Search This Blog

Saturday, February 4, 2012

SIMBA YAGONGWA NA VILLA SQUAD VODACOM PREMIER LEAGUE


Klabu ya Simba ya Dar es Salaam leo imekubali kipigo kutoka kwa Villa SQUAD katika mfulululizo wa ngwe ya lala salama ya Vodacom Premier League.
Katika mchezo huo uliofanyika jijini DSM katika uwanja wa taifa Villa ilifanikiwa kuondoka na pointi 3 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Villa ambao walimaliza mchezo huo wakiwa 10 dimbani walifunga goli lao katika dakika ya 40 likiwekwa kimiani na Nsa Job.
Katika hatua nyingine Coastal Union ya Tanga imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Moro United 1-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Chamazi – Dar es Salaam. Goli la Coastal lilitiwa kimiani na Rashid Yusuf katika kipindi cha pili.
Mashabiki wa Simba wakiwa hawaamini kilichotokea.

Matokeo mengine ya VPL Ruvu shooting wametoka sare pacha na Polisi Dodoma.


MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (16) 34
2. Yanga (15) 31
3. Azam FC (15) 29
4. JKT Oljoro (15) 26
5. Mtibwa Sugar (15) 22
6. Kagera Sugar (15) 20
7. Ruvu Shooting (16) 18
8. JKT Ruvu (15) 17
9. African Lyon (15) 17
10. Coastal Union (16) 17
11. Moro United (16) 15
12. Villa Squad (16) 13
13. Toto Africa (15) 13
14. Polisi Dodoma (16) 13david luis alipomuombea Torres!

EXCLUSIVE INTERVIEW NA MICHAEL WAMBURA!

BOFYA HAPA CHINI UMSIKILIZE MICHAEL WAMBURA AKIZUNGUMZIA MIZENGWE YA SOKA LA BONGO.

BREAKING NEWS! ANGETILEH OSIAH AMELAZWA AGA KHAN HOSPITAL!

TAARIFA AMBAZO ZIMETUFIKIA HIVI PUNDE NI KWAMBA KATIBU MKUU WA TFF ANGETILEH OSIAH AMELAZWA KWENYE HOSPITAL YA AGA KHAN...TUTAKULETEA TAARIFA ZAIDI KUHUSIANA NA AFYA YAKE!

TUNAKUOMBEA UPONE HARAKA KAKA YETU NGETA ILI UWEZE KUREJEA NA KULIJENGA TAIFA LETU.

ETI HUYU NI NANI ?

Na Mwandishi Wetu

Abdalah Mohamed 'Prins Naseem KUTETEA UBINGWA WAKE NA Salehe Mkalekwa
.Februari 24
BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST)
Abdalah Mohamed 'Prins Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake
wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa.
Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 57
na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi
'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New
Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam.
Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho
hilo kuendelea kuwainua mabondia chipkizi ambao hawajawa na majina
makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo.


"Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipkizi na ndio
maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni
kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya.
Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa
kati ya Shaaban Zungu na Hasan Salehe watakaopigana uzito wa kg 55,
Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey
Pacho atakayetwangana na Seleman Shaaban na Abdalah Yusuph
atakayepigana na Omari Kijepa.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye
mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth,
Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali
ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila
‘Super ‘D’.

“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika
pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo
wa ngumi,” alisema Super ‘D’Kocha wa mchezo wa ngumi Saba Joseph (kulia) akimwelekeza bondia Saleh
Mkalekwa jinsi ya kutupa masumbwi katika kambi yake iliyopo Mbagala
Mkalekwa anajihandaa na mpambano wa ubingwa wa PST na Abdalah Mohamed
'Prins Naseem' Februari 24.(Picha na
www.superdboxingcoach.blogspot.com)

MANCINI ALA MATAPISHI YAKE-ASEMA TEVEZ ANAWEZA KUICHEZEA TENA CITY

Kocha wa Manchester City Roberto Mancini amekiri Carlos Tevez anaweza kucheza tena katika kikosi chake ikiwa atamshawishi kwamba yupo fit .
Japokuwa na imani kubwa iliyokuwa imetawala kwamba mshambuliaji huyo mwenye miak 27 angekuwa ameshaondoka City katika kipindi cha usajili, Tevez amebaki na City baada ya timu kama AC Milan, Inter Milan, na PSG kufaeli kumsaini kwa dili la kudumu.
Tevez kwa sasa bado yupo Argentina na kumekuwa hakuna uhakika wowote Carlitos atarejea lini England.

Japokuwa, Mancini ambaye siku za nyuma aliwahi kusema haifikiriki kwa Tevez kuvaa tena jezi ya Man City, lakini sasa muitaliano huyo amemtaja Carlitos katika majina ya wachezaji 25 watakaotumika katika premier league.

“Carlos sio chaguo kwa sasa lakini inawezekana huko mbeleni akarudi kucheza hapa,” alisema Mancini.

“Nina matumaini kwamba amekuwa akifanya mazoezi katika kipindi cha miezi 3 iliyopita.

“Kuna kitu kimoja tu katika kichwa changu , kombe la Barclays premier league. Lakini akirudi na kama yupo fit – theninawezekana akapata nafasi katika kikosi.

FERGUSON: NI MUDA WA KUWAFUNGA CHELSEA UWANJANI KWAO SASA


Alex Ferguson amekiri sasa ni muda sahihi kwa Manchester United kumaliza rekodi yao mbaya katika uwanja wa Stamford Bridge.

Fergie hajawahi kuifunga Chelsea ugenini katika Premier league tangu 2004 na amepata pointi 3 kutoka katika 27 @Stamford Bridge.
Boss huyu wa United alisema: “Tumefanya vizuri sana ugenini msimu huu na tunahitaji kuendelea kufanya vizuri hata sasa.

“Tuna michezo muhimu ya ugenini muhimu mno katika mbio hizi za ubingwa – Chelsea, Tottenham na City.
“Mechi dhidi ya Chelsea katika miaka ya karibuni zimekuwa ngumu sana na tuna bahati mbaya sana pale Stamford Bridge. Wachezaji wangu wanajua nini cha kufanya.”

United wapo sawa kwa pointi na City katika msimamo wa ligi kuu ya England.
Wamepunguza pengo la pointi japokuwa na wakati mgumu walionao kutokana na majeruhi kuwa wengi katika kiksi chao, na sasa inaonekana watarudi katika form yao ya mwanzoni mwa msimu kwa wachezaji wengi wanaanza kurejea.

Fergie ana matumaini mtoto wa maajabu Tom Cleverley, 22, yupo tayari kurudi dimbani tangu alipopata majeruhi katika mechi dhidi ya Bolton mwezi September mwaka jana.
Ferguson : “Alikuwa hatari mwanzoni mwa msimu na itakuwa kama tumesajili mchezaji mpya kwa kuwa na Tom katika kikosi chetu. Nafikiri ni Cleverley ni mchezaji muhimu na anatafanya mabadiliko makubwa katika mbio za ubingwa.”

RIO FERDINAND: SIUTAKI UNAHODHA WA ENGLAND


Rio Ferdinand amejitoa katika mbio za watu wanaotajwa kuweza kumbadili John Terry kama Naohdha wa England.
John Terry alivuliwa kitambaa cha unahodha leo asubuhi ikiwa ni mara ya pili katika maisha ya soka.
Rio Ferdinand ndiye aliyekuwa mrithi wa Terry mara ya kwanza alipovuliwa unahodha, lakini Manchester United defender amesema hataki hata kufukiriwa katika watu wanaopaswa kuchukua jukumu hilo la unahodha safari hii.
“Sitaki kuwa nahodha wa England baada ya yaliyotokea kipindi kilichopita,” Ferdinand alisema katika ukurasa wake wa Twitter.
“(I) Nataka kuweka umakini wangu katika kuichezea United na ikiwa nitachaguliwa katika kikosi cha England nitakuwa mwenye furaha.”
Na katika interview fupi iliyorushwa na BBC Rio alikaririwa akisema: “Nimeshakuwa nahodha wa England hapo nyuma kwa kipindi kifupi. Nilinyang’anywa kitambaa cha unahodha na kwa sasa nataka ni-concentrate katika kuitumikia United, kiukweli . Napenda sana kuichezea vizuri Manchester United.”
Ferdinand alikuwa aiongoze England katika kombe la dunia 2010 lakini akapata maumivu ya goti yaliyomuweka nje ya michuano hiyo

Ferdinand alikasirishwa na jinsi alivyotendewa na Capello wakati unahidha aliporudishiwa Terry mwaka mmoja uliopita huku mlinzi huyo wa United akiwa hajataarifiwa kuwa ameporwa unahodha huo.

Friday, February 3, 2012

HAPPY BIRTHDAY: ATHUMAN IDD MACHUPPA ' BOTTLE '

                   MACHUPPA AKIWA NA CREDO MWAIPOPO
                           HAPA YUPO NA DOGO...

Aliyekuwa Refa wa Kimataifa Gratian Matovu amefariki Dunia leo

Aliyekuwa Refa wa Kimataifa hapa nchini, Gratian Hemans Matovu (pichani), amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam. Kwa mukujibu wa mtoto wake Bw. Stephen Matovu, Mzee Matovu amefariki leo majira ya saa 6 mchana huko nyumbani kwake Mbezi Beach (Makonde) na taratibu za mazishi zinaendelea hapo hapo nyumbani kwake. Mzee Gratian Matovu alianza kuwa refarii wa kimataifa tokea miaka ya 1964 na aliendelea na shughuli hiyo hadi miaka ya 1970 na hadi Mwaka 2006 alikuwa bado katika Kamati ya Marefarii Tanzania. HISTORIA FUPI Mzee Matovu alipata Diploma ya Urefarii kunako miaka ya 1956 na akaja kuwa refarii Daraja la Kwanza mnamo Mwaka 1961. Miaka Mitatu baadae alipata Beji ya FIFA. Mzee Matovu alipata kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Chama cha Marefarii Tanzania.
Kwa Taaria zaidi za wasiliana na STEPHEN MATOVU 0713576666
Mungu Amlaze Mahala Pema Peponi Amina

SOFIA MWASIKILI : ' MUNGU AKIJALIA KESHO NACHEZA MCHEZO WANGU WA KWANZA KWENYE SOKA LA KULIPWA '


SOFIA MWASIKILI AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE NCHINI UTURUKI.

HIKI NDO KIKOSI CHA LULEBURGAZGUCU
kesho Mtanzania Sofia Mwasikili anatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza tangia ajiunge na timu yake ya LULEBURGAZGUCU ya nchini Uturuki dhidi ya timu ya konak bel.
Luleburgazgucu inaongoza ligi  kuu ya wananwake ya nchini Uturuki ikiwa na Pointi 24 huku Konak bel ikishika nafasi ya pili na pointi 15. ligi hiyo inashirikisha jumla ya timu sita.

Official: Mtibwa Sugar Yamsimamisha Mecky Mexime.

Taarifa kutoka huko mkoani Morogoro zinasema kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar FC. Meck Mexime amesimamishwa baada ya wachezaji kumkataa
taarifa inasema wachezaji wa Mtibwa Sugar walikua na mgomo baridi uliosababisha timu hiyo kupoteza michezo miwili mfululizo kwenye uwanja wake wa manungu dhidi ya JKT Oljoro na Coastal Union .
baada ya uongozi wa juu wa Kiwanda kukaa na wachezaji hatimae wachezaji hao wakasema hawamtaki ndani ya timu. Na ndipo utawala wa kiwanda ukaamua kumsimamisha kazi pamoja na wachezaji wengine wawili.

EXCLUSIVE: DAVID DE GEA KUSIMAMA LANGONI DHIDI YA CHELSEA


David De Gea yupo tayari kutoa suluhisho la tatizo la golikipa katika kikosi cha Manchester United at Stamford Bridge baada ya kuitumia siku ya alhamisi kumshawishi Sir Alex Ferguson kuwa yupo fit kwa kufanya session mbili za mazoezi.
Ferguson alikuwa na hofu kumuanzisha the 21-year third choice keeper Ben Amos katika mechi ya Jumapili dhidi ya Chelsea, baada ya De Gea kuumwa ghafla huku Anders Lindegaard akiumia enka.
Lakini jana De Gea alirudi mazoezini na kumpa ahueni Fergie, hivyo mhispania huyo atasimama langoni siku ya Jumapili.

MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI

MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI


Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Machi 29 mwaka huu saa 10 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

 Kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.

Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.

Muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90. Mtihani uliopita ulifanyika Septemba 29 mwaka jana ambapo watahiniwa wanane walijitokeza na kufanya mtihano huo.

 Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.


RAUNDI YA 16 LIGI KUU YA VODACOM


Mzunguko wa 16 wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Februari 4 mwaka huu) kwa mechi tatu. Coastal Union itakuwa mgeni wa Moro United kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Nayo Villa Squad itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Ruvu Shooting na Polisi Dodoma zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

Viingilio kwa mechi ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 15,000 kwa VIP A wakati Uwanja wa Chamazi ni sh. 10,000 kwa Jukwaa Kuu na sh. 3,000 mzunguko.

Kwa mechi ya Mlandizi kiingilio ni sh. 2,000 kwa mzunguko wakati Jukwaa Kuu itakuwa sh. 5,000. Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko ya muda wa kuanza mechi za ligi hiyo kwa kituo cha Dar es Salaam. Mechi zinazochezwa wikiendi kwenye Uwanja wa Taifa zitaaza saa 10 kamili jioni wakati zile zinazochezwa siku za kazi zitaanza saa 10.30 jioni. Mechi zote za Uwanja wa Azam- Chamazi zitaanza saa 10 kamili jioni.


MZUNGUKO WA PILI LIGI DARAJA LA KWANZA (FDL)


Mzunguko wa pili (second leg) wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayochezwa katika makundi matatu tofauti unaanza kesho (Februari 4 mwaka huu) kwa mechi sita. Katika kundi A, Morani FC itakuwa mwenyeji wa Burkina Faso ya Morogoro katika mchezo utakaochezwa Kiteto mkoani Manyara.

Kwa upande wa kundi B timu zote sita zitakuwa uwanjani. Small Kids ya Rukwa itacheza na Polisi ya Iringa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Mbeya City na Tanzania Prisons zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya na Majimaji na Mlale JKT watapepetana katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kundi C litaanza kwa mechi mbili ambapo AFC ya Arusha watakuwa wageni wa Manyoni mkoani Singida na Rhino na Polisi Tabora zitakwaruzana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Mechi nyingine ya kundi hilo itakuwa kati ya 94 KJ na Polisi Morogoro ambayo itachezwa keshokutwa (Februari 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.


SIMBA, OLJORO JKT ZAINGIZA MIL 40


Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT lililochezwa Februari Mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 40,191,000. Jumla ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 105 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A walikuwa 11,860.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 7,023,171, uwanja sh. 2,341,057, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 936,423, TFF sh. 2,341,057, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,170,528 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 234,106.

Nayo mechi namba 104 kati ya African Lyon na Polisi Dodoma iliyochezwa Februari Mosi mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 45,000 kutokana na watazamaji 15 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo. Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni sh. 6,864.41 kila timu ilipata sh. 2,591, Uwanja sh. 514, TFF sh. 514, DRFA sh. 205, FDF sh. 257 na BMT sh. 51.

BREAKING NEWS: JOHN TERRY AVULIWA UNAHODHA WA ENGLAND


John Terry amevuliwa unahodha wa timu ya Taifa ya England kwa mara pili katika maisha yake ya soka.
Terry aliitwa na leo saa 4 asubuhi na Mwenyekiti wa FA David Bernstein na kuambiwa uamuzi uliochukuliwa na bodi ya maamuzi ya FA.
Uamuzi huu FA utakuwa umemuudhi kocha Fabio Capello ambaye yeye siku zote amekuwa akimtetea Terry na aliweka wazi ndiye atakayekuwa nahodha wa England katika EURO 2012.
Pia FA imempa muda wa kufikiria Terry kama bado anataka kuiwakilisha timu yake ya taifa katika EURO, lakini wamesema hatolazimishwa kufanya maamuzi kwa haraka.

Debate:Sekretariet ya TFF ilikuwa wapi toka kipindi hicho kuomba mwongozo hadi wasubiri leo uchaguzi wa DRFA umetangazwa ?

Kamati ya rufaa ilishatoa hayo maamuzi muda mrefu siku chache baada ya uchaguzi wa Mara kufanyika , sasa Sekretariet ilikuwa wapi toka kipindi hicho kuomba mwongozo hadi wasubiri leo uchaguzi wa DRFA umetangazwa na Wambura alionyesha nia ndio wanaomba mwongozo?

Kwasasa Cristiano anataniwa kuwa CR7 =Cristiano Penaldo 7 au Penotric


Je wajua ukweli? Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji aliyeweka rekodi kwenye LA LIGA kwa kufunga magoli mengi ktk nusu ya kwanza ya msimu, ambapo mabao 7 kati ya hayo mabao 24 ameyafunga kwa njia ya PENALTI. Ameweka rekodi ya kufunga magoli ya penalti nyingi zaidi miongoni mwa wafungaji bora waliowahi kuweka record ya ufungaji bora kwenye LigaBBVA. Mpaka sasa  ktk magoli 24 aliyofunga magoli 7 ni kwa njia ya penalti. Mpaka mwishoni mwa msimu uliopita  alikuwa amepewa zaidi ya magoli 10 ya penalti. Vilevile kati ya magoli 22 alofunga Messi goli 1 tu ndo lilikua la penalti. Kwasasa Cristiano anataniwa kuwa CR7 =Cristiano Penaldo 7 au Penotric. Source [él comfidèntial 2011].


KUTOKA KWA MDAU BRYSON SABUNI!

TAKWIMU MBALIMBALI ZA LIGI KUU YA ENGLAND MPAKA SASA.
RATIBA YA ROBO FAINALI YA AFRICAN CUP OF NATIONS 2012


Quarter-finals

4 February 2012
17:00
Zambia v Sudan

4 February 2012
20:00
Côte d'Ivoire v Equatorial Guinea

5 February 2012
17:00
Gabon v Mali


5 February 2012
20:00
Ghana v Tunisia

BREAKING NEWS: FA WAKUTANA LEO KUZUNGUMZA JUU YA UNAHODHA WA JOHN TERRY KATIKA KIKOSI CHA ENGLAND.


Saa chache baada ya moja ya wachezaji wa zamani Jason Roberts kusema John Terry ni sumu katika kikosi cha England, viongozi wa chama cha soka cha England FA wanaweza wakaamua kumvua  kitambaa cha unahodha Terry leo hii Ijumaa.
Mwenyekiti wa FA, David Bernstein amewasiliana na wanachama  12 wa bodi ya juu ya maamuzi jana Alhamisi kusikiliza mawazo yao juu ya suala la Terry.
Inavyoonekana wengi wa wanachama wa bodi hiyo hawadhani kama ni jambo sahihi kwa Terry kuwaongoza waingereza katika EURO 2012 huku akiwa na mashtaka ya matusi ya kibaguzi wa rangi, na wanaona FA kwa haraka inabidi ifanya maamuzi haraka kabla ya mkutano wa February 23 mwaka huu.

GIGGS: TUKIVUKA MWEZI HUU SALAMA TUNACHUKUA TENA UBINGWA.


Ryan Giggs anaamini kombe litabaki Old Trafford ikiwa Manchester United wataupita vizuri huu mwezi.
United watawatembelea Chelsea Jumapili hii, baadae watakutana na Liverpool na Tottenham, huku wakifunga mwezi huu kwa mechi ya ugenini dhidi ya Norwich.
Vijana wa Sir Alex Ferguson waliwakamata City kileleni wiki hii baada ya kuwafunga Stoke.
Na veteran huyu mwenye makombe 12 ya premier leaguae, Giggs anajua thamani ya kombe watakaloshinda kwa kuwashinda mahasimu wao wakubwa.
Alisema, “Tumeshaanza kurudi kwenye form yetu na kama tutapata matokeo mazuri katika michezo hii, confidence itakuwa juu sana.
“Tunafahamu ni mbio ngumu, lakini hiyo ndio michezo ambayo kila mtu anataka kucheza. Tunajua hii ni michezo muhimu sana, na tunafahamu kama tutashinda mechi hizi, then tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kuutetea ubingwa wetu.
“Tunajua kilicho mbele yetu na nini tunapaswa kufanya.”

ENDAPO JOHN TERRY ATAENDA EURO 2012: KIKOSI CHA ENGLAND KITAGAWANYIKA

Chama cha soka cha England kimeonywa juu ya sumu inayowezwa kusambazwa katika timu ya taifa ya England ikiwa John Terry ataitwa na kwenda katika michuano ya EURO  2012.
Terry anatuhumiwa kumtukana kwa kumtolea maneno ya kibaguzi Muingereza mwenzie Anton Ferdinand na kesi yake amabyo ilitajwa jana imepangwa kusikilizwa July 9, tarehe ambayo itakuwa baada ya kumalizika kwa michuano ya EURO.
Lakini Jason Roberts, mchezaji wa zamani wa Blackburn ambaye amehamia Reading na pia ni maarufu kama mchambuzi wa soka katika radio, anasema Terry hapaswi kuitwa na inabidi aondolewe katika kikosi cha England atleast mpaka kesi yake ya ubaguzi itakapoisha.
Pia anasisitiza hoja ya boss Fabio Capello kuwa Terry hapaswi kuhukumiwa kabla hajapatikana na hatia sio sahihi kwa kesi hii kwa sababu hata kaka yake Anton alitimuliwa katika kikosi cha ENGLAND kabla hajapatikana na hatia na FA kwa kukacha kupima vipimo vya matumizi ya madawa.
Akiwa katika mtandao wa Twitter, Roberts aliseama: “Nimeona kesi ya Ferdinand  na Terry imesogezwa mbele. Siamini kama ni sahihi kwa nahodha wa England kwenda katika Euros.
 “Msemo wa hakuna hukumu kabla ya kupatikana na hatia haufanyi kazi mara zote katika soka kama ilivyokuwa kwa Rio Ferdinand in 2003. Pia muhimu zaidi, naamini dressing room ya England at EUROS itakuwa imegawanyika na hiyo inaweza ikawa sumu.”
Situation ya Terry inaweza kuzungumziwa katika kikao kijacho FA.
Lakini inaeleweka Capello anataka kumchukua Terry kwenda nae EURO kama kiongozi wa timu.
Macho yote sasa yategeukia @Stamford Bridge jumapili hii ambapo Terry anakutana na Rio Ferdinand wa Manchester United kaka wa Anton.
The Premier League committee imesema utaratibu wa kupeana mikono utaendelea kama kawaida katika mechi hiyo – tofauti na walivyofanya FA katika mchezo wa Carling cup kati ya QPR na Chelsea.

FIFA: TUNAHITAJI RIPOTI NZIMA YA TUKIO LA VURUGU MISRI


Shirikisho la soka duniani FIFA limeomba kupatiwa ripoti nzima ya tukio la vurugu lilitokea nchini Misri ambalo limeacha watu zaidi ya 70 kufariki dunia.
FIFA imetoa amri kwa mamalaka ya soka  nchini Misri kuelezea kila kitu nini kilitokea katika mechi kati ya AL-Ahly na AL Masry jana jumatano.
Raisi wa FIFA Sep Blatter amemwandikia raisi wa FA ya Misri Samir Zaher.
“Leo ni siku nyeusi katika soka na lazima tuchukue hatua kuhakikisha tukio kama lile halijirudii tena. Soka ni mchezo wa nguvu zinazotumika kwa mazuri na lazima tusiruhusu zitumike vibaya kwa wale wenye mambo mabaya. Nasubiri habari zaidi kuhusu tukio lile.”
Maofisa wakubwa katika chama cha soka cha mji wa Port, ambapo ndipo tukio hilo lilipotokea , na viongozi wengine wa FA tayari wameshafukuzwa kazi.
Pia gavana wa mji wa Port ameshajiuzulu huku maofisa wawili wa juu wa usalama tayari wakiwa washasimamishwa na wapo chini ya ulinzi.
Siku 3 za maombelezo zimetangazwa na serikali. Pia kutakuwa na muda wa kukaa kimya katika mechi za robo fainali za African cup of Nations.

Thursday, February 2, 2012

MADEMU NA WAKE WA WANASOKA WENYE MVUTO DUNIANI

Hakuna ubishi Cristiano Ronaldo ni moto uwanjani na anatajwa kama mmoja ya   wachezaji bora wa dunia. Hivyo mchezaji bora wa dunia mtu ambaye ni nembo ya soka, hivyo anahitaji kuwa vitu bora kimojawapo ni mwanamke, huyu hapa mtot wa kirusi anaitwa Irina Shyk ni kweli kabisa anastahili kuwa demu wa mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo. Irina Shyk ndio anatufungia listi yetu ya wasichana ambao wana mvuto wamewahi ama wapo katika mahusiano na wanasoka.

Antonella Ruccozzo, binti wa kiaregentina ndiye aliuteka moyo wa mwanadamu ambaye inasemekana yupo tofauti na wacheza soka wote kwa uwezo wake wa kulisakata kabumbu. Huyu mtoto ni ndiye usingizi wa Lionel Messi - mchezaji bora wa dunia kwa sasa.


Anaitwa Aida Yespica, alikuwa galfriend wa mcheza soka Matteo Ferrari ambaye alizaa nae mtoto. Kwa sasa huu ni usiungizi wa moja ya viiungo bora duniani Mesut Ozil wa Real Madrid.


Ana mtoto mmoja na moja ya kiungo bora wa ulinzi kuwahi kutokea katika soka la karibuni Claude Makelele. Anaitwa Noemie Lenoir, unaambiwa si tu Makelel alikuwa anajua kuzuia mashambulizi ya uwanjani tu kwani huko Ufaransa mtoto anatingisha hatari lakini Makelele anawatuliza mapedeshee wote wanaomsumbua mama watoto wake.
Mke wa mchezaji wa Tottenham Hotspur Rafael Van Der Vaart ni hatari. Anaitwa Sylivie Van Der Vaart.

Moja kati wengi waliotekwa na mtoto wa Kireno Cristiano Ronaldo. Letizia Filippi moja ya washiriki wa Miss Italy mwaka 2007.

Anajulikana kama ex-wife wa Ashley Cole - Cherly Tweedy aka Cherly Cole. Muimbaji na mwandishi wa nyimbo wa kiingereza. 

Anaujua uwendazimu wote hata ambao kijana Wayne Rooney hatuoneshi uwanjani. Muite Coleen Rooney aka Mama Kai. Mwanamke wa kwanza katika maisha ya Rooney na ndio anayejua kumtuliza Rooney kuliko hata babu Fergie.


English actress amekuwa na mahusiano na wanasoka kadhaa. Alianza na Cristiano Ronaldo, na baadae akachumbiwa na Marcus Bent.

Iker Cassilas hajui tu kudaka mipira pia ana uwezo mkubwa wa kuwakamata watoto waziuri. Huyu Eva Gonzalez nae aliwahi kumpitia katika kipindi cha fainali za kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.

Alipigiwa kura kuwa"Mtangazaji mwenye mvuto kuliko wote na jarida la FHM, Carbonero anafahamika kwa tabia yake ya kupenda kumkiss in public boyfriend wake Iker Cassilas, katika kila mechi ya World Cup 2010. Pia katika fainali hizo alishutumiwa kwa kumkosesha umakini Cassilas katika mechi waliyofungwa na Uswiss. Mmmmh mtoto alivyo mzuri hivi mie hata simlaumu Cassilas.

Mwigizaji wa kike maarufu kwa TV Series maarufu duniani kwa sasa iitwayo NIKITA. Anaitwa Maggie Q demu wa zamani wa mchezaji bora wa Asia Hidetoshi Nakata.

Model huyu wa kibrazil pia yeye mwenyewe aliwahi kuwa mwanasoka. Yumo katika listi hii kwa sababu ya aliwahi kuolewa na mwanasoka bora wa dunia mara 3 Ronaldo De Lima na wana mtoto mmoja. Pia sasa ameolewa na mwanasoka wa kihispania David Aganz.


 Mwanamuziki maarufu kwa sasa ana date na Mhispania Gerard Pique, na ndio maana yupo katika listi hii. Mcolombia huyo anajulikana sana kwa kujua kucheza. Naamini atakuwa akimchezea Pique Pique kila usiku kabla hawajalala.

Model wa kibrazil Raica Oliveira ni binti mwingine aliyeingia katika mikono ya Ronaldo na kutumalizia kipaji cha El Phenomena wetu wa soka.

Demu wa zamani wa mchezaji wa Arsenal Freddie Ljunberg pia ni demu wa sasa wa mchezaji wa zamani wa Manchester United anayeichezea Sunderland Kieran Richardson. Ana miaka 20

Zamani alikuwa anajulikana kama Posh Spice aka Victoria Beckham, Mke wa David Beckham. Yeye na mumewe wanatajwa kama moja ya couples bora kabisa miongoni macelebs walio katika mahusiano. Ndoa yao ina watoto wanne mpaka sasa.

Popote utakapokutana na huyu mwanamke kama wewe ni mwanaume kamili ni lazima umtazame mara mbili. Anaitwa Yolanthe Cabau, mke wa kiungo wa Inter Milan Wesley Sneijder. 

Mrembo wa kiswidishi ameolewa na mmoja wanaosoka bora bora waliowahi kutokea katika historia ya soka, Luis Figo.

Usimuone Diego Forlan anapiga sana mashuti ya mbali ukajua yanakuja hivi hivi tu. Analelewa vizuri na mpenzi wake modo wa Kiargentina Zaira Nara.


Huyu Miss England 2004 na Miss Great Britain 2006, amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanasoka kama vile Teddy Sherigham, Marcus Bent na Jermain Defoe. Aliporwa taji lake la Miss Great Britain mara baada ya picha zake za uchi za jarida la Playboy kutoka, pia aligundulika alikuwa na mahusaino na moja ya majaji wa Miss Great Britain Teddy Sheringham.Ogaaaaadrx9drdpysmv55h1ohaf6llpnld9iwmkwesohhwf2qjfhq1wik67z-izhou9jrf7-nte1wbdeut-bvjmwmxyam1t1uj_bmb_affd96orkwrppgdgda3dc_display_image
Demu wa high school wa Kaka, Carolina Celico ni mzuri hatari. Japokuwa ni vigumu kwa wanasoka au watu maarufu kudumu na mwanamke mmoja kwa muda mrefu lakini mlokole Kaka na utajiri pamoja na umaarufu wote alionao hapa ndio kafika. Wameshaona na wana mtoto mmoja.

Mke wa mwanasoka Joe Cole na vingi vya kui-offer camera. Uzuri wake ni hatari na ndio maana haishangazi kuona Cole akiwa kaamua kumueka ndani.Anajulikana mno kwa mahusiano yake yaliyotingisha mno ndoa ya John Terry - pia Vanessa Perroncel ndiye aliyeleta ugomvi kati ya Wayne Bridge . Ni vigumu kumlaumu Terry kwa uzuri alionao huyu binti.

English model na mwandishi wa makala za urembo katika gazeti la Daily Mirror ndiye mwanamke aliyeuteka moyo wa The Fantastic Captain Steven Gerrard.Mrembo huyu aliyezaliwa Spain ni moja kati ya wanawake wengi wanaomjua Cristiano Ronaldo akitoka kuamka anakuwa na sura gani. Nererida Gallardo pia amewahi kutekwa na Sergio Ramos.
Huyu ni mrembo ambaye alishawahi kushinda tuzo ya mwanamke mzuri kuliko wote nchini Nigeria, ameolewa na mchezaji wa Fenerbahce Joseph Yobo pia ni mtoto wa kufikia mchezaji John Fashanu.

Anajulikana kwa mahusiano yake yaliyowagonganisha wachezaji wa England Peter Crouch na Shaun Wright Philips. Lauren Pope ni mjasiliamari anayefanya kazi kama DJ katika moja ya kumbi huko jijini London.

Huyu ni mke wa kiungo wa timu ya taifa ya Argentina Martin Demichelis - anaitwa Evangelina Anderson.

Model huyu wa kibrazil anaipenda timu yake ya taifa.
Warner alikuwa na mahusiano na Ronaldo de lima mpaka 1999. Baadae akaolewa na golikipa wa taifa hilo Julio Ceaser na sasa wana watoto wawili.


Pamoja na umalya wake lakini huyu ndio mwanamke aliyeweza kumtuliza Kapteni John Terry. Tayari ndoa imeshajibu na ipo imara japokuwa imekuwa ikiandamwa naskendo za umalaya wa mumewe


Carlos Tevez anajulikana kwa kujua kulisakata soka, lakini muaregentina huyo pia ni hatari kwa warembo wakali. Natalia Fassi ni mrembo mwingine aliyeiletea kashikashi ndoa ya Carlitos.

Mrembo huyo Mariana Paesanialishea chumba kimoja na Carlos Tevez kipindi mke wa Carlitos akiwa anamlea mtoto wao mchanga.