Search This Blog

Saturday, December 14, 2013

PAMBANO LA YANGA NA KMKM KATIKA PICHA

 Kocha wa Yanga, Ernstus Brands (kulia), akifuatilia pambano la Yanga na KMKM katika Uwanja wa Taifa leo..mechi hiyo imemalizika kwa Yanga kupata ushindi wa mabao 3-2.

Benchi la Ufundi la timu ya KMKM ya Zanzibar.

 David Luhende wa Yanga akiwania mpira.
 Mshambuliaji wa Yanga, Reliants Lusajo akichuana na mchezaji wa KMKM, Mwinyi Ameir Makungu.
 Beki wa KMKM, Faki Ali Amad (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa pembeni wa Yanga, Simon Msuva katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Msuva akichuana na Faki Ali Hamad.
 Kipa wa Yanga Juma Kaseja akiokoa moja ya hatari langoni mwake.

Mshambuliaji wa KMKM, Nassor Ali Omar akiruka juu kuwania mpira sambamba na Simon Msuva wa Yanga.
 Mashabiki wa Yanga.
Kikosi cha Yanga.

BAADA YA KUUMIA - HIZI NDIO MECHI 8 ATAKAZOZIKOSA ROBIN VAN PERSIE

Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie atakosekana katika kikosi cha Manchester United kwa mwezi mmoja kutokana na maumivu ya nyama za paja.  

Mshambuliaji huyo wa kiholanzi alipata maumivu hayo wakati akipiga kopna katika mchezo wa ushindi dhidi ya Shakhtar Donetsk jumanne usiku na hatocheza tena mpaka mwakani.  

Kwa maana hiyo mshambuliaji atakosa mechi takribani 8 kwa mujibu wa kocha wake David Moyes.

Robin Van Persie atakuwa nje kwa mwezi mzima. Alipata maumivu  wakati akipiga kona katika dhidi ya Shakhtar. Ni wakati mbaya kwetu ukizingatia rekodi nzuri tuliyonayo pindi RVP anapocheza pamoja na Rooney na hawacheza pamoja kwa muda kiasi."

MECHI ATAKAZOKOSA ROBIN VAN PERSIE
Aston Villa (A), Dec 15, Premier League
Stoke (A), Dec 18, League Cup
West Ham (H), Dec 21, Premier League
Hull (A), Dec 26, Premier League
Norwich (A), Dec 28, Premier League
Tottenham (H), Jan 1, Premier League
Swansea (H), Jan 5, FA Cup
Swansea (H), Jan 11, Premier League



Friday, December 13, 2013

CR7 AZINDUA TOVUTI MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA VIVA RONALDO.


MATENGENEZO YA UWANJA WA SOKOINE MBEYA YAENDELEA!



 Saleh Kupaza (kulia ) akiwa na mtaalam wa kutengeneza viwanja...


HATIMAE SIMBA YAMALIZANA NA IVO MAPUNDA NA BEKI DONALD MOSOTI OMWANWA



Simba pia imemsainisha beki wa kati wa Gor Mahia Donald Mosoti Omwanwa,amesaini mkataba wa miaka miwili mbele ya katibu mkuu wa Simba Evodius Mtawala.



Donald Mosoti Omwanwa.....

 Ivo Mapunda akisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba mbele ya katibu mkuu wa timu hiyo Evodius Mtawala.

SIKU ZANZIBAR ILIPOFUKUZWA HOTELINI KENYA!



 Rais wa Chama Cha Soka Nchini Kenya Sam Nyamweya alikuwepo kusawazisha songombingo.



 Katibu mkuu wa CECAFA Nichoras Musonye pia alikuwepo kutafuta ufumbuzi

FA MIKOA YAPATA MIPIRA KUTOKA TFF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa mipira kumi kwa kila chama cha mpira wa miguu cha mkoa ili isaidie kuendesha ligi za mikoa husika.

Mipira hiyo 250 yenye thamani ya sh. 16,250,000 tayari imeanza kutumwa kwa makatibu wa vyama vya mikoa husika. Mpira mmoja una thamani y ash. 65,000.

Ni maratajio ya TFF kuwa mipira hiyo itakuwa chachu kwa vyama vya mikoa katika uendeshaji wa ligi hizo.

MITIHANI YA WAAMUZI KUFANYIKA JUMAPILI

Robo ya mwisho ya mitihani ya waamuzi (Cooper Test) na utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa mwaka 2013 kwa waamuzi inafanyika Jumapili (Desemba 15 mwaka huu).

Mitihani hiyo inayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam inashirikisha waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) na wale wa kundi la waamuzi (elite) ambao wanaweza kupendekezwa kupewa beji za FIFA.

Wakufunzi wa mitihani hiyo ya waamuzi ni Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.

Waamuzi wa FIFA watakaofanya mitihani hiyo ni Ferdinand Chacha, Hamis Chang’walu, Israel Mujuni, Jesse Erasmus, John Kanyenye, Josephat Bulali, Mgaza Kinduli, Oden Mbaga, Ramadhan Ibada, Samwel Mpenzu na Waziri Sheha.

Washiriki kutoka kundi la elite ni Charles Simon, Dalali Jaffari, Hellen Mduma, Issa Bulali, Issa Vuai, Janeth Balama, Jonesia Rukyaa, Judith Gamba, Lulu Mushi, Martin Saanya, Mfaume Nassoro na Mohamed Mkono.

KILIMANJARO STARS YAREJEA DAR

Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika jana jijini Nairobi, Kenya inarejea jijini Dar es Salaam leo.

Kilimanjaro Stars iliyomaliza michuano hiyo katika nafasi ya nne inatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 kamili jilioni kwa ndege ya RwandAir.

Wenyeji Kenya (Harambee Stars) ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Sudan mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa jana Uwanja wa Nyayo.

MOISE KATUMBI: LENGO LETU MSIMU UJAO KUCHEZA KLABU YA BINGWA YA DUNIA NA KUSHINDA

Mmiliki na mwenyekiti wa timu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo Moise Katumbi amesema ana mpango wa kuiimairisha timu hiyo ili iwe na nguvu ya kushiriki katika mashindano ya kidunia, Katumbi anaamini kuwa anaweza kuifikisha timu hiyo katika ngazi ya fainali za kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu.
Pamoja na TP Mazembe kushindwa katika michuano ya kombe la shirikisho la CAF lakini bado Katumbi anasema anajiandaa vyema na msimu ujao na mashindano mengine."Malengo yetu ni kuleta ushindani mkubwa na ninaamini tunaweza kufikia mafanikio kwa kile tulichonacho sasa"alisema Katumbi.
Katumbi pia ameiambia BBC kuwa iwapo wataimarisha zaidi timu yao na kwamba haoni ni kwanini siku moja TP Mazembe siku moja wasishinde kombe la dunia.
Mwaka 2010, timu hiyo ya soka ya Mazembe ndio iliyokuwa klabu ya kwanza toka bara la Afrika kutinga fainali katika mashindano ya kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu lakini wakaondolewa na klabu ya Inter Millan ya Italia.
Baada ya michuano hiyo ya michuano hiyo ya shirikisho timu hiyo toka mji wa Lubumbashi nchini Demokrasia ya Congo wanatarajiwa kurejea tena katika michuano ya ligi ya mabingwa mwaka ujao.
Tambo hizi za Mazembe ni kutokana na vipaji vya kutosha kutoka katika shule ya vipaji vya michezo ambapo wanatarajia baada ya miaka mitatu wantakuwa na wachezaji wenye uwezo wa kuwafikisha na kushinda kombe la dunia.
Hata hivyo Katumbi kiongozi wa miongoni mwa timu tajiri barani Afrika amesema kuwa ameweza kuhakikisha fedha zinapatikana ili kuimarisha kikosi chake,kutengezeza uwanja mpya na wa kisasa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege ya timu.
Mipango yake katika kupata wachezaji wa kimataifa inaendelea ambapo kwa sasa anawachezaji nchi za nje ambapo kwa ana wachezaji kutoka nchi za Tanzania, Ghana, Zambia, Cameroon, Botswana na hivi karibuni amesajili kutoka Malawi.
Timu hii ya TP Mazembe ni miongoni mwa timu ambazo wachezaji wake wanalipwa vizuri kwa viwango vya Afrika ikiwa ni jitihada za Katumbi kupunguza kaksi ya vipaji vya Afrika kupotelea ulaya.
"Wachezaji wazuri wa Afrika wanakwenda ulaya kwa sababu ya malipo mazuri kutokana na kutolipwa vizuri hapa Afrika" anasema Katumbi.
Katumbi anasema kuwa sera yao ni kuwachukua wachezaji toka nchi za Afrika ili kuonyesha umoja ndania ya bara hilo na kwamba Afrika ni nnzuri lakini kinachotakiwa ni umoja hasa kutokana na mapigano ambayo yamekuwa yakitokea kila siku katika bara la Afrika.

Thursday, December 12, 2013

AIRTEL TANZANIA KUMLETA ANDY COLE DAR ES SALAAM KUSHIRIKI PROMOSHENI YA MIMI NI BINGWA

 Andy Cole akionyesha umahiri wake katika kulisakata kabumbu alipokuwa akitoa somo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makongo ya jijini Dar es salaam mara ya mwisho alipotembelea Tanzania.


Na Mwandishi Wetu

MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole anatarajia kutua jijini Dar es Salaam Ijumaa hii, imethibishwa.
Ziara ya Cole nchini inalenga kuwapatia uzoefu washindi wa tiketi za promosheni ya Airtel ya 'Mimi ni Bingwa' ambao watasafiri kwenda kuangalia mechi za klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old Trafford pamoja na kukabidhi vifaa vya mazoezi  kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 17.

Hii ni ziara ya pili Tanzania kwa mchezaji Cole baada ya kutembelea Tanzania mwaka 2011 alipozindua mpango wa kutafuta vipaji wa Airtel Rising Star.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania, Bw Jackson Mmbando alisema kuwa mchezaji huyo mkubwa wa zamani wa Man U atakuwa na wakati wa kuzungumza na kushiriki mazoezi na wachezaji wa timu ya Tanzania chini ya miaka 17, timu ambayo wengi wao ni matunda ya mpango wa kuvumbua vipaji wa Airtel Rising Star.

"Andy Cole ataongea na nyota hao wanaochipukia, na kuwashawishi kuongeza jitihada zaidi katika michezo pamoja na kuwapatia mbinu za jinsi gani ya kufikia mafanikio katika fani yao ya michezo.

"Mbali na kuwaonyesha wachezaji hao njia ya mafanikio, mchezaji huyo mkubwa wa zamani wa Manchester United pia atakabidhi vifaa vya mazoezi kwa timu hiyo," alisema Mmbando.
Alisema kuwa Cole pia atahudhuria droo ya moja kwa moja (live) ya kuwatafuta na kuwatangaza washindi wa tiketi tatu za kwenda Old Trafford, kabla ya kuungana na washabiki wa Man U kuangalia mechi moja kwa moja (live) itakayoonyeshwa Coco beach kati ya Manchester United na Aston Villa itakayochezwa jumapili.

Rashid Jacob Kagomola na Dickson Lyatuu ni washindi wa kwanza wawili wa promosheni ya Mimi ni Bingwa waliojishindia tiketi za kwenda Old Trafford, ambapo zawadi zaidi ya shilingi milioni 40 tayari imetolewa kwa ajili ya washindi wa kila siku na kila wiki.
Mmbando alisema kuwa bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa katika promosheni, na kuongeza kuwa ili mteja kushiriki anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wa neno "BINGWA" kwenda namba 15656.

Aidha, alisema Airtel imeweka vituo mbali mbali ambavyo washabiki wa Man U wataweza kuangalia mechi za Manchester United moja kwa moja (live) kupitia luninga kubwa, na kutaja vituo hivyo kuwa ni Mbeya - Shaba Pub, Mwanza - Shooters Pub, Dodoma - Four ways, Dar es Salaam - Coco Beach, Morogoro - Nyumbani Lounge na Arusha - Empire Sports bar.

Mwaka 2011 kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania ilizindua mpango wa kuvumbua vipaji katika soka kwa ushirikiano na klabu ya Manchester United, uliolenga kuvumbua vipaji na kuviendeleza katika mpira wa miguu Tanzania.
 
Cole amekuwa na dhamira ya kuonyesha uzoefu wake kwa wachezaji nyota wanaochipukia ikiwa ni kama njia ya kuunga mkono maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu duniani.

UNAHISI KWELI MANCHESTER UTD MSIMU HUU WANA NAFASI YA KUBEBA UBINGWA WA UCL


BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA PILI - ARSENAL KUCHEZA 16 BORA DHIDI YA AIDHA BARCA, MADRID, ATLETICO, PSG AU BAYERN - TOA MAONI UNGEPENDA IPANGWE NA TIMU GANI?

TIMU ZA ENGLAND DHIDI YA TIMU AMBAZO ZINAWEZA KUPANGWA NAZO KATIKA 16 BORA YA CHAMPIONS LEAGUE. UNGEPENDA TIMU YAKO IPANGWE NA NANI? TOA MAONI…..

ARSENAL
Real Madrid
PSG
Bayern Munich
Atletico Madrid
Barcelona
CHELSEA
Bayer Leverkusen
Galatsaray
Olympiakos
Zenit St Petersburg
AC Milan
MANCHESTER CITY
Real Madrid
PSG
Dortmund
Atletico Madrid
Barcelona
MANCHESTER UNITED
Galatasaray
Olympiakos
Schalke
Zenit St Petersburg
AC Milan

 

VIDEO: NEYMAR APIGA HAT TRICK YA KWANZA BARCA NDANI YA DAKIKA 13 - WAKIIUA CELTIC 6-1


All Goals - Barcelona 6-1 Celtic - 11-12-2013... by video4all

DAVID MOYES ASAFIRI MPAKA JIJINI MADRID KUMUANGALIA KIUNGO KOKE - ATLETICO MADRID WATAJA BEI YA KUMUUZA


David Moyes alionekana kwenye dimba la Vicente Calderon kwenye mchezo wa  Atletico Madrid dhidi ya Porto usiku wa jana.

Kocha huyo wa Manchester United anategemewa kufanya usajili wakati dirisha la usajili mwezi ujao litakapofunguliwa baada ya kuwa na mwanzo mbovu.  

Huku Atletico nao wakiwa wamefuzu wakiwa hajafungwa na wakiongoza kundi lao, Moyes inawezekana
 hakuwa uwanjani pale kuangalia timu ambayo anaweza kukutana nayo raundi inayofuatia, kiungo wa klabu ya Atletico Koke anatajwa kuwepo kwenye rada ya Man United na usiku wa jana ilifahamika wazi kwamba kiungo huyo ana kipengele kinachoweza kumruhusu kuuzwa endapo tu klabu italipa kiasi kisichopungua €24m.
Hata hivyo, mkurugenzi wa michezo wa Atletico Madrid, Caminero, haamini kwamba Moyes alikuwa uwanjani pale kwa ajili ya kumfuatilia Koke.

“Inawezekana David Moyes alikuja hapa kuja kuangalia moja timu ambazo anaweza kukutana nazo mbeleni katika Champions League. Tumeonana na David, tumeongea lakini hakuniambia hasa kilichomleta hapa."

VIDEO: ARSENAL WAPIGWA 2 - 0 NA NAPOLI NA KUMALIZA KATIKA NAFASI YA PILI KWENYE KUNDI

MATOKEO YA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL APIGWA 2-0, CHELSEA ASHINDA, BARCA YAUA NEYMAR AKING'ARA VILIVYO




Chelsea 1-0 Steaua Bucuresti
Schalke 2-0 Basel

Napoli 2-0 Arsenal
Marseille 1-2 Borussia Dortmund

Barcelona 6-1 Celtic
AC Milan 0-0 Ajax

Atletico Madrid 2-0 Porto
Austria Wien 4-1 Zenit Petersburg

TIMU ZILIZOFUZU HATUA YA 16 BORA
Walioshika nafasi ya kwanza kwenye makundi: MAN UTD, Real Madrid, PSG, Bayern Munich, CHELSEA, Borussia Dortmund, Atletico Madrid, Barcelona.
Washindi wa pili: Bayer Leverkusen, Galatasaray, Olympiakos, MAN CITY, Schalke, ARSENAL, Zenit, AC Milan.

Wednesday, December 11, 2013

HIGUAIN: SIKUWAHI KUZUNGUMZA NA KLABU YA ARSENAL KUHUSU KUNISAJILI


Kikosi cha Arsene Wenger kinacheza na Napoli usiku huu katika mechi ya kuamua msimamo wa mwisho wa kundi F katika michuano ya Champions League.

Na japokuwa Wenger alijaribu kumsajili  Higuain Arsenal, mshambuliaji huyu wa kiargentina anasisitiza hakuwahi kuzungumza na klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

"Ndio," Higuain alijibu alipoulizwa na gazeti la  Times, kama kulikuwa na uwezekano wa kuhamia Arsenal katika kipindi cha kiangazi kilichopita.

"Lakini sikuwahi kuzungumza nao. Kulikuwa na mazungumzo baina ya Real Madrid na Arsenal, lakini ilikuwa ni Napoli ambao walikuja na kuninunua."

Wenger alidhani amefanikiwa kushinda vita ya saini ya Higuain kwa ada ya uhamisho kwa £23million lakini Napoli wakatoa ofa ya  £32m na kumsajili muargentina.

JUVENTUS YAAGA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA



Juventus ya Italia imetolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa katika ngazi ya vilabu barani ulaya baada ya kufungwa bao 1-0,bao hilo pekee limewekwa kambani na kiungo raia wa Uholanzi Wesley Sneijder.

Mchezo huo ilibidi ufanyike tena hii leo baada ya jana kusimamishwa kutokana na hali ya hewa.

RONALDO AWEKA REKODI YA MABAO UEFA CHAMPIONS LEAGUE!



MshambuliajiCristiano Ronaldo usiku wa jana alifunga bao moja wakati timu yake ya Real Madrid ilipopata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya FC Copenhagen.Bao hilo alilofunga Ronaldo lilikuwa la 9 na lilimwezesha kuweka rekodi mpya ya mabao kwenye michuano hiyo ya Uefa Champions League kwenye hatua ya makundi.
Ronaldo pia kwenye mchezo huo alikosa mkwaju wa penati.

MAKALA: KILIMANJARO STARS HAINA CHA KUJIVUNIA KUTOKA CECAFA CHALLENGE CUP


Na Baraka Mbolembole

  Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara ' kilimanjaro stars', ilipoteza mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya ukanda wa Africa Mashariki na Kati ( Cecafa Challenge Cup) na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars katika uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi. Stars ilicheza kandanda safi kwa muda mwingi wa kipindi cha pili, na kuwaweka wenyeji katika wakati mgumu. Kenya, wakicheza kwa tahadhari kubwa hasa baada ya kupata bao la kuongoza katika dakika ya tano ya mchezo, walitumia mbinu ya kupiga mashuti ya mbali baada ya ukuta wa Stars kuonekana kuwa mgumu kupitika.

  STARS IMEFELI KWA MARA NYINGINE

Ndani ya uwanja, kulionekana mabadiliko makubwa ya kiuchezaji, timu inaweza kubadilika katika mifumo tofauti na bado ikaonekana ikicheza vizuri, ila ukitazama michuano ya mwaka huu, timu nyingi zimeonesha kandanda safi na zimeonekana kupiga hatua fulani kiuchezaji. Eritrea, Somalia, Sudan Kusini, ni mataifa ambayo yamezoeleka kwa kugawa pointi kwa timu nyingine, kila mara, ila wakati huu timu hizi zimeonekana kuamka na kucheza mchezo mzuri ambao si tu kuwa ulipendezwa na wengi bali uliwaweka katika mazingira magumu timu nyingine. Timu hizi zilifanikiwa kupunguza idadi ya mabao ambayo walikuwa wakifungwa katika miaka ya nyuma.

Kwa, Kilimanjaro Stars, ambayo ilitwaa ubingwa huo kwa mara ya mwisho mwaka 2010, kabla ya kuondolewa katika hatua ya robo fainali, 2011, nusu fainali, 2012, ikiwa na kikosi chenye uzoefu wa michuano hiyo, Stars imeshindwa kwa mara nyingine kuvuka hatua hiyo ya nusu fainali katika mchezo ambao ulisimamiwa vizuri na mwamuzi pamoja na wasaidizi wake. Bao la mshambuliaji, Clifton Miheso ambaye aliuwahi mpira uliokuwa umetemwa na kipa, Ivo Mapunda baada ya ' kiki kali' ya mlinzi, Jockis Atudo lilizima kabisa mfumo wa kocha Kim Poulsen ambaye aliamua kuichezesha timu yake katika mfumo wa 4-4-2.

Kenya, iliwabana kwa kiasi kikubwa sana Stars katika eneo la kiungo, ambalo viungo Frank Domayo, na Amri Kiemba walionekana kucheza kwa taratibu mno, huku Mrisho Ngassa na Said Dilunga wakicheza kwa mtindo wa ' kuhama hama' wakitokea pembeni ya uwanja. Viungo wa Stars walionekana kuamka zaidi kipindi cha pili, lakini bado wakashindwa kutengeneza nafasi za kufunga, japo mara kadhaa walifanikiwa kufika katika eneo la hatari la Kenya. Umakini mdogo, papara, ni sehemu ya tatizo ambalo limeiangusha kwa mara nyingine tena Stars.

Hatua cha kujivua, kama soka zipo nchini ambazo zilicheza soka zuri zaidi kwa michezo mingi, Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini, Zambia, Uganda na hata Rwanda walionekana kucheza soka la kiwango cha juu pia katika michuano hiyo, hivyo kwa Stars hakuna kitu kipya cha kujivunia katika michuano hiyo, japo tuliweza kuiondoa timu ya Uganda katika robo fainali.

  Thiery Nkurunziza

Mwamuzi huyu raia wa Burundi alifuta dhana ya timu mwenyeji kupendelewa katika michuano hiyo ili itwae ubingwa, aliweza kuchezesha vyema na kuzifanyia maamuzi faulo zote ambazo zilikuwa zikistahili. Stars ilifungwa kwa sababu zao wenyewe na si za waamuzi. Kenya ilicheza vizuri sana katika mchezo huo, Francis Kahata, Anthony Akumu, Mieso, na nahodha Allan Wanga walionekana kuiunganisha timu yao vizuri, wakifanya mashambulizi ya kushtukiza, Wakenya walikuwa bora katika kumiliki mpira jambo ambalo hata Stars walilionesha ila wapo wachezaji wakakosa kujiamini na kujikuta wakipoteza mipira mara kwa mara.

   SAFU YA MASHAMBULIZI....

Kwa nafasi ambayo ilipotezwa na Mbwana Samatta katika dakika za mwisho wa mchezo, Stars ilishafikia mwisho kimbinu uwanjani, Stars ilipata nafasi moja katika kipindi cha kwanza lakini ikapotezwa, wakati kipa wa Kenya, Duncan Ochieng alipopangua vibaya mpira wa kona uliopigwa na Mrisho Ngassa ambao Samatta alichelewa kuuwahi. Zaidi ya hapo, walinzi, David Owino, Atudo, Edwin Lavista, na James Situma walioneka kucheza kwa umakini mkubwa ' mtu na mtu' na washam,buliaji, Samatta, ambaye alichezewa faulo nyingi katika mchezo huo, Tomas Ulimwengu na Ngassa kushindwa kuwapita.

Nachoweza kuseman ni kwamba, Stars inatakiwa kuongeza ubunifu katika namna ya kuwachezesha washambuliaji wetu, ni nafasi gani Samatta anakuwa bora zaidi na anajenga hali ya kujiamini? Bila shaka, huyu tunatakiwa kumtumia kama mshambuliaji wetu namba moja, kwa hivi sasa katika klabu yake ya TP Mazembe ameweza kupata nafasi katika safu ya mashambulizi, huku nahodha wao Tressor Mputu akirudishwa katika nafasi ya kiungo- mshambuliaji, kwa sasa Samatta anatakiwa kupangwa katika eneo hili la kati. Mabao matano katika michezo 19 ya fifa aliyoiwakilisha Stars ni dalili kuwa Stars haitengenezi nafasi za kutosha za kufunga. Akiwa amefunga mabao 15 katika michezo ya klabu Afrika akiwa na TP, bila shaka ni mfungaji hatari.

      SAFI SANA SAFU YA ULINZI
Ndiyo, Stars imetolewa huku ikiruhusu mabao matatu katika michezo miwili ya mwisho. Lakini ukuta ambao ulikuwa chini ya Ivo,  Michael Pius, Erasto Nyoni, SAid Mourad na nahodha Kelvin Yondan ulionesha ukamavu wa hali ya juu, hata pale timu ilipokuwa katika presha ya kushambuliwa. Ilikuwa si rahisi kuifunga Stars ukiwa ndani ya eneo la mita 18, kwa kuwa walinzi hawa walikuwa wakicheza ' soka la ulinzi', walikuwa bora katika kusoma mbinu za Kenya, na japo walionekana kusumbuliwa wakati fulani mchezo wao ulikuwa ni wa utulivu sana. Hawakuwa na msaada sana katika mashambulizi ila walikuwa bora katika ulinzi, bao la Kenya lilikuja baada ya kipa kutema kiki ya mbali na mfungaji kuukimbilia mpira na kufunga. Ni somo kwa safu yetu ya masham,bulizi nayo kuwa na tabia ya kufuatilia mipira hadi mwisho,

      HII STARS HAIKUWA YA ' WAZEE' NI YA VIJANA

Kuna kundi la wapenzi wa soka walikuwa wakisema kuwa Tanzania Bara ilitakiwa kupeleka timu ya vijana kama ilivyo kwa mataifa mengine. Bahati mbaya maneno haya yanatoka kwa watu ambao wanatambua soka la Tanzania lilivyo. Tabia ya kuishi kwa mazoea na kuchoka kitu cha zamani mara kipya kinapotokeza, hipo kila mahali ila kwa kusema kuwa tulitakiwa kupeleka timu yenye damu changa ni sawa na kusema hata sisi wenyewe nje ya wachezaji na benchi la ufundi pia tuna matatizo. Timu ya taifa ni mkusanyiko wa wachezaji bora katika nchi hasa wakati husika.

Wachezaji kama Haroun Chanongo, Ramadhani Singano, Elius Maguli, Himid Mao, Pius, Mourad, Juma Luizio, Joseph Kimwaga, Ngassa, Samatta, Tom, Domayo, Dilunga, Salum Abubakary,  je tunapaswa kusema ni ' wakongwe'?. Athuman Idd, Nyoni, Yondan, Ivo, Kiemba, hawa ndiyo angalu tunaweza kusema ni wachezaji waliopevuka kiumri, ila kama viwango vyao ni bora wanastahili kuendelea kuwepo kikosini, ni kama kwa Maico wa Brazil hivi sasa amemrudisha katika benchi, Dan Alves katika timu ya Taifa.

Wachezaji vijana wanatakiwa kujengewa msingi wao katika timu za taifa za vijana ni huko ndiko walikopitia kina Tom, na Samatta. Ila, wapo vijana ambao wanaweza kuruka bila kuchezea timu za taifa za vijana na kutinga timu ya wakubwa na kuwa wachezaji muhimu, Domayo ni jibu sahihi.

 HII ' SUB' YA  KIM, MH!

Kocha wa Stars, Kim Poulsen aliamua kuwatoa kwa mpigo viungo, Dilunga na Kiemba na kuwaingiza uwanjani, Chuji na Farid Mussa. Kuwatoa viungo hao ilikuwa ni sahihi kwa kuwa timu ilikuwa ikikosa kasi wakati ambao tulikuwa tukihitaji. Mussa aliishia kucheza kwa kiwango cha chini kabisa, huku akionekana kushindwa kumili mpira walau kwa sekunde moja tu. Alikuwa akipoteza mipira hovyo na akakosa kujiamini. Ilikuwa ni mabadiliko mabaya kufanywa na Kim, na yaliizamisha zaidi timu yake. Chuji alitakiwa kuanza kutokana na ' u-sharp' wake, pasi zake za kuhamisha uwanja, pumzi, uzoefu na kiwango alichokionesha katika mchezo wa robo fainali.


Aliionesha kuiinua timu mara baada ya kuingia, lakini ' patna wake wa mabadiliko' , Mussa akawa anaishusha chini. Miezi, nane kabla ya kuanza kwa kampeni fupi za kufuzu AFCON 2015, Ni wakati sahihi wa kumuondoa KIM, au kuwalinda wachezaji wetu wasipoteze viwango vyao. Kiuchezaji timu inacheza vizuri, ila kimbinu, bado Stars ipo chini, nini kazi ya Slivester Marsh? Ilikuwa akaingia, Mussa badala ya Singano au Chanongo?