Search This Blog

Thursday, September 20, 2012

GERARD PIQUE AMJIBU MESSI - AMJAZA MIMBA SHAKIRA

 
Hips hazidanganyi na vipimo vya mimba pia: Shakira ni mjamzito!

Mwanamuziki huyo wa kilatini, 35, alitumia ukurasa wake wa Facebook kutangaza kwamba anatarajiwa kupata mtoto wake wa kwanza na mwanasoka wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona Gerard Pique, aliandika, "Kama baadhi yenuu mnavyojua, Gerard na mimi tuna furaha kwa kutarajia kupata mtoto wetu wa kwanza!"

"Tumeamua kuupa umuhimu wakati hu mzuri sana kwetu katika maisha yetu na kuhairisha kila kitu kuhusu kazi zangu nilizozipanga kufanya hivi karibuni," alisema Shakira na kuongeza. "Hii inamaanisha sitokuwepo katika tamasha la iHeartRadio."

Kwa taarifa hiyo Gerard Pique anaungana na Lionel Messi ambaye nae anasubiri nae kuitwa baba miezi kadhaa ijayo .

No comments:

Post a Comment