Search This Blog

Saturday, March 24, 2012

MAN CITY WATOA SARE, ARSENAL WASHINDA, CHELSEA WATOKA SARE NA SPURS - TOP 4 HATIHATI


Saturday 24 March 2012
17:30Stoke1 - 1Man CityBritannia Stadium
15:00Arsenal3 - 0Aston VillaEmirates Stadium
15:00Bolton2 - 1BlackburnReebok Stadium
15:00Liverpool1 - 2WiganAnfield
15:00Norwich2 - 1WolvesCarrow Road
15:00Sunderland3 - 1QPRStadium of Light
15:00Swansea0 - 2EvertonLiberty Stadium
12:45Chelsea0 - 0TottenhamStamford Bridge

MESSI NAE AVUNJA REKODI YA RONALDO DE LIMA BARCELONA

Lionel Messi nae ameendelea na uvunjifu wa rekodi katika klabu yake ya Barcelona, baada ya hivi leo kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi katika msimu mmoja wa La Liga, kufuatia kutia kambani katika mechi dhidi ya Real Mollorca.

Messi amevunja rekodi ya Ronaldo De Lima aliyefunga magoli 34 katika msimu wa 1996-97, kwa sababu goli lake la leo hii linamaanisha amefikisha idadi ya magoli 35 ya la liga pekee msimu huu.

Messi sasa anaikimbiza rekodi ya Cristiano Ronaldo aliyoiweka msimu uliopita kwa kufunga magoli 40 ndani ya msimu mmoja na kumfanya awe mfungaji bora wa muda wote wa ligi katika kipindi cha msimu.

CRISTIANO RONALDO AFIKISHA MAGOLI 101 KWENYE LA LIGA- AVUNJA REKODI YA PUSKAS

 Cristiano Ronaldo amekuwa ndio mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufikisha magoli 101 kwenye La Liga chini ya mechi 115, kufuatia kufunga goli katika mechi ya usiku huu dhidi Real Sociedad.

Mreno huyo sasa ameweka rekodi mpya katika klabu hiyo baada ya kufikisha idadi hiyo ya magoli baada ya kucheza mechi 92 tu.

Rekodi ya mchezaji aliyefikisha magoli 100 ya La liga kwa haraka ilikuwa inashikiliwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Ferenc Puskas ambaye yeye alicheza mechi 115 mpaka kufikisha idadi hiyo ya magoli 100.

Goli la leo la Ronaldo ni la 45 katika msimu kuifungia Real Madrid na 34 katika La liga akimfikia Lione Messi mwenye 34.

POULSEN YUPO TAYARI KUACHIA NGAZI STARS

Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Jan Borge Poulsen amesema atakuwa tayari kujiuzulu nafasi yake ya kufundisha timu hiyo, iwapo ataombwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza mjini Dar es Salaam, Poulsen alisema kama TFF itampa taarifa ya kumtaka kuachia ngazi, basi atafanya hivyo mara moja.
“Mimi siwezi kulazimisha kufanya kazi Tanzania kama sitakiwi, ila ukiona bado nipo basi fahamu kwamba mwajiri wangu ananihitaji. Siku wakiamua niondoke, basi nitafanya hivyo mara moja," alisema Poulsen na kuongeza:
“Mimi ni mwajiriwa wa TFF, siyo Kamati ya Utendaji na TFF haijanipa barua ya kuacha kazi, kwa mantiki hiyo mimi bado ni mwajiriwa halali wa TFF.”
Kamati ya Utendaji ilitaka kocha huyo aondoke na moja ya sababu ni kushindwa kuleta mabadiliko katika soka la Tanzania badala yake amekuwa akichangia kiwango cha Tanzania kushuka.
Akijibu tuhuma hizo Poulsen, alisema kamwe hawezi kufanya kazi kwa matakwa ya baadhi ya watu, na kwamba yeye ndiye kocha anafahamu saikolojia ya wachezaji pamoja na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.
“Tatizo la Tanzania ni suala la Samata kutoitwa kwenye kikosi cha Stars, hilo mimi halinipi shida ila ukweli ni kwamba siwezi kuacha kazi kwa sababu ya matakwa ya baadhi ya watu,” alifafanua Poulsen.
Poulsen  alirithi mikoba ya Mbrazil, Marcio Maximo mwaka juzi na tangu kuwapo kwake kazini soka ya Tanzania imekuwa ikishuka siku hadi siku, kiasi cha Watanzania kumkumbuka Mbrazil aliyeipeleka Stars katika fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

Friday, March 23, 2012

KUTOKA KUOKOA JAHAZI MPAKA KULIZAMISHA - HAMU YA HARRY REDKNAPP KUIFUNDISHA ENGLAND INAVYOHARIBU MSIMU WA TOTENHAM HOTSPURS.

Mwanaume ambaye anatajwa kuwa manager ajaye wa timu ya taifa anahitaji kuweka jicho lake kwenye mpira na kuongeza umakini katika kuhakikisha Spurs hawaendelei kufanya vibaya katika mechi zilizobaki ili kuweza kugombania nafasi ya kwenda champions league.

Ikiwa Tottenham wakifeli kumaliza katika top four ya premier league msimu huu, lawama hazitokwenda kwa kitu kinachoitwa 'Bahati mbaya'.

Baada ya miezi mitatu katika top 3, Spurs wameshuka chini mpaka nafasi ya nne Jumatano iliyopita walipotoka suluhu na Stoke, wakiendelea na performance yao kubwa  baada ya kupata pointi moja kutoka katika michezo yao minne iliyopita.

Timu ambayo hapo mwanzo ilionekana kuwa itakuwa na uhakika wa kumaliza na kupta nafasi ya kushiriki Champions league  kwa sasa wana changamoto moto kubwa ya kupigana na mahasimu wao wawili wa London, Arsenal na Chelsea, ili kuweza kuepuka na aibu mwishoni mwa msimu ambao ulitoa matumaini makubwa kwa wapenzi wao.

Jumamosi hii, Spurs wataendelea na mbio ngumu wakienda pale Stamford Bridge, uwanja ambao hawajawahi kushinda tangu 1990. Ikiwa Chelsea watashinda, pengo la pointi kati yao na The Blues litakuwa pointi 2 na Harry Redknapp ataanza kulisikia joto la benchi la ufundi.

Haihitaji mwanasayansi wa hali juu kuweza kutambua hili, suala la ukocha wa timu ya taifa, nafasi anayohusishwa nayo Harry Redknapp, imeanza kuharibu akili na umakini kocha huyu kupelekea Tottenham kuanza kupata madhara juu ya suala hilo.

Tnagu Fabio Capello alipokiuzulu kama kocha wa England, Spurs wamepata wastani wa pointi 0.8 kwa mchezo. Kabla ya hapo Spurs walikuwa na wastani wa pointi 2.1 kwa mechi moja.

The North Londoners wameshinda mchezo mmoja tu tangu Capello ajiuzulu.

Wiki iliyopita siri ilitoka kutoka katika base ya mazoezi ya Tottenham in Chigwell kwamba Redknapp ameamua kwamba atachukua nafasi ya ukocha wa England kiangazi kijacho, juku Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy akipoteza matumaini ya kumshawishi Harry mwenye miaka 65 kubaki White Hart Lane.

Wakati Spurs wakiwa bado hawajafuatwa rasmi na FA, hali ya kutokueleweka ndani ya klabu inaonekana imewachanganya wachezaji, huku Harry Redknapp mwenyewe akionekana kushindwa kuhumili joto la kuwania nafasi ya ukocha England, hivyo kupoteza umakini.

Redknapp ni chaguo la nchi kuiongoza England kwenye EURO 2012 lakini Harry anahatarisha mafanikio ya kazi nzuri aliyoifanya tangu alipojiunga na Spurs October 2008 wakati klabu hiyo ilipokaa chini kabisa ya msimamo wa ligi.

Iwe kazi ya ukocha wa England au sio, Redknapp lazima akubali lawama nyingi kwa kuchangia kushuka vibaya kwa Tottenham.

Pia kukosekana kwa wachezaji wao muhimu kutokana na majeruhi, akiwemo Aaron Lenon na Emmanuel Adebayor pia kumechangia, lakini amefanya maamuzi ya kushangaza sana wiki kadhaa za hivi karibuni.

Timu imekosa balance, shape na mbinu. Gareth Bale amekuwa akiruhusiwa kuzunguka popote dimbani, Luka Modric amekuwa akipangwa pembeni, na Redknapp akiacha safu ya kiungo nyepesi kwa kuwapanga washambuliaji wawili dhidi ya timu ngumu kama Arsenal, Everton na Manchester United.

Wanashindwa kupasiana vizuri, safu ya ulinzi inaonekana kuparanganyika na hasa wanaposhindwa kuzuia set-pieces, kitu ambacho mazoezini whawajifunzi na hata wachezaji wamekuwa wakilalamika kuhusu hilo kwa pembeni pembeni.

Redkanpp na manager mzuri sana wakati timu ikiwa inacheza vizuri, lakini mara nyingi maswali yamekuwa yakizuka kuhusu namna anavyo-handle mambo wakati timu inapoanza kucheza hovyo. Walishinda mechi zao 2 tu kati ya 12 za mwisho mwishoni mwa msimu uliopita, matokeo ambayo mwisho wa siku yaliwakosesha nafasi ya kushiriki champions league.

Wakati Sir Alex Ferguson akifundisha na kupanga mipango ya kikosi chake cha Manchester United ku-peak katika hatua za mwisho wa ligi, inaonekana ni tofauti sana na kwa Redknapp. Manager wa Spurs anasisitiza kuchezesha kikosi chake cha kwanza kila wiki, kwa maana wachezaji kama Modric na Scott Parker wanakuwa wamechoka ligi ikiwa inaingia katika hatua za mwisho za msimu.

Kukosea kwake katika kufanya rotation(mzunguko) pia unachangia sana kuwafanya wachezaji wake muhimu kuumia ama kuchoka msimu unapokuwa kwenye crucial moments.

Namna gani Redknapp anavyojuta, kwa mfano, maamuzi yake ya kumuachia Steven Pienaar kuondoka kwa mkopo kwenda Everton in Jnauary. Kiungo huyo wa Afrika ya Kusini angeweza kutoa msaada mkubwa na kubalance timu  lakini alilazimisha kuondoka katika dirisha dogo kwa sababau alikuwa anaudhiwa na ukosefu wa namba ndani ya kikosi cha Spurs.
Matokeo ya mwisho wameanza kupoteza points muhimu na Redknapp ameibuka na visingizio eti Spurs wamepewa mategemeo makubwa kuliko uwezo wao wakati hivi karibuni alikuwa akizungumzia kuchukua ubingwa.

Ama kwa hakika ana asilimia 70 za kuwa kiongozi wa benchi la ufundi la England in Euro 2012 - lakini kwa sasa Redknapp ana kazi ya kumaliza vizuri muda wake wa kukaa White Hart Lane kwa kuisadia Spurs kupata nafasi ndani ya top four.

EXCLUSIVE: SIMBA YAMSAJILI MWANAJESHI NA MCHEZAJI ANAYELIPWA FEDHA NYINGI KULIKO WOTE UGANDA NA KENYA.


Klabu ya Simba imemsajili kiungo Musa Mudde kutoka klabu ya Sofa paka ya Kenya.
Musa Mudde ni raia wa Uganda na ndio mchezaji aliyekuwa akishikilia rekodi ya kuwa mwanasoka anayelipwa mkwanja mrefu kuliko wote katika ligi kuu ya Kenya na Uganda.
Musa Mudde ameingia mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba, na ataanza kuvaa jezi nyeupe na nyekundu kuanzia msimu ujao.
 Kiungo huyo ambaye  ana miaka 22 alianza kuichezea klabu ya jeshi la UPDF - Simba FC ya nchini kwa o Uganda, kabla ya kuhamia nchini Kenya katika uhamisho ulioleta mtafaruku mkubwa.
Akiwa kama mwajiriwa wa jeshi alikuwa haruhusiwi kwenda kucheza soka la kulipwa sehemu nyingine nje ya jeshi, ilibidi mpaka akaombe ruhusa kwa mkuu wa majeshi wa Uganda na amiri jeshi mkuu wan chi Raisi Yoweri Museven ndipo alipokubaliwa kwenda kucheza nchini Kenya, ambapo ndipo alipokuwa mchezaji anayekusanya mkwanja mrefu kuliko mchezaji yoyote ndani ya Uganda ama Kenya, akilipwa kiasi cha shilingi za Kenya 83,000 kwa mwezi.
Mudde sasa anaingia Simba akiwa kama replacement ya kiungo Jerry Santo