Search This Blog

Saturday, July 6, 2013

PAULINHO ATAMBULISHWA RASMI TOTTENHAM HOTSPUR - EKOTTO ADAI HAMJUI KABISA

 Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Paulinho leo ametambulishwa na Tottenham baada ya kukimilisha uhamisho wa paundi millioni 17 Corinthians ya Brazil. Lakini wakati mchezaji huyo akitambulishwa mchezaji mwenzie wa timu hiyo beki wa kimataifa wa Cameroon
Assou-Ekotto ameiambia Goal.com: ' Simfahamu hata alivyo. Simjui, mie sifuatilii habari za namna hiyo. Mfano mzuri ni miaka mitatu iliyopita, Rafael van der Vaart alikuwa ndio amekuja mazoezini mara ya kwanza, nilimsalimia lakini sikuwa najua kama yeye ndio Rafael van der Vaart."


MARIO GOTZE, GOMEZ NA KIRCHHOFF WAPIGWA FAINI NA BAYERN MUNICH KWA KUVAA MAVAZI YA NIKE



Bayern Munich imewapiga faini Mario Gomez, Mario Gotze na Jan Kirchhoff kwa kuvaa mavazi ya Nike wakati wa matukio rasmi ya FC Bayern - hivyo kuleta mtafaruku na wadhamini wa klabu Adidas, amesema afisa wa habari wa klabu hiyo Markus Horwick.

Klabu hiyo ya Bundesliga ina sheria ya kuwalazimisha wachezaji wake kuvaa mavazi ya Adidas katika shughuli rasmi za klabu hiyo - ni viatu pekee ambavyo wanaruhusiwa kuvaa vyovyote.

Ingawa, wote wawili Gotze na Kirchhoff walipokuwa wakitambulishwa kujiunga na klabu hiyo walionekana wakiwa wamevaa mavazi ya fulana zenye logo za Nike - ambao ni wapinzani wakuu wa kibiashara na Adidas.
Bayern tayari wameomba samahani kwa kampuni ya Adidas, lakini wakiwa wamefanya hivyo muda mchache baadae Mario Gomez akapigwa picha akiwa amevaakofia yenye logo ya Nike kwenye uwanja wa mazoezi.

Matokeo yake mabingwa wa ulaya wakaamua kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wachezaji wote watatu kwa kuwapiga faini, ambazo zitaenda kwenye kusaidia wahanga wa mafuriko nchini Ujermani.
Wachezaji wote wamekubali faini zao, lakini hakitajwa kiasi cha faini hizo.

NEYMAR KIBOKO: ASILIMIA 20 YA WATOTO WANAOZALIWA BOLIVIA HIVI KARIBUNI WAPEWA JINA LAKE


Mchezaji wa bora wa mashindano ya kombe la mabara  Neymar ana miaka 21 tu , lakini ni mmoja ya wachezaji wa Amerika ya Kusini ambao wanaweza kuwafanya watu wazimie kwa kujawa na furaha kwa kumuangalia tu mchezaji huyo wa kibrazili na huku akiwa anakaribia kujiunga rasmi na Barcelona, umaarufu wake unaweza ukazidi kukua mpaka kwenye mabara mengine. 
Katika kuonyesha ni namna gani anakubalika huko barani Amerika, watu nchini Bolivia wamewapa watoto wao jina la Neymar katika hali ya kumtukuza winga huyo wa kibrazili. 
Kutoka Sambafoot:
Kwa mujibu wa gazeti la Bolivia La Razon, watoto wawili kati y 10 wanaozaliwa kwenye nchi hiyo wamekuwa wakipewa jina la mchezaji huyo wa selecao. Na wanatabiri kwamba suala hili litazidi kukua kwa kuwa hata baadhi ya wanaume hasa kwenye mji wa La Paz wamekuwa wakijipa jina la nyota huyo wa Barcelona
           "Tunaamini miaka 17 ijayo vijana wengi wa wakati huo watakuwa na jina la Neymar kwa sababu ya huu mtindo mpya ulioingia,' alisema msajili wa raia Remigio Condori . 

KALI YA LEO: DORTMUND WATAMBULISHA JEZI YAO MPYA KWA KUTUMIA MAUA YALIYOPANDWA KWENYE BUSTANI


Borussia Dortmund wamezindua jezi yao mpya ya nyumbani watakaovaa msimu ujao na wamefanya hivyo kwa namna ya kipekee. Watengenezaji wa jezi zao Puma walitengeneza mfano wa jezi za nyumbani za Borussia kwa kutumia maua yasiyopungua 80,600 kutengeneza mfano wa jezi katika bustani ya Dortumund Westfalenpark. 
Kutoka BVB.de:
Usiku wa alhamisi, PUMA ilipanda maua 80,645 , ambayo ni idadi sawa ni ya washabiki wanaoweza kuingia kwenye uwanja wa Dortmund  SIGNAL IDUNA PARK, walifanya hivi katika kubuni na kutambulisha jezi mpya - kwa kutumia maua tofauti ya njano na rangi nyeusi. 


Friday, July 5, 2013

BREAKING NEWS: MOYES ASEMA: ROONEY HAUZWI, ATAENDELEA KUWA MCHEZA WA UNITED - KUHUSU RONALDO ASHINDWA KUKATAA WALA KUKUBALI KUTAKA KUMSAJILI

Kocha wa Manchester United David Moyes leo hii amethibitisha kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney hayupo sokoni na ataendelea kuicheza klabu hiyo kwa mingi ijayo.

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na klabu hiyo akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, Moyes alisema: "Nimeongea na Wayne Rooney. Wayne yupo nyuma ya mabao 40 kumfikia Sir Bobby na Denis Law. Wayne hauzwi - ni mchezaji wa Manchester United - na ataendelea kubakia kuwa mchezaji wa Manchester United. Nimekuwa na mikutano nae kadhaa. Amerudi kwenye hali nzuri na anafanya vizuri mazoezini. Tunajaribu kufanya kila kitu kumrudisha Wayne Rooney kuwa kama alivyokuwa zamani - Wayne Rooney ambaye tunamjua.

"Vyovyote vilivyotokea kabla, tunafanya kazi pamoja sasa. Macho yake yanaonyesha ni mtu mwenye furaha, ni lazima niseme Wayne hauzwi. Kuliwahi kuwepo mkutano wa siri baina ya Rooney na Sir Alex. Mie naendelea mbele sasa, sijui nini kilizungumzwa kwenye mkutano huo. Ninachofikiria sasa ni kusonga mbele na kufanya kazi ya kumrudisha Wayne Rooney kwenye ubora wake. "


Alipoulizwa kuhusu Cristiano Ronaldo, Moyes alijibu: "Sitomzungumzia yeye moja kwa moja na wachezaji wengine wa vilabu vingine. Lakini hii klabu siku zote imekuwa ikivutiwa na wachezaji bora duniani."

Pia Moyes alithibitisha kwamba winga mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace - Wilfred Zaha ambaye amekuwa akiwindwa na vilabu vingi kujiunga navyo kwa mkopo - Moyes amesema mchezaji huyo ataungana na Manchester United kwenye tour ya pre-season, kama ilivyo kwa wachezaji wengine. 

Wakati huo huo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wapya, Moyes amesema angependa kusajili wachezaji mapema lakini mambo yamekuwa yakichelewa kutokana na makocha ambao ndio wanaothibitisha uuzwaji wa wachezaji wengi wamekuwa likizo au ndio wanaingia kwenye vilabu vyao vipya.

PICHA ZA SIKU: MASHINDANO YA MAGARI YA GHARAMA YASIYO RASMI YA WACHEZAJI WA MAN UNITED: ANDERSON KIBOKO AINGIA MAZOEZINI NA GARI LA MILLION 286

MERC-URIAL TALENT ... Anderson turns up in his £168,395 SLS
    Anderson akiingia na gari yake aina ya Mercedez yenye thamani ya  £168,395 
 
Leo asubuhi wachezaji wa Manchester United walikuwa na mashindano yasiyo rasmi ya kuonyesha magari yao ya thamani wakati wakiwasili kwenye uwanja wao wa mazoezi AON Carrington. Mchezaji wa kibrazil Anderson pamoja na kutokuwa mmoja ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sana na United - yeye ndio alikuwa mchezaji aliyekuja na gari la thamani zaidi Mercedez ambalo linauzwa kiasi cha millioni 286,271,500 za kitanzania.
 

Rio Ferdinand — Jaguar XJ Portfolio (£70,385)

Rio Ferdinand

Wayne Rooney — Range Rover Sport Autobiography (£84,895)

Rooney

Nemanja Vidic — Mercedes M Class (£47,385)

Vidic


Ryan Giggs — Range Rover Sport Autobiography (£98,395)

Giggs

Phil Neville — Porsche Cayenne (£86,895)

Neville

Rafael and Fabio da Silva — Chevrolet Captiva (£32,000)

Fabio & Rafael

Michael Carrick — Mercedes M Class (£47,386)

Carrick

Ashley Young — Range Rover Sport Autobiography (£68,995)

Young

Alex Buttner — Chevrolet Camaro Coupe (36,785)

Buttner

DOGO ALIYETANDIKWA NA HAZARD AUZA KOTI LAKE ALILOKUWA AMEVAA WAKATI WA MECHI YA CHELSEA VS SWANSEA - ILI KUSAIDIA WAGONJWA WA KANSA

Wote tunamkumbuka yule kijana muokota mipira aliyepigwa na Eden Hazard msimu uliopita katika mechi ya nusu fainali ya kombe la ligi kati ya Chelsea dhidi ya Swansea - kijana yule sasa ameamua kulipiga mnada koti alilovaa siku ile wakati akipokea kipigo kutoka kwa Hazard.

Charlie Morgan, ambaye aliukalia mpira uliotoka nje wakati Chelsea wakitafuta ushindi wa kuweza kuwapeleka fainali, Hazard alipoenda kuufuata ule mpira dogo akawa bado ameukali ndipo winga huyo wa Mbelgiji alimpopiga teke katika kuujaribu kuuchukua mpira huo. Hazard alitolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa hilo. Lakini baadae wawili hao walikutana na kumalizana kistaarabu na mchezaji huyo wa Chelsea alisaini koti alilokuwa amevaa kijana Charlie Morgan muokota mipira.
 

Sasa ikiwa imepita miezi kadhaa tangu tukio hilo litokee - kijana Charlie ameamua kulipiga mnada koti lake lilosainiwa na Hazard kwenye mtandao wa Ebay - na mapato yatakayopatikana yataenda kusaidia wagonjwa wa kansa.


WABURUNDI KUCHEZESHA MECHI YA STARS DHIDI YA UGANDA - AIRTEL RISING STARS KUONYESHWA SUPERSPORT

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao ni Thierry Nkurunziza atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Jean Claude Birumushahu na Pascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni pacifique Ndabihawenimana.

Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Eritrea na mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya CHAN.

FAINALI AIR RISING STARS ‘LIVE’ SUPERPORT
Fainali za michuano ya Airtel Rising Stars kwa wavulana na wasichana zinazochezwa kesho (Julai 6 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam zitaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport.

Mechi za fainali ambazo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala zitachezwa kuanzia saa 7.30 mchana kwa wasichana wakati ile ya wavulana itaanza saa 9.30 alasiri.

Nusu fainali za mashindano hayo ambazo pia zinaonekana moja kwa moja SuperSport zinachezwa leo (Julai 5 mwaka huu). Kwa upande wa wasichana ni kati ya timu za Kinondoni na Kigoma wakati Ilala inaumana na Temeke.

Kwa upande wa wavulana nusu fainali ya kwanza ni kati ya Mwanza na Ilala ambapo baadaye itafuatiwa na nyingine kati ya Morogoro na Kinondoni. Mechi za kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa kesho asubuhi (Julai 6 mwaka huu).

28 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA 11 FOR HEALTH
Jumla ya makocha wa mpira wa miguu na walimu 28 kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na shule za msingi na sekondari wameteuliwa kuhudhuria kozi ya FIFA 11 For Health inayoanza keshokutwa (Julai 7 mwaka huu) Homboro mkoani Dodoma.

Kozi hiyo itakayomalizika Julai 20 mwaka huu itakuwa chini ya ukufunzi wa Rogasian Kaijage ambaye pia ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars).

Washiriki ni Abdul Mikoroti (Shule ya Msingi Nzasa), Baltazar Kagimbo (Shule ya Msingi Tabata Jica), Baraka Baltazar (Shule ya Msingi Muhimbili), David Kivinge (Shule ya Msingi Temeke), Dismas Haonga (Tambaza Sekondari), Exuperus Kisaka (Shule ya Msingi Mavurunza) na Hadija Kambi (Shule ya Msingi Karume).

Hamis Chimgege (Shule ya Msingi Tusiime), Hobokela Kajigili (Shule ya Msingi Buguruni), Issack Mhanza (Shule ya Msingi Airwing), Job Ndugusa (Shule ya Msingi Upanga), John Sebabili (TFF), Lutta Rucharaba (Shule ya Msingi Montfort), Maua Rahidi (Shule ya Msingi Uhuru Wasichana), Michael Bundala (TFF) na Mussa Kapama (Shule ya Msingi Bunju ‘A’).

Priscus Silayo (Shule ya Msingi J.K. Nyerere), Peter Manyika (TFF), Rajabu Asserd (Shule ya Msingi Mtoni Kijichi), Raphael Matola (TFF), Raymond Rupia (St. Anne Maria Academy), Renatus Magolanga (Ulongoni Sekondari), Ruth Mahenge (Shule ya Msingi Chang’ombe), Said Pambaleo (TFF), Sebastian Nkoma (TFF), Titus Michael (TFF), Wane Mkisi (Jangwani Sekondari),

LIUNDA KUSIMAMIA MECHI YA CHAN
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa Kamishna wa mechi kati ya Burundi na Sudan itakayochezwa jijini Bujumbura.

Mechi hiyo ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) itafanyika keshokutwa (Julai 7 mwaka huu). Liunda anatarajia kuondoka leo usiku (Julai 5 mwaka huu) kwenda Bujumbura..

SJMC,TASWA KUENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI HABARI ZA MICHEZO

SHULE Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) wataendesha mafunzo ya siku tano kwa waandishi wa habari za michezo nchini.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Makamu Mkuu wa SJMC, Dk. Michael Andindilile alisema mafunzo hayo yatafanyika Agosti mwaka huu na yataendeshwa na wahadhiri kutoka chuoni hapo, waandishi wa siku nyingi na wataalamu wa michezo mbalimbali.
“Tunao wahadhiri waliobobea katika tasnia ya habari, lakini pia wapo waandishi wa habari wakongwe ambao ni waalimu kitaaluma, pia tutachukua wataalamu wa michezo mbalimbali kuja kufundisha kwa siku hizo tano,” alisema Dk. Andindilile.
Makamu Mkuu huyo wa SJMC, aliupongeza uongozi wa TASWA kwa wazo lao la kushirikiana na SJMC na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatachukua siku tano na yatafanyika Dar es Salaam yakihusisha washiriki 45 kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika tarehe itakayotangazwa.
Alisema wataalamu wa michezo mbalimbali kama vile soka, riadha, netiboli, gofu, kikapu, wavu na mikono watapata fursa ya kutoa mada kuhusiana na michezo yao na kwamba TASWA na SJMC wanashirikiana katika kuomba wadhamini wasaidie mafunzo hayo.
“Hii ni awamu ya kwanza kwa waandishi wachanga na baadhi ya wa kada ya kati, baada ya hapo tutaendesha mafunzo ya namna hii kwa waandishi wa siku nyingi wa habari za michezo na wahariri wa habari za michezo, tunaamini baada ya hapo kutakuwa na mabadiliko upande wa uandishi wa habari za michezo,” alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto aliishukuru SJMC kwa kukubali kushirikiana na TASWA na kwamba siku zote chama chake kimekuwa kikipigania kuandaa mafunzo kwa wanahabari wa michezo kama sehemu mojawapo ya kukuza weledi.
“Fursa hii ni moja ya jitihada za TASWA kuhakikisha waandishi wa habari za michezo wanapata nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu namna bora ya kuripoti habari za michezo kwa ujumla wake, hivyo nafasi hii si tu itasaidia wanachama wa TASWA bali pia na vyombo vya habari na washiriki hawatalipia chochote.
“Tunaamini waandishi wanapoboresha uandishi wao inachangia kwa kiasi kikubwa kukuza heshima ya vombo vya habari, hivyo tunaomba wadau mbalimbali washirikiane nasi kudhamini mafunzo haya,” alisema Pinto na kuongeza kuwa kwa kushirikiana na SJMC wanaamini siku za usoni wanaweza kuandaaa mafunzo ya muda mrefu.

Morogoro yailaza Temeke 5-2 michuano ya Airtel Rising Stars

Timu za Airtel Rising Stars zikiingia kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam tayari kwa ufunguzi rasmi wa ARS ngazi ya Taifa jana Jumanne Julai 2, 2013..

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano – Mallya akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini  Dar es Salaam jana Jumanne

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini  Dar es Salaam





Timu ya Morogoro wavulana leo Jumatano Julai 3, imeifunga timu ya Temeke 5-2 katika fainali za Taifza za Airtel Rising Stars
zinazoendelea kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Morogoro waliutawala mchezo na kufanikiwa kupata magoli kupitia kwa
 mshambuliaji wa machachali Optatus Lupekenya ambaye alifunga magoli matatu peke yake yaani ‘hat trick’ katika dakika za 27 67 na 87.
Magoli mengine ya Morogoro yalifungwa Salum Mohamed dakika ya 72 na Evance Noshan dakika ya 80 wakati magoli ya Temeke yalifungwa na Mohamed Simba dakika ya 10 na Rajab Jumanne dakika ya 83.

Katika mchezo uliochezwa mapema asubuhi timu ya Ilala wasichana
 ilifanya mauaji ya kutisha baada ya kuifunga bila huruma timu ya Ruvuma 9-0 katika mchezo wa upande mmoja wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars. 

Mchezo huo ulionyesha wazi ya kuwa Ruvuka wanatakiwa
kufanya kazi ya ziada ili kuinua kiwango chao cha soka.

Ilala walifunga magoli yao kupitia kwa Amina Ally (dakika ya 3, 28 na
51), Donisia Daniel (dakika ya 20 na 45), Zuwena Aziz (dakika ya 23 na 35), Madeline Sylvester (dakika ya 8) na Fatuma Bahau (dakika ya 12).

Katika mchezo uliochezwa Jumanne jioni katika uwanja huo huo, timu ya
  kombaini ya Mwanza (wavulana) ilitoa onyo kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo baada ya kuifunga timu ngumu ya Ilala 3-1.

Huo ulikuwa mchezo rasmi wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars Taifa 2013
 ambapo mgeni rasmi Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Kassim Majaliwa aliwataka vijana kuonyesha vipaji vyao.

“Katika dunia ya leo mpira wa miguu ni moja ya vyanzo vya ajira vya
 kutumainiwa kwa vijana”, alisema Majaliwa na kuwahamasisha vijana hao kucheza kwa kujituma na kutumia mashindano ya Airtel Rising Stars kama fursa ya kuonyesha umahiri wao wa kusakata kabumbu. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendeleza kusaidia programu hii ya vijana.

Mchezo kati ya Mwanza na Ilala ulikuwa wa kuvutia huku timu zote
 zikionyesha kiwango kizuri kwa kugongeana pasi za uhakika. Mwanza walifanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya saba kupitia kwa Nassor ambaye aliwapita walinzi wa Ilala na kutia mpira wavuni. Goli hilo lilidumu hadi mapumziko.

Ilala walianza kipindi cha pili kwa nguvu na kupata goli la

kusawazisha dakika ya 50 kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Omary Hassan baada ya walinzi wa Mwanza kufanya makosa nje kidogo ya eneo la hatari. Mshambuliaji Athanas Adam aliifungia Mwanza goli la pili dakika ya 69 na Kelvin Ntalale kugongelea msumari wa mwisho dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika.

HIGUAIN KUFANYIWA VIPIMO LEO NA KUSAINI MKATABA WA MIAKA 3 NA ARSENAL - WENGER AKIVUNJA REKODI YA ADA YA USAJILI



ARSENAL jana usiku walivunja rekodi yao ya usajili baada ya kukubaliana na Madrid kulipa kiasi cha  £23million kwa ajili ya kumsaini Gonzalo Higuain.

Muargentina huyo atafanyiwa vipimo na Gunners leo na anategemewa kusaini mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya100,000 kwa wiki.

Higuain, 25, amepewa ruhusa na Madrid kusafiri kwenda London baada ya mazungumzo marefu yaliyodumu kwa wiki kadhaa.

Dili hili ambalo limethibitishwa na baba yake Higuain linakuja kuleta nafuu kwa mashabiki wa Arsenal waliokuwa wakililia kocha wao asajili wachezaji wa daraja la dunia, ili kuweza kukata kiu ya zaidi ya miaka nane ya kutwaa kombe.

Santiago Cazorla ndio alikuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Arsenal - akiwa amesajiliwa kwa zaidi ya paundi millioni 16 akitokea Malaga.


Golikipa Julio Ceasar ndio anatajwa kumfuatia Higuain kwenda Emirates akitokea QPR ambao wameshuka daraja.

CAMEROON YAFUNGIWA NA FIFA BAADA SERIKALI KUINGILIA MASUALA YA SOKA


Cameroon imefungiwa kwa muda na FIFA kufuatia serikali ya nchi hiyo kujiingiza katika masuala ya chama cha soka nchini humo.

Tangazo la FIFA limesema kwamba kamati ya dharura ya shirikisho hilo la soka duniani imeamua kusimamisha kwa muda chama cha soka cha Cameroon FECAFOOT na uamuzi huo umeanza kutekelezwa mara moja kwa sababu serikali inaingilia masuala ya chama cha soka

Taarifa hizi zimekuja saa moja baada ya Cameroon kuzawadiwa pointi 3, kuwarudisha kwenye uongozi wa kundi I, baada ya Togo kuadhibiwa kwa kumchezesha mchezaji Jacques Alexys Romao, ambaye hakupaswa kucheza wa mwezi uliopita baina ya timu hizo mbili.

Hatua hii ya FIFA inawazuia Indomitable Lions kucheza mchezo wao muhimu wa kufuzu dhidi ya Libya September 6.

Taarifa rasmi ya FIFA ilisema: “"kamati ya dharula ya FIFA imeamua kufungia chama cha soka cha soka cha Cameroon kutokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka ya chama hicho.

“Wakati wa kipindi cha kifungo hichi, Fecafoot inaweza isiwakilishwe katika michuano yoyote ya inayosimamiwa na FIFA na CAF, kuanzia ngazi ya taifa kwenye vilabu kwenye mechi za mashindano mpaka kirafiki."

NICOLAS ANELKA ARUDI TENA ENGLAND - ASAJILIWA NA WEST BROM NA KUWEKA REKODI YA KUCHEZEA KLABU 6 ZA LIGI KUU YA ENGLAND


West Brom wamethibitisha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa Nicolas Anelka.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 34, ambaye alikuwa huru, amesaini mkataba wa kuanzia wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya England.

Klabu hiyo imethibitisha kupitia akaunti yake ya Twitter: 'Albion leo usiku imekamilisha usajili wa @anelkaofficiel kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku kukiwa na hivyo.'

Kocha wa Baggies Steve Clarke, ambaye alishafanya kazi na Anelka kwa muda mfupi ndani ya klabu ya Anelka amefurahia usajili huo.
'Tulikuwa tunakosa nguvu ya ziada kwenye ushambuliaji kutoka mwaka jana, tunajaribu kuweka hilo sawa - na kwa kuanzia kwa usajili wa  Nicolas,' aliuambia mtandklabu hiyo wba.co.uk.

Anelka sasa anazidi kujiandikia rekodi ya kuwa mchezaji aliyevicheza vilabu vingi kwenye ligi kuu ya England baada ya kuitumikia Arsena, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Bolton


VILABU VYOTE ALIVYOCHEZEA ANELKA
Senior career*
YearsTeamApps(Gls)
1996–1997Paris Saint-Germain10(1)
1997–1999Arsenal65(23)
1999–2000Real Madrid19(2)
2000–2002Paris Saint-Germain39(10)
2001–2002→ Liverpool (loan)20(4)
2002–2005Manchester City89(37)
2005–2006Fenerbahçe39(14)
2006–2008Bolton Wanderers53(21)
2008–2012Chelsea125(38)
2012–2013Shanghai Shenhua22(3)
2013→ Juventus (loan)3(0)
2013–West Bromwich Albion0(0

Thursday, July 4, 2013

PICHA YA SIKU: BARCELONA WAMUONDOA THIAGO ALCANTARA KWENYE TANGAZO LA JEZI NA TOUR KWENYE AKAUNTI YAO YA INSTAGRAM


Klabu ya Barcelona imemkata mchezaji wao Thiago Alcantara anayewania na Manchester United kwenye tangazo la kuitangaza tour yao pamoja na jezi mpya waliloweka kwenye akaunti yao rasmi ya mtandao wa kijamii wa Instagram. Thiago kwa muda mrefu sasa ametajwa kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo huku vyombo vya habari vikiripoti kwamba ndani ya wiki hii mchezaji huyo atakuwa ameshajiunga na United chini ya David Moyes. FC Barcelona na United zote hazijakanusha wala kukubali taarifa hizi - ila kwa kitendo cha Barca kukata sura ya Thiago kwenye picha ambayo mwanzoni alikuwepo kimezidi kuzipa nguvu tetesi za mchezaji kuhamia Man United. Lakini hizi zote ni tetesi na hakuna kilichothibitishwa.
Picha ya juu inaonyesha ilivyokuwa mwanzo Thiago akiwepo - wakati hii ya chini ni ya leo ikiwa sura ya Thiago Alcantara haijakwatwa.

ZDRAVKO MAMIC: 'JORGE MENDES' WA CROATIA ANAYEKULA ASILIMIA 20 YA MSHAHARA YA LUKA MODRIC - AGEUZA DINAMO ZAGREB KIBONDE KWA KUIPA UTAJIRI


Timu kubwa na yenye nguvu sana kwenye soka la Croatia haikufanya vizuri katika hatua ya makundi ya michuano miwili iliyopita ya Champions League. Kati ya michezo 12 waliyocheza, walipata pointi moja tu kati ya 36. Hwakufanya vizuri kabisa kwenye michuano hii, lakini kwao kucheza tu ilitosha sana.  Lakini Dinamo Zagreb imetoa vipaji vingi sana kwenye soka na tunavifurahia vipaji hivyo shukrani kwa mtu mmoja aitwaye  Zdravko Mamic.


Zdravko Mamic ni ni mkurugenzi wa michezo wa Dinamo. Amekuwa maarufu sana kwa tabia yake ya kuwatolea maneno machafu baadhi ya waandishi wa habari, akiwatishia kuwafanyia vurugu na kuwatukana wao na kazi yao. Pia amekuwa akihusishwa sana na sajili tata za wachezaji hasa wa nchi hiyo. Aliwahi kukamatwa baada ya kumtukana waziri wa michezo wa Croatia, lakini pamoja na vituko kocha huyu ana mazuri yake. Ni genius linapokuja suala la kufanya biashara ya wachezaji.

Katika kipindi cha miaka 10, tangu Zdravko Mamic ajiunge na Dinamo Zagreb, klabu hiyo imejipatia kiasi cha 160 million kutokana na mauzo ya wachezaji.

Dinamo Zagreb sio timu inayofanya biashara ya kuuza sana wachezaji barani ulaya kama ilivyo kwa Porto, lakini hawapo mbali kwenye. Benfica na Udinese pia nao wanafuatia, lakini inabidi vilabu hivi vyote vina misuli ya kifedha kuliko klabu hii ya Croatia.
Luka Modric mmoja ya wachezaji wanamuingizia fedha nyingi Mamic

Mamic anapata fedha nyingi kwa kukubali kuwauza wachezaji kwenda kwenye vilabu vikubwa. Mfano mzuri ni dili aliloingia na Luka Modric - walikubaliana na mchezaji huyo kupata asilimia 20 ya mshahara wake atakaokuwa akilipwa na klabu yake. Pia dili hilo limeendelea mpaka sasa mchezaji huyo akiwa na Real Madrid - kwa makataba wa miaka mitano na Madrid - Luka Modric atampatia kiasi kisichopungua 900 000 Euros Zdravko Mamic. 

Tangu awe mkurugenzi wa ufundi wa Dinamo mwaka 2003, ameshawabadilisha makocha 15 tofauti - waliokuwa wanatofautiana nae kwenye suala la kuuza wachezaji pale anapoona kuna maslahi yake yake binafsi.
 
BAADHI YA UHAMISHO WALIOWAHI KUFANYA DINAMO ZEGREB

Luka Modric to Tottenham , €21 million
Mateo Kovacic  to  Inter Milan , €15 million
Eduardo da Silva to Arsenal, , €15 million
Vedran Corluka to Manchester City, , €13 million
Dejan Lovren to Lion  , €9.5 million
Mario Mandzukic to Wolfsburg,  , €9 million 
Pia hivi sasa Mamic yupo katika mazungumzo na Tottenham katika kukamilisha baishara ya kuwauza wachezaji wawili Tin Jedvaj na Alen Halilovic ambaye anatajwa kuwa mrithi wa Luka Modric. Dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya paundi millioni 18 - na hapo Mamic ana kato lake pamoja na kuwa na mikataba binafsi na wachezaji hao wawili.

Taarifa nchini Croatia zinasema Mamic yupo katika matayarisho ya kuanzisha kampuni ya uwakala wa wachezaji, ili kufuata nyayo za wakala maarufu barani ulaya Jorge Mendes.

VAN GINKEL MCHEZAJI WA PILI KUSAJILIWA NA JOSE MOURINHO TANGU ATUE CHELSEA - ANGALIA UJUZI WAKE

JOSE MOURINHO amefanya usajili wa pili tangu kujiunga na Chelsea kwa kumsajili kiungo wa kidachi Marco van Ginkel.

Chelsea wamethibitisha asubuhi hii kwamba wamekubaliana ada ya uhamisho, ambayo inaaminika kufikia kiasi cha  £8million, na klabu ya Vitesse Arnhem kwa kwa ajili ya kupata saini ya kiungo huyo anayesifiwa mno na wachambuzi wa soka barani ulaya.

Kilichobaki sasa ili kukamisha usajili huo ni kwa Van Ginkel kufanyiwa vipimo vya afya na makubaliano ya maslahi binafsi, ingawa haya hayaonekani kuja kuwa kikwazo.

MUANGALIE VAN GINKEL HAPA


STORY NZURI YA DAVID BECKHAM AND ISCO NA USAJILI WAO REAL MADRID


Julai 3 mwaka 2003, David Beckham alisaini mkataba wa kuichezea Real Madrid akitokea Manchester United na kuchagua jezi namba 23......................
 
Miaka 10 baadae siku ile ile ya Julai 3, 2013 kijana Isco asaini mkataba wa kuichezea Real Madrid akitokea Malaga na kuchagua jezi namba 23. 

By Derick Lawrence

BREAKING NEWS: RYAN GIGGS ATEULIWA KOCHA/MCHEZAJI MANCHESTER UNITED

Klabu ya Manchester United leo imemtangaza mchezaji mkongwe zaidi wa klabu hiyo kuwa kocha wakati akiwa bado anaendelea kuichezea klabu hiyo.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mtandao rasmi wa Manchester United kwamba Giggs ambaye hivi karibuni alimaliza mafunzo yake ya ukocha atakuwa mmoja ya jopo la makocha watakaomsaidia David Moyes kuendesha jahazi liloachwa na Sir Alex Ferguson.

Pia wakati huo huo kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba David Moyes amemteua Phil Neville kuwa kocha wa timu ya kwanza.

KIBADENI KOCHA BORA, YONDANI MWANASOKA BORA, NA YANGA NDIO TIMU YENYE NIDHAMU - TUZO ZA VODACOM PREMIER LEAGUE



Beki wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya Yanga, Kevin Patrick Yondan amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 na kuzawadiwa donge nono la Sh. Milioni 5. Yondani ambaye alihamia Yanga akitokea Simba amechaguliwa kuwa mwanasoka bora VPL baada ya kuwa na msimu mzuri na klabu yake ya Yanga ambayo ilitwaa ubingwa huo huku akiruhusu mabao machache kuliko timu nyinginezo.
Vodacom pia ilitoa tuzo kwa kocha na bora na wachezaji wengine waliofanya vizuri msimu uliopita na tuzo zilikuwa kama zifuatazo

Top Scorer- Kipre Tchetche Azam (5m)
Best Player- Kevin Yondani (5m)
Best Coach Abdallah Kibadeni Kagera (7.5m),
Best Goalkeeper- David Burhani Prisons (5m)
Mchezaji mwenye nidhamu- Fulli Maganga JKT Ruvu (5m)
Team yenye nidhamu- Yanga (15m)