Search This Blog

Saturday, December 1, 2012

MRISHO NGASSA HATARI - AFUNGA GOLI 5 - BOKO APIGA MBILI - STARS WAKIICHAPA SOMALIA 7-0

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakisalimiana na wachezaji wa Somalia kabla ya mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda


Mrisho Ngassa akipongezwa na Athuman Idd baada ya kufunga goli la kwanza

Mrisho Ngasa wa Kilimanjaro Stars mwenye mpira akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Somalia wakati wa mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda

Beki wa Kilimanjaro Stars, Erasto Nyoni akiambaa na mpira wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge dhidi ya timu ya Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda

Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichopambana na timu ay Somalia katika mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda

Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Mrisho Ngassa akiambaa na mpira uliozaa goli la kwanza sekunde ya 48

Mrisho Ngassa akishangilia moja ya goli kati ya matano aliyofunga wakati wa mchezo na Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda


Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, John Bocco (kulia) akimtoka beki wa timu ya Somalia, Abdallah Mohamed

Boko akishangilia moja ya goli wakati wa mchezo na Somalia

Mashabiki wa Kilimanjaro Stars waishio nchini Uganda wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge dhidi ya timu ya Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda


BAADHI YA MALI ZA SHARO MILLIONEA ZILIZOPATIKANA - MILLION 6 ALIZOKUWA NAZO ZAENDA NA MAJI



LIVE MATCH CENTRE: TANZANIA VS SOMALIA

SHOMARI KAPOMBE ARUDI MAZOEZINI - POULSEN ASEMA WATAPAMBANA MPAKA MWISHO






Na Mwandishi wetu,
Kampala
Kocha wa Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen  amesema mechi ya kesho (Jumamosi) dhidi ya Somalia katika michuano ya Cecafa Challenge yanayoendelea Jijini Kampala, ni ya kufa na kupona na kikosi chake kiko tayari kukamilisha kazi.

Kocha huyo aliyasema hayo wakati Stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanajro Premium Lager, ikifanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wake na Somalia ili kukamilisha michezo ya Kundi B inayojumuisha Burundi, Tanzania, Somalia na Sudan.

“Mechi hii ni sawa na kuwa na risasi moja na risasi hii unatakiwa kuitumia vizuri..ndio mtihani tunaokabiliwa nao katika mechi hii maana lazima tushinde ili tusinonge mbele katika mashindano haya,” alisema n akikosi chake kitapambana hadi dakika ya mwisho.

Alisema ana imani na kikosi chake kwani wachezaji wote wana ari ya ushindi na kuendelea na mashindano kwani wameshaonesha kiwango kikubwa katika mechi mbili zilizopita huku Stars ikishinda mechi moja shidi ya Sudan na kufungwa nyingine na Burundi.

“Katika mechi hii hakuna mchezo na nimeshawaambia wachezaji kabisa maana hapa ukifungwa unaondoka,” alisema.

Kocha Poulsen pia alisema amefarajika kurejea kwa mchezaji Shomari kapombe ambaye alijeruhiwa katika mechi dhidi ya Burundi juzi.

Kwa mujibu wa daktari wa timu, Dk Mwanandi Mwankemwa, mchezaji Mwinyi Kazimoto hataweza kucheza kwa kuwa bado anaendelea kupata nafuu kwa hivyo wamemshauri kocha ampumzishe katika mechi hii na baadaye Stars ikifuzu kucheza mechi zijazo.

Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe alisema mechi hii ni muhimu kwa Stars na kuwaomba watanzania wanaoishi Kampala kujitokeza kwa wingi kuishangilia.

“Vijana hawa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau wote  hasa katika mechi hii ya kesho itakayoamua kama Tanzania itafuzuu kuendelea au la….sisi tukiwa wadhamini wa timu tunafuatilia kwa karibu na tunawaomba Tanzania waishangilie na kuipa moyo timu yao,” alisema.

Kikosi kinachotarajiwa kuanza katika mchezo huu dhidi ya Somalia ni Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, John Bocco, Shaban Nditi na Salum Abubakary.

Mchezaji Amir Maftah ameachwa maana ana kadi mbili za njano.

Friday, November 30, 2012

KENYA YAKATA TIKETI YA ROBO FAINALI CHALENJI IKIING'UTA ETHIOPIA 3-1

Mshambuliaji wa timu ya Kenya, Anthony Kimani akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Ethiopia, Abddulkrim Hassen yigemo wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela Jijini Kampala na Kenya kuibuka na ushindi wa 3-1 na kutinga robo fainali.

Shabiki wa timu ya Kenya akihamasisha kuishangilia timu yao wakati ilipocheza na timu ya Ethiopia katika mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela Jijini Kampala

CECAFA CUP MATCH LIVE CENTER: UGANDA vs SUDAN

CECAFA CUP MATCH LIVE CENTER: KENYA vs ETHIOPIA

PHOTOS: UHURU SULEIMAN MAZOEZINI NA AZAM FC KWA MARA YA KWANZA

Uhuru Suleiman akiwa ndani ya uzi wa Azam FC akifanya mazoezi chini ya kocha Stewart Hall katika uwanja wa Chamazi Complex



Uhuru akiwa na makocha wake Stewart Hall na Kally Ongara

MMILIKI WA GARI ALIYOPATA NAYO AJALI SHARO MILLIONEA AJITOKEZA NA KUZUNGUMZA - WEZI WALIOMUIBIA WAPATIKANA


MMILIKI wa gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na msanii maarufu nchini, Hussein Ramadhan ‘Sharo Milionea’ na kupata nalo ajali iliyosababisha kifo chake huko Muheza, Tanga, Mohammed Ismaili maarufu kwa jina la Mudi Suma, ameibuka na kueleza uhusiano wake na marehemu, huku akisema amekubali hasara.


Akizungumza kwa simu kutoka Muheza jana Suma alisema hana mpango wa kudai fidia au kupeleka malalamiko yoyote kwa ndugu wa marehemu kwa kuwa; “Kilichotokea ni kazi ya Mungu.” “Siwezi kudai hata kidogo hivyo ni vitu vya kupita tu. Marehemu alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu, gari ni kitu kidogo sana katika uhusiano tuliokuwa nao,” alisema Suma na kuongeza kwamba hata Marehemu Sharo Milionea naye alikuwa amemwachia mali zake kadhaa ikiwamo gari.



“Siyo gari tu alilokuwa ameniachia. Kuna mikataba yake ya kazi, Bajaji yake na funguo za chumbani kwake. Nasubiri kukabidhi vitu hivyo baada ya kukaa na ndugu zake. Vitu viko kwenye mikono salama,” alisema.



Kuhusu gari lake lililopata ajali, Suma alisema lilikuwa na bima ndogo, lakini anapanga kwenda TRA atakaporejea Dar es Salaam kufuatilia baadhi ya mambo.

“Kabla ya kuondoka bima ile kubwa ilikuwa imekwisha kwa hiyo nikaamua kuikatia bima ndogo. Nitakapofika kesho (leo) Dar es Salaam, nategemea kwenda ofisi za bima kuzungumza nao,” alisema Suma.


Alipoulizwa kama kuna mtu mwingine atakayeathirika kutokana na gari hilo kuharibika katika ajali mbali na yeye, alijibu: “Hakuna tofauti na mimi mwenyewe na familia yangu.”



Kabla ya ajali

Suma alieleza kuwa kabla ya kuanza safiri yake, Sharo Milionea alifika nyumbani kwake mchana na kumweleza kuwa afya yake haikuwa nzuri.


“Kabla ya kuondoka aliniambia kuwa hajielewi elewi na kifua kilikuwa kinambana. Nikamshauri asiondoke peke yake, atafute mtu wa kuondoka naye ambaye atamsaidia kuendesha gari njiani,” alisema Suma na kuongeza:



“Tulianza kuwapigia simu jamaa zetu wanne wa kusafiri naye lakini kila tuliyemwambia hakuwa tayari. Ilikuwa ni changamoto mpaka ilipofika saa 10:45 hivi jioni, akaamua kuondoka peke yake. Wakati anatoa gari getini kwangu, nikamwambia, basi jaribu kuwa mwangalifu sana, maana alikuwa kweli anasumbuliwa na kifua. Tukakubaliana kwamba atakaporudi aende hospitali kucheki afya yake.”



Kuhusu uhusiano wake na marehemu, Suma alisema: “Mimi ni mfanyabiashara na yeye alikuwa msanii, lakini ilitokea tukawa marafiki sana mpaka ikafikia wakati nikaona kuwa ni ndugu yangu. Nilimwamini nikamtambua kama sehemu ya familia.”



Alisema marehemu alikuwa akitumia gari hilo kila alipolihitaji na safari ya kwenda nalo Tanga kwa wazazi wake ilikuwa ni ya tatu.“Siyo mara ya kwanza kuitumia gari lile, nilikuwa nimemwamini sana. Safari ya kwanza alichukua na kusafiri nalo mwenyewe, halafu safari ya pili ikafuata na hii ilikuwa safari ya tatu,” alisema Suma.



Eneo la ajali wakimbia makazi

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Songa Kibaoni mahala ambako Sharo Milionea alipatia ajali, wamezikimbia nyumba zao baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu kutoa siku moja kwa waliopora mali za marehemu huyo kuzisalimisha mara moja.


Wakati huo huo

Jeshi la Polisi la Polisi Mkoani Tanga na kushirikiana na wasamalia wema wamewatia mbaroni vijana wanne wanadaiwa kumpora vitu mbalimbali marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali mbaya mwanzoni mwa wiki hii.

Habari za kuaminika toka Mkoani humo zinasema kuwa vijana hao wamekamatwa baada ya kazi nzuri iliyofanbywa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kushirikiana na wasamalia wema ambapo hadi sasa vijana hao wako chini ya ulinzi mkali huku wengine wakiwa bado wanatafutwa.

Habari zaidi zilisema kuwa vijana hao wamekamatwa jana usiku na waliokamatwa wamefahamika kwa jina ya Issa Makunera, Farid Hassani, Rashidi Ayubu, Rashid Makunera na imeelezwa watuhumiwa hao wamekutwa na mali mbalimbali za marehemu.

Chanzo chetu toka mkoani humo zilisema watuhumiwa hao pamoja na mali  hizo zimekamatwa katika eneo linanaloitwa Songa Kibaoni na vitu hivyo ni SPEA TAILI, REDIO YA GARI, BETERI YA GARI, SAA YA MKONONI SURUALI AINA YA JINS PAMOJA TISHETI, BEGI PAMOJA NA SIMU YA MKONONI.

Hata hivyo habari  ziliendelea kusema kuwa licha ya Begi hilo kupatikana ambalo lilidaiwa ndani yake kulikuwa na pesa nyinge hazikuweza kukutwa na inasemekana katika ya watuhumiwa wanaotafutwa ndio wamekimbia na fedha hizo.

Kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa hao wananchi mbalimbali wamelipongeza  Jeshi la Polisi pamoja na wananchi waeneo waliyokamatwa watuhumiwa kwani wao ndio waliotoa msaada mkubwa hadi kukamatwa kwao.



Source: http://www.udakuspecially.com - http://xdeejayz.blogspot.com

UZINDUZI WA TUSKER LITE ULIVYOFANA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Epraim Mafuru akizungmza mara baada ya uzinduzi wa bia mpya ya Tusker Lite wakati wa uzinduzi wake rasmi uliofanyika mbele ya maafisa masoko wa makampuni mbalimbali nchini wakati wa tafrija maalum ya ‘Markerts Night’ jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Mpigapicha wetu).

Add caption



Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon akinyanyua juu bia mpya ya Tusker Lite wakati wa uzinduzi wake rasmi uliofanyika mbele ya maafisa masoko wa makampuni mbalimbali nchini wakati wa tafrija maalum ya ‘Markerts Night’ jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Mpigapicha wetu).

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon (wapili kulia) , akiwa pamoja na wafanyakazi wa SBL wakigonganisha chupa zao za Tusker Lite kuashiria furaha ya kuzinduliwa kwa  bia hiyo mpy. Tusker Lite ilizinduliwa wakati wa tafrija maalum ya ‘Markerts Night’ jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Mpigapicha wetu).

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakifuatilia matukio mbalimbali wakati bia mpya ya Tusker Lite ilipozinduliwa sanjari na usiku maalum wa maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Mpigapicha wetu)



Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Epraim Mafuru (mwenye suti kushoto) akimkabidhi zawadi ya Tusker Lite, Meneja bidhaa wa Push Mobile, Gonzoga Rugambwa  baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa shindano maalum la uchezaji mziki lililofabnyika wakati wa uzinduzi wa bia ya Tusker Lite sanjari na usiku wa maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Mpigapicha wetu).

Thursday, November 29, 2012

NDOTO ZA UBINGWA WA 6 WA DUNIA - BRAZIL YAWARUDISHA SCOLARI NA CARLOS ALBERTO KILINGENI

Luiz Felipe Scolari ametangazwa kuwa kocha mpya wa wenyeji wa Kombe la Dunia 2014 Brazil leo, akirejea katika benchi la ufundi la nchi yake kwa mara ya pili katika jaribio la kutwaa ubingwa wao wa sita kwenye ardhi ya nyumbani ndani ya kipindi cha miezi 18 ijayo.

Scolari, ambaye aliiongoza Brazil kutwaa taji lao la tano na la mwisho la dunia katika fainali za mwaka 2002 - miaka 10 iliyopita, alitambulishwa rasmi na Shirikisho la Soka la Brazil kwenye mkutano na waandishi wa habari, akichukua nafasi iliyoachwa na Mano Menezes aliyetimuliwa Ijumaa iliyopita.

Carlos Alberto Parreira, ambaye aliiongoza Brazil kutwaa ubingwa wao wa nne wa dunia mwaka 1994, alitangazwa kuwa mkurugenzi wa ufundi wakati shirikisho hilo la soka la BraziL.

EXCLUSIVE: BAADA YA OPERESHENI YA MASAA 8 YENYE MAFANIKIO - NSA JOB KUREJEA BONGO KESHO

Mchezaji wa Coastal Union Nsa Job ambaye alipata majeraha ya goti na kwenda nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji anatarajia kurudi Tanzania kesho baada ya kupatiwa matibabu mazuri huko nchini India. Nsa anasema alifanyiwa upasuaji kwa muda wa masaa nane na baadae akatolewa na kuwekwa chumba maalum kisha baada ya muda akatolewa na kuruhusiwa. Anasema anaendelea vizuri na kesho mungu akimjaalia anarudi Bongo




ZANZIBAR HEROES KIBOKO YA AKINA NIYONZIMA - WAWAPIGA 2-1

Mfungaji wa goli la kwanza la timu ya Zanzibar Heroes akiambaa na mpira huku mabeki wa timu ya Rwanda wakijaribu kumzuia wakati wa mchezo wa mashindano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Nambole nchini Uganda

Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakishangilia goli wakati wa mchezo dhdi ya timu ya Rwanda uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Nambole nchini Uganda katika mashindano ya Cecafa Challenge


JOSE MOURINHO AWAFUNIKA FERGIE NA WENGER KWA KUVUTA MSHAHARA MREFU ZAIDI

Hii ndio listi ya makocha wanaolipwa mshahara mrefu zaidi duniani. Namba 1 ikishikiliwa na Special One Jose Mourinho.

1. Jose Mourinho – Real Madrid (£12.3m)

2. Carlo Ancelotti – Paris St. Germain (£10.9m)

3. Marcelo Lippi – Guangzhou (£8.7m)

4. Sir Alex Ferguson – Manchester United (£7.6m)

5. Arsene Wenger – Arsenal (£7.5m)

6. Guus Hiddink – Anzhi (£6.7m)

7. Fabio Capello – Russia (£6.3m)

8. Tito Vilanova – Barcelona (£5.6m)

9. Jose Camacho – China (£4.8m)

10. Roberto Mancini – Manchester City (£4.8m)

11. Frank Rijkaard – Saudi Arabia (£4.3m)

12. Jupp Heynckes – Bayern Munich (£4.2m)

13. Andre Villas-Boas – Tottenham (£3.6m)

14. Harry Redknapp – QPR (£3.2m)

15. Jorge Jesus – Benfica (£3.2m)

16. David Moyes – Everton (£2.9m)

17. Manuel Pellegrini – Malaga (£2.9m)

18. Paulo Autuori – Qatar (£2.9m)

19. Abel Braga – Fluminense (2.8m)

20. Luciano Spaletti – Zenit (£2.7m)

21. Antonio Conte – Juventus (£2.4m)

22. Cesare Prandelli – Italy (£2.4m)

23. Vanderlei Luxemburgo – Gremio (£2.4m)

24. Muricy Ramalho – Santos (£2.4m)

25. Tite – Corinthians (£2.4m)

26. Ottmar Hitzfeld – Switzerland (£2.1m)

27. Joachim Low – Germany (£2m)

28. Marcelo Bielsa – Athletic Bilbao (£2m)

29. Martin O’Neill – Sunderland (£2m)

30. Roy Hodgson – England (£2m)

MWINYI KAZIMOTO NA SHOMARI KAPOMBE MAJERUHI STARS

Majeruhi, Shomari Kapombe (kushoto) na Mwinyi Kazimoto wakiangalia wachezaji wenzao wakati wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu Kyambogo nchini Uganda jana. Kapombe na Kazimoto waliumia wakati wa mchezo dhidi ya timu ya Burundi wa michuano ya Cecafa Chalenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela


Wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kyambogo Jijini Kampala jana

Wachezaji wa Kilimanajaro Stars wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kyambogo nichini Jijini Kampala jana kutoka kushoto ni Erasto Nyoni, Athuma Idd na John Bocco


KILIMANJARO STARS WASEMA HAWAJAKATA TAMAA - SOMALIA WAJIANDAE NA KIPIGO

Na mwandishi wetu,
Kampala
Kocha wa Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amesema hajakata tama baada ya kufungwa na Burundi bao 1-0 wakati wa mashindano ya Cecafa Challenge yanayoendelea Jijini Kampala.

Kocha huyo alisema wakati wa mzazoezi kuwa  vijana wake walijituma
sana na kuwasumbua Burundi katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wenye tope zito baada ya mvua kubwa kunyesha Kampala na hivi kuzipa timu zote wakati mgumu.

“Vijana walicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi hivi kuwapa

Burundi shida…mabao tuliyokosa ni mengi kwa hivyo hatujakata
tama…nimeongea na wachezaji na wamenielewa kwa hivyo tunajiandaa vizuri kabla ya kucheza na Somalia Jumamosi kukamilisha hatua ya makundi,” alisema.

Amesema ukiachia Shomari Kapombe na Mwinyi kazimoto waliojeruhiwa
 wakati wa mechi dhidi ya Burundi, wengine wote wako katika hali nzuri na wanajiandaa kuikabili Somalia.

“Tayari tumeshinda mechi moja dhidi ya Sudan kwa hivyo tukishinda
  mechi ya Jumamosi tutakuwa katika nafasi nzuri sana ya kuendelea na mashindano haya,” alisema Poulsen.

Mpaka sasa Burundi inaongoza Kundi B kwa pointi Sita, ikifuatiwa na
Tanzania and Sudan ambazo zina pointi  tatu na Somalia inashikilia mkia bila pointi yoyote.
Baadhi ya watanzania wanaoishi Kampala wamesema wana imani kubwa sana na timu yao kwani imeonesha uwezo mkubwa sana katika mashindano haya.

Mmoja wa mashabiki aliyesafiri mpaka Kampala kuishangilia Stars,
  inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Ali Shaban alisema kuna matumaini makubwa ya Stars kufika mbali katika mashindano hayo.

“Tumeona mechi yao ya kwanza nay a pili na kwa kweli timu iko

vizuri…hatukuwa na bahati ti wa mchezo dhidi ya Burundi lakini timu ilionyesha uwezo mkubwa na hatuwezi kuwalaumu kwa kufungwa kwa penalty,” alisema.

Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe
  akizungumza kutoka Dar es Salaam alisema bado kuna matumaini makubwa na watanzania wasife moyo kwani Stars imeshaonyesha uwezo mkubwa na bado kuna nafasi ya kusonga mbele.

“Tunaofuatilia mashindano haya kwenye runinga tumeshuhudia ni jinsi
  gani vijana wanajituma na ari waliyo nayo ya kushinda,” alisema.

Wakati wa mazoezi, wachezaji wa Stars walipata semina fupi kutoka kwa
  wawakilishi wa Wash United ambalo ni shirika linalohamasisha unawaji wa mikono.
Shirika hili limeiningia katika makubaliano na shirikisho mbalimbali za mpira duniani ili kuhamasisha wachezaji kueneza ujumbe kuhusu unawaji wa mikono.

CECAFA TUSKER CUP LIVE CENTER: RWANDA vs ZANZIBAR

MUSIC VIDEO MPYA YA MTANZANIA ANAYEISHI NCHINI MAREKANI!


Habari,
Kwa jina naitwa  SARAFF, ni mwana HIPHOP mpya wa kibongo ila ninawakilisha kutoka New York. Nataka kutumia fursa hii kuitambulisha nyimbo ya kwanza kwenye album yangu inayokwenda kwa jina la “Next Flight” http://www.youtube.com/watch?v=OA7KYA7OA-U .  Najua kuongea Kiswahili vizuri ila nimeamua kutumia English kwenye nyimbo zangu ili kujitangazisha kimataifa na kitaifa. Album nzima pamoja na video vimetengenezwa chini ya Waya Mkali Production.  Vile vile natoa nyimbo bure kwenye website yangu saraffmusic.com . Nita shukuru kama kazi yangu ikipewa nafasi katika blog/ website hii.
Shukrani za dhati,
Saraff.




KILIMANJARO STARS 0:1 BURUNDI KTK PICHA!

 Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Simon Msuva akimiliki mpira
wakati wa mchezo dhidi ya Burundi kwenye michuano ya Cecafa Challenge
uliochezwa katika Uwanja wa Mandela jana
 Kiungo mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, Mwinyi Kazimoto akimiliki
mpira wakati wa mchezo dhidi ya Burundi kwenye michuano ya Cecafa
Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Mandela nchini Uganda
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, John Bocco akichuana na Beki wa
Burundi, Glberty Kaze wakati wa mchezo dhidi ya Burundi kwenye
michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Mandela
nchini Uganda jana