na sifa, uwezo, uzalendo na hamu ya kuleta mabadiliko katika tasnia ya michezo kwa kuptipa Kamati ya Olimpiki Tanzania.

Pia naamini kwamba kwa kuwa katiba bora na inayofuatwa na watu wote, uwezo na utaalamu wa endeshaji na utawala wa taasisi za kiraia nilio nao; timu nzuri ya wajumbe na viongozi wa TOC wenye sifa na hamu ya kuendeleza michezo itapatika, kutakuwa na mwanzo wa mabadiliko ambayo watanzania wanayatamani kwa muda mrefu.

Mabadiliko ndani ya TOC yanahitajika sasa  kwa kuwa na mafiga matatu makuu makini na mahiri na sikivu. Pia ikiwa kutakuwa na wajumbe imara wa Kamati Tendaji ili kwenda na hali ya sasa ya sayansi na teknolojia na kukidhi kiu ya Watanzania, mabadiliko yatakuwepo.

Mtazamo wangu ni kuleta Mabadiliko ya kimfumo (systemic), kiutawana (managerial) na uendeshaji na Kimkakati (strategic) ndani ta TOC mpya, yenye matumaini na itayoendeshwa kisayansi.

Katika kutekeleza mabadiliko hayo, TOC mpya itaongozwa na maadili (misingi mikuu) ifuatayo:
Umoja miongoni mwa viongzo wa TOC, watendaji na Umoja wa Vyama na wanamichezo. Hakutokuwa na ubaguzi katika kutoa huduma za TOC.
Ukweli na Uwazi. Huu ni msingi mkuu na viongozi wote watatakiwa kuusimamia ipasavyo. Majungu na kuunda kambi hakutopewa fursa ndani ya TOC mpya.
Uwajibikaji: Kila mtu atatakiwa kufanya kazi zake kwa weledi wa hali ya juu na kuhakikisha kuwa dhamira na malengo ya TOC waliyowekwa yanafikiwa. Vikao vya Kamati vitatumika kuelezana ukweli na kuwasaidia wale ambao hawaendani na kasi ya mabadiliko.
Umoja na Mshikamamo: TOC itaongozwa na Utanzania Kwanza. Uzalendo na upendo wa nchi siku zote utawekwa mbele. Ubinafsi na choyo hautokuwa nafasi katika kazi za kamati katika miaka 4 ijayo.

Dira ya TOC katika miaka 4 ijayo ni  kuiona “Tanzania imerejesha imani kwa wananchi katika michezo ya Olimpiki kwa kuanzisha mfumo bora wa kupata ushindi katika mashindano ya Kimataifa”.

Hili litafikiwa kwa kuandaa mipango itakayosaidia kuongeza wigo wa ushiriki wa wanamichezo wa Tanzania na hatimae kupata ushindi (medali) katika mashindano ya Kimataifa na hivyo kurejesha heshima kwa nchi yetu. Mafanikio haya yatakuja ikiwa kutakuwa na uongozi bora na makini na sikivu wenye mtazamo wa mabadiliko chanya; ushirikiano mkubwa wa wadau hasa vyama, viongozi wa jamii na wanahabari; maandalizi ya mapema ya wanamichezo; kuwa na vifaa na miundombinu za michezo na utashi wa kisiasa.

Mabadiliko ambayo watanzania wayatarajie katika miaka 4 ijayo ni pamoja na yale ya  kimfumo, kiutawala na uendeshaji na kimkakati.  

Mabadiliko ya Kimfumo yatahusisha zaidi marekebisho ya katiba ili iende na matakwa ya sasa. Kuna haja ya Katiba kuweka mazingira ambayo haki inaweza kutendeka bila ya mizengwe na pia kuondosha utata ambao unaweza kujitokeza kiuntendaji. Kanuni za uendeshaji (Uchaguzi na za utawala wa fedha) zitaandaliwa na kusimamiwa na wahusika ili kuweka uwanja sawa wa uendeshaji wa kazi za Kamati.

Mabadiliko mengine ni ya Kiutawala na Utendaji ndani ya TOC. Kuna haja ya kuhakikisha kwamba kila mtendaji  anatekeleza majukumu yake  kwa mujibu wa katiba na kanuni ya TOC bila ya kuingilia majukumu ya mtu mwengine. Watendaji wa TOC nao watapimwa kwa matokeo ya utendaji wao na wale ambao hawaendani na kasi ya mabadiliko watawajibishwa kwa mujibu wa sheria za kazi na kanuni zake. Utendaji utapimwa kwa matokeo ya kila mfanyakazi (Perfomance appraisal) kulingana na malengo tyake ya mwaka. Hatoonewa mtu ila pia hatobebwa mtu. Motisha kwa wafanyakazi ikiwemo maslahi yao yataangaliwa na kufanyiwa marekebisho kila inapostahiki. Vongozi wote wa TOC wataomba sana kufanya kazi zo kwa mujibu wa Katiba na si vyenginevyo. Vikao vya Kamati tendaji vitatumika kama mfumo rasmi ya kujadili utendaji wa TOC.

Katika mabadiliko ya kimkakati ndani ya miaka 4 ijayo, watanzania wategemee kuimarika sana kwa uhusiano wa TOC na wadau wengine. Kwanza TOC itashirikiana kwa karibu na Serikali kuu na zile za Mitaa. Mahusiano na mashauriano na Wizara zinayohusu michezo na hasa mabaraza la michezo yataimarishwa yataimarishwa zaidi Tanzania bara na Zanzibar. Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) nayo itakuwa mdau muhimu sana wa TOC ili kuona michezo inafanyika maeneo yote ya Tanzania, ikiwemo mijini na vijijini na fursa zinapatika kwa wanachi wote bila ya ubaguzi hasa kwa kupitia Makatibu wa Serikali wa Mikoa (RAS). Uhusiano wa karibu na Wizara za kisekta (elimu, afya, miundombinu, ulinzi na usalama, mawasiliano nk) utazingatiwa  na kuimarishwa zaidi.

TOC mpya pia itaimarisha mahusiano kati ya wadau wa mandeleo, wafadhili na makampuni binafisi yaliyopo nchini na nje ya nchi. TOC mpya itajipanga kutafuta na wadhamini (sponsors) kutoka kwa mashirika na makampuni makubwa duniani ili kupata nyenzo za kuendeleza michezo. Wananchi wataombwa kutoa maoni yaokuhusu hili juu ya namna bora ya ushirikiano huo.

Uhusiano wa Kamati za Olimpiki za nchi za jiarani na mabara mengine utaimarishwa ili kujifunza na kubadilishana mawazo juu ya uendeshaji bora wa Kazi za Olimpiki. Mafunzo kwa wajumbe wa TOC ili kwenda sambamba  na mabadiliko yatatolewa.

Katiba ya TOC inatoa uwezo wa kuunda kamati mbali mbali. Katika miaka 4 ijayo, kamati hizi zitatakiwa kufanya kazi na kutoa taarifa zake kwa TOC. Kwa kadri hali na uwezo utakavyoongezeka, kamati hizi zitawezeshwa kutekeleza majukumu yake  kikamilifu.

Watanzania pia watarajie kuwaona watu maarufu katika masuala ya michezo wakiombwa kutoa ushauri wao na namna ya keundeleza Michezo. Mikutano maalum na wadau (wananchi, wanasiasa, wasomi, wanamichezo, waandishi wa habari, wanahadhiri, wachambuzi wa mambo ya kijamii na kiuchumu nk) itaandaliwa ili kupata mawazo zaidi ya uendelezaji wa michezo Tanzania hasa katika siku za kuadhimisha sherehe za olimpoki za kila mwaka. Afisa wa Uhusiano atatakiwa kuhakikisha TOC iko karibu sana na Watanzania. Matumizi ya Mitandao (blog na tovuti na simu) itatumika kuelimisha na kupata maoni ya wadau. Tunataka TOC yenye kazi ya 3G (3rd Generation).

Mabadiliko mengine ni ya kuwa na Mipango inayoonyesha malengo mahsusi na yanayotekelezeka. Hii ni pamoja na kuwa Uratibu mzuri wa kazi za TOC, Mafunzo kwa wanamichezo na viongozi, miundo mbinu (Kuwa na eneo la kujenga Kijiji cha Olimiki Tanzania bara na kuendeleza kijiji cha Olimpiki kilichopo Zanzibar) na kadhalika. TOC mpya itaanza kufikiria uwekezaji wa muda mferu wa miundombinu ya Michezo Tanzania.

Vyama Taifa watarajie mahusiano bora zaini na TOC mpya. Makamo wa Rais atatakiwa kuhakikisha mashauriano baina ya TOC na Vyama yanaimarika kila uchao. Hii itajumuisha kuwa na Kalenda za Michezo zinazoonyesha mashindano mbali mbali. TOC inaweza kuvisaidia vyama kupata vyenzo au utaalamu ili kuona kwamba vipaji vinaibuliwa na kunakuwa na ongezeko la wanaridha na wanamichezo Tanzania wanaoshiriki katika mashindano ya Kimataifa. TOC kwa kushirikiana na vyama watahakikisha viwango vinavyotakiwa kimataifa vinapatikana na washiriki wanaostahiki pekee ndio wanakwenda katika mashidano husika.

Watanzania pia watarajie uhusiano bora zaidi wa TOC na vyombo vya habari na wananchi. Maoni, taarifa na mambo yahayohusu michezo yatatolewa kwa waandishi ili nao wawajulishe watanzania. Midahalo ya namna bora ya kuendeleza miechezo ikiwemo ya kuibua vipaji itaandaliwa na TOC kwa mushirikiana na vyombo vya habari. Siku za maadhimisho ya Olimpiki zitatumika kuwa karibu sana na wadau ili kuopata mawazo na maoni yao.

TOC mpya inapanga kutaleta mabadiliko ya kuchechemua hamasa ya michezo katika mawizara, taasisi za umma na binafsi, vyuo vikuu, shule na kwa jamii ili kutekeleza nia ya Michezo kwa wote itakayowajumuisha watu wenye ulemavu.

Lengo moja la TOC ni kuendeleza amani, TOC mpya itashirikiana na Serikali, asasi za kiraia na wadau wengine ili kuhakikisha amani ya Tanzania inaimarika. Michezo na mashindano mbali mbali yatahamasishwa kushajiisha umoja, upendo na mshikamamo miongoni mwa wananchi.

Maadili katika michezo nayo yatasimamiwa na TOC. Wanamichezo watakaotumia madawa na kubainika hawatopata fursa na kushiriki mashindano. Uwekezaji katika kituo cha kupima matumizi ya madawa utatafutwa ili kuifanya Tanzania kuwapima wachezaji. Afya za wachezaji na ziongozi pia zitatetewa. Dhana ya kuwa na Bima kwa wachezaji itapelekewa kwa vyama  vyote. TOC inaweza kuwaunganisha vyama na Makampuni ya Bima ili kupata punguzo maalum kwa wachezaji na viongozi wa michezo.


Utekelezaji wa Mabadiliko haya kwa kiaisi kukubwa sana utategemea umoja, upendo, umakini na ushirikiano wa washika dau mbali mbali. Watananzania  na wapiga kura wanaombwa kuiunga mkono timu ya Mabadiliko ili katika miaka 4 ijayo kuwe na matumani na ushinidi kwenye mashindano ya Kimataifa na kuiletea heshima nchi yetu. Inawezeka, haitokuwa ajabu kama kukiwa na nia ya dhati na viogozi bora na makini, Tanzania itaona mabadilko.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania,

Khamis Said
Mgombea wa Urais, TOC
Imetolewa leo 04/12/2012 ( kwa matumizi ya Umma)Wasifu: Khamis Said ni Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BTMZ)  Zanzibar. Pia ni muanzilishi na kiongozi wa chama cha wafanya mazoezi Zanzibar.  Pia ni kiongozi wa juu kabisa katika chama cha wanfanya mazoezi ya viungo Zanzibar. Awali, amekuwa mchezaji wa soka, table tennis na Volleball. Alipata pia mafunzo wa kuogelea wakati akisoma Chuo cha Bahari na Uvuvi Zanzibar.

Ana uzoefu wa uongozi wa zaidi ya miaka 22. Amefaya kazi Serikalini kwa miaka 7 badae kwa miaka 16 sasa anafanya kazi katika Shirika la Maendelo la Kimataifa. Ameshahudhuria mikutano ya Kitaifa na Kimataifa ndani na nje ya nchi.

Amekuwa Katibu wa Kamati inayoratibu mashindano ya Mapinduzi  maarufu Mapinduzi Cup kuanzia 2011 mpaka sasa na kuwa na mafanikio makubwa katika mashindano yaliyopita amabayo yalijumisha tumu za Zanzibar, Tanzania bara na nchi za jirani. Ametoa muongozo kwa vyama Taifa Zanzibar na mafunzo ya ndani ya uendeshaji.

Mwaka 2012, ameweza kuandika mapendekezo ya Miradi kwa ajili ya Zanzibar inaratijia kupata msaada mkubwa wa  vifaa vya michezo wenye thamani ya Tshs 0.6 billion. Pia ameandika miradi mengine ya kuendeleza viwanja vya michezo Zanzibar yenye thamani ya Tshs 750 milioni. Juhudi za kutafuta wafadhili zinaendelea.

Hivi sasa ameanzisha mawasiliano na mashirika ya kimataifa ya kuendeleza michezo na kuna dalili za kupata makocha wa kimataifa wa kufundisha soka Zanzibar kwa miaka mitatu ili kuwanoa watoto na vijana katika mashule na vijijini. Msaada huu unaweza kuja Tanzania Bara pia.

Elimu: Mtaalamu wa Sayasi ya Jamii (Social Scientist). Amepata shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma alioipata chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Pia ana shahada ya Pili (Masters) ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Kimataifa aliyoipata Chuo Kikuu cha London, nchini Uingereza. Ni mzoefu sana wa Komputa na anajua programu zote za Microsoft Office.

Tabia: Msikivu, mweli, muaminifu na anaechukia dhuluma na rushwa. Anapenda haki na kufanyakazi kwa pamoja. Anakubali kukosolewa na ni mwepesi wa kujifunza haraka sana na kubadilika kutokana na mazingira.

Familia: Ana mke na watoto watatu
OFFICIAL: SHIREFA NAO WAUPIGA CHINI WARAKA WA TFF!

HAWA NDIO MAFUNDI WA PASI ZA MWISHO KATIKA MIAKA 20 YA LIGI KUU YA ENGLAND

Gazeti la Manchester Evening la Uingereza leo limetoa orodha ya wachezaji wanaongoza kwa kutoa pasi za mwisho zilizosababisha magoli katika wakati wa Premier League (1992-2012)

Hii ndio listi kamili ya wachezaji 15 waliotajwa.
1 Ryan Giggs 126
2 Frank Lampard 89
3 Thierry Henry 80
4 Steven Gerrard 78
5 Wayne Rooney 72
6 Cesc Fabregas 71
7 Didier Drogba 55
8 Dennis Bergkamp 49
9 GamstPedersen 48
10 Nani 48
11 Van Persie 46
12 Cristiano Ronaldo 46
13 Paul Scholes 45
14 David Beckham 44
15 Nolberto Solano 42

EXCLUSIVE: YAW BERKO KWENDA FC LUPOPO - NDUGU WA TWITE KUJAZA NAFASI YAKE YANGAKlabu ya Yanga wapo katika hatua za mwisho za kumtoa golikipa wao wa kimataifa kutoka Ghana Yew Berko kwenda klabu ya FC Lupopo ya Congo kwa mkopo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka Yanga ni kwamba klabu hiyo wanampeleka Berko FC Lupopo ili waweze kupata nafasi ya kumuongeza Kabange Twite katika usajili wa dirisha dogo.

Berko jana alionekana akiwa katibu wa Yanga wakiwa katika ofisi za ubalozi wa Congo wakifuatilia taratibu mbalimbali za viza ya kwenda nchini Congo kwa ajili ya kujiunga na Lupopo.

Kabange Twite
Kabange Twite inasemekana ameshamalizana na Yanga na siku chache zijazo atakuja kujiunga na timu yake mpya ili kuanza kujipanga na msafara wa klabu hiyo kwenda nchini Uturuki kwa ajili kuajindaa na ligi kuu ya Tanzania bara. 

TFF WATAKA VIJEBA VYA KONGO KUPIMWA TENA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewasilisha barua ya malalamiko yake dhidi ya matumizi ya wachezaji wenye umri
mkubwa na unyanyasaji uliofanyiwa kwa maofisa wa timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 wa Serengeti Boys wakati wa mechi ya marudiano ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana dhidi ya Congo.

Serengteti Boys iliondolewa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Novemba 18, 2012 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es salaam na baadaye kukubali kipigo cha mabao 2-0 kwenye mechi ya marudiano jijini Brazaville Jumapili iliyopita.

Hata hivyo, mechi hizo mbili zilizingirwa na matukio tata, hasa kuhusu umri wa wachezaji wa Congo ambao kimaumbile walionekana kuwa ni umri mkubwa zaidi na kusababisha TFF kuwasiliana na 

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuhusu njia zinazowezekana kupata uthibitisho wa umri wa wachezaji hao, lakini ilishindikana na ndipo TFF ilipocheza mechi hiyo ikiwa na imeweka pingamnizi.

Katika barua iliyotumwa CAF jana, TFF imerejea barua ya pingamizi aliyokabidhiwa kamisaa wa mechi ya kwanza jijini Dar Es salaam,

Bw. Chayu Kabalamula na malalamiko yaliyowasilishwa kwa kamisaa wa mechi ya marudiano kuhusu vurugu walizofanyiwa maofisa wa
timu.

Katika barua hiyo, TFF imeomba CAF iagize kuwa wachezaji wote wa Congo waliocheza mechi hizo mbili wapimwe tena kwa kutumia kipimo cha M.R.I na gharama za zoezi hilo zilipiwe na TFF; na pili Shirikisho limeomba kuwa CAF ikubali kuipa Tanzania wiki tatu za kukusanya ushahidi na kuuwasilisha Cairo kwa ajili ya maamuzi. 

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, nchi shiriki zinatakiwa kuwapima wachezaji wake kwa kutumia kipimo cha M.R.I ambacho kinaweza kutambua umri wa vijana walio chini ya miaka 17 na kwamba matokeo yake yanatumwa CAF, ambayo itahifadhi matokeo hayo hadi hapo kutakapotokea pingamizi na ndipo itafanyia kazi kwsa kutoa matokeo ya vipimo hivyo.

“Ni matumaini yetu kuwa suala letu litafanyiwa kazi na kutolwewa ufumbuzi ili kulinda soka la vijana barani Afrika dhidi ya vitendo
vilivyokomaa vya udanganyifu wa umri,” alisema katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana, kocha Jacob Michelsen alisema alishangaa kuona wachezaji wenye umri
mkubwa zaidi wakichezeshwa kwenye mechi ya marudiano, lakini akaisifu TFF kuwa inafuata njia sahihi ya maendeleo na haina budi
kuendelea na programu yake ya soka la vijana. 

"Najivunia vijana wangu kwa kuwa walijituma kwa muda wote pamoja na kwamba wenyeji waliongeza wachezaji wenye umri mkubwa zaidi kuliko waliokuja huku," alisema kocha huyo kutoka Denmark.

"Kitu cha msingi ni kufuata njia sahihi ya kuendeleza soka na natumaini TFF iko kwenye njia sahihi na itaendelea na programu yake ya vijana. Hakuna njia ya mkato kama mnataka maendeleo. Ni lazima tufuate njia sahihi na matunda yake tutayaona baadaye. 

"Kila mara nasema mambo (ya vijana) huchukua muda mrefu (Things Take Time) na hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.
"Wenzetu walitumia njia za ajabu na hata hiyo penati ya bao la kwanza haikuwa faulo. Ilitokea nje kabisa ya eneo la penati. Refa
alimuangalia kibendera akaona ametulia, akamuangalia beki mchezaji akamuona amesimama, mara akaangalia juu na kupuliza filimbi kuonyesha kuwa ni penati." 

Naye kocha msaidizi, Jamhuri Kihwelo alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujika machozi wakati alipoelezea jinsi alivyoshambuliwa na askari kabla ya mchezo huo.

AZAM YATHIBITISHA KUMUUZA MRISHO NGASSA KWA $75,000 EL MERREIKH YA SUDAN

Azam FC leo imemuuza mchezaji wake Mrisho Halfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh katika majadiliano yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.
El-Mereik wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.
Kuuzwa kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza Mrisho Ngasa.
Wakati Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye kufikia dau hilo waweze kumuuza.
Meng

i yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa.
Mrisho Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati baada ya TP Mazembe.
Azam FC inamuuza Mrisho Ngasa kwa kuzingatia umuhimu wa maendeleo ya mchezaji mwenyewe kimpira na kwa kipato, pia kwa kuzingatia kwamba Tanzania inahitaji wachezaji wengi wanaocheza nje kwenye vilabu vikubwa ili wanaporudi waweze kuisaidia timu ya Taifa.

STARS WAJIFUA VILIVYO: YAOMBA HAKI KATIKA MECHI YA KESHO DHIDI YA UGANDA

Kocha wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ameomba ‘fair play’ kutoka kwa muamuzi wa mechi ya leo (kesho) dhidi ya The Cranes ya Uganda katika nusu fainali ya mashindano ya Cecafa Challenge Cup Jijini Kampala.

Kocha huyo aliyasema hayo mara baada ya Stars, inayodhamniniwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kumaliza mazoezi  katika Uwanja wa Chuo Kikuu Kyambogo.

“Vijana wamejiandaa vizuri kabisa na wote wako katika hali nzuri ya kucheza ila tunachoomba ni fair play kutoka kwa muamuzi maana tunacheza na wenyeji ambao wana watazamaji wengi,” alisema.

Alisema timu zote mbili ni nzuri na iwapo muamuzi atachezesha vizuri basi utakuwa ni mchuano mkali. “Vijana wana ari na mchezo huu na tukipewa fair play tutacheza vizuri kama tulivyofanya katika michezo  dhidi ya Rwanda,” alisema Poulsen.

Muamuzi wa mechi ya Cranes na Stars ni Mohamed El Fadil kutoka Sudan ambaye pia alichezesha mechi ya Stars dhidi ya Rwanda.

Alisema ana furaha kwa kuwa hakuna majeruhi hata mmoja na pia aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha umoja na nidahmmu ya hali ya juu. “Hawa wanakaa kama familia si unawaona walivyo pamoja?” alisema Poulsen na kuongeza kuwa hilo ni muhimu sana kwa mchezaji.

Naye kocha msaidizi, Sylvester Mash alisema Stars ina nafasi kubwa sana ya kushinda mechi hii kwa sababu wenyeji wao, The Cranes watakuwa wanacheza kwa wasiwasi kwa kuwa wako nyumbani .
“Timu yetu iko motivated kabisa na ukizingatia Uganda wako nyumbani, wao ndio wana tension kubwa zaidi,” alisema na kuongeza kuwa mchezo huu utakuwa wa kusisimua sana.

Akizungumza kutoka Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema Stars ina kila sababu ya kutinga fainali na kunyanyua kombe kwa mara ya nne.

“Sisi kama wadhamini tunasubiri ushindi maana tuna imani na Stars na hatua waliyofikia ni nzuri nay a kutia moyo kwa hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi na kuufuatilia mchezo huu kesho,” alisema Kavishe.

Mchezo wa Stars na Cranes utatanguliwa na semi fainali ya kwanza kati ya Zanzibar na Kenya ambao pia ni mchezo wa kusisimua kwani timu zote mbili zimeshaonyesha uwezo mkubwa.

Kocha wa Zanzibar Salum Nassor ameshatangaza mara mbili akiwa Zanzibar na hapa Kampala kuwa iwapo hataondoka na kombe basi atabwaga manyanga.
Fainali na Cecafa Challenge zinatarajiwa kufanyika Jumamosi Disemba 8 na mechi ya kumpata mshindi wa tatu na nne itachezwa siku hiyo hiyo pia.