Search This Blog

Saturday, March 16, 2013

OFFICIAL: UONGOZI SIMBA WAKANUSHA KUWEPO KWA MKUTANO MKUU KESHO


                      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu wana habari,
KUMEKUWAPO na taarifa za kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba uliopangwa kufanyika Kesho (Machi 17, 2013) jijini Dar es Salaam kujadili mustakabali wa klabu.
Ikumbukwe kwamba Mkutano Mkuu wa Wanachama ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi kwa klabu yetu. Katiba ya Simba SC imeupa Mkutano Mkuu hadhi ya juu mno na ndiyo maana imeweka utaratibu wa kufanyika kwake.
Miongoni mwa utaratibu ni kwamba ni lazima uitishwe na Mwenyekiti aliye madarakani wa klabu. Kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, ndiye atakayepanga ajenda, mahali na wakati wa kufanyika kwa mkutano wenyewe.
Katika miaka ya nyuma, zilikuwepo nyakati ambapo klabu ilikaa hadi miaka mitatu pasipo kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wowote wa wanachama. Hakuna mwanachama au kikundi chochote kilichojitokeza kudai mkutano wa dharura wakati huo ingawa ilikuwa ikifahamika kwamba huo ulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya klabu.
Tangu uongozi huu uingie madarakani takribani miaka mitatu iliyopita, mikutano mikuu miwili ya wanachama imefanyika kwa mujibu wa KATIBA. Mungu akijaalia, uongozi huu utafanya mkutano mwingine wa kawaida wa wanachama baadaye mwaka huu.
Hata hivyo, kwa kuzingatia hali halisi ya klabu, Mwenyekiti wa Simba, Alhaji Ismail Aden Rage (Mb), mwezi uliopita alitangaza dhamira yake ya kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wakati wowote kuanzia sasa.
Rage alisema mkutano huo ungekuwa na ajenda moja tu; Kujadili Mwenendo wa Klabu kwenye mashindano inayoshiriki msimu huu.
Kwa bahati mbaya, Mwenyekiti alishikwa na maradhi na akapelekwa India kwa matibabu na yuko huko hadi Mola atakapomjalia afya njema na kurejea. Kuna uwezekano mkubwa, Inshallah, akarejea mwishoni mwa wiki ijayo.
Hii maana yake ni kwamba uongozi umeridhia kufanyika kwa Mkutano wa wanachama. Kimsingi, kama uongozi umeridhia, hakuna mwanachama mwingine anayeweza kuitisha mkutano mkuu mwingine.
Mwenyekiti ameruhusiwa kuitisha Mkutano Mkuu kwa sababu alichaguliwa na wanachama na hivyo ana nguvu ya kisheria (locus standi) kufanya hivyo. Hawa wengine wanaoitisha mkutano wana nguvu gani ya kisheria kufanya hivyo? Walichaguliwa na nani kuwakilisha wanachama? Lini na wapi?
Uongozi pia unaweza kuitisha mkutano kwa vile wenyewe ndiyo wenye leja ya wanachama. Klabu sasa ina database yake ya kompyuta inayotambua wanachama walio hai na wasio hai.
Kwa kutumia database hiyo, uongozi huu unatambua wanachama walio hai na wasio hai. Hakuna mtu mwingine yeyote, aliye nje ya uongozi huu anayefahamu wanachama walio hai na wasio hai. Hao wanachama wanaoitana kufanya mkutano, wamehakikiwa na nani kubaini uhalali wao huo?
Uongozi wa Simba SC unaona kwamba wale wanaolazimisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wana ajenda binafsi na si za maslahi ya klabu. Kama kweli wangekuwa na nia njema na klabu wangesubiri mkutano ambao utaitishwa punde.
Kwani, kuna uharaka gani wa kufanyika mkutano kesho? Kwanini hawataki Mwenyekiti, ambaye wanachama walimpa mamlaka ya kuongoza klabu kwa kipindi cha miaka minne, awepo kwenye mkutano huo?
Kwanini hawataki kuungana na wana Simba wengine kumwombea Mwenyekiti kwa Mungu ili amwepushe na ugonjwa na kumrejesha salama hapa nyumbani? Kwanini mikutano hii iitishwe katika kipindi ambacho uongozi umefungua mikono yake na kukaribisha kila mmoja mwenye mapenzi mema na klabu kuja kuchangia?
Kwenye macho ya Katiba ya Simba na sheria za Tanzania, huu mkutano wa kesho ni batili na una lengo la kuleta vurugu na mifarakano kwenye jamii na michezo kwa ujumla wake. Michezo ni amani na furaha na michezo si vurugu.
Tayari uongozi wa Simba umetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na ubatili wa mkutano huo. Tunapenda kuwaomba wanachama wetu wasiopenda fujo na vurugu kwenye michezo kukaa mbali na mkutano huo kwa vile vyombo vya dola vitaufuatilia.
Uongozi hautajiingiza katika kutoa dhamana au msaada wa namna yoyote kwa yeyote ambaye atachukuliwa hatua na vyombo vya dola kutokana na kujihusisha na mkutano huo.
Pia, Simba SC inatoa wito kwa vyombo vya habari kuwa makini wakati vinaporipoti matukio ya vurugu kwenye michezo. Kabla mtu hajahojiwa kujieleza kama mwanachama wa Simba, ni vema kwanza akaonyesha kadi yake ya uanachama na risiti za malipo yake.
Wakati mwingine, waandishi huwa tunawapa nafasi kwenye vyombo vyetu vya habari watu ambao hawana mchango wowote kwenye kukuza michezo bali kuleta vurugu. Kwanini, tungejiuliza, ni watu wale wale ambao kila mwaka huonekana wakati wa vurugu na wakati wa amani huwa hawaonekani?
Kwanini, vyombo vyetu vinatoa nafasi kwa watu ambao lengo lao ni kuhakikisha vilabu vyetu vinazidi kubaki nyuma, vinakuwa na vurugu kila wakati na michezo inaonekana kama ni sehemu ya wahuni na watu wasio na utaratibu?
Mpira bado haujaleta tija kubwa kwenye uchumi wa Tanzania na kunufaisha wachezaji kwa sababu baadhi ya watu makini na makampuni makubwa yanaogopa kujiingiza kwenye michezo kwa sababu ya tabia kama hizi.
Ni vema vyombo vya habari vikafanya jitihada kubwa katika kuwatambua waleta vurugu, si katika klabu ya Simba pekee, bali kwenye sekta ya michezo kwa ujumla, ili visiwape nafasi ya kuharibu na badala yake vitoe nafasi kwa wale wenye lengo la kujenga.
Tunasisitiza, uongozi huu utaitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama Wote mara baada ya kurejea kwa Mwenyekiti.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

LIVE MATCH CENTRE: YANGA SC 1 - 0 RUVU SHOOTING FULL TIME

Dk 90 FULL TIME! YANGA 1-0 RUVU

Dk 83 Ruvu imefanya mabadiliko, ametoka Ayoub Kitala ameingia Raphael Kyala.

Dk 80 Yanga imefanya mabadiliko, ametoka Nizar ameingia Didier Kavumbagu.

Dk 78 Mangasini wa Ruvu anamchezea vibaya Nizar wakati akiwa katika harakati za kufunga. Nizar hawezi kuendelea na mchezo.

Dakika ya 75, Ruvu Shooting 0 - 1 Young AfricansDk 72 Yanga inatawala mchezo kwa kucheza mpira wa pasi nyingi.

Dakika ya 60, Ruvu Shooting 0 - 1 Young Africans

Dk 56 Ruvu wanafanya mabadiliko, ametoka Gideon Tepo ameingia Paul Ndauka.

Dk 55 Kiiza anashindwa kuunga kwa kichwa krosi ya Nizar.

Dk 50 Mangasini Mangasini wa Ruvu anampiga kiwiko Domayo lakini mwamuzi hajaona.

Wakati wa mapumziko Yanga ilifanya mabadiliko, ametoka Joshua ameingia David Luhende.

Dakika ya 48, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la kwanza
Ruvu Shooting 0 - 1 Young Africa

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Ruvu Shooting 0 - 0 Young Africans

Dk 45 HALF TIME! YANGA 0-0 RUVU.

Dk 43 Nizar wa Yanga anayecheza kama straika leo, anaonekana amechoka na kushindwa kuziwahi pasi na krosi nyingi zinazopigwa eneo lake.

Dk 39 Kipa wa Ruvu, Benjamin Haule anadaka kwa ustadi krosi ya Msuva huku Nizar akiwa tayari kuiunganisha.

Dk 36 Beki wa Yanga, Oscar Joshua anaonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Jacob Adongo baada ya kumchezea rafu Said Dilunga.

Dakika ya 30, Ruvu Shooting 0 - 0 Young Africans

Dk 28 Said Dilunga wa Ruvu anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Yanga.

Dk 25 Ruvu wanapata kona baada ya Cannavaro kuutoa mpira nje. Kona isiyo na madhara imepigwa.
Dk 23 Mbuyu Twite wa Yanga anachezewa faulo na Said Dilunga.

Dk 22 Cannavaro anamchezea rafu Said Dilunga wa Ruvu.

Dk 19 Yanga imeongeza mashambulizi langoni kwa Ruvu. YANGA 0-0 RUVU.

DK 15, Ruvu Shooting 0-0 Yanga

Dk 10 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amemchezea faulo Abrahman Musa wa Ruvu. Timu zinashambuliana kwa zamu.

Dk 8 Kipa wa Yanga, Ally Mustapha 'Barthez' anapangua shuti kali la Michael Aidan wa Ruvu lililopigwa kutoka nje ya eneo la hatari.

Dk 7 Frank Domayo wa Yanga anachezewa faulo na Ayoub Kitala wa Ruvu.

Dk 4 Hamis Kiiza wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa Ruvu akiunganisha pasi ya Nizar Khalfani lakini kipa Benjamin Haule anaudaka mpira.

Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya Ruvu Shooting Vs Young Africans

Wachezaji wa timu zote na watazamaji wamesimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha kocha na mchezaji wa zamani wa Pan African marehemu mzee Athuman Chilambo.

Young Africans line-up to face Ruvu Shooting today:
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Juma Abdul
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Mbuyu Twite
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Nizar Khalfani
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Said Mohamed
2.Shadrack Nsajigwa
3.David Luhende
4.Nurdin Bakari
5.Said Bahanuzi
6.Jerson Tegete
7.Didier Kavumbagu

RUVU SHOOTING: Benjamin Haule, Michael Aidan, Mau Bofu, Ibrahim Shaban, Mangasini Mangasini, Gideon Tepo, Ayoub Kitala, Ernest Ernest, Hassan Dilunga, Said Dilunga, Abrahman Musa

Friday, March 15, 2013

TAKWIMU ZA MATOKEO YA NYUMA YA TIMU ZILIZOPANGWA KUCHUANA KWENYE ROBO FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE - MOURINHO DHIDI WANAEReal Madrid vs Galatasaray
European Super Cup final -  August 25 2000 Final Galatasaray 2-1 Real Madrid

Champions League quarter-final - April 3 2001 Galatasaray 3-2 Real Madrid
Champions League quarter-final - April 18 2001 Real Madrid 3-0 Galatasaray

Paris Saint-Germain vs Barcelona
Champions League quarter-final - March 1 1995  Barcelona 1-1 Paris Saint-Germain
Champions League quarter-final - March 15 1995  Paris Saint-Germain 2-1 Barcelona
Club World Cup final - May 14 1997 Barcelona 1-0 Paris Saint-Germain

Bayern Munich vs Juventus
Champions League  group stage - October 10 2004 Juventus 1-0 Bayern Munich
Champions League  group stage - November 3 2004 Bayern Munich 0-1 Juventus
Champions League  group stage - October 18 2005 Bayern Munich 2-1 Juventus
Champions League  group stage - November 2 2005 Juventus 2-1 Bayern Munich
Champions League  group stage - September 30 2009 Bayern Munich 0-0 Juventus
Champions League  group stage - December 8 2009 Juventus 1-4 Bayern Munich

Málaga CF vs Borussia Dortmund
Hawajawahi kukutana

BAYERN MUNICH VS JUVENTUS, REAL VS GALA, BARCA DHIDI PSG, MALAGA VS DORTMUND - NANI KUTINGA NUSU FAINALI YA UCL


MADUDU YA LIGI KUU, MECHI ZINAONYESHWA LIVE TIMU HAZILIPWI. CHAMAZI INAONGOZA KWA DHULUMALIGI Kuu ya soka ya Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii katika viwanja tofauti tofauti, lakini kuna jambo moja linalokwenda ndivyo sivyo. Matangazo ya haki za televisheni ya ‘live’ yanayoendelea hayaendi inavyotakiwa.

Kama utagundua, mechi kadhaa za Azam FC zimekuwa zikionyeshwa ‘live’ kwenye Uwanja wa Chamazi bila kuzingatia baadhi ya mambo muhimu ikiwemo timu pinzani kulipwa haki za matangazo hayo bila kuzingatia uenyeji kama ilivyo kawaida.

Kwa muda mrefu klabu za Simba na Yanga zimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mechi zake hazirushwi ‘live’ bila kuwepo makubaliano maalum kutoka kwa chombo husika au kampuni yoyote inayotaka kufanya hivyo.

Sasa hali ni toifauti kwani mechi za Azam zinaonyeshwa live kutoka Uwanja wa Chamazi unaomilikiwa na timu hiyo iliyo chini ya makampuni ya S. S Bakhressa, mbaya zaidi bila kufuata haki za matangazo kwa klabu pinzani.MFANO HAI


Jumatano ya Februari 20, 2013 kwenye Uwanja wa Chamazi, JKT Ruvu ilikuwa mwenyeji dhidi ya Azam na matokeo yakawa Azam mshindi kwa mabao 4-0. Mchezo huu ulionyeshwa live na televisheni ya StarTV.

Inavyotakiwa, kabla ya mchezo huo ni lazima Azam, JKT na Kamati ya Ligi inayosimamia Ligi Kuu ya Bara zikubaliane juu ya uonyeshwaji huo wa moja kwa moja.

Mambo hayo yote yanatakiwa yawemo katika mkataba huru unaowezwa kuona na pande zote muda wowote inapohitajika kufanyika hivyo.STAR TV INALIPWA NA AZAM


Azam kwa kuzingatia kwamba inahitaji zaidi kutangaza bidhaa zake kupitia timu yake ya soka, imelazimika kuwa inailipa StarTV kiasi cha fedha kisichopungua Sh. 5 milioni ili mechi yake moja iweze kurushwa live na kituo hicho.

“Azam huwa wanatulipa ili tuweze kuonyesha mechi zao moja kwa moja. Kwa kweli mambo yanakwenda vizuri maana kwao inawasaidia kwa kujitangaza zaidi na sisi tunaingiza fedha kupitia matangazo hayo kuwa yamelipiwa na wao siyo sisi kuwalipa wao,” kilisema chanzo chetu kutoka StarTV.

Kwa kauli hii, ina maana StarTV haifanyi mazungumzo na klabu inayocheza Chamazi na Azam bali jukumu hilo linabaki kwa Azam wenyewe na klabu husika. Hapa kuna tatizo kwani, Azam haina haki ya 100% ya kurusha live mechi zake zinazochezwa Chamazi hata kama itakuwa mwenyeji.

AZAM YAKIRI KUILIPA STAR TV

Mmoja wa viongozi wa Azam ambaye hakupenda jina lake kutajwa, amesema kila mchezo wao unapokaribia hufanya mawasiliano na StarTV kisha kuwalipa kiasi cha fedha kisichopungua Sh. 5 milioni na mechi zao kuonyeshwa live.

“Sisi tunazungumza na StarsTV kisha tunawalipa gharama za kuonyesha mechi live, ambazo huwa kuanzia Sh. 5 milioni, bada ya hapo mechi inachezwa,” alisema kiongozi huyo na alipiulizwa kuhusu malipo ya klabu pinzani, alijibu:

“Hayo ya kuwalipa klabu pinzani mimi siwezi kukujibu lolote kwani hilo ni suala la watu wa timu moja kwa moja. Nadhani kama kungekuwa na tatizo wangetuzuia,” alisema kiongozi huyo.

JKT RUVU HAIKULIPWA

Baada ya kujiridhisha na maelezo ya Azam na StarsTV, mtandao huu uliwasiliana na mmoja wa viongozi wa JKT Ruvu ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake kwa sababu maalum, ambaye alisema timu yake haikulipwa haki za mechi kuonyeshwa live Februari 20, 2013 kwenye Uwanja wa Chamazi.

“Ndugu yangu, sikudanganyi mimi sikuona malipo yoyote kutokana na mechi ile kuonyeshwa live. Sijuhi labda kwa viongozi wenzangu yawezekna wao wamelipwa lakini kwa utaratibu wetu hapa, tungekuwa tumewasiliana na fedha kuletwa klabuni. Hivyo fedha hiyo ni kama haikulipwa,” alisema kiongozi huyo.

YANGA ILIKATAA MTEGO WA AZAM

Jumamosi Februari 23, 2013, Yanga ilicheza na Azam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Azam ilitaka mchezo huo uonyeshwe live na kulipa Yanga Sh. 10 milioni, lakini Yanga walikataa.

Katika mchezo huo ulioisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Haruna Niyonzima, mashabiki zaidi ya 36,000 waliingia uwanjani na kuingiza kiasi cha Sh. 250 milioni.

Yanga walikuwa wajanja zaidi kwa kuiona thamani yao na kukataa kiasi kidogo cha Sh. 10 milioni ambacho walitaka kulipwa ili mechi yao irushwe live.

KAMATI YA LIGI HAIJUI

Kwa kawaida, mechi yoyote inayotakiwa kuonyeshwa live, ni lazima makubaliano yake yafikiwe na timu zote mbili na kamati ya ligi. Vyombo vyote hivyo vina mgao wake wa fedha.

Mtandao huu ulipowasiliana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia kuhusu hali hiyo, alisema hayupo ofisini na ndiyo kwanza anarejea jijini Dar es Salaam, hivyo apewe muda wa kuwasiliana na wenzake ili kujua kilichotokea.

Lakini Karia alisema, kimsingi klabu zote mbili zinapaswa kukubaliana juu ya uonyeshwaji wa mechi na pia kamati nayo inapaswa kujua hali hiyo pia kufahamu kaisi cha fedha kitakachoingia kwao.

MGONGANANO WA MASLAHI BINAFSI

Mtandao huu, haukuweza kuzungumza na Mwenyekiti wa Azam ambaye ni pia ni makamu mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Said Mohamed kwani jambo hili lipo katika mgongano wa maslahi.

Mgongano huo wa maslahi kwa Said Mohamed unakuja kwamba, yeye ndiye anayepaswa kukubaliana kimaslahi kama mtendaji wa Azam na wakati huohuo akiwa kama kiongozi wa kamati ya ligi.

Hata kama kamati ya ligi ina wajumbe wengine, lakini Said Mohamed anachukua nafasi kubwa kama makamu mwenyekiti na pia kiongozi wa Azam, hivyo uaminifu unaweza kuwa mdogo kwa suala hili.

VIONGOZI HAWAJUHI HAKI ZA KLABU ZAO

Mara kadhaa unaweza kwenda uwanjani na kukuta mambo yanatendeka kinyume na matakwa au kanuni zinavyotaka. Mfano halisi ni hili la matangazo ya live.

Klabu inaweza kufika uwanjani na kukuta mechi inaonyeshwa live na wasiwe na wasiwasi wowote bila kujua kama wanapoteza haki yao ya kimsingi siku hiyo. Nayo ni kulipwa kwa kitendo cha wao kuonekana moja kwa moja.

Kote duniani na hata hapa bara, mechi yoyote ya live ni lazima timu zote mbili zilipwe haki zao tena kwa makubaliano maalum. Hapo kila timu itaangalia thamani yake na kukubaliana na fedha wanayotaka kulipwa.

Kwa Ligi Kuu ya Kenya, timu zote hupata kiasi kisichopungua Sh. 150 milioni (kwa thamani ya fedha ya Tanzania) kutokana na kituo cha Supersport kuonyesha mechi zao live. Hicho ni kiasi kikubwa katika kuiendesha klabu na kuweza kushindana kikamilifu.

Kumbuka hata wakati ule GTV ilipokuja nchini na kuingia mkataba wa kuonyesha live beedhi ya mechi za ligi kuu, kila klabu iliambulia kiasi cha fedha kwa kitendo chao cha kuonekana live.

KWA NINI MECHI ZA CHAMAZI TU?

Azam inacheza mechi zake za ligi kuu katika viwanja vingi chini, lakini mpango huu wa kuonyesha mechi zake live unatumika zaidi katika uwanja wa Chamazi, labda kwa sababu zifuatazo;

Kwamba, ni mbali ambako hata watu mbalimbali wadadisi wa mambo hawawezi kubaini tatizo na hata kuwashtua viongozi wa timu nyingine juu ya haki yao ya msingi ya kulipwa fedha hizo. Ukweli ni kwamba, watu wengi huwa hawaendi katika mechi za uwanja huo zinazochezwa katikati ya wiki.

Kitendo cha Azam kuwa mwenyeji wa uwanjani, kinawafanya timu pinzani kutokuwa na ujasiri wa kuuliza mambo mbalimbali ya yanayoendelea uwanjani hapo kwani unaweza kuziona kamera zaidi ya mbili uwanjani na ukadhani labda ni moja kati ya mipango ya Azam ya kurekodi mechi zake.

Ikumbukwe ya kuwa, ufahamu ya kujua kwamba mechi hii inaonyeshwa live au tofauti haupo kwa kila kiongozi wa timu za ligi kuu.

MSIMAMO WA MTANDAO HUU

Tunaipongeza Azam kwa kutaka kuonyesha live mechi zake zote inazocheza kwenye Uwanja wa Chamazi, lakini ni muhimu kwao kufuata kanuni kwa kuzilipa timu inazocheza nazo ili kufuta manung’uniko.

Viongozi wa klabu zote za ligi kuu kuacha kuona kila kitu ni kawaida kutokea kwani kuna wakati wanapoteza haki zao za msingi na kujikuta wakiendelea kulia na ukata wakati mianya ya fedha wanaiacha bila kujielewa.

Tunaiomba kamati ya ligi kufanya kazi kikamilifu kwa kuzingatia haki na kanuni za mambo yote yahusuyo ligi hiyo. Pia ifanye kazi kwa kwenda viwanjani na kusimamia mambo yote ya msingi kama haya ya mechi kuonyeshwa live.

Tuna imani hiki tulichokiandika kitafanyiwa kazi na kila upande uweze kupata haki zake stahiki.

Mwisho

ZFA YAITAKA TFF MEZA MOJA KUMALIZA TOFAUTI ZAO


CHAMA cha soka Zanzibar (ZFA) kimelitaka shirikisho la soka Tanzania (TFF) kukaa meza moja na serikali kumaliza tofauti zao.
Kauli hiyo imekuja, baada ya malumbano kati ya Serikali na TFF yaliyoibuka kwenye mchakato wa uchaguzi ambao umesimamishwa na Shirikisho la soka la Kimataifa (Fifa).
Fifa imesimamisha kufanyika kwa  Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa TFF, baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika kwenye shirikisho hilo na kutuma ujumbe kushughulikia kwa suala hilo.
Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Haji aliliambia Mwanaspoti jana jijini Dar es Salaam haoni sababu za msingi kwa viongozi wa TFF kurushiana maneno na serikali.
"Nafikiri TFF wakae meza moja na Serikali kumaliza tatizo hilo. Hilo ndilo jambo la msingi ambalo limebaki kwa sasa."
Naye Rais wa TFF, Leodgar Tenga jana alisema jijini Dar es Salaam kuwa TFF imepanga kukutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara Machi 19, mwaka huu.
"Waziri ameshatuahidi kuwepo kikao hicho kati yake na viongozi wa TFF kwa lengo la kumaliza tatizo lililopo." alisema Tenga.
Haji alisema TFF inatakiwa kuelewa kuwa Fifa ni wasimamizi wa mchezo wa soka, lakini haiwezi kuendesha mchezo wowote nchini pasipo serikali kutia mkono wake.

KOCHA WA YANGA: NAHITAJI USHINDI KWENYE MECHI TANO ZIJAZO

KOCHA wa Yanga, Mdachi Ernest Brandts amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanashinda mechi tano ikiwemo ya kesho dhidi ya Ruvu Shooting na kutwaa ubingwa kabla ya ligi kumalizika.
Yanga inaongoza ligi na pointi 45 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 37, bingwa mtetezi, Simba ni ya tatu na pointi 34.
Mholanzi huyo alisema jana jijini Dar es Salaam;"Nafikiri tuna nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu."
Alifafanua kuwa endapo Yanga itashinda mechi tano kati ya saba zilizobaki itafikisha pointi 60 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
"Tuna mechi saba mkononi, lakini tunatakiwa kushinda tano kati ya hizo kutawazwa mabingwa wapya wa ligi."
"Lakini, kama wachezaji wangu watabweteka, tunaweza kukashindwa kupata kile ambacho tulitarajia."
"Kwa hiyo, bado nasema Azam na Simba  ni wapinzani wetu wakubwa na wana nafasi ya kupambana na sisi katika kuwania ubingwa." alisisitiza kocha huyo.

BEKI WA YANGA NA UVIMBE WA SHAVU ALIODUMU NAO TANGU UTOTONI - AFANYIWA UPASUAJI SASA SAFI

Mbogo mwenye uvimbe
BEKI wa Yanga, Ladislaus Mbogo ameeleza kufurahi kuondokana na hali ambao ilikuwa ikimfanya kujihisi tofauti na wengine.
Mbogo alifanyiwa upasuaji kwenye uvimbe wa shavu la kushoto, Jumatano iliyopita katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Beki huyo aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Toto African ya Mwanza alisema;
"Furaha yangu kubwa ni kuondokana na hali ambayo nimekuwa nayo tangu utotoni wangu."
"Pia, ushirikiano ambao nimeupata kutoka kwa wachezaji wenzangu na viongozi wa timu yangu."
Mbogo alisema; "Hali ya uvimbe ilikuwa ikinifanya nijione tofauti na wengine na kunikosesha raha."
"Kubwa ambalo siwezi kulisahau ni shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Yanga kunitibu."
"Nadhani ni jambo la kuigwa na wengine kuwa na moyo wa kusaidia. Nimecheza Kagera na Toto African lakini hawakuweza kunitibu." alisema mlinzi huyo wa kati.
Kuanza mazoezi, Mbogo alisema amepewa wiki mbili ikiwa moja ya kutolewa nyuzi na nyingine kufuatiia hali ya jeraha hilo la upasuaji.
"Daktari amesema kwa sasa hawezi kuniambia siku wala tarehe ya kuanza mazoezi isipokuwa nimepewa wiki mbili kupewa jibu sahihi."
"Wiki moja itakuwa yakutoa nyuzi na nyingine atafuatilia hali yangu kujua kama nitakuwa tayari kuanza mazoezi mepesi." alisema Mbogo.

KOCHA MFARANSA WA SIMBA AWACHANA MASTAA AWAMBIA HAKUNA ALIYE JUU YA TIMU

KOCHA wa Simba, Patrick Liewig ametoa onyo kali kwa nyota wake kwa kusema hakuna mchezaji anayeweza kuwa juu ya timu hiyo.
Kauli hiyo imekuja, baada ya hali ya nidhamu kwa wachezaji wa Simba kuwa mbovu na kuchangia timu hiyo kupata matokeo mabaya kwenye ligi.
Mfaransa huyo alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa tatizo hilo ameona zaidi kwa wachezaji 'mafaza'
Hali ambayo imemlazimu kutumia wachezaji watano hadi sita vijana kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
"Nafikiri kama nidhamu itakuwa mbovu kwenye timu. Kamwe hatuwezi kufikia malengo ambayo tumejiwekea."
"Kwa hiyo ni sahihi kwangu kwenda na wachezaji ambao wananielewa ambacho wanatuma kukifanya uwanjani."
"Hakuna mchezaji anayeweza kuwa juu ya timu." alisema kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic.
Pia, alisema amefundisha soka katika klabu tofauti barani Afrika, lakini anashangazwa na jinsi wachezaji wa timu yake wanavyoendesha maisha yao ya soka.
"Kwa ninavyoelewa mchezaji anatakiwa  kujitambua na kuipenda kazi yake. Lakini ninachokiona hapa ni tofauti kabisa."
"Pia, timu kuwa nzuri ni lazima wachezaji wawe na nidhamu na ushirikiano wa pamoja bila kubaguana."
Hata hivyo, kocha huyo amewapumzisha nyota kadhaa wa timu hiyo kutokana na kutoridhishwa na viwango vyao pamoja na nidhamu.
Pia, Mfaransa huyo ameahidi kuendelea kuwatumia wachezaji vijana katika mechi zilizobaki kwenye ligi.

UZINDUZI WA REDS MISS TANZANIA ULIVYOFANAYANGA KUZIDI KUOSOGELEA UBINGWA AU KUPIGISHWA MWELEKA NA RUVU SHOOTING?

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Machi 16 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Yanga itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwamuzi Jacob Adongo kutoka Musoma mkoani Mara ndiye aliyepewa jukumu la kuchezesha mechi hiyo namba 146. Adongo atasaidiwa na Anold Bugado wa Singida na Milambo Tshikungu kutoka Mbeya wakati mwamuzi wa mezani ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.

Mtathmini wa waamuzi ni Army Sentimea wakati Kamishna wa mechi hiyo inayokutanisha vinara Yanga na Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya saba ikiwa na pointi 29 chini ya ukufunzi wa Charles Boniface Mkwasa na Msaidizi wake Selemani Mtungwe ni Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.

Pia TFF inawaasa washabiki wa mpira wa miguu kuacha kununua tiketi mikononi mwa watu kwa vile wanaweza kuuziwa tiketi bandia. Tiketi zote zitauzwa katika vituo vinavyotangazwa katika magari maalumu, na uwanjani pia katika magari hayo.

Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wenye uwezo wa kuchukua washabiki 25,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Toto Africans na Mgambo Shooting kutoka Tanga. Ugumu wa mechi hiyo unatokana na ukweli kuwa timu zote mbili zinapigana kuepuka kurudi zilikotoka (daraja la kwanza).

Mgambo Shooting inayonolewa na Mohamed Kampira inashika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 24 katika ligi hiyo yenye timu 14. Toto Africans ambayo iko nyumbani itaingia uwanjani ikiwa na pointi 14 katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.

Baada ya kulala 2-1 mbele ya Simba katika mechi iliyopita, Coastal Union itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro.

Ligi hiyo itaendelea tena keshokutwa (Machi 17 mwaka huu) kwa mechi moja itakayozikutanisha JKT Ruvu na Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Azam Complex.

TFF YAWACHINJIA BAHARINI WAPENDA KUINGIA BURE UWANJANI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeondoa utaratibu wa wadau wake kuingia bure kwenye mechi kwa kutumia tiketi maalum (free pass).

Kutokana na uamuzi huo hakutakuwa tena na pasi za bure kwa ajili ya kushuhudia mechi zilizo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa TFF katika viwanja mbalimbali nchini.

Uamuzi huo umetokana na ukweli kuwa free pass zimekuwa zikipunguza au kuchukua mgawo wote wa TFF kwenye mechi, na wakati mwingine Shirikisho hulazimika kutoa fedha za ziada kugharamia pasi hizo.

Pasi zote ambazo imekuwa ikitoa kwa wadau wake hukatwa katika mgawo wa TFF katika mechi husika. Shirikisho hivi sasa linapata asilimia nne tu ya mapato katika mechi za Ligi Kuu, ligi ambayo hivi sasa inaendeshwa na Kamati yake ya Ligi.

Thursday, March 14, 2013

VIWANGO VYA UBORA FIFA: TANZANIA YAPANDA DUNIANI NA AFRIKA- SPAIN YAENDELEA KUONGOZA


Mabingwa wa Ulaya na dunia Spain wameendelea kubaki nafasi ya kwanza kwenye viwango vya FIFA mwezi huu, wakati timu ya taifa ya Tanzania ikipanda kwa pointi nane zaidi, huku Afghanistan wakipanda mpaka kwenye nafasi ya 48 kutoka 141, baada ya kushinda mechi kadhaa kwenye AFC Challenge Cup.

Spain wanawaongoza Germany, Argentina, England na Italy. Colombia wapo nafasi ya sita huku Ureno wakishuka mpaka nafasi ya saba.

Pamoja na kubeba ubingwa Afrika, Nigeria bado haijapita Ivory Coast, huku ikishuka kidunia mpaka nafasi ya 13.


Msimamo ubora wa kidunia ukionyesha Tanzania impanda kwa nafasi nane

Rekodi za Tanzania kutoka mwaka 2010

Tanzania inashika nafasi ya 33 kwa ubora Africa katika Afrika Mashariki ikiwa imepitwa na Uganda pekee wanaoshika nafasi ya 22.

MAKALA: AZAM FC NDIO TIMU MKOMBOZI WA SOKA LA TANZANIA


Sikumbuki mwaka, mwezi wala tarehe, ninachokumbuka ilikua siku ya jumapili. Wakati natoka kanisani kuna ishara nyingi sana nilikutana nazo barabarani, ama kwa hakika ilikuwa siku special sana. Sikuweza kuendelea kufanya utafiti zaidi kutokana na hali yangu ya kiafya, kwa muda huo kichwa kilikua kinagonga huku nikiwa nahisi homa kali sana. Sikuwa na muda wa kupoteza tena njiani. Moja kwa moja nikaendelea na safari ya kuelekea nyumbani, kituo cha kwanza sebuleni huku machozi yakinilenga machoni, usishangae sana kipindi hiko nilikuwa na umri kati ya miaka 8 au 9. Mama yangu hakuwahi kupata mafunzo ya udaktari lakini hakukuwa na dokta mwaminifu kwangu kama mama. Akaacha kazi zake za jikoni na kuniletea dawa mezani sebuleni, sikuwa na haja wala sikumuuliza mama ni dawa gani, nikachukua maji yetu ya bombani na kusukuma dawa mdomoni, taraatibu nikaenda kupumzika kitandani.

Kikosi cha zamani cha simba

Huku nikiwa nasikilizia homa na kichwa kitandani, nikaanza kuvuta taswira ya niliyokutana nayo barabarani, ooops usingizi ulinichukua wakati naanza kutafakari. Sikumbuki baada ya muda gani tangu kuchukuliwa na usingizi. Nikashtushwa kwa kelele kali, nikaamka na kuanza kukimbia huku nikijiuliza ni mwizi au Nyumba Inaungua? Baada ya kufika nje ya kibaraza chetu nikakuta watu wengi sana, wengine wanashangilia wengine wamenuna, nikamuona mama amevalia tisheti nyeupe na kanga nyeupe iliyokuwa na vidoti vya rangi nyekundu Akifurahi na kushangilia sana. Nikatupia jicho upande wa pili nikamuona mzee amevalia tisheti ya njano yenye picha ya mtu fulani hivi Iliyoandikwa Chagua Mkapa, Chagua CCM. Mzee alikuwa amekaa karibu na radio kubwa, ungemuangalia kwa karibu ungelifikiri ni Dj, maskini baba alikuwa na sura ya huzuni sana.


Nikashindwa kuelewa hapa kuna msiba au sherehe? Baba amenuna mama anacheka. Mara watu wote waliokuwa wakishangilia wakanyamaza na kutegesha masikio yao kwenye uelekeo wa radio. Moja kwa moja na mimi nikafanya vivyo hivyo, ikasikika sauti ya mtangazaji mmoja wa RTD sikumbuki kama alikuwa Swedi Mwinyi au Juma Nkamia ikisema “Ni Yule Yule, kwa mara nyingine, Joseph Kaniki anaiandikia Simba bao la kuongoza, Simba moja Yanga sifuri” Waliovaa nyeupe na nyekundu wakapiga mayowe kwa kitambo, huku waliovaa njano na kijani wakiinamisha vichwa vyao chini. Hapo ndipo nilipojiwa na kumbukumbu ya kuwa kulikuwa na mechi kati ya Simba na Yanga. Nikakumbuka bendera za njano na nyekundu zilizokua zinapepea kila kona ya mtaa kipindi natoka kanisani. Nikakumbuka watu jinsi walivyokua wanabishana kila nilipokatiza. Hakika si Mama na Baba yangu peke yao waliyosimamisha kazi zao, bali nchi yote ilisimama.


wachezaji wa zamani


Miaka ya karibuni, mechi ya Simba na Yanga imepoteza mvuto. Ule umati uliokusanyika mbele ya kibaraza chetu utaukuta kwenye msiba au sherehe na si mechi ya Simba na Yanga.


Utawala wa Simba na Yanga umefanya ligi yetu isiwe na mvuto na kupelekea watu kupoteza hamu ya kupenda ligi yetu na mechi ya watani kwa ujumla. Leo hii mama yangu hana muda hata wa kuangalia wala kusikiliza mpira. Mzee ndio kabisa ameshasahau kama kuna kitu kinaitwa Simba na Yanga hapa Tanzania. 

Unajua kwanini League ya Uingereza inapendwa? Kabla ya Barclays premier league mwaka 1992/93 mwaka mmoja nyuma Arsenal na Liverpool walichuana vikali kugombea ndoo ya ligi. Lakini kwenye msimu wa kwanza wa Barclays ni Aston villa waliokua wanatishia ndoto za Fergson na vitoto vyake kuchukua kombe hilo kwa mara ya kwanza. 

Kumbuka Man United walivyokuwa wanasubiria kombe hilo kwa miaka 26, na Fergi kwa miaka 6. Waliwaacha Aston Villa kwa point 10 na kukata kiu yao huku Norwich City ikikamata nafasi ya tatu, msimu uliofuata mambo yakawa tofauti kwa Villa na Norwich baada ya Blackburn na The magpies Newcastle kuwaondoa kwenye namba 2 na 3, 1994/95 mambo yakawa tofauti si Man u, Leeds, Liverpool wala Nottingham Forest aliyethubutu kuchukua kombe hilo mbele ya paka weusi(Blackburn Rovers), huku Alan Shearer akifikia rekodi ya Andy cole ya kufunga magoli mengi kwenye league kwa msimu mmoja magoli 34, na rekodi hiyo haijavunjwa mpaka hii leo.

Arsenal ilipoteana kabisa, ikaja kuibuka msimu wa mwaka 1995/96 kwa kushika nafasi ya nne na msimu unaofuata kukamata namba tatu, kabla ya kuchukua ubingwa msimu wa mwaka 1997/98, Hapo utaona kupanda na kushuka kwa timu nyingi sana. Ndani ya ligi kuna mechi ngumu na nzuri ukiacha mechi za watani. Pia kwenye ligi hiyo kuna timu nyingi zenye uwezo wa kuchukua ubingwa. 

Kwanini usipende ligi yao? Unayo kila sababu ya kuipenda, hata mimi naipenda sana. Wakati huo watu wana hamasa kubwa ya mechi ya Simba na Yanga kulikua na Timu ya Mtibwa sugar iliyotoka kuwa bingwa mara mbili mfululizo miaka ya mwisho ya karne ya 20. Angalau kulikua na mechi ya Mtibwa vs Simba au Yanga kabla ya mechi ya watani. Wakaja Moro wakapotea. Na Sasa ni Zamu ya Azam FC kuturudisha tena kwenye Ligi ya bongo.Timu hii ya Azam ilianzishwa mwaka 2007 na wafanyakazi wa kiwanda cha Bakhresa kama timu ya mazoezi. Shukrani zimuendee Yusuph Bakhresa aliyekuwa na maono ya kuwa na timu ya mashindano. Kwa hekima maarifa na nguvu ya pesa msimu wa mwaka 2008/09 kwa mara ya kwanza Azam wakashiriki ligi kuu na kumaliza kwenye nafasi ya 8. Msimu uliofuata wakakamata nafasi ya tatu. Msimu uliyopita wakamaliza nafasi ya pili na kujikatia tiketi ya kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa na mpaka sasa ni timu pekee ya Bongo iliyobaki kwenye mashindano hayo baada ya timu nyingine kuondolewa kwa vipigo vya mbwa mwizi. Achana na Simba na Yanga, Azam ina uwanja wa kisasa na Academy bora kabisa ya soka nchini bila kusahau gym na hostel za bei mbaya.


Azam si timu ya siasa, Mzee Bakhresa ana dhamira na nia ya dhati ya kufanya yaliofanywa na Motsepe na Katumbi. Nashukuru juzi niliungana tena na mama yangu kuangalia mechi ya Azam na Al Nasri, ni takribani miaka kumi imepita tangu mama kuangalia mechi. Ama kwa hakika amesikia sifa za Azam, na bila shaka anaipenda na kuishabikia Azam. Ahsante Azam kwa kumrudisha Mama kwenye Ulimwengu wa soka, najua si mama pekee aliyerudishiwa hamu ya kupenda mpira wa bongo. Soka letu sasa linapata afya kutoka kwa Azam. Watanzania Tunajivunia kuwa na Azam. Na mimi najivunia kua mshabiki wa Azam.Timu moja, hatima moja Azam fc kwa ajili yangu na kwa ajili yako


By kaijage jr……

Middle ya juu


KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA KAMPENI MPYA YA TUPO PAMOJA.Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo akiongea na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bia ya Serengeti ya "Tupo pamoja
katika shangwe za mafanikio" hii leo
Ratiba

Machi 14, 2013, JB BELMONTE, DAR ES SALAAM:   Leo katika hafla iliyohudhuriwana waandishi wa habari, wageni na wadau mbalimbali Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni mpya na ya kipekee inayoenda kwa kauli mbiu ya TUPO PAMOJA.  Katika hafla hiyo iliyofana asubuhi ya leo pia ilihudhuriwa na wadau wa bia hii katika ishara ya kushereheka mafanikio na shangwe za bia hii.

Akiongea na waandishi wa habari asubuhi la yeo, Mkurugenzi wa mMasoko wa kampuni ya bia Serengeti Bw. Ephraim Maguru alisema kwamba, “ kwa miaka kumi saa, tumeona na kushuhudia ukuaji na mafanikio makubwa”.  Bia hii inajulikana kwa kampeni ya ‘raha kamili kwa wengi wanaifahanu kama Chui.  Pia kwa udhamini wa Taifa stars ambao uliinua hadhi ya soka la Tanzania kwa kiwango kikubwa.  Kuna ufadhili wa Fiesta, ambao wote mnajua mchango Fiesta inatoa katika ukuaji wa tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini.  Aliendelea Bw. Mafuru

 Bia ya Serengeti ni bia ya kipekee ambayo ndio bia ya kwanza Tanzania yenye kimea halisi kwa asilimia mia.    Mwaka jana bia hii pia ilizindua muonekano mpya  wa nembo yake huku ikibaki na ladha ile ile.  Baada ya utafiti, Kampuni ya bia ya Serengeti na wadau wake, wamebaini kwamba watanzania wanahitaji  shangwe za mafanikio yao katika sekta mbalimbali zikiwemo za uchumi, kijamii, kimichezo na kadhalika.

“Tunawakaribisha wote katika hafla mbali mbali ambazo tutaandaa ili kueneza kampeni hii ya Tupo Pamoja kama mlivyoona katika matangazo niliyowaonyesha, tutaleta shangwe popote mlipo., Alieleza meneja wa kinywaji hicho Bw. Allan Chonjo,  baada ya kuonyesha matangazo mbali mbali yatakovyokuwa katika vyombo vya habari.

Hafla hiyo ya uzinduzi pia ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Kampuni ya bia ya Serengeti wakiwemo wasambazaji wa bia.  Kampeni hii inawatambua na kuwathamini  watanzania wote  kwa mafanikio yao katika sekta mbalimbali za maendeleo.


Kampuni ya bia ya bia ya Serengeti inajihusisha na biashara ya  vinjwaji vyenye vileo  kama bia- Premium Serengeti Lager, Tusker Lager, Tusker Malt Lager, Tusker Lite, Uhuru Peak Lager, Pilsiner,  Guinness na vinywaji vikali kama  Johnnie Walker, Smirnoff Vodka, Richot, Bond 7 and Gilbeys. Pia vinywaji visivokuwa na kileo kama Malta Guinness
Serengeti Breweries Limited is subsidiary of EABL/ DIAGEO.


Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkurugenzi wa Mawasilianao na Mahusiano  SBL: Email: evans.mlelwa@serengetibrew.com Meneja Mawasiliano- SBL   imani.lwinga@serengetibrew.com

KALI YA LEO!

BREAKING NEWS: RIO FERDINAND AITWA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND BAADA YA MIEZI 21

Hatimaye baada ya kutoswa kwa muda mrefu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England Rio Ferdinand ameitwa tena kwenye kikosi hicho na kocha Roy Hodgson. Ferdinand hajaichezea England tangu June 2011 chini ya boss wa zamani Fabio Capello

HIKI NDIO KIKOSI KIZIMA CHA ENGLAND KILICHOITWA KWA AJILI YA MECHI ZA World Cup 2014 qualifiers dhidi San Marino na Montenegro.


GOALKEEPERS
Hart, Foster, Forster.

DEFENDERS
Baines, Cahill, A Cole, Dawson, Ferdinand, G Johnson, Smalling , Walker.

MIDFIELDERS
Carrick , Cleverley, Gerrard, Lampard, Lennon, Milner, Osman, Parker, Oxlade-Chamberlain, Walcott, Young.

FORWARDS
Defoe, Rooney, Sturridge, Welbeck.

MUSSA MGOSI: NIPO TAYARI KURUDI SIMBA MSIMU UJAO

MUSSA Mgosi amesema anaweza kurejea Simba kama watampa fedha nzuri msimu ujao  na amedai timu hiyo bado ina nafasi ya kutwaa nafasi moja za juu.
Mgosi ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio msimu wa 2009 alisema kuwa timu yoyote itakayomuhitaji kwenye ligi yuko tayari ili mradi maslahi yawe mazuri.
Mimi nacheza popote, iwe Simba, Oljoro zote sawa tu ili mradi maslahi nitakayotaka yawepo" alisema.
Akizungumzia mwenendo wa Simba kwenye Ligi Kuu Bara, Mgosi alisema bado ina nafasi ya kuchukua nafasi tatu za juu kama watafanya maandalizi mazuri kwa mechi zilizobaki.
"Siwezi kujua maandalizi yao zaidi ya kuisikia tu au kuwaangalia katika baadhi ya mechi, sijui wamejipangaje, lakini mimi naamini kabisa kama watajiandaa katika mechi zilizobaki basi nafasi mbili za juu moja watachukua.
" Ujue hiii ni ligi huwezi kujua ya mbele, unaweza ukawa juu ya mwenzako sasa hivi lakini ukaja kushangaa mwenyewe baadae mambo yamebadilika hivyo Simba bado wana nafasi, watu waache kuwasema sema sana" alisema Mgosi.
Aliongeza:"Simba na Yanga ni timu kubwa ina mashabiki wengi na hakuna shabiki ambaye anapenda timu ipate matokeo mabaya, hivyo yanapotokea matatizo kama haya yanayokumba Simba, mchezaji kama mchezaji anatakiwa afanye kazi yake ipasavyo ili kujiepusha na matatizo hayo, bado naamini wanaweza kutoka mahali walipo na kupanda juu zaidi" alisema Mgosi.

SIMBA HAKIELEWEKI: HUKU KEITA AKIDAIWA KUTOROKA - MAFTAH NA NGELEMA WAGONJWA

SIMBA inakabiliwa na tatizo la beki wa kushoto baada ya mabeki wake wote wa kikosi cha kwanza kuwa majeruhi.
Timu hiyo ina mabeki wa kushoto wawili Amir Maftah na Paul Ngalema ingawa Shomari Kapombe naye humudu kucheza nafasi hiyo.
Maftah anasumbuliwa na 'enka' wakati Ngalema anauguza goti ingawa mwenyewe amekiri kuwa hivi sasa yuko fiti na anasubiri ruhusa ya daktari wa timu kuanza mazoezi mepesi.
Kutokana na tatizo hilo kocha Patrick amelazimika kumchezesha kinda Miraji Adam nafasi hiyo.
Lakini licha ya kudaiwa Maftah ni mgonjwa tangu acheze mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Libolo nchini Angola kuna taarifa za ndani zinadai mchezaji huyo amesimamishwa huku ikidaiwa kuwa kocha Liewig amepanga kutowatumia baadhi ya wakongwe katika michezo iliyobaki kutokana na nidhamu zao kuwa mbovu.
Kapombe ambaye humudu kucheza nafasi hiyo ya beki wa kushoto hawezi kutumika katika nafasi hiyo hivi sasa kutokana na mkanganyiko uliopo Simba hivi sasa hasa katika beki wa kati baada ya Juma Nyoso kuwa na kadi nyekundu huku Komanbil Keita raia wa Mali akitoroka katika timu hiyo na kuzima simu hivyo Kapombe hana budi kucheza nafasi ya beki wa kati kwa sasa.
Ngalema alisema kuwa hivi sasa anaendelea vizuri na ataanza mazoezi muda si mrefu lakini kwanza anasubiri ruhusa ya daktari ingawa aligoma kuhusisha ugonjwa wake na mambo ya kishirikina.
"Mimi naumwa kawaida tu,ingawa nimekaa muda mrefu lakini si kama nimelogwa, ingawa hayo mambo ya kishirikina yapo kwenye soka la bongo lakini huu ugonjwa wangu ni wa kawaida tu na hauhusiani na mambo hayo"alisema Ngalema ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Ruvu Shooting.

TFF YATOA USHAHIDI KUHUSU FIFA KUTISHIA KUIFUNGIA TANZANIA - TENGA AWATAKA WADAU KUWA WATULIVU

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amewataka wadau wa mchezo huo kuwa watulivu kwa vile tofauti zilizojitokeza kati ya Shirikisho na Serikali zitamalizwa kwa taratibu za mpira wa miguu.

Amesema nia ya TFF ni kuhakikisha Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) haliifungii Tanzania kwani tayari Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alishaahidi kuwepo kikao kati yake na viongozi wa TFF kitakachofanyika Jumanne (Machi 19 mwaka huu).

“Suluhu itapatikana kwa mazungumzo kati ya Wizara na TFF. Naamini suala hili tutalimaliza baada ya kikao cha Machi 19 ambacho kimepangwa na Waziri kutokana na maombi ya TFF,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa tatizo lilianzia kwenye mchakato wa uchaguzi ambao umesimamishwa na FIFA.

FIFA ilisimamisha Mkutano Mkuu wa uchaguzi baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika, na yenyewe kuahidi kutuma ujumbe wa kushughulikia suala hilo.

Rais Tenga amesema lisingetokea tatizo hilo, TFF tayari ilishaitisha Mkutano Mkuu ambao ungefuatiwa na uchaguzi. Lakini kwa vile FIFA ndiyo iliyosimamisha mkutano huo, TFF inalazimika kusubiri hadi FIFA itakaposhughulikia suala hilo na kutoa maelekezo ikiwemo lini mkutano ufanyike.

Amesema kwa kuamini tatizo hilo litamalizwa ndani ndiyo maana TFF hadi sasa haijapeleka FIFA maagizo ya Waziri Dk. Fenella ya kutengua marekebisho ya Katiba ya TFF ya mwaka 2012, kuitisha Mkutano Mkuu wa marekebisho ya Katiba na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, kwani ingefanya hivyo Tanzania ingefungiwa mara moja.

TFF inasisitiza kuwa FIFA ilijua tatizo la Serikali kutoa maagizo kwake kupitia vyombo vya habari, hivyo kumuandikia Rais Tenga na kueleza msimamo wake iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia uendeshaji wa shughuli za mpira wa miguu.

Uhalali wa kuwepo kwa barua ya FIFA kwenda kwa Rais Tenga juu ya suala hilo ulihojiwa pia na mwandishi wa Reuters, Brian Homewood baada ya kusoma kupitia vyombo vya habari nchini kuwa Shirikisho hilo huenda likaifungia Tanzania ikibainika Serikali inaingilia shughuli za TFF. Mawasiliano kati ya FIFA na mwandishi huyo ambapo majibu yake pia TFF ilipewa nakala yameambatanishwa katika taarifa hii.

BARUA YA FIFA
Dear Brian,

Thanks for your message.

We can confirm that FIFA Secretary General Jérôme Valcke has sent a letter to the President of the Tanzanian Football Federation, Leodegar Tenga, concerning alleged governmental interference in the internal affairs of the TFF.

FIFA is in contact with the TFF President who is optimistic that the matter can be sorted out within TFF, FIFA and the Tanzanian authorities. Furthermore, we can confirm that FIFA is also planning to send a mission to assess the situation with regard to the electoral process as soon as the current matter of alleged interference has been clarified.

Kind regards

FIFA
Media department
Enquiries: media@fifa.org
Twitter: @fifamedia    YouTube/FIFAtv

USHINDI WA BARCELONA NA UCHAGUZI WA PAPA


Wakati wa uchaguzi wa Papa mwaka 1958, Barca waliwatandika wapinzani wao Real Madrid 4-0 kwenye La liga. Angelo Roncalli - John XXIII aliteuliwa kuwa Papa.
 

Mwaka 1978 wakati wa uchaguzi wa Papa, Barca tena iliiwanyamazisha Las Palmas  kwa bao 4-0...John Paul II aliteuliwa Papa.
 
Na mwaka huu wakati maaskofu wa kanisa katoliki wakiwa kwenye uchaguzi wa Papa, Barca waliwaadhibu AC Milan 4-0...

PICHA YA SIKU!

MALAGA YAINGIA ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA FC PORTO MABAO 2:0

ARSENAL YAIFUNGA FC BAYERN MABAO 2:0 LAKINI YASHINDWA KUFUZU ROBO FAINALI

Wednesday, March 13, 2013

UCHAMBUZI: HAKUNA TIMU AMBAYO INGETOKA NA USHINDI NOU CAMP JANA KAMA BARCA INGECHEZA KAMA ILIVYOCHEZA JANA DHIDI YA MILANMASWALI MENGI YALIULIZWA KUHUSU UWEZO WA BARCELONA HUKU WENGI WAKIONA KAMA ZAMA ZA UTAWALA WAO ZIMEKWISHA NA ILIKUWA INAONEKANA KAMA ZAMA HIZO ZIMEFIKIA UKOMO BAADA YA KUONDOKA KWA TITO VILANOVA . BARCELONA HATA HIVYO WAMEDHIHIRISHA KUWA BADO WAO NI BORA NA WAMETOA UKUMBUSHO MUHIMU WA UWEZO WAO KWA KUWAFUNGA AC MILAN BILA HURUMA KWA MABAO MANNE BILA NA WANABAKI NA NAFASI KUBWA YA KULIPA KISASI KWA REAL MADRID KWENYE LIGI YA MABINGWA ENDAPO TIMU HIZO ZITAKUTANA .

WAKIWA NA MALENGO DHAHIRI KABISA , BARCELONA WALIONYESHA DHAMIRA YA KUSHINDA MCHEZO WA JANA TANGU DAKIKA YA KWANZA NA WALICHEZA WAKIWA NA KITU WANACHOTAKA ZAIDI YA KUJARIBU KUPITA REKODI YA KUPIGA PASI MIA TANO ZAIDI YA WAPINZANI WAO. SI KITU CHA KUSHANGAZA KWA MILAN , ILA BARCA KWA NJAA WALIYOONYESHA NA MASHABIKI WAO WAKIWASHANGILIA SANA WALIFANYA MAISHA KUWA MAGUMU KWA WACHEZAJI WA MILAN HASA IGNAZIO ABATE AMBAYE RAFU YAKE KWA PEDRO NA PASI ILIYOKUWA IKIRUDI NYUMA ALMANUSRA VILETE BALAA JUU YA BALAA HUKU IKIWA IMEPITA ROBO SAA TU BAADA YA KUANZA KWA MECHI.

KITU AMBACHO KINAWEZA KUWA KIMEWAVURUGA MILAN HASA ABATE NI MPINZANI AMBAYE HAKUMTARAJIA KWENYE MCHEZO WA JANA. WAKATI DAVID VILLA MARA NYINGI HUWA ANACHEZA KUSHOTO WAKATI AKIANZA NA MESSI NA PEDRO , ILIKUWA KASI KUBWA YA PEDRO AMBAYO ILIMVURUGA ABATE . ZAIDI YA HAPO , YALIKUWA MAAMUZI YA KUFANYA MABADILIKO HAYO AMBAYO YALIWALIPA BARCA AMBAPO VILLA ALICHEZESHWA KAMA MSHAMBULIAJI WA KATI AMBAYO YALIITIKISA BEKI YA MILAN.

AKIWA HAYUKO KWENYE KIWANGO CHAKE CHA JUU KAMA ALIVYOZOELEKA BAADA YA KURUDI TOKA KWENYE MAJERAHA , DAVID VILLA HATA HAKUGUSA MPIRA KWENYE KIPINDI CHA KWANZA LAKINI ALIKUWA AMEFANYA MAMBO MENGI SANA NYUMA YA MATUKIO YAANI BEHIND THE SCENES . UWEPO WAKE KATIKATI YA ZAPATA NA MEXES ULICHANGANYA JINSI MILAN WALIVYOKUWA WAMEJIPANGA NA WAKAMSAHAU MESSI AMBAYE JANA ALIKUWA NYOTA WA MCHEZO . HUKU XAVI AKIWA AMEREJEA KWENYE KIUNGO CHA KATI KUONGOZA SAFU YA BARCA , MASSIMO AMBROSSINI NA MATHIEU FLAMINI WALIKUWA BUSY MUDA WOTE WAKIMCHUNGA XAVI NA HILI LILIMUACHA MESSI AKIWA HURU NA KUPATA NAFASI KUBWA SANA YA KUFANYA ATAKAVYO NA MPAKA WAKATI MILAN WANAPUMZIKA TAYARI MESSI ALIKUWA AMESHAFANYA MADHARA MAKUBWA . MAAMUZI YA KUTOTUMIA NAMBA TISA WA UONGO YALIWASADIA BARCA .

KWA BARCA KUONDOKA WAKIWA HAWAJAFUNGWA NI KITU MUHIMU SANA KWA BARCA KUFUZU ROBO FAINALI. PAMOJA NA FITNESS YA MASHAKA YA PUYOL , JAVIER MASCHERANO NDIO ALIKUWA CHAGUO SAHIHI KWENYE SAFU YA ULINZI KWA JANA . AKIWA ANACHEZA JUU HUKU AKITAMBUA KUWA KUNA HATARI YA KUKAMATWA KWENYE MASHAMBULIZI YA KUSHTUKIZA AMBAYO YALIWACOST SANA KWENYE MECHI MBILI DHIDI YA MADRID , MASCHERANO AMBAYE KIUMRI NI MDOGO NA BADO ANAMUDU KASI YA VIJANA WA MILAN PAMOJA NA UWEZO WAKE WA KUJIWEKA KWENYE NAFASI NZURI ILIISAIDIA SANA BARCA .

KUKOSEKANA KWA KWA GIAMPAOLO PAZZINI KULIWASAIDIA BARCA LAKINI MBADALA WAKE M’BAYE NIANG ALMANUSRA AWAHARIBIE BARCA . KUANZA NA MATHIEU FLAMINI , AMBROSINI , BOATENG NA RICARDO MONTOLIVO KWENYE SAFU YA KIUNGO KULIMAANISHA KUWA MILAN WALIKUWA WANATEGEMEA ZAIDI COUNTER . NIANG ALIWEZA KUIZIDI MBIO SAFU YA ULINZI YA BARCA WALAU MARA MOJA AKIWA NA NAFASI BORA YA MILAN KULIKO ZOTE LAKINI HAKUWEZA KUHIT TARGET NA HAPO ULIONA KABISA MILAN HAWAKUWA NA CHAO KWA USIKU WA JANA.

BAO LA MILAN LINGEMAANISHA KUWA BARCA WANGEHITAJI MABAO MATATU ZAIDI KUSONGA MBELE , BADALA YAKE MESSI HAKUNGOJA MUDA MREFU BAADA YA NIANG KUKOSA BAO NA AKASAWAZISHA KWENYE AGGREGATE SCORE .

ILIKUWA SUALA LA MUDA TU KABLA BAO LA USHINDI HALIJAFUNGWA . MASSIMIALIANO ALLEGRI ALIMUINGIZA ROBINHO , SULLEY MUNTARI NA BOJAN KRIKIC KWA MARA YA MWISHO KUJARIBU BAHATI YA MILAN NA ROBINHO ALITENGENEZA NAFASI AMBAYO MILAN WANGEWEZA KUPATA GOLI . LAKINI JORDI ALBA ALIWAMALIZA MILAN . DAVID VILLA NA JORDI ALBA WALIMALIZA MILAN NA KUUA MATUMAINI YOYOTE WALIYOKUWA NAYO YA KUSONGA MBELE .

BARCELONA WALIONYESHA DHAMIRA KUBWA NA HALI YA KUJIAMINI NA HILI LILIWAFANYA WADHIHIRISHE UWEZO WAO. HESHIMA NA HADHI YA BARCA ILIREJESHWA RASMI NOU CAMP . AC MILAN WALIHISI KUWA WALIFANYA UZEMBE LAKINI SI HIVYO , SIDHANI KAMA KUNA TIMU AMBAYO INGEWEZA KUTOKA KAMA BARCA WAKICHEZA KAMA WALIVYOCHEZA JANA.

BARCELONA NA TIMU NYINGINE ZILIZOWEZA KUENDELEA MBELE KWENYE HATUA YA MTOANO BAADA YA KUPOTEZA MECHI YA KWANZA KWENYE CHAMPIONS LEAGUE


Kwa ushindi wao 4-0 victory katika hatua ya 16 bora dhidi ya AC Milan, FC Barcelona imekuwa timu ya tano kwenye historia ya Champions League kushinda kwenye hatua ya mtoano baada ya kufungwa kwenye mechiya kwanza kwa bao 2 au zaidi - na timu ya kwanza kufanya hivyo bila kunufaika na goli la ugenini. Hizi ni timu nyingine zilizowahi kupata matokeo mazuri baada ya kufungwa kwenye mechi ya kwanza.

 
AC Milan 4-1 RC Deportivo La Coruña
RC Deportivo La Coruña 4-0 AC Milan
2003/04 robo fainali
Walter Pandiani aliipa uongozi Deportivo San Siro, lakini mambo yalibadilika mpaka kufikia full time, huku Kaká akifunga mara mbili na kuikata maini Deprtivo. Kuelekea kwenye mechi ya marudiano kwenye dimba la Riazor, kocha wa Deportivo Javier Irureta alikuwa hana matumaini yoyote zaidi ya ndoto.
Lakini kwa maajabu, mpaka kufikia mapumziko kikosi cha Depor kilikuwa mbelel kwa aggregate, Pandiani, Juan Carlos Valerón na Alberto Luque waliipa uongozi wa 3-0, baadae mchezaji aliyetokea benchi Fran González aliongeza goli la nne dk 76 na mwishowe wakapita kuingia nusu fainali. 

 
Real Madrid CF 4-2 AS Monaco FC
AS Monaco FC 3-1 Real Madrid CF
2003/04 robo fainali
Matumaini yoyote yaliyokuwepo kwa Monaco kwenda nusu fainali yalipotea baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa pale Santiago Bernabeu tarehe 24 March 2004. Mabao manne ya Madrid mpaka kufikia half time yalishawakatisha tamaa, lakini bao la dakika 83 kutoka Fernando Morientes kwa Monaco lilileta matumaini. Kocha Didier Deschamps akagoma kukubali kutolewa mapema. 

Kwenye mechi ya pili wakatanguliwa lakini Ludovic Giuly akasawazisha, Morientes akiwa Monaco kutoka mkopo Madrid akaongeza la pili na Giuly akapiga la tatu na kufanya matokeo yawe 3-1. Hatimaye magoli ya ugenini yakaipitisha Monaco kwenda nusus fainali. 


Chelsea FC 3-1 FC Barcelona
FC Barcelona 5-1 Chelsea FC (aet)
1999/2000 robo fainali
Kabla ya utawala wa Roman Abramovich, Chelsea hawakuwa na nguvu kama waliyonayo hivi sasa, na ushindi wao wa kwenye mechi ya kwanza robo fainali dhidi ya kikosi cha Louis van Gaal cha Barcelona – mabao ya Gianfranco Zola na mawili ndani ya dakika nne ya Tore André Flo yakiwapa kifua mbele vijana wa  Gianluca Vialli. Mechi ya pili kibao kikawageukia watoto wa darajani, Barcelona iliyoundwa na akina Rivaldo, Figo, Kluveirt na wenzao wakiwa mbelel ya mashabiki wao 90,000 wakaiadhibu Chelsea 5-1 kwenye ulioenda mpaka extra time.

 
SSC Napoli 3-1 Chelsea FC
Chelsea FC 4-1 SSC Napoli (aet)
2011/12 hatua ya 16 bora
Hii ndio mechi ya mwisho kwa Andre Villas Boas kwenye champions league ambapo Chelsea walishushiwa kipigo cha mabao 3-1 mjini Naples; Juan Mata alifunga bao muhimu baada ya Ezequiel Lavezzi kufunga mara mbili na Edinson Cavan kupiga moja, wakimuacha Villas Boas akisema kwamba bao la ugenini linaweza likawapa nafasi ya kusonga mbele kwenye mchezo wa marudiano.  

Kwa bahati mbaya, Mreno huyo hakupata bahati ya kuiongoza Chelsea kwenye mechi ya marudiano alitimuliwa nafasi yake ikachukuliwa na Roberto Di Matteo kwenye mchezo huo ambao Didier Drogba, John Terry and Frank Lampard waliibeba Chelsea kusonga mbelel katika mechi iliyoenda mpaka kwenye muda wa ziada.

MJADALA:KWELI FIFA INAWEZA KUFANYA MAAMUZI KUTOKANA NA HABARI ZA MAGAZETINI ?

TAKWIMU: REAL MADRID HAIJAWAHI KUPOTEZA MECHI YA LA LIGA AMBAYO RONALDO AMEFUNGA

Takwimu zinaonyesha kila ambapo Cristiano Ronaldo anapofunga, Real Madrid haijawahi kupoteza mchezo kwenye mechi ya La Liga. RONALDO mpaka sasa amefunga kwenye mechi 79 za la liga tangu ajiunge na Real, na katika mechi hizo  Madrid imeshinda 75 na nne zilizobakia ziliishia kwenye suluhu


Pia takwimu nyingine zinaonyesha kwamba Ronaldo amekuwa akiimarika kila msimu, idadi ya magoli aliyoyafunga kutoka January 1st mpaka March 11th ndani ya mwaka huu, yamezidi idadi ya magoli ambayo ameyafunga katika miaka mengine kutokea mwaka 2004 mpaka 2012.


CRISTIANO GOAL-SCORING STARTS
Year Goals*
2004 1
2005 5
2006 6
2007 5
2008 12
2009 7
2010 8
2011 12
2012 15
2013 19
* Goals scored between 1st January and 11th March