Search This Blog

Saturday, December 3, 2011

ANELKA NA ALEX NAO KUONDOKA CHELSEA JANUARY-AVB ATHIBITISHAGame over: Anelka and Alex look to have played their last games for the BluesGame over: Anelka and Alex look to have played their last games for the BluesMuda wa Nicolas Anelka na Alex @Stamford Bridge umeisha baada ya kocha Andre Villas-Boas kutangaza kuwa amekubali maombi ya wachezaji hao kutaka kuondoka Chelsea.

Wachezaji hawa wawili hawakuwa wamewekwa katika kikosi kilichosafiri kuelekea ST.James Park leo hii, na jana waliripotiwa kupigwa stop na AVB kushiriki katika mazoezi ya kikosi cha kwanza.

Chelsea wamethibitisha juu ya hatma ya Anelka na Alex mara tu baada ya timu hiyo kushinda mechi yake ya dhidi ya Newcastle.

Villas-Boas alisema: “Mazungumzo yangu na wachezaji(Anelka na Alex) yalikuwa fair and direct. Walionyesha nia ya kutaka kuondoka hapa, na wakaomba kupitia transfer request kwa muda sasa.

“NI wachezaji wa daraja la juu, ma-pro wa ukweli wasiona mashaka, lakini kwa muda huu na matokeo ya hivi karibuni, tumeamua ya kuyakubali maombi yao ya kutaka kuondoka ili kujaribu kupata wachezaji wengine watakaojaza nafasi zao kuweza kuimarisha kikosi chetu.”

MASHABIKI WA YANGA WAISHANGILIA ZIMBABWE IKICHEZA DHIDI YA STARS

Mashabiki wa timu ya Yanga wakifanya kitendo ambacho si cha kizalendo kwa kuishangilia timu ya taifa ya Zimbabwe wakati wa mchezo wa kuwania kuingia robo fainali ya michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011, uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii na Kilimanjaro Stars kufungwa goli 2-1 . Kitendo hicho kimelaaniwa na hata waandishi wa vyombo mbalimbali vya nje waliokuwa wakiripoti mchezo huo na kusema, "Hii haisaidii maendeleo ya soka na haijawahi kutokea katika nchi zao mashabiki wa nyumbani wakawashangilia wageni".

Akifadhaika zaidi mpiga picha wa Kenya Mohamed Amin, ametoa mfano kwamba wao kwa timu yao ya taifa wanaijali na kuipenda vilivyo, tofauti na vituko vya mashabiki wa Yanga alivyoviona leo. Anaongeza kwa kutoa mfano kuwa "Mwaka 1987 timu yao ya Harambee Stars iliwahi kuwa na wachezaji 12 wa timu ya Golmahia, na kati ya hao 12 wachezaji 9 walikuwa wakianza kipindi cha kwanza, lakini mashabiki hawakuwahi hata siku moja kufanya kitendo cha aibu kama hiki cha mashabiki wa Yanga" amemaliza Mohamed Amin, Mwana wa mpiga picha Maarufu wa ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati mzee Mohamed Amin aliyepoteza maisha katika ajali ya ndege miaka kadhaa iliyopita.

Kilimanjaro Stars imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robi fainali ambapo itashuka dimbani tarehe 6 mwezi huu kucheza na timu ya taifa ya Malawi.

MARTIN O'NEILL KOCHA MPYA SUNDERLAND


Klabu ya Sunderland imemtangaza rasmi kocha Martin O’Neill kuwa kocha wao mpya, akimbadili Steve Bruce.

Mtandao rasmi wa “Black cats” ulitangaza taarifa hiyo asubuhi ya leo, wakithibitisha kwamba O’Neill, 59, amesaini mkataba wa miaka 3 ya kuitumikia klabu hiyo.

O’Neill aliuambia mtandao huo: “Najisikia vizuri sana kuweza kurudi tena katika soka na kuwa manager wa Sunderland. Ni wakati mzuri kwangu mimi.

“Nimekuwa nikisikia uzuri wa klabu hii, lakini baada ya kufika hapa na kuuona uwanja na training ground, nimethibitisha uzuri wa klabu hii. Ni pazuri sana kiukweli.

“Natumai nitaisadia Sunderland kufanikiwa sana. Hilo ndilo lilonileta na ndio dhamira yangu.” Alisema O’Neill.

WENGER AKIRI YUPO TAYARI KUSAJILI - ASEMA CHAMAKH AONDOKI KWA MKOPO- KUMUACHA ALMUNIA JANUARY


Kocha Arsene Wenger amethibitisha kuwa yupo sokoni kutafuta wachezaji wazuri katika kipindi cha dirisha dogo la mwezi January.

Wenger anataka kuiboresha timu yake hasa katika safu ya ushambuliaji kwa kuwa na machaguo yaliyo bora tena kwa wingi wa kutosha, lakini amesisitiza hakuna nafasi ya mchezaji aliye nje ya form Maroune Chamakh kutolewa kwa mkopo japokuwa kumekuwa na interest kutoka kwa QPR na PSG.

“Kwa sasa, sifanyi chochote kuhusu usajili wa mwezi Janaury, nina kikosi kikubwa, lakini nikipata mchezaji mzuri na anayefaa katika mipango yangu then itabidi nimchukue.

“Kama tusipopata majeruhi, then tutakuwa hatuna shida kwa sababu tunae Chamberlain, ambaye anaweza kucheza pale, pia kuna kuna Park, Arshavin, na Van Persie. Hivyo bado tuna wachezaji wazuri wenye uwezo wa kumletea adui madhara, lakini tutapata shida sana ikiwa tutapata majeruhi.”

Wenger pia amesisitiza Chamakh-ambaye atakuwa na timu yake ya Morocco katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwezi January-anaweza kurudisha makali yake aliyoyaonyesha msimu uliopita alipowasili kutoka Ufaransa na hawezi kumruhus aondoke kwa mkopo in January.

“Ni vigumu kumtoa kwa mkopo sasa kwa sababu ya African Nations Cup in January, atarudi mwezi February hivyo atakuwa amechoka, so sio rahisi kumtoa kwa mkopo. Wachezaji watakaoenda Afrika wanahitaji wataondoka wiki mbili kabla ya michuano. Then watacheza ile michuano kwa almost 3 weeks, halafu wanahitaji kupumzika kwa wiki mbili jumla zinakuwa wiki 6.

“Chamakh sasa hivi ana tatizo la kutokujihamini na pia kukosa nafasi, lakini naamini atakapopata na nafasi na kuzitumia vizuri atarudisha makali yake.”- Wenger.

Wenger pia amekiri atamruhusu Manuel Almunia aondoke mwezi Janaury.

ANELKA NA ALEX WAONDOLEWA KIKOSI CHA KWANZA - WAPELEKWA KIKOSI CHA PILI NA AVB


Nicolas Anielka na Alex wamefungiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha klabu ya Chelsea na kocha Andre Villas-Boas.

Wachezaji hao wawili wote kwa sasa hawapo katika mipango ya mreno huyo na inaeleweka mbrazil Alex amepeleka ombi la uhamisho huku Anelka akiweka wazi anaondoka mwezi January na kuna uwezekano mkubwa akasajiliwa na big spenders wa kirusi Anzhi Machakhala.

Timu nzima ya Chelsea sasa ipo katika mshtuko kwa kitendo cha Villas-Boas, na wachezaji hao wawili kwa sasa wamekuwa wakifanya mazoezi na kikosi cha pili cha Chelsea huku wakivuta muda kuondoka Stamford Bridge.

FERDINAND AHAMA KWAKE BAADA YA KUTISHIWA MAISHA


Anton Ferdinand amelazimika kuhama nyumbani kwake kwa ajili ya usalama wake mwenyewe baada ya kupokea vitisho vya kuuliwa mwezi uliopita.

Polisi walikuwa concerned na message za vitisho zilizotumwa kwa mlinzi huyo wa QPR usiku wa kuamkia mechi dhidi ya Manchester City, hivyo wakamshauri yeye pamoja na familia yake kuchukua tahadhari mara moja.

Vitisho hivyo vimekuja huku kukiwa na sakata la nahodha wa Chelsea John Terry akituhumiwa kumtukana kibaguzi Ferdinand wakati wa mechi ya lgi kati ya QPR dhidi ya Chelsea at Loftus Road.

Kutokana na ushauri wa polisi, mchezaji huyo ambaye ni ndugu wa damu wa beki Manchester United Rio Ferdinand akaamua kuhama katika nyumba yake pamoja na familia yake kwa kuogopa kudhuriwa na watu waliomtumia msg za kutishia maisha yake

TEVEZ AENDELEA KUCHEZA GOFU KWAO, HUKU VILABU VYA ULAYA VIKIMGOMBEA.
AC Milan wanaamini wapo karibu kuweza kushinda vita ya kumsaini Carlos Tevez japokuwa wanapata upinzani mkubwa kutoka kwa mabillionea wapya kutoka Urusi Anzhi Makhachkala.

Man City wanataka mnunuzi amsaini Tevez kwa dili la kudumu mwezi January, huku Milan wameshatangaza kwamba watakuwa radhi kumsaini Tevez kwa mkopo huru huku wakipewa haki ya kumnunua mwishoni mwa msimu.

Ingawa, mtu wa ndani kutoka kwa mabingwa wa Serie A amesema kuwa City wapo tayari kupokea kiasi cha £2.6 ili kumuacha Tevez aende San Siro hadi mwishoni mwa msimu, according na gazeti la jiji la Milan maarufu kama Gazzetta dello Sport.

Tevez kwa sasa yupo zake Buenos Aires akipumzika na familia yake huku akicheza gofu katika viwanja mbalimbali akisubiri hatma yake na klabu yake ya Man City.

CARLOS TEVEZ AKIWA MKEWE KATIKA UWANJA WA GOFU JIJINI BUENOS AIRES-AREGENTINA.

Akiongea na Waandishi wa habari kocha wa Milan, Massimiliano Allegri ameutetea uamuzi wa kumtaka Tevez akisema: “Tevez ni mchezaji mkubwa, lakini ni mapema sana kumzungumzia.”

Kwa upande mwingine wa shilingi klabu ya Anzhi nayo imeingia katika vita ya kumnasa Carlitos, na wanaweza kwa urahisi kabisa kuilipa City zaidi ya £20m ili kumtia kibindoni Tevez ili ashirikiane na Samuel Eto’o. Timu nyingine ambayo imeonyesha nia kwa Tevez ni Dynamo Moscow, ingawa Milan wana imani na nafasi kubwa ya kumsaini Tevez kwa kuwa mchezaji pamoja na wakala wake wanaonekana kutokuwa tayari kuhamia Russia tena wakati huu baridi.

WALIOMUITA STURRIDGE "NYANI" KUFUNGIWA MAISHA STAMFORD BRIDGE.


Klabu ya Chelsea imetishia kuwafungia maisha mshabiki au mashabiki wowote watakaokutwa na hatia ya kufanya vitendo vya kibaguzi dhidi ya wachezaji weusi ndani ya timu hiyo.

Hivi karibuni mchezaji mwenye asili ya kiafrika Daniel Sturridge alikutwa na mkasa wa kufanyiwa vitendo vya kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa timu yake ya Chelsea.

Huku uchunguzi ukiwa unaendelea at Stamford Bridge baada ya malalamiko kutolewa na uongozi wa Chelsea kwamba baadhi ya mashabiki wenye uwezo wa kiuchumi walimuita ‘nyani’ Sturridge wakati wa mchezo wa Champions league dhidi ya klabu ya Genk, iliyofanyika nchini Ubelgiji wiki mbili zilizopita.

Hivyo klabu hiyo inafikiria kutoa adhabu ya kifungo cha maisha cha kutoingia uwanjani kwa watakaopatikana na hatia juu ya malalamiko hayo.

NGORONGORO WAANZA NA DROO COSAFA CUP


Timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Taifa Ngorongoro Heroes wametoka sare na mabingwa watetezi wa kombe la vijana la COSAFA, Zambia, mchezo uliochezwa katika jiji la Gaborone, Botswana.

Katika mchezo huo Ngorongoro wakishiriki kama timu mwalikwa walikuwa wa mwanzo kufungua ukurasa wa magoli kupitia kwa mshambuliaji hatari wa Azam Academy Msuvan HappyGod katika dakika ya 5 ya mchezo.

Goli hilo la Happygod lilidumu kwa mda wa dakika 5 na mnamo dakika ya 10 Evans Kangwa alisazisha goli hilo akiunganisha krosi ya Reynold Kampamba.

HappyGod alirejea tena kwenye nyavu katika dakika ya 25 lakini goli hilo lilidumu kwa dakika 3 pale Kangwa alipowasawazishia Wazambia kwa mkwaju wa penati kufuatia kuangushwa kwa Kampamba katika eneo la hatari.

Katika dakika 41 Ngorongoro walijipatia goli la 3 kupitia kwa Hassan Kessy na mnamo dakika ya 44 HappyGod alishindwa kuiandikia goli la 4 Ngorongoro na kujipatia Hat-trick na kupelekea timu kwenda mapumziko kwa Tanzania (Ngorongoro) kuwa mbele kwa goli 3 dhidi ya 2 ya Zambia.

Zambia walisawazisha tena katika dakika ya 84 kupitia kwa Alex
Sichone na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 3-3.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo la C ulishuhudia South Africa wakiwachapa goli 4-0 Mauritius, Na kushika usukani wa kundi hilo.

Friday, December 2, 2011

HARRY REDKNAPP NA SCOTT PARKER WANYAKUA TUZO ZA FA MWEZI NOVEMBA


Mwezi wa November umeonekana kuwa bora sana kwa Tottenham Hotspurs sio kwa matokeo uwanjani bali hata katika tuzo za mwezi huo kutoka kwa chama cha soka cha nchini England.

Kupitia tuzo za kila mwezi zitolewazo na FA, kocha wa Tottenham Harry Redknapp na kiungo Scott Parker wamefanikiwa kushinda tuzo wa kocha bora na mchezaji bora wa Barclays premier league kwa mwezi November.

Redknapp na Parker walikabidhiwa tuzo zao leo wakiwa mazoezini.

Mwezi uliopita wawili hawa kwa pamoja waliiongoza na kuiwezesha Spurs kushinda mechi dhidi ya Fulham, Aston Villa, and West Bromwich Albion.

BREAKING NEWS: MAKUNDI YA EURO 2012 - ENGLAND YAPANGWA KUNDI MOJA NA UFARANSA


GROUP A

Poland

Greece

Russia

Czech Republic

GROUP B

Holland

Denmark

Germany

Portugal

GROUP C

Spain

Italy

Republic of Ireland

Croatia

GROUP D

Ukraine

Sweden

France

England

UNAIKUMBUKA HII YA PAOLO DI CANIO?

KIEMBA NA KANONI BYE BYE MSIMBAZI


Wachezaji Amri Kiemba, Salum Kanoni na Shija Mkina ni miongoni mwa nyota wa ‘Wekundu wa Msimbazi’, Simba walioondolewa rasmi kwenye kikosi chao kitakachomalizia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, imefahamika.

Wachezaji hao, pamoja na washambuliaji Shija Mkina na Mohamed Kijuso, wameondolewa Simba kwa kutolewa kwa mkopo na kuuzwa jumla kupitia dirisha dogo la usajili lililofungwa juzi saa 6:00 usiku na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Akizungumza jana, Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa Kiemba amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Polisi Dodoma, Mkina (Kagera Sugar) na Kanoni (Moro United) na Kijuso ameuzwa jumla kwa klabu ya ‘maafande’ wa Ruvu Shooting.

Kamwaga amesema kuwa katika kujiimarisha zaidi, wamemrejesha Derick Waluya waliyetaka kumjumuisha mwanzoni mwa msimu lakini ikashidikana baada ya beki huyo wa kimataifa kutoka Uganda kuumia.

Simba pia wamewapandisha wachezaji watano kutoka katika kikosi chao cha Simba B ambao ni Abdalah Seseme, Miraji Said, Frank Selule, Hassan Rajabu na Ramadhan Seme.

Katika hatua nyingine, kiungo Ramadhani Chombo ‘Redondo’ wa klabu ya Azam ataendelea kuitumikia timu yake na wala sio Moro United kama ilivyokuwa ikivumishwa.

Taarifa zaidi zimedai kuwa Redondo atabaki Azam baada ya kugonga mwamba kwa jaribio la kumtoa kwa mkopo kutoka katika klabu yake kwenda Moro United.

RAMADHAN WASSO, MUKENYA NA WANAIGERIA KUONGEZA NGUVU COASTAL UNION


Timu ya Coastal Union imetangaza majina ya wachezaji waliowasajili wakati wa dirisha dogo
kwa ajili ya kuwatumia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akitangaza majina hayo, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Hemed Aurora alisema wachezaji waliosajiliwa wametoka klabu mbalimbali hapa nchini wengine wakiwa ni wachezaji huru.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Felix Ameche na Samuel Temi wote raia wa Nigeria. Ramadhani Wasso( huru), Ahmed Shiboli kutoka Simba aliyechukuliwa kwa mkopo, Edwin Mukenya (huru), Lameck Dayton (Villa Squad ), David Changula (Azam FC), Laurent Mugia, Mugenzi Philipo na Bakari Mohamed ambao wote ni huru.

Alisema kuwa katika usajili huo wamewatoa baada ya wachezaji kwenye timu za ligi daraja la kwanza hapa nchini na kuwataja kuwa ni kipa Omari Hamis aliyepelekwa kwa mkopo timu ya Kwarara FC ya Zanzibar inayoshiriki ligi daraja la pili.

Wengine ni Konji Yohana na Abdallah Ulasi na Ramadhan Nyumbi waliopelekwa kwa mkopo AFC Arusha na Omari Maligwa (Morani SC).

Aliwataja walioachwa kuwa ni Yahaya Akilimali kutokana na kushindwa kuripoti tangu
alivyosajiliwa, Juma Salum, Sabri Makame, Abdallah Abasi,Hassani Banda na Farouq Ramadhani ambao walienda Oman kushiriki Kombe la Mafuta.

HATMA YA ZANZIBAR CECAFA CUP


Safari ya Zanzibar Heroes katika michuano ya CECAFA Tusker Chalenji Cup itaamuliwa na sheria ya kumpata best losser, kufuatia goli la Amissi Cedric lililo wapa ushindi Burundi wa goli 1-0 pala walipowakabili Uganda.

Katika mchezo wa awali uliokuwa wa upande mmoja, Zanzibar Heroes waliichapa Somalia magoli 3-0, huku wakipoteza nafasi lukuki za kujipatia magoli zaidi.

Zanzibar Heroes iliyokuwa chini ya Kocha muingereza Stewart Hall, wakicheza bila ya mshambuliaji wao hatari Ally Badri Ally waliandika goli la kwanza kupitia kwa Selemani Kasim Selembe katika dakika ya 6 kufuatia makosa ya mabeki wa Somalia katika kuondosha mpira kwenye Hatari. Goli hilo lilidumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili kiliendelea kwa Zanzibar Heroes kuutawala mchezo na ndani ya dakika 5 waliandika goli la pili kufuatia mpira uliomtoka kipa na kumkuta Abdul Halim Hamadi na kufunga goli la pili, huku la tatu likifungwa na beki Aggrey Morise. Mpaka filimbi ya mwisho Zanzibar 3-0 Somalia.


Katika mchezo wa pili ulishuhudia Waganda wakipoteza mchezo mbele ya Burundi kufuatia kwa goli la Amissi Cedric lililo dumu dakika zote za mchezo.

Katika mchezo huo ulio malizika kwa Burundi kuichapa goli moja Uganda. Waganda walipoteza nafasi kadha kupitia kwa washambuliaji wake walio ongozwa na Emmanuel Okwi.

Kwa matokeo hayo Burundi wanamaliza wakiongoza kundi huku Uganda wakiwa wapili. Zanzibar itabidi wangoje hekima za CECAFA kama watapata nafasi katika best loser.

VITA YA RONALDO NA MESSI KWENYE LA LIGA MWEZI NOVEMBER

NOVEMBER STATISTICS370MINUTES PLAYED
279
3GOALS
6
0PENALTIES
3
0ASSISTS1
19 / 7 (36.8%)
TOTAL SHOTS / ON GOAL
16 / 8 (50%)
250 / 200 (80%)
PASSES / COMPLETED135 / 110 (81.5%)
9
FOULS SUFFERED7
6.75GOAL.COM
AVERAGE RATING
7.67
162011-12 LA LIGA GOALS16
26 (22)
2011-12 COMPETITIVE GOALS (APPEARANCES)
20 (19)
http://i1.goal.com/files/images/stats/goal/team-logos/1/451_48x48.jpg

SIMBA: BASENA HANA CHAKE KWETU


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia katibu mkuu wa klabu hiyo umesema hauna chochote unachodaiana na kocha Moses Basena baada ya kumalizanaye kisheria na hana sifa ya kudai fidia kimkataba.

Mbali na kauli hiyo pia uongozi huo umedai haukatishia mkataba na kocha huyo badala yake umesitisha kutokana na kutokuwa na vigezo kutokana na kukosa vyeti vya kufundisha kama kocha mwajiriwa.

Basena aliyechukua mikoba ya kuifundisha Simba toka mikononi mwa Mzambia Patric Phiri katika mzunguko wa pili wa ligi wa msimu uliopita jana alikaririwa na gazeti la mwananchi akidai kama Simba wamemkatishia mkataba wake ni vyema wamlipe kiasi cha Shs 99 Milioni kama mshahara wake baada ya kumatishia mkataba mbali na fidia ambayo ataafikia na uongozi huo.

Katibu mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema ni vyema umma ukafahamu hawana nia mbaya na kocha huyo bali kisheria hana sifa ya kulipwa kimkataba kwani hakuwa na kibali rasmi cha kufundisha kama kocha.

"Napenda watu na mashabiki wa soka waelewe kitu kimoja, Basena hawezi kutudai tumlipe fidia kimkataba kwani hana sifa hiyo, hakuwa na kibali rasmi cha kufundisha na juzi ndio ametuma vyeti vyake ambavyo sisi kama uongozi tayari tumemsitishia baada ya kupata kocha mwingine na tunavyofahamu hatudai na sisi hatumdai,"alisema Mtawala.

Awali uongozi wa Simba ulidai Basena angewasili hapa nchini Disemba 6 kwa ajili ya kumalizana naye huku kocha huyo akisema hafahamu lolote kuhusu kukatishiwa mkataba huo na anakuja kwa ajili ya kuendelea na mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Wakati hayo yakijiri tayari Simba amempa mkataba wa miezi6 kocha Mserbia Milovan Curcovic wa kuifundisha timu hiyo na anatarajia kuanza kazi rasmi Disemba10 mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Chalenji.

Thursday, December 1, 2011

MKWASA AKERWA NA MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA


Manager wa timu ya soka ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) Charles Boniface Mkwasa
ameshutumu tabia za mashabiki wa soka nchini kuingiza siasa za Simba na Yanga katika kushangilia timu ya taifa.

Mkwasa alisema hayo wakati akijibu swali kama kitendo cha kumuingiza kiungo wa Yanga Nurdin Bakari katika mechi ya Kombe la Chalenji juzi dhidi ya Djibouti kilitokana na kutaka kuungwa mkono na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakiizomea timu hiyo karibu muda wote wa mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Stars iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Katika mchezo wa juzi kabla ya Bakari na Godfrey Taita kuingia kipindi cha pili kikosi cha timu hiyo hakikuwa na mchezaji yoyote kutoka Yanga hali iliyofanya mashabiki wa Yanga kuizomea mara kwa mara timu hiyo.

Akizungumzia hali hiyo kocha Mkwasa alisema sio vizuri kwa mashabiki kuingiza siasa za
U Simba na U Yanga katika kushangilia timu hiyo kwani hiyo siyo Simba wala Yanga bali
ni timu ya Taifa.

Mkwasa alisema kuna kipindi timu ya Taifa iliundwa na wachezaji zaidi ya 15 kutoka Yanga na wala hakuwahi kuona mashabiki wa Simba wakiizomea timu hiyo kwa kuwa haikuwa na wachezaji wao wengi.

“Ni jambo la kawaida kuna kipindi Yanga ilikuwa na wachezaji zaidi ya 15 katika kikosi cha timu ya Taifa lakini sijawahi kuona mashabiki wa Simba wakiizomea timu hiyo,”alisema
Mkwasa kwa masikitiko.

Aliwataka mashabiki wa soka nchini kuiunga mkono timu hiyo na kwamba kama ikifanya
vibaya basi wajue aibu ni ya nchi nzima.

Maneno ya Mkwasa yaliungwa mkono na nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja aliyesema
anasikitishwa na hali hiyo na kuongeza wao watakuwa pamoja na wale wote wanaowaunga mkono mpaka mwisho wa mashindano.

“Sio kitu kizuri lakini kama wanatuzomea waache watuzomee lakini sisi tupo pamoja na wale wote wanao tuunga mkono,”alisema Kaseja.

BASEAN SINATAARIFA JUU YA KIBARUA CHANGU KUOTA NYASI SIMBA - NINA MKATABA MPAKA 2013

Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba, Moses Basena ambaye juzi ilitangazwa amefukuzwa kazi ndani ya klabu yake na kibarua chake kuchukuliwa na Mserbia Milovan, ameitaka klabu hiyo kuheshimu mkataba alioingia nao Septemba Mosi mwaka huu, kinyume chake wajiandae kumlipa mamilioni.

Uongozi wa Simba kupitia Ofisa Habari wake, Ezekiel Kamwaga ulisema jana kuwa umemsimamisha kazi kwa muda kocha huyo na nafasi yake imechukuliwa na kocha Milovan Cirkovic, ambaye tayari amesaini mkataba wa miezi sita.

Akizungumza kwa simu kutoka Uganda, Basena alisema: "Kama ambavyo mimi nimekuwa nikiheshimu mkataba wangu na klabu, ndivyo uongozi unavyopaswa kuheshimu.

"Awali nilipewa mkataba wa miezi sita, nikamaliza na kupewa mwingine wa miaka miwili kuanzia Septemba Mosi hadi Septemba 2013. Ninachofahamu, mimi bado kocha wa Simba na si vinginevyo," alisema Basena.

Kocha huyo raia wa Uganda ambaye hekaheka za kutotakiwa Simba zilianza mara baada ya kupoteza mchezo na Yanga, alisema endapo klabu yake itakuwa tayari kuvunja mkataba wake hana tatizo na uamuzi huo.

Aliongeza kuwa, iwapo uongozi wa Simba utaamua kuvunja mkataba wake, jambo la kwanza ni kumpa taarifa na pia sababu za kusitisha ajira yake, na mwisho kulipwa haki zake zote ikiwemo fidia ya kuvunjwa mkataba.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, mshahara wa Basena kwa mwezi ni dola 2500 (sawa na shilingi 4.5milioni), na ni miezi miwili tu imepita tangu amwage wino kwenye mkataba huo mpya.

Iwapo Simba watavunja mkataba wake watalazimika kumlipa misharaha ya miezi 22 iliyosalia kwenye mkataba wake, ambayo ni sawa na shilingi 99milioni mbali na fidia ya kuvunja mkataba.

"Leo Simba wakiamua kuvunja mkataba wangu, sina tatizo na mimi sitakuwa wa kwanza kukutana na hali hiyo, ila cha msingi ni kulipwa pesa zangu zote," alisema Basena huku pia akiushangaa uongozi wa Simba kutofanya naye mawasiliano yoyote.

Alipoulizwa ni kiasi gani anastahili kupewa kama mtakaba wake utavunjwa, alisema: "Hii ni siri yangu na uongozi, siwezi kusema ni shilingi ngapi lakini ni mamilioni ya pesa.

"Mimi si lazima nije Tanzania kuvunja mkataba na kudai pesa zangu. Wanaweza kunitumia nikiwa huku (Uganda). Wanitumie kupitia benki, mbona haya mambo ni rahisi sana," aliongeza.

Pia alishangazwa na uongozi wa Simba kutumia muda mwingi kuzungumza hatima yake kupitia vyombo vya habari kabla ya kufanya naye mawasiliano.

"Wewe leo (jana) unaniambie eti nimesimamishwa kazi--mbona mimi sijui? Mwingine akaniambia Simba wamevunja mkataba wangu, hilo pia sifahamu. Kama haya yote ni kweli kwanini uongozi haunipi taarifa mpaka nisikie toka kwa waandishi?," alihoji.

Alisema zaidi kuwa, hana sababu ya kupingana na uamuzi wa klabu ya Simba katika kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi, ila anajivunia kumaliza mzunguko wa kwanza timu ikiwa inaongoza msimamo.
"Sioni baya nililofanya Simba, nimeacha timu kwenye nafasi nzuri, wachezaji, mashabiki na wapenzi walikuwa wakinipa sapoti kubwa, hili ni jambo la kujivunia kwangu," alisema.

Basena alisema kuwa alipaswa kurejea nchini Desemba 6, lakini kwa vile hajamaliza mambo ya msiba, anawasiliana na uongozi ili aongeze muda zaidi kabla ya kuja kuendelea na kazi yake.

Suala la Basena kwa siku za hivi karibuni limekuwa likiteka kurasa za vyombo, huku baadhi ya taarifa zikidai amefukuzwa kazi na zingine zikidai amesimamishwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ameshindwa kuwasilisha vyeti vya taaluma yake.

Hata hivyo, kuhusu suala la vyeti, Basena alisema kuwa tayari alishavituma Simba, lakini uongozi wa klabu hiyo uliendelea na mchakato wa kumsainisha mkataba kocha mpya kwa vile vyeti hivyo vilichelewa kufika.


Mwananchi

Wednesday, November 30, 2011

HATIMAE USAJILI WA REDONDO KWENDA SIMBA WAKWAMA

KWA MUJIBU WA CHANZO RASMI TOKA NDANI YA KLABU YA SIMBA UHAMISHO WA KIUNGO RAMADHANI CHOMBO 'REDONDO' KUTOKA AZAM UMESHINDIKANA,
'' MWANZONI AZAM WALITAKA KUTUUZIA REDONDO KWA ADA YA UHAMISHO WA DOLA ELFU AROBAINI ( $ 40,000 ) SISI TUKAWAMBIA HATUNA UWEZO WA KUTOA KIASI HICHO CHA PESA BADALA YAKE TUKAWAPA OFA YETU AMBAYO ILIKUA NI KUMCHUKUA REDONDO KWA MKOPO PAMOJA NA KUWAPATIA KIASI CHA TSH MILIONI 10, BAADA YA HAPO TUKAWAACHA WAKIIJADILI OFA YETU. JIONI HII TUMEPOKEA SIMU KUTOKA AZAM WAKISEMA HAWATAWEZA KUMUACHIA KIUNGO CHINI YA ADA YA UHAMISHO WA TSH MILIONI 30''.

OFFICIAL: MALIKA NDEULE AJIUNGA NA VILLA SQUAD KWA MKOPO

KLABU YA VILLA SQUAD IMEFANIKIWA KUWAHAMISHA KWA MKOPO WACHEZAJI WANNE TOKA AZAM FC KWA MKOPO AKIWEMO BEKI MAHILI WA KULIA MALIKA NDEULE, WACHEZAJI WENGINE WALISAJILIWA KWENYE HILI DIRISHA DOGO NI KAMA IFUATAVYO:

LEON KIMATHI-HURU
ALLY MANZI- HURU
SELEMAN MSENGI- HURU
GERALD LUKINDO- HURU
KHATIB KUDUKU- HURU
SIXBERT MOHAMED- HURU
MARTIN LUPART- HURU
JOSEPH MUHANDI- KUTOKA AZAM
FRED COSMAS -KUTOKA AZAM
DAUD GABRIEL- KUTOKA AZAM
IBRAHIM RAJAB 'JEBA' -KUTOKA AZAM

COUNTDOWN DIRISHA DOGO LA USAJILI BONGO: AFRICAN LYON

Wakati dirisha dogo la usajili wa Bongo likielekea kufungwa hivi punde klabu ya African Lyon imefanikiwa kumsajili kiungo Justus Anene kutoka klabu ya URA ya nchini Uganda,pia timu hiyo imefanikiwa kumnasa beki Obinna Mustafa raia wa Nigeria toka klabu ya Zanzibar Ocean View.

WALIONGIA:

SAMUEL NGASA-HURU
JUSTUS ANENE-kutoka URA ya Uganda
Mbera Mike- Lugazi Utd ya Uganda
Erick Majaliwa- kutoka JKT RUVU
Mohamed Hamad-kutoka Mwanza Utd
Obinna Mustafa- Kutoka Ocean View ya Zanzibar.

WALIOTOKA

Shabani Aboma-ameachwa
John Njama -amekwenda Police Central ya Dar Es Salaam
Bakari Nzige- Polisi Dodoma

OFFICIAL:DERRICK WALUYA AREJEA SIMBA

TAARIFA NILIZOZIPATA HIVI PUNDE SIMBA IMEMREJESHA RASMI KIKOSINI BEKI WAKE RAIA WA UGANDA DERRICK WALUYA.
WAKATI HUO HUO DIRISHA DOGO LA USAJILI LIKIELEKEA UKINGONI KLABU HIYO IMEDHIBITISHA KUWATOA KWA MKOPO WACHEZAJI WAKE WATATU KWENDA VILABU MBALI MBALI.
WACHEZAJI HAO NI:
BEKI WA PEMBENI SALUM KANONI - AMEKWENDA MORO UTD
KIUNGO SHIJA MKINA- AMEKWENDA KAGERA SUGAR
KIUNGO AMRI KIEMBA -AMEKWENDA POLISI DODOMA

BREAKING NEWS: UHAMISHO WA RAMADHANI CHOMBO 'REDONDO' KWENDA MORO UTD WAKWAMAUHAMISHO WA KIUNGO RAMADHANI CHOMBO KWENDA MORO UTD KWA MKOPO KUTOKEA AZAM FC UMESHINDIKANA, TAARIFA AMBAZO BLOG HII IMEZIPATA HIVI PUNDE ZINASEMA KWASASA KIUNGO HUYO ATABAKI AZAM AU ATAHAMIA SIMBA IWAPO OFA YA SIMBA KUMCHUKUA KWA MKOPO KWA ADA YA TSH MILIONI 10 ITAKUBALIWA,PAMOJA NA SIMBA KUIPA AZAM MILIONI 10 PIA IPO TAYARI KUMLIPA MSHAHARA KIUNGO HUYO ALIYEBAKISHA MWAKA MMOJA NA NUSU KWENYE MKATABA WAKE NA AZAM FC. WAKATI HUO HUO UONGOZI WA AZAM UPO KWENYE KIKAO WAKIIJADILI OFA HIYO TOKA KLABU YA SIMBA.

SAMIR NASRI NUSURA AZICHAPE NA FRIMPONG


Samir Nasri jana nusura apigane na mchezaji wa Arsenal Emmanuel Frimpong wakiwa njiani kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo katika uwanja wa Emirates baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo uliozikutanisha Manchester City dhidi ya Arsenal.


Kumekuwa na uhusiano mbaya kati yao tangu Frimpong alipo react juu ya uhamisho wa £24m wa Nasri kujiunga na City in August baada ya kutweet: “Pesa ndio mzizi wa ushetani”

Wachezaji hawa wawili walipokutana jana katika mechi ya Carling cup ambayo Arsenal walifungwa waliendelea kuzozana mara tu baada ya mchezo huo.