Search This Blog

Saturday, November 30, 2013

MATOKEO EPL: ARSENAL WAZIDI KUTAKATA, RAMSEY AZIDI KUNG'ARA - WEST HAM WAZIDI KUMCHIMBIA KABURI MARTIN JOL

Cardiff City 0-3 Arsenal (Ramsey x2, Flamini)
Everton 4-0 Stoke City (Deulofeu, Coleman, Oviedo, Lukaku)
Norwich City 1-0 Crystal Palace (Hooper)
West Ham United 3-0 Fulham (Diame, C. Cole, J. Cole)
Aston Villa 0-0 Sunderland

ETHIOPIA YAITANDIKA ZANZIBAR HEROES 3-1

Zanzibar Heroes leo jioni imekubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Ethiopia katika mfululizo wa mchezo wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Chalenji  uliopigwa katika Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

Jahazi za Heroes lilizamishwa na mabao ya Fasika Asfan dk 5, Salahadin Bargicho kwa mkwaju wa penalti dakika ya 37 baada ya Manaye Fantu kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari na baadae Kebede alifunga la tatu dakika ya 83.

Kiungo mpya wa klabu ya Simba Awadh Juma Issa aliifungia bao la kufutia machozi Zanzibar. 

Kwa matokeo hayo, Zanzibar inabaki na pointi tatu na Ethiopia iliyoanza kwa sare ya bila kufungana na wenyeji Kenya, inakuwa na pointi nne.

ROBIN VAN PERSIE NA MABAO: UGONJWA ULIOKUWA UNAWASUMBUA ARSENAL MSIMU ULIOPITA UMEHAMIA MAN UNITED MSIMU HUU.


Goli la mdachi huyu liliamua mechi ya hivi karibuni baina ya Man United na Arsenal, lakini Je Mashetani Wekundu wamekuwa wakimtegemea zaidi Robin van Persie kwenye ufungaji?

Mwaka mmoja uliopita, niliandika makala fupi kuhusu mwanzo m'baya wa Arsenal katika msimu wa
 2012/13, wakiwa na safu butu ya ushambuliaji huku wakiwa wametoka kumpoteza Robin van Persie. Wakati huo Arsenal walikuwa wanahangaika sana kufunga mabao huku mabao ya Van Persie yakiwa tayari yamempa uongozi katika listi ya ufungaji huku Man United wakiwa nyuma kwa pointi moja kutoka kwenye timu iliyokuwa ikiongoza ligi. Ulikuwa ni ushahidi tosha kwamba Arsenal walikuwa wakimtegemea mno mholanzi huyo katika msimu wa nyuma wa 2011/12 , na bado wakati huo pia walishindwa kushindana na safu ya ushambuliaji iliyoundwa Rooney, Hernández, Welbeck, kwa idadi ya mabao.

Mwaka mmoja mbele, hali inaonekana kubadilika. Kama chati inavyoonesha hapo chini, baada ya michezo 11 msimu wa EPL, United imefunga jumla ya mabao 18, saba yakiwa yamefungwa na Van Persie. Ukiondoa mabao hayo saba katika 18, timu ingekuwa na rekodi ya tano kwa ubovu katika upachikaji mabao katika ligi..

Kwa utofauti upande wa Arsenal, ukitoa magoli sita yaliyofungwa na mchezaji anayeongoza Aaron Ramsey, kutoka katika jumla ya mabao yao 22, Gunners bado wangekuwa na rekodi nzuri ya ufungaji wa mabao katika ligi. Mabao ya hivi karibuni ya Van Persie dhidi ya Arsenal, Stoke, na Southampton, yanamaanisha kwamba United imeshinda mechi mbili na kutoa suluhu mara 1, badala ya kutoa suluhu mara mbili na kupoteza mechi moja. Bila mabao ya Van Persie - Pointi tano walizopata United wangejikuta kwenye nafasi ya tisa. Arsenal, hata bila ya pointi nne walizopata kwa mabao ya Ramsey dhidi ya Sunderland na Swansea, bado wangeweza kuwemo katika Top 4. 
Japokuwa msimu uliopita United iliweka rekodi ya kuwa na wafungaji wa mabao 20 tofauti, lakini msimu huu mpaka sasa ni wachezaji sita tu tofauti waliofunga magoli ya United katika EPL tangu mwezi August. Kama ambavyo unaona kwenye chati hapo juu, Arsenal tayari wana wafungaji 10 tofauti wa mabao msimu huu mpaka sasa.

Hii inanipa ishara kwamba Arsenal ndio wana kikosi kilicho na uwiano mzuri. Timu inaonekana kutowategemea sana wafungaji  Ramsey na Olivier Giroud kuliko United wanavyotegemea mabao ya RVP na Rooney. Hata Liverpool, ambao wana tofauti ndogo ya mabao nyuma ya Arsenal, wana utegemezi mkubwa wa mabao ya  Luis Suárez na Daniel Sturridge, ambao wamefunga mabao 16 kati ya 20.
Mashabiki wengi wamekuwa wakitoa maoni yao kwamba tofauti na United pamoja Liverpool, ambao wana bahati ya kuwa safu za ushambuliaji zinazoundwa na Suarez/Sturidge na Rooney/RVP, Arsenal wanamtegemea zaidi Giroud kwa mabao yao. Lakini bado washambuliaji wengine wa Arsenal wameonyesha wana uwezo kumsapoti mshambuliaji huyo wa kifaransa, wakifunga mabao 15 mengine. Idadi hii haijafikia hata na kundi zima la viungo wa Chelsea.

Pamoja na kuwa na wafungaji tofauti msimu uliopita, kiungo pekee wa United ambaye alichangia mabao mengi alikuwa Shinji Kagawa na mabao sita. Na mabadiliko pekee yaliyofanyika kwenye safu hiyo ni kuondoka kwa Paul Scholes na kuja kwa Maroune Fellaini, ambaye abado ameshindwa kuwa na kiwango alichokuwa nacho msimu uliopita na Everton ambapo alifanikiwa kufunga mabao 11.

Kuna habari nzuri kwa Arsenal kwamba wamekuwa wakicheza karibia msimu mzima bila washambuliaji tegemeo ambao walikuwa kwenye top 3 ya wafungaji bora msimu uliopita kwenye timu yao, Theo Walcott na Lukas Podolski. Kurejea kwa washambuliaji hawa wawili kutamuongezea machaguo Wenger katika kukiongezea makali kikosi chake.

Liverpool na United wanaweza kuwa na washambuliaji wazuri zaidi kwenye ligi, lakini bado ni Arsenal wanaonekana kuwa na safu kali zaidi kwenye msimu huu. Van Persie na Rooney walionyesha ubora wao wakati timu hizi mbili zilipokutana wiki kadhaa zilizopita, lakini endapo majeruhi wa Arsenal watakaporejea, kikosi cha Arsenal kitakuwa vizuri zaidi. Ikiwa watasajili mshambuliaji mwezi January itakuwa bora zaidi kwa Gunners. Ni United ambao wanategemea zaidi mabao ya Van Persie msimu huu, na ni Arsenal wenye kikosi cha makali zaidi msimu huu. 

*TAKWIMU ZA MAKALA HII HAZIHUSISHA MECHI ZA WIKIENDI HII NA ILIYOPITA*

SALAMU ZA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA KWENYE HAFLA YA KUPOKEA KOMBE HALISI LA DUNIA TANZANIA


Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dk. Fennela Mukangara- Waziri wa

Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Dioniz Malinzi- Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

Mkuu wa msafara wa FIFA/Coca-Cola

Bw Yebeltal Getachew- Meneja Mkazi wa Coca-Cola

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
Wageni waalikwa
Mabibi na mabwana

Mheshimiwa Rais, nianze kwa kukushukuru kwa heshima uliyoupatia mpira wa Tanzania kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika hafla yetu hii ya kupokea Kombe halisi la Dunia.
Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kupewa heshima hii na FIFA na washirika wake kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola.

Coca-Cola ni washirika wetu wa karibu na wamekuwa wakidhamini mashindano ya kitaifa ya vijana tangu mwaka 2007, mashindano ambayo kwa kiasi kikubwa yamesaidia kuibua vipaji vingi ambapo baadhi yao wameweza kuchezea timu zetu za Taifa na klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza.

Tunawashukuru sana Coca-Cola na tunaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano katika jitihada zao za kuendeleza soka ya vijana.

Mheshimiwa Rais, tarehe 19 Novemba, 2009 wakati unapokea kombe hili hili hapa Tanzania ulitoa changamoto kadhaa kwa uongozi wa mpira wa Tanzania.
Ulitushauri tuimarishe uongozi na utendaji wetu kuanzia ngazi ya Taifa, Mikoa, Wilaya hadi klabu, ulitushauri tupate walimu wenye uzoefu wa kutosha kufundisha timu zetu za mpira na pia ulitushauri tuwekeze katika kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji toka wakiwa na umri mdogo.

Mheshimiwa Rais ushauri wako kwetu tuliuzingatia na tulifanya jitihada za kuufanyia kazi. Hali ya utulivu katika uendeshaji mpira wetu imeimarishwa na pale palipoonyesha dalili za migogoro tulikemea na ikibidi tulichukua hatua madhubuti kutatua migogoro.

Tumefanya kozi mbalimbali za kuwaendeleza walimu wetu wa mpira, waamuzi, madaktari na viongozi wetu wa ngazi mbalimbali na matokeo yake yanaonekana katika kuinuka kwa viwango vyao vya ufundishaji na utoaji uamuzi uwanjani.
Mheshimiwa Rais kama ulivyotuelekeza mwaka 2009 maendeleo ya soka ya vijana ndio ufunguo wa maendeleo ya mpira kwa Taifa letu. Uongozi mpya wa TFF ulioingia madarakani alfajiri ya tarehe 28, Oktoba 2013 tayari unalifanyia kazi jambo hili kwa umakini mkubwa.
Uongozi wetu umeamua kuwa ufunguo wa mpango endelevu wa soka ya vijana utakuwa ni Tanzania kuwa mwenyeji wa fainali za Afrika za vijana chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2019.

Fainali hizi uhusisha mataifa manane yanayogawanywa katika makundi mawili ya awali akiwemo mwenyeji ambaye anaingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya fainali hizi. Aidha timu mbili zinazoongoza makundi haya mawili moja kwa moja huwa zinacheza fainali za dunia za vijana chini ya umri wa miaka17.

Fainali hizi ndizo ziliwaibua akina Luis Figo, Ronaldino, Nwankwo Kanu, Michael Essien, Nii Lamptey, Celestine Babayaro na wengine kadhaa.

Ili tupate timu nzuri ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 itabidi mwaka kesho 2014 tufanye mashindano ya kitaifa ya vijana chini ya umri wa chini wa miaka 12 ili tupate kikosi cha kwanza cha Taifa U-12, kikosi ambacho kitakuwa pamoja kuelekea 2019.

Katika kuboresha kikosi hiki mwaka 2015 tutafanya mashindano ya kitaifa ya umri chini ya miaka 13, 2016 yatakuwa ya umri chini ya miaka 14, 2017 yatakuwa ya umri chini ya miaka 15 na 2018 yatakuwa ya umri chini ya miaka 16 na ambayo yatatupatia kikosi cha mwisho cha kuingia nacho fainali za vijana mwaka 2019.
Tunaamini timu nzuri za Taifa U-17 ya mwaka 2019 itatuzalishia kikosi imara kitakachoshiriki Olimpiki za 2020, kucheza CHAN na AFCON zitakazofuata na hatimae kufaulu fainali za dunia 2026 ambayo ni miaka kumi na tatu kuanzia sasa.

Ninashukuru tarehe 21 Novemba 2013, Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF) liliniteua kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya michuano ya Afrika umri

chini ya miaka 17 (CAF U-17 Organizing Committee), tunaamini kuwepo kwangu katika kamati hii muhimu ya CAF kutasaidia Tanzania ipate wenyeji huu mwaka 2019.

Mheshimiwa Rais kwa mujibu wa kanuni za CAF nchi inayoomba uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika haina budi ionyeshe barua ya kuungwa mkono na nchi yake(Letter of support from Government).

Wiki ijayo tutawasilisha barua kwenye Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ya kuomba kuungwa mkono na Serikali katika azma yetu hii, tunaomba Serikali ituunge mkono katika jambo hili.

Mheshimiwa Rais nimalizie kwa kukushukuru tena kwa uwepo wako katika shughuli hii muhimu, ninaishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ushirikiano wanaotupa katika shughuli zetu za kila siku, FIFA nawashukuru sana kwa kutuwezesha kuwa moja ya nchi 88 duniani zilizopokea kombe hili, Coca-Cola asanteni sana tuzidi kuwa karibu.

Watanzania wenzangu ninaomba tuje kwa wingi kesho Jumamosi kutembelea Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuliona Kombe hili na kupiga nalo picha. Imani yangu ni kuwa ipo siku Kapteni wa Timu yetu ya Taifa atamkabidhi Rais wa Tanzania kombe hili.

Asante


Thursday, November 28, 2013

PICHA: HIVI NDIVYO KILIMANJARO STARS ILIVYOTOKA SARE NA ZAMBIA

 Timu ya Taifa, kilimanjaro Stars Leo imecheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup  na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos, ambao uko takriban kilometa 60 kutoka Nairobi. Timu hizo zimefungana 1-1. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua sana, Katika mechi iliyotangulia ambayo iliwakutanisha Burundi NA Somalia, Burundi iliwafunga Somalia goli 2. Yafuatayo ni matukio katika picha
 Hapa vijana wetu wakiwa katika Picha ya Pamoja Kabla ya kwanza kwa kipindi cha kwanza
 Bwana shiyo Pamoja na Gavana wa Machakos wakiwasalimia wachezaji.
 Mtanange ukiendelea uwanja wa Machakos
 Kilimanjaro Stars wakipata dua kabla ya mchezo 
 Kocha wa Zambia akihojiwa na wanahabari
 Mashabiki wa Kilimanjaro Stars wakishangilia timu yao
 Wachezaji wetu wakitoka nje ya uwanja baada ya mchezo huo
 Makocha wa timu zote mbili wakihojiwa baada ya mchezo
Bwana Innocent Shiyo wa tatu  kutoka kushoto wakati wa wimbo Wa Taifa wa Tanzania ukipigwa. kulia kwa Bwana Shiyo ni Balozi  wa Zambia nchini kenya Mh Josephine Mumbi Phiri. Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya

ZLATAN: SIHITAJI BALLON d'OR, NAJUA MIMI NI BORA."

Cristiano Ronaldo au Franck Ribery oyote anaweza ksuhinda tuzo ya Ballon d'Or, Zlatan Ibrahimovic haihitaji tuzo hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Sweden amekuwa kwenye fomu nzuri sana msimu huu na klabu yake ya Paris St Germain, akifunga mabao nane katika Champions League - sawa na Cristiano Ronaldo.

Ronaldo anaonekana kupewa nafasi kubwa kushinda tuzo hiyo ya  Fifa-Ballon d'Or baada ya hat trick yake katika ushindi wa Ureno dhidi ya Sweden wiki iliyopita na hivyo kuiwezesha nchi yake kufuzu kushiriki michuano ijao ya dunia. 

Winga wa Ufaransa Ribery aliisaidia Bayern Munich kushinda makombe matatu msimu uliopita na alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kutwaa mwanzoni. 
"Sihitaji Ballon d'Or kujua kwamba mimi ni bora," alisema Ibrahimovic, ambaye pia amesaidia timu yake ya PSG jana usiku kuvuka hatua ya makundi. 
"Hii tuzo ina maana kubwa kwa wachezaji wengine."
Hakuna msweden aliywahi kushinda Ballon d'Or au mchezaji bora wa mwaka wa FIFA lakini hilo jambo halimkoseshi usingizi hata kidogo Cadabra. 
"Sio kitu ambacho nakifikiria sana na sio kitu ambacho kina umuhimu kwangu," alisema.

PICHA YA SIKU: MASHABIKI WA REAL MADRID WANAVYOMPA SAPOTI RONALDO ASHINDE BALLON D'OR

ZLATAN IBRAHIMOVIC AINGIA KATIKA LISTI YA WACHEZAJI WALIOFIKISHA MECHI 100 ZA CHAMPIONS LEAGUE

Zlatan Ibrahimović amejiunga na listi ya wachezaji waliocheza mechi 100 au zaidi ya UEFA Champions League baada ya kuweza kuicheza timu yake ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa kundi C game dhidi ya Olympiacos FC – na hivyo kuwa mchezaji wa 18 kufikisha idadi hiyo ya mechi. 

Mshambuliaji huyo wa kisweden amevichezea vilabu sita barani ulaya katika michuano hii, akianzia AFC Ajax, halafu Juventus, FC Internazionale Milano, FC Barcelona na AC Milan kabla ya kujiunga na PSG MSIMU ULIOPITA. Pia Zlatan ameweza kufunga jumla ya mabao 39 katika michuano hii. 

LISTI YA WACHEZAJI WALIOCHEZA MECHI NYINGI ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE (MAKUNDI MPAKA FINALI)142 Raúl González (Real Madrid CF, FC Schalke 04)
138 Ryan Giggs (Manchester United FC)
136 Xavi Hernández (FC Barcelona)
131 Iker Casillas (Real Madrid CF)
125 Clarence Seedorf (AFC Ajax, Real Madrid CF, AC Milan)
124 Paul Scholes (Manchester United FC)
120 Roberto Carlos (Real Madrid CF, Fenerbahçe SK)
115 Carles Puyol (FC Barcelona)
112 Thierry Henry (AS Monaco FC, Arsenal FC, FC Barcelona)
109 Paolo Maldini (AC Milan)
109 Gary Neville (Manchester United FC)
107 David Beckham (Manchester United FC, Real Madrid CF, AC Milan, Paris Saint-Germain)
104 Víctor Valdés (FC Barcelona)
103 Oliver Kahn (FC Bayern München)
103 Luís Figo (FC Barcelona, Real Madrid CF, FC Internazionale Milano)
102 Ashley Cole (Arsenal FC, Chelsea FC)
100 Andriy Shevchenko (FC Dynamo Kyiv, AC Milan, Chelsea FC)
100 Zlatan Ibrahimović (AFC Ajax, Juventus, FC Internazionale Milano, FC Barcelona, AC Milan, Paris Saint-Germain)
99 Alessandro Nesta (SS Lazio, AC Milan)
99 Petr Čech (AC Sparta Praha, Chelsea FC)
98 Andrea Pirlo (FC Internazionale Milano, AC Milan, Juventus)
98 Edwin van der Sar (AFC Ajax, Juventus, Manchester United FC)
97 Guti (Real Madrid CF)
97 Javier Zanetti (FC Internazionale Milano)
96 Claude Makelele (FC Nantes, Real Madrid CF, Chelsea FC)
96 Cristiano Ronaldo (Manchester United FC, Real Madrid CF)
96 Frank Lampard (Chelsea FC)

MAN UNITED, REAL, PSG, NA MAN CITY ZASHINDA NA KUFUZU HATUA YA 16 UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Real Madrid C.F. 4-1 Galatasaray
Bayer 04 Leverkusen Fussball 0-5 Manchester United
Juventus 3-1 F.C. København
Manchester City FC - Official 4-2 FC Viktoria Plzeň
FC SHAKHTAR 4-0 Real Sociedad de Fútbol
PSG - Paris Saint-Germain 2-1 Olympiacos B.C.
RSC Anderlecht 2-3 Sport Lisboa e Benfica

Wednesday, November 27, 2013

ZANZIBAR HEROES YACHINJA - WAIPIGA SUDAN NA KUONGOZA KUNDI - KENYA NA ETHIOPIA ZATOKA SARE

Zanzibar Heroes imeanza nzuri kampeni yake ya kugombea kombe la GOtv Cecafa Senior Challenge Cup baada ya kuifunga timu ngumu ya South Sudan 2-1 katika mchezo mgumu wa ufunguzi wa michuano hiyo katika uwanja wa Nyayo National Stadium.
Heroes walihitaji dakika 5 tu kupata bao la kuongoza kupitia  Suleiman Kasim.  
Zanzibar waliongeza bao lao la pili katika dakika ya 67 wakati mchezaji aliyeingia akitokea benchi Adeyum Saleh Ahmed alipofunga bao zuri kwa shuti kali lilomshinda golikipa Juma Jinaro.
Japo walikuwa nyuma kwa mabao mawili, Sudan waliweza kujikaza na kufunga bao la kufutia machozi katika dakika ya 75 kupitia mchezaji wao Fabiano Lako. Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Zanzibar waliweza kuondoka na ushindi ambao umeweza kuwafanya kuongoza kundi lao baada ya wenyeji Kenya kutoka sare ya bila kufungana na Ethiopia. 

MAN UNITED WANUSURIKA KUPATA AJALI YA NDEGE WAKIELEKEA UJERUMANI KUCHEZA NA BAYER LEVERKUSEN


Manchester United jana nusura wapate ajali kama iliyowahi kuwakumba miaka kadhaa iliyopita huko Munich baada ya ndege waliyopanda kusitisha zoezi la kutua mita 400 kutoka kwenye sehemu ya kutulia ndege kwenye uwanja wa Konrad Adenauer uliopo huko Cologne Ujerumani.
Ndege ya shirika la Monarch Airlines A321, namba MON 9254, ilipangwa kutua uwanjani hapo  5.30pm kwa muda wa Ujerumani, lakini rubani alilazimika kusitisha kutua kwa ndege hiyo kwa sababu kulikuwa na ndege nyingine kwenye sehemu ya kutulia. Ndege hiyo waliyopanda United ikabidi izunguke uwanja hewani na kuja kutua dakika 10 baadae saa 5.40pm.
Abiria mmoja katika ndege hiyo, ambayo ilikuwa na wachezaji wote wa United na maofisa wengine wa timu hiyo akiwemo CEO wa zamani wa klabu hiyo David Gill waliokuwa wakielekea kwenye mchezo wa klabu bingwa ya ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen, alisema kwamba tukio hilo lileta hali ya kutisha miongoni mwa abiria huku akifhamika kwamba ilitolewa taarifa rasmi kwamba kulikuwa na tatizo lilokuwa likiendelea. 
Mlinzi wa United Rio Ferdinand alitweet kuhusu tukio hilo muda mfupi baada ya kutua salama akisema, 'Landed in Germany....just....I’ve only just recovered after that choppy landing!
Kwenye msafara huo hakuwemo Sir Bobby Charlton, mtu mmojawapo aliyenusurika katika ajali iliyopita ya Munich, pia hakuwemo kocha mstaafu wa timu hiyo Sir Alex Ferguson.
Pamoja na kuchelewa kutua kwa ndege hiyo huko Cologne, Moyes na mlinzi Chris Smalling walienda kwenye mkutano wa waandishi wa habari wakiwa watulivu na wasiokuwa na chembe ya wasiwasi juu ya tukio hilo. 
Usiku wa leo United inacheza mechi muhimu na Leverkusen huku wakiwa wana mapengo ya wachezaji wao muhimu kama Van Persie, Carrick, Jones na Vidic.

RATIBA YA MECHI NYINGINE ZA LEO




MATOKEO YA JANA
Group E
Basel 1-0 Chelsea
Steaua Bucuresti 0-0 Schalke 04

Group F
Arsenal 2-0 Marseille
Borussia Dortmund 3-1 Napoli

Group G
Zenit Petersburg 1-1 Atletico Madrid
FC Porto 1-1 Austria Wien

Group H
Ajax 2-1 Barcelona
Celtic 0-3 AC Milan

CECAFA CHALLENGE CUP 2013 KUANZA RASMI LEO, STAR v ZAMBIA…TAKWIMU ZA TIMU ZOTE

Na Baraka Mbolembole

Timu ya Taifa ya Kenya ' Harambee Stars', leo itakata ' utepe' wa
michuano ya Mataifa ya ukanda wa CECAFA, kwa kucheza na timu ya Taifa ya Ethiopia. Wenyeji hao wa michuano ya sasa na makamu bingwa wa taji hilo, wanapewa nafasi kubwa ya kuvuka kundi A, mbele ya Ethiopia,
Zanzibar, na Sudan Kusini.

Mabingwa watetezi, Uganda wao wapo kundi C, pamoja na Rwanda, Sudan, na Eritrea katika kundi linalotarajiwa kuwa gumu zaidi katika michuano hiyo. Moi Kasarani na Nyayo Stadium, ni viwanja viwili vilivyopo
katika jiji la Nairobi, Kisumu Stadium, Mombasa, na Machakos ni idadi
ya viwanja vitano ambavyo vitazipokea timu 12. Mapema leo mchana wawakilishi wengine wa Tanzania, timu ya Zanzibar Heroes itacheza na  Sudan Kusini katika mchezop wa kwanza kabisa mwaka huu.

  KILIMANJARO STARS vs ZAMBIA
Timu ya Taifa ya Tanzania Bara itaanza kibarua chake cha kwanza siku ya kesho, Alhamis kwa kucheza na timu ' alikwa' ya Zambia katika mchezop unaosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa soka. Zambia, mabingwa wa michuano ya Mataifa ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika, COSAFA, iliifunga Kilimanjaro Stars katika mchezo wa mwisho kukutana katika michuano hii, walipoalikwa kwa michuano iliyofanyika, Dar es Salaam, 2010.
Mbele ya Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Stars ilipoteza kwa kulala bao 1-0 siku ya ufunguzi. Disemba mwaka uliopita, Taifa Stars iliifunga timu ya Zambia kwa bao 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki huku ' Chipolopolo' wakiwa na nyota wao waliotwaa taji la mataifa ya Afrika, februari, 2012.
  STARS, MATUMAINI YOTE KWA NGASSA
Moja kati ya silaha za hatari katika michuano hiyo ni kiungo mshambuliaji, Mrisho Ngassa. Ni mchezaji ambaye huvuta hisia kubwa za mashabiki hasa timu yake inapokuwa nje ya Tanzania, kasi, ujanja, unyumbulifu, na kucheza kwa kuhaha sehemu kubwa ya uwanja ni sifa ambazo zinampa nafasi ya kipekee kutamba katika michuano hii.
Wakati, kocha wa Stars itambidi asubiri hadi mapema mwezi ujao kupata huduma za washambuliaji wake wawili, kati ya watatu katika safu ya mashambulizi, Mbwana Samatta na Tomas Ulimwengu, ambao watakuwa na mchezo wa marejeano wa fainali ya kombe la shirikisho Afrika, wikiendi hii wakiiwakilisha klabu yao ya TP Mazembe, Kim Poulsen atamtegemea mfungaji huyo bora wa michuano iliyopita nchini Uganda.
Elius Maguli, Juma Luizio, Joseph Kimwaga, na Amri Kiemba wawili kati yao wanataraji kuanza sambamba na Ngassa katika safu ya mashambulizi. Itakuwa ni nafasi nzuri kwao na pengine kijana Said Dilunga anaweza kufanya vizuri zaidi yao kama atapewa nafasi ya kutosha.
Katika nafasi ya kiungo, KIM, bado anao wachezaji ambao wana uwezo na uzoefu wa kutosha, SAlum Abubakary atakuwa akicheza michuano yake ya pili, sambamba na Frank Domayo na wawili hao waliweza kucheza vizuri japo waliambulia nafasi ya nee baada ya kufungwa na Zanzibar katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu. Kwa upande wa uzoefu itakuwa ni pigo kubwa kwa Stars kama wachezaji hao vijana watashindwa kuendena na michuano kwa kigezo cha uzoefu wao mdogo. Ni vijanma ambao wameshikilia namba katika vilabu vyao vya Azam FC, na Yanga kwa zaidi ya miezi 14 sasa, na wamekuwa chaguo la kwanza katika michezo zaidi ya 15 ya Kilimanjaro Stars, na Taifa STars katika kipindi cha mwaka mmoja sasa
Wanatakiwa kujiam,ini zaidio na kuongeza uimakini katika mchezo dhidi ya Zambia, timu ambao husifika kwa kasi yao mchezoni na mchezo wa pasi za haraka haraka zile fupifupi, Kwa, Salum sina shaka ataweza kuwazima kama ilivyo kawaida yake, ni mtaalamu wa pasi fupi na ndefu, ni nadra kupoteza au kupiga pasi ' fyongo' uwanjani, wakati Domayo akisifika kwa utulivu wake, bado viongo hao wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kushindwa kutengeneza nafasi za mwisho japo muda mwingine huoneka kumiliki mchezo kwa kiasi kikubwa.
Wakati, Samatta na Ulimwengu tukisubiri huduma zao silaha yetu kubwa sasa ni Ngassa, ni vipi tunaweza kumchezesha na akaisadia timu, mbio zake, akili yake na uwezo wake alionao wa kutambua afanye nini atapokuwa amefika katika lango la adui, Domayo anaweza kupiga pasi ndefu zilizotimilifu itakuwa vyema kumtumia huyu kupiga pasi za haraka kwa Ngassa. Ni wazi Zambia watamili mpira mpira hiyo ni kutokana na namna tunavyoshindwa kuwa mashindanoni. Kwa nini nasema hivyo? Wakati mwingine ni lazima tuwe wazi wachezaji wetu hutuangusha hasa pale tunapokuwa tunaweka imani kubwa juu yao.
Kufungwa michezo mitatu, kati ya sita katika michuano iliyopita ni sawa na kutoa udhibitisho huo, wakati tulipofungwa mchezo wa kwanza na Burundi, ilitukumbusha kupandisha kiwango chetu cha uchezaji, hiyo ilitusaidia hadi kuwa na wafungaji bora wawili siku ya mwisho wa michuano. Tulicheza vizuri katika michezo miwili tu iliyofuata, lakini kipigo kutoka kwa Uganda kilikuwa ni ' kizito sana' katika vichwa vya mashabiki wa soka nchini. Tulifungwa kidhaifu sana katika mchezo wa nusu fainali huku Watanzania wakiamini kuwa ilikuwa nafasi yetu kuvunja utawala wa zaidi ya miaka kumi wa Uganda kutofungwa nyumbani.
Uzoefu wa wachezaji kama Kelvin Yondan, Athumani Idd ' Chuji' , Kiemba, Ngassa, Erasto Nyoni, Ivo Mapunda, usiishie katika uwakilishi wa uwanjani tu, wanatakiwa kuwakumbusha wachezaji vijana kama kina Ramadhani Singano, Domayo, Dilunga, Kimwaga na wengine umuhimu wa kuona fahari kushinda mataji wakiwa katika jezi ya taifa. Wakati tulipopata taji la mwisho mwaka 2010 kuna vijana ambao walitoka mitaani na kupata nafasi ya kukutana na watawala wa juu wa nchini. Ni fahari kuichezea timu yako ya Taifa. Ila mafanikio ndiyo kipimo sahihi cha ubora wa jambo lolote. HIvyo wachezaji wanatakiwa kufahamu kuwa tangu kizazi na kizazi wapo wachezaji ambao wamekuwa wakiiwakilisha nchi, ila wale waliofanikiwa kushinda chochote ndiyo waliopata nafasi ya kufika bungeni, ikulu na sehemu nyingine ambazo si rahisi kufika.
 KUJIAMINI KUPITA KIASI
Japo umakini limekuwa tatizo kubwa kwa Stars, kujiamini kupitiliza imekuwa ni sumu ambayo imekuwa ikituangamiza sisi wenyewe. WAtazame, Salum, Domayo na safu ya ulinzi. JInsi wanavyokuwa wanacheza wakati tukimiliki mpira imekuwa kama hawajui umuhimu wa kutengeza nafasi za kufunga mabao. Hii ni michuano ya mtoano. Nafasi moja, bao moja, kufungwa inamaanisha kuwa mchezo ujao utakuwa ni mgumu kuliko kama mngeshinda, na nafasi inakuwa ndogo ya kusawazisha mambo.
Safu ya ulinzi, Nyoni, anatakiwa kupevuka kiuchezaji sasa na kuacha na soka la ' kipima joto', huwa hatabiriki , ingawa akiwa katika siku yake nzuri utapenda kuona anavyokuwa akiisaidia timu katika mashambulizi na kuzuia, ila akiwa hovyo utatamani apasi, akisumbuliwa mara mbili au tatu hupoteza kujiamini na umakini wake unakuwa chini zaidi. Kwa kifupi safu za ulinzi wa pembeni zikiwa imara na kufanya kazi ipasavyo hufanya ulinzi wote kuimarika, ila wakiwa katika kiwango cha kupoteza mipira hovyo na kushindwa kujiamini katika maamuzi yao hupelekea kuvuruga mambo na wakati walinzi wa kati wakishirikiana na viungo kujaribu kuweka mambo sawa mara nyingi tunajikuta tukipotea kabisa uwanjani. Wachezaji wa ulinzi watakiwa kucheza soka lililokamilika kwa wakati huu wakiwa na michezo mingi katika historia yao.
" Kama utacheza vizuri na kushinda hilo ni bora, ila kama hautocheza vizuri kwa namna yoyote ile, hakikisha ushanda kwa  namna yoyote" aliwahi kusema, Luis Aragones, kocha wa kwanza kuipa Hispania taji baada za kupita miaka zaidi ya 40.
 BURUNDI, UGANDA, ETHIOPIA
Stars itacheza tena na Burundi katika kundi la B, na matokeo yao dhidi ya ' Risasi za Shaba' hapo kesho yanaweza kuufanya mchezo dhidi ya makamu bingwa hao wa mwaka 2004 kuwa mgumu zaidi na kuamua hatma ya kundi. Mwaka jana bao lililofungwa na Suleimani Ndikumana lilizamisha Stars nchini Uganda katika mchezo wa hatua ya makundi. Burundi, sambamba na Uganda, na Ethiopia wanaitumia michuano hii ili kujiweka sawa na michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN 2014, nchini Afrika ya Kusini, mapema mwaka ujao.

TAKWIMU
Hizi ni takwimu za kila nchi katika michuano hiyo tangu kuanzishwa.
Namba ni nafasi ambayo timu huonesha ilimazima katika nafasi gani
1' Huonesha ni nafasi ya kwanza, Namba mbili huwakilisha nafasi ya pili, Namba tatu kwa nafasi ya tatu kama ilivyo kwa namba nne kwa nafasi ya nne.

Burundi
1 –
2 2004
3 –
4 1999, 2007, 2008
Ivory Coast
1 –
2 2010[b][i]
3 –
4 –
Eritrea
1 –
2 –
3 –
4 1994
Ethiopia
1 1987, 2001, 2004, 2005
2 –
3 2000
4 1995, 2010
Kenya
1 1975, 1981, 1982, 1983, 2002
2 1979, 1985, 1991, 1999, 2001, 2008, 2012
3 1978, 1988, 1989, 1994, 1995, 2003
4 1977, 1984, 1996, 2004
Malawi[i]
1 1978, 1979, 1988
2 1975, 1984, 1989
3 1977, 1980, 1985
4 1983, 1992
Rwanda
1 1999[b]
2 2003, 2005, 2007, 2009, 2011
3 1999, 2001, 2002, 2006
4 2000, 2001[b]
Sudan
1 1980, 2006, 2007
2 1990, 1996[b]
3 1996, 2004, 2011
4 1991, 2003
Tanzania
1 1974, 1994, 2010
2 1973, 1980, 1981, 1992[b], 2002
3 1979, 1990, 2008
4 2009, 2011, 2012
Uganda
1 1973, 1976, 1977, 1989, 1990, 1992, 1996, 2000, 2003, 2008, 2009, 2011, 2012
2 1974, 1982, 1994, 1995[b], 2000
3 1983, 1984, 1987, 1991, 2007, 2010
4 1978, 1981, 1985, 2002, 2005, 2006
Zambia[i]
1 1984, 1991
2 1976, 1977, 1978, 1988, 2006
3 1981, 1992
4 1980, 1989
Zanzibar
1 1995
2 –
3 2005, 2009, 2012
4 1979, 1982, 1987, 1990
Zimbabwe[i]
1 1985
2 1983, 1987
3 1982
4 1988
By number of titles won and editions participated in Team 1ST 2ND 3RD 4TH Pld Pldlst Uganda 13 5 6 6 35 2012 Kenya 5 7 6 4 34 2012 Ethiopia 4 – 1 2 17 2012 Tanzania 3 5 3 3 33 2012 Malawi 3 3 3 2 21 2012 Sudan 3 2 3 2 19 2012 Zambia 2 5 2 2 20 2010 Zimbabwe 1 2 1 1 16 2012 Zanzibar 1 – 3 4 32 2012 Rwanda B 1 – – – 2 2001 Rwanda – 5 4 2 16 2012 Burundi – 1 – 3 13 2012 Côte d'Ivoire B – 1 – – 1 2010 Eritrea – – – 1 10 2012 Djibouti – – – – 10 2011 Kenya B – – – – 2 1994 Seychelles – – – – 2 1994 Somalia – – – – 23 2012 South Sudan – – – – 1 2012 Sudan B – – – – 1 1996 Tanzania B – – – – 1 1992 Uganda B – – – – 2 2000 Zimbabwe U23 – – – – 1 2

"MWENYE KIWANGO KIKUBWA NDIO NITAMPANGA." KOCHA WA YANGA AWAAMBIA KASEJA, DIDA NA BARTHEZ

KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amewaambia makipa wake Juma Kaseja, Ali Mustapha 'Barthez' na Deogratius Munishi 'Dida' kuwa kipa mwenye kiwango kikubwa ndiye atampa nafasi kwenye kikosi chake hicho.
Hiyo ni siku moja tangu kocha huyo aanze mazoezi na timu yake iliyoanza mazoezi jana kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Brandts alisema hatampanga mchezaji kutokana na ukubwa badala yake kiwango chake uwanjani.
Alisema, kwenye kikosi chake hadi hivi sasa hakuna kipa namba moja, yeye anaangalia uwezo na kujituma kwa mchezaji katika mazoezi yake.
"Nitampanga golini kipa mwenye uwezo katika wakati muafaka katika mechi zote tutakazozicheza na siyo kingine, sitaangalia ukubwa wa jina," anasema Brandts.
mwisho