Search This Blog

Saturday, September 14, 2013

FRANCIS CHEKA APONGEZWA NA MKUU WA MKOANI WA MOROGORO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akiwasili Kwenye Uwanja wa Shujaa Mkoani morogoro Akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Said Amanzi Wakati  wa hafla fupi ya kumpongeza Bondia Francis Cheka aliyeiletea sifa nchi kwa kushinda ubingwa wa dunia kwa Kwa kumchapa  bingwa wa dunia Mmarekani Bondia Williams 
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akimpokea Bondia Francis Cheka wakati akiwasili uwanjani  katika halfa ya kumpongeza Bondia huyo aliyenyakua Ubingwa wa Dunia Kwa Kumchapa bondia kutoka Marekani.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akikabidhiwa Mkanda wa Ubingwa wa Dunia kutoka kwa Bondia Francis Cheka Leo Mjini Morogoro
Bondia Francis Cheka akitoa neno la Shukrani na Pembeni yake Ni Mke wa Bondia Huyo
Kocha wa Bondia Huyo Aliyefahamika kwa jina la Komando Akisema Machache wakati wa Halfa hiyo leo
Mkuu wa wilaya ya Mvomero na rais wa Riadha Tanzania Mh Antony Mtaka Akisema machache
Akizungumza katika hafla Mkuu wa Mkoa Mh Joel  Bendera alisema  ushindi wa Cheka ni sifa kwa tanzania katika  mchezo wa ngumi. Bondia Francis Cheka amezawadiwa kiwanja  mabati, na Tani moja ya saruji  Picha na MATUKIO NA MICHAPO BLOG

LIVE SCORE VODACOM PREMIER LEAGUE: YANGA 1-1 MBEYA CITY - SIMBA 2-0MTIBWA - KAGERA 1-1 AZAM FCFull time Mbeya City 1-1 Yanga

Dakika ya 85, Mbeya City 1 - 1 Young Africans

Dakika ya 75, Mbeya City 1 - 1 Young Africans

Dk 90+4. FULL TIME! SIMBA 2-0 MTIBWA 

Kavumbagu anaisawazishia Yanga hapa Sokoine - Mbeya City 1-1 Yanga.

Dk 90 GOOOO....! Mwombeki anaipatia Simba bao la pili baada ya kupokea pasi ya Ramadhan Singano. SIMBA 2-0 MTIBWA 

Dk 88 Mwombeki anakosa bao baada ya kushindwa kupiga shuti kuelekea lango la Mtibwa. SIMBA 1-0 MTIBWA 

Dk 70  Mbeya City 1 Yanga 0

Dk 80 SUB: Simba inafanya mabadiliko ametoka Chanongo ameingia Ramadhan Singano. 

Dk 76 SUB: Mtibwa inafanya mabadiliko ametoka Kisiga ameingia Abdallah Juma. 

DK 53 Mbeya City wanapata bao la kuongoza dhidi ya mabingwa watetezi Yanga

Dk 74 Kisiga anakosa bao la wazi akiwa ametengewa mpira sehemu nzuri langoni kwa Simba. 

Dakika ya 50 Mbeya City 0-0 Yanga

Dakika 56' Kagera Sugar 1-1 Azam Mcha Khamis anaisawazishia Azam 

Dk 67 GOOOOOO....! Henry Joseph anaipatia Simba bao la kwanza kwa kichwa akiunganisha krosi fupi ya Kiemba. SIMBA 1-0 MTIBWA 

Dk 64 SUB: Simba inafanya mabadiliko ametoka Twaha Ibrahim ameingia Betram Mwombeki. 

Dk 61 Kisiga wa Mtibwa anakosa bao la wazi la mbali baada ya Dhaira kukosea kuanzisha mpira. 

Dk 59 SUB: Mtibwa imefanya mabadiliko ametoka Masoud Mohamed ameingia Awadhi Juma. 

Katika uwanja wa Sokoine mpira ni mapumziko na hakuna timu iliona goli la mwenzake.

Dk 56 SUB: Simba inafanya mabadiliko ametoka Said Hamis ameingia Henry Joseph. 

Dk 52 Owino wa Simba anamchezea rafu Mgosi nje kidogo ya eneo la hatari la Simba. 

Dakika 52' Simba 0-0 Mtibwa Sugar 

Dk  44 Mbeya City 0 Yanga 0

Dk 46 SUB: Mtibwa imefanya mabadiliko ametoka Juma Liuzio ameingia Mussa Hassan Mgosi. 

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA! 

 Dakika ya 30, Mbeya City 0 - 0 Young Africans

Dk 45 HALF TIME! SIMBA 0-0 MTIBWA 

Dk 24' Kagera Sugar 1-0 Azam Fc ( Themi Felix) 

DK 15 - Milango bado haijafunguka katika mchezo kati ya Yanga na Mbeya 

Dk 40 YELLOW CARD....! Masoud Mohamed wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Jonas Mkude wa Simba. 

Dk 33 Chanongo wa Simba anamchezea rafu Kisiga wa Mtibwa. SIMBA 0- 0 MTIBWA 

Dakika ya 10- Mbeya City 0-0 Yanga

Dk 27 Joseph Owino wa Simba anamchezea rafu Ally Shomari wa Mtibwa nje kidogo ya lango la Simba. 

Dk 24 Ngalema wa Mtibwa ameumia baada ya kuwekewa mguu na Chanongo, wakati huohuo Mtibwa imepata kona lakini haikuzaa matunda. Simba 0-0 Mtibwa 

Dk 15 Chanongo wa Simba anachezewa tackling na Ally Shomari wa Mtibwa na mpira unakuwa kona kuelekea lango la Mtibwa. Mashabiki wa Simba wanalalamikia maamuzi hayo.

Mpira umeanza mjini Mbeya kati ya Yanga vs Mbeya City

Dk 11 Vincent Barnabas wa Mtibwa anakosa bao la wazi akiwa ndani ya eneo la hatari la Simba baada ya mpira alioupiga kutoka nje ya lango. 

Dk 9 Dickson Daud Mbeikya anamchezea faulo Tambwe wa Simba. Mtibwa wanacheza soka la nguvu zaidi. 

Dk 7 Paul Ngalema wa Mtibwa  anamchezea faulo Amis Tambwe wa Simba. Timu zinashambuliana kwa zamu lakini Simba ndiyo inayofika langoni kwa Mtibwa mara kwa mara.

Uwanja wa taifa mpira umeanza kati ya Simba na Mtibwa - Dakika 2 za kwanza Simba wanalisakama sana lango la Mtibwa na kupata kona mbili tasa. 

BAADHI YA VIKOSI VYA TIMU ZINAZOCHEZA LEO
AZAM FC

1. Mwadini Ali Mwadini
2. Erasto Edward Nyoni
3. Waziri Sallum Omar
4. Aggrey Moris Ambrosi
5. Jockins Otieno Atudo
6. Bolou Wilfred Michael
7. Jabir Aziz Stima (C)
8. Sallum Abubakar Sallum
9. Gaudence Exavery Mwaikimba
10. Kipre Hermann Brice Tchetche
11. Mcha Khamisi Mcha
Akiba
1. Aishi Sallum Manula
2. Malika Philipo Ndeule
3. David John Mwantika
4. Said Hussein Morad
5. Ibrahim Joel Mwaipopo
6. Himid Mao Mkami
7. Seif Abdallah Rashid Karihe


Simba 
line up: Abel Dhaira, Nassor Masoud (Captain), Issa Rashid, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Twaha Ibrahim, Said Hamis, Amisi Tambwe, Amri Kiemba na Haruni Chanongo.

Benchi: Abuu Hashim, Miraji Adam, Henry Joseph, Ramadhan Singano 'Messi', Betram Mwombeki, Abdulhalim Humud na Adeyum Ahmed.

Mtibwa Sugar line up: Hussein Sharrif 'Casillas', Hassan Ramadhan, Paul George, Dickson Mbeikya, Salim Abdallah, Shaaban Nditi (Captain), Ally Shomari, Masoud Mohamed, Juma Liuzio, Shabani Kisiga na Vincent Barnabas.

Benchi: Said Mohamed, Ally Ally, Musa Hassan, Abdallah Juma, Awadh Juma, Salum Sued 'Kussi', na Said Mkopi.


YANGA
1.All Mustapha 'Barthez' - 1
2.Mbuyu Twite - 6
3.David Luhende - 3
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' - 23
5.Kelvin Yondani - 5
6.Athuman Idd 'Chuji' - 24
7.Nizar Khalfani - 16
8.Frank Domayo - 18
9.Didier Kavumbagu - 7
10.Hussein Javu - 21
11.Said Bahanuzi - 11

Subs:
1.Deogratius Munishi 'Dida' - 30
2.Juma Abdul - 12
3.Oscar Joshua - 4
4.Rajab Zahir - 14
5.Salum Telela - 2
6.Shaban Kondo - 15
7.Jerson Tegete - 10

YANGA WASHAMBULIWA NA MASHABIKI WA MBEYA CITY WAKIINGIA KWENYE UWANJAWA SOKOINE - BASI LAVUNJWA VIOO

Dakika chache zilizopita wakati basi la klabu ya Yanga likiwa linaingia katika uwanja wa sokoine mjini Mbeya limeshambuliwa na mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Mbeya City kwa kupigwa mawe, kitu kilichopelekea vioo vya gari hilo kupasuka.

Mpaka sasa hakuna taarifa kama kuna mchezaji yoyote wa klabu hiyo aliyejeruhiwa.

MAKALA: SIMBA KULIPA KISASI DHIDI YA MTIBWA SUGAR AU KUENDELEZA UTEJA LEO TAIFA?MTIBWA SUGAR

SIMBA

                                                Simba watakuwa wakicheza wakitaka ushindi wa pili mfululizo katika ligi kuu ya Vodacom watakapokutana na Mtibwa Sugar leo hii katika uwanja wa taifa. Simba pia watakuwa wakitafuta namna ya kulipa kisasi cha msimu uliopita ambao walifungwa mechi zote mbii na wakata miwa wa Turiani.
Huu ni mchezo wa kwanza wa Simba kucheza uwanja wa nyumbani msimu huu, wakiwa tayari wamecheza ugenini Tabora na Arusha katika michezo miwili ya kwanza ya msimu. Walishinda mechi yao ya kwana kwa kuwafunga JKT Oljoro 1-0 jijini Arusha shukrani kwa bao la Haroun Chanongo katika dakika ya 34 ya mchezo. 


Simba wamecheza mbili za kujipima nguvu kabla ya mchezo wa leo dhidi ya mabingwa wa Zanzibar KMKM na timu ya ligi ya daraja la kwanza, Lipuli. Wachezaji wake wote muhimu wapo vizuri kucheza akiwemo mchezaji mpya, nahodha wa zamani wa timu hiyo, Henry Joseph Shindika.

Mechi 3 zijazo za Simba: Mgambo JKT and Mbeya City (zote za nyumbani), JKT Ruvu (Ugenini)


Mtibwa pia itakuwa ikiutaka ushindi wa pili mfululizo katika VPL baada ya kupata ushindi wa kwanza kuwafunga wakata miwa wenzao, Kagera Sugar wiki mbili zilizopita. Chini ya makocha ambao wameishatumikia timu hiyo wakiwa wachezaji Mexime na Zuberi Katwila, watakuwa wakitafuta namna ya kuendeleza umwamba wao dhidi ya vijana wa mitaa ya msimbazi. 


Mechi 3 zijazo za Mtibwa Sugar: Mbeya City (Nyumbani), Tanzania Prison na Ashanti United (Ugenini).

TAKWIMU ZA SIMBA VS MTIBWA: Simba imefungwa mechi mbili za mwisho ilizokutana na Mtibwa. Mtibwa Sugar hawajaruhusu wavu wao kuguswa katika mechi mbili zilizpita dhidi ya Simba. 


Kikosi cha Simba katika mechi iliyopita ambacho kinaweza kuanza leo: Abel Dhaira, Nassor Chollo, Issa Rashid, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Abdulhalim Humud, Amis Tambwe, Betram Mwombeki, Haroun Chanongo


Wachezaji muhimu: Amisi Tambwe na Betram Mwombeki (Simba). Simba watawategemea washambuliaji wao wawili wakati Mtibwa itategemea zaidi maujuzi ya Shaban Kisiga na Juma Luizio ambao pia wanaweza kuungana na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Hassan Mgosi.


MAKALA HII IMETAFSIRIWA KUTOKA LONESTRIKERTZ BLOG

OKWI AJIUNGA NA URA KUSUBIRI HATMA YAKE KWA WAARABU - FIFA YAWAPA ETOILE MPAKA MWISHO MWA MWEZI HUU KUWALIPA MIL 480 SIMBA


STRAIKA wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi amejiunga na URA ya Uganda ili kujiweka fiti akisubiri hatma yake kwenye klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Okwi amegoma kuichezea Etoile du Sahel mpaka itakapommalizia malipo yake ya kusaini mkataba pamoja na kumlipa malimbikizo ya mishahara ya miezi mitatu.
“Nimetulia kwanza nione suala langu linaendaje na suluhisho ni nini. Ninataka sana kurudi uwanjani kucheza soka la ushindani,” alisema Okwi.
“Ishu ni kwamba hawajanimalizia pesa ya kusaini mkataba pamoja na mishahara yangu ya miezi mitatu sasa,” alisema Okwi ambaye anaendelea kujinoa na URA ingawa haruhusiwi kucheza mechi ya mashindano kwa sababu ana mkataba wa miaka mitatu na Etoile du Sahel.
Wakala wa mchezaji huyo amesema kwamba wanaendelea na mazungumzo na Etoile ili kutatua suala la Okwi ingawa habari za ndani zinasema kwamba anafanya mpango wa kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu moja ya Daraja la Kwanza Ulaya.
Okwi aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda na kucheza dhidi ya Senegal wiki iliyopita katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia na kushuhudia kikosi cha Kocha Sredojevic Milutin ‘Micho’ kikiambuliwa kipigo cha bao 1-0.
Wakati Okwi akiwa na malumbano hayo na klabu hiyo ya Tunisia, Simba ambayo ilimuuza nayo inasubiri malipo ya Sh480 milioni kutoka kwa Etoile du Sahel ambayo iliahidi kulipa fedha hizo kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetoa mpaka mwisho wa mwezi huu Simba iwe imelipwa.
SOURCE: MWANASPOTI

Friday, September 13, 2013

DANIEL STURRIDGE NA KOCHA WAKE BRENDAN ROGERS WAIBUKA TUZO ZA MWEZI AUGUST EPL

Baada ya kuiwezesha Liverpool kuanza vizuri msimu wa ligi kuu ya England - Kocha Brendan Rogers na mshambuliaji wa timu hiyo Daniel Sturridge wameshinda tuzo za mwezi za EPL.

BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA SERIKALI KUMJENGEA NYUMBA YA KISASA FRANCIS CHEKA

Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia mkuu wa mkoa wa Morogoro leo hii imemfanyia hafla fupi ya kumpongeza Bondia Francis Cheka aliyeiletea sifa kubwa nchi baada ya kushinda ubingwa wa dunia kwa kumtandika aliyekuwa bingwa wa dunia Phil Williams kutoka nchini Marekani.

Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika katika viwanja vya Shujaa katika manisapaa ya Morgoro na kuhudhuriwa na mamia ya wakzi wa mji wa Morogoro wakiongozwa na mkuu wa mkoa Mh.Joel Bendera.

Akizungumza katika hafla hiyo Bendera alisema serikali imefurahishwa sana na ushindi wa Cheka ambao umeiletea nchi sifa kubwa katika anga ya kimataifa ya mchezo wa ngumi. Kutokana na jambo hilo serikali imeamua kumzawadia Francis Cheka kiwanja kikubwa, mabati ya nyumba nzima, mifuko 80 thamanini ya saruji na pia usimamizi na taratibu zote mpaka nyumba ya kisasa itakapokamilika kwa ajili kukabidhiwa kwa Cheka.

OFFICIAL: MAROUNE FELLAINI ATAMBULISHWA RASMI MAN UNITED
Fel
Close to failure: Fellaini admitted that he was worried about the deal falling through on deadline day

Debut: Fellaini is ready to start for United against Crystal Palace

Fell
Fell

RATIBA LIGI KUU KESHO: YANGA DHIDI YA MBEYA CITY - SIMBA VS MTIBWA - AZAM TV KUANZA MAZOEZI KESHO


Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya tatu kesho (Septemba 14 mwaka huu) kwa timu zote 14 kushuka viwanjani huku masikio ya washabiki wengi yakielekezwa kwenye mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar na ile kati ya Mbeya City na Yanga.

Simba inaikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana kutoka Dodoma. Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.

Pia Azam TV itautumia mchezo huo kwa ajili ya mazoezi (broadcast training) kwa wafanyakazi wake. Hivyo mechi hiyo haitarekodiwa au kuoneshwa moja kwa moja.

Katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, shughuli itakuwa kati ya mabingwa watetezi Yanga na wenyeji wao Mbeya City SC. Mwamuzi Andrew Shamba kutoka Pwani ndiye atakayepuliza filimbi wakati Kamishna wa mechi hiyo James Mhagama kutoka Songea.

Mechi nyingine za ligi hiyo ni Coastal Union na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Ruvu Shooting na Mgambo Shooting (Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani), Oljoro JKT na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Kagera Sugar na Azam (Uwanja wa Kaitba, Bukoba), na Ashanti United na JKT Ruvu (Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam).

WACHEZAJI 620 WATHIBITISHIWA USAJILI FDL
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imethibitisha usajili wa wachezaji 620 kati ya 624 wa timu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoanza kutimua vumbi kesho (Septemba 14 mwaka huu).

Wachezaji wanne ambao usajili wao umezuiwa mpaka watakapokamilisha taratibu ni Emmanuel Simwanza Namwando wa African Lyon, Godfrey Bonny Namumana (Lipuli FC), na Enyinna Darlington na Chika Keneth Chukwu wote wa Mwadui FC ya Shinyanga.

Darlington na Chukwu ambao wote ni Wanigeria wamezuiwa mpaka watakapowasilisha vibali vya kufanya kazi nchini kutoka Idara ya Uhamiaji wakati Namumana aliyekuwa akicheza nchini Nepal bado hajapata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).

Nayo African Lyon imetakiwa kufikia muafaka na AYOSA Academy ambayo Namwando anatoka juu ya usajili kabla ya kuanza kumtumia mchezaji huyo.

Klabu ambazo zimemaliza nafasi zote 30 usajili katika FDL ni Friends Rangers FC ya Dar es Salaam, na Stand United FC ya Shinyanga wakati iliyosajili wachezaji wachache zaidi ni Burkina Faso FC. Klabu hiyo ya Morogoro imesajili wachezaji 19 tu.

Vilevile Kamati hiyo vilevile imethibitisha usajili wa wachezaji wanane wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) waliosajiliwa katika hatua ya pili ya usajili iliyoanza Agosti 14 hadi 30 mwaka huu.

Wachezaji hao ni Samir Ruhava na Amani Simba (Ashanti United), Robert Machucha na Said Ndutu (Yanga U20), Ayoub Masoud na Abdallah Selemani (Coastal Union U20), Ramadhan Kipalamoto (Simba U20) na Henry Joseph (Simba) ambaye tayari Hati yake Uhamisho wa Kimataifa (ITC) imeshawasili.YANGA WAPEWA SIKU 14 KUWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA DENI LAO LA MILLIONI 15.5


Yanga imepewa siku 14 kuanzia leo (Septemba 13 mwaka huu) kuwalipa waliokuwa wachezaji wake msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa na Stephen Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya sh. milioni 15.5.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilisikiliza madai ya wachezaji hao.

Fedha hizo ni ada ya usajili ambayo klabu hiyo ilikubaliana na wachezaji hao wakati ikiwasainisha mikataba. Yanga imeshawalipa sehemu ya fedha walizokubaliana na kiasi hicho ndicho bado hakijalipwa. Nsajigwa anadai sh. milioni 9 wakati Mwasika ni sh. milioni 6.5.

TENGA ASIFU KAMATI YA LIGI - ATAMBIA MKATABA WA AZAM TV - TIKETI ELEKTRONIKI KUANZA KUTUMIKA HIVI KARIBUNI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ameishukuru Kamati ya Ligi kwa usimamizi mzuri tangu ilipokabidhi Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) katika mzunguko wa pili msimu uliopita.

Amesema TFF iliamua kuanzisha Kamati ya Ligi kwa lengo la kutaka klabu zijisimamie zenyewe ili kuongeza ufanisi, jambo ambalo limeleta mabadiliko kwa vile hivi sasa hakuna matatizo katika kuwalipa marefa na makamisha wanaosimamia VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

“Fedha za udhamini sasa zinakwenda moja kwa moja kwenye Kamati ya Ligi. Ni matarajio yangu kuwa ufanisi utaongezeka, kwani tumeanzisha jambo hili kwa lengo la kuleta tija, maendeleo na utulivu,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na Wahariri wa Michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

Rais Tenga amesema mahali penye utulivu na utawala bora watu wanakuwa na imani hasa katika masuala ya fedha, hivyo ni lazima kwa kampuni kuwekeza kwa vile kunakuwa hakuna vurugu.

Amesema ukiondoa Afrika Kusini na Angola katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Ligi Kuu ya Tanzania ndiyo yenye udhamini mkubwa kupitia mdhamini wa ligi na udhamini wa matangazo ya televisheni.

Pia amesema kuanzia msimu ujao 2014/2015 klabu za Ligi Kuu hazitaruhusiwa kusajili wachezaji hadi zitakapowasilisha TFF ripoti zao za mapato na matumizi zilizokaguliwa (Audited accounts), hivyo klabu husika zijiandae kwa ripoti hizo za Januari hadi Desemba 2013.

Kuhusu tiketi za elektroniki, Rais Tenga amesema bado linafanyiwa kazi na CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo na liko katika hatua nzuri, kwani nia ya TFF na benki hiyo kuona kuwa linaanza haraka iwezekanavyo.

“Tiketi za elektroniki zimechelewa kuanza kwa sababu ambazo haziwezi kuzuilika, lakini CRDB imeshatengeneza miundombinu katika karibu viwanja vyote. Kulitokea uchelewaji katika kuleta printer (mashine za kuchapia), zilizokuja hazikuwa zenyewe. Kwa upande wa Uwanja wa Taifa, system (mfumo) iliyopo inatofautiana na ile ya CRDB. Hivyo sasa tunaangalia uwezekano wa zote mbili zitumike kwa pamoja, kwa sababu Uwanja wa Taifa una system yake tayari. Printer zimeshafika, tunataka ili suala lisitucheleweshe,” amesema.

SEMINA YA KAMATA FURSA TWENDE ZETU YAFANA DODOMA


Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu,iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea mapema leo asubuhi.

 Wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya kamata fursa twendzetu,mapema leo asubuhi mkoani Dodoma.

 Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali yatokanayo na faida za kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu iliofanyika mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
  Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
 Meneja wa  NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Maxmalipo,Renard Munuri akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.

 Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya  mafanikio katika kupambana na maisha.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.

 Baadhi ya wasanii ambao wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la NSSF,shoto ni Queen Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau Phillipon mapema leo,wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa ikiendelea.
 Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa kwa vijana
 Sehemu ya meza kuu ya watoayo mada wakishangilia jambo.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.

ETO'O: 'NISHAWAHI KUAPA KUTOCHEZA KWENYE TIMU INAYOFUNDISHWA NA MOURINHO - LEO HII KOCHA NA RAFIKI YANGU'


Samuel Eto'o amefunguka na kusema kwamba aliwahi kuapa kutokuja kucheza chini ya kocha Jose Mourinho.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alisema alikuwa na mahusiano yasiyoridhisha na na kocha wa kireno kabla ya hawajafanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan, mahala ambapo walishinda vikombe vitatu kwa msimu mmoja. 

Eto'o ameungana tena na Mourinho wakati alipojiunga na Chelsea hivi karibuni akitokea klabu ya Anzhi Makhachkala kwa mkataba wa mwaka mmpja utaoisha wakati ujao wa kiangazi. 

Huu ulikuwa uhamisho ambao Eto'o mwanzoni asingeweza kukubaliana nao.

"Kabla hatujakutana kule Inter, Jose na mimi hatukujuana vizuri kwa ukaribu, hivyo mahusiano yetu hayakuwa yakieleweka," alikaririwa Eto'o alipohojiwa na gazeti la The Sun.

"Nadhani nilisema huko nyuma kwamba nisingekuja kuichezea klabu inayofundishwa na Jose.
“Lakini mungu anajua zaidi. Alitaka kunionyesha sikuwa sahihi na leo hii Jose ni rafiki yangu mkubwa, pia ni kocha wangu kwa mara nyingine tena."

FRANCIS CHEKA KUFANYIWA HAFLA YA KUPONGEZWA LEO HII - SHAFFIH DAUDA MGENI MWALIKWA


Nikiwa bado nipo mjini Morogoro leo hii nimepokea mwaliko kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh.Joel Bendera kwenda kuhudhuria gafla fupi ya kumpongeza shujaa wa taifa na mkoa wa Morogoro Bondia Francis Cheka kwa kutwaa ubingwa wa duniani wa WBF kwa kumdunda bondia mmarekani hivi karibuni.

Hafla hiyo inafanyika leo katika uwanja wa Shujaa uliopo katika manisapaa ya Morogoro kuanzia 8:30 mchana.


HATIMAYE LIONEL MESSI AKIRI FRANK RIBERY NDIO MCHEZAJI BORA WA ULAYA KWA SASA

Nyota wa Barcelona  Lionel Messi amekiri kwamba winga wa Bayern Munich Franck Ribery anastahili kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ulaya kwa mwaka huu.

Muargentina huyo na Cristiano Ronaldo walikuwa wanashindania tuzo hiyo lakini wakashindwa na Ribery jijini Monaco mwezi uliopita na sasa mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 amesema kwamba mafanikio ya Ribery kushinda makombe matatu yanamaanisha kwamba ndio mchezaji sahihi kutwaa tuzo hiyo.
"Ilikuwa ni heshima kubwa kuwa katika kinyang'anyiro kwa mara nyingine tena, miongoni mwa wachezaji wa tatu bora brani ulaya, aliiambia Uefa.

"Kuna wachezaji wengi wazuri duniani na ni jambo kubwa kushindani lakini kwa hivi ni Ribery anayestahili kushinda tuzo hiyo."

Messi na timu yake ya Barcelona waliondolewa kwenye mashindano ya Champions league msimu uliopita kwa aibu ya kufungwa jumla ya mabao 7-0 na Bayern Munich.

Thursday, September 12, 2013

BAADA YA KUFUNGIWA NA TFF WAAMUZI MARTIN SAANYA NA JESS ERASMUS WARUDI MORO KUFUNDISHA KANUNI NA SHERIA ZA UREFA

Leo nikiwa mjini Morogoro katika kufanya maandalizi ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza katika viwanja vya Moro Youth  - mahala ambapo bonanza hilo litafanyika jumamosi hii - nimefanikiwa kukutana na waamuzi waliofungiwa na shirikisho la soka nchini TFF kwa madai ya kushindwa kuumudu vizuri mchezo raundi ya pili ya ligi kuu ya Tanzania bara kati ya mabingwa watetezi Yanga dhidi ya Wagosi Coastal Union.

Katika mazungumzo yangu na waamuzi hao wawili ambao ni waajariwa wa jeshi la magereza nchini wamesema baada ya kufungiwa na TFF wanaendelea na ajira yao ya jeshi la magereza huku wakitoa mafunzo ya urefa kwa vijana wadogo kupitia Taasisi ya  Morogoro Referee's Youth Talent.

Pamoja na hayo waamuzi hawa wawili wameteuliwa kusimamia michezo ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza itakoyofanyika siku ya jumamosi.

MESUT OZIL AANZA RASMI MAZOEZI ARSENAL HUKU FAMILIA YAKE IKITISHIA KUISHTAKI REAL MADRID

Happy to be here: Mesut Ozil (right) trains for the first time at Arsenal, with Germany team-mate Per Mertesacker

Familia ya mchezaji Mesut Ozil imetishia kumshataki raisi wa  Real Madrid  Florentino Perez juu ya madai kwamba mahusiano yake na mrembo wa kivenezuela yalimfanya ashuke kiwango alipokuwa Santiago Bernabeu. 

Baba yake Ozil, Mustafa alimshambulia vikali Perez, huku mwanae akiwa anatambulishwa rasmi kwenye klabu yake ya Arsenal na kuanza mazoezi, Mr. Mustafa Ozil alisema kwamba hatua za kuanza kumshtaki zimeanza. 
Mzee huyo ameonekana kukasirishwa vibaya kufuatia taarifa zilizochapishwa na gazeti la kihispania Marca kwamba Perez amesema kiwango cha Ozil akiwa na Real Madrid kilishuka kufuatia kuhangaika kwake na mpenzi wake ambaye ni mrembo wa zamani wa Venezuela, Aida Yespica.


Ozil Snr pia alikasirishwa na mawazo kwamba ubinafsi wake wa kutaka fedha nyingi zaidi ndio uliochangia mjerumani huyo kujiunga na klabu ya Arsenal akitokea Madrid. 
‘Ni wazi Perez sio mwanadamu mwenye heshima, anaweza kuwa na fedha nyingi lakini hilo halimfanyi kuwa mtu mwenye heshima na adabu. 
'Anajaribu kufanya kwamba Mesut hakuwa mweledi kutoka na staili ya maisha yake akiwa Madrid na mimi baba yake nina uroho wa fedha tu. Haya yote ni ya uongo, na ndio maana nafikiria kumshtaki. 

‘Tutaangalia kila kitu, mawakili wameanza kuangalia kama kesi itakuwa na nguvu au la kabla ya kuangalia mbele, na baada ya hapo tutaamua hatua za kisheria za kuchukua. 

‘Anataka kumgeuza Mesut mbuzi wa kafara na kuonyesha kwamba ana mzazi mroho wa fedha, wakati hay mambo yapo mbali na ukweli. Tupo tayari kujitetea, kwa sababu ninachokitaka kwa mwanangu ni kufanikiwa. Hilo ndilo limekuwa jukumu langu siku zote.’Mesut Ozil Mesut Ozil
Dummy run: Ozil really gets into training at London Colney
Mesut Ozil
Mesut Ozil


ROBERTO CARLOS AWAONYA CHELSEA JUU YA TABIA ZA UBINAFSI NA KUJIONA KWA SAMUEL ETO'O

Roberto Carlos amewaonya Chelsea kwamba mshambuliaji wao mpya Samuel Eto'o anaweza kawa na ushawishi mbaya ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa timu ya Anzhi Makhachkala amesema kwamba mshambuliaji huyo mcameroon aliingilia majukumu yake ya kazi wakiwa pamoja katika klabu hiyo ya Russia mpaka kufikia hatua kwamba alianza kufikiria kujiuzulu.
Mwaka 2011, Carlos alikuwa Anzhi wakati timu hiyo ilipomnunua Eto'o kutoka Inter Milan, na kumfanya mchezaji huyo kuwa mwanasoka anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani. 


Baada ya kufunga mabao 36 katika mechi 71 akiwa na Anzhi, Eto'o amehamia Chelsea kwa uhamisho huru na anaweza kuanza katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Everton jumamosi hii.

Lakini mahojiano na gazeti la Globo, Carlos ameelezea na namna Eto'o alivyomfanyia wakati wakiwa Anzhi.
Alisema: 'Nimemfahamu Eto'o tangu nikiwa na miaka 16, na kutokea wakati huo amekuwa mtu mzuri kwangu niliyempenda. 
'Ni mtu mzuri, lakini kuna kitu kuhusu yeye 'ubinafsi' ndio kinachoharibu sifa yake. 
'Wakati mchezaji ambaye badala ya kucheza vizuri - hukaa na kujariu kulazimisha kusajiliwa kwa wachezaji ambao ni marafiki zake - ni suala la kusikitisha na linachanganya na kushangaza hasa kwa mchezaji kama Eto'o. Alifanya yote haya akiwa Anzhi lakini sio kucheza soka la kiwango kikubwa.'Akizungumiza namna mahusiano yao yalivyoharibika, Carlos alisema: 'Nilienda kwenye klabu na katika mwaka wangu wa kwanza timu ilimaliza kwenye nafasi tano za juu.
'Tuliweza kuiweka timu kuwa katika ueledi wa 100%. Mwaka wa pili, tukamsaini Eto'o na nilikuwa na control ya timu - Nilifanya kazi na wachezaji na makocha. Nilifanya kazi nzuri katika kuifanya Anzhi kuwa miongoni mwa timu bora.

'Kuwasili kwa Eto'o, huku thamani ya kila ikijulikana, nilipata matatizo kidogo katika chumba cha kubadilishia nguo na ikabidi niongee na wachezaji wa kirusi na kuwaelezea kwanini Eto'o alikuwa pale. 
'Japokuwa, ukafika wakati Eto'o akaanza kuingilia majukumu yangu, kutaka kuwa na mamlaka ndani ya timu, majukumu yangu na yale ya kocha Guus [Hiddink].

'Tuliongea kuhusu jambo moja, na baada hapo alikuwa anaenda kwa wachezaji anawaambia jambo lingine. Hilo lilinikera sana na nilionya ningeondoka.
'Hakuna aliyeniamini kwa sababu nilikuwa na mkataba wa miaka minne. Lakini baadae niliwaita Anzhi na kufikia makubaliano.'
Carlos, 40, tangu wakati akaondoka na sasa anafanya kazi kama mkurugenzi wa timu Sivasspor huko Turkey. Mmiliki wa Anzhi Suleyman Kerimov aliamua kuondokana na matumizi makubwa ya klabu na kupelekea kuuzwa kwa wachezaji kadhaa.