Search This Blog

Saturday, September 22, 2012

LIVE MATCH CENTRE: YANGA 4 - 1 JKT - AZAM 1-0 MTIBWA

 Mpira umemalizika, Young Africans 4 - 1 JKT Ruvu
Cannavaro dkk 4
Didier dkk 31, 65
Msuva dkk 53



 FULL TIME: Kutoka Chamazi Azam 1 - Mtibwa 0

Dakika ya 74, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Jeryson Tegete anatoka Didier Kavumbagu

 DK70: Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la nne


 Dakika ya 69, Credo Mwaipopo anaipatia JKT Ruvu bao la kwanza
Kutoka Chamazi mchezaji wa Mtibwa Salvatory Ntebe anapigwa kadi nyekundu huku Azam wakiongoza 1-0

Dakika ya 60, Young Africans 3 - 0 JKT Ruvu

Dakika ya 57, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Shamte Ally anatoka Nizar Khalfan

Dakika ya 53, Saimon Msuva anaipatia Young Africans bao la tatu
Young Africans 3 - JKT Ruvu


Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 2 - 0 JKT Ruvu
Mpira ni mapumziko, Young Africans 2 - 0 JKT Ruvu
Cannavaro dkk 4
Didier dkk 31

Wakati huo huo kwenye dimba la Chamazi Kipre Tchetche anaipatia Azam bao la kuongoza katika dakika ya 35.

DK 31: Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la pili

 DK 30: Yanga bado wanaongoza katika mechi hii inayochezwa kwa timu kucheza kwa nidhamu ya hali juu kwenye safu za ulinzi. Yanga 1- 0 JKT.

DK15: Yanga 1 - 0 JKT RUVU

DK 4: Nadir Haroub Cannavaro anaipatia Yanga bao la kuongoza

1.Yaw Berko
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Kelvin Yondani
5.Nadir Haroub 'Cannavaro'
6.Athuman Idd 'Chuji'
7.Nizar Khalfan
8.Haruna Niyonzima
9.Didier Kavumbagu

10.Hamis Kiiza
11.Saimon Msuva

Subs:
1.Ally Mustapha 'Barthez'
2.Godfrey Taita
3.Stephano Mwasika
4.Ladisalus Mbogo
5.Rashid Gumbo
6.Shamte Ally
7.Jeryson Tegete

FIESTA YAITIKISA MBEYA USIKU WA JANA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya.

 Mashabiki kibao.
 Wasanii wa Filamu hapa nchini Aunt Ezekiel,Wema pamoja na Shilole wakiwasikiliza mashabiki wao wanataka nini.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Diamond akiwaimbisha mashabiki na wapenzi wa muziki huo waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,kwenye uwanja wa Sokoine,mkoani Mbeya.
 Shemejiii....Wema Sepetu akiwachetua kidogo wapenzi wa mambo ya filamu.
Msanii wa bongofleva kutoka THT,Barnaba akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.



Wadau wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu.
Watu kibao ndani ya sokoine usiku huu.
Mmoja wa wasanii mahiri wanaotikiza kwenye anga ya muziki wa bongofleva hasa katika miondoko ya R&B,Ben Paul akikamua vilivyo jukwaani huku mashabikiwa wake wakishangilia kwa shangwe. 
Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya  Mh. Dkt. Norman Sigallah akimtaja mshindi wa gari aina ya Vits itolewayo na kampuni ya Push Mobile,ikiwa ni sehemo mojawapo ya mchakato wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,anayeshuhudia ni Meneja masoko wa Push Mobile Rugambo Rodney na kulia ni Chiku Saleh kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ,ambapo  katika bahati nasibu hiyo iliyochezeshwa,aliyeibuka mshindi ni   Eva B Mgovani. 
 ni full kujiachi tuu ndani ya uwanja wa sokoine usiku huu.
Pichani kati ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya  Mh. Dkt. Norman Sigallah akiwa katika picha ya pamoja na Meneje vipindi wa Clouds FM,na mdau mwingine.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya anaefananishwa na mashabiki wake kama Ray C,aitwaye Recho kutoka THT akitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012
 Mashabiki wakishangilia vilivyo usiku huu,huku makamuzi ya wasanii yakiendelea jukwaani.
 Msanii wa bongofleva anaetikisa kwa nyimbo kadhaa ikiwemo,Mama halima,Aifora na nyinginezo akiwaimbisha mashabiki wake kama waonekanavyo pichani usiku huu.
Mkali mwingine anaekuha juu katika mambo ya kuchana a.k.a kughani Stamina akiamsha kitim kitim kwa wakazi wa mji wa Mbeya usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta.

OFFICIAL: YANGA YAMTIMUA KOCHA TOM SAINTFIET

Wote wametimuliwa Yanga
Fukuza fukuza ya klabu ya Yanga iliyoanza leo mchana baada ya mkutano wa wajumbe wa kamati ya utendaji uliofanyika leo katika makao makuu ya klabu imeendelea imemkumbuka kocha mkuu wa klabu hiyo Mbelgiji Tom Saintfiet.

Taarifa za uhakika kutoka kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ni kwamba  uongozi wa timu hiyo umefikia maamuzi ya kumtimua kazi kocha huyo aliyeajiriwa miezi mitatu iliyopita kutokana na kutofautiana sera za namna ya kuiendesha klabu na uongozi wa juu wa mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati.

Mchana leo kamati ya utendaji ilisimamisha ajira za viongozi waajiriwa wote wa klabu hiyo akiwemo katibu mkuu Celestine Mwesigwa na msemaji Luis Sendeu huku ikitoa onyo kwa kocha Saintfiet kwa tabia yake ya kuongea na waandishi wa habari bila mpangilio wa klabu. Lakini baada ya taarifa hizo kutoka usiku wa leo kocha huyo akaonekana akiongea kwenye television mojawapo nchini akizungumzia mambo mbalimbali kuihusu Yanga.

Kwa mujibu wa Sanga anasema kwamba sakata lote la jinsi kocha huyo alivyopoteza kazi yake litatolewa ufafanuzi hapo kesho.

Wakati huo huo aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga kabla ya Mwesigwa, Lawrence Mwalusako amepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo ya ukatibu mkuu wa Yanga kwa muda, wakati mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Seikolojo Chambua amekabidhiwa majukumu ya kuwa meneja wa timu hiyo akichukua nafasi ya Hafidh Salehe ambaye nae aliondolewa leo mchana.

Nafasi ya usemaji wa Yanga mpaka sasa imekuwa kitendawili, tetesi zinasema kuwa mtangazaji wa Clouds FM NA Clouds TV Abdul Mohamed na Mwanahabari Mahmoud Zubeiry mmojawapo anaweza kula shavu la kumrithi Sendeu.

Friday, September 21, 2012

DOCUMENTARY: WAFALME WA ULAYA - STORY YA CHELSEA NAMNA WALIVYOBEBA UBINGWA ULAYA

GOLI LA SIKU: MLEMAVU WA MGUU APIGA GOLI LA TICK TAK

YANGA WAANZA KUTIMUANA - SENDEU, MWESIGA, KOCHA SAINTFIET ANUSURIKA APEWA ONYO KALI

Siku chache baada ya kuazna ligi kuu vibaya, uongozi wa klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Yusuph Manji leo umeanza harakati za kujipanga upya kwa kufanya mabadiliko kadhaa kwenye safu ya uongozi wa klabu hiyo.
 
Katika kikao cha kamati ya utendaji wa klabu hiyo iliyokaa leo mchana chini ya makamu mwenyekiti Clement Sanga imefikia maamuzi ya kuwaondoa kwenye uongozi wa timu hiyo katibu mkuu wa klabu hiyo Celestine Mwesigwa, ofisa utawala Masoud Saad, na Luis Sendeu aliyekuwa msemaji wa klabu - sababu ikielezwa ni kushindwa kutimiza majukumu ipasavyo.
 
Katika hatua nyingine kamati ya utendaji imewabadilishia majukumu Philip Chifuka aliyekuwa mhasibu wa klabu, huku aliyekuwa meneja wa timu Hafidh Salehe nae akibadilishiwa majukumu. Meneja mpya wa timu atatangazwa baadae kidogo.
 
Nae kocha wa klabu hiyo Mbelgiji Tom Saintfiet aliepuka panga lilowakuta wenzie lakini amepewa onyo kali kwa kitendo chake kilichoitwa cha kuzungumza "ovyo" na uongozi wa klabu.
 

REVEALED! OKWI KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA YANGA!


Kamati ya Ligi ya Kitengo cha michezo cha CLOUDS MEDIA GROUP(Sports Xtra/Bar) iliyokutana Dar es Salaam jana (septemba 20 mwaka huu) imetoa adhabu kwa mchezaji Emmanuel Okwi na onyo kali kwa mwamuzi Judith Gamba.

Emmanuel Okwi wa Simba amefungiwa jumla ya mechi tano za Ligi Kuu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu Kessy Mapande kwenye mechi hiyo namba 10.
mgawanyiko wa adhabu ya okwi upo kama ifuatavyo:mechi tatu ni kutokana na kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu na michezo miwili ni kutokana na kuwatupia mashabiki chupa ya maji.



Pia Kamati iyo imetoa onyo kali kwa mwamuzi Judith Gamba aliyechezesha mchezo namba 5 kati ya Coastal Union na JKT Mgambo.


Kanuni YA 25 ( C ) ya udhibiti wa wachezaji : Tff itadhibiti mienendo ya wachezaji kwa kuchukua hatua kama ifuatavyo.

MCHEZAJI ATAKAYETOLEWA NJE KWA KADI NYEKUNDU KWA KOSA LA KUPIGA AU KUPIGANA ATASIMAMA KUSHIRIKI MICHEZO MITATU INAYOFUATA YA KLABU YAKE NA ATALIPA FAINI YA TSH 500,000

Mwigizaji kwa jina la James Bond akiwa juu la dhamira ya siri katika kampeni maalumu ya Heineken®



Daniel Craig akiigiza pamoja na mwigizaji wa filamu ya  SKYFALL Bond akiitwa Bérénice Marlohe katika kapeni hii mpya

Heineken ®, ikileta filamu ya SKYFALL ™ Afrika Mahariki ikizinduliwa nchini Kenya, Uganda Na Tanzania


Tarehe 20 Septemba 2012 - Heineken®, bidhaa inayoongoza katika bia yenye hali ya juu duniani, leo imezindua kampeni mpya ya TV na digitali, ikingojea uzinduzi wa filamu inayoitwa  SKYFALL™ ikiwa filamu ya 23 ya James Bond, kwenye igizo hili tunamona Daniel Craig akileta mwigizaji wakulipua ya James Bond katika tangazo maalum ya Heinken kwa mara ya kwanza. Wakitoa changamoto kwa wateja kuwapinga maadui zao na ‘tatua tatizo’, watazamaji watachukuliwa katika safari pamoja na mwigizaji mpya mrembo Bérénice Marlohe.

Uzoefu wakidigitali inaanza mahali tangazo ya TV inapoishia, watazamaji wakialikwa kwenye treni na Bérénice kabla haijaendelea na safari katika muamko mzuri kwenye milima yenye barafu. Kuwaweka watazamaji katika wenendo zao, kutakuwa na vipimo ambayo itawapeleka ‘kutatua tatizo’ wakilinda yaliyomo kutoka wale watu wabaya.

Heineken® inaubia ya kimataifa katika igizo hii la James bond na watatoa uzoefu kwa wateja wao wa Afrika mashariki kwa kuleta matukio haya tarehe 25 Oktoba ndani ya IMAX nchini Kenya, ndani ya Mlimani City nchini Tanzania na Oasis nchini Uganda, wiki moja baada ya filamu hii kuzinduliwa.

Kampeni hii ikiendelea, wateja wa Heineken® watapata fursa yakushinda tiketi wakishiriki katika promosheni katika menendo za usiku nchini hapa Tanzania na wakibofya www.facebook.com/heineken.

Picha zikipigwa ndani ya Shepperton Studios, kampeni hii yakidigitali inawakumbuka filamu ya James Bond zikiwa na vipande vya filamu zingine za awali. Magari ya treni yalivutiwa na muvie ya Ken Adam, wakati muvie za James bond zilitumika katika tangazo hii.
Koen Morshuis, Mkurugenzi Mkuu, HEINEKEN Afrika Mashariki alisema ‘ Tumefurahishwa kuleta uzinduzi huu kabla ya uzinduzi rasmi wa filamu hii na kubadilishana uzoefu wa igizaji wa Bond na wateja wetu nchini Kenya, Tanzania and Uganda. Kama Heineken, James Bond ni mali yakimataifa ambayo inawafikia wateja ulimwenguni. Siyo kuwa shujaa tu, Bond ni ‘mwanaume wa taifa’ – anajiamini, anajiweza na yuko tayari kwa kila jambo, maadili ya Heineken.
 
Interesting facts on the ‘Crack the Case’ Television Commercial:
·         The film was primarily shot at Shepperton Studios. Elements were also filmed at a train station in TimiÈ™oara, Romania, with a team who were able to transform a 28 degree set into a snowy landscape. 
·         Replica James Bond film props were used throughout the film as a tribute to the franchise and fans alike. Eagle-eye spectators will also spot the Spectre ring from ‘Dr. No’, the Zorin industries and Spectre logos and the Faberge Eggused in‘From Russia with Love’ and ‘Goldeneye’.
·         The soundtrack titled ‘Man Like That’ was written and performed by rising New Zealand music star Gin Wigmore, who also makes an appearance in the film.


Heineken and James Bond
Heineken has developed a strong and successful relationship with James Bond spanning global partnerships with ‘Tomorrow Never Dies’, ‘The World is Not Enough’ , ‘Die Another Day’, ‘Casino Royale’ and ‘Quantum of Solace’ .
About SKYFALL™
Daniel Craig is back as Ian Fleming’s James Bond 007 in SKYFALL™, the 23rd adventure in the longest-running film franchise of all time. In SKYFALL, Bond’s loyalty to M is tested as her past comes back to haunt her. As MI6 comes under attack, 007 must track down and destroy the threat, no matter how personal the cost. The film is from Albert R. Broccoli’s EON Productions, Metro-Goldwyn-Mayer Studios, and Sony Pictures Entertainment. Directed by Sam Mendes. Produced by Michael G. Wilson and Barbara Broccoli. Written by Neal Purvis & Robert Wade and John Logan. 
About Heineken®:
The Heineken brand bearing the founder’s family name - Heineken - is available in almost every country around the globe, and it is the world’s most valuable international premium beer brand. Additional information is available on www.heineken.com and on www.theHEINEKENcompany.com, www.Facebook.com/Heineken.
About Albert R. Broccoli's EON Productions
EON Productions Limited and Danjaq LLC are wholly owned and controlled by the Broccoli/Wilson family. Danjaq is the US based company that co-owns, with MGM, the copyright in the existing James Bond films and controls the right to produce future James Bond films as well as all worldwide merchandising. EON Productions, an affiliate of Danjaq, is the UK based production company which makes the James Bond films. The 007 franchise is the longest running in film history with twenty-two films produced since 1962. Michael G Wilson and Barbara Broccoli succeeded Albert R ‘Cubby’ Broccoli and have produced some of the most successful Bond films ever including CASINO ROYALE and QUANTUM OF SOLACE. They are currently producing the 23rd film, SKYFALL.
About Metro-Goldwyn-Mayer Studios Inc.
Metro-Goldwyn-Mayer Studios Inc. (“MGM”) is a leading entertainment company focused on the production and distribution of films and television content globally. The company owns one of the world’s deepest libraries of premium film and television programming. In addition, MGM has ownership interests in domestic and international television channels, including MGM-branded channels. For more information, visit www.mgm.com
About Sony Pictures Entertainment
Sony Pictures Entertainment (SPE) is a subsidiary of Sony Corporation of America, a subsidiary of Tokyo-based Sony Corporation. SPE's global operations encompass motion picture production and distribution; television production and distribution; home entertainment acquisition and distribution; a global channel network; digital content creation and distribution; operation of studio facilities; development of new entertainment products, services and technologies; and distribution of entertainment in 159 countries. For additional information, go to http://www.sonypictures.com

Press enquiries:
Koen Morshuis
General Manager
Heineken East Africa

TOFAUTI YA KATI YA MABASI YA SIMBA NA YANGA NA LA GOR MAHIA

 yasemekana hili ni basi lililo nunuliwa na mashabiki wa Gor Mahia kwa ajili ya timu yao
 
 
 Mabasi ya Simba na yanga - PICHA KWA HISANI YA http://moronew.blogspot.com

RATIBA YA MECHI ZA SIMBA, YANGA, MTIBWA NA AZAM KATIKA SUPER SPORT SUPER WEEKEND

Mechi tano za Ligi Kuu ya Vodacom za Super Weekend katika mzunguko wa kwanza zitakazooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport zitaanza kati ya saa 1.30 jioni na saa 1 kamili usiku.
 
Septemba 28 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku. Mechi ya Simba na Tanzania Prisons itakayochezwa Septemba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 11 kamili jioni.
 
Yanga na African Lyon zenyewe zitapambana Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni wakati Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar zitaoneshana kazi Oktoba 1 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
 
Mechi ya mwisho katika Super Weekend itakuwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba, na itaanza kutimua vumbi saa 1 kamili usiku.

Thursday, September 20, 2012

GERARD PIQUE AMJIBU MESSI - AMJAZA MIMBA SHAKIRA

 
Hips hazidanganyi na vipimo vya mimba pia: Shakira ni mjamzito!

Mwanamuziki huyo wa kilatini, 35, alitumia ukurasa wake wa Facebook kutangaza kwamba anatarajiwa kupata mtoto wake wa kwanza na mwanasoka wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona Gerard Pique, aliandika, "Kama baadhi yenuu mnavyojua, Gerard na mimi tuna furaha kwa kutarajia kupata mtoto wetu wa kwanza!"

"Tumeamua kuupa umuhimu wakati hu mzuri sana kwetu katika maisha yetu na kuhairisha kila kitu kuhusu kazi zangu nilizozipanga kufanya hivi karibuni," alisema Shakira na kuongeza. "Hii inamaanisha sitokuwepo katika tamasha la iHeartRadio."

Kwa taarifa hiyo Gerard Pique anaungana na Lionel Messi ambaye nae anasubiri nae kuitwa baba miezi kadhaa ijayo .

KALI YA LEO: BARCELONA WAWAKATAA WAHUDUMU WA KIUME KWENYE NDEGE - WAOMBA WALETEWE MADEMU TU



Mwaka 2010, Turkish Airlines alilipa kiasi cha €7.7 ili kuwa wadhamini wa rasmi wa masuala ya usafiri, wakiwa wanahusika na kuwasafirisha ndani ya Spain na popote duniani.

Miaka miwili ndani ya mkataba huo, wakatalunya sasa wamepeleka ombi la kampuni hiyo ya kituruki kupeleka wahudumu wa kike tu kwenye ndege wanayopanda timu hiyo kwa ajili ya safari zao. Sababu kubwa waliyoitoa ni kwamba wahudumu wa kiume mara nyingi huwa wanasumbua kwa kuwa washabiki wao hivyo wanakosa utulivu safarini. Gazeti la kituruki Hurriyet linaripoti:

"Wahudumu wa kiumemara nyingin wanakuwa wanasumbua kwa kutaka autographs na jezi kutoka kwa wachezaji vipenzi vya mashabiki wengi duniani kama Lionel Messi na Andres Iniesta, jambo ambalo muda mwingine linakuwa kero kwa timu."

Kwa maana hiyo Turkish Airline wamekubali ombi la Barca na wamewachagua mademu 20 kwa ajili ya kuwahudumia Barcelona katika safari zao. Na hapo chini ndivyo Lionel Messi alivyopokewa taarifa hizo za watoto wa kike 20 kumuhudumia kwenye ndege.

''HAPA BAHANUZI,KULE KIIZA,NYUMA TWITE NA YONDANI,HATOKI MTU ' ZAIMALIZA YANGA.

Kocha wa Dar es salaam Young Africans Tom Saintfiet amesema kwamba kuanza vibaya kwa michezo yake ya ligi kuu kumetokana na baadhi ya wachezaji wake kujihisi wakubwa na muda mwingi wamekuwa wakitumia kubadilisha mitindo ya nywele na viatu. Akizungumza na Sports Extra mara baada ya mchezo kumalizika kwenye uwanja wa jamhuri jana kocha huyo amefafanua kwamba pia vyombo vya habari vimewafanya wajione wakubwa na hivyo muda mwingi wanatumia akili zao kufikiria namna ya kutokea katika vyombo habari badala ya kufikiria mchezo. Ama kwa upande mwingine kocha huyo amekiri kama amefungwa mchezo huo kihalali baada ya wachezaji wake kupata nafasi zaidi 8 na kushindwa kufunga bao ilihali mtibwa wamepata nafasi nne na kufanikiwa kupachika mabao 3. Aidha Tom ameongeza kwamba hakukuwa na tatizo la uwanja, mwamuzi wala Hoteli waliyofikia.

AZAM - "HUU NDIO UOZO WA MAREFA WA TFF WALIVYOISADIA SIMBA KUSHINDA NGAO YA HISANI"

SIMBA NA JKT WAINGIZA MIL.73, WAGAWANA MIL.16 KILA TIMU - AFRICAN LYON NA POLISI ZAINGIZA 185,000 - TIMU ZAPATA 40,000


Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya JKT Ruvu na Simba iliyochezwa jana (Septemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 73,611,000.
 
Washabiki 12,884 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 16,154,161.02 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 11,228,796.61.
 
Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 150,000, waamuzi sh. 70,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, tiketi sh. 3,175,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 5,384,720.34, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,230,832.20, uwanja sh. 5,384,720.34, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,076,944.07, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,076,944.07.
 
61 WASHUHUDIA MECHI YA AFRICAN LYON v POLISI MORO
Watazamaji 61 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African Lyon na Polisi Moro iliyofanyika jana (Septemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
 
Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 5,000 ni sh. 185,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 20,287.91, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 27,457.62 na tiketi sh. 89,916.
 
Kamati ya Ligi sh. 6,762.63, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,057.58, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,703.05, gharama za mchezo sh. 6,762.63 na uwanja sh. 6,762.63.

SD TV: MABAO YA MTIBWA DHIDI YA YANGA!

SD TV:HII NDIO KADI NYEKUNDU ALIYOPEWA OKWI ! MDAU TOA HUKUMU.




 

UJUMBE WA LEO!

AIRTEL yaahidi kuendelea kusaidia maendeleo ya michezo nchini

KAMPUNI ya mawasiliano nchini ya Airtel imeahidi kuendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya vijana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika hafla fupi ya kukabidhi shilingi milioni tano pamoja na fulana mia moja kama udhamini wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu zenge kauli mbiu ‘tukuze utalii wa ndani kupitia michezo’, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwemo riadha ili kukuza maendeleo ya vijana.

“Udhamini wetu wa shilingi milioni tano pamoja fulana mia moja katika mbio za Rock City mwaka huu unalenga katika kusukuma maendeleo ya vijana kupitia michezo kwa tunaamini kuwa michezo imekuwa ni chanzo kikubwa cha ajira duniani. “Tunaahidi kuendelea kusaidia michezo mingine kwa kuwa pia tunaamini kupitia michezo mbalimbali tunaweza kutangaza vivutio vyetu vya utalii duniani. Mfano nzuri ni mbio za mwaka huu za Rock City Marathon zitakazowakutanisha wanariadha mbalimbali kutoka nchi jirani,” aliongeza Bi. Matinde. Akipokea hundi na fulana hizo, Mratibu wa mbio hizo kutoka katika kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bi. Grace Sanga aliishukuru kampuni ya Airtel kwa kuendelea kusaidia mbio za Rock City na kuyahasa mashirikia na makampuni mengine kuiga mfano wa kampuni hiyo.

“Tunaishukuru Airtel kwa msaada wao kwa kuwa msaada huu utatusaidia tujiandae vizuri na Rock City Marathon ya mwaka huu itakayofanyika Oktoba tarehe 28 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,” alisema Grace. Grace alisema kuwa mbali na Airtel wadhamini wengine ni pamoja na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Parastal Pension Fund (PPF), Geita Gold Mine, African Barrick Gold, Air Tanzania Company Ltd (ATCL), Mamlaka ya Taifa ya Mbuga za Wanyama nchini (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Nyanza Bottles, New Africa Hotel na New Mwanza Hotel.

Aidha, Bi Sanga aliwaasa wanariadha kujitokeza na kuanza kujisajili ili kushiriki katika mbio hizo na kusema kuwa fomu za usajili zinapatikana katika ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo katika jengo la ATCL ghorofa ya tatu, ofisi za Bodi ya Utalii jengo la IPS ghorofa ya tatu, Dar es Salaam, na zinapatikana katika tovuti ya www.rockcitymarathon.blogspot.com. CPI ilitangaza kuwa atakaeibuka kinara katika mbio za kilometa 21 mwaka huu kwa wanaume na wanawake atazawadiwa shilingi milioni moja na laki mbili wakati mshindi wa pili ataweka mfuko shilingi laki tisa na mshindi wa tatu ataondoka na shilingi laki saba.

 Afisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni tano Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel pia walikabidhi fulana mia nne zitakazotumika katika mbio hizo.
Afisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi moja kati ya T-sheti mia nne Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel walikabidhi T-sheti mia nne pamoja na milioni tano kusaidia mbio hizo.

MICHEAL CARRICK AIPA MAN UNITED USHINDI WA 100 KWENYE CHAMPIONS LEAGUE DHIDI YA GALATASARAY


szólj hozzá: M1-0G www.fasthighlights.com

OSCAR AFUNIKA ULAYA - AFUNGA MAGOLI MAWILI NA KUIPA CHELSEA SARE DHIDI YA JUVE


szólj hozzá: JUV

LIONEL MESSI APIGA BAO MBILI NA KUIKOA BARCA NA AIBU MBELE WARUSI


B0-3-0-2S by ourmatch

Wednesday, September 19, 2012

MTIBWA WALIVYOIKANDAMIZA YANGA KWENYE PICHA

Wachezaji wa Moro United wakishangilia baada ya kufunga goli lao la kwanza









Picha zote kwa hisani ya http://straikamkali.blogspot.com/

HAYA NDIO MABASI MAPYA YA KISASA YA SIMBA NA YANGA WALIYOPEWA NA MDHAMINI WAO

Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.

Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.

Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.

Mabasi mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.
KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager hatimaye inatarajia kukabidhi mabasi mapya ya kisasa kwa timu za Simba na Yanga siku ya Ijumaa asubuhi.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na makabidhiano hayo yatafanyika katika viwanja vya ofisi za TBL Ilala.

“Zaidi ya wageni 100 wamealikwa kwenye hafla hii itakayofanyika Ijumaa hapa TBL na kati ya hawa wageni kutakuwa na baadhi ya mashabiki wa timu hizi mbili kwa hivyo tunatarajia makabidhiano ya aina yake,” alisema Kavishe.

Kwa mujibu wa ratiba, baada ya makabidhiano, kila timu itaondoka na basi lake na wachezaji na mashabiki na kupita katika matawi yao kwa msafara maalumu utakaoambatana na burudani mbalimbali huku mashabiki wa timu hizi wakitarajiwa kuyapokea mabasi hayo na kuwashangilia wachezaji wakipita katika matawi.

Msafara wa timu ya Simba ukiondoka TBL Ilala utaelekea katika Tawi la Vuvuzela lililopo Makao Makuu ya klabu hiyo Kariakoo Mtaa wa Msimbazi kisha utaelekea katika Tawi la Magomeni Mpira Pesa, Ubungo katika kituo cha mabasi na hatimaye Tawi la Wailes Temeke.

Msafara wa Yanga nao ukiondoka TBL Ilala utaelekea katika Tawi la Ubungo katika kituo cha mabasi na kuelekea katika Tawi la Manzese, Lango la Jiji Magomeni, Buguruni, Mwembe Yanga, Mtoni kwa Aziz Ali, Mkombozi na hatimaye kumalizia katika makao makuu ya Jangwani, Kariakoo.

"Tunawaomba mashabiki wa timu hizi mbili wajitokeze kwa wingi katika matawi yao ili wajionee mabasi haya mapya ambayo ni ya kisasa na pia wapate fursa ya kukutana na wachezaji wa timu zao," alisema Kavishe.

Kilimanjaro Premium Lager imedhamini klabu hizi hivi tangu mwaka 2008.


Source/http://straikamkali.blogspot.com/

SIMBA WAENDELEA KUTISHA LIGI KUU - WAWATAFUNA WANAJESHI WA JKT RUVU 2 - 0

Mabingwa wa Tanzania bara Simba SC leo hii wameendeleza makali yao waliyoanza nayo ligi kwa kuitandika timu ya wanajeshi wa JKT Ruvu kwa mabao mawili kwa sifuri.
Simba ambao walicheza mchezo kwa dakika nyingi baada ya mshambuliaji wao tegemeo Emmanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza cha mchezo, walipata mabao yao kutoka kwa kiungo Amri Kiemba aliyefunga bao la kwanza na Haruna Moshi Boban aliyepiga kidude cha pili.
Kufuatia matokeo hayo Simba inaendelea kukamata usukani mwa ligi kwa kukusanya pointi 6, magoli matano ya kufunga na wakiwa hawajuruhusu nyvu zao kuguswa. Simba walishinda mechi ya kwanza ya ligi kwa 3 - 0 dhidi ya African Lyon.
Kwa upande mwingine huko jijini Mwanza Azam FC wametoka sare ya kufungana 2-2 na Toto Africa, wakati Tanzania Prisons wametoka 1 - 1 na Coastal Union ya Tanga, Kagera Sugar wametoka sare tasa na JKT Oljoro, huku Ruvu Shooting wakiifunga Mgambo JKT 2-1.

 

YANGA WADUNGWA 3 - 0 NA MTIBWA MOROGORO

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati, klabu ya Yanga ya Dar es Salaam leo hii imekula kichapo mabao matatu kwa nunge kutoka kwa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro.

Katika mchezo huo ambao umekuwa na matokeo hasi kwa upande wa timu ya Jangwani ulianza kwa kwa timu kusomana lakini dakika ya 11 ya mchezo akaipatia timu yake ya Mtibwa bao la kuongoza, kabla ya Juma Javu kuongeza la pili katika dakika ya 45 ya mchezo katika kipindi cha kwanza na timu zikaenda mapumziko Mtibwa wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili Yanga wakafanya mabadiliko kwa kuwaingiza Saimon Msuva na Stephano Mwasika kuchukua nafasi za Frank Domayo na David Luhende lakini haikusadia chochote. Dakika ya 66 akatoka Mbuyu Twitte na kuingia Didier Kavumbangu lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwa upande wa watoto wa Manji.
Dakika ya 77 ya mchezo alikuwa yule yule Juma Javu akaenda kumtungua golikipa Ally Mustapha Barthez goli 3 na la mwisho katika mchezo huo. Dakika ya 90 Yanga wakapata penati lakini Hamis Kiiza akashindwa kufunga na mwamuzi akapuliz kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo.

BAADA YA MIAKA 10 JUVENTUS WANARUDI KWENYE CHAMPIONS LEAGUE LEO - WAKIANDAMWA NA HISTORIA YENYE UTATA KATIKA MICHUANO YA ULAYA

 
Wakati fulani katika miaka ya 1980, wakurugenzi wa klabu ya Juventus walwakusanya kwa pamoja wachezaji wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kuzungumza nao. Klabu ilikuwa na tatizo kubwa na ilibidi kulitafutia ufumbuzi: haikuwa imeshinda kombe la ulaya.

Kwa wakati huo, mshambuliaji Paolo Rossi alisema kitendo cha wao kutoshinda ubingwa wa ulaya ni 'ajabu'. Lakini hata baada ya Juventus walipofanikiwa kushinda ubingwa wa ulaya na kwa mara ya pili katika historia ya klabu hiyo mwaka 1996, klabu hiyo bado haijawa na mafanikio mazuri kwenye michuano hiyo.

Ni jambo la kushangaza kuona klabu yenye mafanikio kuliko zote nchini Italia ina rekodi isiyo nzuri kwenye michuano ya juu kabisa katika ngazi ya vilabu. Juventus wameshindana katika champions league mara 26 - idadi ya juu kuliko timu zote za ulaya kasoro AC Milan(26), Ajax na Bayern Munich (42), Dynamo Kiev (29), Benfica (31) na Real Madrid (42). Kati ya timu zote hizi ni Dynamo Kiev ndio ambayo imepata mafanikio kiduchu.

Kutokufanikiwa kwa Juventus kunaendelea mbele zaidi. Wamefanikiwa kufika katika nusu fainali ya klabu bingwa ya ulaya mara nyingi zaidi kuliko timu zote kasoro Manchester United, Milan, Barcelona, Bayern na Real lakini, kutokea hapo, timu hiyo iliyoshinda mara nyingi ubingwa wa Italia imeshindwa kuleta umwamba wake katika michuano ya UEFA. Juventus ni moja ya timu tatu, pamoja na Benfica na Bayern , zilizopoteza fainali za Champions league kuliko zilivyoshinda.

Na katika mechi zote hizo zilikuwa zikiandamwa na matukio yenye utata. Juventus walikuwa wakituhumiwa kutumia madawa ya kuongeza nguvu na upangaji wa matokeo huku balaa ya lilitokea katika mechi yao ya fainali dhidi ya Liverpool na kukatokea vifo vya mashabiki wengi -(Heysel Tragedy 1985)



Katika michuano yao ya kwanza ya ulaya msimu wa 1957-58 waliingia na aibu ya aina yake. Pamoja na kuwa wachezaji wawili waliokuwa bora kwa wakati huo Omar Sivoru na John Charles, walifungwa 7-0 na Wiener Sports Club na kutolewa kwenye mashindano.

Baada ya mchezo huo, Charles alilamika juu ya mchezo wa nguvu na rafu waliokuwa wakicheza Waustralia: "Mchezo huu ulikuwa wa kutisha zaidi tangu nianze kucheza soka. Nilipigwa mateke sana na niliumia kiasi madaktari walitaka kunifanyia upasuaji wa mguu ulioumia."

Juventus waliendelea kuusotea ushindi wao kwanza katika michuano hiyo. Baada ya kufungwa na CSKA Sofia msimu wa 1960-61, ikawabidi wasubiri mpaka jaribio lao la tatu, msimu uliofuatia, ambao Juventus wakashinda mechi ya ya kwanza, na wakawatoa Panathinaikos na Partizan Belgrade, na wakaenda kuwachafulia historia Real Madrid baada ya kuwafunga nyumbani kwao 1-0 katika dimba la Bernabeu - mchezo wa kwanza kwa Madrid kupoteza kwao. Katika mechi ya pili ya play off jijini Paris Madrid wakshinda 3-1.

Kutokufanikiwa kwa mabingwa wa Italia katika michuano ya Ulaya kulitoa picha ya matatizo ya ndani ya klabu ya ambayo ilikuwa inatawala vilivyo katika ligi ya ndani katika kipindi fulani, kama ilivyokuwa kwa Manchester United katika miaka ya mwanzo ya 90 na hata Real wenyewe mwishoni mwa miaka ya 70, kiwango cha waitaliano hakikuwa kikitosha kuweza kupambana katika michuano ya ulaya kwa wakati huo. Uwezo wao ulikuwa chini huku Real na Benfica wakiendelea na kuimarika vizuri.

Mpaka kufikia muda ambao Serie A imeimarika, hatua kubwa zilikuwa zimepigwa na miji mingine tofauti na Turin. Klabu mbili za jiji la Milan zikaimarika na wakawa na timu nzuri zilizoenda kutawala ulaya katika miaka  ya mwanzo ya 60 wakibeba makombe manne kati yao ndani ya kipindi cha miaka saba. Wakati huo pia Italia yote ikaanza kufuata mfano wa klabu za jiji la Milan.

Katika wakati wote wa miaka 60, Inter Milan walimuajiri mtu mmoja kutoka Hungary Deszo Solti. Kupitia utafiti wa mwandishi Brian Glanville wa gazeti la Sunday Times, ilifichuka siri kwamba Solti aliwahonga na pia alijaribu kuwahonga marefa wengi wa bara la ulaya . Refa mmoja aitwaye Gyorgy Vadas alimuambia Glanville namna alivyopewa fedha ambazo zingetosha kununua magari matano aina ya Mercedes ili kuhakikisha kwamba Real Madrid hawaendi mbele katika nusu fainali ya 1965-66.

Kwa wakati hu Solti alikua anafanya kazi Inter na secretary wa klabu hiyo Italo Allodi. Wakafukuzwa na unajua wapi walipata kazi mpya katika miaka ya mwanzo ya 70? Waliajiriwa kwenye klabu ya Juventus.

Refa mwingine akajitokeza, safari hii alikuwa mreno Francisco Marques Lobo, alimwambia mwandishi Glanville namna, kuelekea kwenye mchezo wa nusu fainali kati ya juventus na vijana wa Brian Clough Derby County msimu wa 1972-73, anasema Solti alimfuata akiwa na funguo yingi za magari mapya na kiasi cha fedha cha £5,00. Lobo akakataa kuchukua mlungula lakini vijana wa Clough wanasema kuna mtu mwingine alichukua rushwa baada ya kufungwa 3-1 katika mechi ya kwanza.

Kwa wakati huo. UEFA hawakuwa na kikosi cha uchunguzi wa matukio kama hayo. Juventus wenyewe hawakuwahi kuwashtaki Sunday Times kwa kuandika tuhuma zile lakini hawakushinda ubingwa wa ulaya.

Wakamuajiri kocha mpya, mtaalamu Giovanni Trapattoni, lakini pamoja na kuwa na rekodi nzuri, kocha huyo akiwa na Juventus alishindwa kuwa na matokeo chanya alipoingia kwenye michuano ya ulaya.

Trapattoni alikuwa na rekodi nzuri sana na Juventus katika michuano ya ndani lakini hali ilikuwa tofauti kila alipotia mguu kwenye UEFA. Katika majaribio matano, walitolewa nje katika kila hatua iliyopo ndani ya michuano hiyo, ikiwemo fainali ya 1983 waliyofungwa na Hamburg 1-0. Na baadae ikaja kutokea balaa la Heysel, ambapo watu 39 walipoteza maisha.

Baada ya kusubiri kwa muda kwa muda mrefu Juventus  wakafanikiwa kuwafunga Ajax mwaka1996 katika fainali ya UEFA Champions league na kufanikiwa kubeba ubingwa kwanza wa ulaya chini ya kocha wao mpya Marcello Lippi.

Katika msimu huo wa 1995/96, kocha wa Rangers Walter Smith alimwambia mwandishi wa habari Hugh Mcllvanney kwa mshangao. "Umeona mapaja ya yule Ravanelli?" alisema. "Unawaangalia wachezaji ambao wapo vizuri sana kwa upande wa misuli kuliko mchezaji yoyte tuliyenaye. Siku zote tumekuwa tikpata taabu ya kutafuta namna ya kushindana nao kimbinu na sasa wameongeza kitu kingine wana nguvu ajabu - vigumu kushindana nao." - alisema Walter Smith

Katika msimu wa 1982-83, Trapattoni ilibidi akanushe madai kwamba timu yake ilikuwa ikitumia madawa ya kutanua misuli. Katika miaka ya mwishoni ya miaka ya 90, klabu hiyo tena ilikumbwa na tuhuma hizo tena. Alikuwa kocha mropokaji Zdenak Zeman aliyepelekea kuanzishwa kwa uchunguzi wa kisheria na mwendesha mashtaka wa Turin Raffaele Guariniello,  ambaye alikuwa shabiki wa Juventus.

Uchunguzi ulipomalizika ikagundulika kwamba kuna madawa yalikuwa yakitumika visivyo, zikaondolewa dawa takribani 100 kutoka kwenye klabu hiyo, mwezi November 2004, jambo lilopelekewa kusimamishwa udaktarii na kufungwa jela kwa daktari wa klabu Riccardo Agricola. Miezi kadhaa baadae, mkuu wa taasisi ya kuzuia matumizi ya madawa michezoni, Dick Pound, akataka Juve wavuliwe makombe yote waliyoshinda katika miaka hiyo likiwemo kombe la ulaya mwaka 1996. Hilo halikuwezekana, baada ya Daktari Agricola alipokata rufaa na kushinda kesi na Juventus wakasafishwa juu ya tuhuma hizo. Ingawa mtoa tuhuma Zdenak Zeman aliendelea kushikilia msimamo wake juu ya utumiaji madawa wa Juve akisisitiza timu hiyo ilikuwa ikitumia vibaya madawa ya kifamasia. Tuhuma zake zilikuja kuacha pale Juventus walipkutwa na kesi nyingine ya upangaji wa matokeo  maarufu kama Skenddo ya Calciopoli.

Usiku wa leo Juventus wanarejea katika michuano ya mabingwa ulaya wakiwa kama mabingwa Italy kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2002-03, walipofungwa fainali na Milan, wanarudi wakiwa bila kocha wao mkuu Antonio Conte katika benchi. Kocha huyo, ambaye alicheza katika fainali ya mwaka 1996, amefungiwa kwa miezi 10 kwa kosa la kujihusisha na upangaji wa matokeo wakati akiwa katika klabu ya Siena. Jambo ambalo linaiweka historia ya klabu hiyo katika mashaka makubwa ya uadilifu.