Search This Blog

Saturday, February 15, 2014

LIVE SCORE: MBEYA CITY 1 - 1 SIMBA SC - YANGA 5 - 2 KOMORIZINE FULL TIME


FT' Mbeya City 1 - 1 Simba

90+4' Mbeya City 1 - 1 Simba

90' Mbeya City 1 - 1 Simba

Ashanti United 0- 0 Kagera Sugar - Full time

85' Mbeya City 1 - 1 Simba

Ruvu Shooting 1 - 0 Coastal Union

Komorozine de Domoni 2 - 5 Yanga 
Kiiza 13, Ngasa 22, 87, 90 Msuva 37

75' Mbeya City 1 - 1 Simba

 52' Mbeya 1 Simba 1 Amisi Tambwe

Kipindi cha pili cha mchezo tayari kimeanza uwanja wa Sokoine.

Mpira ni mapumziko Mbeya City wanaongoza kwa bao moja.

Wakati huo huo  - 55` Ashanti utd 0-0 Kagera Sugar

26`Mbeya City 1-0 Simba


18" Mbeya city 1-0 Simba (Bao la penati)


10" Mbeya City 0-0 Simba SC


5" Mbeya City 0-0 Simba SC


CAF CHAMPIONS LEAGUE: KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA LEO DHIDI YA KOMOROZINE DE DOMONI


1. Deogratias Munish "Dida" - 30
2. Mbuyu Twite - 6
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Kelvin Yondani - 5
6. Athuman Idd "Chuji" - 24
7. Saimon Msuva - 27
8. Haruna Niyonzima - 8
9. Didier Kavumbagu - 7
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamis Kizza - 20

Subs:
Barthez, Juma Abdul,Luhende, Rajab, Domayo, Dilunga n Bahanuzi

MAONI KUHUSU USAJILI WA OKWI: MMEIFIKIRIA RUHUSA YA ANGALIZO KUTOKA FIFA KUHUSU OKWI?

 • Na Baraka Mbolembole

 • Emmanuel Okwi, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, ameruhusiwa kuichezea klabu yake ya Yanga na Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA. Awali, Okwi alizuiwa kuiwakilisha Yanga na kamati ya sheri na hadhi ya wachezaji ilimsimamisha kwa muda mchezaji huyo kuitumikia, Yanga ili kuulizia, FIFA uhalali wa mchezaji huyo kuichezea Yanga. Majuzi, FIFA, wametoa taarifa kuwa Okwi anaweza kuichezea klabu yake mpya kwa sasa, ila wakisema kuwa sheria itachukua mkondo wake endapo mchezaji huyo ataonekana ni tatizo katika ' ukungu' uliotawala katika usajili wake.

 •  JE, OKWI ANAPASWA KUICHEZEA YANGA MSIMU HUU?. 

 • Ndiyo, kama walivyosema, FIFA, Okwi amepewa ruhusa ila kitendo cha Yanga kumtumia kinaweza kuwaletea matatizo katika siku za mbele, endapo itabainika Okwi alifanya udanganyifu katika klabu yake ya awali, Etoile du Salehe ya Tunisia, ambao bado wanasisitiza kuwa mchezo huyo ni mali yao na hawajui alipo tangu, mwezi Mei, 2013.

 • TFF KATIKA MTEGO?

 • Wao wenyewe tayari wamesema kuwa watakaa na kulipitia suala hilo katika mtazamo wa ndani ya nchi. Shirikisho hilo la soka Nchini, limesema kuwa ruhusa ambayo FIFA, wametoa katika matumizi ya Okwi kwa wakati huu , wameikubali. Umejaribu kujiuliza itakuwaje siku za mbele mchezaji huyo akionekana ni tatizo?
 • Itavuruga mpira wa Tanzania, hasa endapo Yanga watakuwa wamemtumia katika michezo ya ligi kuu.Labda kwa vile kuna kumbukumbu kubwa mbaya kuhusu uvunjifu wa kanani na sheria mbalimbali katika soka la Tanzania, Yanga wakamtumia kwa kigezo cha kutumia udhaifu huo hata kama itakuja kugundulika kuwa mchezaji huyo ni ' batili kwao'. Ila, sheria iliwafunga katika suala la kumcheza mchezaji hasiyetakiwa katika mchezo, wakati wa mchezo dhidi ya Coastal Union, misimu miwili iliyopita. Walipoteza ushindi katika mchezo mgumu, kisa ilikuwa kumchezesha Nadir Haroub aliyekuwa na adhabu. Ni tofauti na suala hili la Okwi, ila wakati mwingine ni lazima tahadhari ichukuliwe mapema.
 • TFF, kusema kuwa watalitazama vizuri suala hili kwa ndani ya nchi kutokana na matatizo ambayo yanaweza kuja kutokea katika soka la Tanzania, endapo Okwi atacheza michezo yote ya timu yake ya Yanga na kuisaidia kushinda. Na baadae ikagundulika kuwa mchezaji huyo alikiuka mambo mengi na kuingia mitini bila taarifa, Yanga itakuwa katika nafasi gani?. Je, sheria ikishikilia mkondo wake itamaanisha nini?. Je, itakuwaje kuhusu matokeo yake?. Kiushabiki, Okwi ataanza kuitumikia Yanga haraka sana, ila kwa manufaa ya soka la Tanzania, ni lazima jambo hili lichunguzwe kwa kina kabla mchezaji huyo hajaanza kuichezea Yanga katika ligi ya ndani.
 • Wammchezeshe tu, katika michuano ya kimataifa kama wanahitaji kufanya ujinga wa kufikiri kimantiki. Ni kweli, tupo tayari kuvuruga mpira wa Tanzania kwa makosa ya mchezaji wa ng'ambo?. Huwezi kuona athari zake kwa sasa, sababu wote tumekuwa tukisukumwa mtazamo wa ' tambo na majisifu', wale mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiwapiga vijembe mashabiki wa Simba, baada ya kupewa ruhusa ya angalizo kumtumia Okwi. WAmejitahidi kuweka hisia zao zote kwa Mganda huyo huku nao wakiwasukuma viongozi wao, ' kuwa kama noma na iwe noma, Okwi aichezee timu yao'. Na, acheze sasa. Ila wasije kuwatumpia lawama viongozi wao siku wakiambiwa kuwa kutokana na matumizi ya mchezaji huyo katika michezo ya ligi kuu, nafasi ya Yanga ni hii…..

 • UNAYAKUMBUKA, YA JAMAL MALINZI NA VICTOR COSTA?
 • Yanga walimsaini, Victor Costa kutoka Simba bila ruhusa ya klabu yake. Baadaye Jamal Malinzi, rai wa sasa wa TFF, akiwa kiongozi wa juu wa klabu yake ya Yanga. Aliingia uwanjani na Victor Costa na mchezaji huyo alikuwa amevaa jezi namba tano, yenye jina la DEWJI. Nini kilikuja kutokea?. Costa aliishia kuoneshwa kwa mashabiki wa mashabiki wa timu hiyo waliokuwa katika michuano ya MAPINDUZI CUP, huko Zanzibar na aliporudi Dar es Salaam, akaonekana katika mazoezi ya Simba akiwa na jezi namba tano, yenye jina la MALINZI. Ilimaanisha nini?
 • Tambo za viongozi wa juu wa klabu za Simba na Yanga, Kassim Dewji kwa upande wa Simna, na Malinzi kwa upande wa Yanga. Ulikuwa ni wakati ambao hata viongozi wa juu wa mpira wa Tanzania walikuwa wakifanya kazi yao kwa mapenzi ya klabu zao. Je, tunapaswa kuishi katika dunia yenye fikra kama hizo hadi wakati huu?. Suala la Okwi, ni tofauti na lile la Costa, na lipo mbali na lile na Nadir. ILA, Malinzi anaweza kutumia historia ya adhabu aliyoipata katika utawala wake Yanga hasa baada ya kuwaadaa mashabiki wa timu yake kwa kuwadanganya kuhusu usajili wa Costa, pia anaweza kuchukulia adhabu ambayo TFF, waliisimamia wakati Yanga walipomtumia, Nadir walikatwa pointi na kumaliza katika nafasi ya tatu.
 • Msimamo wangu kuhusu suala hili upo palepale, kuwa bado hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuhusu suala la uhamisho wa Okwi. Hila muda bado umebaki kidogo tu ili jibu hili kufumbuliwa kwa uhakika. Wenzentu hawazungumzi, Etoile wapo kimya, Fifa wametoa ruhusa ya angalizo, caf wamemruhusu, TFF, wanatafakari. Duuh! Huyu, Okwi ni zaidi ya wachezaji wote Tanzania. ILA, asifikie hatua ya kuharibu soka la Tanzania katika siku za mbele. CAF, ni wajanja waliitega TP Mezembe na kuiondoa kimizengwe, miaka mitatu iliyopita wapotoa ruhusa kwa mchezaji hasiye halali. Wakairudisha mashindanoni, W. Casablanca, ambayo iliitoa Simba na kufika hadi fainali na kufungwa na Esperance.
 • Subiri baada ya gemu ya  Yanga na wale Waarabu. Nguvu iendane na fikra pia, mapenzi kila mtu anayo. Kwa suala la Okwi, Simba ipo karibu pia. Hila kwa sasa haliwahusu. Naisubiri jezi namba 25 ya Yanga kwa hamu kubwa. Okwi, ni mtihani au mtego kwa utawala wa Malinzi?. Tusubiri tuone kwa kuwa uchunguzi wa kitaalamu unaendelea, hivi ile miezi sita ya fifa inamalizika lini?. Okwi, mwenyewe kafunga mdomo, je anatambua kosa lake?. Au, hapendi kuzungumzia mambo yaliyopita?. Unakumbuka ila makala, ' Yanga wamemnunua wapi Emmanuel Okwi?', sasa nauliza, MMEIFIKIRIA RUHUSA YA ANGALIZO KUTOKA FIFA KUHUSU OKWI? Ata, macho yanapenda kutazama vitu vizuri, ila vitu vibaya pia huonekana.
 • 0714 08 43 08
 • Friday, February 14, 2014

  NIONAVYO MIMI:SAKATA LA OKWI,MCHEZO UMEKWISHA


  Na Oscar Oscar Jr .
  0789-784858

  Sakata la usajili wa mshambuliaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi hatimaye limefikia ukomo tarehe 13.02.2014 baada ya Shirikisho la soka Duniani FIFA kuthibitisha kuwa mchezaji huyo yuko huru kukipiga na mabingwa watetezi wa Tanzania bara klabu ya Dar es salaam Young Africans.

  Rais wa Etoile Du Sahel,Ridha Charfeddie klabu ambayo mshambuliaji Emmanuel Okwi alikuwa akiitumikia baada ya kuondoka Simba sc kwa kitita kinachosemwa kufikia dola za kimarekani 300,000 ameibuka baada ya FIFA kuthibitisha kuwa Okwi ruksa kukipiga na wababe hao wa Jangwani na kudai kuwa,mchezaji huyo bado ni mali yao.

  Ukichunguza vizuri utagundua kuwa,Rais huyo wa Etoile Du Sahel klabu yenye makazi yake nchini Tunisia,ameshastukia kuwa Okwi sio wao tena na deni wanalodaiwa na klabu ya Simba,kwao ni kama hasara.Kulipa dola 300,000 wakati mchezaji yuko zake mitaa ya Twiga na Jangwani,hiki ndicho kinachomfanya aweweseke!!

  Lakini sakata la Okwi linatakiwa kuwa somo sana kwa viongozi wa vilabu Tanzania hasa Simba na Yanga.Hakukuwa na sababu kwa viongozi wa simba sc kujihusisha kwa aina yoyote ile na Usajili wa Okwi kwenda Yanga,wao nadhani wangejikita zaidi kuomba msaada wa kisheria toka TFF na FIFA ili kuhakikisha kwamba wanalipwa fedha zao za mauzo ya Okwi na klabu ya Etoile Du Sahel.

  Mashabiki na wapenzi wa timu hizi za Kariakoo kuna kitu nawalaumu sana.Hivi kwa nini wanapenda kujua pesa za mauzo ya mchezaji zilikokwenda bila kujua pesa za kumleta mchezaji huyo klabuni zilitoka wapi? Nadhani ukiwa mwanachama unatakiwa kujua pesa za kuwaleta hao "MAPRO" zinatoka wapi,ukijua hilo,haitokusumbua wanapouzwa kujua pesa zinakokwenda.

  Ni kweli mpira ni biashara na sina tatizo na klabu ya Simba kumuuza Okwi kwa kitita hicho cha dola laki tatu lakini,unawezaje kumuuza mchezaji wa aina ya Okwi kwa mkopo? Okwi alikuwa miongoni mwa wachezaji muhimu sana kwenye klabu ya Simba.Sikushangaa kuuzwa,nilishangaa kuuzwa bila timu kupokea hata senti moja!

  Hivi ungewaelewa kweli klabu ya Tottenham Hotspurs endapo wangemuuza Gareth Bale kwenda Real Madrid kwa mkopo? ungewaelewa bodi ya Arsenal endapo wangemuuza Roben Van Persie kwenda Manchester united bila kupata chochote? kesho ukiamka na kusikia Eden Hazard kajiunga na klabu ya PSG bila Chelsea kupewa chochote,utawaelewa kweli?

  Kuna baadhi ya watu wanaamini usajili wa Okwi bado unautata,binafsi siamini hilo.Utata wa Okwi ulimalizika pale FIFA ilipothibitisha uhalali wa Okwi kukipiga na mabingwa hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani,full stop.FIFA wanatambua mgogoro kati ya Simba na Etoile Du Sahel unaohusu malipo,FIFA wanatambua mgororo wa Okwi na Etoile Du Sahel unaohusu madai ya Okwi ya fedha zake na yale ya Klabu kuhusu utovu wa nidhamu wa Okwi na kukiuka mkataba wake,FIFA inatambua kujiunga kwa Okwi Sc Villa,FIFA inatambua kama Okwi kauzwa Yanga,FIFA inajua kama TFF wamemzuia Okwi kucheza VPL na pia wanatambua kama CAF imemzuia kucheza michuano ya klabu bingwa Afrika.Leo hii wameridhia Okwi kucheza Yanga,utata unatoka wapi?

  Kama klabu ya Yanga itamtumia Okwi kwenye michezo yake ya ndani na ile ya Afrika halafu baadae ikagundulika kuwa Yanga wamemtumia mchezaji ambaye hakustahili na kupelekea kunyang'anywa pointi,hapo ndipo nitakapo amini kuwa shirikisho la soka Duniani,yaani FIFA linaongozwa na wahuni na sio watu wenye taaluma ya mchezo wa soka.i'm sorry!

  TWIGA STARS YALALA 2-1 ZAMBIA

  Twiga Stars imepoteza mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Zambia (Shepolopolo) kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.

  Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika katika mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga timu hizo zilikuwa suluhu.

  Wenyeji ndiyo walianza kupata bao lililofungwa na Hellen Mubanga dakika ya 75. Mfungaji huyo aliyeingia kipindi cha pili nchini alimalizia wavuni mpira uliotemwa na kipa Fatuma Omari.

  Dakika nne baadaye Zambia ambao walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu na washabiki wao baada ya kufunga la kwanza, walipata bao la pili ambalo nahodha wa Twiga Stars, Sophia Mwasikili alijifunga mwenyewe.

  Mwasikili alikuwa akijaribu kutoa nje mpira uliopigwa na nahodha wa Shepolopolo, Mupopo Kabange ambapo ulipishana na kipa Fatuma Omari kabla ya kujaa wavuni.

  Bao la Twiga Stars lilifungwa na Donisia Daniel dakika ya 90. Beki huyo wa kushoto ambaye pia ni mchezaji wa Tanzanite alipanda mbele kuongeza mashambulizi ambapo akiwa nje ya eneo la hatari alipiga shuti lililomshinda kipa Hazel Nali.

  Akizungumza baada ya mechi, Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage alisema amebaini upungufu katika kikosi chake ambao ataufanyia kazi kabla ya mechi ya marudiano ili timu yake iweze kusonga mbele.

  “Kwa matokeo haya bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano nyumbani na kusonga mbele,” alisema Kaijage.

  Twiga Stars iliwakilishwa na Fatuma Omari, Fatuma Bashiru, Donisia Daniel, Fatuma Issa, Evelyn Sekikubo, Sophia Mwasikili, Vumilia Maarifa, Mwapewa Mtumwa/Amina Ali, Asha Rashid, Etoe Mlenzi/Zena Khamis na Shelida Boniface.

  Timu hiyo inarejea nyumbani kesho kwa ndege ya Fastjet ambapo itatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Ofisa Habari na Mawasiliano
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
  Lusaka, Zambia

  MBEYA CITY VS SIMBA: JE MNYAMA KUVUNJA MWIKO WA MBEYA CITY SOKOINE????


  Na Baraka Mbolembole 

  Bao lililofungwa na kiungo- mshambuliaji, Richard Peter dakika kumi kabla ya kumalizika kwa mchezo. Lilitosha kuwapa sare ya kufungana mabao 2-2 timu ya Mbeya City. City walipata sare hiyo dhidi ya Simba katika uwanja wa Taifa, Oktoba mwaka uliopita katika mchezo wa duru la kwanza. Timu hizo zitapambana tena wikendi hii katika mchezo wa marejeano jijini, Mbeya.

  City wametoka kupata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita, wakati Simba imetoka kulala kwa timu ya Mgambo JKT. Simba wanaonekana kuwa na safu kali ya mashambulizi, kwani baada ya Yanga SC iliyofunga mabao 34, Simba ndiyo wanafuatia wakiwa wamefunga mabao 32 katika michezo 17. City wanaonekana kutokuwa na makali sana katika kufunga mabao ila safu yao ya ulinzi ikiwa moja safu ngumu katika ligi. Wamefunga mabao 22, na wameruhusu mabao 13. Wanaweza kuisumbua Simba na kuiangamiza kwa kuwa timu hiyo ya Dar es Salaam, imekuwa si imara sana katika ngome.

     SIMBA INAWEZA KUIFUNGA CITY?

  Ni vigumu, ila inaweza kuwa rahisi kama watajipanga vizuri. Hakuna timu ambayo imeweza kuifunga City katika uwanja wake wa nyumbani msimu huu. Lakini, timu hiyo imekuwa ikiruhusu mabao uwanjani hapo na kuna timu zilikaribia kuondoka na ushindi ila zikashindwa kuhimiri presha ya timu hiyo na kujikuta zikiondoka na sare au vipigo. Ikiwa na kumbumbuku mbaya katika uwanja wa Sokoine, Simba inaweza kujipanga na kwenda kushinda kama walivyofanya dhidi ya Tanzania Prisons, miaka mitano iliyopita wakati bao la David Naftal lilipowapatia ushindi wa kwanza dhidi ya timu hiyo ya Magereza katika kipindi cha miaka 11.

  Mwenyekiti wa Simba, Mh. Ismail Aden Rage tayari ametoa tambo kuwa watakwenda Mbeya kuchukua pointi zote tatu. Simba imezidiwa pointi tatu na timu hiyo ya kocha Juma Mwambusi, na tayari wamejibiwa kuwa hawatishi. Mtibwa ilipata bao la kuongoza katika mchezo uliopita dhidi ya City ila wakajikuta wakichapwa mabao 2-1. City itakuwa ikimkaribisha kikosini kiungo wake mahiri, Steven Mazanda, pia watakuwa na mshambuliaji wao mwenye nguvu Paul Nongwa, Morgan Yeya ' ticha', Hassan Mwasipili. Simba inaweza kushinda Mbeya kama alivyodai Rage, ila timu hiyo ya Mbeya ni kali sana na inayohitaji uvumilivu wa mchezo kutoka kwa wachezaji wao.

    CITY NI TIMU KALI

  Waliweza kuthibitisha hilo walipotoka nyuma ya mabao 2-0 hadi kutengeneza sare ya 2-2 katika mchezo wa awali kati ya timu hizo. Awali, waliweza kusawazisha dhidi ya Yanga na walitia fora waliposawazisha mara tatu dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Chamanzi, na kupata sare ya mabao 3-3. Hiyo inaonesha dhahiri kuwa timu hiyo ni imara na isiyokata tamaa. Simba walinyanyaswa katika eneo la kiungo wakati wa mchezo wa kwanza, na tatizo hilo lilionekana katika michezo yao miwili ya mwisho dhidi ya ligi kuu, dhidi ya Mtibwa na Mgambo. Waliteswa sana na Shaaban Kisiga na Shaaban Nditti wakati wa mchezo wa sare ya bao 1-1 na Mtibwa na wakafunikwa kwa muda mwingi na kiungo Mohammed Samatta wa Mgambo, sasa watakuwa na mtihani wa kujipanga dhidi ya Mazanda.

  City si tu kuwa wanajivunia kuwa na timu isiyokata tamaa uwanjani, pia imekuwa chini ya mipango mizuri ya kocha Mwambusi ambaye ameweza kuifanya timu yake kuwa na nidhamu ya mchezo ndani ya uwanja. Tofauti na wachezaji wa Simba, ambao mara zote huishia kucheza kwa viwango vya chini, City wachezaji wao hawachezi kwa kufuata maelekezo ya watu kutoka nje ya bechi la ufundi. Wamepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Yanga, wiki mbili zilizopita, ila waliweza kucheza kwa zaidi ya dakika 40 soka la nguvu ambalo lilifuta pengo la mchezaji wao mmoja aliyeondoshwa uwanjani (Mazanda).

  Kama wachezaji wa Simba wataendelea kucheza soka lao kwa kufuata maelekezo ya nje ya benchi la ufundi, watachapwa. Ila kama watacheza kwa nguvu na uvumilivu kwa muda mwingi wa mchezo wanaweza kuwa timu ya kwanza kuvuka ' mwiko na kuifunga' City katika uwanja wake. Sijui kitu gani kilichompa jeuri Rage na kusema kuwa timu itashinda. Alikuwa mbali na timu kwa muda kiasi na mara zote amekuwa akisema kuwa ' Yeye si kocha' anapoulizwa kuhusu matokeo mabaya. Sasa amekuwa kocha? Amechukua nafasi ya Logarusic na kuwaambia wapenzi wa timu yake kuwa watashinda.

   SIMBA IMEIMARIKA...

  Walionesha udhaifu mkubwa katika mchezo wa mwezi Oktoba, na kuwaacha City watawale katika mchezo wao wa kwanza ndani ya uwanja wa kisasa, Taifa. Golini kulikuwa dhaifu sana, kipa Abel Dhaira alifungwa mabao marahisi sana, huku lile la mshambuliaji, Nongwa likimfanya watu waanze kuhoji uwezo wake hasa na ubora wake wa kuichezea timu hiyo. Sasa, Dhaira hayupo, na kipa ambaye alionekana kutibu tatizo hilo Ivo Mapunda amekuwa sehemu ya timu hiyo kufungwa na Mgambo alipoutema mpira uliozaa bao pekee, na alifungwa bao la kipuuzi na Mtibwa. Kama ataendelea kupoteza kujiamini kwake bila shaka itakuwa hatari kwa Simba, na ninafikiri ni wakati wa Yaw Berko kucheza mchezo huu kwa kuwa Ivo, yupo katika wasiwasi kwa sasa baada ya timu kupoteza pointi sababu ya makosa yake.

  Amis Tambwe alifunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya City, ila ameshindwa kufunga katika michezo dhidi ya Mtibwa na Mgambo huku wengi wakiamini kuwa anakosa msaidizi mzuri katika safu ya mbele ya mashamublizi. Alitengeneza ushirikiano mzuri na Betram Mwombeki na bila shaka mahusiano yao yana faida kubwa kwa timu hiyo. Harouna Chanongo amepoteza kila kitu. Nguvu, hamu ya kuisaidia timu, na amekuwa mchezaji asiye na mchango mkubwa sana katika michezo ya karibuni. Labda pia huu ni wakati wa kocha Logarusic kumuamini kijana William Lucian katika safu ya ulinzi wa kulia, na kumpatia nafasi ya kutosha Mwombeki. Nani mshindi wa mchezo huu?

  KIUFUNDI: FOMU MBOVU YA ARSENAL DHIDI YA TIMU KUBWA INAIGHARIMU NDOTO YAO YA KUMALIZA UKAME WA MIAKA 9 WA UBINGWA

  Msimu uliopita Arsenal ilimaliza msimu ikiwa kwenye kiwango cha juu, ikishinda me chi mfululizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki Champions League. Jambo moja ambalo limekuwa likiangusha Arsenal kwa misimu kadhaa iliyopita - ni kupata point chache kutoka vilabu vyenza vya Top 4. Arsenal ilichukua jumla ya point 2 tu kati ya 18, walifungwa me chi 4, wakitoa sare mara mbili na hawakushinda mchezo hata moja dhidi ya Man United, Chelsea, na Man City. Je hii inajirudia pia msimu huh na itaigharimu Arsenal na ndoto yake ya kutwaa ubingwa?

  Kama tunavyoona hapo juu fomu ya Arsenal dhidi ya vilabu vinavyoshika nafasi za juu msimu huu ni sawa sawa tu ilivyokuwa msimu uliopita. 
  Liverpool, ambao wamefungwa mechi zao 3 za ugenini dhidi ya timu za juu, ina pointi 3 tu kutoka kwenye mechi dhidi ya timu za Top 4, pointi hizo imezipata kutka kwa Arsenal. Jambo la kusikitisha zaidi pamoja na msimu huu kujirekebisha kidogo kwenye ulinzi lakini Arsenal imeruhusu mabao 11 kwenye mechi mbili dhidi ya Manchester City na Liverpool. Hili ni jambo la kutia wasiwasi.

  Kuna wasiwasi au mtazamo kwamba timu haijiandai vizuri na michezo dhidi ya timu kubwa, wanaruhusu mabao mengi. Jambo lingine la kutia shaka safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao manne tu, namba ndogo zaidi miongoni mwa mechi za timu za top 4. Chelsea wana rekodi nzuri, wameruhusu mabao 3 tu na ndio timu pekee iliyoenda Etihad na kushinda - na kutoka na clean sheet pia. 
  Manchester City wana kikosi kizuri mno na itakuwa vigumu kufungwa watakapoenda Emirates na Anfield. Chelsea wana mchezo mmoja wa ugenini dhidi ya Liverpool na mmoja wa home dhidi ya Arsenal. Fomu ya Chelsea dhidi ya timu za juu ni nzuri sana na chini ya Jose Mourinho  wameweza kujua namna ya kupata matokeo katika mechi kubwa kwa mbinu zozote zile. 
  Wenger inabidi ajipange vizuri katika mechi mbili zijazo dhidi ya Manchester City na Chelsea, endapo watapoteza mechi hizo ni wazi ndoto yao ya kubeba ubingwa msimu huu itabaki kuwa ndoto. 
  Arsenal wana mkusanyiko wa michezo migumu sana katika siku za hivi karibu. Jana walishindwa kuifunga Man United walio kwenye hali mbaya kabisa, wakitoka hapo wanaenda kukutana Liverpool kwenye kombe la FA, then wanaikaribisha Bayern Munich Emirates wiki ijayo, then watakutana na mahasimu wao Spurs, na Chelsea kisha Everton, huku wakisubiri kuikaribisha City Emirates. 

  Mpaka kufikia mwishoni mwa 3 tunaweza kujua hatma ya Arsenal msimu huu - watamaliza ukame wa miaka 9 bila kombe au wataingia mwaka wa 10 bila kuvaa medali.

  SAKATA LA USAJILI WA OKWI BADO BICHI -TFF WASIHARAKISHE KUMRUHUSU OKWI KUICHEZEA YANGA,ETOILE WADAI BADO OKWI NI MCHEZAJI WAO..

  Sakata la mshambuliaji Emmanuel Okwi limeshika hatamu tena baada ya FIFA kutoa ruhusa kwa mchezaji huyo kuichezea klabu ya Yanga.
  Taarifa hii imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka hapa nchini, kuna walioipokea kwa vifijo na nderemo na kuna wengine taarifa hii ilikuwa ni kama vile ya msiba.
  Pasipo kutawaliwa na hisia za upenzi miongoni mwetu sakata hili si jepesi kama tunavyolifikiria,
  Raisi wa Etoile Du Sahel, Ridha Charfeddine amefanya mahojiano maalum na mtandao huu nkuuambia kwamba wao bado wanamtambua Okwi  kama mchezaji wao, Okwi alipoondoka kujiunga na timu yake ya Taifa ya Uganda mnamo mwezi mei mwaka 2013 hakurejea tena klabuni.
  ‘‘Mnamo May 19 mwaka 2013 shirikisho la soka nchini Uganda kupitia mtendaji wao mkuu ndugu Edgar Watson lilituma barua kwa shirikisho la soka nchini Tunisia likimuombea ruhusa Okwi ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa iliyokuwa inajiandaa na michezo miwili dhidi ya (Angola na Liberia) ya kufuzu kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil, michezo hiyo ilikuwa ichezwe mnamo June 8 na 15 jijini Kampala kwenye uwanja wa  Mandela, baada ya michezo hiyo Okwi hakurejea tena klabuni kwetu’’.
  Mr Charfeddine  aliendelea kusema ya kwamba baada ya kumsubiria Okwi kwa karibia wiki nzima bila kutokea huku akipigiwa simu na meneja wa timu bila mafanikio ilibidi wamuandikie barua ya kumueleza namna utovu wake wa nidhamu utakavyomgharimu.
  ‘’Ilibidi tumuandikie notisi ya kumfahamisha ya kwamba akiwa kama mchezaji wa kulipwa kutokana na kutofika klabuni tangu mnamo tarehe 23/6/2013 alikuwa anavunja vipengele vya mkataba  baina yake na  klabu, mkataba wa Okwi na  Etoile du Sahel  unamalizika mnamo june 30 mwaka 2016 kwahiyo kwa kitendo chake cha kutorejea klabuni ndani muda muafaka alikuwa anavunja vipengele vya 2,8 na 16 vilivyomo kwenye mkataba baina yake na klabu.
  "Baada ya hapo tulimpa muda hadi July 10 mwaka 2013 awe amerejea klabuni la sivyo tulikuwa tunalipeleka shauri lake kwenye vyombo husika vya kisheria’’.
  Wao kama Etoile wana mpango gani na Okwi?
  Emmanuel Okwi bado ni mchezaji wetu kwasababu tuna mkataba nae mpaka tarehe 30/06/2016 na kwasasa tumepeleka kesi yake FIFA kwa kitendo chake cha kutorejea klabuni, tunaamini FIFA watalifanyia uchunguzi suala hili na haki itapatikana.
  Baada ya kufanya hayo mahojiano na Raisi wa Etoile du Sahel tumepata mawazo yafuatayo ya kuwashauri TFF na YANGA kwa ajili ya manufaa ya mchezo wa soka hasa YANGA na mchezaji husika.
  1.
  TFF WASIWE NA HARAKA KUTOA MAAMUZI YA KUMRUHUSU OKWI KUICHEZEA YANGA.
  Naamini maamuzi ya barua ya FIFA ni kitanzi kwa TFF na YANGA, kwahiyo wanahitaji kuwa makini sana kuisoma na kuielewa kwa kina kabla ya kutoa maamuzi. 
  Naamini FIFA hawana tatizo na Okwi kuicheza YANGA kama atakuwa hana matatizo na klabu yake ya Etoile du Sahel.
   
  Mapungufu makubwa ya utawala uliopita wa TFF yalikuwa ni kufanya maamuzi ya msingi kishabiki pasipo kuwapa nafasi wataalamu wenye uweledi wa jambo husika kulifanyia kazi, sasa katika hili la Okwi itakuwa jambo la busara kama wataalamu wa mambo ya kisheria watapewa nafasi ya kulifanyia kazi kwa kina ikiwa ni pamoja na kuwapatia hiyo nakala ya barua ya FIFA kuisoma neno kwa neno ili kujihakikishia kwa kilichomo kwenye barua hiyo, kwasababu kwenye FIFA  Regulations on status and transfer of players .
   
  ARTICLE 5 kwenye kipengele kidogo cha pili kinazungumzia mchezaji lazima asajiliwa na klabu moja tu (A player may only be registered with one club at a time.)
  Sasa hapa imekaaje kama Etoile wanadai wana mkataba na Okwi na wakati huo huo Yanga nao wameshamsajili mchezaji huyo huyo?
  Article 18 IV. MAINTENANCE OF CONTRACTUAL STABILITY BETWEEN PROFESSIONALS AND CLUBS
   
  3. A club intending to conclude a contract with a professional must inform the
  Player’s current club in writing before entering into negotiations with him. A
  Professional shall only be free to conclude a contract with another club if his
  Contract with his present club has expired or is due to expire within six months.
  Any breach of this provision shall be subject to appropriate sanctions.
  Kutokana na hicho kipengele hapo juu, najiuliza baada ya Etoile du Sahel kudai wana mkataba na Okwi, SC Villa walimuuzaje kwa  mkataba wa miaka miwili Yanga? Ni klabu ipi kati ya VILLA na SAHEL iliyokuwa na haki ya kuwasiliana na YANGA kabla ya usajili wa Okwi?
  Naamini kuna vipengele vingine vingi tu ambavyo vinahitaji kuangaliwa kwa jicho la kisheria na kujihakikishia kwanza, iwapo maamuzi ya kesi zilizopo FIFA yatakapotolewa basi yasije yakaiathiri YANGA na Mchezaji husika wakati tayari atakuwa ameruhusiwa kucheza.
  Nawasilisha

  YANGA YAWASILI COMORO


  TWIGA STARS YATUA LUSAKA, YAAHIDI MAPAMBANO

  Kikosi cha wachezaji 19 wa Twiga Stars kimetua Lusaka, Zambia leo
  (Februari 13 mwaka huu) huku Kocha Mkuu Rogasian akiahidi ushindani kwenye
  mechi dhidi ya wenyeji itakayochezwa Uwanja wa Nkoloma.

  Kocha Kaijage aliwaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa
  Kimataifa wa Kenneth Kaunda mara baada ya kikosi chake kutua kwa ndege ya
  Fastjet saa 3.30 asubuhi kwa saa za Zambia kuwa wamekuja kushindana, na si
  kushiriki.

  Twiga Stars ambayo mara ya mwisho ilikutana na Zambia kwenye michuano ya
  COSAFA miaka miwili iliyopita na kuibuka na ushindi imefikia hoteli ya
  Golden Peacock, na katika uwanja wa ndege ilipokewa na viongozi wa Chama
  cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ) na Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini
  Zambia, Jeswald Majuva.

  Timu hiyo leo saa 9 alasiri kwa saa za Zambia ambapo Tanzania ni saa 10
  jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nkoloma ambao ndiyo utakaotumika
  kwa mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC)
  itakayochezwa kesho.

  Wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho ni Amina Ali, Anastazia Katunzi,
  Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine
  Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari,
  Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwapewa Mtumwa, Sherida Boniface,
  Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.

  Thursday, February 13, 2014

  PICHA MBALI MBALI ZA AZAM FC WAKIWA TAYARI NCHINI MSUMBIJI WAKIFANYA MAANDALIZI.


    Wachezaji wakiwa tayari mazoezini....
     Himid Mao,Aggrey Moris,Brian Umony,Jabir,Mcha na Bocco.   Katibu mkuu Nassor Idrissa 'Father' na Meneja wa timu Jemedari Said  Picha zote kwa hisani ya Azam FC.

  MAHOJIANO NA KATIBU MKUU WA TFF KUHUSU SUALA LA OKWI - SOMA NA SIKILIZA ALICHOSEMA

  Hivi punde mtandao huu umepata nafasi ya kufanya mazungumzo na Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Celestine Mwesiga ili kujua undani wa suala la FIFA kumuidhinisha mchezaji Emmanuel Okwi kuichezea klabu ya Dar Young Africans.

  Katika mazungumzo hayo Mwesiga amesema kwamba ni kweli FIFA wamemruhusu Okwi kuendelea kucheza soka wakati wenyewe wakishughulikia madai ya vilabu vya Simba SC na Etoile Du Sahel.

  "Kwanza ningependa kusema kwamba kazi ya FIFA kwenye hili suala ilikuwa sio kumruhusu mchezaji kuichezea au kutoichezea Yanga, hilo suala lipo chini ya shirikisho la soka nchini TFF.

  "Kilichotokea ni kwamba kulikuwa na malalamiko ya klabu ya Simba SC, juu ya uhalali wa uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi kutoka SC Villa kwenda Yanga na pili juu ya deni lao wanaloidai klabu ya Etoile Du Sahel. FIFA wameridhika na suala la uhamisho wa Okwi kwenda Yanga kwa maana ulifuata vigezo vyote na walipata ITC.
  "Pia kuhusu suala la deni la Simba wanayoidai Etoile, FIFA imeeleza kwenye email yake kwamba suala lipo pale pale lakini halina uhusiano na suala la Okwi kusajiliwa Yanga. Sisi kama TFF tutaendelea kulifuatilia kiundani kuhakikisha Simba wanapata haki yao."

  Alipoulizwa kama suala la uhamisho wa Okwi kwenda Yanga halina tatizo lolote, hivyo Okwi ataruhusiwa kuichezea Yanga, Mwesiga alisema: "Kilichobaki sasa ni masuala ya ndani ya shirikisho. Tutaangalia kama mchezaji husika amekidhi vigezo vya kuweza kushiriki kwenye michuano mbalimbali hapa nchini, ikiwa atakuwa amekidhi basi tutakuwa hatuna kipingamizi chochote."

  HATIMAYE MUNGU ASIKILIZA MAOMBI YA OKWI, FIFA YAMPA RUKSA KUCHEZA.  Taarifa zilizopatikana hivi punde zinasema FIFA imebaliki taratibu za uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka SC Villa kujiunga na Yanga.


  Taarifa kutoka ndani ya shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF zinasema FIFA imemruhusu mchezaji huyo kuendelea kucheza, nakuhusu suala la deni la Simba shirikisho hilo limesema bado linalifanyia kazi.

  MSAFARA WA AZAM FC WAFIKA SALAMA NCHINI MSUMBIJI


  UMRI WA MCAMEROON WALETA GUMZO BARANI ULAYA: ADAI ANA MIAKA 17 - SHIDA ZA KIMAISHA UTOTONI ZIMEMKOMAZA


  Moja ya story kubwa sana kwenye ulimwengu wa soka wiki hii inamhusu mchezaji mpya wa klabu ya Lazio, Joseph Minala, ambaye watu wengi wamekuwa na mashaka na umri sahihi wa kiungo huyo wa Cameroon kwamba ana miaka 17 au 40 na zaidi.

  Kulikuwa na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, akionekana kukasirishwa na kejeli na matusi ya mashabiki Joseph Minala aliamua kujibu mapigo kwa ujumbe wenye maneno makali kupitia akaunti yake ya Twitter kabla ya kuifunga, pia akaifunga ya Facebook na kuiweka ya instagram private.

  Wakala wake Diego Tavano nae amezungumzia suala hili huku akimtetea mteja wake kwamba "shida za kimaisha" zimechangia muonekano wa kiutuzima wa mteja wake. Akiongea na Gazzetta dello Sport alisema: "Suala la Joseph Minala lipo wazi. Alikuwa amelelewa kwenye mazingira ya shida sana wakati wa udongo wake, hali iliyopelekea muonekano wake huu wa hivi sasa."

  Mmiliki wa klabu iliyomuuza kwenda Lazio, bwana Mauricio Perconti, nae alimtetea: "Siwezi kukataa kwamba anaonekana mtu zima sana, lakini vielelezo vyote vinaonyesha umri wake ni miaka 17."


  TAZAMA PICHA ZA MINALA KISHA TOA MAONI YAKO. UNADHANI ANA MIAKA 17 KWELI?
  BgR 1SJCEAEbzPz Joseph Minalas agent says his 17 year old client who looks 40 appears older because of a difficult childhood
  BgDmZIgIgAAbpp2 Joseph Minalas agent says his 17 year old client who looks 40 appears older because of a difficult childhood


  ROBINHO NA MWANAE- MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO!

  VIDEO: MESSI AIPELEKA BARCA KWENYE FAINALI YA EL CLASSICO - COPA DEL REY


  Real Sociedad 1-1 Barcelona (All Goals) 12... by ourmatch

  VIDEO: ARSENAL WASHINDWA KUIFUNGA MAN UNITED NA KURUDI KILELENI

  VIDEO: GERRARD AISOGEZA LIVERPOOL KWENYE MBIO ZA UBINGWA NA PENATI YA DAKIKA ZA MWISHO

  Wednesday, February 12, 2014

  BREAKING NEWS: MCHEZO WA MAN CITY VS SUNDERLAND WAGHAIRISHWA

  Mchezo wa Manchester City dhidi ya Sunderland uliokuwa uchezwe katika dimba la Etihad Stadium umeghairishwa kutoka na hali mbaya ya hewa. 

  Polisi wa jijini Manchester wamethibitisha habari hiyo saa moja kabla ya kuanza kwa mchezo huo huku kukiwa na upepo mkali ambao umeufanya mchezo huo kughairishwa na kutokana masuala ya usalama.

  Nahodha wa City Kompany aliandika kwenye Twitter: "Mchezo umeigharishwa. Hakikisha unarudi nyumbani salama, hali ya hewa sio nzuri."

  NANI ATAKUWA MCHEZAJI WA 100 KUPEWA KADI NYEKUNDU KWENYE UTAWALA WA WENGER NDANI YA ARSENAL ?

   Dennis Bergkamp akilimwa kadi nyekundu...mpaka anaondoka Arsenal alikusanya jumla ya kadi nyekundu 4.
    Adebayor akila chuma....toka kwa mwamuzi Howard Webb


   Chini ni orodha ya wachezaji wa Arsenal waliopata kadi nyekundu kwenye michezo dhidi ya Manchester Utd.


  Chini ni majina ya wachezaji wa Arsenal waliopewa kadi nyekundu kwenye kipindi cha Wenger ndani ya Arsenal.

  jumla ya kadi nyekundu 99 zimetolewa kwa wachezaji mbali mbali wa Arsenal katika kipindi chote ambacho Mfaransa Arsene Wenger amekuwa madarakani klabuni hapo.

  SWALI ?
  Ni mchezaji gani atapewa kadi nyekundu ya 100 ?

  SUAREZ NDIYE KINARA KWA KUFUMANIA NYAVU KWASASA BARANI ULAYA.


  ARSENAL VS MAN UNITED - MAJERUHI WAWILI WANAPOGOMBANIA TIBA YA USHINDI USIKU WA LEO EMIRATES. NANI KUPONA?


  Arsenal inaikaribisha Manchester United katika mchezo ambao ni muhimu kwa timu zote mbili.Mechi hii kawaida ni mechi inavuta hisia za mashabiki wengi duniani bila kujali vilabu vipo kwenye hali gani lakini ukifikiria matokeo ya wikiendi iliyopita, mchezo huu unazidi kuwa muhimu zaidi.
  Arsenal wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kipigo kitakatifu cha 5-1 kutoka kwa Liverpool jumamosi iliyopita. Majogoo wa jiji waliipiga Arsenal 4-0 ndani ya dakika 20 tu, kitu ambacho itabidi Gunners wakiwekee umakini ili wasikutane nacho katika mchezo wa leo.Huku mbio za ubingwa zikiwa zimepamba moto, Arsenal leo wanahitaji kushinda ili warudi kileleni vinginevyo wanaweza kujikuta wakizidi kuteremka chini kwenye msimamo. Matokeo ya wiki hii hayakuwa mazuri kabisa ukizingatia ratiba ngumu waliyonayo. Baada ya kucheza na United leo, Arsenal watakutana tena Liverpool lakini safari hii kwenye FA Cup, baada ya hapo watacheza na Bayern Munich katika Champions League. 
  Man Utd kwa upande mwingine wapo katika nafasi ya saba, wakitoka kutoka sare ya 2-2 na Fulham wanaoshika nafasi ya mwisho kwenye ligi. Ilikuwa ni mechi ambayo United ilishambulia sana, lakini wakakosa makali kwenye lango la wapinzani na mwishoni wakaonjeshwa utamu wa dawa yao wenyewe kwa kuruhusu bao la dakika ya mwisho kabisa ya mchezo na kupoteza pointi mbili muhimu. Huku matumaini yao ya kucheza Champions League yakianza kupotea, matokeo ya wikiendi yaliwafanya kuwa nyuma kwa pointi tisa kutoka kwa wanaoshika nafasi ya nne Liverpool, ambao pia wana wastani mkubwa wa mabao. United watakuwa na matumaini ya kurudisha utamaduni wao wakati Sir Alex Ferguson alipokuwa kocha, huku wakiomba timu nyingine zinazogombea nafasi ya nne za juu zipatae matokeo mabaya.
  Mechi ya Arsenal vs Man Utd siku zote imekuwa na upinzani mkubwa kuanzia miaka ya mwanzoni miaka ya 2000. Timu hizi mbili zimekuwa zikigombea ubingwa zenyewe kwa zenyewe na upinzani wao ulikuwa ukionekana wakati wa mechi zao. Enzi za ugomvi wa Viera na Roy Keanezimepita lakini upinzani bado upo. Huku usajili wa Van Persie kutoka Arsenal kwenda Old Trafford, imezidisha uhasama miongoni mwa mashabiki, hasa zaidi baada ya Van Persie kufunga mara kadhaa dhidi ya Arsenal tangu ajiunge na United, likiwemo bao la ushindi katika raundi ya kwanza. 

  Habari za Timu

  Arsenal

  Arsenal walikosa ubunifu na walikuwa wepesi kwenye kiungo siku ya jumamosi huku pengo la Flamini likionekana wazi. Kiungo huyo wa kifaransa anatumikia adhabu ya mechi 3 hivyo kwa mara nyingine atakosekana kwenye mchezo wa leo. Mchezaji mpya Kim Kallstrom ni majeruhi kama ilivyo kwa Walcott na Diaby. Vermaelen anakaribia kurejea lakini sio rahisi kucheza kwenye mchezo huu, Ramsey atakuwa nje mpaka mwezi ujao. Wenger anategemewa kufanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza huku Gibbs, Rosicky  NA Podolski wote wakitegemewa kuanza. 

  Man United

  Phil Jones anaweza kurudi kwenye kikosi cha kwanza cha United mara baada ya kurudi kutoka kwenye majeruhi. Fellaini, Nani na Ferdinand wote watakuwa nje kwa pamoja na Cleverley na Evans ambao walipata majeruhi hivi karibuni. 

  Vikosi vinavyoweza kuanza

  AFC vs MUFC 529x410 Arsenal vs Manchester United Preview | Team News, Key Players, Stats

  Takwimu mbalimbali za kuvutia

  • Gunners wameshinda mechi zao sita kati ya nane zilizopita za Barclays Premier League walizocheza nyumbani kwa mabao 2-0. 
  • Arsenal wameshinda mechi moja tu kati ya 10 za premier league dhidi ya Arsenal (W1 D2 L7).
  • Hii ni mara ya kwanza Arsenal na Manchester United zinakutana kwenye Premier League baada ya kushindwa kushinda kwenye zao za nyuma tangu April 2008.
  • Arsenal wameweza kuwa na clean sheets 10 katika mechi 11 zilizopita katika mashindano yote ndani ya dimba la Emirates. 
  • Robin van Persie amefunga katika mechi 5 zilizopita za premier league baina ya timu hizi mbili - mabao 3 kwa United - mabao mawili kwa Arsenal. 
  • Wayne Rooney amefunga mabao 10 ya premier league dhidi ya Arsenal. ndio mchezaji anayeongoza kufunga mabao mengi katika historia ya timu hizo mbili.