Search This Blog

Saturday, May 18, 2013

MPAMBANO WA SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA.


    Haruna Shamte akipambana na Simon Msuva wa Yanga...
    Nahodha wa Yanga Nadir Haroub akinyanyua ubingwa wa ligi kuu ya VODACOM msimu wa 2012/2013


    kikosi cha Simba kilichoanza hii leo....
    Makocha wa Yanga Ernst Brandts pamoja na Felix Minziro wakijadiliana jambo.....
    Sir Juma Nature pia alikuwepo kutoa burudani.....
  Hili ndo lilikuwa bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Didier Kavumbagu kwa kichwa....
   Mrisho Ngassa akiwa amevalishwa jezi ya YANGA kwa mara nyingine tena huku akiwa amefurahi kweli kweli...   Mwamuzi wa mchezo wa leo Saanya akiwa chini mara baada ya kuumia.....

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 0 - 2 YANGA SC

Mpira umemalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC
Kavumbagu ddk 4
Kiiza dkk 63

Dk 85 Nizar Khalfan anapiga shuti kali langoni kwa Simba lakini Kaseja anaokoa na kuumia. Simba 0-2 Yanga

Dk 76 SUB....! Simba imefanya mabadiliko ametoka Haruna Chanongo ameingia Ramadhan Singano 'Messi'

Dakika ya 75, Young Africans 1 - 0 Simba SC
Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza

Dk 69 Sunzu wa Simba anamchezea faulo Mbuyu Twite wa Yanga. Mpira unasimama kwa muda ili Twite atibiwe.

Dakika ya 63, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili - Young Africans 2 - Simba SC

DK 60 Yanga wanaendelea kuongoza hapa dhidi ya Simba

Dk 47 SUB: Simba imefanya mabadiliko, ametoka Abdallah Seseme ameingia Felix Sunzu.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Simba SC

Dk 38 Simba inapata kona ya pili.
Dk 35 Kiiza wa Yanga anakosa bao la wazi baada ya mpira alioupiga kutoka juu ya lango la Simba. Simba 0-1 Yanga.

Dk 32 Mwinyi Kazimoto wa Simba anamchezea vibaya Frank Domayo wa Yanga.

Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosa
Dk 27 PENALLLLTTY......! Simba inapata penalti baada ya Cannavaro kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.

Dk 21 Hamis Kiiza wa Yanga anauwahi vizuri mpira katikati ya mabeki wa Simba waliojichanganya kuokoa lakini shuti lake hafifu linaokolewa na kipa wa Simba, Juma Kaseja.

Dk 20 Cannavaro wa Yanga anachezewa faulo na Haruna Shamte wa Simba.

Dk 16 YELLOW CARD......! Haruna Shamte wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Simon Msuva. Simba 0-1 Yanga

DK 15 Simba 0 - 1 Yanga

Dk 10 Didier Kavumbagu wa Yanga anamchezea faulo Shomari Kapombe.

Dk 8 Simba inapata kona ambayo haizai matunda

Didier Kavambagu anaipatia Yanga bao la kuongoza

Dk 1 YELLOW CARD...! Mbuyu Twite wa Yanga anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Haruna Chanongo wa Simba.

Mpira unaanza uwanja wa Taifa

Simba line up: Juma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba na Haruna Chanongo. Sub: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano 'Messi', Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude na Hassan Mkude

Yanga line up: Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Athuman Idd 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima. Sub: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuz na Jerry Tegete

CLOUDS THE DREAM TEAM ILIVYOPEPETANA NA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA IFM NA KUTOKA SARE 1-1

Ibrahim Masoud Maestro akitoa maelekezo kwa timu yake ya Clouds wakati wa mapumziko

Alex Luambano hoiiiiiiiiiii

    Wachezaji wa IFM wakiwa hawaamini wanachokishuhudia.....
 Kocha wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha Dotto Mokili akiwapa maelekezo wachezaji wake.
   Nikiwa na washikaji zangu wa IFM....Kulia kwangu ni mwanangu mwenyewe Mohammed Killer pamoja golikipa wangu TALIB enzi zile za SHIMIVUTA.....

Mchezo mkali wa kirafiki kati ya CLOUDS MEDIA 'The Dream Team' dhidi ya Wafanyakazi wa chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM ) ulimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1:1.
Mchezo huo ulifanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers maeneo ya kawe jijini Dar Es Salaam.
RONALDO NA MOURINHO WAMALIZA MSIMU KWA AIBU YA KUTOLEWA NJE YA UWANJA - REAL MADRID WAKIFUNGWA NA ATLETICO MADRID KWENYE FAINALI YA COPA DEL REY


Copa del Rey Final: Real Madrid 1-2 Atletico... by ourmatch
Mourinho sent off by Counterpoint1
CR7 Red by Counterpoint1

Friday, May 17, 2013

BAYERN MUNICH VS DORTMUND: WIKI KABLA YA FAINALI DORTMUND WAWAKUMBUSHA BAYERN MACHUNGU YA GOLI LA SOLSKJAER

Oh no you di'int, Dortmund! (101GG)

Huku zimebakia siku chache kabla ya fainali yao ya Champions League dhidi ya Bayern Munich ndani ya dimba la Wembley, Borussia Dortmund wameanza mind games kwa kuwakumbusha Mabavarian moja ya kumbukumbu zao mbaya kabisa za fainali ya UCL.
BVB wameweka jezi ya Manchester Utd iliyokuwa ikivaliwa na  Ole Gunnar Solskjaer katika jumba lao la makumbusho. Hii itawakumbusha Bayern Munich alichowafanya Mnorway huyo alipofunga goli la ushindi katika dakika ya 93 ya mchezo katika fainali ya mwaka1999 ya Champions League. Tukio hili limekuwa moja ya muhimu katika historia ya michuano hiyo.

Jezi hiyo ni ya Ole Gunnar Solskjaer sio ile aliyoivaa kwenye fainali ya mwaka 99, hii ni ile ambayo alivaa kwenye mchezo wa nusu fainali ya European Cup dhidi ya Dortmund ambapo United walifungwa na Solskjaer - Baby-Faced Assassin alibadilishana na jezi na Knut Reinhard.

KALI YA LEO: MOURINHO AGOMA KWENDA KWENYE MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI - MWANDISHI AMALIZIA HASIRA ZAKE KWENYE PICHA YAKE


Jose Mourinho hakutokea kwenye mkutano wa waandishi wa habari siku moja kabla ya mchezo wa fainali wa Copa del Rey baina ya Real Madrid na Atletico Madrid, hivyo Sergio Ramos aliachwa kujibu maswali ya waandishi mwenyewe. Mwandishi mmoja wa kibrazil hakuridhishwa na suala la Mourinho kutotokea hivyo akaamua kuonyesha hasira zake kwa kuchana chana picha ya Mourinho.

Mwandishi huyo alikuwa akichana picha huku akisema kwamba kocha huyo wa kireno ni mpumbavu.

EXCLUSIVE: HIZI NDIO ORODHA MBILI ZA MAREFA WALIOPANGWA KUCHEZESHA MECHI ZA MWISHO ZA LIGI KUU - KABLA NA BAADA YA KUBADILISHWA NA TFF - MWAMUZI WA MCHEZO WA WATANI TU NDIO ABADILISHWA

Hii ndio orodha ya marefa watakaochezesha mechi za mwisho za ligi kuu kabla ya kubadilishwa kwa mwamuzi mmoja tu wa mchezo wa Simba vs Yanga.


Hii ndio orodha ya pili ilitolewa na TFF baada ya kumbadilisha refa wa mchezo wa Simba na Yanga huku mechi nyingine kukiwa hakuna mabadiliko yoyote ya waamuzi.PAZIA LA LIGI KUU YA VODACOM LAFUNGWA KESHO - TIMU ZOTE 14 DIMBANI

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu (2012/2013) inafikia tamati kesho (Mei 18 mwaka huu) kwa timu zote 14 kupambana katika viwanja saba tofauti.

Mechi zote zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Ni jukumu la kamishna wa mechi husika kuhakikisha mchezo unaanza katika muda uliopangwa, vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom toleo la 2012.

Yanga ambayo tayari imeshatwaa ubingwa itakuwa mgeni wa Simba katika mechi namba 180 itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo mwamuzi atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro na Kamishna ni Emmanuel Kavenga wa Mbeya.

Mgambo Shooting vs African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mwamuzi ni Amon Paul wa Mara wakati Kamishna ni Ally Mkomwa kutoka Pwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Mwamuzi ni Israel Mujuni wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Salum Kikwamba kutoka Kilimanjaro).

Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mwamuzi ni Ibrahim Kidiwa wa Tanga wakati Kamishna ni John Kiteve kutoka Iringa), Oljoro JKT vs Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha. Mwamuzi ni Athuman Lazi wa Morogoro wakati Kamishna ni Juma Mgunda kutoka Tanga).

Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro utatumika kwa mechi kati ya Polisi Morogoro na Coastal Union ya Tanga ambapo Mwamuzi atakuwa Said Ndege wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Hakim Byemba kutoka Dodoma. Toto Africans itacheza na Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mwamuzi ni Geoffrey Tumaini kutoka Dar es Salaam na Kamishna ni Josephat Magazi wa Singida.

MECHI ZA MARUDIANO RCL WIKIENDI HII
Mechi za marudiano za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zinachezwa wikiendi hii katika viwanja kumi tofauti wakati mechi ya Flamingo ya Arusha na Machava FC ya Kilimanjaro yenyewe itachezwa Jumatatu (Mei 20 mwaka huu).

Uamuzi wa mechi hiyo kuchezwa Jumatatu ni kutokana na Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid kutumika kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kesho wakati Jumapili utatumika kwa shughuli nyingine za kijamii kwa mujibu wa wamiliki wa uwanja huo (CCM Mkoa wa Arusha).

Mechi nyingine zitachezwa keshokutwa (Jumapili) ambapo Abajalo watakuwa wenyeji wa Red Coast kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara utatumika kwa mechi kati ya wenyeji Coast United na Kariakoo ya Lindi.

African Sports ya Tanga itaoneshana kazi na Techfort ya Ifakara mkoani Morogoro katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani. Nayo Simiyu United ya Simiyu itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida.

Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ndiyo utakaotumika kuzikutanisha timu za Polisi Jamii Bunda kutoka Mara na wenyeji UDC wakati Biharamulo FC ya Kagera na Polisi SC ya Geita zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Milambo FC ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Saigon FC ya Kigoma kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora huku Mbinga United ya Ruvuma ikiikaribisha Njombe Mji ya Njombe kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa utatumika kwa mechi kati ya wenyeji 841 KJ dhidi ya Kimondo SC kutoka Mbeya. Nazo Rukwa United na Katavi Warriors zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya pili zitacheza mechi zao za kwanza kati ya Mei 25 na 26 mwaka huu wakati mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

PICHA YA SIKU: WOTE WAMESTAAFU KASORO BABU GIGGSMABAO BORA YA DAVID BECKHAM YAKIWEMO 85 ALIYOIFUNGIA MANCHESTER UNITED

VIDEO: DAVID BECKHAM AKIHOJIWA NA GARY NEVILLE KUTANGAZA UAMUZI WAKE WA KUSTAAFU

Thursday, May 16, 2013

EXCLUSIVE: SIMBA NA YANGA - BILA MILLIONI 100 HATUTAKI MECHI YETU IONYESHWE NA KITUO CHOCHOTE CHA TV

Wakati ikiwa imebaki siku moja kabla ya mtanange wa tani wa jadi Simba na Yanga kufanyika huku kukiwa na taarifa kwamba mchezo huo unaweza kuonyeshwa kwenye moja ya kituo cha TV, leo hii viongozi wa klabu hizo mbili wamezungumza exclusively na mtandao huu kuhusiana na mchezo wa timu zao kurushwa moja kwa moja na kituo chochote cha Television.

Awali shirikisho la soka nchini kwa pamoja na kituo cha SuperSport cha Afrika Kusini lilikuwa na utaratibu wa kile kilichoitwa SUPER WEEK ambapo baadhi ya mechi hizo zingeonyeshwa live kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lengo la SuperSport la kuonyesha mechi hizo live ni ‘kuipromoti’ ligi ya Tanzania na wachezaji wake ili waweze kupata kuonekana na watu wengine na kuingia katika biashara nzuri ya soka. 


Lakini viongozi wa vilabu vya ligi kuu waligoma mechi hizo kuonyeshwa bila wao kupata malipo hivyo mpango huo ukafa bila majibu ya kujitosheleza.

Lakini leo zimeibuka taarifa kwamba kituo hicho na shirikisho wapo katika hatua za kutaka mechi hiyo ya watani wa jadi ionyeshwe live.

Wakiongea na mtandao huu Ktibu Mkuu wa Simba Mtawala na makamu mwenyekiti wa Clement Sanga walisema: "Ikiwa kama  kama kuna mpango huo TFF wakae watambue kwamba hatutokubali mechi yetu ionyeshwe bure. Ni wakati sasa tupate kile tunachostahili sio kuwaingizia watu wengine fedha wasizostahili. Tamko letu la pamoja tunasema kwamba ikiwa kuna kituo chochote kinachotaka kurusha mechi yetu basi kitoe Millioni 100 - millioni 50 kwa kila timu na si vinginevyo. Ikiwa hakuna atakayeweza kufikia kulipa fedha hizo basi mechi yetu haitoonyeshwa na kituo chochote cha TV."

BAADA YA FERGIE NA SCHOLES - DAVID BECKHAM NAE ATANGAZA KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU

Kustaafu ndio habari iliyoshika hatamu nchini Uingereza hiv sasa - wiki moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo hii mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa England DAVID BECKHAM ametangaza kutundika daluga.

Beckham, 38, ameisadia Paris Saint-Germain kubeba kombe la  Ligue 1 kwa mara ya kwanza ndani miaka 19 mwishoni mwa wiki hii.
Pamoja na kupewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa, mkongwe huyo atastaafu baada ya mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huuA.
Alisema: “Shukrani sana kwa PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa hapa lakini sasa nadhani ni muda sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka la kiwango cha juu
Becks alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid.
Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer.

MAKALA: UTITIRI WA TIMU ZA JESHI LIGI KUU UTAZAMWE UPYA - FIFA HAIZITAKI KAMATI YA LIGI YAZILEA


KLABU mbili kongwe za Simba na Yanga ndizo zimetawala soka kwa miaka mingi na wapenzi nchini wamegawanyika katika timu hizo.
Shabiki wa soka anaweza kudai ni mpenzi wa Azam lakini ukweli ama yuko Simba au Yanga. Vile vile, atakayesema ni mpenzi wa Ashanti ndani kuna u-Simba au u-Yanga.
Pamoja na Simba na Yanga kuteka mashabiki wa soka nchini, klabu zinazomilikiwa na majeshi ndizo zinanogesha Ligi Kuu ya Bara inayomalizika keshokutwa. Ligi inashirikisha timu 14 msimu huu ambazo ni; JKT Oljoro, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Mgambo JKT, Prisons, Polisi Morogoro, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Azam FC, Simba, Yanga, African Lyon, Coastal Union na Toto African.

TIMU SITA ZA JESHI LIGI KUU, HAZIONYESHI USHINDANI LAKINI ZA WENZETU NI BALAA
JKT RUVU

Timu sita kati ya hizo zinamilikiwa na majeshi. Jeshi la Polisi lina (Polisi Morogoro) na Magereza (Prisons) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linamiliki nne ambazo ni JKT Oljoro, JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Mgambo JKT.
Kwa tathmini yangu, tofauti na timu za majeshi kutoka nchi nyingine za Afrika hasa kutoka Afrika Kaskazini na Magharibi, ushiriki wa timu za majeshi ya Tanzania ni wa wastani katika ligi kiasi cha kutoweka hamasa ya kutosha ya ushindani. Miaka yote zimekuwa zikishika nafasi za katikati.
Azam FC, klabu inayomilikiwa na kampuni ya S.S.Bakhressa safari hii ilishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo baada ya kuitoa Al Nasri Juba katika raundi ya awali ilikumbana na timu ya Barrack Young Controllers ya Liberia ambayo inamilikiwa na jeshi la nchi hiyo. Azam ilitoka jasho kuitoa timu hiyo kwa mabao 2-1 na kuvuka hatua hiyo.
Hatua iliyofuata Azam ikapangiwa timu nyingine ya jeshi ambayo ni Association Sportive des Forces Armées Royales yaani FAR Rabat ya Morocco. Ulikuwa muziki ‘mnene’. Azam ililazimishwa sare ya bila kufungana na kisha ikatolewa mjini Rabat kwa 2-1.
Ukitazama kwa haraka, utaona timu zinazomilikiwa na jeshi kutoka nchi za Morocco, Algeria, Misri na Libya si nyingi katika ligi husika na nguvu kubwa ya maandalizi inakuwa ya kutosha tofauti na hapa nchini. Hali ni tofauti nchini.
JKT ina timu nne katika ligi kuu, pia ina timu katika Ligi Daraja la Kwanza zinazopambana kupanda daraja huku Polisi ikiwa na timu moja na mlolongo wa timu za daraja la kwanza. Hata Prisons nayo ina timu katika madaraja ya chini.
Mtigwa Sugar na Kagera Sugar ni timu ndugu zote zinalikiwa na kampuni ya Superdoll Group of Companies. Ushiriki wa timu hizo si haba.
Mlolongo huu wa timu zinazomilikiwa na kampuni moja au jeshi moja au mfadhili mmoja, ndio unazifanya taasisi hizi za serikali kushindwa kupata huduma nzuri kutoka kwa wamiliki wake ili kuwa na ushiriki wenye tija katika michuano hiyo.
JKT haiwezi kuzihudumia ipasavyo timu zake kuhimili ushindani kutoka kwa timu zenye nguvu ya fedha kama Simba, Yanga na Azam.

FIFA HAIZITAKI TIMU HIZO, TFF, KAMATI YA LIGI YAZILEA

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeona tatizo hilo na limeagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liangalie uwezekano wa kupunguza utitiri huo ili zisiathiri matokeo.
Kwa mfano sasa Mgambo inahitaji pointi moja tu ili iweze kubaki ligi kuu, tazama imecheza mechi mbili dhidi ya Simba na Azam na kufungwa mechi zote kwa mabao 3-1 na 3-0.
Kamati ya Ligi imejitahidi kupanga ratiba mechi za mwisho timu ndugu zisikutane, lakini zilipokumbana zenyewe katikati ya ligi hali ilikuwaje. Mechi za mwisho Mgambo itamaliza na African Lyon, Toto itakwaana na Ruvu, JKT Ruvu na Mtibwa Sugar, Prisons na Kagera Sugar, JKT Oljoro na Azam na Polisi itakuwa mwenyeji wa Coastal Union.
Ofisa mmoja wa JKT anayeshughulikia michezo anasema hilo la kuwa na timu moja katika ligi na kuiandaa kikamilifu hata wao wameliona lakini vyama vya soka vya mikoa ndivyo vinavyozing’ang’ania timu zao.
“Kwa mfano ukitaka Oljoro uivunje, Chama cha Soka Arusha (ARFA) kitakwambia hakitaki na wanahitaji timu ya ligi kuu na ukitishia kutoihudumia watakwambia wapo tayari kuihudumia. Hata mikoa mingine hali ni hiyo hiyo.
“Timu hizi zinakuwa zetu zikiwa madaraja ya chini lakini zikifika madaraja ya juu vyama vya soka vinazing’ang’ania kuwa nazo. Hatuwezi kukataa kuwa na timu kwani michezo ni miongoni mwa vitu tunavyovipa kipaumbele jeshini,” anasema ofisa huyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia anasema; “Ni kweli hizo timu zipo na hata Fifa hairuhusu timu mbili zinazomilikiwa na taaasisi moja kushiriki ligi kuu.”
“Kutokana na mazingira yetu ya soka hasa suala la kiuchumi, sisi tumeruhusu timu hizo kucheza ligi lakini tukiziangalia kwa karibu huku tukibana mazingira ya kupanga matokeo kuanzia katika ratiba na mambo mengine,” anasema.
Ligi Kuu ya Bara inafikia tamati keshokutwa Jumamosi huku Yanga itakayokwaana na Simba ikiwa imeshatwaa ubingwa baada ya kujikusanyia pointi 57.
MAKALA HII IMECHOTWA KATIKA GAZETI LA MAWIO IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI

SIMBA VS YANGA: - KUJIAMINI KUNAWEZA KUKAIGHARIMU YANGA DHIDI YA WATANI WAO WA JADI

GUMZO lililotawala medani ya soka nchini ni pambano la funga dimba ya Ligi Kuu ya Bara litakalowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo itafanyika huku Yanga ikiwa tayari imeshatwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 57 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki michuano hiyo. Mchezo huu utakuwa wa kulinda heshima tu kwani Simba haiwezi hata kutwaa nafasi ya pili.
Mashabiki wa Yanga wamejiaminisha kwamba mechi hiyo itakuwa ya kulipa kisasi cha kipigo cha mabao 5-0 ambacho ilikipata katika mechi ya mwisho msimu uliopita. Yanga wanajipa imani hiyo kutokana na mzozo ‘ulioko’ ndani ya Simba.
Siku chache baada ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hii, Simba haikuwa ikipata matokeo ya kuridhisha kiasi cha kutafuta mchawi. Uongozi ukawasimamisha wachezaji wake kadhaa kwa madai ya kuhujumu timu.
Wachezaji waliosimamishwa ni Haruna Moshi ‘Boban’, Felix Sunzu, Amir Maftah, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Paul Ngalema, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ na Abdallah Juma. Lakini baadaye Kazimoto na Sunzu walisamehewa na kurejeshwa kundini.
Baada ya kuwasimamisha wachezaji hao ikaanza kuwatumia vijana kama Haruna Chanongo, Christopher Edward, Abdallah Seseme, Ramadhan Singano ‘Messi’, William Lucian, Miraji Adam, Hassan Khatib na Jonas Mkude.

TAZAMA KINACHOITWA KIKOSI CHA WATOTO
Hivyo kikosi cha sasa cha Simba mara nyingi hujumuisha wachezaji; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa, Messi, Felix Sunzu, Mkude na Haruna Chanongo.
Mashabiki wa Yanga wanabeza wanakiita kikosi hicho cha watoto, hivyo wanajipa imani timu yao inaweza kuinuka na ushindi wa mabao mengi wakiwa na ndoto ya kurudisha mabao 5-0 waliyofungwa katika mechi kama hii mwaka jana.
Uchambuzi unaonyesha Simba haina watoto. Katika kikosi hicho kinachoitwa cha watoto, unaweza kuona wachezaji watatu tu chipukizi au wasio na majina makubwa ambao ni Messi, Mkude na Chanongo.
Wachezaji wanane waliobaki ambao ni Kaseja, Chollo, Shamte, Kapombe, Mudde, Kiemba, Ngassa na Sunzu, wote ni wazoefu na wanaoweza kubadili matokeo wakati wowote ule. Mbali ya wachezaji hao, Simba ina Kazimoto ambaye yuko kikosini japokuwa tangu arudishwe amecheza mechi chache.
Hata hao chipukizi watatu ambao kuna uwezekano mkubwa wakawepo kikosi cha kwanza cha Simba,  ni wazoefu kwani wapo katika kikosi hicho kwa msimu wa pili sasa. Kikosi hicho kinaweza kutoka sare na Yanga au hata kushinda.
Wachezaji wanaoweza kuihofia Yanga ni chipukizi ambao msimu huu wanaichezea kikosi cha kwanza cha Simba kwa mara ya kwanza wakiwemo Lucian, Miraji na Khatib ambao hata hivyo kuna uhakika mdogo mno wa wao kuwemo kikosi cha kwanza.

YANGA WAKIJIAMINI, WAMEISHA
Wakati Yanga wataingia uwanjani wakijiamini, Simba kwa upande wao wataingia dimbani kufanya mambo mawili; kwanza kuthibitisha uwezo wao, pili kuwatibulia Yanga ili washerehekee kukabidhiwa kombe na kichapo juu.
Tatizo kubwa la kikosi cha Simba kwa sasa linaweza kuwa ni saikolojia kwa wachezaji baada ya kukosa hata nafasi ya tatu; pia kutoelewana miongoni mwao. Hata kufanya vibaya kwa Simba katika mechi za kwanza za mzunguko huu, kulisababishwa zaidi na uongozi.
Simba ilifanya vibaya katika mechi zake za Kanda ya Ziwa, kwani ilikubali kipigo cha bao 1-0 na Kagera Sugar kisha  ikatoka sare ya mabao 2-2 na Toto African ya Mwanza. Huo ulikuwa wakati ambao baadhi ya wanachama wa timu hiyo walikuwa wakipambana kumtoa madarakani Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage.
Katika mzozo huo Makamu mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ akajiuzulu. Mwingine aliyejiuzulu ni mjumbe wa kamati ya utendaji na mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hanspope, lakini sasa amerudi kundini.
Ghafla ‘watoto’ wa Simba chini ya Mfaransa, Patrick Liewig wakaanza kutoa darasa, wakailambisha JKT Mgambo 3-1, huku Yanga ikitoka sare na Coastal Union katika mchezo wake wa mwisho kabla ya kuivaa Simba keshokutwa.
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts na benchi lote la ufundi la Yanga, wanapaswa kutoruhusu mawazo ya mashabiki na baadhi ya viongozi wanaoibeza Simba.
MAKALA HII IMECHOTWA KATIKA GAZETI LA MAWIO IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI

TANZANIA YAJIONDOA MICHUANO YA COSAFA BAADA YA RATIBA KUINGILIANA NA CHAN

Tanzania (Taifa Stars) imejitoa kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika nchini Zambia kuanzia Julai 2-26 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah amesema Stars ambayo iliingizwa katika michuano hiyo kama timu mwalikwa imejitoa kutokana na mwingiliano wa ratiba kati ya michuano hiyo na mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Amesema awali Tanzania ilithibitisha kushiriki michuano kwa matarajio kwamba Uganda ingekubali ombi la TFF la kubadilisha ratiba ya mechi za CHAN, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) likagoma kwa vile kipindi ambacho kilipendekezwa lenyewe litakuwa na uchaguzi wa viongozi wao.

Taifa Stars itacheza na Uganda (The Cranes) katika mechi za CHAN ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu wakati ya marudiano itafanyika jijini Kampala kati ya Julai 26-28 mwaka huu.

Akizungumzia michuano ya COSAFA, Kocha Kim amesema angependa kushiriki michuano hiyo kwani ingekuwa kipimo kizuri kwa kikosi chake, lakini kwa sasa malengo makubwa ya Stars kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo fainali zake zitafanyika mwaka 2015.

HARUNA CHANONGO WA SIMBA, ZAHORO PAZI WAITWA TIMU YA TAIFA VS MOROCCO

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.

Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.

Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.

Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;

Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar (Azam).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).

Kocha Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 ambapo Samata na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.

Awali TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya mashindano Juni 8 mwaka huu.

Kwa upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.

CLOUDS THE DREAM TEAM KESHO KUKIPIGA NA IFM UWANJA WA NYUMBANI TANGANYIKA PARKERS

The Dream team ya Clouds FM kesho itadondoka kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Tanganyika Parkers kukipiga na timu ya chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM kuanzia majira ya saa 10 jioni.

SIKU KAMA YA LEO MWAKA 2012: PATRICK MAFISANGO ALIPOTEZA MAISHA YAKE KWA AJALI YA GARIHILI NDIO GOLI LA MWISHO KUFUNGWA NA MAFISANGO WAKATI WA UHAI WAKE


Tarehe kama ya leo mwezi wa tano mwaka 2012, klanu ya ya Simba ilimpoteza kiungo wao wa kutumainiwa Patrick Mafisango Mutesa aliyepata ajali ya gari maeneo ya Tazara wakati akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na kwa bahati mbaya gari lake likakosa balance na kuingia mtaroni na hapo ndipo alipopeteza maisha.

CHELSEA WAWEKA HISTORIA YA KUBEBA UEFA CHAMPIONS LEAGUE NA EUROPA LEAGUE MFULULIZO


Benfica 1 Vs 2 Chelsea Final Europa League 15... by f100000904719795

Wednesday, May 15, 2013

MAALUM KWA MASHABIKI WA MAN UNITED: KAMPENI YA KUICHANGIA MAN UNITED FEDHA ZA KUMRUDISHA CRISTIANO RONALDO YAANZISHWA


Baada ya kuwa na wiki mbaya ya kuwaaga wapendwa wao kwenye klabu yao Sir Alex Ferguson na Paul Scholes, washabiki wa Manchester United wanaweza wakawa wanamkaribisha kipenzi chao Cristiano Ronaldo - ikiwa wao wenyewe wataweza kupata fedha za kumrudisha kutoka Real Madrid.

Kundi la mashabiki wa klabu hiyo kutoka Australia wametengeneza mtandao ambao mashabiki wa United wataweza kuchangia fedha za kuweza kumnunua mchezaji huyo kutoka Real Madrid, Ronaldo ana kiengele ambacho kimemuwekea thamani ya paundi millioni 100 kwa timu yoyote inayomtaka.

Harakati za mtandao wa 'BringRonaldoHome' zimeanza kuzaa matunda baada ya mashabiki maelfu kutuma maombi ya kununua jezi yenye jina la Ronaldo - lakini ili kampeni kufanikiwa inatakiwa wachangiaji millioni 10 watoa kiasi cha £10 kila mmoja ili kutimiza lengo.

Kwa kuwa United wanaripotiwa kuwa na mashabiki mil. 659 duniani kote, kufikisha £100 litakuwa jambo rahisi. 

Kampeni hiyo ya kumrudisha Ronaldo OT imezinduliwa siku 3 zilizopita, huku video kibao za mashabiki wa United wakihamasishana zikifurika kwenye mitandao ya facebook na Twitter. 

Fedha zitakazopatikana kupitia mtandao huo zitapelekwa kwa United kwa masharti - kuwawezesha kutumia fedha hizo za mchango wa mashabiki kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid. 

Ikiwa United watafanikiwa kumrudisha Ronaldo basi fedha zote zilizopatikana kupitia mtandao huo basi mashabiki wote waliochangia watatumiwa jezi zenye jina la Ronaldo - na ikiwa itashindikana kumrudisha CR7 Old Trafford basi kila aliyechangia atarudishiwa fedha zake. 
Mashabiki wanaweza kuchangia kupitia  www.bringronaldohome.org/

KITABU CHA MWAKALEBELA KUUZWA KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI

Na Mwandishi Wetu
KITABU cha kwanza nchini kinachozungumzia soka la Tanzania kijulikanacho kwa jina la “Soka la Tanzania” kitaanza kuuzwa siku ya mechi ya watani wa Jadi, Yanga na Simba iliyopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa.
Akizungumza na jijini jana, mtunzi wa kitabu hicho, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na yamedhaminiwa  na kampuni TSN Group kupitia kinywaji chake cha kuongeza nguvu Chilly Willy, Events World, Vannedrick Tanzania Limited na  Inbox Pub.
Wadhamini wengine ni Clouds FM, Times FM na Street Soul kwa mujibu wa Mwakalebela. Alisema kuwa kwa sasa ametoa nakala 10,000 kwa ajili ya kuuzwa Tanzania nzima. Alisema kuwa kitabu hicho kimezungumzia historia ya soka la Tanzania katika Nyanja za vijana, wanawake na wanaume, ligi kuu ya Tanzania Bara, Taifa Cup, Timu ya Taifa na Utawala Bora.
Mbali ya hayo, kitabu hicho kimezungumzia ujio wa kocha Marcio Maximo, mchango wa serikali katika kuinua mpira wa miguu, wadhamini, uhusiano kati ya waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira wa miguu Tanzania.
“Pia nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar Tenga kwa kipindi cha miaka mine nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka kwa makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa kwanza  Juni 15, 2006,” alisema Mwakalebela.
Alisema kuwa kitabu hichi ni muhimu sana kwa wana-habari, wachezaji, makocha, waamuzi na wadau wengine wa mchezo huo kwani kuna kumbukumbu zote za mechi za timu ya Taifa ikiwa mabao ya kufunga, wafungaji, vikosi tofauti vya timu za taifa na mambo mengine.

EUROPA LEAGUE FINAL: CHELSEA VS BENFICA - THE BLUES KUWEKA REKODI YA KUBEBA CHAMPIONS LEAGUE NA EUROPA LEAGUE MFULULIZO

Haijawa kutokea timu kuchukua ubingwa wa UEFA Champions League kisha kuchukua Europa League mfululizo, lakini hii ni rekodi ambayo Chelsea anaweza wakaiweka leo hii watakapocheza fainali ya Europa League na Benfica jijini Amsterdam Uholanzi. Katika kuelekea kwenye fainali hiyo tuangalie mambo muhimu kuhusu timu hizi mbili.

SAFARI YA TIMU ZOTE MPAKA KUFIKA FAINALI

Benfica
Ilishinda 1-0 vs Bayer Leverkusen
Ilishinda 2-1 vs Bayern Leverkusen
Ilishinda 1-0 vs  Bordeaux
Ilishinda 3-2 vs Bordeaux
Ilishinda 3-1 vs  Newcastle
Sare 1-1 vs Newcastle
Lost 1-0 vs Fenerbahce
Won 3-1 vs Fenerbahce

Chelsea
Ilishinda 1-0 vs Sparta Prague
Sare 1-1 @Stamford Bridge vs Sparta Prague
Walifungwa 1-0 vs Steaua Bucharest
Wakashinda 3-1 @Stamford Bridge Steaua Bucharest
Walishinda 3-1 Rubin Kazan
Wakafungwa 3-2 @Stamford Bridge vs Rubin Kazan
Walishinda 2-1 vs Basel
Wakashinda 3-1 @Stamford Bridge vs Basel
  
 

TAARIFA ZA TIMU

Benfica manager Jorge Jesus ana majeruhi mpya kwenye timu kuelekea fainali ya leo, ingawa mlinzi wa kulia Maxi Pereira amesimamishwa kwa kuwa na kadi za njano nyingi na hatocheza mchezo wa leo.
Chelsea boss Rafael Benitez tayari ameshathibitisha Eden Hazard hatocheza mechi ya leo na pia kuna wasiwasi kuhusu hatma ya John Terry.


BENFICA ITASHINDA IKIWA

Benfica wamefunga mabao 14 kwenye hatua za mtoano za Europa League, mabao sita yamefungwa na Oscar Cardozo.
Mparaguay huyo atakuwa miwba mchungu ikiwa atakuwa anapokea mipira mizuri kutoka kwa viungo wake, ingawa pia kuna hatari nyingine kwa Chelsea kutoka kwa Gaitan, Lima na Eduardo Salvio.
Katika safu ya ulinzi Benfica itabidi wacheze vizuri zaidi kuliko ilivyokuwa kwa Basel katika kuweza kuzuzia mashambulizi ya Chelsea - yenye watu hatari wanaoelewana kama Oscar, Juan Mata na Moses atakayechukua nafasi ya Hazard.

Fernando Torres anaweza kawa ndio mfungaji bora wa Chelsea kwenye michuano hii, lakini tishio la  Moses, Oscar na Juan Mata ambao watacheza nyuma yake ndio wakaisumbua sana safu ya ulinzi ya Benfica - na ikiwa Benfica wataweza kucheza vizuri dhidi watatu hao basi watakuwa wamejirahisishia kazi kwenye mchezo huo.

 CHELSEA ITASHINDA IKIWA
Inaonekana kama Chelsea wameweza kufika mpaka fainali lakini jasho haliwakuvuja la kutosha.
Ndio, kuna wakati walipata shida (hasa dhidi ya Rubin Kazan), lakini bado hawakuonekana kujali sana kuhusu kombe hili. na njia pekee ya kuweza kuwashinda Benfica walio kwenye bora kabisa itabidi wavuje jasho kweli kweli na kuweka umakini wao vizuri kwenye mechi ya leo.

Hazard, hatocheza leo, hivyo Mosses ambaye hutumia nguvu zaidi atachukua nafasi yake. Huku David Luiz akitarajiwa kucheza kwenye kiungo, hivyo The Blues watakuwa wapo vizuri kwenye ulinzi kiasi.

Wakati viungo wa Chelsea wanaokuwa kwenye kiwango chao, ni vigumu sana kushindana nao, ingawa mara nyingi inakuwa tatizo wanapocheza mabeki wa ulinzi imara na wenye kuelewana kama Luisao na Ezequiel Garay.
Gary Cahill na Branislav Ivanovic pia watakuwa na kazi ya kuhakikisha kijana wa kiparaguay na hatari Oscar Cardozo hakutani uso kwa uso na Peter Cech na kuwadhuru - Cordozo na hatari kwenye mipira hivyo itabidi wasimame nae kama wamegandanishwa nae na gundi.

 VIKOSI VINAVYOTARAJIWA

Benfica XI: Artur; Almeida, Garay, Luisao, Melgarejo; Matic, Perez; Salvio, Lima, Gaitan; Cardozo

 Chelsea XI: Cech; Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole; Ramires, David Luiz; Oscar, Mata, Moses; Torres

MSIMU MPYA WA THE LEGEND IS BACK!

Msimu mpya wa the legend is back , unaokwenda kwa jina la NIGHT OF THE LEGENDS au USIKU WA MALENGEDARI unaofanyika kila jumamosi katika ukumbi mpya ISUMBA LOUNGE zamani jollys club, wadau wote hasa wapenda burudani na mashabiki wa JOHN DILLINGA mnakaribishwa.