Kocha wa zamani wa Senegal Bruno Metsu amekiri kwamba aliwahi kuwaambia wachezaji wake kwamba wacheze mechi kama wanapigania maisha yao - ikiwa ni njia ya kuwahamasisha, lakini sasa kocha huyo mwenye miaka 59 anapigania maisha lakini sio kwenye soka bali ni dhidi ya ugonjwa wa kansa.

Wakati alipoiongoza Senegal kwenye kombe la dunia 2002 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa, wachache wangeweza kutabiri kilichokuja kutokea baadae. Goli la ushindi wa Papa Bouba Diop liliwapa ushindi Sengal dhidi ya mabingwa wa dunia, lakini kocha huyo mwenye nywele ndefu aliiwezesha timu ya Simba wa Teranga kucheza robo fainali ambapo wakaja kutolewa kwa ushindi mwembamba na Uturuki katika dakika za nyongeza. 

Miaka 10 baadae Oktoba 2012, baada ya kuanza kuumwa akiwa Dubai na kukimbizwa hosptiali, Metsu aliambiwa alikuwa ameanza kuugua ugonjwa wa kansa ambao ulikuwa unashambulia ini lake na mapafu.

"Ilikuwa ni habari iliyonistua sana. Nilikuwa na Viviane, mke wangu na tulikuwa tunalia tu. Unaanza kufikiria kuhusu watoto wako na kila anayekuzunguka na kukutegemea. Nilianza matibabu ya chemotherapy mara moja na nilipoenda hospitali nilikuwa nipo kwenye kiti cha wagonjwa wasiweza kutembea, nilikuwa mdhaifu sana lakini hakujawahi kutokea muda nikakata tamaa. 
"Mara nyingi kama kocha, ni kawaida kuwaambia wachezaji wako 'leo chezeni kama mnapigani maisha yenu'. Lakini sasa na mie nacheza mechi ya maisha yangu. Nilipomuona Eric Abidal na kipindi chake cha TV, nilipata hamasa na nguvu kupigania maisha yangu," alisema Metsu akizungumzia namna alivyohamasisha na Abidal ambaye hivi karibuni alishinda vita yake na ugonjwa ulikuwa uliokuwa unashambulia ini lake.



Metsu aliwahi kucheza soka lakini kwa muda mfupi kabla ya kuamua kuingia kwenye maisha ya ukocha lakini alikuja kupata mafanikio wakati alipoanza kufundisha soka barani Afrika mnamo mwaka 2000 wakati alipoanza kuifundisha Guinea kabla ya kuhamia Senegal. Aliiongoza nchi hiyo kucheza fainali ya kwanza na pekee ya kombe la mataifa huru ya Afrika nchini Mali walipofungwa katika mikwaju ya penati na Cameroon, miezi sita kabla ya kuiongoza nchi hiyo kucheza kombe la dunia  enjoyed a modest playing career before an equally unspectacular start to life as a coach until his African adventure began in 2000 when he took over the Guinea helm for two years before moving to Senegal.

Sasa baada ya kushindwa kubeba makombe huko nyuma, sasa Bruno Metsu anataka ushindi wake dhid ya magonjwa ili aweze kupata zwadi ya kuendelea kuishi. Mwenyezi mungu atamsaidia kushinda vita hii. Ameen