Search This Blog

Sunday, April 8, 2012

HATIMAYE LULU AZUNGUMZA ASEMA HAKUMSUKUMA KANUMBA

Baada ya kugoma kutoa maelezo kwa takribani siku nzima ya jana, mwanadada Lulu hatimaye amezungumza na polisi na kuelezea kilichotokea baina yake na marehemu Steven Kanumba. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi uliotokea kati yake na rafiki yake wa kike Lulu.

 "Kanumba amefariki usiku wa kuamkia leo (jana) majira ya saa tisa usiku, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ugomvi kati yake na rafiki yake wa kike anayejulikana kwa jina la Elizabeth Michael 'Lulu' mwenye umri wa miaka 18.

Alisema kabla ya ugomvi huo kutokea kati yao wakiwa chumbani, simu ya Lulu iliita na akaamua kutoka nje kupokea kitendo kilichomuudhi Kanumba.

Kamanda Kenyela alisema Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti akitaka aelezwe kwanini alitoka nje kupokea simu huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.

Aliongeza baada ya Lulu kuona Kanumba akimfuata aliamua kukimbia kutoka nje ya geti , lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba  alimkamata na kumrudishwa ndani.

Kamanda Kenyela, alisema Kanumba akiwa amemshikilia waliingia wote chumbani na kufunga mlango.

Hata hivyo, alisema haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu anadi kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba.

Kamanda huyo alisema Lulu anaeleza kuwa baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini.

Alibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Kanumba alikuwa amekunywa Whisky (pombe kali) aina ya Jacky Daniel, hata hivyo, bado wanachunguza zaidi kujua kama kweli Kanumba alilegea tu na kuanguka, ama alipigwa na kitu kizito kichwani au alisukumwa kwa nguvu na kumfanya aangukie kisogo.

“Uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani kwa tuhuma za mauaji,” aliongeza Kamanda Kenyela.


SOURCE: mwananchi.co.tz

59 comments:

 1. HII NI MOJA YA USHAHIDI YA UTENDAJI MBOVU WA JESHI LETU LA POLISI ,YAANI UTOWAJI WA TAARIFA ZA KIPOLISI HOVYO KABLA UCHUNGUZI HAUJAKAMILI INAWEZA HATA USHAHIDI KUINGILIWA KWA NIA MOJA AMA NYENGINE KWA UPANDE WOWOTE ULE YAANI MLALAMIKAJI AMA MLALAMIKWA,,,RABBI TUPE SUBIRA

  ReplyDelete
  Replies
  1. MBONA WATZ HUWA HATUISHI KULAUMU? HAO POLICE WANA TAALUMA ZAO ZA UPELELEZI, TUWAACHE WAFANYE KAZI YAO!

   Delete
 2. Alitoka nje vipi sasa wakati mdogo wa marehemu alikua humo ndani na akataka kuamua lakn wakafunga mlango?Jeshi la polisi halitakiw kutoa taarifa nusunusu si wangekaa kimya tu hadi uchunguz ukamilike,.hapa ni kutaka kupindisha kitu,.but if its tru Lulu anahusika huku kwetu tunasema "dhulma kafara" Mwenyez Mungu hatakuacha bila kukuadhibu kabla ya umauti wako haujakufika

  ReplyDelete
 3. Mdau tuache mazoea ya kulaumu kila kitu,kutoa taarifa ya tukio kuna ubaya gani?kumbuka watu wengi wengependa kusikia taarifa ya jeshi la polisi,ulitaka waendelee kukaa kimya ili mseme pia?wametoa taarifa iliyopo hadi sasa na wao ndio wanajua wamefikia wapi

  ReplyDelete
 4. Na majeraha ya kichwani aliyatoa wapi pamoja na Lulu naye katoa wapi majeraha kulingana na taarifa tunazopata kutoka vyombo vya habari kv magazeti na mitandao?

  ReplyDelete
 5. Kutoa taarifa si jambo baya, lakini nampa pole sana huyu mdogo wangu Lulu kama mwabsheria wake kamshauri hili basi anefungwa, alipolegea means alishapunguza umbali wake na flow hvo basi kuanguka kwake hakutegenwa kuleta fatal wound. Siwezi kusema ni uongo bali kuna kazi kisayansi kuprove maneno ya LuLU .

  ReplyDelete
 6. watu wengine kukurupuka kutoa maoni..!
  sasa kama jeshi la polisi lingekaa kimya wewe mpumbavu si ungepiga kelele zaidi kusema jeshi limekaa kimya.jeshi la polisi sio kama halina mbinu,wewe unafikiri kuwa LuLu amesema hayo tu?usipende kulaumu.pia kuhusu wao kutoka nje,jamani HAKUNA ALIYEKUWEPO,pia unafikiri kuwa jeshi la polisi halitamuuliza lolote huyo. nakushauri usiwe mkimbiliaji kulalamika.kifo ni kitu kingine, sio mchezo wa kuigiza,embu fikiria kidoogo, W.Houston, alifariki lini na majibu ya sababu za kifo chake yalitoka lini,au Michael Jackosn alikufa lini na majibu yalitoka lini.sasa iweje bongo iwe leo kwa kesho?
  swahiba.

  ReplyDelete
 7. kiukweli tuwe makin jaman tukumbuke kanumba ni mpenzi wa wengi kila jicho lipo kwenye habari zinazotolewa na jeshi la polisi kama asingesukumwa nywele zingebaki ukutani? na mapovu yangetoka mdomoni? na mapovu yanahusika vp kama kasukumwa jaman mapolisi tunawaamin sana. na tunaamini kazi yenu

  ReplyDelete
 8. Ni namna ambavyo jeshi la Polisi limeshindwa kazi ya kulinda taarifa muhimu!

  Hata hivyo nampongeza Lulu kwa kushindwa kuzungumza chochote jana! Haki yake ya raia bado anayo; Hata hivyo bado lawama ziende kwa watu wa haki za binadamu kwani hawatakiwi kuangalia nani kapotea ni kuangalia haki ya aliyebaki! Wanatakiwa wamuwekee wakili ili asimamie maelezo anayotoa Polisi
  Hatuwezi kuhukumu kwa sababu ya mapenzi yetu!
  Pole

  ReplyDelete
 9. whatever the case,she is guilty

  ReplyDelete
  Replies
  1. Samahani,unaitwa Judge nani? Na ruling yako umetumia ushahidi gani. Mbona hata kesi haijaanza,Elimu ya upe ya Nyerere imeua Taifa .

   Delete
  2. umenichekesha kweli ! lol:

   Delete
  3. acheni mahakama n vyombo vingine vya sheria vifanye kazi yake.Mapenzi na ushabiki si mahali pake kwa sasa

   Delete
 10. yaliyomo yamo na mshikwa na ngozi ndio mla nyama so kama uchunguzi haueleweki duniani basi si wapenzi wa kanumba basi uchunguzi wetu tutaufanyia mbinguni na kuurudisha duniani siku zote penye ukweli giza haliwezi ingia sababu hii si masihala lakini kumbukeni ukifanya nawe utafanywa haijalishi siku gani ameni....R.I.P KANUMBA

  ReplyDelete
 11. its sad life. kila kitu kinawezekana kuwa hajasukumwa au kasukumwa na here ni mfano nilioandika ktk ma wall:

  Kanumba Anaweza Kuwa Kafa Na Heart Attack, Or Pressure Ilimpanda Au Kushuka. Haya yote yanawezekana lkn pale lawama tunaziweka juu ya Lulu na wakati hakuna anaejua pale nyuma za zile kuta cha chumba kuliendelea nini ni kujichumia DHAMBI ZA HISIA na hizi dhambi zimelaaniwa n hausameheki ktk dhambi za hisia.

  Kanaumba anaweza kuwa alianguka baada ya moyo kusimama ghafla kwa hasira alizokuwa nazo au pressure either ilipanda au kushuka na kujikuta ameangukia kitu kwenye kichwa chake na ukute lulu hata hakumgusa kwa kumsukuma kabisa na pia inawezekana Lulu alimsukuma katika kujitetea asipigwe! so yote yanawezekana , wacha tuhukumu baada hayo wajuzi wa kuchunguza watupe habari kamili.

  ReplyDelete
 12. Na yale makovu tuliyosoma kwenye vyombo mbalimbali vya habari wameyatoa wapi?

  ReplyDelete
 13. Huyo lulu inawezekana akashtakiwa kwa MAN SLOT LAW kama hausiki kama anayodai lakini bado tunataka kujua zaidi kutoka kwa police na Madaktari wanaochunguza! R.I.P Kanumba the Great!

  ReplyDelete
 14. Jamani kuropoka ni kosa makosa mawili ya ushaidi wa matata waweza kumtoa mtuhumiwa hatiani hivyo tuwe wapole tuone Polisi wanasema nini

  ReplyDelete
 15. mi i guess siku ilikuwa imefika ...kama wanavyoseama he was from the bathroom so he was wet ...i guess katika kuvutana vuta aliteleza akaanguka na siku ilikuwa imefika ya Kanumba ..ambapo hakuana hajuaye siku ya kufa so i guess we shudnt judge things just like that. kwani wa ngapi wanatoka juu ya gorofa mpaka chini and still survive so it was the day .

  ReplyDelete
 16. tumwombe tu alale mahala pema peponi the great hakuna kifo kishokuwa na sababu.

  ReplyDelete
 17. askari wacheni hizoooo, unusunusu wa habari tena kwa tukio kama hilo haupendezi, aidha mtamfanya Lulu awe katika wakati mgumu, ilhali pengine hahusiki katika icho kifooo, yeye ni sababu tuu, unajua kua kila kifo kina sababu nae lulu amekua kama ni sababu tuu, ila sio muuaji namutetea na hata kama kaua basi si kwa makusudio, hapo labda itekelezwe sheria ya kuua bila makusudio ya kifuungo cha miaka mitatu.Poleni na msiba - RIP Kanumba na heri ya
  pasaka wana FB
  Nimekua nikafatilia judgements
  zinazotolewa sehemu tofauti kuhusiana
  na msiba wa Kanumba tangu jana, ni
  kweli hki kifo kinauma na kusikitisha sana!
  ILA.......
  Tukumbuke kwamba hawa vijana
  walipigana na hata polisi wanasema
  huyo lulu nae ana majereha
  Kweli mtoto lulu amekua mkorofi sana na asiesikia ya wakubwa!!
  Mtoto lulu amekua akiulilia ukubwa kwa
  gharama yoyote ile - ila kwa hili ni
  kubwa mno jamani hata kwetu watu
  wazima kulibeba si shughuli
  ndogo.................. kwa hili Watu wengi tumekua
  tukimsemea maneno makali mno lulu
  bila kuangalia upande wa pili wa
  shilingi.
  Naamini kabisa lulu hakuwa amekusudia
  kuua........... Ingewezekana pia katika hilo yeye lulu
  ndio angekuwa amekufa na kanumba
  kuwa jela.....je hili lingechukuliwaje??
  Ninachoweza kusema mimi tusubiri
  sheria ifanye kazi yake na kama itatoke
  lulu kuwa huru basi tumpe sapoti......naamini kwa hili atakua
  amejifunza kitu kikubwa sana na
  atabadilika.
  Kwa huu umri wake bado ana nafasi
  kubwa sana ya kubadilisha maisha yake
  kama atapata ushauri nasaha, upendo na kutonyanyapaliwa na naamini atakuwa
  mtoto mwema tena kuweka historia
  mpya ambayo kila mtu ataipenda
  Kwa wale wakristo nadhani
  wanaikumbuka historia ya Saul (Paulo)

  ReplyDelete
  Replies
  1. Uko sawa kabisa, hii ni story wimbo wa Kafia getho, sisi raia wa nje ya 2kio si rahis kuelewa, ila nadhan nibahati mbaya sana iliyotokea na pia Pengine imetokea ilikumpa fundisho huyo mtoto lulu, kwan Perception yake mbaya kwa jamii!! Ni kifo cha bila kukusudia na ndio maana walikutana ili watoke out tht nyt..

   Delete
 18. Sheria na vigezo vitumike kumtia hatiani kama atabainika basi apelekwe mahakani
  BY ANDREW NGALAWA

  ReplyDelete
 19. Ivi hayo maelezo yantolewa kwa polosi ama kwa waandishi wa habari, mbona zinakuja tofautitofauti.ivi kanumba aweze kumkimbiza adi getini na kumludisha ndani kwa nguvu thn ndio adondoke na kujigonga sio ina maana aliishiwa nguvu kwa kumkimbiza au lulu anatuelezaje,pia mdogo wake hakuona wala kusikia hayo makimbizano adi atoe maelezo tofauti?Jeshi la polisi lichunguze vizuri

  ReplyDelete
 20. Yote tisa,kumi Mungu Lulu na Marehemu Kanumba ndio wajuao ukweli ila shahidi wapili ndio kashatuacha na Judge mkuu ambae ni Mungu,ukweli wote ataudhihirisha hiyo siku ambayo siri zote atazifichua na tukumbuke kuwa mambo yote tunayo fanya hapa duniani nimifano tu ila ukweli kamili Mungu ndie mjuzi wa kila kitu.
  sote ni wamungu na kwa mungu ndio maregeo

  ReplyDelete
 21. Mapenzi bwana, mimi naumia sana na hawa watu wanaowapronounce wenzao dead bila kujaribu cpr na kuwarecucitate hospital for sometime or even days. Wewe unamkuta mtu kalala chini kaanguka , utasemaje keshakufa?? Ilihali watu wanazimia hata siku tatu. Jamani in d future tujaribu kuokoa life rather than kuwapeleka watu mochuary wakiwa wazima. Watu tujaribu kuwa na angalau watu wa2 wa3 wanaotupenda kwa moyo mmoja ili ktk janga lolote kubwa wao ndio wawe wa kwanza kupigiwa simu. Hao ndio wangeweza kumfanyia cpr na kumpeleka hosp na kumwomba dr amwekee machine ya kustua moyo hata kwa siku tatu. Sio wanakuja watu ambao wanakushika tu mkono na kukufumba macho na kuanza kukutangaza kwamba umekufa!! Je walijaribu mouth by mouth (cpr) kumsaidia kupumua???? SaaAd!

  ReplyDelete
  Replies
  1. my friend,unasema daktari kucheki wakati wametoka ktk mgomo wana stress zao..hiyo machine ya kushtua moyo unaichaji bongo ipo wapi...dockta kufanya operation ya jicho hadi retina au jicho lipo mkononi akurudishie na uone ckudanganyi tanzania nzima yupo mmoja tuu..mtafute sasa utackia apo ulaya,south africa,madocta wa macho wengne ni kutoa cataract basi...hamna vyombo muhim kutazama maendelea ya mgonjwa,watu wanazimia miaka 30...kwa wale watu wanaopataga stroke na kushindwa kuongea,huwezi amini tanzania nzima ni docta mmoja tena yupo rwanda last three years i heared..docta mwingine wa speech ni mama frm germany..sasa sie makabwela tawapata wapi apointment laki tatu kuona sura. Raisi wetu naye anajenga studio,kweli nzuri...hosptal unapaka rangi majengo jamani jamani tunauana bongo.
   Kuhusu lulu anaweza walk out clean..hao pokice watajuaji kama alisukumwa au laa,frensic wenyewe uchwara mtupu hawana vifaa wala kujua wapi kuanzia nakwambia hawajachunguza ukuta hapo alipojigonga au sakafu ni watatazama kichwa basi..yule mtu mzima ana weight,jumla pombe..wanasemaga kumsukuma mlevi,mlevi hata ukimshika unadondoka naye sembuse hako katoto..ujue hata kanumba aliweza mpa hug akimwambia 'baby nakuoenda sana'wote chini puu..sasa je hajafa hapo..waende zao.

   Delete
 22. I think we have something to learn from the death....Hasa mastar ho to live like a star... bt also how death come to us haina hod so lets prepare ourselves...!!!!!!!

  ReplyDelete
 23. embu futa hiyo kauli ya kusema she is guilty, coz u dont have that jurisdiction

  ReplyDelete
 24. Tatizo la wabongo mnavamia fani ambazo sio zenu wala hamna taaluma nazo. Acheni polisi wafanye kazi yao.

  ReplyDelete
 25. Tusipate shida kuzungumza mengi, kulaani Polisi, kumlaani Lulu mtoto wa watu. Sote tuungane kuomba Lulu aachiwe huru, halafu tutaona dhamira ya nafsi yake, wala asipewe adhabu yoyote!

  ReplyDelete
 26. Inasikitisha sana,kwa vyovyote vile lulu ana hatia,kama kweli ni mtu wake na hakufanya kibaya kwa nini akatoroka baada ya kuona mwenzie kazidiwa? ilitakiwa angekuwa wa kwanza kutafta namna ya kumsaidia,pia aeleze ukweli wa yaliyotokea humo ndani,this is sand na aelewe dhambi kuu imemuangukia,sipaswi kuhukumu ila namshauri atubu kwa mola wake.

  ReplyDelete
 27. wamchunguze vizuri huyo lulu kwa sababu maelezo yake yanaonekana ya uongo kabisa

  ReplyDelete
 28. mbona inasemekana kanumba hanywi pombe?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Yaani hata mie hapo ndipo kichwa kilinizunguka.Hagusi kilevi na wala hapigigani...tazama Clip ya mahojiano yake na Mkasi.

   Delete
 29. ilishatokea kikubwa ni kumwombea kwa mungu amlaze mahali pema peponi maana hakuna mpaka sasa aliyethibisha kwamba chanzo cha kifo chake ni nini. Na tusiwe wepesi wa kuhukumu 2vute subira uchunguzi ufanyike ndo 2jue lipi la kufanya. poleni wote 2lioguswa na msiba kwa namana moja au nyingine.

  ReplyDelete
 30. Yote kwa yote kama lulu alitoka na akamludisha basi zilikuwa zimetimia usiwe mjadala mkubwa taifa bado linatungoja tulitumikie.

  ReplyDelete
 31. Ril cpendagi tabia za lulu ila tuachane mambo ya kumlaumu cuz sote hatujui what happened there na hope lulu anajua kila k2 so tuwaachie polisi wafanye kazi yao ila mi simuhusishi kabisa yule dogo na kifo cha the great...R.I.P kanumba 2nakupenda sana na ctak kuammini tutamiss movie zako, nitamiss kolabo lako ukiwa na benny.

  ReplyDelete
 32. Wote mnao laumu mnakosea ingkuaa hvvyo tuxngfka xo xbiri mambo yaishe xio mnatoa lawama bila uhakiki ingekua wewe ndio victim halafu watu wanalaumu kitu wasichokijua ungejisikiaje tuweke emotion pmbeni tuangalie uhalisia lolote linawezekana mda wwte xo nivizuri tuwe wawazi n tusitafute mahali pa kutolea hasira let us b truly!

  ReplyDelete
 33. Replies
  1. Kwa wote.Marehemu na mtuhumiwa!

   Delete
 34. 2muombee ndugu yetu ahifadhiwe mahara pema peponi ss hatuwezi kutoa hukum isipokua 2waache police wafanye uchunguzi zaidi na watupe jibu kamili. 2likupenda xana n' tutakumic xana kwenye game. r.i.p kanumba da grt!

  ReplyDelete
 35. Pamoja na Ubishi wote..............ninachokielewa mimi ni kuwa kanumba ameaga dunia, na mapenzi ndiyo yaliyomponza..................and TUTAIMIC SANA KAZI YAKE..........Acheni kugeuza kifo kuwa uwanja wa siasa za KIJINGA KAMA ZILE ZA ARUMERU MASHARIKI

  ReplyDelete
  Replies
  1. unasema coz siyo ndugu yako

   Delete
 36. mimi naona tuwaachie police tutajua mwishi wake,nakila mtu atakufa kwa staili yake.na pia wote walikua na makosa maana wanafanya tendo la ndoa bila kufunga ndoa au mnaonaje jamani?

  ReplyDelete
  Replies
  1. kazi ya mungu haina makosa tumwombe Mungu amjalie maisha yasiyo ya misukosuko kama hapa duniani. Yote mapenzi ya Mungu tutasema mengi bt siku iku ifika imefika.

   Delete
 37. kwa mujibu wa maelezo ya mdogo wake na kanumba (tuliyoyaona ktk tv) hakusema kwamba lulu alikimbilia nje na kanumba kumrudisha so nakuwa sielewielewi.Lakini,mtu akidondokea kichwa matokeo yake huwa ni kutokwa na damu puani au mdomoni sasa inakuwaje kanumba akatokwa na mapovu???

  ReplyDelete
 38. kwakweli hasa na mimi hicho cha kutokwa povu ndo kinanishangaza. yawezekana lulu hausiki na kifo cha kanumba au katumiwa kama chambo indirect bila yeye kujua kinachoendelea au yawezekana anahusika na kifo hicho but bila kukusudia kutoa uhai wa aliyekuwa mpenzi wake. nadhani uchunguzi ufanyike na haki itendeke

  ReplyDelete
 39. Hapa ndipo roho inaponiuma sana mnapotamka neno mpenz wake, kiukwel ni kwamba Kanumba alikuwa mtu mashuhuri sana ktk kazi yake, ameitangaza vema sana sanaa yetu, lkn ktk issue ya LULU, mungu anisamehe sana nipo against nae, LULU ni mtoto mdogo na Kanumba alikuwa analifahamu hilo, hakupaswa kuwa na mahusiano nae hasa ukizingatia kuwa yeye ndiye aliyekuwa anamfahamu sana binti huyu, alikuwa anamrubuni, waliulizwa sana kuhusu uhusiano wao, wote walikataa na ni kwa sababu walijua fika kuwa huyu binti ni mdogo na ikionekana kuwa Kanumba ana uhusiano nae watu watapiga kelele na Kanumba angefikishwa kwa pirato,ngoja tuone naamin sheria itachukua mkondo wake na haki itatendeka japo me nasikitika kwa nn sikusomea sheria ili niwatetee watu kama hawa, nitaendelea kumuombea LULU kwn hili si kosa lake na kama ni lake nitamuombea ili mungu amsamehe kwn atakuwa amefanya hivyo sababu ya ulevi wa mapenzi.

  ReplyDelete
 40. Ishengoma, lulu mdogo kwako, kwna uliambiwa kanumba ndo mwanaume wake wa kwanza??? ukipewa list unaeza shika kichwa tena utakuta katka mawaume aliotembea nao ni ALI KIBA na KANUMBA ndo wadogo kiumri

  ReplyDelete
 41. Ama kweli Freemason wakiamua kufanya jambo Lao hamna mtu wakuzuia.

  ReplyDelete
 42. Ama kweli Freemason wakiamua kufanya jambo Lao hamna mtu wakuzuia.

  ReplyDelete
 43. Ama kweli Freemason wakiamua kufanya jambo Lao hamna mtu wakuzuia.

  ReplyDelete
 44. huyo LuLu ni muuwaji kabisa ameisha onekana, Tanzania inakuaga natabiambaya mtu akipata kipaji chake wanadamu hawamupendi tena, watakua ni hawohawo wenzake ndo walipanga mamboyao mabaya wakaona LuLu ndoyuko karibu naye yafaa wampange iliwapate njia ya kumuuwa. Wasaniiwenzake walimusikilia wivu, yafaa muwafatilie hayo wat wawili Alikiba na LuLu wanaweza wakatoa sili, nisili yawo na Mungu ndo wanajua, kama walimuuwa mungu anaweza akawalipa nahao walio muuwa

  ReplyDelete
 45. huyo LuLu ni muuwaji kabisa ameisha onekana, Tanzania inakuaga natabiambaya mtu akipata kipaji chake wanadamu hawamupendi tena, watakua ni hawohawo wenzake ndo walipanga mamboyao mabaya wakaona LuLu ndoyuko karibu naye yafaa wampange iliwapate njia ya kumuuwa. Wasaniiwenzake walimusikilia wivu, yafaa muwafatilie hayo wat wawili Alikiba na LuLu wanaweza wakatoa sili, nisili yawo na Mungu ndo wanajua, kama walimuuwa mungu anaweza akawalipa nahao walio muuwa

  ReplyDelete
 46. Kurudisha roho iliyopotea au kulipiza ili kufidia kosa sioni kama ni jambo la msingi hapa. Marafiki hukosana na kupatana, au kutosamehana kila mtu akachukua njia yake. Hawa wawili inawezekana hii sio mara ya kwanza kukosana kama ni kweli basi kanumba hasingekufa ilikuwepo nafasi ya kupatana wakaendelea na maisha yao bila ya sisi kuhusishwa. Wengi tunaoishi leo tunajua kuwa migongano katika maisha ni jambo la kawaida. Kwa kupitia juu juu maisha ya kanumba inaonyesha namna alivyokuwa mtu wa kuhubiri amani na msamaha. Kama kweli issue katika hili tukio lilihusisha kilevi, wivu na jazba; kuna uwezekano tukio la kifo kutokea kwa bahati mbaya. Uhusiano wa wawili hawa ulijaa usiri kwa namna ambayo tukio la kifo ndio imekuwa fursa ya kufunua ukweli wa mambo. Naamini tukio zima ni fundisho kwa sisi tulio hai kuchagua namna ya kutengeneza hadithi nzuri tutakayoicha nyuma baada ya kuaga dunia. Issue ya kujali maadili mema ni jambo muhimu sana katika tukio hili la watanzania wenzetu. Haipendezi kuhukumu, kuhalalisha, kukosoa au kuwafanyia kazi polisi. Kama walivyo wasanii kama kioo cha jamii, basi tujifunze yanayotufaa toka kwenye tukio lao.

  ReplyDelete
 47. hii kesi imeshaisha kifamilia hapa ni kusubili kumuona lull kitaa

  ReplyDelete
 48. hi jamani mimi nionavyo kesi imeisha kifamilia ushaidi hii subilini kumuona lulu kitaa

  ReplyDelete