Search This Blog

Saturday, September 7, 2013

TAIFA STARS YAPIGWA 2-0 NA GAMBIA KATIKA KUHITIMISHA KUSHINDWA KWAO KWENDA BRAZIL 2014

Timu ya taifa ya Gambia inayoshika mkiani mwa kundi la C kwenye michuano ya kugombea nafasi ya kushiriki michuano ijayo ya kombe la dunia imemaliza mbio hizo kwa ushindi wa kulinda heshima dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania kwa kushinda 2-0 katika uliomalizika hivi punde huko Gambia.
 

Kiungo Mustapha Jarjue alifunga mabao yote mawili katika mchezo huo - kila kipindi akifunga bao moja.

Jarjue aliiweka mbele Gambia kwa bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza dakika za mwisho kabla ya kuongeza la pili dakika 6 baada ya mapumziko.

Pamoja na ushindi lakini Gambia imeshindwa kuiondoa Tanzania katika nafasi ya 3 ya kundi hilo baada ya kumaliza nafasi ya nne - wakiwa na pointi sita kutoka michezo sita iliyopita ya kundi hilo.
Cote d'Ivoire wamemaliza wakiwa juu ya kudni hilo wakiongoza kwa pointi 13 huku wakielekea kwenye mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba dhidi ya Morocco.

THIAGO SILVA: NILIIKATAA BARCELONA BAADA YA KUONA WALIVYOMFANYIA ABIDAL

Mlinzi wa PSG Thiago Silva amekiri alikataa kujiunga na Barcelona wakati wa dirisha la usajili lilopita kwa sababu ya namna walivyomfanyia beki wa kushoto wa timu hiyo Eric Abidal.

Abidal aliachwa na Barca mara baada ya msimu kuisha na hivyo akaenda kujiunga na AS Monaco.
Thiago Silva akiongea na El'equippe alisema: "Kuna vitu vilitokea kwa bahati mbaya ay nzuri vikanifanya nisiendelee na mazungumzo ya kuhamia Barca. 
"Halikuwa jambo zuri kwangu na familia yangu. Ilikuwa ni ndoto yangu kuvaa jezi ya Barcelona, lakini haikuweza kutokea.
"Tangu ilipoamuliwa kwamba ningebaki PSG, nilivaa jezi yangu na nina furaha sana kuwa hapa kuisadia timu yangu. 
"Niliona namna ilivyokuwa kwenye suala la Abidal na sikupenda walichomfanyia. Hawakuwa sawa - hawakutunza na kuitimiza ahadi yao kwa Abidal ambaye ni mtu mzuri na hawakufanya lolote kumsaidia wakati alipotoka kwenye matatizo."

HIVI NDIVYO SERENGETI FIESTA 2013 ILIVYOITIKISA JIJI LA MBEYA - SOKOINE YAFURIKA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga za muziki huo,Neylee akiimba kwa hisi jukwaani huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kwa shangwe ndani ya uwanja wa Sokonine.
Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine,ndio kwanza shoo inaanza ambapo msanii aliyewahi kuiwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu.

 Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea usiku huu kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya
 Mama wa miduara ya Kibongofleva,Shilole akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
 Sehemu ya umati wa watu.
Mkali mwingine wa hip hop (bongofleva),Ney wa Mitego akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine,mjini Mbeya.
 Wakazi wa jiji la Mbeya wakitoa heshima kwa baadhi ya wasanii waliotangulia mbele za haki, kwa kuwasha tochi za simu zao usiku huu.
 Rich Mavoko na skwadi lake wakilishambulia jukwaa. 
 Shilole akiimba jukwaani.
Wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop,Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine usiku huu.
 Ni shangwe tu kwa wakazi wa jiji la Mbeya usiku huu ndani ya uwanja wa Sokoine. 
Mmoja wa sanii mahati wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akiwaimbia mashabiki wake singo yake mpya iitwayo Tupogo usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
 MKali wa kukamua mangoma kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwarusha maelfu ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wanaondelea kumiminika kwenye uwanja wa Sokoine usiku huu.
Msanii aliyewahi kulwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu,pichani akitumbuiza mbele ya mashabiki wake.
Baadhi ya watu wakifuatilia yanayojiri usiku huu kwenye tamasha la Seremgeto Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Mkali wa Mahaba,a.k.a tajiri wa Mahapa kutoka mwambao wa Pwani,Cassi Mganga akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine mkoanni Mbeya.Picha na Michuzi Media Group-Mbeya.

KIUFUNDI ZAIDI: KWANINI ROBIN VAN PERSIE HAJAPIGA HATA SHUTI MOJA GOLINI KATIKA MECHI DHIDI YA LIVERPOOL NA CHELSEA?

Robin van Persie alikuwa kwenye kiwango kizuri dhidi ya Swansea katika mchezo wa ufunguzi wa msimu. Mshambuliaji huyo wa kidachi alionekana ameuanza msimu kama alivyoumaliza uliopita akiwa kwenye fomu nzuri. Pamoja na kufunga mabao mawili katika mechi ya kwanza, van Persie ameshindwa kupiga hata shuti moja lilolenga goli katika michezo miwili iliyopita - mechi ambazo Manchester United ilifeli kufunga bao hata moja. 

Kiwango cha van Persie kwa ujumla katika mechi mbili zilizopita.
Okay! kama tulivyoona kwamba RVP hakupiga mpira wowote uliolenga goli huku wastani wake wa kupiga mipira ukipungua mpaka  33%. Dhidi ya Liverpool,mambo yakawa mabaya zaidi huku akipoteza nafasi mbili kwa kupiga mipira nje huku jaribio lake la 3 likizuiwa na walinzi wa lango la Liverpool. 
Sio tu kwamba alionekana kutokuwa mchezoni pia alikosa ideas kabisa mbele ya lango (kwa ubora wake) lakini pia mchango wake kwenye umekuwa wa chini sana. Namba ya pasi kwa mchezo imekuwa ikipungua vibaya sana tangu siku ya mchezo wa kwanza, kama ilivyo wastani wake wa usahihi wa pasi:
rvp3
Dhidi ya Liverpool huu ulikuwa ushahidi kwamba mdachi huyo alipiga pasi sahihi 13 tu sahihi ukilinganisha na pasi 27 kwa mchezo msimu uliopita.
rvp2
Katika pasi hizi zote hakukuwa hata na moja ya kupenyeza na katika katika pasi zilizofika 9 zilikuwa za kurudi nyuma katika safu ya kiungo, tofauti tulivyomzoea mdachi huyo ambaye alitengeneza nafasi 71 kwa wachezaji wenzie msimu uliopita. Mwaka huu anaonekana kushindwa kufikia aliyoyafanya msimu uliopita, akitengeneza nafasi moja tu katika mechi tatu. Hiyo nafasi moja ilikuja kwenye mchezo dhidi ya Swansea, hivyo kufanya mchango wake katika mechi mbili kuwa zero kabisa. 

Nini tatizo?
Ni sawa sasa hivi ni mapema sana kupaniki, lakini ni vizuri kugundua udhaifu. Van Persie alikaukiwa kama hivi msimu uliopita, hivyo ni suala la kuliangalia kwa umakini  kwa United. Katika kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool van Persie alikuwa mpweke sana mbele kwa mara kadhaa, akikosa huduma muhimu kama ilivyozoeleka.
Huku Wayne Rooney akiwa hachezi katika mchezo dhidi ya Liverpool Danny Welbeck alipewa jukumu la kucheza pembeni ya RVP - kumsaidia na kumpa huduma huduma muhimu mdachi huyo. . Welbeck, ni mzuri katika kumiliki mpira, lakini hana uwezo mzuri wa kuingiza mipira ndani na ilivyo kwa RVP nae alitengeneza nafasi moja tu msimu huu, katika sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea, akifeli kabisa kuiunganisha timu dhidi ya Liverpool. Rooney, ambaye alicheza kidogo katika mechi dhidi ya Swansea na dhidi ya Chelsea tayari ametengeneza nafasi 3 jambo ambalo linaonyesha tofauti anayoweza kuleta kwenye timu anapokuwa anacheza.
Dhidi ya Liverpool ingawa ilikuwa 4-4-2, huku Welbeck akicheza karibu sana na van Persie kitu ambacho kilikuwa kizuizi kucheza kwa kubadilishana, kwa kawaida Rooney huingia kati ya mistari na kuchukua mpira kutoka kwenye kiungo na baada ya hapo kumtengenezea RVP katika njia nyuma yake, au kumpenyezea mpira kwa mbele:
united 11
RVP (20) yupo karibu sana na Welbeck (19) na huku wachezaji walioanza inaonekana ni 4-4-2 zaidi. Msimu uliopita mfumo ulikuwa tofauti na huu, huku mfumo wa 4-4-2 ukiwa hatumiki saa na makocha wa kisasa. Mfumo huu unatajwa kutengeneza nafasi chache sana kwa Manchester United, ambao wametengeneza wastani wa nafasi 8 tu kwa mchezo msimu huu, ukilinganisha na namba kubwa ya msimu uliopita wastani wa 11.5 kwa mchezo. Hivyo, kesi inaweza kuwa kwamba United haina ubunifu hivi sasa. Katika michezo miwili iliyopita United ilitengeneza nafasi 7 tu  - hii ni rekodi mbovu kabisa katika historia ya hivi karibuni ya timu hiyo. 

Kukosekana kwa Rooney’ kunasababisha hili, huku mshambuliaji huyo wa England akitengeneza 12%ya jumla ya nafasi zote walizotengeneza United msimu huu, pamoja na kucheza pungufu ya dakika 150. Inawezekana ikawa jambo la busara sasa kwa Moyes kuanza kumtumia Shinji Kagawa nyuma ya RVP katika michezo ambayo Rooney hachezi. Kagawa anaweza kucheza katikati ya mistari na kuinganish timu kati safu ya kiungo na ushambuliaji kwa ubora mkubwa kuliko afanyavyo Danny Welbeck. Kagawa ingawa inaonekana kama hana nafasi kubwa sana kwa kocha mpya David Moyes.

Hitimisho
Ingawa ni mapema sana mwa msimu lakini kumekuwa na wasiwasi wa namna United wanavyokosa ubunifu katika kulishambulia lango hasa katika michezo miwili mikubwa iliyopita - ambayo tumeshuhudia mshambuliaji wao tegemeo akishindwa hata kupiga shuti moja akilenga goli. Kumuingiza Kagawa katika timu kunaweza kusaidia kutibu ugonjwa unaisumbua timu hasa katika wakati huu mtu ambaye huifanya kazi kwa ufanisi Wayne Rooney akiwa nje ya dimba. 

VIDEO: WELBECK APIGA BAO 2 - ENGLAND IKIIUA 4-0 MOLDOVA

VIDEO: UJERUMANI YAITANDIKA AUSTRIA MABAO 3-0

CRISTIANO RONALDO ALIVYOWAFUNGA MIDOMO MASHABIKI WA IRELAND YA KASKAZINI KWA HAT TRICK - URENO IKISHINDA 4-2

Friday, September 6, 2013

ABIDAL: BARCELONA HAWAKUNILIPA HATA SENTI TANO MIEZI YOTE NILIYOKUWA NAUMWA

Eric Abidal amekasirishwa na namna maisha yake ya soka ndani ya Barcelona yalivyoisha na kusema kwamba hakulipwa chochote na klabu hiyo wakati wote alipokuwa akiugua.

Beki huyo mwenye miaka 34 alifanyiwa upasuaji wa kuwekewa ini jipya mnamo mwezi April mwaka jana, kumfanya akose michuano ya Euro na kumuweka nje ya soka kwa muda wa mwaka mmoja. Airudi kuichezea Barcelona kwenye mechi kadhaa kabla ya kuondokakujiunga na Monaco.
"Tatizo lilikuwa kwamba mkataba wangu ulikuwa unaenda mwishoni. Kwa maana hiyo ilikuwa aidha niongeze au uishe. Nilijiandaa kwa vyote," Abidal alisema katika interview aliyofanya na sports daily L'Equipe ya leo Ijumaa. "Ilikuwa ni vigumu kukubali lakini siku na jinsi. Maisha yangu ndani ya Barcelona yalikuwa yamefikia mwisho, lakini nina furaha nimeanza maisha mapya na Monaco."
Lakini Abidal amesema alikerwa na kusikitishwa namna kuondoka kwake kulivyotangazwa.
"Kitu kigumu kuelewa kilikuwa walichosema Barcelona katika mkutano wangu wa mwisho wa waandishi wa habari. Kwa kusema uamuzi ule ulitokana na sababu za kiuledi zaidi, ulivifanya vilabu vingine viwe na mashaka," Abidal alisema. "Haikuwa hata suala la fedha. Na ushahidi upo wazi kwamba miezi yote niliyokuwa kitandani naumwa, klabu haikunilipa chochote. Sasa nina bahati Monaco wameniamini - Kocha na Raisi wote wana imani juu yangu."
Abidal amecheza kwa dakika 90 katika kila mchezo wa ligi na  anategemewa kuichezea Ufaransa katika mechi ya kugombea nafasi za kucheza kombe la dunia dhidi yat Georgia.

NINI MAONI YAKO JUU YA HIZI FAULO ZA DIDIER KAVUMBAGU.

GOLI LA SIKU!

STARS YAWASILI BANJUL, KUIVAA GAMBIA KESHO

Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama hapa Banjul, Gambia tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji itakayochezwa kesho (Septemba 7 mwaka huu).

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imewasili hapa jana (Septemba 5 mwaka huu) saa 11 jioni ikitokea Dakar, Senegal ambapo ilichelewa kuunganisha ndege, hivyo kuamua kutumia usafiri wa barabara kwa vile ni karibu na baadaye kupanda kivuko kuingia Banjul badala ya kulala na kuchukua ndege nyingine siku inayofuata.

Wachezaji wako katika hali nzuri na leo jioni wanatarajia kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Independence ulioko Bakau ambao utatumika kwa mechi ya kesho. Timu imefikia hoteli ya Seaview iliyoko kandokando ya Bahari ya Atlantic.

Mechi hiyo itaanza saa 10.30 jioni kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 1.30 usiku, na itachezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda Munyemana Hudu. Waamuzi wasaidizi ni Theogene Ndagijimana, Honore Simba na Issa Kagabo. Kamishna ni Andy Quamie kutoka Liberia.

Washabiki na vyombo vya habari vya hapa wanaizungumzia mechi hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kwa pande zote, huku Gambia ikiwa imeita wachezaji tisa wanaocheza barani Ulaya na Marekani. Gambia ambayo imepata uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Gambia (GFA) imepania kuhakikisha haimalizi mechi za mchujo ikiwa na pointi moja tu.

Kwa upande wa Tanzania, Kocha Kim Poulsen amesema nia ni kuona Stars yenye pointi sita inamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast ambayo tayari imechukua tiketi pekee ya kucheza raundi ya mwisho kutoka kundi hili la C.

“Mechi hii ni muhimu kwetu kwa vile tunataka matokeo mazuri ugenini. Lakini kikubwa ni kuwa matokeo mazuri si tu yatatuweka katika nafasi ya kuwa wa pili, lakini vilevile yatatusaidia kuongeza pointi kwenye viwango vya ubora vya FIFA, na kikubwa zaidi hii ni sehemu ya maandalizi ya sisi kucheza Fainali za Afrika za 2015,” amesema Kim.

Stars inatarajiwa kupangwa hivi; Juma Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
+2207362384 Banjul

SEMINA YA FURSA KWA VIJANA YAFANYIKA LEO MKOANI MBEYA

 Mdau wa Kilimo kutoka mkoani Mbeya,Bwa.Yona Daniel akizungumzia fursa zinazopatikana kwenye kilimo,ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye suala zima la kilimo. 
 Sehemu ya vijana waliojitokeza k wa wingi kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana
Muwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akizungumza mbele ya vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,iliofanyika mapema leo  kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil,TPSF.
Mmoja wa Vijana Wajasiliamali ,ambaye ana mradi mkubwa wa kuuza juisi,Gasto Sony mkazi Uyole mkoani Mbeya,akieleza zaidi kwa vijana wenzake waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo,namna ambayo ameweza kuitumia fursa alioipata na kuwa mjasiliamali wa kuuza juisi kisasa kabisa.
  Baadhi ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya  wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. 
 Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea
 Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza na wakazi wa Mbeya (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,f iliofanyika leo asubuhi kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
 Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa Mbeya,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mkoa huo namna ya kuzitumia,Semina hiyo imefanyika leo ndani ya ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopoo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza jambo na msanii wa muziki wa kizazi kipya aitway Niki wa Pili ndani ya semina ya Fursa kwa vijana.
Muwakilishi kutoka shirika la TPSF,Bwa.Louis Accaro akifunguka kuhusiana na mambo ya fursa kwa vijana na nanmna ya kuzichangamkia mara zipatikanapo.

UONGOZI WA YANGA WAWAJIBU AKINA MZEE AKILIMALI - MWALUSAKO KUENDELA KUWA KATIBU MKUU WA YANGA

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga (katikati) akiongea na waandishi wa habari , kulia ni Mohamed Bhinda (mjumbe wa kamati ya utendaji) , kushoto Baraka Kizuguto Afisa Habari


Makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Clement Sanga leo amefanya mkutano na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi juu ya habari zilizokuwa zimeenea kuhusiana na taarifa za mabadiliko ya kaimu katibu mkuu Lawrence Mwalusako kuondolewa kwenye nafasi yake na kuchukukuliwa na mtu mwingine.

Akiongea na waandishi wa habari Sanga amesema taarifa hizo hazina ukweli kwamba tayari kuna mtu anachukua nafasi ya Mwalusako, bali kilichotokea ni kutokuwepo kwa mawasiliano mazuri katika suala hilo kati ya viongozi na wazee.

Kilichopo ni kwamba uongozi wa klabu ya Young Africans upo katika mchakato wa kuhakikisha unajaza nafasi zilizopo wazi za mkurugenzi wa ufundi, mkurugenzi wa masoko, mkurugenzi wa fedha na zoezi hilo linaendeshwa na kampuni moja ambayo waliipa nafasi ya kuendesha zoezi hilo.

Zoezi likiwa ndani ya mchakato mmoja wa waombaji wa nafasi hizo Patrick Naggi aliwasili makao makuu ya klabu ya Yanga kwa lengo la kutaka kujua mazingira ya ufanyaji kazi yakoje na kufahamu baadhi ya mambo kuhusiana na klabu ndipo kulipotokea kutokuelewana na baadi ya wanachama wakiwemo wazee waliokuwepo eneo la klabu.

Kwa maana hiyo napenda kutoa taarifa kwa umma na wanachama wa Yanga kuwa uongozi bado haujatoa baraka za ajira kwa mtu yoyote katika nafasi hizo, isipokuwa ni muombaji aliwahi kufika makao makuu kabla ya mchakatao wa usahili kukamilika.

Lawrence Mwalusako anaendelea kuwa kaimu katibu mkuu wa Yanga mpaka hapo kutakapokuwa na taarifa nyingine zozote za mabadiliko kwa nafasi zote zilizopo wazi katika idara mbalimbali.
Uongozi unawaaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa soka kuwa kitu kimoja katika kuunga mkono harakati za kimaendeleo ili kuifanya timu iende katika hatua nyingine ya ushindani wa kimatifa.

HATIMAYE CEO WA MAN UNITED AKIRI KUFANYA MADUDU KWENYE USAJILI

Ryan Giggs, Group Managing Director Richard Arnold, CEO Ed Woodward and Club Secretary John Alexander honours King Bhumibol of Thailand at Siriraj HospitalHatimaye baada kusemwa sana CEO wa Manchester United Ed Woodward amekiri kwamba hajafanya kazi nzuri kwa mabingwa hao katika dirisha la usajili liloisha hivi karibuni.

David Moyes, kocha mpya wa United, alitaka kuwasajili viungo wawili na beki wa kushoto wa kusaidiana na  Patrice Evra.
Lakini usajili pekee wa maana uliofanywa Old Trafford ni wa Maroune Fellaini - aliyenunuliwa dakika ya mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa kwa ada ya uhamisho wa  £27.5million.
Na Woodward ameripotiwa kutambua kushindwa kwake kuwaleta wachezaji wa waliotakiwa na Moyes - kumemfelisha.
United walishindwa katika majaribio yao ya kuwasajili  Cesc Fabregas, ambaye alichagua kubaki Barcelona, Thiago Alcantara, aliondoka Barca kujiunga na Bayern Munich, Ander Herrera wa Athletic Bilbao na kiungo wa Roma  Daniele De Rossi.
 
Pia United walishindwa katika jaribio lao la kumsaini beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines na mkopo wa Fabio Coentrao ukashindikana. 

 


PICHA YA SIKU: TIMU YA MPIRA WA KIKAPU YA WANAWAKE, DON BOSCO LIONESS WAKIWA NA MAMA MALENGA.


TFF YAOMBWA KUWATUMIA VIBALI WANASOKA WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI.

Vijana wawili raia wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini wamesikitishwa na kitendo cha Shirikisho la soka nchini TFF kushindwa kuwatumia ITC walizoziomba takribani wiki moja sasa,
Vijana hao Mohamed Ally Ibrahim (18 )  na Robert Titus Kobelo (21 ) wanaombewa vibali na timu ya CACADU UNITED FC inachoza ligi daraja la pili ya nchini Afrika Kusini,
ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya VODACOM.
Vijana hao ni zao la JAKI ACADEMY ya Mbagala jijini Dar Es Salaam wanataka kujiunga na timu hiyo yenye maskani yake kwenye kitongoji cha Alexandria huko mjini Port Elizabeth.

Mmoja wa wakurugnzi wa timu hiyo ndugu BONGANI MASHIBO wakati Akiongea na Blog hii amesema
'' Nasikitika sana mpaka sasa hatujapata jibu toka TFF,Tangu tumewaombea vibali hawa vijana,kila tukiwasiliana nao wanasema wanatuma lakini hawatumi,kama unaweza nenda kawasisitize TFF watutumie hivyo vibali ''.

     Hawa  ndio vijana wanaomba vibali vya kucheza nchini AFRIKA KUSINI.


  Mkurugenzi wa timu ya CACADU UTD BONGANI MASHIBO.

HIKI NDO ALICHOKIANDIKA BONDIA CHAULEMBO PALASA.


KALIZA WA TRA DODOMA AFAGILIA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI


Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza katikati akiwa na promota na mdau wa masumbwi Mohamedi Bawazir kushoto Bondia Fransic Cheka na Fransic Miyeyusho wakati walipokwenda Dodoma kutembelea bunge la jamuhuri ya muhungano wa Tanzania baada ya Cheka kutwaa ubingwa wa Dunia wa WBF na kualikwa chakula cha jioni na meneja huyo mjini Dodoma  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya wadau wa masumbwi na mabondia wakigongesheana grass na Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza wakati wa kutakiana heri baada ya wadau hawo wa masumbwi kupewa heshima ya kutembelea bungeni kwa mara ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baadhi ya wadau wa masumbwi na mabondia  wakiwa katika picha ya pamoja na  Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya wadau wa masumbwi na mabondia wakigongesheana grass na Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza wakati wa kutakiana heri baada ya wadau hawo wa masumbwi kupewa heshima ya kutembelea bungeni kwa mara ya kwanza  na kuarikwa kwa chakula cha jioni na meneja huyo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya wadau wa masumbwi na mabondia wakigongesheana grass na Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza wakati wa kutakiana heri baada ya wadau hawo wa masumbwi kupewa heshima ya kutembelea bungeni kwa mara ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com