Search This Blog

Thursday, September 12, 2013

BAADA YA KUFUNGIWA NA TFF WAAMUZI MARTIN SAANYA NA JESS ERASMUS WARUDI MORO KUFUNDISHA KANUNI NA SHERIA ZA UREFA

Leo nikiwa mjini Morogoro katika kufanya maandalizi ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza katika viwanja vya Moro Youth  - mahala ambapo bonanza hilo litafanyika jumamosi hii - nimefanikiwa kukutana na waamuzi waliofungiwa na shirikisho la soka nchini TFF kwa madai ya kushindwa kuumudu vizuri mchezo raundi ya pili ya ligi kuu ya Tanzania bara kati ya mabingwa watetezi Yanga dhidi ya Wagosi Coastal Union.

Katika mazungumzo yangu na waamuzi hao wawili ambao ni waajariwa wa jeshi la magereza nchini wamesema baada ya kufungiwa na TFF wanaendelea na ajira yao ya jeshi la magereza huku wakitoa mafunzo ya urefa kwa vijana wadogo kupitia Taasisi ya  Morogoro Referee's Youth Talent.

Pamoja na hayo waamuzi hawa wawili wameteuliwa kusimamia michezo ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza itakoyofanyika siku ya jumamosi.

No comments:

Post a Comment