Search This Blog

Thursday, August 29, 2013

HATIMAYE ARSENAL WENGER ASAJILI MCHEZAJI MWINGINE - AMRUDISHA RASMI FLAMINI KWA MKATABA WA MIAKA 3

Arsene Wenger amefanya usajili wa pili katika dirisha hili la usajili linaloelekea mwishoni kwa kumsajili kiungo wa zamani wa timu Mathieu Flamini kwa uhamisho wa bure kutoka AC Milan.

Kiungo huyo ambaye aliondoka Gunners mwaka 2008 kujiunga na  AC Milan, amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya  £40,000 kwa wiki.
Flamini, 29, ni mchezaji wa pili kusajiliwa baada ya mshambuliaji kinda wa kifaransa Yaya Sanogo, ambaye amejiunga na Arenal akitokea Auxerre bure. 

Flamini amekuwa akifanya mazoezi na Arsenal wakati wote wa pre season baada ya kuachwa na AC Milan mwishoni mwa msimu uliopita.  



1 comment:

  1. Shaffih Dauda, try to be serious sometimes! hii habari bado haijathibitishwa rasmi na mtandao rasmi wa Arsenal wewe tayari umeshaipa kichwa kizito namna hiyo, ni kupagawisha tu mashabiki - as hakuna source yoyote uliyoweka kwamba umepata hiyo habari, last time ulikuja na habari kama hii ukidai kwamba hatimaye Gonzalo Higuan atua rasmi Arsenal, ikawa ni uwongo kabisa, tafadhali kama huna hakika na habari usifanye ukanjanja, inaboa

    ReplyDelete