Search This Blog

Saturday, February 18, 2012

ZLATAN IBRAHIMOVIC: VAN PERSIE ONDOKA ARSENAL

Robin Van Persie ameambiwa na Zlatan Ibrahimovic aondoke Arsenal kama anataka kushinda vikombe.

Nahodha wa gunners alishindwa kuisadia timu yake juzi Jumatano wakatika Gunners walipopewa kipigo cha 4-0 na AC Milan na kuweka matumaini finyu ya kuendelea na hatua ya mbele katika champions league.

Akiongea na The Sun Zlatan alisema: “Inapofikia kipindi hujashinda kombe lolote kwa miaka mingi watu wanaelewa unapoondoka kama Cesc Fabregas. Soka ni kila kitu kuhusu kushinda. Kama usiposhinda inabidi uondoke. Simjui kiundani Robinlakini nakumbuka jinsi alivyokuwa na kipaji kikubwa tangu akiwa Uholanzi – na sasa amekamilika.
“Sijui nini anafikiria kuhusu hatma yake kisoka lakini ningekuwa mimi ningejua cha kufanya tayari. Nimeshahama sana katika maisha yangu ya soka – nachukulia suala kama changamoto ya kufanya vizuri kwangu. Na nimeshashinda makombe 8 katika miak 8 na klabu tofauti katika nchi mbalimbali.
“Lakini kama utakaa sehemu moja katika maisha yako yote ni rahisi kucheza soka, unajihisi kama upo nyumbani na katika zone ambayo unakuwa comfortable kucheza soka., lakini ikiwa unahama katika sehemu tofauti inakuwa ni tofauti ni kama mtihani. Ikiwa utafanikiwa hapo ndipo unapokuwa bingwa wa kweli na hapo ndipo utakapopata heshima.”

SIMBA NAO WATOKA SARE NA KIYOVU KIGALI RWANDA

Wawakilishi wa Tanzania Bara katika kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) Simba SC imetoa sare ya goli 1-1 na Kiyovu ya Rwanda mchezo uliochezwa nchini Rwanda.

Simba walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa kiungo Mwinyi Kazimoto katika dakika ya 42 ya mchezo, na kupelekea Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli hilo moja.

Wakati mashabiki wa Kiyovu wakiwa wameshakubali matokeo ya kufungwa goli moja bila, na kuanza kutokomea uwanja katika dakika ya 90 walisazisha goli hilo na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Simba na Kiyovu watarejeana tena baada ya wiki mbili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na matokeo hayo ya leo yanawapa hauweni Simba katika mchezo wa marudiano kwani watahitaji sare ya bila kufungana.

YANGA YATOKA SARE NA ZAMALEK TAIFA - AMRI ZAKI AINYIMA USHINDI
Klabu ya Dar Young African leo imeshindwa kuifunga Zamalek ya Misri kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa wa Afrika baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja.
Katika mchezo huo ambao Yanga waliutawala kwa kiasi kikubwa huku Zamalek wakicheza kwa kijihami na kufanya mashambulizi ya kushtukiza, wanajangwani itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kupoteza nafasi nyingi za magoli ya wazi.
Yanga ndio walikuwa wa kwanza kuzitingisha nyavu za Zamalek kwa goli lilofungwa na Hamis Kiiza katika kipindi cha kwanza kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Wigan Athletic Amri Zaki aliyeingia akitokea benchi kuisawazishia Zamalek.
Kwa matokeo hayo ni dhahiri Yanga wamejiweka katika wakati mgumu atika mchezo wa marudiano dhidi ya Waarabu hao utakaopigwa wiki 2 zijazo katika venue ambayo bado haijawekwa wazi. 

Thursday, February 16, 2012

ERASTO NYONI: AZAM FC WAMEBADILISHA MAISHA YANGU


Mchezaji star wa club ya soka ya AZAM FC beki Erasto Nyoni,  amekiri kwamba club ya Azam imechangia kuyabadilisha maisha yake katika kipindi chote cha miaka minne toka ajiunge nayo.
Erasto mwenye umri wa miaka 29 akiwa ni baba wa mtoto mmoja, tayari mpaka sasa ametumia zaidi ya milioni 15 kwenye ujenzi wa nyumba yake Tabata hapahapa 88.4 Dar es salaam, nyumba ambayo ni matunda ya mshahara na posho za Azam na pia anatembea amekaa ndani ya Carina ya milioni 7 aiyoinunua mwaka jana.
Japo alifanya kazi za muda mfupi na club tofauti zisizo pungua tatu, Hicho ndicho kikubwa alichovuna Erasto nyoni toka amekuja Dar kwa mara ya kwanza mwaka 2001 akitokea 89.8 Singida ambapo alikua kumsalimia kaka yake, lakini baadae akaanza kucheza soka kwenye uwanja wa sifa Mtoni kwa Aziz Ally.
Baadae alipata kazi aliyoifanya kwa mwaka mmoja, kazi ya ujenzi huko Tabata kwenye kampuni moja iliyokua inamlipa elfu 90 kwa mwezi, pembeni na kazini kulikua na uwanja wa mpira wa Segerea Rangers kwa hiyo akawa akimaliza kazi saa kumi alafu akawa anaingia uwanjani kupiga mazoezi.
Wakati huo kulikua na timu ya ligi daraja la nne ya Segerea Rangers kocha alikua Sebastian Mkoma ambae yuko TFF kwa sasa ambae ndio alihusika kumtoa na kumtafutia nafasi katika klabu mbalimbali za soka ikiwemo ya AFC na nyingine ya Burundi ambapo alipokua huko ndio alipigiwa simu na kujiunga na Azam miaka minne iliyopita.

CHRISTIAN ERIKSEN NILICHAGUA KUJIUNGA NA AJAX NA KUKATAA OFA ZA TIMU ZA ENGLAND.In action: EriksenBig challenge ahead: Eriksen in training

Unapokuwa na miaka 20 matumaini mazuri uanyoweza kuwa nayo hasa unapokuwa mwanasoka na kuweza kuiangamiza  timu aina ya Manchester United, inasaidia katika kuwa na uzoefu zaidi katika maisha yako ya kucheza kandanda.

Kwa bahati nzuri kiungo mshambuliaji wa Ajax Christian anayo nafasi hiyo leo hii katika mechi ya Europa league dhidi ya mabingwa wa Uingereza Manchester United.
Eriksen pia leo hii atapata uzoefu japo kidogo kuhusu soka la kiingereza.

Anakumbuka: “Nilienda Chelsea mara 2 nilipokuwa na miaka 14 na 15. Nilikuwa nacheza katika klabu ya Odense kipindi hicho na tulienda Chlesea kufanya majaribio tukacheza mechi moja dhidi ya Milwall na West Ham za watoto.

“Nilishangazwa na aina ya mchezo waliokuwa wanacheza. Nilijua aina ya mchezo wa kiingereza kwamba ni tough, wenye kutumia nguvu kwa kiasi kikubwa. Ni mchezo tofauti sana na Denmark. Wanacheza kwa nguvu sana na kufanya tackles za hatari lakini nashukuru mungu sikuumia mpaka niliporudi Denmark.”

Eriksen alifanya vizuri kiasi cha kumvutia Jose Mourinho lakini kinda hilo liliamua England hapakuwa mahali sahihi hivyo akaamua kujiunga na academy ya Ajax.
Kinda ambalo liliitwa katika timu ya taifa ya DENMARK iliyoshiriki World Cup 2010 na ndio alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote katika mashindano hayo.

Uwezo wa kutisha aliounyesha dhidi ya England mwaka mmoja uliopita uliwafanya maskauti wa vilabu vya premier league kuuanza kumtafuta, huku Manchester United na Liverpool wakiungana na Chelsea, AC Milan na Bayern Munich wakimgombea kinda hili kidanish.

“Siku zote nimekuwa nikiamini mahala pazuri kwa kuanzia career yangu ni Holland, especially kwa sababu na upinzani ninaokutana nao na soka linalochezwa huku, anasema Eriksen ambaye ni mwembamba kiasi kwamba ni vigumu kuamini kama ni mwanasoka.

“Ajax wana utamaduni mzuri wa soka zuri na wanacheza mfumo wa 4-3-3,  ambao unanifaa sana mie. Pia wanatumia pesa nyingi katika kutafuta na kukuza vipaji vya wanasoka wachanga ambao hukuzwa hadi kuwa kiwango kizuri.

“Timu kubwa nchini England wana ulazima wa kucheza Champions league kila mwaka hivyo hawawezi kumnunua mcheza mwenye miaka 17 na kumuweka katika kikosi cha kwanza moja kwa moja. Wanawanunua wachezaji wanaoweza kuwatumia sasa. Unaweza ukakosa kucheza mpaka unatakpokuwa na miaka 21. Hivyo kwanini uende kule?”

AFC NAYO YASHUKA DARAJA

Timu ya AFC ya Arusha imeshindwa kutokea kwenye mechi ya Kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya 94 KJ iliyokuwa ichezwe jana (Februari 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Kwa mujibu wa Kanuni ya 21 ya FDL timu yoyote inayoshindwa kufika kituoni na kusababisha mchezo husika kutochezwa itashushwa daraja hadi Ligi ya Taifa na matokeo ya michezo yake yote itafutwa ili kutoa uwiano sahihi kwa timu zilizobaki kwenye mashindano. Si Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), msimamizi wa ligi hiyo Kituo cha Pwani wala Kamishna wa mechi hiyo Ramadhan Mahano waliokuwa na taarifa yoyote ya mapema juu ya AFC kushindwa kufika kituoni. AFC ambayo mbali ya kushushwa daraja inatakiwa kulipa faini ya sh. milioni moja kabla ya kucheza Ligi ya Taifa msimu ujao. Sh. 500,000 kati ya hizo zitakwenda kwa timu ya 94 KJ iliyoingia gharama za kujiandaa kwa mechi hiyo ambapo wapinzani wao hawakufika uwanjani.  Kundi C la ligi hiyo sasa linabakiwa na timu nne baada ya Manyoni FC ya Singida nayo kushuka daraja kwa kushindwa kucheza mechi yake dhidi ya Polisi Tabora iliyokuwa ifanyike Februari 12 mwaka huu Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.  Timu zilizobaki katika kundi hilo ambalo baada ya mbili kujitoa hakuna itakayoshuka daraja ni 94 KJ ya Dar es Salaam, Polisi Tabora, Polisi Morogoro na Rhino FC ya Tabora.

POULSEN ATAJA 23 KUIVAA MSUMBIJI


Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Jan Poulsen leo (Februari 16 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambalo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Afrika Kusini. Kabla ya kuivaa Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi itakayochezwa Februari 29 mwaka huu, kikosi hicho kinatarajia kucheza mechi ya kirafiki Februari 23 mwaka huu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) itakayofanyika kwenye uwanja huo huo. Wachezaji wapya walioitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi hicho kitakachoingia kambini Februari 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni viungo Jonas Gerald (Simba) na Salum Abubakar (Azam). Kikosi kamili kinaundwa na makipa Shabani Kado (Yanga), Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Juma Jabu (Simba), Stephen Mwasika (Yanga) na Kelvin Yondani (Simba). Viungo ni Jonas Gerard (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe (Simba), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Abdi Kassim (Azam). Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), John Bocco (Azam), Nizar Khalfan (Philadelphia Union, Marekani), Mrisho Ngasa (Azam), Ally Badru Ally (Canal Suez, Misri), Uhuru Selemani (Simba) na Nsa Job (Villa Squad).

CHEMSHA BONGO! GUESS WHO ?

ARSENAL YACHEZEA KICHAPO CHA 4:0 MBELE YA MILAN.

Matumaini ya Arsenal kuvuka salama robo fainali za klabu bingwa Ulaya ni kitumbua kilichotiwa mchanga, baada ya Jumatano jioni kunyoroshwa magoli 4-0 na AC Milan ya Italia katika mechi ya mkondo wa kwanza, ikiwa ni kati ya timu 16 zilizosalia katika mashindano hayo.
The Gunners hawakuwa na lao tangu Kevin-Prince Boateng alipoiwezesha Milan kupata bao la kuongoza.
Mchezaji wa zamani wa Manchester City, Robinho, aliongezea bao la pili kwa kichwa, na kuongezea na la tatu, kuihakikishia timu yake ilikuwa na uhakika wa kupata ushindi.
Zlatan Ibrahimovic alikamilisha kibarua kwa kuandikisha bao la nne la penalti, na wakati huohuo akiandikisha historia kwa upande wa Arsenal, ikiwa ndio matokeo mabovu zaidi ya Arsenal kufungwa kwa mabao mengi kiasi hicho katika pambano la Ulaya.
Miaka minne iliyopita, Arsenal ilikuwa ni timu ya kwanza ya Uingereza kufanikiwa kuishinda AC Milan ikiwa nyumbani, katika uwanja wa San Siro, wakati ilipopata ushindi wa magoli 2-0 katika mechi ya mkondo wa pili, na kuiondoa timu hiyo kutoka vilabu 16 vilivyokuwa vimesalia katika mashindano hayo ya klabu bingwa.
Arsenal ya wakati huo ilikuwa tofauti kabisa na timu iliyoshiriki katika mchezo wa Jumatano jioni.
Mwaka 2008 Arsenal ilikuwa na uhodari mkuwa wa ulinzi, na ilicheza kwa ustadi na ikawa ni burudani kwa mashabiki wengi, kinyume na Arsenal ilivyopambana katika mechi hiyo ya San Siro.
Mshambulizi Robin van Persie amekuwa ni nyota msimu huu, lakini katika uwanja wa San Siro, inaelekea alikuwa zaidi ni abiria, na mkwaju wake uliokuwa na matumaini katika kipindi cha pili ukizuiwa na Christian Abbiati, na hata nguvu mpya za Thierry Henry alipoingia uwanjani baadaye hazikubadilisha lolote.
Bila shaka akiwa katika ndege kuelekea New York, Henry atawaza ni kwa nini aliamua kuichezea tena Arsenal.
Meneja wa Arsenal alikuwa na matumaini kwamba Henry angelibadilisha mambo alipoingia katika kipindi cha pili, lakini hata kabla ya kuupata mpira, Milan tayari walikuwa wameandikisha bao la tatu.
Wenger atawaza pia juu ya umuhimu wa kufuzu kushirikishwa katika mechi za klabu bingwa, halafu kupigwa mabao mengi kiasi hicho.

JAMANI NINI KIMEMSIBU HUYU NDUGU YETU ?

TUNAHITAJI VIJANA KUENDELEZA SOKA LETU

Na Simon Chimbo
Hapo zamani vijana walichukuliwa na jamii kanakwamba hawajui kitu na
tena ni 'wahuni' hivyo hawawezi kuongoza. Lakini hebu twende katika
siasa kidogo, ni nani hazijui changamoto kutoka kwa wabunge vijana
Pale mjengoni kwa Makinda? watu kama akina Kabwe, Mnyika, Kafulila na
wengine vijana wengi wamekua mstari wa mbele kutetea na kuleta
changamoto katika suala zima la siasa, hebu tuachane na huko na turudi
katika soka letu la bongo.
Hatuwezi kufikia mafanikio ya Zambia 'mabingwa wa AFCON 2012' kama
hatutofanya mabadiliko ya kusudi katika uongozi wa mpira wa miguu
'soka'. Sijasema wazee hawawezi kuongoza na kufikia mafanikio, La
hasha! Lakini twende mbele turudi nyuma, ni lazima uwe na malengo
(objectives) katika kutimiza azma fulani. Waswahili wanasema katikati
ya ukweli, uongo  hujitenga, hivi ni nani anaamini au kayaona malengo
(objectives) ya TFF na maendeleo ya soka letu? Jibu mnalo.
Mwaka 2006 wakati mbrazili Marcio Maximo akitua nchini alisema maneno
yafuatayo, NANUKUU,"while we're refining stars, we should progress
youth soccer." mwisho wa kunukuu, Maximo alieleza kua ili kujenga
ubora wa stars ni lazima tuendeleze soka ya vijana, nani alimsikia?
Jibu unalo.
Katika kumbi mbali mbali za kuoneshea mpira, nilikua nikisikia
'wabongo' wengi wakisema "dah, natamani Zambia ingekua Stars"..."hivi
Tanzania tuna matatizo gani?" n.k n.k n.k Mie naongeza yangu, "hivi
Zambia waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini?" Bila program
endelevu hatuwezi fikia malengo, AFCON, world cup vyote tutaendelea
kuwasifia wenzetu akina Ghana na Zambia. Wakati umefika kwa vijana
kushika hatamu za uongozi ili kuleta changaoto kama zile za pale
mjengoni kwa Makinda, tunawahitaji akina Kabwe katika soka ili nasi
siku moja  tuwe kama Zambia na Ghana.. Vijana mnaweza jitokezeni.

MZEE YUSUF AKARIBISHW​A VALENTINE'​S DINNER NA KUTUNIKIWA ZAWADI NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE

Angalia Video ya Mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, alivyokaribishwa rasmi valentines dinner, nyumbani kwa Missy Temeke, akishirikiana na Sophia Mmombasa, Salama Salma Jay Jay, Auntie Waheeda Margaret Gathesha, na Baadhi ya mabanati wa Wasington DC na kutunukiwa zawadi mbali mbali na wakaazi wa MD kwa hisani kubwa ya kutumbuiza siku ya Jumamosi ya Feb 5, 2012 ndani ya Washington DC Nchini Marekani. Daima tutamkumbuka Mzee Yusuf Al-batwa!! http://swahilivilla.blogspot.com/

NDONGA

Bondia Fabiani Gaudence (kushoto) akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na iddi Pialali  wakati wa mashindano ya kuchagua mabondia watakaowakirisha taifa katika mashindano ya Kimataifa yanayotaraji kufanyika hivi karibuni  Gaudence alishinda kwa point.(Picha na

MESSI AVUNJA REKODI YA MABAO KATIKA HATUA YA MTOANO YA CHAMPIONS LEAGUETHE TOP FIVE SCORERS IN THE CHAMPIONS LEAGUE KNOCKOUT STAGES

PLAYERCLUBPERIOD GOALS
Lionel Messi Barcelona   2005-19
RaulReal Madrid/Schalke1995-18 
Andriy ShevchenkoD. Kiev/AC Milan/Chelsea1994-18
Filippo InzaghiJuventus/AC Milan1997-16 
Wayne RooneyManchester United2004-14 
Hii ni listi ya wachezaji waliofunga mabo mengi katika hatua ya mtoano katika historia ya Uefa Champions League.

ZAMBIA WAENDELEA KUVUNJA REKODI - WAPANDA KWA NAFASI 28 KATIKA RANKING ZA FIFA HUKU IVORY COAST WAKISHIKA USUKANI AFRICA.Zambia wameweka rekodi nyingine siku chache baada ya kunyakua ubingwa wa kwanza wa wa AFCON,  baada ya kuvuka nafasi 28 katika rankings za FIFA ikiwa ni mara yao ya kwanza kuingia hata katika top 50 ndani ya kipindi cha miaka 11.

The Copper  Bullets waliruka mpaka nafasi ya 43, nafasi yao ya juu zaidi tangu February 2001, baada ya kuwafunga Ivory Coast kwa mikwaju ya penati mjini Libreville.
Pamoja na kupoteza nafasi ya kuchukua ubingwa, Ivory Coast wamepanda kwa nafasi 3 mpaka ya 15 na ikiwa ndio timu iliyoshika nafasi ya juu zaidi barani Afrika. Tembo hao wa Afrika hawakuruhusu nyavu zao kuguswa katika dakika za kawaida katika mashindano yaliyoisha jumamosi.

Mali, ambao walishika nafasi ya tatu, walisogea mbele kwa nafasi 25 na wakashika nafasi ya 44.

Mataifa mengine kama wenyeji Equatorial Guinea timu ambayo iliundwa na wachezaji wengi wanaocheza ligi za madaraja ya chini nchini Spain waliruka kutoka nafasi ya 151 mpaka ya 110 baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali.

FIFA RANKINGS: TOP 10

1 Spain    
2 Germany    
3 Netherlands    
4 Uruguay    
5 England    
6 Portugal    
7 Brazil    
8 Italy    
9 Croatia    
10 Denmark

Wakati huo huo Spain waliendelea kuongoza kwa kuwa nafasi ya kwanza, wakifuatiwa na Ujerumani waliowashusha Uholanzi walioshika nafasi ya 3, Uruguay wameshika nafasi ya 4 wakifuatia na England waliofunga dimba la top 5.

ARSENAL WAMUAGA VIBAYA THIERRY HENRY - WAPIGWA 4-0 NA AC MILAN


HENRY AKISIKITIKA BAADA YA MCHEZO KUISHA.

Siku ya mwisho wa Thierry Henry akiwa amevaa jezi za Arsenal imekuwa mbaya zaidi kuliko ambavyo aliweza kudhani.

Gunners wamechezea kichapo cha goli 4-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya champions league.

WAUAJI WA GUNNERS HAO.Magoli ya AC Milan yalifungwa na Kevin Prince Boeten, Robinho na Ibrahimovich aliyepiga msumari wa mwisho katika jeneza la washika bunduki wa London.

IBRAHIMOVICH AKISHANGILIA GOLI LAKE DHIDI  YA ARSENAL.Mechi hii ndio ya mwisho kwa Thierry Henruy akiwa amemaliza mkataba wake wa kutumikia klabu yake hiyo kwa mkopo wa miezi 2 na sasa anarudi kuichezea klabu yake ya New York Red Bull

UNADHANI FERGUSON ALIKUWA ANAMWAMBIA NINI VAN DER SAR HAPA?

"Edwin fanya urudi bwana, Scholes karudi njoo na wewe umpe dogo De Gea uzoefu." - Fergie akiongea na Van Der Sar wakati wa mazoezi ya United mjini Amsterdam.

Wednesday, February 15, 2012

VIINGILI VYA MCHEZO WA YANGA NA ZAMALEK VYATAJWA!

 Mwakilishi wa kampuni ya Prime Time Promotions, Balozi Kindamba akionyesha mashine maalum ya kukagua tiketi zitakazotumika.


   

VVIINGILIO VYA MCHEZO WA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA KATI YA YANGA NA ZAMALEK YA MISRI VIMETAJWA.

 VIP A= 50,000
VIP B= 30,000
VIP C= 15,000
VITI VYA RANGI YA CHUNGWA (ORANGE) = 10,000
VITI VYA RANGI YA BLUE = 7,000
VITI VYA RANGI YA KIJANI (GREEN) = 3,000

VITUO VYA TICKETS

-OIL COM UBUNGO
- OIL COM TABATA
-OIL COM MBAGALA ZAKHEM
- SHULE YA SEKONDARI BENJAMINI MKAPA
- STEERS MJINI
- TANDIKA MWEMBE YANGA
- BIG BON KARIAKOO
- OIL COM VETA
- UWANJA WA UHURU
- GAPCO BANANA UKONGA

KUONDOKA KWA CAPELLO KUTAWAFAIDISHA WAINGEREZA?


Ni zaidi ya miaka ishirini sasa, Waingereza wamekua na kiu ya kufanya
vizuri katika michuano ya kimataifa. Pamoja na kufanya vizuri sana
katika ngazi ya vilabu lakini hali ni tofauti kabisa kwa upande wa
timu ya taifa.

 Tangu kuisha kwa zama za akina Paul Gascoigne 'GAZZA'
mwanzoni mwa miaka ya tisini, pamoja na kuwa na wachezaji wazuri kama
Michael Owen, Steven Gerrald, Frank Lampard na sasa Wayne Rooney bado
waingereza hawajaweza kata kiu yao.

Baada ya kushindwa kufuzu  kucheza fainali za Euro 2008 chini ya Steve
McClaren, Waingereza waliamua kumpa mkataba 'mnono' muitaliano FABIO
CAPELLO, huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika
michuano ya kombe la dunia 2010 pale bondeni kwa mzee Madiba, mambo
yalienda mrama kabisa na simanzi ilitanda zaidi pale ambapo watani wao
wa jadi Ujerumani wakiwazamisha kwa jumla ya goli 4-1 na kuwatoa
mashindanoni, kwa upande wangu sikuwa na budi kusema kuwa Fabio Capello
alichangia kwa kiasi kikubwa kutofanya vizuri pale kwa Jacob Zuma.

Aina ya mpira aliokua anafundisha 'slow but sure' ilikua ni ngumu kwa
Gerald na Lampard 'wazee wa counter attack' huku timu ikiwa haina mtu
kama Pirlo au Seeldorf, pia Capello alishindwa kuwaamini 'young stars'
kama Joe Hart, badala yake akimtumia Robert Green 'pazia' eti azuie
mashuti ya London Donovan na Clint Dempsey, huku akimuacha Scott
Parker eti hana uwezo, mmh...! haingii akilini. Shaun wright Phillips
kwa Walcott? jibu mnalo.

Kuelekea Euro(2012) mwaka huu, kujiuzuru kwake nakuchukulia kama ni
kuogopa lawama na aibu kwani sidhani kama Capello angekata kiu ya
Waingereza zaidi ya kurudia machungu yaliyotokea  pale kwa mzee
Madiba. 

Skendo ya John Terry na kauli za Capello zilikua ni 'excuses'
kwa kitakachotokea Euro kama angekua 'incharge'. Kwa mtazamo wangu
Waingereza hawana cha kupoteza baada ya kuondokewa na Fabio Capello,
kwani hakupata funzo 'lesson' kutoka kwa Joachim Loew ambae aliwaamini
'madogo' akina Mesut, Muller, Khedira n.k huku Capello akimpigia simu
Rio Ferdinand  eti anamhitaji Euro mwaka huu kanakwamba hawaoni
'madogo' kama Chriss Smalling, Walker, Micah, Cahil n.k

Mwisho kabisa naweza kusema kua Waingereza wanamhitaji kocha anaeujua vizuri mpira wa kiingereza, pia mwenye uwezo mkubwa wa kuwasaikoloji wachezaji.

By Simon Chimbo

NANI NA WELBECK NUSURA WAACHWE NA NDEGE - UNITED WAKIELEKEA UHOLANZI
Nani na Welbeck wakiwa wanachoma mahindi uwanja wa Taifa.
Kituko kimetokea leo hii jijini Manchester baada ya mastaa wawili wa Manchester United Luis Nani na Danny Welbeck walishindwa kusafiri na timu yao baada ya kusahau passport zao.

Nani na Welbeck  hata hivyo walibaki uwanjani kwa msaa kadhaa kabla ya hawajafanikiwa kujiunga na wachezaji wenzao waliokuwa wakiwacheka mno.
Kikosi cha wachezaji 20 cha United kimesafiri kuelekea Holland kwa ajili ya mchezo wa Europa League dhidi ya Ajax.
De Gea na Rooney wakiwa wenzao.Hii itakuwa mechi ya kwanza ya United kucheza nje ya Champions league  tangu walipofungwa na Rotor Volgograd ya Russia katika round ya kwanza ya UEFA Cup in 1995.

Nani na Phil Jones wamerudi katika kikosi cha kwanza cha United baada ya majeruhi, wachezaji wengine waliokuwa majeruhi na walikuwepo katika msafara huo ni Tom Cleverley, Ashley Young pamoja na makinda Paul Pogba na Zeki Fryers.

TONY ADAMS AENDA NA ARSENAL MILAN KUMUAGA THIERRY HENRY AMBAYE ANACHEZA MECHI YA MWISHO AKIWA NA GUNNERS.

"Fanya urudi tena Emirates kijana, tutakumiss."Henry akiwa mazoezini kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya Milan.MESSI NA SANCHEZ WAIINGIZA MGUU MMOJA BARCA ROBO FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE

JOSE MOURINHO ATUHUMIWA NA RAISI WA PORTO KUMUHUJUMU VILLAS-BOASJose Mourinho jana usiku alituhumiwa kumchimba Andre Villas-Boas kwa kutumiana meseji na wachezaji wa Chelsea.

Makocha wote wawili walipata majina wakiwa Porto chini ya uongozi wa raisi wa klabu hiyo Jorge Nuno Pinto da Costa, ambaye amesisitiza Special One amekuwa na mawasiliano ya karibu kuhusu hali ya Chelsea na wachezaji wake wa zamani.
Maneno ya Pinto da Costa yanazidi nguvu uvumi uliozuka wiki mbili zilizopita kutoka kwa mtu wa karibu wa Jose kwamba boss huyo wa Real Madrid anajiandaa kurudi Stamford Bridge.

Da Costa alisema: “Bado sijawa disappointed na namna Villas-Boas anavyo perform @Chelsea.
“Anafanya vizuri, amefuzu katika hatua ya 16 bora wa Champions league nab ado yupo katika kugombea kila ubingwa. Atapata mafanikio na The Blues kwa sababu mkataba wake sio wa muda mfupi.

“Anapaswa kuibadilisha timu kucheza katika mfumo wake autakao, lakini hawezi kufanya hivyo wakati kuna baadhi ya wachezaji bado wanatumiana na meseji na Mourinho kuhusu hali ya klabu, na mmiliki Abramovich analifahamu hili.”

Chelsea walilipa £14million kuweza kumchukua Villas-Boas kutoka Ureno akiwa Porto last summer na Pinto da Costa anasisitiza AVB inabidi aendelee na kazi ikiwa Blues watabaki katika top 4 mwishoni mwa msimu la sivyo ataenda Inter Milan.

Lakini pia Raisi huyo wa Porto anasema hakuwa sahihi kujiunga na Chelsea.
Pia wakati akiongea na gazeti moja nchini Italia, Pinto alisema: “Kitu pekee kitakachomgharimu kazi yake ni kutokufuzu kwa Champions league msimu ujao.
“Ikiwa ataondoka Chelsea, atakuwa kocha atakayefutia pale Inter Milan. Villas Boas aliondoka kwetu kutokana na ofa nzuri waliyotoa Chelsea.

“Kikubwa zaidi, ni zile fikra shida ambazo angezipata katika kuhakikisha anapata mafanikio ya Mourinho katika Champions league in 2004.
“Aliondoka kwenda Chelsea akidhani ni amepata nafasi ya upekee, ingawa kwangu niliona ni makosa kwa kuwa niljua haukuwa muda sahihi.”

GUUS HIDDINK AZIWEKA VITANI CHELSEA NA ANZHI MAKHACHKALA
Plan ya Chelsea kumrudisha tena Guus Hiddink @Stamford Bridge inaweza ikawa imeingia mdudu baada ya matajiri wa kirusi Anzhi Makhachkala kuamua kuingia rasmi katika mbio za kuwania saini ya mdachi huyo.

Andre Villas-Boas yupo katika wakati mgumu ndani ya klabu ya Chelsea baada ya wachezaji wake kuziponda mbinu zake waziwazi katika uwanja wa mazoezi kufuatia kipigo cha 2-0 kutoka kwa Everton last weekend.

Hiddink, amekuwa ni kipenzi cha Roman Abramovich kwa siku zote, lakini mdachi huyo pamoja na Fabio Capello ni watu wanaongoza katika listi ya makocha wanaosakwa kuchukua majukumu ya benchi la ufundi la Anzhi.

Manager wa Anzhi Yuri Krasnozhan alijiuzulu wiki hii na warusi hao wanataka kocha wa hadhi ya juu kumrithi Yuri kabla ya dirisha la usajili la nchini kwao halijafungwa ijumaa wiki hii.
Hiddink aliifundisha Chelsea kwa kipindi kifupi mwaka 2009 na akamaliza na timu ikiwa top 4 huku wakishinda kombe la FA Cup.


Imefahamika kuwa sasa baada ya mfululizo wa matokeo mabovu Abramovich ameanza kukosa uvumilivu, wiki iliyopita alienda mazoezini kabla ya suluhu ya 3-3 na Man United na baadae akatumia siku 5 kati ya 6 zilizofuatia @Cobham training centre kabla hawajafungwa na Everton @Goodison Park.

Na sasa baada ya baadhi ya wachezaji kukosoa mbinu zake huku wengine wakitajwa kuwa na mawasiliano na mwalimu wao wa zamani Jose Mourinho kuhusu hali mbaya iliyopo darajani wakiwa na mchezo wa FA Cup dhidi ya Birmingham wikiendi ihayo huku wakiwa na mchezo mgumu dhidi ya Napoli.


PER MERTESACKER AONGEZA IDADI YA MAJERUHI ARSENAL - AHOFIWA KUKAA NJE HADI MSIMU UJAO.


Mlinzi wa kati wa Arsenal Per Mertesacker anahofiwa kuwa atakaa nje ya dimba mpaka mwishoni mwa msimu.
Mertesacker amerudi nyumbani kwao Ujerumani kwenda kukutana na specialist ambaye huwa anamtibia matatizo yake ya enka ambayo ilijitonesha katika mechi ya Sunderland jumamosi iliyopita.
Anasubiri  majibu scan, ambayo yanaweza yakaharibu ama kupoteza matumaini yake ya kucheza Euro 2012.
Boss wa Arsenal, Arsene Wenger alisema: “Kwa hakika zaidi mwezi huu na ujao Mertesacker hatakuwa nasi.”

Tuesday, February 14, 2012