Search This Blog

Saturday, October 1, 2011

KOCHA WA AZAM AWAONYA WAGHANA


Kocha wa Azam FC, Stewart Hall amewatetea Waghana Nafiu Awudu na Wahabu Yahya akisema kwamba bado kabisa hawajaimudu Ligi Kuu Bara wala hawastahili lawama lakini akakiri atawaangalia mpaka wakati wa dirisha dogo.

Azam ilisajiliwa Waghana hao ambao wamo katika kikosi cha vijana cha timu ya taifa ya Ghana U-23 kutoka klabu ya Kings Faisal wakaungana na kipa Mserbia Obren Curkovic, Muivory Coast Kipre Tchetche na Mkenya Ibrahim Shikanda.

Katika mechi zake, Stewart amekuwa hawatumii wachezaji hao wa kigeni akiwemo Nafiu ambaye ni beki wa kati aliyefanikiwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Moro United waliyoshinda bao 1-0 na baada ya hapo akaanza kumtumia Said Morad ambaye ni Mtanzania.

Wahabu anayecheza kama straika amemtumia dakika za mwishoni kwa mechi ya Moro United na African Lyon na kwa mara ya kwanza alimwanzisha mechi iliyopita dhidi Coastal Union, Tanga aliyocheza dakika 70 akatoka kumpisha Zahoro Pazzi.

Kocha huyo alisema; "Kulingana na mechi nilizowatumia, Waghana hawako sawa, ligi imekuwa ngumu kwao, hawaendani na kasi ya wengine, lakini naendelea kuwaangalia dirisha dogo nitakuwa nimepata jibu kamili."

"Wahab nilikuwa namtumia kama wa akiba, mechi iliyopita nilimwanzisha, lakini sikuona mabadiliko kwa hiyo siwezi kumchezesha kama hayuko sawa na wenzake kama ilivyo kwa Nafiu,alisema Stewart ambaye anaondoka Novemba kwenda Zanzibar kuinoa Zanzibar Heroes itakayokuwa ikijiandaa na mashindano ya Kombe la Chalenji.

Akimzungumzia Obren aliyedaka mechi tatu ambazo ni Moro United, African Lyon na JKT Oljoro alisema: Obren aliumia kiganja cha mkono kama mwezi, akawa amejitonesha naendelea kumwangalia.Kipre ni mgonjwa pia,

lakini hadi mechi ijayo atakuwa amepona kabisa na Shikanda ni hali ya mchezo, kulingana na ushindani wa namba, alisisitiza Stewart raia wa Uingereza ambaye habari za chini ya kapeti zinasema huenda akasitisha mikataba ya wachezaji wawili wa kigeni na kuziba nafasi zao na tayari ameshaueleza uongozi kuhusu hilo.

VITA YA NAMBA KWENYE KIUNGO CHA SIMBA NI BALAA-KAZIMOTO AANZA MAZOEZI


Vita kubwa inanukia baina ya wachezaji hao wanne wa safu ya kiungo ya Simba ambao kila mmoja ni bandika bandua na Kocha Moses Basena atakuwa katika mtihani mkubwa wa kuchagua wachezaji wawili wa kutawala katikati.

Simba ambayo inaongoza ligi kwa pointi 18, ilikuwa ikiwatumia wachezaji wawili wa kigeni mara nyingi katika safu ya ulinzi ambao ni Mkenya Jerry Santo na Patrick Mafisango wa Rwanda lakini sasa kazi imekuwa tete.

Shomari Kapombe ambaye amecheza mechi ya mwisho dhidi Mtibwa na kufanya mambo makubwa kwenye kiungo alipochukua nafasi ya Mafisango ambaye hakuchezeshwa kabisa kwenye mchezo huo amemchizisha kabisa Basena.

Lakini kama hiyo haitoshi kiungo mahiri wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto naye ameanza mazoezi na ameonekana kuwa fiti na kumvutia zaidi Basena ambae habari za ndani kutoka kwenye benchi la ufundi zinadai anafikiria kuwachezesha Mwinyi na Kapombe kwenye kiungo kutokana na kuvutiwa na tabia, kujituma na uwezo wao.

Hiyo inamaanisha kwamba Mafisango na Santo watakuwa kwenye wakati mgumu utakaozidisha ushindani kwenye safu ya kiungo ya Wekundu wa Msimbazi ambao wachezaji kama Haruna Moshi, Ulimboka Mwakingwe, Amri Kiemba na Shija Mkina nao wanaweza kuicheza lakini huchezeshwa safu zingine hasa za winga.

Basena alisema kuwa kurejea kwa Kazimoto ni changamoto kubwa kwa Simba lakini akakiri kwamba hakuna mchezaji wa kiungo aliyeko fiti na anamkosha kwa sasa kama Kapombe.

Kauli ambayo inamaanisha Mafisango ambaye hivi karibuni alisimamishwa kwa madai ya utovu wa nidhamu atakuwa kwenye wakati mgumu na huenda akapewa nafasi ya kudumu kwa muda kwenye benchi.

Friday, September 30, 2011

VODACOM PREMIER LEAGUE STATISTICS


Wakati mechi za Simba, Yanga na Azam FC ikiwa imesimama kupisha michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki mataifa ya Africa mwakani nchini Gabon na Equatorial Guniea. Si vibaya kupata takwimu mbalimbali za ligi hiyo msimu huo.

MSIMAMO WA LIGI.

Simba SC ndio inaongoza ligi wakiwa na point 18 wakifuatiwa na Azam FC wenye point 15, wakati Yanga ikiwa nafasi ya 6 wakiwa na pointi 12. Coastal union ndio wa Mwisho wakiwa na point 4 wakifuatiwa na Villa squad wenye point 5 baada ya kucheza michezo 8.

MSIMAMO WA WAFUNGAJI.

Mshambuliaji wa Moro United Gaudence Mwaikimba pamoja na wa Azam FC John Bocco wanaongoza kwa kufumania nyavu wakiwa wameziona mara 5. Wakifuatiwa na kiungo toka Rwanda anaecheza Simba Patrick Mafisango mwenye magoli 4.

Mfungaji bora wa msimu uliopita Mrisho Khalfani Ngassa Bado hajaziona nyavu baada ya kupata nafasi ya kuteremka uwanjani mara 6 akicheza kwa dakika zaidi ya 500.

MORADI NA AGREY NI ZAIDI YA COSTA NA NYOSO.

Safu ya ulinzi wa Azam FC ndio ya safu imara zaidi baada ya kuruhusu magoli 2 katika michezo nane. Safu hiyo iko chini ya nahodha Agrey Morris na Said Moradi wakati ile ya Simba inayoongozwa na Nyosso na Victor Costa ikiruhusu magoli 4.

Kipa Mwadini Ally wa Azam FC ndie kipa pekee ambayo ajafungwa baada ya kuonekana uwanja katika michezo mitano katika ya 8 timu yake iliyo cheza.

Wakati Moro Utd na Villa Squad zinaongoza kwa kufungwa mabao mengi, Moro imeruhusu mabao 15, wakati Villa imefungwa 13 katika michezo minane iliyocheza kwenye ligi hiyo.

JKT RUVU NA SIMBA HAWAFUNGWA.

Timu ya Simba na JKT Ruvu hawajapoteza mchezo wowote kati ya 8 waliyocheza. Simba SC imeshinda michezo mitano na kutoka sare mitatu, wakati JKT Ruvu wameshinda miwili na kutoa sare michezo 6 kati ya nane waliyocheza.

Azam FC na Jkt Oljoro wamepoteza mchezo mmoja wakati Coastal union wakiwa kinara kwa kupoteza mchezo, baada ya kupoteza michezo 6.

KADI ZILIZOTOKA.

Ikiwa michezo 55 imeshachezwa mpaka sasa jumla ya kadi 223 zimetoka, huku kadi nyekundu zikiwa 15 na njano 208. Simba, Villa Squad, Kagera Sugar na Toto African zimeibuka vinara kwa kadi nyekundu na njano.

Villa imeibuka kinara wa kadi za njano baada ya kumiliki kadi hizo 20, Simba 19 na Toto African 18 huku ikiwa kadi 208 zimeshatolewa na waamuzi wa ligi hiyo kwa michezo 55 iliyochezwa sawa na uwiano wa kadi tatu kila mechi.

Kagera Sugar imeibuka kinara wa kadi nyekundu baada ya kumiliki kadi hizo tatu kati 15 zilizotolewa na waamuzi kwa michezo yake minane iliyocheza.

YANGA NA SAFU KALI YA USHAMBULIAJI.

Yanga ina safu kali ya ushambuliaji baada ya kutikisa nyavu za wapinzani mara 13 ikifuatwa na Moro United iliyotikisa nyavu mara 12 katika michezo 8 waliyocheza. Huku jumla ya magoli 108 yakiwa yamefungwa ndani ya michezo 55 ya Ligi Kuu.

Costal union ina safu butu baada ya kufunga magoli manne 4 katika michezo 8 waliyocheza ikifuatiwa na Villa squad waliotikisa nyavu mara 5.

Azam FC msimu huu safu yake ya ushambuliaji iliyosajiliwa kwa mamillion imeshindwa kutamba baada ya kuingia kwenye nyavu mara 6.

LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA

Wakati Ligi Daraja la Kwanza imepangwa kuanza Oktoba 15 mwaka huu, klabu saba kati ya 18 bado hazijalipa ada ili timu zao ziweze kushiriki katika ligi hiyo iliyogawanywa katika makundi matatu. Klabu ambazo hazijalipa ada ya kushiriki ya sh. 200,000 ni AFC ya Arusha, Majimaji ya Ruvuma, Polisi ya Iringa, Polisi ya Tabora, Rhino Rangers ya Tabora, Small Kids ya Rukwa na Transit Camp ya Dar es Salaam. Mwisho wa kuwasilisha usajili wa wachezaji na kulipa ada ya ushiriki ni Oktoba Mosi mwaka huu. Klabu ya Burkina Faso ya Morogoro imelipa nusu ya ada ya ushiriki ambapo imetakiwa kumaliza kiasi kilichobaki ifikapo Oktoba Mosi mwaka huu. Vilevile kuna klabu tatu ambazo bado hazijawasilisha usajili wa wachezaji wa timu zao kwa ajili ya ligi hiyo. Klabu hizo ni AFC ya Arusha, Morani ya Manyara na Temeke United ya Dar es Salaam. Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakutana Oktoba 2 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine itaidhinisha timu zilizokidhi kanuni za kucheza ligi hiyo ili Kurugenzi ya Mashindano ya TFF ipange ratiba ya ligi hiyo. Timu 18 za Ligi Daraja la Kwanza ni Burkina Faso, Mgambo Shooting ya Tanga, Morani, Polisi ya Dar es Salaam, Temeke United na Transit Camp ambazo ziko kundi A. Kundi B lina timu za Majimaji, Mbeya City Council, Mlale JKT ya Ruvuma, Polisi ya Iringa, Small Kids na Tanzania Prisons ya Mbeya. Kundi C lina timu za AFC, Polisi ya Morogoro, Polisi ya Tabora, Rhino Rangers na Samaria ya Singida.
Boniface Wambura
Ofisa Habari

Gidamis Shahanga- WC Helsinki 1983 10,000m final

Mtanzania Gidamis Shahanga alifanya balaa kwenye mashindano ya dunia mbio za mita 10,000 huko Helsinki nchini Finland.






DEWJI:POULSEN HANA JIPYA TAIFA STARS


MFANYABIASHARA na mwanamichezo maarufu nchini, Azim Dewji amesema kuwa, kamwe haafikiani na utetezi unaotolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah anayedai Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen hawezi kufukuzwa kwa sababu ana mkataba wa miaka miwili.

Dewji aliyewahi kuifadhili Simba na kuipa mafanikio makubwa Afrika, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, wadau wana nafasi kubwa katika ustawi wa soka ya Tanzania, hivyo wasipuuzwe kwa majibu ya juu juu.


Alisema: “Nimesoma taarifa inayomnukuu Katibu Mkuu wa TFF kwamba Poulsen hawezi kutimuliwa kwa sababu ana mkataba wa miaka miwili, tena kwa sababu ya maoni ya wadau.


“Binafsi nasema hii si sahihi. Kocha anapimwa kwa vigezo vingi, lakini kama ameshindwa kazi na haoneshi dalili za kuelekea kufanikiwa, kwanini aendelee kuachwa kazini? Nahisi Angetile amepotoka na kamwe siafiki utetezi wake.”


Dewji aliongeza kuwa, kocha huyo raia wa Denmark alipaswa kuifanyia mapinduzi ya soka Stars, lakini anashangazwa kuona kila kukicha akifanya sawa na waliomtangulia, kuita kikosi kwa ajili ya mechi fulani huku akiwatumia wachezaji `wazee’ badala ya kuibua na kulea vipaji vipya kwa ustawi wa soka katika miaka ijayo.


“Hakuna jipya na wadau wanakata tamaa, ndiyo maana wanatoa ushauri kwa sababu wanaipenda timu yao.


Wakiendelea kukatishwa tamaa, nani atakwenda uwanjani na TFF itapata wapi fedha?


Ni vyema wakalitafakari hili, kwani tunashuhudia makocha wenye mikataba wakiachishwa kazi baada ya kushindwa kukata kiu ya waajiri wao,” alisema Dewji.


Osiah, jana alikaririwa na vyombo vya habari akimtetea Poulsen baada ya wadau mbalimbali wa michezo nchini kuhoji uhalali wa kocha huyo kuendelea kutafuna fedha za Watanzania, ilhali haoneshi mwelekeo wowote, zaidi ya kuporomosha kiwango cha wachezaji wa Taifa Stars.


Miongoni mwa wadau hao ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu aliyeonesha hofu ya Tanzania kutonufaika na lolote kutoka kwa kocha Poulsen.


Akizungumza na waandishi wa habari za michezo juzi, Osiah alisema: “Tunaheshimu maoni ya wadau wetu, akiwamo Mbunge Mangungu (Murtaza), ila lazima tuelewe kuwa Poulsen yupo kisheria na mkataba wake ni wa miaka miwili, hivyo hatuwezi kumuacha kwa mtindo wanaoutaka wao.


Poulsen aliyetua nchini kuirithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo mwaka 2010, hajapata mafanikio makubwa akiwa na kikosi cha Stars, ukiondoa `ngekewa’ ya kutwaa Kombe la Challenge, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994.


Ilishinda kwa `matuta’ kuanzia hatua ya makundi hadi fainali. Na hata baada ya kuingia katika michuano ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2012 na ile ya Kombe la Dunia mwaka 2014, Stars imeendelea kuwa ile ile ya kubahatisha uwanjani, hali inayompa wakati mgumu Poulsen aliyewabwaga wenzake watano katika mchujo wa mwisho wa kundi la makocha 59 waliokuwa wameomba kumrithi Maximo.

TIMBE: TEGETE NA KADO WANAKAA BENCHI KWA SABABU YA VIWANGO VIBOVU




Mapigo ya moyo ya kocha wa Yanga, Sam Timbe yameanza kurudi katika hali yake ya kawaida na sura furaha ikionekana tena baada ya ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Coastal Union.

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa juzi Timbe ambaye alikuwa hapendi kuzungumza na vyombo vya habari kutokana na timu yake kuanza vibaya aliwasifia nyota wake kwa kuonyesha kiwango cha juu huku akiweka wazi kwamba kiwango kibovu cha Jerryson Tegete na kipa Shabaan Kado ndicho kinachowanyima namba.


Uwezo wa mkubwa ulionyeshwa na Shamte Ally na Idrisa Rashid katika michezo miwili iliyopita umekuwa ni faraja kubwa kwa Mganda huyo.Tangu Timbe alipoanza kuwatumia katika mchezo dhidi ya African Lyon, Villa Squad na Coastal Union wachezaji hao wameonyesha uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga zilizowawezesha mabingwa hao kufunga mabao kumi tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

Akizungumzia uwezo wa wachezaji hao, Timbe alisema anafarijika sana kuona vijana hao wapo katika kiwango kizuri hivi sasa jambo linalompa matumaini makubwa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi wakishirikiana na wachezaji wengine wa kikosi chake."Katika mechi tatu ambazo vijana hao wamecheza kwa hakika wameonyesha uwezo mkubwa na wamekuwa wakishirikiana vizuri na wenzao katika kuhakikisha tunapata ushindi," alisema Timbe.

Pamoja na kusifia nyota hao Timbe alisema sababu ya kutompanga Tegete na kipa Kado ni kutokana na kutoonyesha viwango vya kuridhisha wakati wa mazoezi na kusisitiza anapanga kikosi kutokana na uwezo wa mchezaji.Timbe ambaye anaondoka leo kuelekea nchini Uganda kwa mapumziko mafupi alisema haoni sababu ya kuwapanga wachezaji waliokuwa kwenye kiwango cha chini katika kipindi hiki ambacho timu yao bado ina deni kubwa kwa mashabiki.
Awali Kado alikuwa mgonjwa wa kidole, lakini tayari amerejea katika hali yake kiafya na kujiunga na wenzake mazoezini, kwa mujibu wa kocha huyo mchezaji huyo bado hajarudi katika kiwango chake cha awali.


"Napanga timu kwa kuangalia uwezo wa mchezaji, siwezi kumpanga Tegete au Kado wakati kuna wachezaji wanaofanya vizuri zaidi yao, ninapokuwa nao mazoezini ndio napata muda wa kufahamu yupi aanze na yupi abaki hiyo ndiyo sababu yangu ya msingi,"alisema kocha huyo.

Timbe alisema timu yake hivi sasa ipo katika kiwango kizuri isipokuwa kuna baadhi ya mapungufu hususani kwenye safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikifanya makosa mara kwa mara.

Alisema jukumu la kuhakikisha safu hiyo inakuwa imara zaidi lipo mikononi mwake na ameahidi kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo ili kuhakiksha timu hiyo inaendelea kufanya vizuri katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu

Thursday, September 29, 2011

YANGA, COASTAL ZAINGIZA MIL 29/-


Mechi namba 51 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa Septemba 28 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 29,146,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 7,982 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 rangi ya chungwa, sh. 7,000 kwa VIP C, sh. 10,000 kwa VIP B na sh. 15,000 kwa VIP A.
Eneo lililoingiza watazamaji wengi ni kwenye viti vya bluu na kijani ambapo waliingia 6,760 wakati lililoingiza watazamaji wachache ni la VIP A ambapo waliingia 27.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo ambazo ni sh. 10,606,400 na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,446,000 kila klabu ilipata sh. 4,228,080.
Mgawo mwingine ulikwenda kwa gharama za mchezo (sh. 1,409,360), uwanja (sh. 1,409,360), TFF (sh. 1,409,360), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 704,680), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 563,744) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 140,936).
MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI
Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) umefanyika leo (Septemba 29 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Watanzania wanane walijisajili kwa ajili ya kufanya mtihani huo. Watano kati ya hao ndiyo wamejitokeza na kufanya mtihani huo ambao ulikuwa na sehemu mbili. Maswali kutoka FIFA na mengine kutoka TFF.
Walioomba uwakala na kufanya mtihani huo ni Adam Kapama, Aziz Sharif, Dk. Cyprian Maro, Florian Kaijage na Valence Mayenga. Mtihani mwingine wa uwakala utafanyika Machi mwakani.
Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.
Boniface Wambura
Ofisa Habari

SALUM MACHAKU AONDOLEWA POP, SUNZU KURUDI DIMBANI


SIMBA imepata matumaini ya kuendelea kufanya vema katika Ligi Kuu soka Tanzania Bara, baada ya nyota wake waliokuwa majeruhi akiwemo kiungo mshambuliaji, Salum Machaku, kutolewa plasta ngumu (POP).

Machaku aliwekewa POP baada ya kuumia alipokuwa na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ilipokuwa inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu ushiriki wa Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Algeria.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema jana kwamba baada ya Machaku kutolewa POP juzi, tayari ameanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiweka sawa na Ligi Kuu.

Alisema Machaku anaungana na Mwinyi Kazimoto, ambaye pia aliteguka mguu katika fainali za kuwania Kombe la Kagame, michuano iliyofikia tamati Julai 10 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alisema kupona kwa wachezaji wake ni faraja kwani wana uhakika timu yao itaendelea kufanya vema katika ligi hiyo, ambao kwa sasa wanashikilia usukani kwa kuwa na pointi 18.

Kamwaga aliongeza kuwa, mshambuliaji wake Mzambia Felix Sunzu, ambaye alishonwa nyuzi nne usoni baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Toto Africa uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, naye ameanza mazoezi.

Aliongeza kuwa wachezaji wa timu hiyo ambao wako katika mapumziko ya wiki moja, wanatarajiwa kuanza kujinoa keshokutwa kwa kuanza mazoezi mepesi.

Aidha, Kocha Mkuu, wa Simba, Moses Basena, aliyekwenda kwao kwa matatizo ya kifamilia anatarajiwa kurejea Oktoba mosi kwa ajili ya kuendelea na kazi yake.

CAMEROON NA NIGERIA ZAALIKWA CECAFA CHALLENGE CUP


Timu za soka za Cameroon na Nigeria zinatarajiwa kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ya mwaka huu.


Miamba hiyo itashiriki kama timu mwalikwa katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Tanzania Bara kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 9, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye kwenye vyombo vya habari vya Rwanda na Kenya, tayari wameshafikia muafaka juu ya ushiriki wa timu hizo na kwamba Baraza lake limetafuta timu nyingine kubwa ili kuifanya michuano iwe na ushindani zaidi.

Mali, Zambia na Malawi zinakamilisha idadi ya timu za kigeni zitakazoshiriki michuano hiyo. Hata hivyo, habari kutoka Nairobi zinasema tarehe hiyo ya kuanza kwa michuano itawaweka kwenye wakati mgumu kwani Ligi Kuu ya Kenya inatarajiwa kumalizika Novemba 26.

Lakini Musonye alisema: “Ratiba imebana na hakuna la kufanya zaidi ya kuipeleka mbele mechi ya kwanza ya Kenya, lakini nahofu inaweza kuwa Novemba 27.

“Hakuna tarehe nyingine ya kupanga kuanza kwa michuano hiyo, fainali zitafanyika Desemba 9, siku ya Uhuru wa Tanzania,” alisema.

Tanzania inakuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuiandaa mwaka jana, hiyo ni mara ya kwanza kutokea katika historia ya michuano hiyo.

Katika michuano ya mwaka jana, timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ilitwaa taji lake la tatu la Chalenji baada ya kuifunga Ivory Coast bao 1-0 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Cameroon ilionesha nia ya kushiriki mwaka jana, lakini haikuthibitisha mpaka dakika za mwisho ratiba ilipoapangwa. Musonye alisema wameamua kufanya michuano hiyo Tanzania kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana kufanyika kwa mafanikio makubwa.

Nchi nyingine zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni Rwanda, Sudan, Djibouti, Eritrea, Kenya, Ethiopia, Burundi, Rwanda, Somalia, Sudan, Zanzibar, Uganda na wenyeji Tanzania Bara.

BARCELONA ALL-TIME TOP SCORERS LIST


1. Cesar Rodriguez (Spain) 1942-55 235
2. Lionel Messi (Argentina) 2004-11 194
2. Ladislao Kubala (Hungary) 1951-61 194
4. Josep Samitier (Spain) 1919-32 178
5. Josep Escola (Spain) 1934-49 167
6. Paulino Alcantara (Philippines) 1912-27 137
7. Angel Arocha (Spain) 1926-33 134
8. Samuel Eto'o (Cameroon) 2004-09 130
9. Rivaldo (Brazil) 1997-02 130
10. Mariano Martin (Spain) 1940-48 124

TOTO TUKUTU BALOTELLI AKIWA NA DEMU WAKE

KAMWAGA: PARTNERSHIP YA COSTA NA NYOSSO YAMCHOMESHA MAHINDI YONDANI.


Partnership iliyopo kati ya beki Victor Costa na Juma Nyoso ndiyo inayomnyima namba katika kikosi cha kwanza beki wa Simba, Kelvin Yondani na wala sio ana matatizo na uongozi wa klabu hiyo.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kitu kinachomfanya mchezaji huyo kutokuonekana katika mechi za Simba hivi sasa ni kutokana na uelewano katika safu ya ulinzi ulioonyeshwa na Nyoso na Costa katika michezo yao yote waliyocheza.

''Hayo ni maamuzi ya kocha kumpanga au kutompanga, lakini safu ya ulinzi ni moja ya nafasi muhimu katika timu, unatakiwa ufanye maamuzi mazuri na makini katika upangaji, kocha kaona Costa na Nyoso wanaelewana zaidi kuliko wachezaji wengine katika nafasi hizo,'' alisema Kamwaga.

Alisema kwa mfano katika mechi yao dhidi ya Toto African ya Mwanza kocha alimpanga Obadia Mungusa na Costa, lakini walikuwa hawaelewani kabisa na kusababisha kuiachia safu ya ushambuliaji ya Toto kupita kilaini na kupata mabao matatu.

Kuhusiana na suala la mchezaji huyo kutoroka kambini, Kamwaga alisema kwa upande wao kama uongozi hawalijui hilo kwa kuwa wachezaji wao wote wamewaruhusu kwenda mapumziko makwao.

''Hatuwezi kujua kama katoroka au la kwa kuwa siku zote tulikuwa naye kasoro wakati tunaenda Kagera tulimuacha kwa kuwa tulienda na wachezaji ambao walikuwa wanacheza tu na tuliporudi hakulipoti kambini na baada ya mchezo wa Mtibwa tulivunja kambi,''alisema Kamwaga.

Hivi karibuni zilikuwapo taarifa za kutoroka kambini mchezaji huyo kwa madai kuwa hapangwi katika mechi kwa kuwa ana ugomvi na kocha wa Simba, Moses Basena pamoja na viongozi wake na hii itakuwa ni mara ya pili mchezaji huyo kutoweka katika timu hiyo.

Kamwaga alisema timu yao itaingia kambini Oktoba mosi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya African lyon Oktoba 16 Jijini Dar es Salaam.

SIMBA WAONGOZA LIGI NA NIDHAMU MBOVU


Vinara wa Ligi Kuu Simba pamoja na kuongoza kwa pointi 18, pia wanaongoza kwa utovu wa nidhamu sambamba na Villa Squad wakiwa na jumla ya kadi 20.

Msimu huu umeonekana kushamiri kwa matukio ya utovu wa nidhamu kulingana na kadi ambazo zimeshatolewa na waamuzi wa ligi mpaka sasa, ambapo tayari zimetolewa kadi 223, huku kadi nyekundu zikiwa 15 na njano 208.

Simba, Villa Squad, Kagera Sugar na Toto African zimeibuka vinara kwa kadi nyekundu na njano.

Villa imeibuka kinara wa kadi za njano baada ya kumiliki kadi hizo 20, Simba 19 na Toto African 18 huku ikiwa kadi 208 zimeshatolewa na waamuzi wa ligi hiyo kwa michezo 55 iliyochezwa sawa na uwiano wa kadi tatu kila mechi.

Kagera Sugar imeibuka kinara wa kadi nyekundu baada ya kumiliki kadi hizo tatu kati 15 zilizotolewa na waamuzi kwa michezo yake minane iliyocheza.Katika michezo hiyo 55 ya Ligi Kuu bara jumla ya mabao 108 yamepachikwa kimiani sawa na uwiano mabao mawili katika kila mchezo.

Washambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Moro Utd na John Boko wa Azam FC wanaongoza kwa kuzifumania nyavu baada ya kila mmoja kuifungia timu yake mabao matano kwa michezo minane waliyoshuka dimbani.

Hata hivyo, timu zilizopanda Ligi Kuu bara msimu huu, Moro Utd na Villa Squad zinaongoza kwa kufungwa mabao mengi, Moro imeruhusu mabao 15 kuingia kwenye wavu wake na kufunga 12, wakati Villa imefungwa 13 na kufunga matano katika michezo minane iliyocheza kwenye ligi hiyo.

AFRIKA KUSINI KUANDAA AFRICA CUP OF NATIONS 2013

MOJA YA VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA KWENYE AFCON 2013

AFRIKA Kusini watakuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 kuchukua nafasi ya Libya, ilitangaza Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).Libya imekubali kuachia wenyeji kwa sababu ya machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo.
Hivyo wamategemewa kuwa wenyeji wa fainali za 2017, zilizokuwa zikitegemea kufanyika Afrika Kusini. Kubadilishana huko kwa nchi hizo mbili kulipata baraka za CAF.Afrika Kusini pia watachukua fainali za 2014 za Mataifa ya Afrika wa Wachezaji wa Ndani CHAN zilizokuwa zifanyike Libya.

Mapema mwaka huu waandaji wa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-20 yaliyokuwa yafanyike Libya waliyaondoa mashindano hayo.

Caf pia walitangaza wenyeji wengine wa mashindano yao makubwa.Namibia watakuwa wenyeji wa fainali za Mataifa ya Afrika 2014 kwa wanawake na Niger watakuwa wenyeji wa U-17 mwaka 2015.
Madagascar watakuwa wenyeji wa U17 mwaka 2017 na mwaka 2015 mashindano ya vijana U20 yatafanyika Senegal.

Wednesday, September 28, 2011

MATOKEO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE



ZENIT ST.PETERSBURG 3-1 FC PORTO



BAYER LEVERKUSEN 2-0 GENK



MARSEILLE 3-0 BORRUSIA DORTMUND



SHAKTAR DONETSK 1-1 APOEL NICOSIA



BATE 0-5 BARCELONA



ARSENAL 2-1 OLYMPIAKOS



AC.MILAN 2-0 PLZEN



CHELSEA 1-1 VALENCIA


BREAKING NEWZ: MAN CITY YAMSIMAMISHA CARLOS TEVEZ


Klabu ya Manchester City imemsimamisha mshambuliaji wake Carlos Tevez baada ya kukataa kuingia uwanjani kama sub katika ya jana dhidi ya Bayern Munich.

Taarifa rasmi ya klabu ilisema:

“Manchester City inathibitisha kwamba mshambuliaji Carlos Tevez amesimamishwa mpaka hapo itapotolewa taarifa nyingine katika kipindi kisichopungua wiki mbili.

“Kusimamishwa huku kwa Tevez kunafuatia madai ya vitendo alivyovifanya wakati wa mchezo wa Jumanne tuliofungwa 2-0 na Bayern Munic.

“Mchezaji hatoruhusiwa kushiriki katika mechi wala mazoezi wakati wote wa adhabu.”

REAL MADRID KUFUNGUA ACADEMY ZA MICHEZO TANZANIA




The technical staff of the Realmadrid Foundation has been in Tanzania imparting a formation course to 50 coaches from 11 different countries.

They also made a technical visit to the Don Bosco Centre facilities and Kilimanjaro Hospital. The first is located next to the Youth Training Center, which has students who are between 14 and 20 years old, and also boasts sports facilities.

The Foundation expects to start a project by which to open social and sports academies that will serve to integrate albino youngsters and physically handicapped children into society. Medicine students will also benefit from the academies.

This is part of the Realmadrid Foundation's boost of its work in the continent this season thorugh 'Project Africa', which covers 20 different projects in 17 countries.



YANGA WAITANDIKA COASTAL UNION BAO 5-0

KIPINDI CHA PILI: ASAMOAH ANAIPATIA YANGA GOLI LA TANO

MPIRA NI MAPUMZIKO NA YANGA WANAONGOZA KWA MABAO MANNE KWA BILA. NURDIN BAKARY, SHAMTE ALLY NA DAVIS MWAPE WAMETUPIA NYAVUNI MAGOLI YA YANGA.

Jan Poulsen Azindua mashindano ya Muivaro cup huko mkoani Arusha.






kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jan Poulsen akikagua timu ya Newlife wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mashindano ya ligi ya vijana na watoto yaliyoanza leo mjini hapa





kocha wa timu ya taifa Jan Poulsen akiwa timu ya Future academy wakati wa uzinduzi wa muivaro cup, mashindano ambayo yameanza jana jijini hapa(picha zote na Woinde Shizza,Arusha)

Tevez Refuses to Play

Real Madrid win all first Bernabeu UCL matches in the last 14 years


The team has scored 48 goals and conceded only nine in this series of games.

.Last season, an own goal from Anita and a strike by Higuain gave Real Madrid a home victory against Ajax in their first UCL match at the Bernabeu. In the 2009/10 they defeated Olympique Marseille 3-0 with goals from Cristiano Ronaldo (2) and Kaka. This success in first UCL home games of the season started 14 years ago and the team keept it up against Ajax tonight.

Back in the 1997/98 campaign, the Madridistas defeated Rosenborg 4-1 in the first Bernabeu clash in the group stage thanks to goals from Panucci, Ze Roberto, Raul and Morientes. The following season Inter Milan were the first to fall at the Madrid stadium in the championship (2-0).

In this series of games, Real Madrid have scored 48 goals and conceded only nine. Their largest victory was their 6-0 win over Belgian side Genk in the 2002/03 season. The Whites have kept clean sheets in seven of these games.



FIRST UCL HOME GAMES
1997/98 Real Madrid 4 - 1 Rosenborg
1998/99 Real Madrid 2 - 0 Inter de Milán
1999/2000 Real Madrid 4 - 1 Molde
2000/01 Real Madrid 1 - 0 Spartak Moscow
2001/02 Real Madrid 4 - 0 Lokomotiv Moscow
2002/03 Real Madrid 6 - 0 Genk
2003/04 Real Madrid 4 - 2 Olympique Marseille
2004/05 Real Madrid 4 - 2 AS Roma
2005/06 Real Madrid 2 - 1 Olympiacos
2006/07 Real Madrid 5 - 1 Dynamo Kiev
2007/08 Real Madrid 2 - 1 Werder Bremen
2008/09 Real Madrid 2 - 0 BATE Borisov
2009/10 Real Madrid 3 - 0 Olympique Marseille
2010/11 Real Madrid 2 - 0 Ajax
2011/12 Real Madrid 3-0 Ajax
TOTAL P W D L GF GA
15 15 0 0 48 9

Azam na pass zao 31.

Tuesday, September 27, 2011

COMING SOON!



KIKOSI CHA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI YA MOROCCO


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo (Septemba 27 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Morocco.

Kikosi hicho kitaingia kambini Septemba 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na kinatarajiwa kuondoka nchini Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Oktoba 9 mwaka huu kwenye mji wa Marrakech.

Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga).

Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba).

Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).

Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) na Jabir Aziz (Azam).

Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Ramadhan Chombo (Azam).

Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).