Search This Blog

Thursday, April 25, 2013

MARCO REUS APONDA MUDA WA KUTANGAZWA UHAMISHO WA GOTZE KWENDA BAYERN

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus amesema kitendo cha kutangazwa kwa dili la uhamisho wa Mario Gotze kwenda Bayern Munich kwa wakati huu ni cha kijinga mno wakati timu yake ikiwa katika kuelekea fainali ya Ligi ya mabingwa wa ulaya.

Tangazo la kuondoka kwa Gotze lilitolewa masaa 48 kabla ya mchezo wa raundi ya kwanza wa nusu fainali ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Madrdi - na maandalizi ya mchezo huo yakawa yamegubikwa na taarifa za kuondoka kwa kijana huyo wa kijerumani mwenye umri wa miaka 20.

Reus anakiri taarifa hiyo imekuja wakati m'baya sana kwa Dortmund lakini akawaomba mashabiki wakae nyuma ya Gotze nakumsapoti mpaka mwisho wa msimu.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Facebook mfupi kabla ya mechi dhidi ya Madrid Reus alisema, "Leo ndio siku ya mechi, tunaangalia mbele kukutana na Real Madrid na tunataka kufika fainali. Hakuna cha umuhimu zaidi ya hii mechi, kuliko hata kuhusu ile habari ambayo Ujerumani yote inaizungumzia.

"Mario amefanya maamuzi kwa ajili ya maisha yake. Inabidi tuheshimu kuhusu hilo. Muda wa kutangaza uamuzi huo kiukweli haukuwa mzuri - na wa kijinga. Lakini inabidi wote tuungane kwa sasa - wachezaji wenzangu na mashabiki tuwe kitu kimoja.

"Nafikiri baadhi ya maoni kuhusu Mario niliyoyasoma kwenye facebook sio mazuri, hastahili kutusiwa, ana mengi ya kuishukuru Dortmund na mashabiki lakini pia sie tunapaswa kumshukuru - tusisahau hilo.
"Tafadhali tuangalie kusherehekea usiku mkubwa soka kwa pamoja - na Mario akiwepo pia." Alimaliza Reus ambaye jana akicheza kwa pamoja na Gotze walisababisha madhara makubwa kwenye ukuta wa Real Madrid - Gotze akitoa pasi ya goli la kwanza huku Reus akisababisha penati ya goli la nne.

No comments:

Post a Comment