Search This Blog

Saturday, September 1, 2012

CHEMSHA BONGO: TAJA MAJINA YA WACHEZAJI WOTE WALIOPO KWENYE KIKOSI HIKI


MICHEAL ESSIEN ALIVYOKUTANA JOSE MOURINHO KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUJIUNGA NA MADRID

BAHANUZI AIVURUGA COASTAL UNION UWANJA WA TAIFA LEO

 Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, akimtoka beki wa Coast Union, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jioni ya leo. 
Katika mchezo huo Yanga imeshinda 2-1, ambapo Coast Union ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao katika kipindi cha kwanza, ambalo lilidumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza na kufanya timu hizo kwenda mapumzi huku Coast ikiwa mbele kwa bao 1-0.
 Kipindi cha pili Yanga ilianza kucheza kwa presha na kasi iliyowachanganya zaidi Coast na kukosa mabao ya wazo na mipira mingine kigonga miamba. 
Alikuwa ni Ally Shamte aliyepiga krosi matata iliyounganishwa moja kwa moja na beki wa Cost, Phillip Kaila, aliyeruka na kuuweka kimiani katika lango lake. bao la pili liliwekwa kimiani na Said Bahanuzi, bao lililodumu hadi kumalizika kwa kipute hicho. 
 Niyonzima, akikwepa kwanja la beki wa Coast Union.
 Joshua (kulia) akimdhibiti Nsa Job wa Coast.
 Kavumbangu, akimiliki mpira mbele ya beki wa Coast.
 Mbuyu Twite, akijiandaa kumimina krosi mbele ya Nsa Job.
Jerry Tegete, akiruka tiktak na kukosa bao...... PICHA na http://sufianimafoto.blogspot.com/

AKUFFO NA KEITA: VISU VIPYA VINAVYONOLEWA NA MILOVAN MAFICHONI ARUSHA


MICHAEL MOMBURI, ARUSHA
KUNA watu wawili wako Simba ambao mashabiki wengi wa soka hususan wa Dar es Salaam hawajawaona. Watu hao walitua Dar es Salaam wakakaa siku chache kisha Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic akafanya uamuzi mgumu kuwapeleka porini.

Aliwapeleka kwenye pori la mibuni Arusha linaloitwa Krein Down. Unaingia ndani umbali wa dakika kama 10 kutoka Barabara Kuu ya Arusha-Monduli katika eneo la Kisongo.

Ndani ya eneo hilo kuna uwanja mzuri wenye nyasi safi, upepo mwanana na hakuna raia wanaoruhusiwa kuingia zaidi ya Simba na raia wa kigeni ambao wako makambini maeneo hayo wakijiandaa kwenda kutalii porini.

Watu hao wawili ambao Milovan amewaficha huko ni beki raia wa Mali, Komanbilli Keita na straika Mghana Daniel Akuffo.

Hakuna shabiki wa Dar es Salaam aliyeyaona majembe haya mapya ya Simba na pengine siku yakionekana Uwanja wa Taifa itakuwa balaa.

Wachezaji hao hawazungumzwi sana, lakini wamefiti ndani ya Simba na wanafanya kazi ambayo mchezaji yeyote wa kigeni anastahili kufanya.

Keita amefuta matatizo ya Simba kwenye ulinzi huku Akuffo akiongeza vitu adimu kwenye fowadi ambavyo pengine vinaweza kufanya mashabiki wasahau kelele na siasa za soka la mjini.

KEITA
Ni kijana mdogo wa Mali mwenye umri wa miaka 24 ambaye anazungumza Kingereza kwa taabu kidogo lakini shughuli yake ni nyingine.

Ni fundi wa mipira ya juu, krosi, ametulia, ana nguvu na anatumia akili kabla ya kufanya uamuzi.

Mastraika wa Simba wanamwogopa kwa kitu kimoja, anachapa sana viatu kisirisiri na ukimwingia vibaya siku yako inaweza kuwa imekwisha.

Keita anayezungumza Kifaransa alicheza kwenye klabu maarufu ya Stade Malian kwa miaka saba kabla ya kuhamia Jeanne Dare Arc ambako ndiko Simba ilikompata kupitia kaka yake ambaye ni wakala aliyeko Dubai.
Kaka yangu aliponipigia simu kwamba nenda Tanzania kafanye majaribio nilimshangaa sana. Nikauliza mara ya pili Tanzania? Wewe una matatizo, kuna soka gani huko?

Nilisema vile kwa sababu nilikuwa sijui chochote kuhusiana na soka ya hii nchi, alisema Keita mwenye rasta kama Amri Kiemba.

Anaongeza: "Lakini nilipofika Simba nimefuta kauli yangu. Nimegundua kwamba ni sehemu ambayo haina tofauti na Mali, kuna wachezaji wenye vipaji vikubwa na wanaocheza mpira wa pasi na nguvu.

Sizijui klabu nyingine lakini ukiangalia wachezaji kama Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Chombo, Haruna Moshi, Shomari Kapombe na wachezaji wengine inatosha kujua kwamba Tanzania iko vizuri.

�"Nilipomwona Ngassa siku ya kwanza vurugu zake nilishangaa sana, inahitajika akili za ziada kwa beki kucheza na mchezaji wa aina yake.

Si mchezo. Ushindani ni mkubwa sana ndani ya Simba ndiyo maana nimeridhia kusaini kwa kuwa napenda timu inayocheza soka la nguvu, pasi kwa spidi na staili ya Simba.

Ni timu ambayo kila mchezaji yeyote atapenda kuchezea,� anasema mchezaji huyo aliyechezea timu ya taifa ya vijana ya Olimpiki mwaka 2004.

Inabidi kufanya mazoezi ya nguvu sana kumshawishi kocha kwa vile namba yangu ina wachezaji wenye uwezo na waliozoweleka kama Kapombe na Nyosso, lakini wanaojua historia yangu wanajua mimi ni mtu wa kazi muda wote na napenda mechi ngumu kwa vile ndiyo zinanijenga na kunisafishia njia.

Kwa kuwa malengo yangu ni kucheza misimu miwili kwa kiwango cha juu ninyooshe njia yangu nipae Ulaya.

�Naamini Mungu amenileta Simba kwa makusudi ili nipite kuelekea kwenye mafanikio. Nimependa sana staili ya kocha Milovan anachezesha timu kwa staili ya soka ambayo ninaipenda, yaani timu inachezea sana mpira kwa haraka,� alisema shabiki huyo wa Manchester United na Real Madrid.

Akizungumzia tofauti ya Tanzania na Mali anasema:

Mali hakuna timu kubwa, zote ziko kawaida na kila timu inashinda mchezo si kama Tanzania ambapo klabu tatu ndiyo zinaongoza halafu kule kuna akademi nyingi za soka."

AKUFFO

Amecheza mechi mbili na kufunga mabao mawili tena ya kwanza lakini amekuwa akichezeshwa dakika 50 kutoa nafasi kwa wachezaji wengine. Ni straika mrefu kwenye futi 5.8.

Uchezaji wake hautofautiani na Emmanuel Okwi lakini yeye ana shabaha zaidi, haogopi, ana kasi, anakaba na anajua kujiweka kwenye nafasi.

Ni Mghana aliyechezea klabu za Hearts of Hoak, New Edubiase kabla ya kwenda Stella Club ya Ivory Coast ambako ndiko alikotokea akaja Msimbazi.

Kabla hajaja Tanzania alikuwa anajua mambo mawili tu kwamba kuna klabu kubwa za Simba na Yanga na lugha inayotumika ni Kiswahili.

�Nilitarajia kukutana na ushindani mkubwa sana wa namba kwa vile niliifuatilia Simba kwenye mitandao nikaangalia rekodi zake, nimependa sana mazingira ya kirafiki yaliyopo kwani sikutarajia kwamba ningeweza kujenga urafiki na wachezaji kwa kipindi kifupi hivi.

�Wachezaji ni wakarimu sana ndiyo maana unaona kazi yangu inakuwa rahisi, nimefunga mabao mawili kwenye mechi mbili nilizocheza hiyo haimaanishi kwamba nimekuwa fiti sana lakini ni mwanzo wa safari yangu.

Nitacheza sana kwenye ligi, sijajiwekea malengo kwamba nifunge mabao mangapi lakini nitataka kufunga kila mechi.

Ili kunyoosha njia ya yangu, kwavile sehemu nilipo kuna mastraika wengi kama Abdallah Juma, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu na wengine wengi ambao wako fiti kucheza.

�Ili kupata namba na kuitendea haki klabu na mashabiki lazima ufanya kazi ya ziada uwanjani, ninachoahidi ni nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja, kufanya kazi kwa nguvu kupitia malengo ya klabu na kuwaheshimu mashabiki.

Akuffo ambaye anacheza namba zote kwenye fowadi, anaitamani Taifa Stars: �Natamani sana kupata namba ya kuichezea Tanzania kwa kuwa naona kabisa kwamba nina uwezo wa kuisaidia ikafika mbali na ni sehemu tulivu ambayo nitafanikiwa zaidi kwa kucheza timu ya Taifa na klabu kubwa kama Simba.

�Hayo malengo yapo na nitauonyesha umma wa Watanzania kwa vitendo kwamba nina uwezo wa kuvaa jezi ya timu yao ya Taifa na kuwafanyia kazi, Akuffo ni mtu wa vitendo zaidi si maneno.

�Nimecheza timu yangu ya taifa ya vijana U-17 mwaka 2005, ninapenda sana soka la nguvu na ushindani na uzuri ni kwamba sina rekodi ya majeruhi ingawa ni kitu kinachoweza kumtokea mchezaji wakati wowote.

Naitaka Tanzania haimaanishi kwamba Ghana hakuna amani lakini napenda kucheza soka kwenye mazingira ninayopewa nafasi, ukiangalia timu yetu imejaa wachezaji wengi wa Ulaya,� alisisitiza mchezaji huyo anayetumia simu ya kisasa aina ya Samsung Galaxy.


KOCHA MILOVAN
�Mpaka sasa nimeridhika na uwezo wa wachezaji hawa, ni watu wanaojituma sana na ambao nadhani msimu huu wataibadili sana Simba.

Ukianzia na Keita ameongeza kitu cha ziada pale kwenye ulinzi amefuta tatizo lililokuwapo, anaweza kucheza vizuri na Ochieng (Paschal) hata Juma Nyosso.

�Akuffo ni mwepesi na amefanya vizuri katika mechi alizocheza ndiyo maana unaona anafunga kila anapocheza.

Story kutoka Gazeti la Mwanaspoti

FIESTA 2012 ILIVYOTINGISHA MUSOMA - YATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA


Bofya hiyo video uone jinsi palivyokuwa hapatoshi ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipokuwa linaunguruma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoriki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
 Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
 Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
 Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
 Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma. 
 Kati ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya Karume mjini Musoma. 
 Ray na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
Rais wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Profesa Jay akionesha uwezo wake wa kukamua jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mwasiti akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.
Mmoja wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super Nyota 2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Dimpoz na wanenguaji wake, wakiwajibika kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya viwanja vya Karume mjini Musoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Rachel (kushoto), akionyesha uwezo wake katika uwanja wa Karume mjini Musoma, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 na wanenguaji wake.
Rachel akikamua kwenye uwanja vya Karume mjini Musoma ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Msanii wa michano ya Bongo Fleva, Nay wa Mitego akipagawisha jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">


Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva wakiongozwa na baadhi ya Wafanyakazi wa Clouds Media Group wakiwa katika picha ya pamoja jioni ya leo na watoto wanaolelewa  na kituo cha watoto Yatima/waishio katika mazingira sambamba na walezi wao kiitwacho Jipe Moyo Center,kilichopo kata ya Mwisenge,Musoma mjini mkoani Mara.Kampuni ya Clouds Media Group ikishirikiana na wasanii mbalimbali ambao jioni ya leo watatumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya kituo hicho chenye jumla ya watoto 17 waliopo kituoni hapo.
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akishiriki kukabidhi sehemu ya msaada kwa niaba ya wasanii wenzake kwa baadhi ya watoto wanaolelewa na kituo hicho,kushoto ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group akikabidhi pia sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo kwa walezi wa kituo hicho,kilichopo Musoma Mjini.
Mratibu Msaidizi wa kituo hicho cha Jipe Moyo Center,Bi.Imelda Odoyo akitoa mkono wa shukurani kwa ujio wao kwa baadhi ya Wasanii  mahiri wa hip hop hapa Bongo Prof. Jay na Fid Q . 
Afisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Simalenga akizungumza machache kwa niaba ya Kampuni na pia kwa wasanii aliombatana nao,katika suala zima la kukabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo hicho mapema leo jioni,kulia kwake ni Mratibu Msaidizi wa kituo hicho cha Jipe Moyo Center,Bi.Imelda Odoyo na kushoto ni Mratibu wa kazi za kijamii wa kituo hicho,Bwa.Pantaleo Magesa Kuyenga.
Mratibu wa kazi za kijamii wa kituo hicho,Bwa.Pantaleo Magesa Kuyenga akiwakaribisha vyema baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Clouds Media Group na Wasanii walioambana nao jioni ya leo,akiwemo Prof Jay,Fid Q,Chege,Mwasiti,Bibi Cheke,Omy Dimpo,Bob Junior,Roma,Barnaba na wengineo. 
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakiongozwa na mkongwe wa muziki wa Bongofleva,Prof Jay wakitia saini kitabu cha wakati,mara walipowasili kwenye kituo cha Jipe Moyo Center jioni ya leo,wasanii hao watatumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambapo kesho pia watakamua kwenye uwanja wa Kambarage,mjini Sinyanga. 
Mmoja wa wasanii anaekuja kwa kasi katika anga ya bongofleva,Ommy Dimpo a.k.a Pozi kwa Pozi akijitambulisha mbele ya wenyeji,ambapo wageni wote wakiwamo wasanii walijtambulisha.
  Mkongwe kwa umri lakini anakamua vilivyo kwenye anga ya bongofleva,Bibi Cheka nae akijitambulisha mbele ya wenyeji.
 Sehemu ya misaada kama inavyoonekana mara baada ya kukabidhiwa kwenye kituo hicho.
Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiwasili kwenye kituo cha kulelea watoto Yatima/waishio katika mazingira magumu kiitwacho Jipe Moyo Center,kilichopo kata ya Mwisenge,Musoma mjini mkoani Mara.Kampuni ya Clouds Media Group ikishirikiana na wasanii mbalimbali ambao jioni ya leo watatumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya kituo hicho chenye jumla ya watoto 17 waliopo kituoni hapo.

SAMUEL ETO'O AWAONYESHA CAMEROON NINI WANAKOSA - AFUNGA BONGE LA BAO URUSI

RADAMEL FALCAO NI HATARI MNO - APIGA HAT TRICK, ATLETICO MADRID AKIVUNJA DARAJA NA KUIBAMIZA CHELSEA MABAO 4-1 KWENYE UEFA SUPERCUP

  KIMINYATO ZAIDI tumblr m9mw7ujUvG1r1fq7do1 500 Gif : Radamel El Tigre Falcaos Golazo V Chelsea tumblr m9mwkwJPA11r1fq7do1 500 Gif : Radamel El Tigre Falcaos Golazo V Chelsea

AKINA SHEKHAN RASHID WAZIDI KUTESA SWEDEN - FC KILIMANJARO YAITANDIKA APOLLON SOLNA FK


Add caption