Search This Blog

Saturday, August 31, 2013

WAKAZI WA MTWARA WAIPOKEA KWA SHANGWE SEMINA YA FURSA KWA VIJANA LEO

Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume  akizungumza mapema leo kwenye semin ya FURSA iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini  yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa  Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha. 
Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba  akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPO.COM

VIDEO: CHELSEA WALIVYOFUNGWA NA BAYERN MUNICH KWA MIKWAJU YA PENATI KATIKA UEFA SUPER CUP

VIDEO: ANGALIA CHEKA ANAVYOMGARAGAZA MMAREKANI KATIKA PAMBANO LAO LA UBINGWA WA WBU

PICHA: LULU ALIVYOZINDUA FILAMU YAKE YA KWANZA MLIMANI CITY BAADA YA KUTOKA JELA KWA DHAMANAWaigizaji wa filamu na wageni mbalimbali wakifuatilia filamu ya Lulu. 10
Tapeli Dude akifanya mambo yake wakati wa uzinduzi huo. 11Mwanamuziki Barnaba Classic akiimba kwenye uzinduzi huo. 12
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.1
Elizabeth Michael (Lulu) akiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam tayari kwa uzinduzi wa filamu yake inayokwenda kwa jina la  Foolish Age
14
Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotion akizungumza na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya Foolish Ege.

1a
Jonson Lukaza akizungumza na baadhi ya wageni wake waliohudhuria katika uzinduzi wa filamu hiyo 4
Muigizaji wa filamu Jacob Steven akizungumza na wageni wa kampuni ya Proin Promotion katika uzinduzi huo 5
Muigizaji Vicent Kigosi Ray akiwasili katika uzinduzi huo unaofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City. (PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE)

HIVI NDIVYO FRANCIS CHEKA ALIVYOMYOOSHA MMAREKANI NA KUSHINDA UBINGWA WA DUNIA WA WBU


 
 Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo, Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake, katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi, Fransous Bhotha.
 Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake, Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point.
Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinzani wake,Francis Cheka.hadi mwisho wa mchezo uliokuwa wa raundi 12,Francis Cheka aliweza kuibuka Kidedea kwa kumchapa mpinzani wake huyo kwa point na kufanikiwa kumnyang’anya mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU.
 Chukua hiyoooooo…
 Hapa lazima ukae,mie ndio kisiki cha mpingo:  hivyo ndivyo Bondia Francis Cheka alivyoonekana kuifanya kazi yake vilivyo.
 Refa wa Mchezo huo akimzuia Bondia Francis Cheka baada ya kumkoleza makonde kisawasawa mpinzani wake,yaliyompelekea kwenda chini.
Mpambano ukiendelea.
Wanahabari wakipata taswira za mpambano huo.
SOURCE DAILY NEWS

Friday, August 30, 2013

MAN UNITED YATUMA OFA YA £25M KWA ANDER HERRERA YAPIGWA CHINI - AS ROMA YAGOMA KUFUNGUA NAO MAZUNGUMZO JUU YA USAJILI WA DE ROSSI

Inaonekana klabu ya Manchester United ina bahati mbaya katika soko la usajili la wakati huu baada ya leo hii ofa ya £25million kwenda Atheltic Bilbao kwa ajili ya kumsajili Ander Herrera kupigwa chini - huku Roma wakigoma hata kuanzisha mazungumzo juu ya usajili wa Daniele De Rossi.

Kiungo mwenye miaka 24 wa kihispania, Herrera, aliwavutia United kwa muda mrefu sasa tangu Bilabo ilipowachakaza United katika Europa League misimu iliyopita.

Na De Rossi, 30, mshindi wa kombe la dunia ambaye ameshaichezea mechi 91 Italy na mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa na wanaolipwa fedha nyingi katika Serie A.

Raisi wa Bilbao Jose Urrutia alikaririwa akisema kwenye mtandao wa Twitter: 'Kuna ofa imetumwa kwa ajili ya Ander Herrera. Tumeipokea jana na tumejibu kwamba hatuna mpango wa kuuza wachezaji wetu.
'Klabu yetu ni tofauti. Tunajenga mahusiano ya kihisia na wachezaji wetu. Kwetu fedha sio jambo muhimu sana, ikitokea mchezaji anataka kuondoka basi inabidi aseme na klabu inayomtaka ilipe kiasi ambacho kimepangwa kwenye mkataba.'

Wakati huo huo Moyes ameshindwa kukanusha kwamba walituma kwa Herrera lakini akasema kamba ana matumaini ya kuongeza wachezaji kwenye kikos chake.
'Ninatumaini tutafanya baishara ya ununuzi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.'

GARETH BALE AFIKIA MAKUBALIANO MASLAHI BINAFSI NA REAL MADRID

Gareth Bale amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na Real  Madrid kuelekea uhamisho utakaovunja rekodi ya dunia kutoka  Tottenham.
Pamoja na hilo lakini miamba ya soka ya kihispania bado kwenye mazungumzo ya mwisho na Spurs juu ya ada ya uhamisho wa  £86m .
"Wakati mazungumzo yakiendelea jijini Madrid, tayari mchezaji ameshakubaliana maslahi binafsi na klabu," amesema mwandishi mkuu wa habari za michezo wa BBC Dan Roan.
. "Kilichobakia sasa ni Spurs kukubali rasmi ofa ya Real Madrid ambayo watalipwa kwa vipande katika muda wa miaka minne."

DAVID MWANTIKA ACHUKUA NAFASI YA KELVIN YONDANI TAIFA STARS

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

Mwantika ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye ni majeruhi. Wachezaji ambao ni majeruhi na Kim amewaondoa kwenye kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao ni Athuman Idd, Shomari Kapombe na John Bocco.

Taifa Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.

OFFICIAL: TFF NA AZAM MEDIA WASAINI MKATABA WA BIL.5.5 KUONYESHA MECHI ZA LIGI KUU - AZAM TV KUANZA MWEZI UJAO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.

Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.


KALI YA LEO: ANGALIA VIDEO YA MASHABIKI WA MAN UNITED WALIVYOIDHIHAKI ARSENAL NA WIMBO WA P SQUARE - PERSONALLY

ARSENAL HATA KAMA WANGEFUNGWA NA FENERBAHCE - BADO WANGEWEZA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA WA ULAYA

Klabu ya soka ya Uturuki, Fenerbahce, imepigwa marufuku ya kushiriki katika michuano ya bara Ulaya msimu huu, baada ya mahakama ya upatanishi ya michezo CAS, kuidhinisha uamuzi uliokuwa umetolewa na shirikisho la UEFA kuwa klabu hiyo ilihusika na sakata ya kupanga matokeo ya mechi.

Klabu hiyo ilikuwa, tayari kujiunga na ligi hiyo ya UEFA Cup, baada ya kuondolewa na Arsenal katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Shirikisho la UEFA, liliipiga marufuku Fenerbahce mwezi Juni mwaka huu, baada ya kuwapata maafisa wa klabu hiyo na hatia ya kupanga matokeo ya mechi ili kushinda ligi kuu ya soka nchini Uturuki.

Kwa maana hiyo hata kama wangefanikiwa kuitoa Arsenal katika mechi ya kufuzu champions league isingekuwa na maana kwao kutokana kufungiwa huko.

WAKATI AKIMWAGA FEDHA CHELSEA - ROMAN ABRAMOVICH ASITISHA UFADHILI WA SOKA NCHINI MWAKE

Mfanyabiashara tajiri na mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amesema amesitisha ufadhili wake wa soka nchini Urussi.
Msemaji wa kampuni ya uwekezaji ya Millhouse inayomilikiwa na Abramovich, amesema, chuo cha mafunzo ya soka nchini Urusi kilichokuwa kikifadhiliwa na mfanyabiashara huyo kimeafikia malengo yake.
Mtandao wa Forbes umechapisha habari kuwa tangu mwaka wa 2010, Abramovich amekuwa akipunguza ufadhili wake kwa shughuli za kuimarisha soka nchini Urusi.
Hata hivyo hakuna mzozo wowote uliosababisha uamuzi huo.
Ripoti zinasema kampuni ya NFA ilifadhili ujenzi wa viwanja mia moja thelathini nchini Urusi na kutumia zaidi ya dola milioni mia mbili.
Kampuni hiyo iliyoundwa mwaka wa 2004, pia iligharamia mafunzo ya makocha nchini Urusi.
Abramovich alianza kufadhili soka nchini Urussi muda mfupi baada ya kununua klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu ya Premier ya Uingereza.

Tangu mwaka wa 2005 hadi mwaka wa 2010 Abramovich alisaidi kufadhili timu ya taifa ya soka ya Urussi, ikiwa ni pamoja na mshahara wa dola milioni saba kwa kocha wake Guss Hiddink raia wa Uholanzi.
Dick Advocaat aliteuliwa kuwa kocha wa Urusi mwaka wa 2010 kuchukua mahala pa Hiddink.
Lakini mwaka wa 2010 Urussi ilishindwa kufuzu kwa fainali ya kombe la dunia iliyoandaliwa nchini Afrika Kusini.
Jarida la Forbes limechapisha ripoti kuwa Abramovich anashikilia nafasi ya kumi na tatu miongoni mwa watu tajiri zaidi nchini Urusi na inakadiriwa kuwa ana mali inayokisiwa kuwa zaidi ya dola bilioni kumi nukta mbili

HATIMAYE MAROUNE FELLAINI AOMBA KUONDOKA EVERTON BAADA YA MAN UNITED KURIPOTIWA KUONGEZA DAU

Marouane Fellaini amemwambia kocha wake Roberto Martinez kwamba anataka kuondoka Everton.
Uamuzi huo wa Fellaini unakuja baada ya Manchester United kuongeza dau lao kwa mbelgiji huyo - na beki wa kushoto wa timu hiyo Leighton Baines — mpaka kufikia £36million.
Fellaini, 25, bado hajapeleka ombi rasmi la kuhama lakini ameomba kwa maneno kuruhusiwa kujiunga na klabu ya Manchester United. 

Everton tayari wameshakataa ofa ya £26 million kutoka kwa kocha wao wa zamani, David Moyes. Lakini ofa mpya ya United imeongeza presha kwa klabu ya  Merseyside kuwauza nyota wake zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Thursday, August 29, 2013

SAMUEL ETO'O ATAMBULISHWA RASMI CHELSEA

MAKALA: YANGA DHIDI YA COASTAL ILIKUWA MECHI NZURI ILIYOHARIBIWA NA MWAMUZI

Na Baraka Mbolembole  
 
Kiki ya mkwaju wa penati kutoka kwa kiungo na nahodha wa timu ya Coastal Union, Mkenya, Jerry Santo katika dakika ya mwisho ya muda wa ziada, ilifanya timu hiyo kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga. Didier Kavumbagu aliifungia Yanga bao la kuongoza katika dakika ya 69 akimalizia vizuri mpira uliokuwa umepigwa na mlinzi wa kushoto, David Luhende.


Katika pambano gumu na la kukamiana, mwamuzi, Martin Saanya alitoa kadi sita za njano kwa wachezaji, Juma Nyosso, na Haruna Moshi ' Boban' kwa mchezo mbaya wa rafu, na Suleiman Kassim ' Selembe' kwa kosa la kujiangusha kwa upande wa timu ya Coastal, huku, Salum Telela, na Saimon Msuva kwa upande wa Yanga, pia mwamuzi huyo alitoa kadi nyekundu za moja kwa moja kwa wachezaji, Msuva na Crispine Odula wa Coastal kwa kukosa uungwana mchezoni.


Mchezo ulianza taratibu, na kuzidi kuonekana mgumu kadri dakika zilivyokuwa zinasonga mbele, na katika dakika ya kwanza tu, Coastal walikuwa wamefika katika eneo la Yanga, lakini, kiungo mshambuliaji, Daniel Lyanga akawa katika eneo la kuotea.
 

ILIKUWA NI MECHI YA UFUNDI?.

 Kocha wa Coastal, Hemed Morocco aliwapanga, Santo, Boban, na Odula katika safu ya kiungo , wakati yule wa Yanga, aliamua kuwapanga, Telela, Frank Domayo, Msuva na Haruna Niyonzima, katika mfumo wa 4-4-

Achana na uchezeshaji ‘mbovu’ wa mwamuzi, Saanya na wasaidizi wake , Jesse Erasmo, na Charles Chambea, ambao walionekana kuzidiwa na presha ya mchezo na kujikuta wakifanya maamuzi yaliyowakera wengi. Katikati ya uwanja mpira ulipigwa, viungo wakacheze kwa kadri ya walivyoweza na kufanya asilimia kubwa ya mpira kuwa unazunguka katikati ya uwanja. Frank Domayo, alijaribu kadri alivyoweza kumsumbua Haruna Moshi ‘Boban’, Domayo alionekana kuwa juu ya Boban kimchezo na kupelekea kiungo huyo wa Coastal kumchezea rafu ambayo ilifanya apewe kadi ya manjano.
Salum Telela alikuwa na jukumu la kuhakikisha anaziba njia zote za Boban, kazi ambayo aliifanya vizuri kwa dakika chache na pale Boban alipokuwa akiendelea kupata ‘ moto’, Telela akajikuta akishindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo. Hali ambayo iliwafanya viungo wawili wa ulinzi wa Coastal, Santo na Odula, nao kuwa na jukumu rahisi tu la kumzima, Niyonzima ( ambaye inasemekana alicheza huku akiwa na maumivu). Nilipenda namna Santo ilivyokuwa makini na mwenye maamuzi ya haraka, miguu yake mirefu ilimsaidia kucheza mipira ya ‘tackling’ kwa usahihi na alionekana akipandisha mashambulizi kwa tahadhari kubwa, akihofia uwepo wa Niyonzima. Alifanikiwa kwa kila alichofanya, alikuwa mlinzi wa walinzi wake, Marcus Ndehela na Nyosso.
 

Unawezaje kumzima, Niyonzima kwa muda mwingi wa mchezo?. Kuwa na viungo kama Santo na Odula ambao wana uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo na njia za hatari za wachezaji hatari za wapinzani wao ni sawa na kuwa na faida mara mbili zaidi, hawa wanakuwa viongozi wa ziada mchezoni, ni wachezaji ambao wanauwezo wa kuwatuliza wenzao hata wakiwa katika presha. Ndiyo maana hata pale, Niyonzima alipoamua kupandisha kiwango chake na kujaribu kukimbia uwanjani huku akiwachezesha washambuliaji wake, Jerry Tegete, ‘ Kavu’ na Msuva akakuta kote huko ‘ kumefungwa’ na walinzi wanne wa Coastal, Juma Ahmad ambaye aliweza kucheza kwa mtindo wa kupanda na kushuka katika beki ya kulia, Banda akawa na jukumu la kukimbia na Msuva kila mahali alipokuwa akipitishiwa mipira, huku Nyosso na Ndehela wakicheza ‘ ng’ando kwa ng’ando’ na Jerry na ‘ Kavu’.
Mechi ikazidi kuwa ngumu na ufundi wa walimu ukawa kando, Telela, akapote uwanjani kwa kuwa Uhuru Suleiman ( kabla hajaumia’ alikuwa akicheza kwa mtindo wa kubadilisha nafasi na Lyanga, na kumfanya Boban kushuka chini kidogo na kuanza kuisukuma timu mbele.


 Mshambuliaji, Yayo Lutimba bado anahitaji muda zaidi ili kuendana na ligi kuu, lakini akionekana kuwa ni mmoja ya washambuliaji ambao wanaweza kuja kufanya vizuri katika siku za usoni kwa sababu aliwafanya, walinzi Mbuyu Twite na Nadir Haroub ‘ Cannavaro’ kuwa bize kwa muda  fulani mchezo, aliwafanya wafanye makosa lakini uwezo wao mdogo katika umaliziaji uliwanyima mabao zaidi. Ilikuwa ni mechi nzuri iliyoharibiwa na waamuzi.

 SAANYA; Alichezesha mchezo wa Yanga na Coastal misimu miwili iliyopita wakati Yanga wakiwania nafasi ya pili na Coastal ikipigana kushuka daraja. Ilikuwa ni mechi iliyokuwa na presha kubwa, mashabiki wengi walitoka Dar hadi Tanga kushuhudia mchezo huo ‘ uliokuwa batili’ na Yanga kushinda kwa bao 1-0. Pia alichezesha mechi ya Simba na Yanga, Mei, mwaka huu, na alionesha udhaifu mkubwa wa kuendana na kasi ya mchezo kadri ilivyokuwa inaongezeka. Na jana ameishia kuonesha uchezeshaji wa kiwango cha chini zaidi katika mechi iliyokuwa na upinzani mkubwa. Hakuwa fair kwa maamuzi mengi, lakini atabaki ni mtu wa mwisho mwenye maamuzi makubwa zaidi katika mchezo huu wa soka hasa wakati mshindi anapotakiwa kuonekana.
Alitoa kadi za kutosha, alikuwa sahihi katika maamuzi yake na nilipenda alivyokuwa akisimamia maamuzi yake kwa kile alichokuwa anakiamua, lakini alifanya ujinga usio kuwa na maana na kuharibu mchezo wote pale alipomtoa nje Odula kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. Ni hadi lini tutakuwa na waamuzi kama, Saanya? Ilikuwa ni penati? Ulitaka mwamuzi afanye nini pale? Boban alikuwa katika ‘ moto’ na timu yote ya Coastal ilikuwa langoni mwa Yanga na mpira uliolazimishwa na Boban ukaishia katika mkono wa Niyonzima na Jerry Sato akatengeneza matokeo sahihi katika dakika ya mwisho ya mchezo.


 Soka linahitaji waamuzi kama Saanya ambao wakati mwingine wanapitiwa na kujikuta wakifanya makosa makubwa lakini yanayoongeza msisimko wa mchezo huu. Huyu ni mwamuzi wa mechi kubwa, tuendelee kumkosoa kwani bado anakua kiuchezeshaji. Samahani kama kauli hii itakukwanza. ‘ Mkuki, kwa Nguruwe kwa binadamu ni mchungu saaaaana’ Siyo lazima kila siku matokeo ya kushanaza yaletwe na Simba na Yanga, tunahitaji kuona nazo zikiadhibiwa katika muda mbaya.’ YANGA WALIFUNGA BAO LAO KATIKA MUDA MAALUMU, LAKINI WAKAFUNGWA KATIKA MUDA MAALUMU’

 0714 08 43 08

HATIMAYE ARSENAL WENGER ASAJILI MCHEZAJI MWINGINE - AMRUDISHA RASMI FLAMINI KWA MKATABA WA MIAKA 3

Arsene Wenger amefanya usajili wa pili katika dirisha hili la usajili linaloelekea mwishoni kwa kumsajili kiungo wa zamani wa timu Mathieu Flamini kwa uhamisho wa bure kutoka AC Milan.

Kiungo huyo ambaye aliondoka Gunners mwaka 2008 kujiunga na  AC Milan, amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya  £40,000 kwa wiki.
Flamini, 29, ni mchezaji wa pili kusajiliwa baada ya mshambuliaji kinda wa kifaransa Yaya Sanogo, ambaye amejiunga na Arenal akitokea Auxerre bure. 

Flamini amekuwa akifanya mazoezi na Arsenal wakati wote wa pre season baada ya kuachwa na AC Milan mwishoni mwa msimu uliopita.  SAKATA LA ADHABU YA NGASSA: TFF YAWAJIBU YANGA - YASEMA VIELELEZO VYA MAANDISHI VIMETHIBITISHA NGASSA ALIFANYA MAKOSA


Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa amesema kamati yake haikumhoji winga wa Yanga, Mrisho Ngassa ilijitosheleza na maelezo ya kimaandishi.
Ngasa amefungiwa kucheza mechi sita za mashindano na kutakiwa kuilipa Simba kiasi cha Sh45 milioni kufuatia kubainika kusajili mikataba ya klabu mbili kwa wakati mmoja.
Klabu yake ya Yanga imekata rufaa kupinga uamuzi huo, ambapo pamoja na mambo mengine inaona mchezaji wake hakupewa haki ya kujieleza kufuatia tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo.
Lakini jana wakati Mwenyekiti, Mgongolwa akizungumza na gazeti hili alisema kamati yake inafanya kazi na vielelezo vya maandishi, hivyo hawakuona sababu ya kumwita Ngasa.
“Kimsingi, watu wanatakiwa kufahamu, sisi kama kamati tunatumia maelezo ya maandishi ambayo ndio vithibitishoi vyetu, na kama ushahidi wa vielelezo utakuwa na upungufu ndipo tunapomwita mchezaji,” alisema Mgongolwa. Akifafanua alisema: “Kuna wachezaji wengi usajili wao umeonekana kuwa na matatizo, lakini hatukuwai kuwahoji.”

SOURCE: MWANANCHI

HATIMAYE VILLAS BOAS AKIRI BALE ANAKARIBIA KWENDA MADRID - LAKINI ASEMA WATAMPIGA FAINI KWA KUGOMA KUFANYA MAZOEZI

Klabu ya Tottenham huenda ikalazimika kumpiga faini nyota wake anayesakwa na Real Madrid, Gareth Bale baada ya kukosa kufika uwanja wa mazoezi kwa siku ya pili mfululizo.
Kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas amesema Bale ni sharti kutimiza wajibu wake licha ya kuwa huenda akajiunga na Real Madrid.
Real wametangaza azma yao ya kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 86, kiasi ambacho ndicho kubwa zaidi duniani kwa klabu yoyote kumnunua mchezaji mmoja.
Bale, mweye umri wa miaka ishirini na minne, alitarajiwa kurejea kambini siku ya Jumanne baada ya timu hiyo kwenda likizoni katika eneo la Marbella.
''Kwa sasa Real inataka kumsajili Bale, ikiwa hilo litatokea tunamtakia kila la heri, lakini kwa kuwa hajafika kambini, hilo ni kosa na sharti airekebishe'' Alisema Villas-Boas.
Bale amehusishwa na klabu ya Real na kocha huyo wa Tottenham anasema usajili huo huenda ukakamilika hivi karibuni.
Klabu ya Tottenham haitaki kumuuza mchezaji huyo hadi pale watakapomsajili atakayechukua nafasi yake.
Ripoti zinasema Tottenham huenda ikamsajili mshambulizi wa klabu ya Roma kutoka Argentina Erik Lamela kuchukua mahala pa Bale.
Bale hajaichezea klabu ya Tottenham au timu ya taifa ya Wales msimu huu kutokana na Jeraha, lakini mapema siku ya Jumatano alitajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Wales itakayocheza mechi ya kufuzu ya kombe la dunia dhidi ya Macedonia na Serbia baadaye mwezi huu.

PICHA: MASHABIKI WA YANGA WALIPIGA MAWE BASI LA COASTAL UNION NA KUVUNJA VIOO NA KUMPASUA MCHEZAJI WA WAGOSI

Siku ya jana baada ya mchezo wa Yanga vs Coastal Union kuisha - timu ya Coastal ikiwa inaondoka uwanja wa taifa ilifanyiwa vurugu na mshabiki wanaosadikika kuwa wa Yanga. Katika vurugu hizo inasemekana watu kadhaa wamejeruhiwa na huku mchezaji wa Coastal Union  Hamad Juma 'Basmat', amepasuliwa kichwani na ameshona nyuzi kadhaa.

SAMUEL ETO'O AWASILI LONDON TAYARI KUFANYIWA VIPIMO NA KUJIUNGA NA CHELSEA - MOURINHO AKIKIRI KUMSHINDWA ROONEY.

Full steam ahead: Samuel Eto'o arrived at St Pancras station on Wednesday night ahead of his move to Chelsea
Samuel Eto'o akiwasili London usiku wa jana

Chelsea inakaribia kumsajili mshambuliaji Samuel Eto’o kwa dili la mwaka mmoja lenye thamani ya £7million kwa mkataba wa mwaka mmoja leo Alhamisi baada ya kukiri kushindwa kumpata mshambuliaji wa  Manchester United Wayne Rooney.
Eto’o, 32, amekubali kupunguza dau lake alilokuwa akilipwa na Anzhi kiasi cha £17m kwa mwaka na sasa atasaini atasaini akiwa huru. 

Pamoja na hilo, lakini inaeleweka kwamba Anzhi wamemlipa Eto'o millioni kadhaa ili kuweza kumuondoa katika listi wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ndaniya klabu ya Anzhi.
Eto'o aliwasili jijini London jana usiku na anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya mchana wa leo katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham.

London calling: Eto'oChelsea bound: Cameroon striker Eto'o arrives at St Pancras

YANGA ILIVYOVUTWA SHATI NA WAGOSI WA KAYA COASTAL UNION UWANJA WA TAIFAWaamuzi wa leo wakiwa na manahodha wa timu zote mbili Jerry Santo wa Coastal Union na Nadir Haroub wa Yanga.
 Uhuru Suleiman akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Yanga kwenye mechi ya leo iliyoisha kwa suluhu ya 1-1.

Haruna Moshi 'Boban akipambana na Cannavaro
 Kimenukaaaaaaaa mashabiki wa Wagosi wa kaya kutoka Tanga moja kwa moja mpaka uwanjani, na kutoka uwanjani moja kwa moja mpaka Tanga. Ama kweli waja leo waondoka leo. (PICHA KWA HISANI YA COASTAL UNION BLOG)

                         Kikosi cha leo hiki kilichoanza dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
  
Hamad Juma akitafuta mbinui za kumtoka mchezaji wa Ynga, Mbuyu Twite huku Crispin Odula akiwa tayari kumsaidia.
                   Hapa Nadir Haroub akijaribu kumdhibiti 'toto tundu' Yayo Kato lakini alishindwa.

Abdi Banda kati kati ya wachezaji wa Yanga.
                             'Selembe' Suleiman Kassim akizongwa na Juma Abdul (12) wa Yanga.

Kulitokea tafrani kidogo wachezaji wa Yanga na Coastal Union, hatimaye mwamuzi akatoa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili Odula (Coastal Union) na Simon Msuva (Yanga).
 Hii ndiyo penalt aliyofunga Jerry Santo dakika ya 90 baada ya David Luhende wa Yanga kuunawa mpira eneo la hatari.