Search This Blog

Thursday, April 25, 2013

MJADALA: MDAU MAJALIWA ANAULIZA FIFA WALITUMIA VIGEZO GANI KUTEUA KIKOSI BORA CHA MWAKA ?

FIFA wana kipi cha kutuambia kupitia data chache kama hizi?

 1. Ligi bora-La liga

2. Mchezaji bora-La liga

3. Timu yao wachezaji wote-La liga 

4. Kocha bora-spain

UDHAIFU: La liga ina ushindani kwa timu mbili tu kwa zaidi ya miaka 10 sasa, hii imetokana na utofauti mkubwa wa mapato baina ya timu mbili kubwa na timu zingne zczo na kipato kikubwa, hata hivyo FIFA wameziba mackio na kujitoa akili kwa kuiona ndio ligi bora.

Hata chelsea waliochukua ubingwa wa UEFA japo ilikuwa kwa kubahatisha hawakutoa mchezaji yeyote kwenye kikosi cha FIFA matokeo yake mtu km Pique ambaye cjawahi kuukubali uwezo wake aliingizwa licha ya kutocheza kwa muda mrefu kutokana na kutoelewana na aliyekuwa kocha wake Pep Gudiola hivyo FIFA walimuingiza kwenye timu yao labda kwa kumtia ujauzito Shakira! Vivyo hivyo timu za La Liga hat fainali ya UEFA hazikucheza but bado zikaendelea kuhesabika bora.

MWISHO: TIMU YA FIFA imepigwa 8-1 na timu ambayo ligi yake huingiza timu 3 tu kwenye UEFA. Inasikitisha sana, maghumashi hadi kwenye fani ipendwayo na walimwengu wote!

Naitwa Majaliwa Mayala wa Buswelu Mwanza Tanzania, naishi kwa mkopo Dodoma

6 comments:

  1. Nakuunga mkono ligi gani timu 2? Hawa watu lazima watakuwa malienge!! Hawaoni vizuri si bure!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii ni blog ya Man U, so sishangai kuona criticism anapokosekana mtu wa Utd kwenye ishu kama hizi

      Delete
  2. ...sasa mtu anapoanza kuzungumzia mchakato wa tuzo za msimu wa 2011-2012,kwamba FiFA walikosea kuna mantiki ama mdau unakosa uelewa mdogo kwamba kilichofanyika pale ni kuwatunza wachezaji na makocha waliofanya vizuri msimu huo..??na kinachoendelea sasa ni msimu mwingine wa 2012-2013..??wakati mwingine tuwe na malalamishi yenye mashiko kidogo.
    Na jambo la muhimu ni kuelewa mpira wa miguu ni kama cycle leo unakua juu kesho unashuka,so sioni haja ya mtu kuanza kuhoji uwezo wa wachezaji wa ligi ya hispania kwa msimu ule na hata ligi yenyewe ubora wake kama tutaangalia takwimu kuanzia ligi ya mabingwa,kombe la dunia na hata olimpiki

    ReplyDelete
  3. tusiwe wanafki wa kila jambo likitokea ndio tuhoji na kuacha yaliopita yaani tayasi 2mesahau timu za hispani zivyoinyanyasa ulaya msimu uliopita kama c chelsea 2 ndio iliojitutumua? na je matokeo yakigeuka game za marudio? matahoji nn

    ReplyDelete
  4. Cdhan km hoja hii imetendewa haki na ndio maana watu wanapata matokeo mabovu ktk mitihan yao ya kidato cha nne, haiwezekan hoja ya msingi iwe kutoa tu vigezo na c kinginecho, nadhan hapo kuna mifano km fainali kuwa ya Bayern na chelsea, euro ni spain na italy sasa je La Liga imeinyanyasa ligi ipi kwa huo mcmu na mtu km Pique alikuwepo na mkwaruzano na kocha wakati hadi ilifikia wakati akaondoka kambini kwenda kula bata Marekan kutokana na kuchomeshwa mahindi, hayo hamuyaoni hadi muanze kuongelea Man U? Ishu sio Man U bt msingi wa swali ni namna FIFA wanavyoweza kuondoa huu utata wa cfa zote zlizotolewa kwa La Liga.
    Hapa naomba tujadili tu uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kwa msimu uliopita, mf. Marcelo alikuwa na mafanikio gani dhidi ya performance ya Ashley Cole?
    Naomba kuwaclisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. hivi mnaojadili na aliyeweka mada mnamapungufu ya fikra na mmejaa hisia kuliko wataalamu wa mpira huko ulaya,hivi kati ya nyinyi na hao wataalamu wa uefa na wako karib na hao wachezaji?msijifanye mnajua waachen wataalam wa mpira ulaya,achen ushabiki wa ligi yenu ya magazetin

      Delete