Search This Blog

Saturday, June 30, 2012

OFFICIAL: LAURENT BLANC AJIUZULU KUIFUNDISHA UFARANSA

CHECKING OUT ... Laurent Blanc
Laurent Blanc amejiuzulu rasmi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Taarifa zilianza kusambaa mapema leo kwamba kocha huyo wa zamani wa Bordeaux hatoendelea na kazi ya bosi wa benchi la ufundi wa Les Bleus baada ya mktano wake na viongozi wa Shirikisho la soka la Ufaransa.

FFF baadae wakathibitisha kwamba kocha huyo mwenye miaka 46 hatoengeza mkataba mpya kufuatiwa Ufaransa kuondolewa kwenye Euro 2012 kwa kufungwa 2-0 na Spain kwenye hatua ya robo fainali.

JERRY TEGETE APIGA BAO MBILI: YANGA IKIWAFUNGA WAGANDA EXPRESS 2-1


Mabingwa watetezi wa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (KAGAME) timu ya Young Africans Sports Club imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya Mabingwa wa ligi kuu ya Uganda timu ya Express FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans iiliyotimia fursa hiyo kuwatambulisha wachezaji wapya iliyowasajili katika msimu mpya wa ligi kuu ya VPL na mashindano ya kimataifa Kagame,lianza mchezo kwa kasi na katika dakika ya 1 ya mchezo, mshambuliaji aliyesajiliwa kutokea Moro United Saimon Msuva alipiga shuti kali liliotoka sentimeta chache ya lango la Express.
Dakika ya 3 ya mchezo mshambuliaji Jeryson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza, mara baada ya kumalizia krosi safi iliyopigwa na mshambuliaji mpya mwenye misuli kutoka Mtibwa Sugar Said Bahanunzi.
Huku ikicheza soka safi nala kuvutia, Young Africans iliendelea kulishambulia lango la Express muda wote wa mchezo huku eneo la kiungo likimilikiwa vizuri na chipukizi Frank Domayo aliyesajiliwa kutoka JKT Ruvu, Chuji, Nizar Khalfan.
Jeyson Tegete aliendelea kuwa mwiba kwa waganda hao, kwani katika ya 19 ya mchezo, Tegete aliipatia tena Young Africans bao la pili akimalizia krosi safi ya Said Bahanunzi aliyeonekana kuisumbua gome ya Express.
Mpaka mpira unakwenda mapumziko, Young Africans ilikuwa mbele kwa mabao 2- 0.
Kipindi cha pilik kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo iliwapumzisha Kelvin Yondan, Oscar Joshua, Jeryson Tegete, Nizar Khalfan, Said Bahanunzi na Saimon Msuva na nafsai zao kuchukuliwa na Ladisalus Mbogo, Stephano Mwasika, Hamis Kiiza, Omega Seme, Idrisa Rashid na Shamte Ally.
Mabadiliko hayo yaliipa uhai timu ya Express kwani ilianza kulishambulia lango la Young Africans na katika dakika ya 73 ilipata bao la kufutia machozi, baada ya kupiga faulo iliyowachanganya walinzi wa Young Africans na kukuta wakijifunga.
Mpaka dakika 90 za mwamuzi Oden Mbaga zinamalizika Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi wa wageni Express kutoka Uganda.
Young Africans iliwakilishwa na:
1.Barthez, 2.Juma Abdul, 3.Oscar/Mwasika, 4.Cannavaro, 5.Yondan/Mbogo, 6.Chuji, 7.Nizar/Shamte, 8.Frank Domayo, 9.Said Bahanunzi/Omega, 10.Tegete/Kiiza, 11.Msuva/Idrisa

EPIQ BONGO STAR SEARCH YATIMBA LINDI LEOMajaji wa EBSS - Master J, Madam Rita na Salama J wakipozi kwa camera wakati wa kufanyika kwa auditions za kutafuta superstar atakayewakilisha Lindi kwenye Epiq Bongo Star Search 2012.

Master J akiwa makini kumsikiliza mshiriki wa auditions za EBBS Lindi.

Anajaribu bahati yake - mshiriki akicharaza gitaa

Wananchi wa mkoa wa Lindi walijitokeza wengi kuja kushiriki katika EBSS 2012.


YANGA WAFANYA DUA 'HITMA" YA KUOMBEA WALIOTANGULIA AKHERA

Waungwana baada ya kisomo wakisubiri sadaka

Sheikh Mussa kulia, kushoto ni Katibu wake Almasi lailly Mussa na nyuma yao ni mwanachama wa Yanga, Mustafa Mohamed, Katibu wa Tawi la Kurasini

PHOTO CREDITS: Bongostaz.blogspot.com

Madega kulia, akiwa na Sanga kushoto kwake

Waungwana wakisubiri sadaka baada ya dua

Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa kulia, Madega na Sanga

Sheikh Mussa katikati, kulia Juma Mnonji mwanachama wa Simba, na kushoto Katibu wake, Almasi

Waungwana baada ya dua wakisubiri sadaka 

Akina mama wakichambua mchele


Akina mama wakichambua mchele

Eneo la kusomea ibada ya hitima
Waungwana tayari kwa kisomo cha hitima


Mwanachama maarufu wa Simba, Mzee Juma Mnonji wa tatu kutoka kushoto akiwa kwenye hitima kama mmoja wa wageni waalikwa
Masufuria jikoni


Jamaa anatengeneza viungo
Ng'ombe anaiva

PHOTOC CREDITS: BONGOSTAZ BLOG

ANDRE VILLAS BOAS KUZIKOSA ZAIDI YA BILLIONI 20 ZA CHELSEA IKIWA ATAKUWA KOCHA WA TOTTENHAM WIKI IJAYO

Andre Villas Boas atapoteza kiasi kinachokaribia £11million wakati atakapotangazwa kuwa kocha mpya wa Tottenham wiki ijayo.

Mreno huyo, 34, hakupokea fidia yote kwa pamoja ya kuvunjika kwa mataba wake alipofukuzwa na Chelsea mwezi wa tatu mwaka huu, ikiwa ni miezi nane tu tangu aliposainishwa mkataba wa miaka 3.

Badala yake, Chelsea walikubaliana na AVB kuendelea kumlipa msharaha wake wa kawaida wa £100,000 kwa wiki mpaka pale atakapopata kazi mpya.

Mpaka sasa ameshapokea mshara wa miezi mitatu tangu kuanza mpaka mwishoni mwa mwezi huu.

Lakini ikiwa atakuwa kocha wa bosi wa White Hart Lane, Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ataachana na mpango wa kumlipa mshahara AVB, na kocha huyo atapoteza mkwanja wa malipo ya miezi 25 iliyobaki yenye thamani ya £10.8million.

Ripoti kutoka nchini Ureno zinasema kwamba mazungumzo kati ya AVB na Spurs yamekwamia kwenye suala la fedha.

Friday, June 29, 2012

BAADA YA KUTOLEWA EURO: ROONEY NA ASHLEY COLE NI BATA TU NDANI LOS ANGELESHIVI NDIVYO MAGAZETI YA UJERUMANI YALIVYOWAKEJELI WAITALIA JANA MCHANA - KABLA YA BALOTELLI HAWAJAFUNGA MIDOMO


Kwa kuangalia rekodi yao nzuri kwenye Euro 2012, watu wengi waliamini kwamba Ujerumani wangekuwa na kazi rahisi ya kuwaondoa waitaliano kwenye mchezo wa nusu fainali wa Euro.

Mario Balotelli akawafanya watu wengi jana kukosea kwenye utabiri wao na sasa Wajerumani na mashabiki wao wanajiuliza nini hasa kilichotokea.
(Shukrani kwa wachezaji wa Bayern kwenye kikosi angalau wanaweza kuwaonyesha wenzao namna ya kuugulia maumivu ya kupoteza ubngwa ambao takribani nusu ya washabiki wa mpira duniani tulikuwa tunaamini wangeweza kuuchukua safari hii.)

Kwa upande mwingine gazeti la kila siku la Bild la Ujerumani nalo liliingia mkenge kwa kuiamini sana timu yao taifa dhidi ya Italy - walichapisha picha kubwa kwenye website yao ikionyesha ndege kubwa ya Italy ikiwa imewabeba wachezaji wa Azzuri tena wakiwa wamepangwa kwa formation kabisa - wakielekea nyumbani baada ya kutolewa kwenye mashindano na Ujerumani - na wakaandika maneno ya "Tunawatakia safari njema ya kurudi nyumbani."

Kwa sababu wazijuazo wenyewe - ile picha ya waitaliano wakiwa mfumo wa kiuchezaji wakirudi nyumbani kwenye ndege imetolewa kwenye mtandao wa Bild.

Bild halikuwa gazeti pekee la kijeumani lilopata aibu kwa matokeo ya jana usiku. Hamburger Morgen Post - wenyewe walichapisha picha kubwa kwenye ukurasa wao mbele wa gazeti - wakiweka Pizza ya pepperoni ya kiitalia huku ndani yake zikionekana picha za wachezaji wa Italia.

Chini ya picha ile wakaandika maneno ya kejeli kwa Waitaliano yaliyosomeka, "Mwisho wa Pizza" kama kichwa cha habari kikuu huku vkichwa cha habari kidogo kikiandika - "Sababu 11 kwanini tutawaondoa Waitalia mashindanoni leo usiku"

Lakini kwa bahati mbaya sana kwa gazeti hili la kijerumani kitu pekee walichokuala jana suiku ni maneno yao - shukrani kwa Balotelli.

BAADA YA KUSHINDWA KUPIGA PENATI - CRISTIANO RONALDO AACHWA NA NDEGE YA TIMU YA TAIFA KURUDI URENO

Cristiano Ronaldo alilzamika kukaa kwa masaa kadhaa nchini Ukraine baada ya kuikosa ndege ya Ureno kuelekea nyumbani. Nahodha huyo wa timu na mfungaji bora wa kikosi hicho, ambaye mapema juzi alikosa nafasi ya kupiga penati kwenye mchezo wa nusu fainali ya Euro 2012 dhidi ya Spain ambao walikamilisha kufunga penati zao za ushindi kabla ya Ronaldo kuifikia zamu yake - aliachwa akisikitika na kufura kwa hasira baada ya ndege kuondoka na kumuacha.

"Nilikuwa naongea na muhusika wa upangaji wa safari. Nikamwambia nataka kukaa nyuma kabisa kwenye ndege akanikubalia then nikaenda kwenye restauraunts kuchukua vyakula vyangu nilivyonunua na yeye akaiachia ndege iondoke bila mimi. Haikuwa haki."

Ingawa kocha Ureno aligundua kutokuwepo kwa Ronaldo kwenye ndege baada ya kutua Lisbon, nahodha wa ndege, Ted Mendes, hakuwa tayari kupokea lawama za kuachwa kwa Ronaldo.

"Ikiwa Ronaldo alitaka kuwemo ndani ya ndege alipaswa kuingia mapema kwenye ndege, lakin alichelewa mwenyewe."

Lakini hatimaye Cristiano Ronaldo alipata ndege ambayo ilimpeleka nyumbani kwao Ureno huku akijuta kwa kwenda kufuata misosi yake iliyomfanya achelewe ndege.

MUIGIZAJI AFANYA UZINDUZI WA FILAMU YAKE MPYA KWA KUTOA MSAADA KWA YATIMAMsanii wa filamu nchini, Vicent Kigosi 'Ray' akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es Salaam jana kwa mlezi wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni, Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho, kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage. Picha na Mpiga picha Wetu

Vicent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kugawa vyakula…


HII LISTI YA WACHEZAJI 13 WALIOACHWA NA YANGA: KADO, GODFREY BONNY, MBEGA, ASAMOAH, MWAPE NA MROPE NJE

Klabu ya Young Africans Sports Club imewasilisha jumla ya majina 13 ya wachezaji ambao imeachana nao mwishoni mwa msimu ulioisha kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.
Wachezaji waliomaliza mikataba yao ni:
1.Godfrey Bonny
2.Kiggi Makasi
3.Abuu Ubwa
4.Bakari Mbega
5.Chacha Marwa
6.Atif Amour

Wachezaji ambao klabu imeamua kuvunja nao mikataba ni:
1.Davies Mwape
2.Kenneth Asamoah
3.Julius Mrope
4.Iddi Mbaga
5.Zuberi Ubwa
6.Pius Kisambale
NB: Shaban Hassan Kado ametolewa kwa mkopo kwenda timu ya Mtibwa Sugar

COASTAL UNION YASAJILI JEMBE LINGINE KUTOKA JKT OLJORO

Klabu ya Coastal Union imeendeleza balaa kwenye usajili, baada ya juzi kumsainisha kiungo Pius Kisambale kutoka Yanga, leo hii hii klabu hiyo imemsainisha mchezaji Othman Omary kutoka timu ya Taifa ya Zanzibar aliyekuwa akiichezea klabu ya wanajeshi ya JKT Oljoro.

KAGAME CUP: YANGA KUFUNGUA MASHINDANO NA ATLETICO YA BURUNDI - SIMBA NA URA


Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye kulia akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za TFF, mchana huu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
MABINGWA watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame watafungua dimba na Atletico ya Burundi katika mchezo wa Kundi C wa michuano hiyo, Julai 14, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliowekwa Kundi A, wataanza na URA ya Uganda Julai 16, kwenye Uwanja huo huo.
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano hiyo, Azam FC wao wataanza na Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa Chamazi, Julai 15.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana huu, ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam kwamba, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itashiriki kama timu mualikwa.
Aidha, habari za kusikitisha ni kwamba, Musonye amesema Sudan, Ethiopia, Eritrea na Somalia hazitaleta wawakilishi wao kwa sababu mbalimbali.
Wakati Ethiopia ligi yao inaanza wiki hii, Sudan wawakilishi wao wapo kwenye michuano ya Afrika na wameshindwa kuteua timu mbadala, Somalia wawakilishi wao Elman wamebadilisha uongozi, hivyo bado hawajajipanga na Eritrea kutokana na desturi ya wachezaji wao kuzamia kila wanapokuja kwenye mashindano, wameondolewa.
“Wameondolewa, kwa sababu mbili, kwanza nchi yao imeomba ipewe muda kulifanyia kazi sual hilo, na sisi pia (CECAFA) tunalitafutia ufumbuzi,”alisema Musonye.  
Lakini Musonye amekiri kitendo cha kuyatoa mashindano hayo mwanzoni mwa mwaka hadi katikati ya mwaka kumechangia baadhi ya timu kutoshiriki na amesema tayari amewasilisha pendekezo kwenye Mkutano Mkuu, mashindano yarejee kufanyika mwanzoni mwa mwaka kama ilivyokuwa awali.
Kuhusu mechi ya ufunguzi ya Simba kuchezwa Julai 16, ambayo itakuwa Jumatatu badala ya Jumapili, Musonye alisema kwamba imetokana na kwamba Julai 15, Uwanja wa Taifa kutakuwa na fainali za Copa Coca Cola, ambayo maandalizi yake yote yamekamilika.
Yanga ndiye bingwa mtetezi wa mashindano, baada ya kuifunga Simba SC katika fainali mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Source:bongostaz.blogspot.com

ITS SUPER MARIO BALOTELLI: AWATANDIKA GOLI WAJERUMANI NA KUIPELEKA ITALY FINALI YA EURO DHIDI YA SPAIN


Germany vs Italy 1-2 All Goals & highlights UEFA... by kofiswag

OKWI KWENDA ITALIA TAREHE 4 JULAI KUFANYA MAZUNGUMZO YA KUJIUNGA NA PARMA

Hayawi hayawi sasa yanaeleka kutimia.

Kumbuka siku chache zilizopita nilitoa taarifa juu ya mshambuliaji Emmanuel Okwi kuwa lulu kwenye soko la usajili, akitakiwa na vilabu vikubwa vya South Africa Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns huku kukiwa na klabu inayoshirki ligi kuu ya Italia Serie A nayo ikimuwania.

Sasa zilizothibitishwa na uongozi wa Simba ni kwamba mnamo tarehe nne mwezi ujao, Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda na mabingwa wa Tanzania bara Simba anatarajiwa kukwea pipa kuelekea nchini Italia kufanya mazungumzo ya klabu ya Parma kwa ajili kuweza kujiunga nayo kwenye msimu ujao.

Ikiwa Okwi atafanikiwa kufikia makubaliano na Parma na kuweza kujiunga nayo Simba inategemea kuvuna kiasi cha fedha kisichopungua billioni mbili mpaka nne kama ada ya uhamisho wa Okwi.

Kila kheri la Okwi.

Thursday, June 28, 2012

KATUNI TIME!

FIESTA SOCCER BONANZA SAFARI HII KUANZIA MKOANI MBEYA!

Lile bonanza lililoteka nyoyo za mashabiki wa vilabu mbali mbali vya soka barani ulaya la Fiesta Soccer Bonanza linataraji kuanza mwishoni mwa juma hili pale Mkoani Mbeya.

Bonanza hilo ambalo mwaka huu litashirikisha mashabiki wa vilabu vya MANCHESTER CITY,MANCHESTER UTD,CHELSEA,ARSENAL NA LIVERPOOL toka nchini England,kutoka nchini Hispania mashabiki wa vilabu vya REAL MADRID na FC BARCELONA pia watashiriki bonanza hili litakalofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Uhasibu hapo siku ya Jumapili tarehe 1/7/2012.


KUTOKA MAKTABA: mwaka jana mabingwa wa Fiesta Soccer Bonanza walikua ni mashabiki wa klabu ya INTER MILAN ya nchini Italia. JE NANI ATAIBUKA KIDEDEA WA FIESTA SOCCER BONANZA MWAKA WA 2012 HUKO MOANI MBEYA ?
Mchezaji Mwaikimba (kushoto) wa timu ya mashabiki wa Inter Milan akipokea kombe la ushindi kutoka kwa meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo, mara baada ya mchezo wa fainali kumalizika katika viwanja vya chuo cha uhasibu (TIA) jijini Mbeya leo jioni.
Tamasha la Mwendelezo wa Dhahabu na Serengeti Fiesta Soccer Bonanza limefanyika leo jijini humo, kwenye uwanja wa Chuo cha Uhasibu (TIA), tamasha lilikuwa limechagamka sana na mashabiki wamejitokeza kwa wingi na kumekuwa na upinzani mkubwa kati ya timu za mashabiki zinazokutana kwenye uwanja huo. Dalili zilionyesha mapema kwamba huenda tamasha hilo lingevunja rekodi kwa matamasha yaliotangulia katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma na sasa Mjini Mbeya jambo ambalo limedhihirika mara baada ya kuhudhuriwa na mashabiki wengi tena waliochangamka sana.
Wachezaji wa timu ya mashabiki wa klabu ya Inter Milan ya Italia wakiwa katika picha ya pamoja na kombe lao mara baada ya kuibuka mabingwa wa tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza

Wachezaji wa timu ya Inter Milan na Real wakiwania mpira wakati wa mchezo wa fainali katika tamasha la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza.
Umati Mkubwa umehudhuria katika tamasha hilo ambapo kulikuwa na kila shamrashamara za mashabiki wa vilabu hivy kutoka Ulaya.
Mchezaji wa timu ya mashabiki wa klabu ya Shafii Dauda Inter Milan ya Italia (kulia) akichuana na mchezaji wa mashabiki wa klabu ya Real Madrid ya Hispania,
Hapa nilikua nikitoa maelekezo, kwa wachezaji wa timu za mashabiki wa Real Madrid na Inter Milan kabla ya kuanza kwa mchezo wao.
Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo akiwaelekeza jambo mashabiki wa timu ya Liverpool ya Uingereza, wakati walipokuwa wakipiga picha kabla ya kuanza kwa bonanza hilo.

Mashabiki wa timu ya Inter MilaN wakati wa kupiga na timu yao.
Hawa ni mashabiki wa timu ya mashabiki wa Manchester United kabla ya kuanza bonanza hilo.
Hii ni timu ya mashabiki wa klabu ya Arsenal ya Uingereza
Hii ni timu ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid ya Uhispania.
Hii ni timu ya mashabiki wa klabu ya Chealsea ya Uingereza wakiwa tayari kwa gemu lao.
Hii ni timu ya mashabiki wa klabu ya Barcelona ya Hispania kama kawa.
Hapa timu zote zikishiriki maandamano kutoka katika stendi ya mabasi ya Kabwe Mwanjelwa mpaka viwanja vya chuo cha Uhasibu (TIA).
Kikundi cha matarumbeta kilichoongoza mandamano hayo kutoka mwamelwa mpaka eneo la Mafiati mjini Mbeya.
Mashabiki wa Inter Milan wakishoo Love kwa staili ya aina yake.
Wazee wa Emirates mjini Mbeya nao walikuwepo kama unavyowaona katika picha.
Mashabiki wa timu mbalimbali wakishagilia wakati wa maandamano ambayo yalianzia katika kituo cha mabasi ya Kabwe Mwanjelwa na kuishia katika uwanja wa Chuo cha Uhasibu Mbeya (TIA)