Search This Blog

Saturday, April 27, 2013

WENGER: CARRICK ANAWEZA KUCHEZA HATA BARCELONA - ANASTAHILI KUWA MCHEZAJI BORA WA ENGLAND MSIMU HUU

ARSENE WENGER amezungumza kwa mara ya kuhusu tuzo ya mchezaji bora wa England msimu huu, akiwashangaza wengi Wenger amemtaja kiungo wa Manchester United Micheal Carrick kuwa ndio mchezaji anayestahili tuzo hiyo msimu huu.

Meneja huyo wa Gunners alisema: “Mimi ningemchagua Carrick. Angeweza hata kucheza ndani ya kikosi cha Barcelonakwa sababu anafiti katika staili ya uchezaji wao. 

“Ana uono mzuri na ni mchezaji mwenye akili sana uwanjani."

Mshambuliaji Van Persie mwenye mabao 24  ya Premier League katika mechi 31 alizoanza yamechangia kwa kiasi kikubwa United kuurudisha ubingwa Old Traford - na sasa mdachi huyo anapewa nafasi kubwa ya kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa England.
Lakini Wenger anasema ni mchezaji mwenzie RVP -  Carrick, 31, ambaye anastahili kuchukua tuzo hiyo ya PFA.

Aliongeza: “Robin alikaa muda mrefu kidogo bila kufunga. Kura zilipigwa wakati ule hivyo hilo linaweza likaenda dhidi yake.
“Suarez amejiangusha mwenyewe, pia yupo Gareth Bale lakini nadhani hapewi heshima ya kutosha hapa England. 

“Muda mwingine sio lazima mfungaji bora awe anazawadiwa - kuna watu nyuma pia. Carrick anastahili. Ningemchagua Carrick kama ilivyokuwa Robin mwaka uliopita. Tuzo apewe mtu mwingine, Carrick ni mtoa pasi bora."

GEORGE BANDA: KINDA LA YANGA LINATOSHIA UWEPO WA JERRY TEGETE KIKOSI CHA KWANZA



KOCHA wa Simba, Patrick Liewig amethubutu kuwatumia vijana kwenye kikosi chake bila kujali matokeo ya timu hiyo kwenye ligi.
  
Mfaransa huyo mwenye msimamo na kazi yake alisema; "Nitawatumia wachezaji vijana kwenye kikosi changu hadi ligi itakapomalizika bila kujali matokeo ya timu.

"Ni vijana ambao wameonyesha nidhamu ya hali ya juu na moyo wa kujituma uwanjani kwa ajili ya timu yao.Binafsi ninavyojua, hakuna mchezaji anayeweza kuwa juu ya timu. Nafikiri bila nidhamu, hatuwezi kufikia kwenye malengo ambayo tumejiwekea." alisema kocha huyo.

George Banda ni mshambuliaji wa Yanga aliyepandishwa kikosi cha timu ya wakubwa pamoja na winga Rehan Kibingu. Makinda hayo yamepandishwa kutoka timu ya vijana iliyokuwa ikinolewa na beki wa kushoto wa zamani wa Yanga, Kenneth Pius Mkapa, lakini kwa sasa benchi hilo linaongozwa na kiungo Salvatory Edward 'Mtaalam'. Hiyo ni baada ya Mkapa kurudi darasani kwenda kuongeza taalum yake ya kufundisha mchezo wa soka.

Banda kwa sasa yupo nyuma ya mastraika wanne, Hamis Kiiza wa Uganda, Mrundi Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi na Jerry Tegete. Ni nani huyo Banda?

Familia ya Michezo

Banda anasema kuwa Baba yake mzazi, Joseph Banda alikuwa akicheza soka, lakini alipoumia aliamua kujikitiza kwenye biashara.

"Alikuwa akicheza soka, lakini baada ya kung'oa kucha kwenye kidole gumba cha mguu wake aliamua kuachana na soka."

Anaeleza kuwa hakubahatika kucheza na timu yoyote ya Ligi Kuu isipokuwa alikuwa akikipiga na timu mbalimbali za mtaani. Mwanzo wa soka Banda anasema aliupenda mchezo wa soka tangu akiwa mdogo na kuanza kucheza timu tofauti za mtaani.

"Mwaka 2004 nilishiriki Ligi ya TFF Ngazi ya Taifa iliyokuwa ikishirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 14."

"Nilishiriki na timu yangu ya mtaani, River Heroes ya Banana
Ukongo, jijini Dar es Salaam. Baada ya ligi hiyo kumalizika. Nilifanikiwa kuchaguliwa kwenye kikosi bora cha mashindano hayo.

"Tuliahidiwa kupelekwa Ulaya kwenda kujifunza zaidi soka. Lakini, ghafla nilienguliwa kwenye safari hiyo. Sijui hadi leo sababu za msingi ambazo zilinifanya kuondolewa kwenye msafara huo." anasema Banda.

Soka na Shule

Banda aliyecheza kwa mara ya kwanza kikosi cha Yanga dhidi ya Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Januari, mwaka huu kwa dakika 45 za kwanza ambapo Yanga ililala kwa bao 1-0.

Anaeleza kuwa elimu yake ni ya darasa la saba aliyohitimu katika shule ya msingi Karakata iliopo Kipawa jijini Dar es Salaam.

"Nimehitimu darasa la saba katika shule ya msingi Karakata, Kipawa (Dar es Salaam). Sikutaka kuendelea. Niliamua kuelekeza nguvu zangu kwenye soka. Binafsi niliamini ndiyo njia yangu sahihi kutoka kimaisha."

"Familia ilinitaka kuendelea na shule. Lakini niliwaambia niacheni kama nilivyo, nitajua mwenyewe. Mambo yalikuwa magumu. Lakini nilipata nafasi yakujiunga na timu ya Mogo FC ya Ukonga (Dar es Salaam." anaeleza kinda huyo ambaye amekiri kuwa iwapo atapata mfadhili wa kumlipia ada yupo tayari kuendelea na elimu ya sekondari.

Atua Mtibwa, aula Yanga

Kinda huyo mwenye umbo kubwa na nguvu za kusukuma na mabeki wa timu pinzani anaeleza kuwa timu ya Mtibwa ilimwona na kuvutiwa na kiwango chake.

"Baada ya kuvutiwa na kiwango changu, walinichukua kwenye timu yao ya vijana. Nilidumu nao kwa misimu miwili tu na kurejea tena kwenye timu yangu ya zamani Mogo FC. Maslahi yalikuwa madogo.

"Mwaka 2011, Mlezi wa Mogo FC Ally Ruvu aliamini kiwango changu na kunipeleka Yanga kufanya majaribio na kufaulu siku hiyo hiyo."

Anaeleza kuwa majaribio hayo alifanya na kikosi cha timu ya vijana kilichokuwa kikinolewa na kocha Kenneth Mkapa na Abubakari Salum 'Sure Boy'.

Banda anasema kocha Ernie Brandts alipomwona kwa mara ya kwanza na kikosi cha timu ya vijana katika mashindano ya Kombe la Itihad yalifanyika Mwananyamala Dar es Salaam na kumpandisha timu ya wakubwa siku hiyo hiyo.

"Kocha Brandts aliponiona kwa mara ya kwanza alikoshwa na kiwango changu na kunipandisha timu ya wakubwa pamoja na Kibingu (Rehan).

"Sikuamini ukizingatia bado umri wangu bado mdogo. Vile vile, sina uzoefu. Niliona ni kazi kubwa kwangu kupata namba mbele ya Tegete, Bahanuzi, Kiiza na Kavumbagu ambao wana uzoefu mkubwa na ligi." anaeleza yosso huyo anayevutiwa na staa wa Anzhi Makhachkala na Cameroon, Samuel Eto'o 'Fils'.

Matarajio yake

Banda anaeleza kuwa ndoto zake haziwezi kutimia bila kujituma
kwa bidii na nidhamu kwa wote.

"Naamini kuwa ili kutimiza ndoto zangu nilizojiwekea. Lazima kujituma na nidhamu kwa kila mtu. Kwanza nafikiri ni kupambana kupata namba kikosi cha kwanza cha Yanga. Pia, kucheza timu ya
Taifa Stars na kujitangaza zaidi kimataifa.

"Itakuwa njia rahisi kwangu kuonekana na kujitangaza kucheza soka la kulipwa nje ya nje kama walivyo Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu." anaeleza Banda.

Historia

Banda ni mtoto wa tatu katika familia ya Mzee Joseph Joseph Banda yenye watoto saba, watano wakiwa wakiume na wawili wa kike.
Anaeleza kuwa kaka yake wa kwanza aitwae Gabriel ndiye anayecheza soka, lakini wengine hawataki kabisa kusikia mchezo huo.


GEORGE BANDA

Kuzaliwa; Julai 19, 1993
Mahali; Ilala, Dar es Salaam
Klabu alizocheza;
River Heroes; 2002/04
Mogo FC; 2005/O7
Mtibwa Sugar; 2008/10
Yanga; 2013
Taifa; Tanzania

PICHA YA SIKU: ANGALIA WADHAMINI WA MAN CITY WALIVYOIPONGEZA MAN UNITED KWA KUBEBA UBINGWA


Friday, April 26, 2013

HATIMAYE YANGA YATAWAZWA KUWA MABINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE 2012/12

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati klabu ya YANGA leo imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania katika msimu wa 2012/13. 

Yanga imefanikiwa kutangaza ubingwa huo huku ikiwa imebakiwa na michezo na michezo miwili baada ya Azam FC ambao wanashika nafasi ya pili kutoka sare ya 1-1 na Coastal Union leo hii katika dimba la uwanja wa Mkwakwani.
  
Matokeo hayo yanamaanisha, Azam FC ambao walikuwa wakiikimbiza Yanga kwa karibu katika mbio za ubingwa, hawawezi kuzifikia pointi za Yanga yenye pointi 56, huku Azam ambao wamebakiwa na michezo miwili vilevile wakiwa na pointi 48 - hivyo hata wakishinda mechi zao zilizobakia watakuwa na pointi na poinri 54.

MSIMAMO WA LIGI ULIVYO HIVI SASA

                                    P W D L GF GA GD Pts
1 Yanga SC        24 17 5 2 44 13 31 56
2 Azam FC          24 14 5 5 42 20 22 48
3 Kagera Sugar   23 11 7 5 25 18 7 40
4 Simba SC         22 9 9 4 32 21 11 36
5 Mtibwa Sugar   24 9 9 6 27 23 4 36
6 Coastal Union   24 8 10 6 24 21 3 34
7 Ruvu Shooting  22 8 6 8 21 21 0 30
8 JKT Oljoro 24 7 7 10 22 27 -5 28
9 Prisons            24 6 8 10 14 21 -7 26
10 JKT Ruvu 24 7 5 12 20 37 -17 26
11 Mgambo JKT   23 7 4 12 16 23 -7 25
12 Toto African     25 4 10 11 22 34 -12 22
13 Polisi Moro      23 3 10 10 12 22 -10 19
14 African Lyon 24 5 4 15 16 36 -20 19
 

Thursday, April 25, 2013

AZAM KUKATA TIKETI YA KUSHIRIKI MICHUANO YA KIMATAIFA LEODHIDI YA COASTAL UNION??

AZAM FC leo (Ijumaa) inashuka kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuvaana na wenyeji wao Coastal Union katika mchezo wa ligi soka Tanzania Bara.

Wawakilishi hao pekee wa nchi katika Kombe la CAF iwapo wataibuka na ushindi kwenye mchezo huo watakuwa wamekata tiketi kwa mara nyingine kushiriki michuano hiyo mwakani.

Pia, iwapo Azam itashikwa na kulazimishwa sare ya aina yoyote na Coastal, Yanga itakuwa imetwaa rasmi ubingwa wa ligi hiyo.

Yanga ambayo inaongoza ligi na point 56 huku ikiwa na mechi mbili mkononi dhidi ya Coastal Union na Simba, inahitaji pointi moja tu kutawazwa mabingwa wapya wa ligi.

Azam ambayo inashika nafasi ya pili kwenye ligi ndiyo timu pekee ambayo inaweza kufikisha
pointi 56 iwapo itashinda mechi zake zote tatu zilizobaki dhidi ya Coastal, Oljoro JKT na Mgambo
JKT.

Kocha wa Azam, Mwingereza Stewart Hall amesema kikosi chake kitapigana hadi tone la mwisho kwavile katika soka lolote linawezekana.

"Kazi yangu ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri bila kujali matokeo ya wengine, tupo vizuri kuikabili Coastal Union na kunyakua pointi tatu,"alisema Hall.
Katika mtanange huo Hall atawakosa mabeki wake Jockins Atudo na Haji Nuhu ambao ni majeruhi ingawa nafasi ya Atudo inatarajiwa kuzibwa na beki Aggrey Morris aliyekuwa amesimamishwa kwa tuhuma za rushwa.

BENDERA: IKIWA MFUMO WA SOKA UTAENDELEA KUWA HIVI - SOKA LETU LINA SAFARI NDEFU KUENDELEA MBELE


KOCHA wa zamani wa timu ya taifa Taifa Stars ambaye aliwahi pia kuwa naibu waziri wa vijana,
Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, amesema kuwa soka la Tanzania bado linasafari ndefu kufikia mafanikio ikiwa mfumo wa uendeshaji mchezo huo hautabadilika.

Bendera ambaye mwaka 1980 aliweka rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo ya kuiwezesha Tanzania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuifunga timu ya taifa ya Zambia
(Chipolopolo) katika uwanja wa Independence mjini Lusaka, Zambia huku mechi hiyo ikishuhudiwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Dk Kenneth Kaunda, alisema nilazima Tanzania kurudi kwenye mfumo wa awali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Bendera ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Morogoro alisema kuwa katika kipindi ambacho yeye alikuwa kocha wa Taifa Stars alipata wachezaji wa timu hiyo
kwa kuzunguka mikoani wakati wa mashindano ya UMITASHUMITA, UMISETA, Taifa CUP na SHIMIWI na kuweza kukusanya wachezaji wenyevipaji na wanaojituma.

“Leo hii timu yetu ya taifa inashindwa kufanya vizuri kwa sababu ya wanaohusika kushindwa kufanya selection (uchaguzi) unaofaa kwa kuelekeza nguvu zaidi katika kuchagua wachezaji kutoka timu zinazoshiriki ligi kuu pekee,” alisema Bendera.

Pia, alisema kuwa mbali ya mfumo mbovu wa kuchagua wachezaji uliopo kwa sasa, lakini bado Tanzania inachangamoto kuwa ya kukosa viwanja vya michezo, vifaa na walimu wanaofundisha
michezo mashuleni.

Alisema kuwa hali hiyo imewafanya wachezaji wengi wanaoingia katika timu ya taifa na hata vilabu vinavyoshiriki ligi kuu kukosa vitu vitatu muhimu katika mpira ambavyo ni uzalendo, ari na nidhamu.

Kuhusu matumizia ya lugha ya kiingereza inayotumiwa na makocha wengi wa kigeni kuwafundishia wachezaji wa timu za tanzania ikiwa ni pamoja na taifa staa, kocha huyo wa zamani alisema kuwa lugha za mpira zinafanana kote duniani kufundishwa kwa kishwahili au kiingereza hakubadilishi lugha hiyo.

Kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Afrika, Tanzania imeingia katika mkumbo wa kuwatumia
makocha wa kigeni ambao hutumia lugha ya kiingeza kufundishia, lugha ambayo huzungumzwa na
wachezaji wachche wa timu ya taifa.

SIMBA YAKERWA NA MECHI KUAHIRISHWA KWA MECHI GHAFLA - YATOA TAARIFA RASMI JUU YA KUREJEA KWA HANS POPE MADARAKANI

KLABU ya Simba inapenda kutoa taarifa hizi mbili muhimu kwa umma siku ya leo.

KUAHIRISHWA KWA MECHI YA RUVU SHOOTING
UONGOZI wa Simba umekubaliana na hatua ya serikali kuzuia kuchezwa kwa mchezo uliopangwa kuchezwa leo wa Ligi Kuu ya Tanzania baina ya Wekundu wa Msimbazi na Ruvu Shooting Stars.
Hata hivyo, uongozi wa Simba haujafurahishwa na namna uzuiaji huo ulivyofanyika. Taarifa imetolewa leo kwenye siku ya mechi yenyewe wakati maandalizi yote yakiwa yamefanyika na hivyo kusababisha matatizo katika sehemu kubwa tatu.
Mosi, uongozi wa Simba umeingia gharama kubwa ya kuweka timu kambini na kujiandaa na mechi. Pili, benchi la ufundi na wachezaji walikuwa tayari wamejiandaa na mechi kimwili na kiakili na kuahirishwa huku kwa mechi kumesaidia tu kuvuruga programu. Tatu, wapenzi na washabiki wa Simba wamepata usumbufu wa kwenda uwanjani na kukuta hakuna mechi.
Uongozi wa Simba unapenda kutumia nafasi hii, katika namna ya kipekee kabisa, kuwaomba radhi wapenzi na wanachama wake ambao walifika Uwanja wa Taifa kutazama mechi ambayo haikuwapo.
Washabiki ndiyo wanaoifanya Simba na mchezo wa mpira wa miguu nchini uwe na umaarufu ulionao na bila wao ligi yetu inaweza kupoteza nguvu na ushindani ilionao.
Simba SC inapenda kuwe na utaratibu unaojulikana wa kuahirisha mechi wa walau saa 48 kabla ya siku ya mechi. Hii itasaidia pande zote zinazohusika. Kama mechi imeshindikana kwa sababu za nje ya uwezo wa kibinadamau (Force de Majeure) kama vile mafuriko, tetemeko la ardhi na vimbunga, mechi inaweza kuahirishwa ghafla lakini si kwa mechi ambayo uwepo wake ulifahamika miezi kadhaa nyuma.
Tunashauri pia kwamba siku za mechi ambapo Ligi Kuu inachezwa (match days), inatakiwa kuwa zinafahamika na isiwe kila siku mechi zinachezwa. Simba ilikuwa na mechi wikiendi iliyopita na Ruvu ilikuwa na mechi Mbeya zaidi ya wiki moja iliyopita na hivyo mechi hii ingeweza kuchezwa hata jana (Jumatano) ambayo ni siku ya kawaida kwa mechi kuchezwa badala ya leo Alhamisi.
Ni matumaini yetu kwamba kuahirishwa kwa mechi hii kutakuwa fundisho kubwa katika upangaji wa ratiba na uahirishaji wa mechi ambao una faida kwa pande zote husika.


Poppe arejea Simba
MWENYEKITI wa Simba, Mhe, Ismail Aden Rage, amemshukuru aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu, Zacharia Hans Poppe, kwa kukubali kurejea kushikilia nyadhifa zake zote.
Poppe alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake za uongozi ndani ya Simba Machi 7 mwaka huu, kutokana na hali ya migogoro iliyokuwapo wakati huo.
Hata hivyo, Rage alikataa kujiuzulu huko kwa Poppe na akasema atamshawishi abadili maamuzi kwa manufaa ya Simba.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwaarifu wana Simba popote walipo kwamba Poppe amerejea na yuko tayari kuitumikia Simba kama Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,” alisema Rage.
Kwa upande wake, Poppe alisema amerejea Simba kutokana na utulivu ulioanza kujitokeza klabuni na kwamba nia yake ni kuhakikisha klabu inafanya usajili mzuri na wa kiwango kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

ZAHA: MIE NI SHABIKI WA DAMU WA ARSENAL ILA UNITED NI KLABU KUBWA NA BORA DUNIANI SIKUWEZA KUKATAA KUJIUNGA NAYO


WILFRIED ZAHA hakuweza kukataa uhamisho wa £15million kwenda  Manchester United — japokuwa ni mshabiki wa damu wa klabu ya Arsenal.

Winga huyo ambaye anachezea Crystal Palace kwa mkopo, ni mshabiki wa tangu utotoni wa Gunners, na alikuwa na ndoto na kujiunga na Arsenal kabla ya United hawajaingia katika mbio za kumsaini.

Zaha, 20, alisajiliwa na United mwezi January kabla ya kurudishwa Palace kwa mkopo.

Winga huyo alisema: “Siku zote ilikuwa ni Arsenal, Arsenal, Arsenal, Arsenal katika kuchagua timu ambayo ningejiunga nayo.

“Siku zote nimekuwa mshabiki wa Arsenal. Sikudhani kama United watakuja kunihitaji lakini ikawa vinginevyo. Arsenal ni timu nzuri lakini United ni moja ya klabu kubwa sana duniani ilinibidi nijiunge nayo.

GARY NEVILLE AIOKOA TIMU YA MTAANI KWAO KUFILISIKA - ALIPA MISHAHARA YA WACHEZAJI

Nahodha na mchezaji wa zamani Man United  Gary Neville amesaidia kulipa mishahara ya klabu ya nyumbani kwao inayokabiliwa na ukata mkubwa.

Bury FC — ambayo imeshuka daraja hivi karibuni mpaka ligi daraja la pili — inahitaji kiasi cha £1million ili kijihakikishia uwepo wake.
Klabu hiyo itashindwa kuendelea kuwepo mpaka pale watakapopata wafadhili wa kuwasaidia.
Gary Neville ambaye kwa sasa kocha msaidizi wa England na mchambuzi wa soka wa TV, aliingia mfukoni mwake na kuamua kulipa mishara ya wachezaji wote baada ya kuombwa na klabu hiyo.


MARCO REUS APONDA MUDA WA KUTANGAZWA UHAMISHO WA GOTZE KWENDA BAYERN

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus amesema kitendo cha kutangazwa kwa dili la uhamisho wa Mario Gotze kwenda Bayern Munich kwa wakati huu ni cha kijinga mno wakati timu yake ikiwa katika kuelekea fainali ya Ligi ya mabingwa wa ulaya.

Tangazo la kuondoka kwa Gotze lilitolewa masaa 48 kabla ya mchezo wa raundi ya kwanza wa nusu fainali ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Madrdi - na maandalizi ya mchezo huo yakawa yamegubikwa na taarifa za kuondoka kwa kijana huyo wa kijerumani mwenye umri wa miaka 20.

Reus anakiri taarifa hiyo imekuja wakati m'baya sana kwa Dortmund lakini akawaomba mashabiki wakae nyuma ya Gotze nakumsapoti mpaka mwisho wa msimu.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Facebook mfupi kabla ya mechi dhidi ya Madrid Reus alisema, "Leo ndio siku ya mechi, tunaangalia mbele kukutana na Real Madrid na tunataka kufika fainali. Hakuna cha umuhimu zaidi ya hii mechi, kuliko hata kuhusu ile habari ambayo Ujerumani yote inaizungumzia.

"Mario amefanya maamuzi kwa ajili ya maisha yake. Inabidi tuheshimu kuhusu hilo. Muda wa kutangaza uamuzi huo kiukweli haukuwa mzuri - na wa kijinga. Lakini inabidi wote tuungane kwa sasa - wachezaji wenzangu na mashabiki tuwe kitu kimoja.

"Nafikiri baadhi ya maoni kuhusu Mario niliyoyasoma kwenye facebook sio mazuri, hastahili kutusiwa, ana mengi ya kuishukuru Dortmund na mashabiki lakini pia sie tunapaswa kumshukuru - tusisahau hilo.
"Tafadhali tuangalie kusherehekea usiku mkubwa soka kwa pamoja - na Mario akiwepo pia." Alimaliza Reus ambaye jana akicheza kwa pamoja na Gotze walisababisha madhara makubwa kwenye ukuta wa Real Madrid - Gotze akitoa pasi ya goli la kwanza huku Reus akisababisha penati ya goli la nne.

MJADALA: MDAU MAJALIWA ANAULIZA FIFA WALITUMIA VIGEZO GANI KUTEUA KIKOSI BORA CHA MWAKA ?

FIFA wana kipi cha kutuambia kupitia data chache kama hizi?

 1. Ligi bora-La liga

2. Mchezaji bora-La liga

3. Timu yao wachezaji wote-La liga 

4. Kocha bora-spain

UDHAIFU: La liga ina ushindani kwa timu mbili tu kwa zaidi ya miaka 10 sasa, hii imetokana na utofauti mkubwa wa mapato baina ya timu mbili kubwa na timu zingne zczo na kipato kikubwa, hata hivyo FIFA wameziba mackio na kujitoa akili kwa kuiona ndio ligi bora.

Hata chelsea waliochukua ubingwa wa UEFA japo ilikuwa kwa kubahatisha hawakutoa mchezaji yeyote kwenye kikosi cha FIFA matokeo yake mtu km Pique ambaye cjawahi kuukubali uwezo wake aliingizwa licha ya kutocheza kwa muda mrefu kutokana na kutoelewana na aliyekuwa kocha wake Pep Gudiola hivyo FIFA walimuingiza kwenye timu yao labda kwa kumtia ujauzito Shakira! Vivyo hivyo timu za La Liga hat fainali ya UEFA hazikucheza but bado zikaendelea kuhesabika bora.

MWISHO: TIMU YA FIFA imepigwa 8-1 na timu ambayo ligi yake huingiza timu 3 tu kwenye UEFA. Inasikitisha sana, maghumashi hadi kwenye fani ipendwayo na walimwengu wote!

Naitwa Majaliwa Mayala wa Buswelu Mwanza Tanzania, naishi kwa mkopo Dodoma

DORTMUND 4-1 MADRID: LEWANDOSKI AWA MCHEZAJI WA KWANZA KUIFUNGA MADRID MABAO MANNE KWENYE HISTORIA YA CHAMPIONS LEAGUE - CRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI 2 BINAFSI

Dortmund* Mshambuliaji wa Dortmund Robert Lewandowski ndio mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne dhidi ya Real Madrid katika historia ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

* Ilikuwa ni mara ya 10 kwa mchezaji mmoja kufunga mabao zaidi ya manne katika mechi moja ya Champions League. Lionel Messi pekee ndio mchezaji aliyefunga mabao manne mara mbili katika mechi 2 za ligi ya mabingwa wa ulaya.

* Huu ndio msimu wa kwanza ambapo timu zimeruhusu nyavu zao kuguswa mara 4 katika mechi za hatua ya kutoana kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya. Bayern 4-0 Barcelona, Dortmund 4-1 Real Madrid.

* Cristiano Ronaldo nae ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 3 kufunga kwenye mechi sita mfululizo za ligi ya mabingwa ulaya, wengine waliofanya hivyo ni Chamakh na Burak Yilmaz.

* Ronaldo amekuwa mchezaji wa tano kuweka rekodi ya kufikisha mabao 50 ya Champions League. Akiwafuatia Raul 71, Lionel Messi 59, Ruud van Nistelrooy 56 and Thierry Henry 50.

* Timu pekee iliyowahi kugeuza matokeo baada ya kufungwa 4-1 katika mchezo wa kutoana wa Champions League ni Deportivo La Coruna ambao walifungwa 4-1 na AC Milan katika mechi ya kwanza jijini Milan lakini wakaenda kushinda 4-0 kwao Hispania.

* Katika historia michuano ya ulaya ya klabu kumekuwepo na fainali moja tu iliyowakutanisha timu kutoka Ujerumani. 1979-80 UEFA Cup, Frankfurt wakiwafunga Borussia Moenchengladbach.

USHAHIDI WA PICHA ZA MNATO WA MATUKIO MUHIMU YA MECHI YA DORTMUND VS MADRID: INTERVIEW YA MOURINHO AKISEMA MADRID WAMEMSAIDIA LEW4NDOSKI KUWA MAN OF THE MATCH

is2tnmoymJn9u GIF. The Marco Reus penalty claim v Real Madrid
Je hapa Dortmund walinyimwa penati?? Maoni
lewandowski onside HD Quality: Robin van Persies incredible volley v Aston Villa
Ushahidi kwamba Lewandoski alikuwa onside wakati akifunga bao la pili
i0N8j6jzst1bP GIF: Xabi Alonso foul on Marco Reus for Dortmund penalty
JE HII ILISTAHILI KUWA PENATI AU SIO?? MAONI


INTERVIEW YA JOSE MOURINHO BAADA YA MECHI DHIDI YA DORTMUND

SOKA LIPO UJERUMANI SASA?? UJERUMANI 8-1 HISPANIA - MADRID WAKIFUATA NYAYO ZA BARCA KWA KUPIGWA 4-1 NA DORTMUND


MKWASA TUTAKUFA NA SIMBA - LAZIMA TUWAFUNGE MSIMBAZI

Kocha wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa ametabiri kuwa mchezo dhidi ya Simba utakuwa mgumu na wenye kila aina ya ushindani, ingawa ametamba kushinda.

Simba ambayo imechemka kutetea taji lake la ubingwa wa ligi msimu huu, Alhamisi itakuwa kwenye kibarua kigumu kuvaana na Maafande hao, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mkwasa alisema jijini Dar es Salaam kuwa vijana wake wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo na kuahidi ushindi.

"Tumepata muda mzuri wakujiandaa na mchezo wa Simba. Pia, hali za wachezaji wangu wote ni wazima wa afya."

"Simba ni timu nzuri, nimewaona wakicheza katika mechi tofauti. Wana vijana wenye kasi na uzoefu na ligi."

"Lakini kwetu hilo haliwezi kututisha na kucheza bila malengo ya ushindi." alisema Mkwasa ambaye alijiuzulu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars.

Kocha huyo alieleza kuwa mchezo huo utakuwa mkali na wenye ushindani kutokana na timu zote mbili kuundwa na vijana wenye vipaji vya soka na kasi uwanjani.

Simba inashika nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi 37 wakati Ruvu akiwa na pointi 30 na kukamata nafasi ya saba kwenye msimamo huku kila moja ikiwa na michezo mitatu mkononi.

YANGA Vs JKT RUVU HIGHLITES: ANGALIA VIZURI BUILD UP YA GOLI L A NIZAR AFU TOA COMMENT.

Wednesday, April 24, 2013

MJADALA: KIFUNGO CHA MICHEZO 10 ALICHOPEWA SUAREZ KINASTAHILI?

Leo hii mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez amepewa adhabu ya kufungiwa jumla ya michezo 10 kwa kitendo cha kumg'ata Branislav Ivanovic. Je adhabu aliyopewa ni kubwa mno au inastahili ?

WACHEZAJI SIMBA WAWEKWA KITIMOTO KUHAKIKISHA TIMU INAMALIZA NAFASI YA 3


Benchi la ufundi la Simba jana liliwekwa kitimoto na uongozi wa klabu hiyo kutakiwa kuakikisha  inamaliza ligi katika nafasi ya tatu.

Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alithibitisha kuwepo kwa kikao hicho jana ambapo alisema kilikuwa cha kupanga mikakati ya mechi zilizobaki.  "Ni kweli tulikuwa na kikao jana kati ya benchi la ufundi na uongozi.

"Tageti ni kupanga mikakati jinsi gani tufanye kuakikisha timu yetu inamaliza ligi katika nafasi yatatu. Pia, wao walitoa maoni yao. Kwa hiyo kilichobaki ni utekelezaji kutimiza malengo ambayo tumejiwekea." alisema Kamwaga.

"Azam ambayo inashika nafasi ya pili, wametupita na pointi 11. Kwa hiyo nafasi ya pili itakuwa ngumu kwetu." 

Aliongeza kuwa labda itokee Azam wapoteze michezo yao yote iliyobaki na kisha wao washinde kitu ambacho ni kigumu kwa upande wao.

Simba imebakiza mechi tatu dhidi ya Ruvu Shooting, Polisi Moro, Mgambo JKT na Yanga ambayo akishinda yote atakuwa na pointi 48.

Kwa sasa, Simba inagombea nafasi ya tatu na Kagera Sugar ambayo ina pointi 40 na kubakiwa na mechi mbili. Alisema wamekubali kuwa msimu huu wamepoteza lakini wazishuke zaidi ya nafasi ya tatu hivyo iliwaweze kujipanga kwa ajili ya mwakani.

ADHABU ALIYOPEWA SUAREZ YA KUFUNGIWA MECHI 10 UKILINGANISHA NA ADHABU ZA MATUKIO MENGINE YALIYOFANYWA NA WACHEZAJI WENGINE NCHINI ENGLAND


 Muda mchache uliopita Chama cha soka cha England kimetangaza kufungiwa kwa mchezaji Luis Suarez kwa mechi 10 kwa kosa la kumng'ata Branslav Ivanovic katika mchezo wa ligi kuu ya England wiki iliyopita.

Huko nyuma kumekuwepo na matukio ya vurugu uwanjani yaliyofanywa na wachezaji na adhabu zake zikaishia katika kufungiwa mechi kadhaa - sasa tujaribu kuangalia matukio hayo na adhabu zilizotolewa na kufananisha na hii ya sasa Suarez

ADHABU YA MECHI 12

Duncan Ferguson (Rangers): Mchezaji huyu alipewa adhabu ya kufungiwa mechi 12 kwa kumpiga kichwa mchezaji wa Raith aitwaye John McStay mnamo mwaka 1994

Joey Barton (QPR): Mtukutu Joey Barton nae yupo katika nafasi ya kwanza kwa kufungiwa mechi 12 kwa kumpiga kichwa mchezaji wa Manchester City katika mechi ya mwisho ya ligi kuu msimu uliopita.

 

MECHI 11

Paolo Di Canio (Sheffield Wednesday): Kocha wa sasa wa Sunderland ni mmoja kati ya wachezaji watukutu ambao wameshawahi kucheza kwenye ligi kuu ya England - mnamo mwaka 1998 alimsukuma refa Paul Alcock na kwa kitendo hicho akafungiwa mechi 11.

MECHI 10 

Kevin Keegan (Liverpool) na Billy Bremner (Leeds): hawa magwiji wa soka walifungiwa mechi 10 kwa kitendo chao cha kupigana katika mechi ya kombe la hisani mwaka 1974
David Putton (Southampton): Kama ilivyokuwa kwa Di Canio - Alan Wiley nae alimsukuma refa mwaka 2005 na akafungiwa mechi 10.

NINE MATCHES

Paul Davis (Arsenal): Alifanya kosa la kumpiga ngumi Glenn Cockerill mwaka 1998.
Steve Walsh (Leicester) kwa utovu wa nidhamu mnamo mwaka 1987
Frank Sinclair (West Brom): Kwa kitendo cha kujaribu kumpiga kichwa refa mnamo mwaka 1992

EIGHT MATCHES

Luis Suarez (Liverpool): Kwa kumtolea matusi ya kibaguzi mchezaji wa Manchester United Patrice Evra mnamo mwaka  2011
Ben Thatcher (Manchester City): Kwa kosa la kumpiga kiwiko Pedro Mendes mwaka 2006
Mark Dennis (QPR): Alifungiwa mwaka 1987 kwa kupata kadi nyekundu ya 11 ndani ya ligi kuu ya England.

BREAKING NEWS: LUIS SUAREZ AFUNGIWA MECHI 10 KWA KOSA LA KUMNG'ATA IVANOVIC

LUIS SUAREZ amefungiwa mechi 10 kwa kitendo chake cha kumng'ata Branislav Ivanovic.

Mshambuliaji huyo wa Liverpool ambaye haiishi vituko uwanjani jana alikiri kwamba alifanya kweli shambulio hilo. Na leo hii FA wamemaliza msimu wake kwa kumpa adhabu ya mechi 10. 

Kwa kawaida adhabu ya kitendo cha vurugu huwa ni mechi zisizodi 3 lakini wamesema kwamba adhabu hiyo haitoshi kwa Suarez ambaye amekuwa mtukutu kwa matukio ya ajabu ajabu kila mara. 

Suarez jana usiku alikataa kukubaliana na adhabu ya zaidi ya mechi 3. Lakini leo FA wameamua vinginevyo kwa bad boy Suarez na hivyo atakumbana na adhabu ya kutocheza mechi 10 za mashindano yaliyo chini ya FA. l

Mkurugenzi wa Liverpool  Ian Ayre alisema: "Sote klabu na mchezaji husika tumeshtushwa na kutopendezewa na maamuzi haya - tunasubiri sababu za kimaandishi kabla hatujatoa uamuzi wowote hapo kesho."

Suarez ana muda mpaka Ijumaa kupinga adhabu hiyo kwa kukata rufaa.

TAIFA STARS KUSHIRIKI MICHUANO YA COSAFA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itashiriki michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika Julai mwaka huu nchini Zambia.

Taifa Stars inashiriki michuano hiyo ya timu za Taifa za nchi wanachama wa COSAFA ikiwa timu mwalikwa. Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoro, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.

Michuano hiyo itafanyika kuanzia Julai 6 hadi 21 mwaka huu katika miji ya Lusaka, Ndola na Kabwe. Ratiba ya makundi ya michuano hiyo itapangwa Mei 3 mwaka huu jijini Lusaka.

Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika miaka mitatu iliyopita. Hii itakuwa mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo baada ya kucheza ya kwanza iliyofanyika mwaka 1996 nchini Zimbabwe.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajia kuingia kambini mwishoni mwa mwezi ujao kujiandaa kwa mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.

Juni 16 mwaka huu Taifa Stars itacheza na Ivory Coast jijini Dar es Salaam katika mechi nyingine ya mchujo ya Kombe la Dunia wakati Juni mwishoni na Julai mwanzoni itacheza mechi ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.

Wakati huo huo, waandishi wa habari wanaotaka kuripoti michuano hiyo wanatakiwa kuwasilisha majina yao TFF kabla ya Aprili 27 mwaka huu ili maombi yao yatumwe COSAFA kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho (Accreditation).

CHELSEA NDIO TIMU YA MWISHO KUIFUNGA BARCA MABAO 4 KWENYE CHAMPIONS LEAGUE: MESSI ANA NUKSI NA MULLER

* Mara ya mwisho mshambuliaji Lionel Messi kuichezea timu iliyofungwa mabao 4-0 ilikuwa dhidi ya wajerumani. Argentina ilipofungwa kwenye robo fainali ya kombe la dunia 2010. Pia siku hiyo kama ilivyokuwa leo Thomas Mueller, alifunga mabao mawili tena. 

 * Barcelona wameruhusu wavu wao kuguswa mara nne katika mechi ya Champions League kwa mara ya kwanza tangu walipofungwa 4-2 na Chelsea katika hatua ya 16 bora March 2005.

* Timu ya kwanza kuifunga Barcelona 4-0 katika michuano ya ulaya ilikuwa ni Dynamo Kiev katika hatua ya makundi mnamo November 1997.

* Hakuna timu iliyofungwa kwenye raundi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Champions League/European Cup kwa mabao manne kwa bila au zaidi iliyoweza kufuzu kuendelea raundi ya pili. 

* Barcelona walipiga shuti moja tu liloenga goli la Bayern leo, idadi ndogo zaidi katika Champions League msimu huu. 

* Katika mashindano yote - Barcelona hawajafungwa 4-0 tangu walipoonyoshwa na Getafe katika kombe la mfalme May 2007. Miaka sita iliyopita.

ANGALIA KWA PICHA ZA MNATO MATUKIO YOTE YA UTATA BAYERN VS BARCA KUSHIKA MIPIRA NDANI YA BOX KWA PIQUE NA SANCHEZ, ALBA, GOLI LA GOMEZ

iSLmkr9gZkVEo GIF: The ball hits Alexis Sanchezs hand in the Barca box, no penalty given
ALEX SANCHEZ - JE HII ILIKUWA PENATI AU SIO??

GOLI LA MARIO GOMEZ

bayern munich scores second goal against barcelona GIF: Another angle of Mario Gomezs goal v Barcelona










ANGLE YA KWANZA

i68jaEHig0MgA GIF: Mario Gomez sweeps Bayern 2 up v Barcelona
 ANGLE YA PILI

Handball_medium
Je hii ilipaswa kuwa penati au sio - mpira wa shuti uliopigwa na Lahm ukizuiliwa na Pique kwa mkono

ipfEIQw57MhSC GIF: Jordi Alba throws the ball in Arjen Robbens face
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

BARCELONA YAPIGWA 4-0 NA BAYERN MUNICH - MARA YA MWISHO KUFUNGWA 4-0 ILIKUWA MIAKA 16 ILIYOPITA

Tuesday, April 23, 2013

KOCHA KIM POULSEN ATANGAZA YOUNG TAIFA STARS



Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.


Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23 mwaka huu) kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.


Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.


“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.


Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.


Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily Mgeta (Simba).


Viungo ni Haruna Chanongo (Simba), Edward Christopher (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), William Lucian (Simba), Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah Seseme (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar).


Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).


AFRICAN LYON, JKT RUVU KUUMANA CHAMAZI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 24 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya wenyeji African Lyon na JKT Ruvu.


Mechi hiyo namba 165 itachezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Kamishna Hamisi Kisiwa wa Dar es Salaam. Waamuzi wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Hashim Abdallah, Omari Kambangwa, Abdallah Selega na Said Ndege wote wa Dar es Salaam.


BAYERN MUNICH VS BARCELONA: BARCA HAWAJAWAHI KUIFUNGA BAYERN JIJINI MUNICH - ILA HAWAJAFUNGWA UJERUMANI KWA MIAKA 10

Klabu za Ujerumani mara nyingi huwapa wakati mgumu wapinzani wao wakiwa kwenye ardhi yao, lakini Barca, ambao leo wanacheza na Bayern Munich wana rekodi nzuri katika ardhi ya Ujerumani. Hawajawahi kupoteza mechi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ndani ya Ujerumani - wakicheza mechi nane dhidi ya vilabu vya Bundesliga.

Hizi ndio mechi za Champions League walizocheza Barca dhidi ya vilabu vya Bundesliga.

2011/12: Bayer Leverkusen-FCB (1-3). Raundi ya kwanza ya hatua ya 16.

2009/10: Stuttgart-FCB (1-1).
Raundi ya kwanza ya hatua ya 16.

2008/09: Bayern-FCB (1-1). Raundi ya pili ya robo fainali.

2007/08: Schalke-FCB (0-1): Raundi ya kwanza ya robo fainali.

2007/08: Stuttgart-FCB (0-2): Makundi

2006/07: Werder Bremen-FCB (1-1). Makundi.

2005/06: Werder Bremen-FCB (0-2). Makundi.

2002/03: Bayer Leverkusen-FCB (1-2). Makundi.

Miaka 11 baada ya kipigo

Inabidi urudi nyuma mpaka msimu wa 2001/02 kwa mara ya kwanza FC Barcelona walipoteza mchezo nchini Ujerumani, dhidi ya Bayer Leverkusen katika hatua ya makundi (2-1). Tangu wakati  Barcelona hawajafungwa na klabu ya Ujerumani, wakiwa na rekodi ya nzuri nyumbani na ugenini, wakishinda mechi 14 na suluhu 3.

Hawajashinda jijini Munich

Ukisoma hapo juu utaona hali nzuri tu kwa upande wa Barca, lakini rekodi ya Barca ndani mji wa Milan sio nzuri sana, vijana wa Tito Vilanova hawajawahi kushinda mechi yoyote rasmi dhidi ya Bayern ndani ya mji Munich. Walitoka sare kwenye nusu fainali ya UEFA Cup 95/96 na pia kwenye robo fainali ya Champions League  2008/09. Mara ya mwisho walifungwa na Bayern kwenye hatua ya makundi msimu wa  98/99.

CHEMSA BONGO! TAJA MAJINA YA KIKOSI HIKI CHA YANGA.

MAGUMASHI DOT COM : JKT RUVU KWA STAILI HII KWANINI WASISHUKE DARAJA ?

Zingatia tofauti za wazi zinazoonekana kwenye orodha ya watu wanaopaswa kuwepo kwenye benchi la ufundi la timu za Yanga na Jkt Ruvu. Kwa upande wa Yanga kila kitu kiko wazi kocha amewekwa,wasaidizi wake na kila mmoja amekaa kwenye nafasi yake kama inavyostahili kwenye timu inayoshiriki ligi kuu ya soka . Upande wa Ruvu Jkt kuna walakini mkubwa . Kila mmoja anafahamu kuwa kuna sheria inayozibana timu za ligi kuwa na watu wenye sifa fulani zinazohitajika kwa kocha mkuu wa timu ya Ligi kuu . Azish Kondo hana hizo sifa. Jina la Keneddy Mwaisabula limeandikwa kwa kalamu na sio kuchapishwa kama upande wa Yanga. Kennedy Mwaisabula hakuwepo uwanjani siku hiyo wakati Ruvu walipocheza na Yanga , na sababu kubwa ya jina lake kuandikwa kwa kalamu ni ukweli kwamba Ruvu walijaza jina lake ili watimize kanuni ya TFF inayohitaji makocha wenye vigezo ambavyo Azish Kondo hana. Kwa mwenendo huu Ruvu wakishuka daraja watamlaumu nani?

JE WAJUA :SIO WACHEZAJI WOTE WA MAN UNITED WA KIKOSI CHA KWANZA WATAPEWA MEDALI ZA UBINGWA WA 20?

Usiku wa kuamkia leo Manchester United imeweza kutwaa ubingwa wa 20 wa ligi kuu ya England baada ya kuifunga Aston Villa kwa mabao 3-0.

Lakini Manchester United hawakupewa kikombe leo hii wakisubiri mpaka mechi ya mwisho ya nyumbani dhidi ya Swansea ndio wakabidhiwe kombe lao pamoja na medali zao za ushindi wa Barclays Premier League

Katika kikosi cha kwanza Manchester United msimu huu karibia wachezaji wote wamecheza mechi zaidi ya 10 za Premier League kasoro Nick Powel na Alexander Butner ambao hawajatimiza michezo 10 na hata kama wakicheza mechi zote zilizobakia hawatoweza kutimiza idadi ya mechi hizo ili waweze kuwa miongoni mwa wachezaji wa United watakaokabidhiwa medali baada ya mechi ya Swansea.

Sheria za Premier League kuhusu wachezaji watakaoweza kupewa medali zinasema

Mchezaji anatakiwa awe amecheza mechi zisizopungua 10 kwa klabu yake husika ili aweze kufuzu kupata medali ikiwa timu yake itachukua ubingwa.

Aidha klabu husika inaweza kutuma maombi ya medali za ziada kwa ajili ya wachezaji ambao hawakufikia idadi ya mechi 10.

MAAJABU: MTOTO KIPOFU AWATAMBUA WACHEZAJI WA BARCA KWA KUWASHIKA TU JAPO HAONI


Hi there: The nine-year-old managed to recognise Lionel Messi and Co
Hapa akijaribu kuwatambua Lionel Messi na Iniesta

Mtoto wa miaka tisa ambaye ni shabiki wa Barcelona ambaye ni kipofu, amewashangaza watu wengi wakiwemo mastaa wa Barca kwa kuweza kuwatambua kwa kuwashika tu. 

Mamadou Lamine, ambaye alizaliwa akiwa kipofu, alialikwa katika kituo cha kufanyia mazoezi cha Barca ili kukutana na mashujaa wake. 

Mtoto huyo alikuwa anashika mikono, paji la uso na vichwa vya Messi, Eric Abidal na Carlos Puyol, na akafanikiwa kuwatambua wote


I know you: He recognised Eric Abidal by rubbing the top of his head
Hapa akijaribu kumtambua Eric Abidal kwa kumshika kichwa na alifanikiwa

KALI YA LEO: HIVI NDIVYO EVRA ALIVYOSHANGILIA UBINGWA WA 20 WA UNITED KWA KUMUIGA LUIS SUAREZ

iPbSAGy6DUntY.gif

ROBIN VAN PERSIE AIONGOZA MAN UTD KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA ENGLAND.

FALSAFA YA SOKA LA KIDACHI TARATIBU YAANZA KUONEKANA MITAA YA JANGWANI……

YANGA imeifunga JKT Ruvu mabao 3-0 katika mchezo namba 106 wa Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mchezo huo, mashabiki wa Yanga walifurahia matokeo hayo kutokana na ukweli kwamba, timu hiyo yenye pointi 56 inahitaji pointi moja tu iweze kutangaza ubingwa kwani timu inayoifuata ambayo ni Azam FC ina pointi 47.

Azam imebakisha mechi tatu na ikishinda zote itakuwa imefikisha pointi 56 ambazo Yanga inazo sasa. Yanga imebakisha mechi mbili tu dhidi ya Coastal Union na Simba. Hivyo sare tu inatosha kuipa Yanga ubingwa msimu huu. Wakati mashabiki na wanachama wa Yanga wakifurahia timu yao kuelekea kutwaa ubingwa, kuna kitu kilikuwa kimetokea katika mechi za jana dhidi ya JKT Ruvu, nacho ni soka la kuvutia ambalo kitaalam tunaweza kuita ni TOTAL FOOTBAL lililokuwa likichezwa na Yanga.


FALSAFA YA SOKA LA KIDACHI ILIIUA JKT
Katika mchezo wa jana, Yanga ilicheza ‘total football’ katika muda mwingi wa mchezo huo kiasi cha kuichanganya JKT Ruvu ambayo angalau kipindi cha kwanza iliweza kuizuia Yanga.

Tangu alipowasili katika klabu ya Yanga akitokea APR ya Rwanda, Kocha Ernie Brandts amekuwa akitilia mkazo ufundishaji wa soka la Kiholanzi, nchi anakotokea.

Ndani ya total football, kila mchezaji anawajibika ipasavyo na wachezaji wote wanacheza mahala popote ili mradi lengo la timu litimie. Kwa muda mrefu total football imekuwa ikitumiwa na Uholanzi na kuvitetemesha vigogo vya soka.

Tunaposema kila mchezaji anacheza namba yoyote mbali ya ile aliyokabidhiwa kucheza siyo kwa kujichezea tu, bali mchezaji anapaswa kuwajibika ipasavyo kuweza kutimiza lengo la timu.

Mchezaji anapokuwa katika mfumo wa total football ni lazima awe na vitu vifuatavyo, KWANZA awe na skills yaani uwezo wa kuwa na mbinu za kumuwezesha kuufanya mchezo uendelee katika mazingira yoyote yale.

Hapa unaweza kuona jinsi viungo Athuman Idd Chuji, Haruna Niyonzima na Frank Domayo walivyokuwa wanaweza kuwa na mbinu mbalimbali za kuendesha mpira bila ya matatizo.

Tazama bao la tatu lililofungwa na Nizar Khalfan, mpira ulianzia kwa Kelvin Yondani kisha kwa Niyonzima nyuma kabisa ya lango la Yanga, lakini kiungo huyo aliyekuwa anacheza kama winga wa kushoto, aliweza kurudi nyuma kabisa kufuata mpira kisha akaanzisha shambulizi lililozaa bao bora tena yeye akiwa ndiye ametoa pasi ya mwisho.

Kitu cha PILI katika total football ni pasi, lazima timu icheze kwa pasi kuanzia nyuma kwa mabeki hadi kwa washambuliaji wake. Hata Barcelona wanacheza hivyo na ndiyo maana leo hii wanasifika kwa mchezo huo.

Katika bao la tatu pasi ilianzia kwa beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani ambaye alipeleka mpira kwa Niyonzima, naye akaondoka na mpira kwa kutumia mbinu za kawaida kabisa akacheza pasi ‘one-two’ na Domayo, kisha Twite na Msuva na kufanya hivyo hadi alipofika katika lango la JKT Ruvu kwa Niyonzima tena kisha Domayo akapiga shuti lililogonga nguzo ya goli kisha Nizar akafunga bao.

Kitu cha TATU katika total football ni jinsi timu inavyotembea kwenda mbele. Vitu vyote vitatu lazima vifanye kazi ili mfumo huu uweze kuleta faida katika timu.

Yanga ilicheza kwa kutumia mbinu, kisha pasi zikapigwa na mwisho move ilikuwepo kwa timu nzima ndiyo maana mpira uliweza kuanza golini kwao na ukafika kwa JKT Ruvu bila shaka yoyote.

Tukirudi katika mfano wetu wa bao la tatu, utaona jinsi Niyonzima alivyokuwa aki-move na mpira huku akiuweka vituo kwa Domayo na Chuji ambao nao walikuwa wakienda naye sawa kwa kumfuata hadi katika lango la JKT Ruvu na kufunga bao.

Timu ilionekana ‘imeiva’ katika kutekeleza mfumo huu wa total football kiasi cha kuichachafya ngome ya JKT Ruvu itakavyo na kuweza kupata mabao matatu muhimu kwao
.
    Erns Brandts akimpa maelekezo kiungo Frank Domayo...

RINUS MICHELS NDIYE ALIYEMPA FALSAFA HII BRANDTS?
Katika soka la Kidachi,Total Football ndiyo inayotamba na ndiyo maana siku zote timu ya taifa ya Uholanzi inaonekana ni moto wa kuotea mbali.

Rinus Michels mwasisi wa TF na ndiye aliyeeneza hii falsafa nchini mwake Uholanzi pamoja na nchi ya Hispania alipokwenda kwenye Klabu ya Fc Barcelona na kuiongoza kushinda taji la ligi ya nchi hiyo mnamo mwaka 1974.

Rinus Michels alimrithisha Johan Cruyff ambaye aliuendeleza kwenye vilabu vya Ajax na Barcelona akiwa kama kocha,

Falsafa hii ndo imekuwa siri kubwa ya mafanikio ya FC Barcelona tunayoishuhudia leo hii ikitandaza soka la hali ya juu.

http://thefootballasylum.com/wp-content/uploads/2011/08/t02_nl_jubel_michels_1988_enpropertyoriginal.jpg
Rinus Michels akiwa na kombe la mataifa ya Ulaya mnamo mwaka 1988

Tukumbuke ya kwamba, katika fainali za Kombe la Dunia za 1978, Brandts alikuwepo katika kikosi cha Uholanzi chini ya kocha mwingine nguli Ernst Happel kilichocheza fainali hizo huko Argentina. Kikosi cha Ernst Happel kilifika fainali na kufungwa na wenyeji Argentina mabao 2-1,Ndani ya kikosi hicho kulikuwa na wachezaji zaidi ya wanane waliokuwepo kwenye kikosi kilichoundwa na Rinus Michels mwaka 1974 na kufungwa kwenye mchezo wa fainali na mwenyeji iliyokuwa Ujerumani Magharibi, mfano majina kama mapacha Willy van de Kerkhof na René van de Kerkhof,Johan Neskeens,Ruud Krol, Rob Rensenbrink, Arie Haan hao ni baadhi ya majina yaliyokutana na Ernst Brandts kwenye kikosi cha Uholanzi cha mwaka 1978 kilichoendeleza falsafa ya Rinus Michels,

Namnukuu Rinus Michels mnamo mwaka 1988 alipoiongoza Uholanzi kutwaa kombe la mataifa ya ulaya ‘’ nimekirithisha FALSAFA yangu kizazi cha kati ya 1965-1980, hata kama sitakuwepo duniani siku moja naamini kitalisambaza neno langu kwa vizazi vijavyo ‘’

Miongoni mwa vizazi hivyo yumo Ernst Brandts ambaye naamini ameileta FALSAFA ya nguli Rinus Michels nchini Tanzania kupitia mitaa ya Jangwani.

Wakati Cruyff akiipeleka FALSAFA hiyo huko Catalunya kwenye klabu ya FC Barcelona ambayo hata akija kocha gani, bado mfumo huo utaendelea kutumika.

Gwiji huyo wa Uholanzi alipandikiza total football kwa wachezaji chipukizi waliokuwa wakijifunza soka katika kituo cha michezo cha La Masia ambako Lionel Messi na wenzake kibao wa kikosi cha kwanza cha Barcelona wapo.

Ni wazi kwamba, mafaniko ya total football kwa Cruyff ndiyo yaliyomsukuma Brandts kutumia mfumo huo katika Yanga na leo hii Yanga inafaidika na hali hiyo
.
    Johan Cruyff ...Ndiye siri ya mafanikio ya FC Barcelona ya leo...

YANGA KIWANGO KIMEPANDA, BRANDTS AMEFANIKIWA
Kwa soka lililochezwa katika mechi ya jana, ni wazi  kiwango kimeongezeka na pia Brandts amefanikiwa kuingiza falsafa ya mpira wa kidachi ndani ya kikosi cha Yanga.

Tazama siku hizi uchezaji wa Cannavaro, si yule aliyekuwa akiokoa kwa kubutua mpira juu au bora liende mbele kwa kuutoa katika lango lake.

Cannavaro sasa anaweza kuanziwa mpira, akatulia, akapiga pasi kisha akapanda na move, hivyo siku hizi anaisadia timu kwa kiasi kikubwa ndiyo maana anafunga hata mabao muhimu kwa timu yake.

Katika mechi ya jana, kuna muda Yanga ilipata faulo jirani na lango la JKT Ruvu, Cannavaro alienda kucheza faulo ile na ilibaki kidogo afunge kwa kichwa mpira wa adhabu hiyo uliopigwa na Domayo.

Sasa Cannavaro anajua mpira unaokuja auzuie vipi na hata kukaa kwenye maeneo husika kwenye muda muafaka (Positioning) na hata apige vipi mpira ili uweze kufika kwa mlengwa, hata namna ya kufunga kwa kutulia pia anajua. Cannavaro ana mabao matano katika Ligi Kuu ya Bara kama ilivyo kwa straika wa Simba, Felix Sunzu.

Hata beki mwingine wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani naye kiwango kimeongezeka chini ya Brandts na sasa ameongeza ufanisi zaidi (Focus) katika kumiliki mpira na kuanzisha mashambulizi.